Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104809 articles
Browse latest View live

Wadada: Wanaume Warefu Wanajisikia na Wana Dharau Sana Kwenye Swala la Mahusiano

$
0
0
Kuna mdada mmoja aliniambia kuwa aliwahi kutoka kimapenzi na wanaume watatu kwa nyakati tofauti-tofauti. Mdada huyo ameniambia kuwa wanaume warefu wanakera, kwani wanajiona sana na kujisikia, pia wana dharau na hawapendi mazungumzo mengi kama watu wafupi walivyo.

Nimejaribu kuuliza kwa wa baadhi ya wadada wanasema kuwa wanaume warefu ni wazuri nje ila tabia zao sio, wengi wanawaona watu walio wafupi kama takataka. nimeona nililete kwenu Tujadili Kama Kuna Ukweli wowote wa Jambo Hili.....

Je  Kuna Ukweli ?

Hivi Ndivyo Wanawake wa Mjini Wanavyoendesha Wanaume Hapa Mjini...Pesa Pesa Pesa

$
0
0
Hivi Ndivyo Wanawake wa Mjini Wanavyoendesha Wanaume Hapa Mjini...Pesa Pesa Pesa...Soma Hizo Baadhi ya Message Hapo chini : Bila Pesa Mjini hapa wewe Mwanaume si Kitu...Ukibahatika Kusoma Meseji kwenye Inbox ya Simu ya Mkaka wa Mjini Inbox nzima imejaa Meseji za Mizinga kutoka kwa Wadada wa Mujini...Uongo Kweli ?

EdwardLowassa ni Adui Mbaya kwa CCM Kuliko Adui Yeyote Waliyewahi Kupambana Naye

$
0
0
Kwenye maswala ya kiusalama na kivita huwa tunajifunza dhana mhimu sana isemayo, kumjua adui ni nusu ya ushindi. Adui wa Lowasa ni ccm chini ya "kitengo" kilichochini ya Jakaya Kikwete. Na adui wa ccm ni Lowasa.

Chadema waliumizwa mda mrefu sana na Zitto kwakuwa walikuwa wanapambana na adui wasiyemjua, siku walipomjua walimtupa nje na sasa usalama wa chadema umeimarika maradufu.

Ni bora kupambana na Adui aliyejitangaza rasmi kuwa yeye ni adui kwako kuliko yule unaekula nae na kulala nae bila kujitangaza kwamba ni adui kwako.


Lowasa anaweza kuwa adui mbaya kwa ccm kuliko adui yeyote waliyewahi kupambana nae. Kwa habari njema nikuwa majemadari wa ukombozi wakiongozwa Ally Bananga diwani wa Sombetini wamevamia kwa mikutano Monduli ilipo Ngome ya Lowasa. Habari njema zilizopo ni kwamba amevuna madiwani wa ccm na huko pia.


Ccm watapata wakati mgumu sana endapo Lowasa ataendelea kuwa mwanachama wao kuliko endapo wangemfukuza. Madiwani kumi tayari wamerudisha kadi na wanachama wengine 30,kupitia mitandao ya kijamii imeoneshwa watu wakichana chana kadi za ccm.

Lowasa ataendeleza mapambano akiwa ndani ya jahazi. Hakika litazama. Huu ni mwaka wa UKAWA kuchanga karata zao vizuri.

Mh Lowasa, nakutahadharisha, epuka mpango wowote wakutaka maridhiano na ccm, kwani mpango huo ni hatari kwa uhai wako.


Mpango mkakati huu wa lowasa ni hatari kwa ccm kuliko yote iliyowahi kutokea.

By Yericko Nyerere/JF

CHADEMA Kilichofanyika Monduli ni Unafiki Mkubwa Sana...Mlio Mwita Mwizi na Fisadi Sasa ni Dili Kwenu....

$
0
0
Mtume Mohammad (SAW) katika moja ya hadithi zake aliainisha tabia kuu tatu za mtu mnafiki.

Kwanza, mtu mnafiki akizungumza husema uongo.

Pili, mtu mnafiki akiahidi hatekelezi

Tatu, mtu mnafiki akiaminiwa hufanya hiyana.

Chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) kimetuonesha sifa hizi za mnafiki dhahiri kwenye sakata hili la kuwapokea kwa mbwembwe madiwani waliotoka CCM Monduli.

Madiwani hawa wametoka CCM kufuatia kukatwa jina kwa Waziri mkuu 'mstaafu' Edward Ngoyai Lowassa kwenye kinyang'anyiro cha kuwania kuteuliwa kugombea nafasi ya urais kwa kupitia CCM.

Kitendo cha kuwapokea madiwani hawa kwa mbwembwe tena huku pakitumika maneno kama "safari ya matumaini bado inaendelea" ni kitendo cha fedheha sana kwa chama.

Wakati Zitto Kabwe akiondoka/ akiondolewa CHADEMA tuliona wale walioamua kuondoka nae walivyoitwa kila jina baya mitandaoni na hata baadhi ya viongozi walijitokeza kuwakandia waziwazi.

Tumeona namna gani Edward Ngoyai Lowassa alivyotukanwa kila tusi na viongozi wa CHADEMA. Ameitwa mwizi, fisadi, , mnyang'anyi na majina mengine mengi. Na hata wafuasi wake 4u movement tuliona walivyopewa maneno mabaya humu.

Tumeona viongozi wa CHADEMA wakiponda tabia ya kupokea wanachama waliokimbia vyama kwa sababu ya migogoro ya kimaslahi mara kwa mara.

Kwa hayo machache najiuliza hivi yale maneno ya kuponda watu yalijitokeza sababu walihama CHADEMA? Kumbe kuhama ni kosa lakini kuhamia ni sahihi? Kumbe hawa wafuasi wa Lowassa walikuwa wachafu walipokuwa CCM lakini wakiwa CHADEMA ni wasafi? Hivi mtu akija CHADEMA anasamehewa dhambi??

Tabia ya kuyarudi maneno yenu imekuwa ya kawaida sana lakini kwa hili sasa mmejifedhehesha sana. Miaka michache iliyopita mliwaita CUF kila jina baya mara CCM B, mara vibaraka, mara mas**ga nk lakini baada ya muda mkaungana nao na kuunda UKAWA. Mlimfukuza Kafulila kwa mbwembwe lakini leo mpo nae UKAWA huku mkimsifu.
Sitashangaa kesho mkiungana na ACT ili tu mtimize malengo yenu.

CHADEMA tambueni mlichokifanya ni kitendo cha hovyo mno, mmewaonesha watanzania mlivyo walaghai na opportunist wakubwa. Mmeonesha kila tabia za kinafiki na kizandiki na msivyo na msimamo.

Tabia kama hizi zitawafanya ikulu muisikie redioni tu na kuishia kulalamika kwamba mnaibiwa kura kumbe mnajihujumu wenyewe.

Baada ya Ushindi wa Tuzo, Diamond Atupa Dongo kwa Jokate, Jokate Naye Ajibu

$
0
0
~~Usiku wa jana kuamkia leo July 19 2015 Diamond Platnumz kanyanyua ushindi mwingine kwenye Tuzo za MTVMAMA2015, zilizokuwa zikitolewa Durban Africa Kusini.

Leo Diamond alipost Video inayomwonesha staa wa Mitindo Bongo, mrembo Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ akicheza wimbo wa ‘Mdogomdogo‘ alafu akaandikia hivi >>>> ‘Mbona Bado, Mtanyooka tu..‘ >>>> @ diamondplatnumz

Baadae Jokate nae akaandika kwenye ukurasa wake wa @Instagram kuhusu video hiyo ambayo alimpost Diamond:

Tuki-support mtu ndio kama hivi matokeo yake mtu anatumia baadae kukudhalilisha. Hii video aliyo-post kwanza ni TBT kama sijakosea mwaka jana mwishoni nilikuwa sehemu na my friends @bikira_wa_kisukumaakani-record na kumtumia@diamondplatnumz bila mimi kujua. Kiukweli sijui kwanini walifanya hivyo. Nikaja kujua baadae sana na nikaona sio big deal cause kila mtu anapenda mziki na sio dhambi kucheza mziki wowote uupendao.

Ila kitendo cha@diamondplatnumz kwenda kuitafuta huko ilikokuwa hii video clip na kui-post leo najiuliza maswali mengi
1, anataka ionekana kama nilikuwa nashangilia ushindi wake? Which is not bad hakuna ubaya hapo kama unaamini ushindi wake ni sifa kwa taifa ila
2, Kwanini a-post na caption ya Na Bado Mtanyooka? Ili amkomoe nani? Au kwasababu niko karibu saaana na @alikibaofficialanatafuta kutuchonganisha? Ili iweje? Mimi I believe life goes on na kila mtu ana uhuru wa kumpenda au kuwa karibu na yule apendaye na kum-support ndio maana hata mimi nimekuacha na your new life
3, Pengine ni kweli anaendeleza zile hulka zake za kudhalilisha wanaweke aliokuwa nao waonekane sio kitu just because hawako na diamond platnumz chibu dangote. Which to me is just dead wrong.

@diamondplatnumz hizi sio tabia tunazozitegemea kwa mtu anayejisema anakomboa mziki wa Tanzania sio kwa kuweka visasi na fitna zako wazi wazi hivi. Unatu fanya tukose imani nawewe zaidi na tunaogopa ku-support cause hukawi kutugeuka.

Kuwa tofauti basi, onyesha mfano kwamba kweli hupendi beef unapenda mziki wa Tanzania uendelee ila kwa ulichoki-post unaonyesha wazi UNA visirani na hutaki mema unatafuta drama, kiki, vurugu unataka kila siku uwe wewe tu ambazo kiukweli mimi binafsi siziwezi utaendelea kushinda wewe tu katika hilo na sitashindana nawewe katika hilo kwasababu siwezi nawewe unajua kama ulivyoniimba mimi mpole, sinaga maneno ( ila kwenye kazi ndio nakuwa mkali kama pilipili ). Ila ungetumia busara kidogo.

Just move ON kiroho safi. Naomba pia nitumie fursa hii kukupongeza kwa tuzo yako ya MTV ila@babutale hata wewe ndugu yangu? Is this how tunaendeleza so called uzalendo?

Inshallah Kheri lakini yote maisha wanyonge sisi iko siku Mungu atatunyanyua.

Did You Know This About CORAZON KWAMBOKA? She Has Been Hiding it From Men

$
0
0

Corazon Kwamboka has finally revealed that she has been struggling with acne just like Avril. Corazon says that she has visited several dermatologists with no permanent solution but she is now using a new product which she hopes will work for her skin.

Here is what she wrote;



What If You Were UHURU And This “Secret Lover” From Tanzania Tells You This?

$
0
0

Aging Tanzanian singer, Rehema Chalamila, who is popularly known as, Ray C, has confessed that she has had a crush on President Uhuru Kenyatta for so long.

While laying her sentiments on social media, the mellow voiced singer claimed  that she has been holding her secret back for long but it’s high time she let the world know about it.

“Lemme tell you a lil secret about Uhuru!!! I love this guy to death! I have had a crush on him for soooo long!!! ” She said.

Ray C further confessed that everything about our President is awesome and no woman can resist him.

“I love everything about him. His accent, his attitude. Total package” the singer added.

Ray C’s confession comes just a few weeks after she listed crazy demands any man who wants to marry her must meet. Among those demands includes, sharing the shame phone and ability to cook for her when she is tired.

The aging singer is yet to find a husband despite her popularity.

BIKIRA WA KISUKUMA Ampigia Magoti JOKATE na Kumuomba Msamaha Baada ya Video Aliyomrekodi Akicheza Wimbo wa Diamond Kuzua Utata leo...

$
0
0
Hata siku Haijaisha toka Diamond Platnumz Apate Tuzo ya MTV Mama, Mchana wa leo Ametibua Mashabiki wake Baada ya Kupost Video ya Mpenzi wake wa Zamani Joketi Akicheza Moja ya Nyimbo zake huku akiandika caption ya Maneno haya'Mbona Bado, Mtanyooka tu"

Video Hiyo inasemekana ilirekodiwa na Bikira wa Kisukuma Aka Seth miezi sita iliyopita na leo Diamond kaipost kama Dongo kwa Jokate ambae siku za karibuni ameonyesha Kumsupport Ali Kiba...

Seth Ameingia Mtandaoni na Kuandika Haya:

Bikira_wa_kisukuma - IAM DEEPLY SORRY!Kama rafiki yako,sikujua yatakuja kuwa hivi...Tulirekodi Video hii tukiwa tunaenjoy NEWS CAFE zaidi ya MIEZI 6 iliyopita na haikuwa na madhara na nilipenda ulipopigwa wimbo huu na wewe ukaanza kuucheza and I liked it kwamba u still support ur Ex Music na sio maadui..A good thing!
Leo imeleta matatizo na kukusababishia maumivu ya moyo...Haikuwa dhamira yangu na Unajua na hata tulipoongea tulicheka na kufurahi na tulitaniana kuhusu Video ile.. I hope Diamond hakuwa na nia mbaya kiivyo kuiweka kwa sababu inaonyesha ulikuwa unacheza wimbo wake which means u love his music na unamsapoti...Pengine Diamond alipaswa kutumia maneno mazuri zaidi kuhusu Video ile instead of what he wrote kwa sababu imeonekana kama ni uchonganishi wakati bottom line haiko hivyo... Again JOKATE mpenzi,Iam sorry!

USHAURI WANGU KWA DIAMOND:
Jaribu kuepuka Misunderstanding zisizo za lazima,haikuwa na sababu kulikoroga kiasi hiki especially kwa muda huu ambao tulipaswa kama Watanzania kushangilia Ushindi wako..This was very Unnecessary especially kwa muda huu ambao Mashabiki waliokuwa wamegawanyika wameanza kurudi pamoja kama WATANZANIA...Ulipaswa kutumia moment hii kama GUNDI...From my heart IAM DEEPLY SORRY!

Kwanini Diamond Alishinda: Tofauti za Wazi na za Msingi Kati ya KTMA na MTV Awards!

$
0
0

Maoni Huru Kutoka Kwa Ndau Anaitwa  Matumbo Huko Jamii Forums
Jisomee Mwenyewe Hapa Chini:



Toafauti ya kwanza kabisa, inayotofautisha kati ya KTMA na MTV Awards ni kwamba, kwa KTMA, msanii ana uwezo wa kutoka na kontena moja la tuzo peke yake na kwa wakati mmoja wakati kwa MTV ni ndoto kufanya hivyo! Hadi sasa, msaniii anayeongoza kutoka na kontena la tuzo za KTMA kwa wakati mmoja ni Diamond Plutnumz ambae aliibuka na tuzo 7 kisha wanafuatia Ali Kiba na 20% ambao kila mmoja amepata kuibuka na tuzo 5.

Ukweli huo hapo juu unatokana na tofauti za kimsingi zinazounda Tuzo za KTMA na MTV ambazo ni:
>>>Wakati MTV Awards inakutanisha wanamuziki MAHIRI kutoka majiji makubwa kabisa barani Afrika kama vile Dar es salaam, Nairobi, Lagos, Johannesburg, Cape Town, Accra, Kinshasa n.k, KTMA kwa kiasi kikubwa inakutanisha wasanii kutoka kaeneo kadogo tu duniani kanakoitwa Wilaya ya Kinondoni!
>>>Tofauti na MTV Awards, pia MC wa KTMA most likely atatoka wilaya ya Kinondoni, wakabidhi tuzo watatoka huko huko, venue, wilaya ya Kinondoni… tumeenda mbali sana, Wilaya ya Ilala! Majority ya watakaopita Red Carpet-- wilaya ya Kinondoni, watakaokuja kuburudisha, majority watatoka wilaya ya Kinondoni and, to cut story short, almost everything, for KTMA kitakuwa ni Wilaya ya Kinondoni!
>>>Wakati host mkubwa wa KTMA ni wilaya ya Kinondoni na kidogo Ilala na hivyo kuzifanya tuzo za KTMA kuwa ni tuzo za WA HAPA HAPA, hosts wa MTV Africa Awards wanakuwa nchi mbalimbali!! Hawa WA HAPA HAPA wasubirie host city awe Dar es salaam ndipo labda waje kuambua kama ambavyo Wakenya walipata kuzizoa mwaka 2009 baada ya Host City kuwa Nairobi!!!
>>>Wakati kwenda kwenye tuzo za MTV, majority ya wasanii watatakiwa kuchukua air flight, kwa KTMA, in fact, hata kupanda gari ni mbwembwe coz’ majority ya wasanii wana uwezo wa kufika kwenye venue hata kwa Bajaj simply because Tuzo zenyewe zinakutanisha WA HAPA HAPA!!!
>>>Wakati MTV Awards inakutanisha wasanii wanaofanya kazi zao kwa lugha mbalimbali za kimataifa kama vile Kiingereza, Kifaransa, Kireno n.k, KTMA, kwa kiasi kikubwa, inakutanisha Wamatumbi peke yao, kwa maana ya watumiaji wa Lugha ya Kiswahili kwa kuwa ni tuzo za WA HAPA HAPA!

Dah! Tofauti zipo nyingi sema wakati ukuta! Je, ewe mwenzangu unaweza kutaja tofauti zingine za WAZI (sio za KIUFUNDI) kati ya MTV Awards na Kinondoni Tanzania Music Awards?

Hata hivyo, kabla sijakusanya kila kilicho changu na kusepa wacha niseme jambo moja! Nimeona watu hapa eti wanaponda Tuzo ya Best Live ACT na kufananisha na suala la kukata mauno! Short and clear, ukitoa hiyo hoja mbele ya watu wanaoifahamu tasnia ya muziki moja kwa moja watakauona muziki huufahamu! Ingekuwa Live Act ni kukata mauno basi hizo tuzo kila mwaka, sio Afrika tu bali hata duaniani zingeenda DRC!!

Biashara ya muziki duniani imebadilika sana, mauzo ya CDs sio deal tena kwa wasanii! Africa ambako hata masuala ya hati miliki ni hovyo, ukiacha endorsement wasanii wanategemea zaidi performance jukwaani na kupitia hili eneo, ndipo pekee msanii kwa kiasi kikubwa anaweza kuwa na uwezo wa kuuza kazi au bidhaa zake zingine inculding hizo CD kwa kuwa fans wako wanakuwa wamekusanyika sehemu moja kuliko kuwataraji kwamba wataenda dukani kununua CDs zako au nguo zako!! Live Act ni eneo lenye faida na mzunguko mkubwa wa pesa pengine kuliko eneo lingine kwenye biashara ya muziki na ndio maana, leo hii tukiambiwa mathalani Lady Gaga anakuja Dar, basi Dar mzima itakuwa full vurugu; kuanzia promotions kwenye medias, maandalizi ya venue, deals za kuuza ticket, kampuni kubwa kutaka kudhamini na kadhalika bila kusahau mzunguko wa pesa utakaotokea kwa wauza vinywaji na chakula!! Huko kote, ni mzunguko wa pesa … watu watapanda magari kutoka hata Mwanza kuja Dar es salaam only for Live Act! Kwahiyo ni kichekesho mtu akisema this’s all about kukata mauno! Mauno yanakatwa kitandani, jukwaani is all about performance, nyie watu wa wapi!!!

In short, kwenye Best Live Act wanaangalia pamoja na mambo yafuatayo:
>>>ENERGY: Kuwa Mkata Mauno Bora kuliko wote duniani lakini kama hauna ENERGY, pisha wenye pumzi wafanye kazi yao!
>>>CROWD ENGAGEMENT: Kuwa na pumzi za kutosha lakini ikiwa hauna uwezo wa kushirikisha crowd na kuleta shangwe kwenye show, please, pack and go because you’re not BEST LIVE ACT
>>>BEST MUSIC: Huwezi kuwa na muziki wa hovyo halafu ukaota kuwa Best Live Act unless kama ni kwenye hizi tuzo za WA HAPA HAPA!! Huwezi kuwa na crowd engagement or crowd feedback wakati muziki wako ni mbovu unless kama ni kwenye hizi tuzo za WA HAPA HAPA! ​

Halafu mwambieni jamaa, haya mambo mi natembelea kwenye akaunti yake halafu ananiambia nisiue tembo wakati hata Mikumi sijawahi kufika isn't fair at all... huu ni uonezi wa wazi wazi! Yaani mie nimetulia zangu tuli na ka-Techno kangu halafu unaniambia nisiue tembo?

Benard Membe Atangaza Kuachana Na Siasa.......Asema Hatagombea Wadhifa Wowote Mwaka Huu

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na  ushirikiano wa kimataifa, Bernard Membe, amesema hatogombea wadhifa wowote kwenye uchaguzi mkuu wa  mwaka huu na kwamba anapanga kujishughulisha na masuala yake ya kibinafsi.

Membe ambaye alikuwa akitafuta tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ili kuwania urais mwezi Oktoba lakini akashindwa kufikia lengo hilo, amesema kuwa, hatotafuta nafasi ya ubunge katika jimbo lake la Mtama.

Hata hivyo amesema ataendelea kukiunga mkono chama chake cha CCM na atampigia debe mgombea urais aliyeteuliwa na chama hicho, Bw. John Magufuli.

Awali kulikuwa na tetesi kwamba Membe angegombea ubunge baada ya kukosa nafasi ya kuwania urais kwa tiketi ya CCM.

Huku hayo yakijiri, chama cha Mapinduzi  (CCM) kinaendelea kupata pigo baada ya baadhi ya wabunge wake kutangaza kuwa hawatogombea tena nafasi zao kupitia chama hicho kwenye uchaguzi mkuu ujao.

Tayari madiwani 20 wa CCM katika jimbo la Monduli wametangaza kuhamia Chadema na kumtaka mbunge wao, Edward Lowassa kufuata mkondo huo.

Lulu Michael Ni Demu FEKI na Tapeli

$
0
0
Staa wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amedai kwamba yeye ni ‘demu feki’ tena mwenye tabia za kitapeli huku kauli yake hiyo ikiacha baadhi ya watu midomo wazi na kutaka kujua kulikoni.

Akizungumza na mtandao huu, Lulu amesema kuwa ni kweli yeye ni demu feki lakini kama watu wanataka kujua kwa nini yeye ni feki na ana tabia za kitapeli wasubiri kujua kwa nini ameamua kujiita hivyo.

“Kama mtu anataka kujua ufeki wangu anisikilizie maana kuna kitu nimefanya kitathibitisha hilo,” alisema Lulu

Video: Baada ya ushindi wa Tuzo za MTV, Davido athibitisha ujio wa collabo mpya na Diamond mwezi ujao

$
0
0
Baada ya wote wawili kuibuka washindi kwenye tuzo za MTV MAMA 2015 zilizotolewa Jumamosi iliyopita Durban, Afrika Kusini, Davido na Diamond wameweka wazi ujio wa collabo yao mpya.

Wakiwa na furaha huku wakiwa wamebeba tuzo zao mikononi mara baada ya tukio la utolewaji tuzo hizo kuisha, staa wa Nigeria Davido akiwa na Diamond ametoa ahadi ya collabo yao mpya.

Katika kipande cha video (hapo chini) Davido ametamka kwa kinywa chake:

“New F*ckin Diamond and Davido we gonna dropin next month, we do this f*ckn East Africa West Africa biggest artist we do this…we are uniting…” Wakati Davido akiyaongea hayo, Diamond alikua akiitikia “I’m telling you”.

Diamond aliibuka mshindi wa tuzo ya ‘Best Live Act’ na Davido naye aliibuka mshindi wa tuzo kubwa ya Best male ambayo pia alishinda mwaka jana.

CUF Yasema CCM Ilimuonea Edward Lowassa.......Yasema Ipo Tayari Kumpokea Kwa Kuwa Ni Mtu Safi, Asiye Na Doa lolote

$
0
0
Chama  cha Wananchi (CUF), kimeibuka na kumtetea aliyekuwa Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa (pichani juu), kwamba Chama Cha Mapinduzi (CCM), kilimuonea kwa kukata jina katika ngazi ya Kamati ya Maadili na kushindwa kulifikisha  Kamati Kuu ya CCM (CC).

Lowassa alikatwa jina lake akiwa ni miongoni mwa wagombea 38 wa urais kupitia CCM, lakini inadaiwa kwamba aliondolewa katika hatua za awali kwenye Kamati ya Maadili.

Kadhalika, CUF kimesema kipo tayari kumpokea Lowassa ndani ya chama hicho kwa kuwa ni msafi na hajawahi kufikishwa hata mahakamani kwa ajili ya kushitakiwa kutokana na madai ya rushwa.

Kauli hiyo ilitolewa jana na Kaimu Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa CUF, Abdul Kambaya, alipokuwa akizungumza katika kipindi cha Pilikapilika za uchaguzi nchini kinachorushwa na kituo cha Televisheni cha Star Tv.

Kambaya alirejea ripoti ya Kamati teule ya Bunge iliyoongozwa na Dk. Harrison Mwakyembe mwaka 2008 kuchunguza kashfa ya Richmond ambayo ilimng'oa Lowassa katika nafasi ya Waziri Mkuu.

Alisema katika kamati hiyo, Dk. Mwakyembe aliweka bayana kwamba kila mtu aliyehusishwa ama kutajwa katika kashfa ya Richmond angefikishwa mahakamani kujibu mashtaka.

Kambaya alisema mpaka sasa Lowassa hajawahi kufikishwa mahali popote kushitakiwa na kwamba hatua hiyo inaoonyesha kwamba kiongozi huyo hakuwa na kashfa yoyote.

Alisema lengo la CUF ni kuing'oa CCM na kwamba ukiona kuna mtu mwenye uwezo mkubwa wa kuitikisa chama hicho na kukipasua wapo tayari kumkaribisha ili washirikiane naye.

Alifafanua kuwa mtu ambaye siyo msafi hawezi kukaribishwa CUF na kwamba Lowassa kama angekuwa mchafu angekuwa ameshitakiwa mahakamani tangu alipojiuzuru mwaka 2008. Katika mjadala huo washirki walijadili matumizi makubwa ya fedha yaliyojionyesha ndani ya CCM tangu mchakato wa kuelekea Uchaguzi Mkuu ulipoanza.

Watu wengine waliojitokeza kumtetea Lowassa ni pamoja mwanachama mwenye kadi namba nane ya CCM, Kingunge Ngombale Mwiru, ambaye alitamka wazi kwamba kanuni na sheria ndani ya chama zilikiukwa.

Kingunge alisema haki haikutendeka kwa sababu Kamati ya Maadili kwa mujibu wa kanuni na taratibu za CCM haina mamlaka ya kukata jina la mgombea kwa sababu siyo kikao cha maamuzi. Wakati hayo yakisemwa, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye amewaonya watu wanaokisema vibaya chama hicho na kwamba kitawachukulia hatua.

TETESI:Lowassa Aandaa Waraka Kumchanachana Kikwete, Kisha Kutimkia Ng'ambo...

$
0
0
Hatimaye mbunge wa Monduli Edward Lowassa kesho atatoa waraka mzito utakaoelezea namna ambavyo alifanyiwa kile alichokiita 'hila' na rais Kikwete.

Waraka huo unatarajiwa kulitikisa taifa na huenda ukaigawa vibaya CCM.

Baada ya waraka huo pia Edward Lowassa anatarajiwa kutoa rasmi hatima yake kisiasa huku kila dalili ikionyesha kuwa ataisambaratisha vibaya CCM kutokana na maamuzi atakayochukua.

=======
UPDATES:

- Miongoni mwa mambo mazito yaliyo kwenye waraka huo ni hatua ya Edward Lowassa kumuunga mkono Dr. Willbrod Slaa kama mgombea urais anayekubalika na wengi baada ya yyeye kuenguliwa.

- Pia kuna dalili (ingawa siyo za wazi na zimetawaliwa na giza nene kwamba huenda Lowassa atatangaza rasmi kuhamia Chadema ingawa hatagombea urais).

- Taarifa nyingine zinabainisha kuwa EL baada ya kubwaga manyanga, atatimkia ng'ambo wakati CHADEMA wakimwandalia mapokezi "mazito"

By G Sam

Magufuli Anatumia Ndege ya Serikali Kufanya Kampeni...Vyama vya Upinzani Vyaja Juu.....

$
0
0
Wanasiasa wa upinzani nchini wamepinga kitendo cha
Mgombea urais wa CCM, Dk John Magufuli kutumia
ndege ya Serikali kwenye shughuli za kichama za
kujitambulisha wakisema hatua hiyo ni matumizi mabaya
ya rasilimali za Taifa. Hata hivyo, Katibu wa Itikadi na
Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alisema walifuata taratibu
zote kuikodi ndege hiyo na kwamba chama chake ni
kikubwa na hakiwezi kushindwa kukodi usafiri huo.
Source: Mwananchi

Breaking News: Majambazi Walioua Polisi na Raia Kituo cha Polisi Stakishari Wakamatwa

$
0
0
Polisi Jijini Dar es Salaam wamesema wamewakamata watu watano waliohusika na tukio la ujambazi katika Kituo cha Stakishari, pia silaha kadhaa zimekamatwa.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, ameapa kwamba Jeshi hilo litawakamata wale waote waliohusika na tukio hilo, pia amesema kama wapo watu waliohusika na tukio hilo wajisalimishe.

Silaha zilizopatikana ni SMG 7, Sar, 7, Risasi 28 za SMG zote za Kituo cha Polisi Stakishari, Pia wamekamata sanduku lenye fedha za Kitanzania milioni 170.

Nampa Kila Anachostahili Mke Wangu Lakini Sina Amani na Ndoa yangu....

$
0
0
Mke wangu nampenda sana kila anachotaka nampa. Yeye ni mwalimu wa msingi. Uwezo wangu wa kifedha si mkubwa lakini nimejitahidi hadi nimemnunulia walau kigari cha kuendea kazini katika jitihada za kumfanya nae ajisikie vizuri mbele za watu.

Mshahara wake ni chini ya laki 5 lakini huwa namwekea mafuta ya shilingi laki 3 kwa mwezi ili aende kazini. Nampa matunzo yote anayotaka kama mke wa ndoa anavyostahili.

Kinachonisikitisha ni dharau anazonionyesha ndani ya nyumba. Akiamua kunitukana inachukua siku tatu kumaliza matusi. Nyumba haina amani naishi kama mhamiaji haramu. Kuna wakati ananiangalia tu na kunisonya bila kumkosea chochote.

Anadai nikisafiri anaishi kwa amani nikirudi anakereka. Kwa kifupi mimi huwa ni mara chache huwa najibizana nae ninapozidiwa na hasira lakini mara nyingi hukaa kimya.

Nimejaribu kujiuliza ni wapi nakosea sipati jibu. Natunza familia vizuri, unyumba nampa, sina vimada na wala hajawahi kunihisi.

Tatizo ni nini? Nisaidieni wadau niishije na huyu mke? Akiugua anajitahidi kuonyesha jamii kuwa simjali anaamka mapemaa anawahi hospitali ili nionekane simjali.

Akiamua kunitukana anatumia matusi na kashfa nzito dhidi yangu. Bado sijamsimulia mtu yeyote kwa ajili ya kulinda heshima ya familia lakini naona kama nazidiwa.

Naombeni ushauri wenu.

Diamond Platnumz Adai Jokate ni Mnafiki Sana...Ananipongeza Leo Baada ya Kushinda Wakati wa Kupiga Kura Hakuwa na Habari Nami wala Kunipost...

$
0
0
Diamond Platnumz Akiojiwa na Clouds FM kuhusu Video aliyopost jana ikionyesha Jokate Akicheza Wimbo wake na Kuandika "Mbona Bado, Mtanyooka tu".Amesema kuwa yeye amempost kwa nia nzuri tu na si kumzalilisha amedai yeye mara nyingi huwa anawapost watu wakicheza nyimbo zake hivyo kumpost Jokate kwake ni Kawaida...
Pia ameulizwa kuhusu maneno aliyotumia kwenye video hiyo kuwa ni ya kichokozi Diamond akadai kuwa yeye ni Mswahili wa Tandele kuandika Maneno haya ni kawaida kwake kwani amekuwa akiyatumia katika post zake mbali mbali....lakini leo ametumia kwa Jokate basi watu wengine wamepanic.....

Mwisho Diamond Akafunguka ya Moyoni kuhusu Jokate na Kusema kuwa si mzalendo kwa vile anajidai kumpongeza leo baada ya kushinda wakati kabla ya kushinda yeye na wenzake walikuwa Bize wakishawishi watu wampigie kura Davido...Amedai hata siku moja hakuwahi kumposti  kwa page zake kumpa sapoti hivyo asijadai leo kulia lia....

‘’Nikasikia kuwa kasema kuwa ndiyo maana wanaogopa kusapoti wasanii wa Tanzania kwa sababu wakisapoti wanadhalilishwa yeye mpaka naenda kuchukua tuzo ya Mtumbuizaji Bora yeye amenisapoti nini hajawahi kunipost hata tuzo moja sasa hivi ndiyo anajishaua eti ananipa hongera kwa tuzo ningemuona wa maana angepost watu wapige kura na kuwahamasisha ili ushindi urudi nyumbani lakini kwa chuki alizojazwa pasipo na sababu na roho mbaya aliyowekwa na watu imemfanya ashindwe kunipost na kutengeneza chiki za chinichini wakidhani wakiwapigia kura Wanageria mimi nitakosa tuzo Mungu amewalaani mimi nimeshinda halafu anajifanya anatoa hongera eti wanasapoti muziki wa Tanzania au kwasababu wameona tuzo imekuja ndiyo wanajifanya wanatoa hongera tuache unafiki,’’alimalizia Diamond.

Shamsa amsapoti Nay Wa Mitego kui’push’ ngoma yake mpya ya ‘Sina Muda’.

$
0
0
Mwigizaji wa filamu za Kibongo,Shamsa Ford ambaye amekuwa akidaiwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Staa wa Bongo Fleva,Nay Wa Mitego amemsapoti msanii huyo kwa kuongozana naye kwenye vituo mbalimbali vya redio na tv ikiwemo Clouds TV na kufanya mahojiano pamoja na kuipush ngoma yake mpya iitwayo Sina Muda.

Akizungumza na Clouds FM,Nay alisema kuwa wamekuwa wakiongozana na Shamsa kwenye vituo mbalimbali vya redio na TV ili kuipa nguvu zaidi na kuitangaza ngoma yake mpya kwa kuwa ni rafiki yake na amekuwa akimsapoti kwenye mambo mengi zaidi ya muziki wake.

‘’Shamsa ni rafiki yangu na amekuwa akinisapoti kwenye mambo mengi tu zaidi ya muziki wangu ndiyo maana nimekuwa nikiongozana naye kwenye vituo mbalimbali vya TV na redio kwa ajili ya mahojiano na kuitangaza zaidi ngoma yangu mpya ya Sina Muda,’’alisema Nay.

Hata hivyo Nay alisema kuwa ngoma yake hiyo mpya hakuitegemea kama itafanya vizuri kwa kuwa aliichukulia poa na hakuipa nguvu sana lakini ilivyopokewa vizuri na mashabiki ndiyo maana ameona aipe nguvu zaidi kwa kuitangaza kwenye vituo vya redio naTV.

‘’Unajua sikutegemea kama hii ngoma itapokelewa vizuri niichukulia poa tu lakini illivyopokelewa vizuri na mashabiki nimeona bora niipe haki yake nitumie nguvu zaidi kuitangaza nikiwa na binamu yangu Shamsa,’’alisema Nay.

Hizi ndio silaha na vitu vilivyokamatwa na Polisi vikihusishwa na uvamizi wa Kituo cha Polisi Stakishari.. (Picha)

$
0
0
Imetufikia ripoti kutoka Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Dar kuhusu idadi ya watu waliokamatwa na wanahojiwa na Jeshi la Polisi wakihusishwa na tukio la uvamizi wa Kituo cha Polisi cha Stakishari, Dar.
DSCI0033
Helmet za pikipiki pamoja na bunduki.
Kingine ni kwamba watu hao wamekutwa na vitu mbalimbali… Vitu vyote vilivyopatikana vimekutwa na Polisi eneo la Mkuranga vikiwa vimefichwa ndani ya shimo.
Tayari nimepata picha kutoka Makao Makuu ya Polisi Dar es Salaam, silaha zilizopatikana zimeoneshwa hapa.. kulikokutwa hizo silaha kumekutwa na vitu vingine pia, ikiwemo pesa Milioni 170.
DSCI0042
Kamanda wa Polisi, Suleiman Kova.
DSCI0045
Kamanda Kova akionesha moja ya silaha zilizopatikana.
DSCI0052
DSCI0055
DSCI0059
DSCI0066
Hizi ni sehemu ya pesa zilizokamatwa ambazo jumla yake ni Milioni 170.
DSCI0080
Hapa kuna picha na majina ya watu ambao bado wanatafutwa na Polisi.
DSCI0085
Kati ya watu waliokamatwa wapo ambao walikutwa na hizi pikipiki ambazo zilitumika kwenye tukio la uvamizi.
DSCI0091
Kazi imeanza, sasahivi Vituo vya Polisi vitakuwa na CCTV camera kwa ajili ya Usalama.
DSCI0092
Camera tayari zimeanza kufungwa, hapa ni Makao Makuu ya Polisi Dar.
DSCI0095
Kamanda wa Polisi, Simon Silo ndio anayeongoza Oparesheni ya kusaka watuhumiwa wa tukio la uvamizi Kituo cha Polisi.
Source:Millard Ayo
Viewing all 104809 articles
Browse latest View live




Latest Images