Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104799 articles
Browse latest View live

Joshua Nasssari Achaguliwa tena Kupeperusha Bendela ya CHADEMA Jimbo la Arumeru Mashariki

$
0
0
Aliekuwa Mbunge wa Arumeru Mashariki mkoani Arusha,Joshua Nassari akizungumza namna alivyotekeleza ahadi zake katika kipindi kilichopita wakati wa mkutano Mkuu wa Jimbo uliofanyika kwenye Mji mdogo wa Usa River ambapo  alichaguliwa bila kupingwa ili kupeperusha bendera ya Chadema katika uchaguzi utakaofanyika Oktoba mwaka huu.


Wanachama wa Chadema wakipiga kura za maoni kwaajili ya kumchagua mgombea ubunge jimbo la Arumeru Mashariki katika Mji Mdogo wa Usa River,Joshua Nassari alipata kura 387  na kura 2 za hapana.


Wanachama wa Chadema wakifurahia jambo katika mkutano huo


Mwenyekiti wa Kanda ya Kaskazini ambaye alikua Mbunge wa Chadema jimbo la Karatu mkoa wa Arusha,Israel Natse(kulia)na Katibu wa Chadema mkoa wa Arusha,Kalist Lazaro wakimtambulisha mgombea ubunge wa jimbo la Arumeru Mashariki, Joshua Nassari(kati)baada ya kutangazwa mshindi.

WEMA SEPETU Aingiwa na Hofu Baada ya Jina la Edward Lowassa Kukatwa....Ahofia na yeye Kukatwa...

$
0
0
DU! Kazi kwelikweli! Habari ya mjini kwa sasa ni mtoto mzuri Bongo Movies, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ kuwania Ubunge wa Viti Maalum Mkoa wa Singida kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), lakini nyuma yake kuna habari zinazodai kuwa mrembo huyo ameingiwa na hofu ya kukatwa jina kama ilivyotokea kwa Mbunge wa Monduli, Edward Ngoyai Lowassa aliyekuwa mmoja wa watia nia ya kugombea urais, Amani lina mkanda kamili.


ALIVYOENGULIWA LOWASSA

Lowassa alikuwa miongoni mwa makada 33 kati ya 38 walioenguliwa na Kamati ya Maadili ambayo ilipitisha majina matano pekee katika kikao cha Kamati Kuu, Halmashauri Kuu na baadaye Mkutano Mkuu kupitisha Mbunge wa Chato, Dk. John Pombe Magufuli kuwa mgombea urais kwa Tiketi ya CCM.

TUJIUNGE NA CHANZO

Chanzo kilicho karibu na staa huyo kimepenyeza ‘ubuyu’ kuwa, Wema ambaye anashikilia Taji la Miss Tanzania 2006/07, ameingiwa na hofu hiyo baada ya kuona Lowassa ambaye ana sifa ya kukubalika kama alivyo yeye ameenguliwa na kikao cha Kamati ya Maadili ya CCM.

“Bibie (Wema) anajiamini, anakubalika kweli lakini kitendo cha Lowassa ambaye alikuwa anaonekana kukubalika kimemtia hofu na kuona kumbe kukubalika pekee si silaha ya ‘kuwini’ kupitishwa na chama,” kilisema chanzo hicho.

CHANZO CHAZIDI KUTIRIRIKA

Chanzo hicho kilizidi kwenda mbali zaidi kwa kudai hofu hiyo iliongezeka kwa Madam hususan baada ya kusambaa kwa kuwepo kwa watu wasiompenda kupandikiza chuki kwamba baadhi ya skendo zilizomgusa zinaweza kumpotezea sifa ya jina lake kupitishwa na Halmashauri Kuu ya chama chake.

“Si unajua tena Madam kwenye maisha yake ya sanaa amepitia skendo za hapa na pale, hiyo inaweza kuchangia kumtia hofu maana wabaya wake wanaweza kuitumia kama silaha hivyo amekuwa akitoa chozi na kumuomba Mungu amfanikishe,” kilisema chanzo hicho.

SKENDO INACHANGIA KUMPOTEZEA SIFA?

Duru mbalimbali za habari zinaonesha kwamba kitu kikubwa kinachoangaliwa kwa kiongozi ni suala la uwajibikiaji na si tabia binafsi au skendo.

Wapo viongozi ambao walikuwa na skendo lakini wameweza kupitishwa na wananchi wao na kuwatumikia vizuri kuliko hata wale walionekana wasafi.

“Si kweli kwamba skendo ndiyo kigezo kikuu cha kumpitisha mgombea, mbona watu kama akina Mike Sonko (alikuwa Mbunge wa Kenya), marehemu Amina Chifupa (alikuwa Mbunge Viti Maalum, Vladimir Vladimirovic Putin (rais wa urusi) na wengine wengi, walikuwa au walipata skendo lakini walifanya vizuri katika uongozi wao,” alisema mwanaharakati mkubwa wa siasa nchini aliyeomba hifadhi ya jina.

NAPE ANENA

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alipoulizwa kama kuna uwezekano wa kumuengua mgombea yeyote kutokana na skendo au chuki zinazoezwa na baadhi ya wanachama wa chama hicho, alisema si kweli bali wao wanafUata taratibu na kanuni walizojiwekea na si vinginevyo.

“Sisi tuna kanuni na taratibu za chama, hiyo ndiyo misingi yetu. Hatumuengui mtu kwa chuki binafsi wala kitu kingine chochote zaidi ya kufuata kanuni zetu,” alisema Nape.

WEMA ANASEMAJE?

Akizungumza na mwanahabari wetu hivi karibuni, Wema alikiri kupata hofu hiyo kwa muda lakini ameshajiamini kutokana na kumuomba Mungu ambaye amekuwa akimtanguliza katika kila jambo analolifanya.

“Kusema kweli mtu unapotaka kufanya jambo unapaswa kujiamini, hata mimi mwanzo nilikuwa nimejipa matumaini ya hali ya juu kwamba Lowassa atapita, lakini bahati mbaya akakatwa, naamini Mungu yupo, mimi naswali usiku na mchana, Mungu atanisimamia katika hili,” alisema Wema.

MBUNGE Sugu Awakana Wasanii..Adai yeye Hakuwa Mbunge wa Wasanii bali wa Mbeya Mjini

$
0
0
Mbunge wa Mbeya Mjini na msanii wa muziki Joseph Mbilinyi, maarufu kama Mr. Sugu ameelezea kujivunia kipindi chake cha miaka 5 bungeni.

Mbunge wa Mbeya Mjini Mh. Joseph Mbilinyi aka Sugu
Hii imekuja baada ya lawama na fikra za wengine kuwa amekuwa na mchango mdogo tu katika kuipigania sanaa kwa nafasi aliyopata.
Mr. Sugu ameeleza hayo na kusisitiza kuwa, hakuwa mbunge wa wasanii bali mbunge wa Mbeya, akieleza kuwa, kama msanii hakuwa anajituma na kazi yake, ni lazima abakie kuwa mtu wa lawama mara zote.

Profesa Anna Tibaijuka Azomewa Tena Kwa Mara ya Pili Jimboni Mwake.......

$
0
0
Aliyekuwa Mbunge wa Muleba Kusini, Prof Anna Tibaijuka anayewania jimbo hilo kwa mara ya pili, jana alishushwa jukwaani kwa kuzomewa na wananchi wake katika kata ya Nshamba wilayani Muleba. Prof Tibaijuka alishushwa jana wakati wa kampeni za kura za maoni kupitia CCM. Hali ya kuzomewa ilidumu kwa dakika kadhaa jambo lililofanya Wagombea hao kulazimika kuondoka. Kwa mara ya kwanza alizomewa juni 8, wakati wa ziara ya katibu mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana katika kata hiyo hiyo. Akiwa na Kinana wananchi walimtuhumu ufisadi wa fedha za Escrow na kushindwa kutekeleza ahadi ya kuwajengea barabara ya lami.
Source: Mwananchi
Nini maoni yako kuhusu hilo?

Nyeti: Mbowe, Mdee na Lipumba Hawamtaki Slaa, ACT-Wazalendo Kutosimamisha Mgombea Lipumba Akisimama

$
0
0
Jana ilikuwa siku ya kwanza kati ya siku kumi za kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura kwa kutumia mfumo wa Biometric Voters Registry (BVR) katika jiji la Dar es Salaam.

Namshukuru Mungu tayari nina kadi yangu kwa ajili ya kuwapata viongozi wangu bora hapo 25 Oktoba mwaka huu.

Sikufaidi tu kupata hiyo hati, la hasha! Katika kubadilishana mawazo na wajiandikishaji wenzangu, nikabahatika kuongea na kiongozi wa chama cha Wananchi CUF ngazi ya kijiji.

Pamoja na mambo mengine nilivuna kutoka kwake msimamo wa CUF kwenye UKAWA,nani mgombea urais kupitia UKAWA na nani hakubaliki na kwanini.

Ambalo lilinivutia sana ni msimamo wa ACT kuhusu mgombea wa UKAWA atakayeteuliwa.

Kimsingi kiongozi huyo alinihakikishia kuwa CUF bado hawajajitoa kwenye UKAWA. Kuhusu mgombea ambaye viongozi wengi kutoka vyama vinavyounda UKAWA wanaona anafaa kupeperusha bendera ya UKAWA ni Prof. IBRAHIM HAROUNA LIPUMBA.

Lipumba anaungwa mkono na FREEMAN MBOWE na HALIMA MDEE kwa vigezo kuwa ana busara, ni mtu mwenye subira na staha na asiyekurupuka kufanya maamuzi.

Slaa anaelezwa kuwa mwenye jazba na visasi jambo ambalo kwenye kuunda serikali linaweza kuwagharimu.

Nilitaka kujua sababu za Mbowe kutomkubali Katibu wake Mkuu, Wilbroad Slaa kupeperusha bendera ya UKAWA.

Inasemekana kuna maandamano waliandaa yeye MBOWE na SLAA lakini mambo yalipoharibika, Slaa akamruka na akashtakiwa yeye jambo ambalo Mbowe aliona ni usaliti na anachokifanya sasa ni kulipiza kisasi. Kitendo cha Lowassa kutakiwa na Mbowe ndani ya CHADEMA huku SLAA hamtaki nayo ni sababu nyingine.

Chama cha Alliance for Change & Transparency ( ACT) kama chama cha Upinzani na ambacho bado ni kichanga kabisa kwa mujibu wa kiongozi huyo wa CUF kinasema endapo UKAWA watamsimamisha LIPUMBA kama mgombea urais wao ACT hawatamsimamisha mgombea na badala yake watamuunga mkono Lipumba vinginevyo watamsimamisha mgombea wao.

kwa mujibu wa kiongozi huyo, kuna uwezekano mkubwa wa CUF kujitoa UKAWA na kutengeneza muungano na ACT na kumuweka mgombea urais atakayepeperusha bendera ya vyana hivyo viwili.

Tusubiri tuone namna itakavyokuwa.

CNN Yawachokoza Wakenya kwa Kuiita nchi yao ‘Kitovu cha Ugaidi’, inakiona cha Mtema Kuni Kwenye Twitter!

$
0
0
#SomeOneTellCNN ni mada inayotrend nchini Kenya kwa sasa na hiyo ni baada ya CNN kutangaza na kuandika habari iliyowakera.

CNN imedai kuwa taarifa yake ya habari kuwa wasiwasi wa usalama unazidi kuwa mkubwa wakati Rais Barack Obama akijiandaa kwenda nchini humo ambako imesema ni ‘kitovu cha ugaidi.’
OBAMA’S TRIP RAISES SECURITY CONCERNS

“President Barack Obama is not just heading to his father’s homeland, but to a region that’s a hotbed of terror,” wameripoti CNN.

Taarifa hiyo imewaudhi wakenya wengi ambao wanaiona CNN kama kituo kinachoichafua nchi hiyo.

D’Banj amlalamikia Diamond kwa kumzungusha kufanya collabo, Platnumz atoa sababu za kumkwepa

$
0
0
Muimbaji mkubwa wa Nigeria, D’Banj amemlalamikia Diamond kwa kumzungusha kufanya naye collabo.

Kokomaster amesema kuwa toka walipokutana na Diamond walizungumza na kukubaliana kufanya collabo lakini amekuwa akimpiga chenga mpaka sasa.

Star huyo ambaye aliibuka na tuzo ya ‘MAMA Evolution’ katika MTV MAMA 2015, ameongeza kuwa kabla mwaka huu haujaisha anaamini collabo hiyo itakuwa tayari imefanyika.

Diamond ametoa sababu za kuchelewa kufanya collabo na D’Banj.

“Tulikutana kule kwenye Do Agric tukafanya Cocoa na Chocolate, tukatakiwa kufanya nyimbo ya mimi na yeye lakini nikaogopa ukianza na msanii mkubwa sana itakuwa kurudi tena itakuwa tabu lazima uanze kwa ngazi kwa ngazi kwa ngazi ili kesho na kesho kutwa ukitoa nyimbo uonekane unazidi kupanda, sio unafanya nyimbo na mkubwa halafu kesho unashuka, nafikiri ndio ikawa sababu pia nyimbo yangu ya kwanza sikuweza kufanya na yeye ya kwanza.” alisema Diamond kupitia 255 ya XXL ya Clouds Fm.

Afande Sele Amchana Sugu, Adai Hajafanya lolote Bungeni Kutetea Muziki, Sugu Ajibu

$
0
0
Rapper Afande Sele amesema wasanii hawajanufaika na ubunge wa Joseph Mbilinyi aka Sugu licha ya kumsaidia kumpigia kampeni katika uchaguzi uliopita.

Akizungumza na Planet Bongo ya East Afrika Radio, Afande alisema Sugu ameshindwa kuwatumikia wasanii na kujinufaisha yeye mwenyewe.

“Sisi tuliamini akienda kule ndio mdomo wetu, kasahau kabisa wasanii wenzake,” alisema. “Kipindi ambacho wasanii wa antivirus wanalalamika kwamba kawatosa porini, akasema yeye sio mbunge wa wasanii ni mbunge wa Mbeya. Huyu ni msaliti kwa wenzake, sasa mtu msaliti namna hii jinsi kumuondoa ni sisi kuamua kuingia bungeni wenyewe kupigania maslahi yetu,” aliongeza.

Baada ya kauli hiyo, Sugu amemjibu kwa kusema kuwa yeye hakuwa mbunge wa wasanii bali alikuwa mbunge kwaajili ya watu wake wa Mbeya mjini.

“Nafikiri hafuatilii bunge, unajua uzuri wa vitu vya bunge vinaenda kwa rekodi, labda atakuwa hafuatili bunge. Lakini kwa wanaofuatilia bunge wanajua. Mimi sio mbunge wa wasanii, mimi ni mbunge wa Mbeya mjini,” alisema Sugu.

“Kwahiyo chochote ninachokifanya bungeni ninakifanya kwa mapenzi yangu na pia kama waziri kivuli. Kwa msanii anayefanya kazi sawa ila kwa mtu anayelala lala kama yeye lazima atakufa njaa. Lazima utakufa njaa lakini kwa msanii kama Professor Jay, msanii kama Shetta wana- appreciate kazi ambayo tunaifanya bungeni kwa kauli zao.”

This is What RAY C Did in Her House That Has left MEN Salivating (VIDEO)

$
0
0

After confessing that she has always had a crush on President Uhuru Kenyatta for long, Tanzanian singer, Ray C, has decided to tempt “team mafisi” with her s3ductive dancing skills.

The aging singer decided to twerk vigorously in her house while dancing to a catchy African tune. Her crazy dancing skills have left men salivating and few can get enough of the s3xy moves.

Watch the action in the video below.

Why Would A LADY do This in The Gym? A Must Watch VIDEO for men.

$
0
0

Some ladies have perfected the skill of tempting men but this bootylicious lady has decided to take things to another level.

One even wonders whether she had gone to the gym for a work-out or to s3duce men.
Just click play and see what she did.


Duh! Shilole na Mziwanda Wametudanganya Kumbe ni Kiki tu

$
0
0
BAADA mikasa na vituko kibao vya kidume kuchezea kichapo na kuvumilia kitambo huku thamani ya uume ikidhalilishwa front, kijana Nuhu Mziwanda kabwaga mazima, ni Couple iliyounganishwa na yeye na mwanadada mwenye kesi kwa Pilato Basata kwa kumwaga radhi Ughaibu Shilole.

FC baada ya kupata mtonyo iliwaibukia artist hao wenye uwezo wa kuact kila kunapokucha katika kupata data kama ni sinema na wanaendelea na Movie yao mpya ya maisha kama walivyozoeleka? Lakini hii ni real mtu kambwaga mtu naye kaipokea safi.

“Mwanaume umjali mpenzi wake na kumfanyia kile atakacho, lakini si kwa huyu ni mwanamke asiyejua kupendwa na chochote nilichofanya ilikuwa kwa ajili ya upendo tu, nimemwacha na aje mwanaume mwingine naye ajaribu,”Mziwanda

Pia msanii huyo wa muziki amekanusha kuwa kuwepo kwake na mwenye jina la Zuwena Mohamed jina linalofunikwa na hili la ugali la Shilole kuwa hakuwa anamtegemea sana kama ni kwenda Uropa ilikuwa ni mialiko ya kila mmoja kwa dili lake.

FC ilimtafuta mdada makeke awapo kwa stage hadi kusaula viwalo na kuingia matatizoni na wenye mamlaka ya sanaa simu zake zote zilikuwa hazina majibu once mambo yanaendelea, FC imebaini kuwa hakuna watu kubwagana wala nini bali ni mchongo wa machizi hao kutafuta kiki wamepata.

Ilikuwa ngumu kwa wanaomjua Mziwanda eti akijitoe kirahisi hivyo kwa Shilole? Bali wamejipa majina yao ambayo Shilole anaitwa Asha ngedere na Mziwanda jina la Ganda la Ndizi utelezi mwanzo mwisho afanye nini kijana wa watu, maisha ndio yalivyo.

Kumbe walikuwa wanataka Kiki tu, kama Ulaya au wapi hiyo hizi Kiki bhana kuna siku mtu anamua hata Mshua ili mambo yaende. Danganya toto hiyo imebainika baada ya wimbo wao walioshirikiana wasanii hao kuachiwa katika moja ya Redio hivyo hiyo ni movie tu.

Kajala Afungukia Kuingia Kwenye Siasa

$
0
0
Staa wa sinema za Kibongo, Kajala Masanja ‘Kay’ amefungukia kuingia kwenye siasa kuwa ni bora abaki kwenye upenzi na chama fulani kwani hawezi kugombea.

Akizungumza na Amani juzikati, Kajala alisema kuwa, japokuwa wasanii wengi wakiwemo wa tasnia ya filamu Bongo, wamekuwa wakichukua fomu za kutaka kugombea nafasi mbalimbali za udiwani na ubunge lakini kwake hafikirii kitu kama hicho.

“Mimi siasa siiwezi kabisa, kifupi haipo kwenye damu ndiyo maana unaona wenzangu wote wamechukua fomu za kugombea mimi wala sijajitokeza kuchukua,” alisema Kajala.

Faiza Ally Afunguka Kuhusu Mavazi Yake, Mtoto, Dini, Umaarufu…..

$
0
0
Staa wa Bongo Movies, Faiza Ally  amefunguka mengi kuhusu yeye mwenyewe kwenye kipindi cha Nirvana kinachorushwa na EATV usiku wa jana.

Ishu kubwa ilikuwa kuhusu mavazi yake “Napenda kuvaa vitu ninavyovaa, sina mavazi special naweza kuvaa vyovyote, niliipenda idea ya kuvaa nepi (diapers) na sina tatizo nayo kabisa”

Faiza ni mama wa mtoto mmoja wa kike, kwenye upande wa malezi ikoje? “Mimi ni mama mzuri sana, ninamtazama mtoto wangu saa 24… mavazi yangu hayaingiliani kabisa na malezi ya mtoto wangu… namlea kwa mazingira ya heshima, heshima na nguo ni vitu tofauti… ninavaa mavazi ninayopenda na bado nina heshima kwa watu. Sio lazima kila mtu akubali ninachofanya, ninapofanya kitu kwa watu kukubali au kukataa ni matatizo yao”   Faiza Ally alieleza.

Kuna kitu chochote anachojutia kutokana na mavazi yake?  “Sina ninachojuta, niko sawa… tukio ambalo sijafurahia ni moja la kupelekwa Mahakamani na kunyang’anywa mtoto wangu kitu ambacho ninakifanyia kazi  na kinaenda vizuri.. sioni tukio  baya zaidi ya watu kunitukana na ni kawaida… ninaenjoy na ninapenda mavazi yangu” Faiza Alieleza.

Haya ndio maneno yake kuhusu nguo aliyoivaa kwenye KTMA 2015  “Idea ilikuwa ni nzuri mpaka pale ambapo nguo iliachana… lengo lilikuwa sio kuacha makalio wazi, ile nguo baada ya kukaa kwenye gari ilishuka na sehemu ya makalio ikabaki wazi… Wakati natoka nyumbani ilikuwa imekaa tu vizuri, nilivyoshuka kwenye gari sikujiangalia, nilipofika red carpet nikapigwa picha”

Anatoka kwenye familia inayofuata Dini?  “Baba yangu sijawahi kumwona anakwenda Msikitini, sio kwamba naikana dini lakini sijazaliwa kwenye familia ya kidini.. maisha yangu yako hivi miaka yote na hakuna kilichobadilika kwenye maisha yangu… nafurahia maisha yangu”

Huu ndio ushauri wake kwa wasichana kuhusu ishu ya fashion za mavazi  “Wasichana wajue kwamba kilicholeta gumzo ilikuwa bahati mbaya, ila wawe huru wavae vitu wanavyovifurahia ila isitokee kama ile… kuna mavazi navaa na kuna mavazi siwezi kuvaa”

Matukio ya mavazi yake yamempa umaarufu? Amepanga kufanya chochote? “Sijapanga chochote, sikujua kama itakuwa ni umaarufu… mimi ni mwigizaji na ninaandika kitabu, labda kwa kazi zangu hizo… kipande kilichoonekana sio maisha yangu yote, ni sehemu ya mwili… Faiza ni mwanamke mzuri, anayejielewa, mwenye akili timamu, mama bora, anayejipenda, mtu wa watu”   Faiza Ally.

Kwenye Interview hiyo alikuwepo pia mwanamitindo Ally Rehmtullah, haya  ndio maneno yake kuhusu nguo ya Faiza “Ubunifu wake ulikuwa mzuri labda mawasiliano kati ya yeye na mbunifu wake hayakuwa mazuri, vazi kama lile kwa utamaduni wetu lazima watu watashtuka watakusema, ni muhimu kujua yeye mwenyewe Faiza alikuwa anataka nini… Naamini ilikuwa bahati mbaya, ingekuwa ni mimi ile gauni nisingevaa”  Ally Rehmtullah

Abiria Mmoja Ndani ya Daladala Jijini Dar, Ameshambulia Abiria Wengine kwa Kisu Bila Sababu Yoyote..Wananchi Wamuua

$
0
0
Mtu mmoja aliyekuwa abiria ndani ya daladala lililokuwa likitoka mjini kuelekea Makumbusho amewashambulia kwa kisu abiria kadhaa ndani ya gari maeneo ya Magomeni na kuwasababishia majeraha makubwa, majeruhi wote wamekimbizwa Mwananyamala. Mshambuliaji huyo ameuawa na wananchi wenye hasira. Hadi sasa haijafahamika nini lililkuwa lengo la mshambuliaji huyo.

Kambi ya Halima Mdee yasambaratika..Wapambe Wake Wakimbilia Kwa Zitto Kabwe

$
0
0

KAMBI ya aliyekuwa Mbunge wa Kawe, Halima Mdee (Chadema), imeanza kusambaratika baada ya wafuasi wake kujiunga na Chama cha ACT-Wazalendo.

 

Wafuasi wake hao wakiongozwa na diwani aliyemaliza muda wake katika Kata ya Kunduchi, Janeth Rithe, wamejiunga jana ACT-Wazalendo na kukabidhiwa kadi na Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Msafiri Mtemelwa.

 

Wengine waliopewa kadi za ACT ni Mary Mongi aliyekuwa Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Bawacha, Jimbo la Kawe, James Wambura (Katibu wa mbunge Kawe) na Manase Busa aliyefanikisha kwa kiasi kikubwa kuhakikisha Mdee anaingia bungeni katika uchaguzi wa 2010.

 

Wamo pia Katibu Bawacha Tawi la Wazo, Modesta Kalukula na Sizya Issa, Yamoyo Salehe, Sheilah Khamis, Tabia Mohamed, Ashura Salehe, Sophia Makoba na Fatuma Mikidadi.

 

Mbali na hao, chama hicho pia kimepokea wanachama wengine 198 kutoka CCM, Chadema na NCCR-Mageuzi waliojiunga kutoka jimbo hilo.

 

Akizungumza baada ya kuwapokea, Msafiri alisema wanachama hao wameungana ili kuendeleza uzalendo kwa Taifa, hivyo chama hicho kinawakaribisha na wengine.


NEC yaombwa kuongeza muda uandikishaji BVR DSM

$
0
0
Tume ya taifa ya Uchaguzi (NEC),imetakiwa kuongeza muda wa Kujiandikisha katika Daftari la kudumu la Wapiga kura kwa jiji la Dar es Salaam kutokana na wingi wa watu lakini ibadilishe baadhi ya sheria ili kila mtu mwenye sifa apate haki ya kupiga kura

Mwenyekiti wa Chama cha Alliance for Democratic Change (ADC), Said Miraji, akizungumza katika moja ya mikutano yao.

Akizungumza katika Mkutano maalum wa chama cha ADC leo jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa Chama hicho Said Miraji Abdallah amesema kuwa kuna watu wenye sifa ambao wanakosa haki yao ya msingi wakiwemo wafungwa, wagonjwa, na watanzania walio nje ya nchi ambao wanashindwa kupata haki yako kutoka na mfumo wa sasa wa uandikishaji.
Bw. Miraji ameongeza kuwa kuna watu ambao wanaweza kuachiwa magerezani wakati zoezi la uandikishaji limeshapita hivyo litawafanya washindwe kushiriki katika uchaguzi mkuu hivyo tume haina budi kuziangalia sheria zake upya.

Wakati huo hou Aliyekuwa mbunge wa Wawi Zanzibar kupitia Chama cha WanancHi (CUF) Hamad Rashid amejiunga rasmi na chama chake kipya cha ADC leo na kukabidhiwa kadi namba moja.
Akiongea na waandishi wa habari Hamad Rashid ametumia fursa hiyo kutangaza nia ya kuwania urais wa Zanzibar ifikapo Oktoba 25 mwaka huu kwa tiketi ya chama hicho.

Mastaa Wamliza Kajala usiku, Kisa..!

$
0
0
Imelda mtema
Machozi ya furaha! Staa wa filamu Bongo, Kajala Masanja juzikati alijikuta akiangua kilio baada ya kufanyiwa ‘sapraizi’ na mastaa wenzake katika siku yake ya kuzaliwa.
Tukio hilo lilichukua nafasi usiku wa Julai 22, mwaka huu nyumbani kwake Sinza Afrikasana jijini Dar ambapo akiwa hana hili wala lile, mastaa hao akiwemo Jacob Steven ‘JB’, Jennifer Kyaka ‘Odama’, Zuwena Mohammed ‘Shilole’, Nuh Mziwanda, Leah Richard ‘Lamata’ na wengineo walifika nyumbani hapo mida ya saa 6 usiku kisha wakajibanza nje.

Baada ya muda, Lamata aliyekuwa kwenye msafara huo aligonga mlango wa nyumba ya Kajala na kufunguliwa huku wakiendelea na mazungumzo, Lamata alinyanyuka na kwenda kuzima taa kisha ghafla likaingia kundi la mastaa kila mmoja akiwa ameshika mshumaa unaowaka na keki.
Tukio hilo lilimfanya Kajala apate mshituko na kitendo bila kuchelewa taa iliwashwa kisha mastaa hao wakaanza kumuimbia huku wakimmwagia vimiminika kama vile maji na ‘wine’.
Hali hiyo ilimfanya Kajala alie sana na kuwapa kazi mashosti zake kumtuliza na baadaye walisherehekea hadi asubuhi.

Akizungumzia tukio hilo, Kajala alisema kuwa, furaha aliyokuwa nayo siku hiyo ndiyo iliyomfanya alie kwani amebaini ana watu wengi wanaompenda licha ya kuwepo wachache wenye chuki zao binafsi.
“Kwa kweli sikuamini kile kilichotokea usiku ule ndiyo maana nililia kwa furaha, wenzangu wameonesha upendo wa hali ya juu kwangu,” alisema Kajala huku akifuta machozi.

Nikiridhishwa Faragha Sharti Nimsifie Mume- Joyce Kiria

$
0
0
Hamida Hassan
Mtangazaji wa Kipindi cha Wanawake Live, Joyce Kiria ametoa kali ya mwaka kwa kueleza kuwa, akishibishwa vilivyo na mume wake ‘chakula cha usiku’, haoni sababu ya kumsifia kupitia mitandao.
Joyce ambaye amekuwa na kusumba na kumpa sifa kemkemu mume wake kila atokapo kula ‘chakula’ hicho ameeleza kuwa, haoni tatizo kufanya hivyo kwa kuwa kila mtu anajua ukiolewa lazima upewe ‘chakula cha usiku’ na ushibe ndipo utaifurahia ndoa.
“Mi sioni ajabu jamani kwa sababu ni vitu vya kawaida kabisa, nani asiyejua tumetoka kwa wazazi wetu kwa ajili ya kufuata ‘chakula cha usiku?’ Kwa hiyo sioni hatari kwa kweli, nitaendelea kumsifia mume wangu atakaponipa furaha, ” alisema Joyce.

Wastara: Ulemavu Unanikosesha Hamu ya Kuolewa

$
0
0
Leo kwenye safu hii mwanadada Wastara Juma yupo hapa kujibu maswali 10 aliyoulizwa na Mwandishi Wetu Imelda Mtema. Unataka kujua kaulizwa nini na akajibu nini? Fuatilia hapa chini…
Ijumaa: Hivi ulipopata kilema cha kukosa mguu mmoja wakati ulishazoea kutembea na miguu miwili ulijisikiaje?
Wastara: Nakumbuka nilipoteza matumaini kabisa na kuona ndoto zangu zimefutika.
Ijumaa: Changamoto gani ulikutana nazo tangu ulipopata ulemavu?
Wastara: Ni nyingi sana, kwanza kubadili aina ya mwendo wakati watu walizoea kukuona ukidunda. Kifupi wengi walinishangaa kwa jinsi nilivyoanza kutembea, pilika za kimaisha kama utafutaji pia vilinifanya nipate changamoto kubwa kwani sikuwa nikisaidiwa.
Ijumaa: Uliwezaje kukabiliana na badiliko kubwa kama hilo katika mwili wako?
Wastara: Ilikuwa kazi kubwa sana kuzoea hali hii maana nilikuwa naanguka kila siku kwa kujisahau na kuona bado nina miguu yote. Kutokana na hali hiyo nilichelewa sana kupona mpaka daktari aliyekuwa ananitibu akaamua kunipa dawa ambazo zilinifanya nilale saa 24.
Ijumaa: Ulemavu wako haukupi mawazo hasa unapofikiria ishu ya kuolewa tena?
Wastara: Hili suala la kuolewa ndiyo gumu kabisa na naweza kusema ulemavu huu unanikosesha hamu ya kuolewa kwani kila mwanaume anayekuja naona hana mapenzi ya kweli na mimi, naamua kughairi.
Ijumaa: Uliwaza nini kuamua kugombea ubunge na hiyo hali yako?
Wastara: Nimefikiria vitu vingi sana na lengo ni kuwasaidia walemavu kwa kila hali.
Ijumaa: Wewe ulishawahi kunyanyapaliwa kutokana na hivyo ulivyo?
Wastara: Nilishawahi kwani nakumbuka siku moja nilitembelea nchi fulani nikapewa chumba nilale na mwenyeji wangu lakini alipoona ni mlemavu alihama.
Ijumaa: Ni maumivu gani uliyoyapitia kwa kipindi chote hiki?
Wastara: Kubwa zaidi ni maumivu ya mwili kwani kuvaa mguu wa plastiki ni mateso makubwa asikwambie mtu.
Ijumaa: Ni yapi umepanga kuyafanya kwenye siasa?
Wastara: Kwanza nitahakikisha serikali inaweka huduma nzuri hospitalini, benki na kwenye mabasi kwa walemavu.
Ijumaa: Je, umejipangaje katika kuikabili mizengwe kwenye siasa?
Wastara: Siasa siiogopi, nimejipanga kwa kila kitu na watu wasubiri waone.
Ijumaa: Huogopi mchezo mchafu unaofanywa na wanasiasa?
Wastara: Hakika nimejipanga na niko tayari kukabiliana na changamoto zote.

SOURCE: GPL/Ijumaa

Edward Lowassa Sasa Rasmi Ukawa

$
0
0
Na Neophitius Kyaruzi
BAADA ya vuta nikuvute katika vyama vya siasa vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), kuhusu kukubaliwa au kutokubaliwa kwa Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Ngoyai Lowassa kujiunga na umoja huo ili kuongeza nguvu ya kisiasa, hatimaye mwanasiasa huyo maarufu nchini amekubaliwa na tayari amejiunga rasmi Ukawa akiwa mwanachama halisi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), imefahamika.

Taarifa rasmi kutoka Ukawa na kwa msemaji wa Lowassa ambaye hakutaka jina lake litajwe, imeeleza kuwa uamuzi huo ulifikiwa baada ya majadiliano ya kina katika Mkutano Mkuu wa Ukawa uliofanyika mapema wiki hii huku ajenda kubwa ikiwa ni kumpokea Lowassa ili kuimarisha kambi ya upinzani ikiwa ni pamoja na kumsimamisha kama mgombea urais wa umoja huo.
Taarifa rasmi zilizolifikia gazeti hili zimeeleza kuwa Lowassa anatarajiwa kutangazwa rasmi Jumapili hii hivyo maadalizi ya mkutano mkubwa wa aina yake yanaendelea. Chanzo chetu kutoka katika mkutano huo kilisema kwa moyo mmoja, wenyeviti wa vyama vyote vinavyounda umoja huo, yaani Freeman Mbowe (Chadema), Profesa

Ibrahim Lipumba (CUF), James Mbatia (NCCRMageuzi) na Emmanuel Makaidi (NLD), wameridhia kuungana na Lowassa katika safari yao ya kuking’oa CCM madarakani huku wakiamini kuwa wakimsimamisha kuwa mgombea wa Ukawa watafanikisha azma ya vyama vya upinzani kuingia ikulu.
“Katika kikao chetu tulijadili mikakati kadhaa ya kuchukua dola lakini kubwa zaidi lilikuwa ni jinsi ya kuungana na Lowassa ili kutimiza azma hiyo, ikizingatiwa kwamba hivi sasa anaungwa mkono na Watanzania wengi na hasa jinsi ambavyo hawakuridhishwa na mchakato wa kumuengua kuwania urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), hivyo tuna uhakika kwa mkakati huu lazima tuking’oe CCM madarakani,” alisema mjumbe mmoja wa Mkutano Mkuu (jina limehifadhiwa).

TUNDU LISSU AFUNGUKA
Akizungumzia suala hilo, Mnadhimu Mkuu wa Kambi
Rasmi ya Upinzani Bungeni, Tundu Lissu, aliliambia gazeti hili kuwa majadiliano kuhusu Lowassa yalikuwa ya lazima kwa kuwa katika muungano wa vyama kila kiongozi ana mtazamo wake hivyo, kila jambo la muhimu lazima lifanyike kwa majadiliano ili kufikia mwafaka kwani lengo ni kuhakikisha kwamba kunakuwapo na mkakati wa pamoja kuhakikisha kuwa CCM kinag’olewa madarakani ili makada wa chama hicho waelewe kuwa sasa Watanzania wanahitaji mabadiliko na si maneno matupu ya majukwaani.
LIPUMBA NAYE ANENA
Kwa upande wake, Mwenyekiti Mwenza wa Ukawa, Profesa Ibrahim Lipumba alisema kwamba Ukawa hivi sasa wamejipanga kimkakati kuhakikisha wanachukua dola na kuongeza kwamba waliokuwa wakieneza propaganda kuwa anawakwamisha wataendelea kuumbuka kwa kuwa vyama vyote vinavyounda Ukawa ni kitu kimoja.
Aliongeza kwamba, kamwe umoja huo hauwezi kusambaratika kwani ajenda kuu ni kuindoa CCM madarakani na kuongeza kwamba, mambo mengine kama mgawanyo wa ruzuku yatafuata baadaye kwani yanazungumzika katika ngazi ya uongozi.
MSIMAMO WA LOWASSA
Msemaji wa Lowassa ambaye kawa sasa ndiye gumzo la taifa ukiachana na Dk. John Magufuli aliyepitishwa na CCM kuwania kiti cha urais amelihakikishia gazeti hili kuwa Lowassa ameamua kuingia Ukawa ili kuendeleza siasa za kistaarabu kutimiza azma yake ya Safari ya Matumaini kama ambavyo amekuwa akiwaahidi Watanzania.
Alisema ameamua kuungana na Ukawa kwa kuwa anaamini kuwa lengo la vyama vyote vya siasa ni kuhakikisha vinatimiza malengo yao ya kuwahudumia wananchi, hivyo inapotokea katika chama kimojawapo, bado kuna nafasi ya kutumia vyama vingine kutimiza malengo ya kisiasa. Msemaji huyo aliongeza kwamba baada ya kuenguliwa alikuwa na kazi ngumu ya kubaini nini cha kufanya ili kutimiza azma yake ya kisiasa, ndiyo maana alikaa kimya ili kuepusha mivutano kati yake na CCM lakini hakuwa amekata tama kuhusu jinsi anavyoweza kuwakomboa Watanzania kutoka katika dimbwi la umaskini, jambo ambalo alikuwa akiwaeleza katika safari yake ya kusaka wadhamini nchi nzima.

MKAKATI WA KAMPENI
Msemaji huyo alisema kuwa akiwa katika Ukawa, Lowassa ameandaa mkakati kabambe wa uhamasishaji wananchi ili watambue kwamba azma ya kuwakomboa ipo palepale na kuongeza kuwa ana uhakika watamuunga mkono kwani anatambua kwamba wapo pamoja naye katika safari ya matumaini.
Alisema kwamba kazi iliyo mbele yake ni kuhakikisha kuwa anaisuka upya ‘Team Lowassa’ na atakuwa makini na baadhi ya watu waliomsaliti ili wasiharibu mkakati wake na kuongeza kwamba watazunguka nchi nzima kufanya kampeni za kistaarabu, zisizokashfu wanasiasa wengine ili wananchi wapime ni kiongozi gani anafaa kati ya yeye na wengine.

TATHMINI YA USHINDI
Chanzo chetu ndani ya Ukawa kilieleza kwamba, tathmini iliyofanywa hadi sasa inawapa uhakika wa kuchukua dola kwani katika maeneo mengi, Lowassa anaungwa mkono zaidi kuliko mgombea mwingine yeyote yule. Kilisema kuwa katikamaeneo mengi CCM haikubaliki kutokana na kuendesha siasa za kibabe na mizengwe, jambo ambalo limekuwa likiwakera wananchi kwani kinachotokea ni kwamba wanachaguliwa viongozi badala ya wao kuchagua viongozi wanaowataka.
Kilisema Lowassa ana nguvu zaidi katika Mikoa ya Kaskazini, Kanda ya Ziwa, Kusini, Nyanda za Juu Kusini na Zanzibar hivyo CCM kama inataka kushindana naye ijipange vyema.

ZITTO AJUMUISHWA
Katika mkakati huo wa ushindi, inaelezwa kwamba, umoja huo utamjumuisha kundini Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe ambaye chama chake nacho kitaongeza nguvu ya ushindi.
Lowassa alikuwa mgombea urais kwa tiketi ya CCM kati ya wagombea 38 ambao walichukua fomu lakini jina lake lilikatwa katika kikao cha Kamati ya Maadili na Usalama ya CCM, jambo ambalo lilizua sintofahamu miongoni mwa wanasiasa wengi waliokuwa wakimuunga mkono, hatua ambayo ilisababisha mtikisiko wa kisiasa nchini.
Viewing all 104799 articles
Browse latest View live




Latest Images