Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104799 articles
Browse latest View live

Mkwanja wa dili la Voda ni ‘fifty fifty’ kati ya Diamond na Zari?

$
0
0
Wiki kadhaa zilizopita, Diamond Platnumz alisaini mkataba wa mamilioni ya shilingi kuwa balozi wa kampuni ya simu ya Vodacom Tanzania.

Dili hilo limemfanya muimbaji huyo wa ‘Make Me Sing’ aonekane kwenye matangazo ya TV, yale ya barabarani, kwenye magezeti na vipeperushi vingine pamoja na kusikika kwenye matangazo ya redio.

Kwenye tangazo la TV, si Diamond pekee anayeonekana, bali familia yake nzima – wapo mpenzi wake Zari, mwanae Tiffah na mama yake. Lakini pia kuna tangazo moja la redio ambalo Zari anasikika akiwemo pamoja na Diamond na Mpoki.

Yeye mwenyewe Dangote alidai kuwa familia yake nzima ni brand na hilo halina ubishi. Lakini huenda Zari akawa anamega kipande kikubwa pia cha keki hiyo iliyotokana na mkataba wa Vodacom. Si jambo la kushangaza kwakuwa Mganda huyo sasa ni ubavu wa kushoto wa staa huyo na hakuna anayebisha kuwa mrembo huyo amekuwa akipush zaidi kampeni ya Ongea Deilee kwenye akaunti yake ya Instagram.

Lakini kibiashara, tunajua kuwa hata kama Zari ni mpenzi wake na Diamond mwenye ubalozi huo, na kwa ukubwa alionao, hawezi kupiga promo tu kwasababu anamsaidia mume wake. Yaani kwa mfano haijawahi kutokea Jay Z akimsaidia Beyonce kupromote kampeni za Pepsi kisa anamsaidia mke wake.

Kwanini? Kwasababu ni kila mmoja anasimama kama brand inayojitegemea. The same applies kwa Zari na Diamond. Na hivyo kwakuwa tunaona jinsi Mama Tiffah alivyo mstari wa mbele kupush kampeni hiyo, tunaanza kufikiria kuwa huenda wawili hao wamekula pasu mkwanja huo unaotokana na ubalozi wa Diamond – fifty fifty!

It’s good to be famous.

Mtangazaji Gadner Afunguka 'Ndoa Yangu na Jide Ilivunjwa Kwa Simu'

$
0
0
Mtangazaji nyota wa redio nchini, Gardner G. Habash ambaye hivi karibuni aliachana rasmi na mkewe Lady Jaydee (Judith Wambura Mbibo) kwa talaka iliyotolewa mahakamani, amesema ndoa yake ilivunjika kwa kupigiwa simu ikitokea nchini Marekani.

Katika mahojiano maalum yaliyofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita jijini Dar es Salaam, Gardner alisema hata hivyo, licha ya kutengana kwao, yeye hana chuki na mwanamke huyo aliyeishi naye takriban miaka kumi mfululizo.

Yafuatayo ni mahojiano kamili:

RISASI: Kuna uhusiano gani kati yako na Jide (Lady Jaydee) baada ya kutengana?

GARDNER: Hakuna tunapokutana wala hatuna mawasiliano, kwa hiyo hatuna uhusiano japo mimi sina tatizo lolote wala uadui na yeye, hata hivyo sitashangaa yeye kuonyesha uadui maana ilivyotokea hivyo miezi kadhaa iliyopita.

RISASI: Miezi kadhaa iliyopita kilitokea nini unachotafsiri kama uadui?

GARDNER: Niliona dalili ya chuki wakati fulani nilimshauri tutoe tamko la pamoja kuhusu kutengana kwetu, sababu watu walikuwa wanatuuliza maana hawakutuona pamoja, hakukubali na akataka niwe nasema tu siyo kweli ni uzushi, tuko pamoja japo hatukuwa pamoja hivyo kwa ujinga wangu nilikubali na ndiyo maana nilikuwa najibu watu kuwa sio kweli.

Sasa siku niliyoshtuka ni kwamba mimi nilikuwa nazifuata akaunti zake za mitandao kama mtu niliyekuwa nasimamia kazi zake na niliendelea hivyo miezi kadhaa baada ya kutengana, kwanza nikaambiwa ameenda redioni kutangaza kuwa ameniacha huku mimi ameniambia niseme tu kuwa siyo kweli, ikawa aibu kwangu.

Halafu baadaye nikaona katika mtandao wake kaongea vitu ambavyo aliweka kama anajibu maswali aliyoruhusu aulizwe, lakini kwangu mimi ilikua shambulio, ndipo nilipotafsiri kuna chuki lakini mimi sitamchukia wala siyo adui yake. Kwa sasa ninashukuru talaka imepatikana na najua huu sio mwisho wa kupenda.

RISASI: Hivi ni nini hasa chanzo cha kuvunjika kwa ndoa yenu?

GARDNER: Chanzo anaweza kukisema yeye aliyekataa kuendelea na ndoa, mimi sikuwa na tatizo na yeye, ijapokuwa kutofautiana kwa hapa na pale katika ndoa ni jambo la kawaida, lakini sijajua hadi leo kipi kipya kizito kilifanya yeye atake kutengana.

RISASI: Kwani ilikuwajekuwaje sasa?

GARDNER: Nakumbuka ilikuwa Julai 2014, nilipata booking ya show yake aende kuimba Marekani, ilikuwa ni safari ambayo ingedumu kwa siku saba, lakini mimi nikamshauri akae mwezi mzima yaani aongeze wiki tatu zaidi baada ya show ili iwe ni likizo yake. Basi ilipofika wiki ya tatu ya mwezi huo, ndiyo akanipigia kuniambia akirudi hataki tena kuendelea kuwa katika ndoa.

RISASI: Ulijisikiaje baada ya kupata ujumbe huo?

GARDNER: Kibinadamu mtu umekaa naye miaka mingi ghafla akiwa safarini anakutaarifu kuwa hataki muwe wote tena wakati kaondoka mko sawa, na jana yake mmeendelea kuweka mipango ya maendeleo, nilijisikia vibaya na nilijaribu kutafuta maongezi, alikataa na hakurudi tena nyumbani, ikabidi kukubali ingawa kishingo upande. Nashukuru Mungu nikaanza upya nikaona maisha mapya.

RISASI: Unaweza kusema wakati unakutana na Jide ulimkuta akiwa na nini na wakati mnaachana ulimuacha na nini?

GARDNER: Si uungwana mimi kutangaza nilimkuta na nini labda aseme yeye, lakini tulizalisha mali za kutosha, tulikuwa na vyanzo kadhaa vya fedha na kwa bahati nzuri wewe ulikuwa karibu nasi uliona na wengi waliokuwa jirani nasi wanajua. Mimi nimelelewa kushirikiana na kushea na kamwe siyo kunyang’anyana, ndiyo maana sitasema mambo ya mali, kama kipo ninachostahili nt’akipata tu.
Ijapokuwa yeye amekuwa akipotosha watu kuwa mimi sikuwa na kitu, sikuwa na mchango wa kipato wala wa taaluma katika muda tuliokaa pamoja yaani ni kama Mario ninayemtumia na nilisikitika zaidi pale mahakamani Sinza hakimu alipomuuliza, ninanukuu ‘Kuna mali zozote mlipata wakati mko pamoja katika ndoa,? Yeye akajibu hamna. Hata hivyo mimi sijawahi kuonesha hata nia ya kutaka tugombee mali, nilimpa yeye aamue kila kitu ili kuepuka kulumbana lakini baadaye nikalipuliwa, hahahaha, najua mengi yatasemwa nipakwe ubaya.
Baada ya mahojiano hayo mafupi, gazeti hili lilimtafuta Jaydee na kufanikiwa kumpata kupitia simu yake ya mkononi.

RISASI: Mambo sista?
JAYDEE: Poa, nambie
RISASI: Mashabiki wa kapo yenu wangependa kujua nini hasa kilitokea katika ndoa yenu.
JAYDEE: Hivi stori moja mnaandika mwaka mzima? Kuna kipya gani hapo ambacho hamjaandika? Halafu kulikuwa na mashabiki wa Jaydee, hakukuwa na mashabiki wa couple.
JAYDEE: Hebu kuwa positive, kuna vitu vingi vizuri vya kuandika kuhusu mimi.

Chanzo:Risasi

Baada ya Lundenga Kukemea Matusi ya Mange, Wizara ya Mambo ya Ndani na Jeshi la Polisi Latoa Onyo

$
0
0
Wiki iliyopita kupitia mtandao wa Instagram,Blogger Mange Kimambi alimshambulia kwa matusi Aliyekuwa Miss Tanzania Hoyce Temu kwa kisa ambacho hata hakihusiani nae.Vilevile katika kashfa na tuhuma hizo walihusishwa hata watu wasiohusika katika ugomvi wa Mange na Ndugu yake Hoyce kinyume na sheria.

Hoyce Temu alieleza kusikitishwa kwake na maneno ya kashfa yasiyokuwa na chembe ya ukweli yaliyoelekezwa kwake na blogger huyo

Wadau mbalimbali walitoa maoni yao akiwepo Mratibu wa Miss Tanzania Hashim Lundenga aliyelaani vikali tabia hiyo iliyofanywa na Blogger huyo kuchafua majina ya watu kwa kashfa na tuhuma za uongo kwa malengo yasiyoeleweka.

Alisema inasikitisha kuona mtu ambaye anaisaidia jamii kwa hali na mali akitungiwa kashfa za uongo na kuchafuliwa jina pasipo sababu yoyote ya msingi.

Vilevile waziri wa mambo ya ndani ameonya kuwa Jeshi la polisi litachukua hatua kali bila huruma na bila kujali mhusika alipo kwa wale wote wanaotumia mitandao ya kijamii vibaya huku msemaji wa jeshi hilo akitoa msimamo mkali dhidi ya wale wote wanaotumia mitandao vibaya.

Amewataka wote ambao wanachafuliwa kwa njia ya mitandao waripoti TCRA au jeshi la polisi kwa hatua kali bila kujali jiografia ya makazi ya wahusika au mipaka.

Flaviana Matata Amjia Juu Anayedai Kumfikisha Alipo Kwenye Mafanikio yake

$
0
0
Nimesoma nukuu inayosema kwamba binadamu siku zote tunapenda kupata sifa isiyo stahili kwa mazuri tu lakini mabaya tunasingizia bahati mbaya. ​
We always take credit for the good and attribute the bad to fortune. Maneno haya yamenichoma moyoni kwani nimeona kuwa yana ukweli katika maisha yetu ya kila siku. Nimefanya kazi siku zote bila kujali mwenzangu au wenzangu wanafanya nini, na sipendi kutangaza mafanikio yangu yote. ​
Ila kuna watu maishani ambao wamenisaidia kufika hapanilipo na hata wao huwa wanaishi kwa kufuata msingi wa kuwa “tendawema uende zako”, na hawajawahi kukaa na kujitangazia kuwa wao ndo wamenifikisha hapa nilipo ingawa ni kweli. ​
Cha ajabu ni pale kuona kuwa kuna mtu ambaye namfahamu kawaida tu na hatuna mazoea wala hajuiniishivyona nimefika vipi hapa nlipo inasemekaana kuwa yeye ndo kanifikisha hapa nilipo. Kibaya zaidi si kuwa kaongea hadharani na marafiki zake bali ni kuiweka bayana katika gazeti. ​
Kitendo hiki kimenishtua na kunisikitisha kwanimimi binfasi sijawahi kuongea katika magazeti kuhusu maisha ya mtuwala kudai kuwa mi ndo nimemfikisha mahala fulani. Lakini chakusikitisha zaidi, watu ambao kweli wamenisaidia katika maisha yanguhawajawahi kukaa na ‘kuuza sura’ kwa kutumia jina langu. ​
Mafanikio yangu madogo nilonayo sasa ndani na nje ya nchi yamefikiwa kwa juhudi zangu na zawatu wachache, hii ni pamoja na kupatikana kwa mkataba wangu wa nje(Afrika Kusini) na mkataba na maelewano yote ni kati yangu mimi,kampuni yangu ya Afrika Kusini na kampuni yangu mama ya CompassCommunications. ​
Hatua zozote zilizochukuliwa hazikumhusisha mtanzaniamwingine. Na hata katika siku zijazo, itaendelea kuwa hivyo. Kwaheshima na taadhima naomba mhusika na wahusika, waache kuongeleamaisha yangu, mafanikio yangu, kwani haiwahusu. ​
Pia naomba wanajamii wenzangu mkisikia kitu kinazungumzwa ambacho hakijatoka kwangu au kampuni yangu mama, basi wajue atakuwa ni binadamu mwingine ambaye ametetereka na kuingia katika mtego ule wakutaka kupata sifa asizostahili.​
Mwisho kabisa napenda kuwashukuru wote ambao wapo sambamba na watanzania wote kwa ujumla ​
Regards,​
Flaviana Matata​

Kampuni Ya Kichina Matatani Kwa Kutengeneza Vibao Vya Namba Za Magari Kinyume Cha Sheria

$
0
0

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imefanya msako wa kushtukiza katika kampuni ya Tanzania China Trade and Tourism Development Ltd iliyoko Barabara ya Nyerere Dar es salaam baada ya kupata taarifa kutoka kwa msamaria mwema na kukamata vifaa pamoja na malighafi za kutengeneza na kutoa vibao vya namba za pikipiki kinyume na sheria.

Katika msako huo uliofanyika tarehe 19 Februari 2016 katika kampuni hiyo, Maofisa wa TRA waliweza kukamata na kutaifisha vibao vyenye namba za pikipiki 2,500 na vibao 5,600 ambavyo havikuwa na namba. Pia maofisa wa TRA walikamata malighafi za rangi ya vibao katoni tatu, pamoja na mashine ya kupaka vibao rangi yenye uzito wa kilo 155.

Mashine nyingine iliyokamatwa katika msako huo ni ya kutengeneza namba za magari yenye uzito wa kilo 902 ambayo imezuiwa isihamishwe kutoka katika kampuni hiyo pamoja na kompyuta mpakato ambayo imepelekwa katika maabara ya uchunguzi TRA kwa ajili ya uchunguzi zaidi.
Taarifa za kuwepo kwa utengenezaji wa vibao vya magari kinyume na taratibu na sheria zilitolewa na msamaria mwema ambapo Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni husika Donglinh Guo, Meneja wa Kiwanda Yong Qing Cheng na Meneja wa ghala Peng Zhan walikamatwa baada ya kutokea fujo wakati wa msako na kufikishwa katika kituo cha Polisi Changombe.

Kampuni ya Tanzania China Trade and Tourism Development LTd ndio waingizaji pekee wa pikipiki za Falcon tangu mwaka 2008 ambapo inatuhumiwa kutoa vibao vya namba za pikipiki kwa wateja wake kwa shilingi 5,000 kinyume na sheria.Uchunguzi wa thamani ya kodi iliyopotea bado unaendelea.

Vibao vya magari na pikipiki hutolewa na kampuni ambazo zinatambuliwa na TRA baada ya kupewa idhini. Kampuni hizo ni Masasi Sign, Auto Zone, Sign Industry, Kiboko, Budda Auto works, Parkinson Ltd na Next Telecom.

Ili kujiridhisha kuwa kadi za pikipiki zinazotolewa kwa wateja wa kampuni hiyo ni halali, TRA ilifanya uchunguzi na kugundua kuwa kadi hizo zinatolewa kihalali.

TRA inawatahadharisha wananchi kufuata taratibu na sheria ili kuepuka usumbufu unaoweza kutokea endapo watagundulika kujihusisha na vitendo ambavyo ni kinyume na sheria.

Agnes Masogange na Wenzako Tumieni Ujana Wenu Vizuri

$
0
0
KWAKO Agness Gerald ‘Masogange’ pamoja na wenzako wengi ambao baadhi yao nitawataja kwa majina hapo chini. Nawasalimu katika jina la Bwana, vipi mko poa? Mnajionaje na hali? Mishe zenu zinakwenda kama kawaida?

Mkitaka kujua afya yangu, mimi namshukuru Mungu. Naendelea vizuri. Nazidi kupambana ndani ya huu mjengo mkubwa wa Magazeti Pendwa Tanzania, Global Publishers Ltd. Kazi yetu ni ngumu kidogo, kila siku wasomaji wanataka habari mpya. Kuzitafuta si kazi ya kitoto.

Dhumuni la kukuandikia barua Masogange na wenzako leo ni moja tu, kutaka kuwakumbusha kwamba kuna maisha baada ya ujana. Umaarufu mnaoupata kwenye mitandao, hauna maana kama mnakuwa hamna shughuli ya kufanya.

Watanzania hawafurahishwi na mnavyoposti picha zenye viashiria vya ngono na kuziweka mtandaoni. Unajipiga picha ya nusu utupu, unaiweka mtandaoni ili iweje? Umekaa mkao wa kuhamasisha ngono unataka kutafsirika vipi? Unajiuza? Kama ndiyo biashara, kwa nini usitafute nyingine?

Mbona biashara zipo nyingi jamani. Kupitia urembo wenu mbona kuna ishu kibao tu za kutengeneza fedha? Kuna makampuni yanataka kufanya kazi na nyinyi kwenye matangazo yao, kuna wasanii wanataka muwapambie video zao, yote hayo hamyaoni? Njia pekee ya kuishi ni hiyo mliyoichagua?
Wiki iliyopita niliona moja kati ya habari iliyopamba magazeti ya Global ni ile ya mtindo mpya wa mastaa kujiuza. Kwamba siku hizi taarifa zinaeleza kwamba wengi wenu mnapoweka picha kwenye mtandao wa Instagram, mnapata dili nchi za nje.

Hii ni aibu. Kweli warembo wa Tanzania mmefika hapa? Yaani biashara inafanyika mtandaoni, mnasafiri kwenda nchi za watu kweli? Sikushtuka sana nilipoona ile habari maana Masogange wewe na wenzako mmekuwa mkisafiri pasipo kueleweka kinachowasafirisha.
Utasikia tu Masogange yupo Sauz, sijui Gigy Money yupo wapi mara sijui Kidoa alikwenda kufanya shopping Dubai na kurudi, mnakwenda kule kwa kipato gani? Kazi gani zinazowaingizia kipato hadi muende kule kufanya shopping?

Niliwahi kuzungumza na wewe Masogane siku moja katika Global TV Online. Nilikubana maswali kuhusu kazi inayokufanya uishi mjini, hukuwa na jibu la kueleweka. Bado pia ulisema wasanii hawawalipi vizuri pindi mnapotumika katika video zao.

Hiyo ilitosha kunifanya mimi nikuone kwamba unahitaji kubadilika. Unahitaji kutafuta kazi ya kufanya kuliko kuishi kimjinimjini. Mbona unaonekana unaweza hata kuigiza, kwa nini usiigize? Unafikiri aina ya maisha unayokwenda nayo itadumu hadi lini?

Mimi nakushauri kama kaka yako, badilika. Wenzako pia wenye kamchezo kama ka kwako nao pia nawaambia wabadilike ili na wao wafanye kazi, waache kuweka picha za nusu utupu mitandaoni.
Ni matumaini yangu wewe pamoja na wenzako wote wanaofanya mambo hayo watabadilika mara moja maana si ungwana.
Mimi kaka’ko;
Erick Evarist

Tekno Kahojiwa Kwenye Radio…Hataki Tena Kuulizwa Kuhusu Mrembo Mtanzania Gigy Money..Adai Hamjui

$
0
0
Kwa wale wanaofatilia stori za burudani Tanzania hasa ujio wa mwimbaji wa Nigeria Tekno kwenye show ya Dar es salaam walipata kilicho-trend kuhusu mwimbaji huyo staa wa hit single ya ‘wash‘ kuripotiwa kulala na Mrembo wa kitanzania aitwae Gigy Money.

Baada ya hizo taarifa kusambaa, Tekno alipost na kuandikiwa caption ya picha yake kwenye Instagram kwa Kiswahili akionekana kukasirishwa na kilichosambazwa na Mrembo huyu ambapo moja ya sentensi zilisomeka ‘umelala na meneja wangu ukaletwa chumbani kwangu maana uliomba upige picha sasa unaleta stori kwamba umelala na mimi‘

Hii ishu ilimfanya Tekno aendelee kupokea maswali mengi ya media aliporudi Tanzania tena Waandishi wakimuuliza kuhusu Gigy huyohuyo… Tekno amesema hatopenda tena kuiongelea hii ishu wala kuulizwa ila akasisitiza...
‘Kabla ya yote sijui Gigy ni nani, ni mtu ambaye nilipiga nae picha tu, sina chochote cha kufanya naye… namuheshimu na wala sio namdharau ila ni kwamba simjui’
Msikilize Hapa:

Mtazame Rais wa TFF Jamal Malinzi Akieleza Kuhusu Tuhuma za Upangaji wa Matokeo...Adai Ahusiki Katika Ujinga Huo...

$
0
0
Rais wa shirikisho la soka Tanzania TFF Jamal Malinzi February 23 wakati wa kusaini mkataba wa kusaidia maendeleo ya soka la wanawake Tanzania na taasisi ya Karibu Tanzania, amezungumzia kuhusu tuhuma za upangaji matokeo katika michezo ya mwisho ya Ligi daraja la kwanza iliyomalizka hivi karibuni.

Jamal Malinzi aliyasema haya 
“Upangaji wa matokeo ni kosa kubwa katika soka, na halitakiwi kufumbiwa macho, TFF imeshitaki suala hili kwa kamati ya maadili ya TFF na majibu yatapatikana March 20, kuhusu mimi kuhusika huo ni uzushi, mimi naongoza taasisi kubwa siwezi kuunga mkono au kushiriki katika huo ujinga”
Chanzo: Millardayo

Alikiba Aeleza Kwanini Hakuweza Kumuoa Mwanamke yeyote Kati ya Watatu Aliozaa Nao

$
0
0
Alikiba ameitaja sababu iliyomfanya ashindwe kumuoa mwanamke yeyote kati ya watatu aliozaa nao.

Hitmaker huyo wa Lupela alikiambia kipindi cha Chill na Sky kuwa hakupenda kulazimisha iwe hivyo.
“Unajua hauwezi kumuoa mtu kama hamuelewani. Nia yangu ilikuwa ni kustick na kila mama wa mmoja toka nilipoanza. Lakini mambo yanaenda tofauti, huenda mnagombana anapata mtu mwingine,” anasema Kiba.
“Kwahiyo hautakiwi kuforce mapenzi, mimi nataka nikae na mtu ambaye tutaelewana,” ameongeza.

Alikiba ana watoto wawili wa kike, Amiya Kiba, Chamy Kiba na mmoja wa kiume, Sameer Kiba. Wote ni watoto wa mama tofauti.

Hanscana ampa Vidonge Q Chief, ni Baada ya Kusema Directors wa Video wa Bongo Hawana Lolote..Amtaka Aache tu Music Miaka 17 Hana Hata Baiskeli..

$
0
0
Muongozaji wa video nchini Hanscana, amemjibu Q Chief kuhusu tuhuma alizowarushia directors wa video wa bongo kwamba hawana lolote na hawezi fanya nao kazi tena.

Akizungumza katika kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio Jumanne hii, Hanscana amesema Q Chief ana stress za maisha ndio maana amekuwa akiongea ovyo.

“Ye ana stress za maisha, haiwezekani ukafanya muziki zaidi ya miaka 17 halafu huna hata pikipiki wakati kuna watoto wamekuja tu juzi kirahisi rahisi alafu wana kila kitu,” alisema Hanscana.

“Kwa hiyo lazima upate mastress uanze kutapatapa, si unajua mfa maji, u can see ur self jamaa ana more than 17 yrs in the game alafu he got nothing, halafu kuna watoto tu wadogo wanafanya kitu, kwa hiyo unaweza ukafikiria, suala dogo kama hilo kitaalamu hizo ni stress za maisha,” aliongeza Hanscana.

Pia Hanscana amemtaka Q Chief akae pembeni na kuwaachia wasanii wachanga wafanye kazi kwa sasa, na yeye abaki kuwa mtazamaji.

“Ninachomshauri atuachie tu new generation tufanye vitu vyetu , tuna mwaka mmoja ndani ya game tuna drive, tunaishi vizuri, atuache tu vijana aangalie tu game awe anatuangalia Youtube,” alisema Hanscana.

Nay wa Mitego Akimbilia Polisi..Achukua RB Adai Kuna Watu Wanamfuatilia Kutaka Kumtendea Mabaya

$
0
0
MKALI wa Bongo Fleva, ambaye wimbo wake wa ‘Shika Adabu Yako’ umefungiwa na Baraza la Sanaa Nchini (Basata), Emmanuel Elibariki ‘Ney wa Mitego’, ameibuka na kudai kwamba ameamua kuchukua R/B kituo kidogo cha polisi ili kuwadhibiti watu anaodai wanamfuatilia kwa nia ya kumtendea mabaya.

“Kiukweli sina ugomvi na mtu na hii ni dunia haina siri, kama kuna mtu ananifanyia hivyo vitu basi itajulikana maana mimi nimeimba kama wimbo mwingine na sina ugonvi nao, sasa kama wananitafuta nitawatafuta kwa R/B,” alieleza.

Aliongeza kwamba, kwa sasa mtoto wake wa kike amefanyiwa upasuaji wa uvimbe katika koo na maendeleo yake ni mazuri, huku akisisitiza kwamba Ijumaa ya wiki hii atatoa video ya wimbo wake huo.

“Mwanangu alikuwa anaumwa lakini kwa sasa nashukuru Mungu hajambo na wiki hii nitatoa video ya wimbo wangu, mtaona tofauti na mnavyofikiria tofauti katika wimbo wenyewe,’’ alimaliza


Jibu la Idris Sultan kwa Mtu Aliyeuliza kuhusu Wema Sepetu Kufuta Picha zake Instagram

$
0
0
Swali kubwa kwa sasa kwenye mitandao tofauti ya kijamii ni jee Wema Sepetu na Idris Sultan wameachana.

Swali hili limeibuka baada ya staa Wema Sepetu kufutilia mbali picha za Idris Kwenye kurasa yake ya Instagram

Haijulikani ni nani kamkosea mwenzake lakini inaonekana kuwa ni Wema ndiye aliyechukia zaidi kiasi cha kuamua kufuta picha zote za Idris alizowahi kuzipost kwenye akaunti yake ya Instagram.

Shabiki alivyomuuliza Idris Kuhusu picha zake kufutwa sasa, hili jibu alilopewa.

Mtoto wa Miaka Mitatu Abakwa Na Kunyongwa Hadi Kufa

$
0
0
Mtoto mwenye umri wa miaka 3 na miezi 4 Mariam Deogratius mwanafunzi wa shule ya awali ya Makoko iliyopo katika Manispaa ya Mji wa Musoma mkoani Mara, amebakwa kisha kunyongwa hadi kufa na mtu asiyejulikana Usiku wa kuamkia leo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara kamishna msaidizi Philllip Kalang amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa Jeshi la Polisi linafanya Msako kuhakikisha Mhalifu anapatikana.

Kikwete Kuwatumbua MAJIPU Wanachama Wasaliti wa CCM Waliokihujumu Chama Wakati wa Uchaguzi Mkuu

$
0
0
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Jakaya Kikwete amesema kuwa chama chake kitawachambua na kuwaadhibu wote ambao walikisaliti katika Uchaguzi Mkuu uliopita, kuanzia ngazi za matawi, kata, wilaya, mkoa hadi Taifa.

Dk. Kikwete ametoa kauli hiyo Jumatatu ya wiki hii mjini Kibaha alipohudhuria sherehe za uzinduzi wa ofisi mpya ya chama hicho mjini humo.

“Baada ya mchakato wa Dodoma wapo ambao walisusa kabisa na wakawa wanajificha. Unakuta hahudhurii mikutano yetu ya kampeni, lakini ya wenzetu upinzani unamkuta na akiulizwa anasema eti alialikwa,” alisema na kusisitiza kuwa wanachama kama hao ni wasaliti na uanachama wao una mashaka.

Kikwete alisema mchakato wa kuwaadhibu wanachama wasaliti utafanyika wakati wowote baada ya kuyapitia majina ya wote wanaotuhumiwa kukihujumu chama.

“Tayari tuna majina ya watu ambayo yanadhaniwa walikihujumu chama. Tutayapembua katika vikao mbalimbali halali kuanzia ngazi za matawi, kata, wilaya, mkoa na Taifa na tutaamua kwa haki wakati wa kuwaadhibu,” alisema.

Aliwataka wanachama hao kufanya tathmini na kutambua waliokisaliti chama lakini alionya vikao vya kuwabaini vitende haki bila kumuonea mtu akisema yapo baadhi ya majina yanatajwa kuwa ni wasaliti kutokana na migogoro binafsi baina yao.

HALIMA MDEE Afunguka...'Hakuna Ufisadi Uliofanyika Kwa Bahati Mbaya Bila ya Mawaziri na Wakurugenzi '

$
0
0
Mbunge wa jimbo la Kawe jijini Dar es Salaama katika kwa tiketi ya Chadema, Mh. Halima Mdee amefunguka na kuweka wazi kuwa hakuna ufisadi ambao umefanyika nchini kwa bahati mbaya.

Mdee amesema kuwa kila ufisadi uliofanyika viongozi wa serikali walikuwa wakitambua sababu kuna muda mwingine walipokea memo kutoka katika uongozi wa juu ya nchi.

Halima Mdee amesema hayo alipokuwa kwenye mkutano wa hadhara na wananchi wa jimbo la Kawe na kusema kuna wakati wakurugenzi walikuwa wanapewa vimemo kutoka kwa Rais wa nchi na wengine walikuwa wakipewa memo hizo kutoka kwa mawaziri mbalimbali.

"Hakuna ufisadi ambao umefanyika kwa bahati mbaya, hakuna ufisadi ambao umefanyika nchi hii pasipo waziri au aliyekuwa waziri kwenye serikali ya Chama Cha Mapinduzi kujui. Hakuna ufisadi uliofanyika leo hii bila wakurugenzi kupewa vimemo ama kutoka kwa Rais, au kutoka kwa waziri wafanye maamuzi waliyofanya leo wanajifanya wanatumbua vijipu kumbe wanatumbua vipele, sababu wale walifanya kwa maelekezo ya wakubwa." Alisema Halima Mdee.

Katika hatua nyingine mbunge huyo wa Kawe amesema kuwa wao wanapozungumza leo hawazungumzi tu kwa sababu ya Chadema na UKAWA bali wanazungumza kwa maslahi mapana ya watanzania walio wengi ambao maisha yao ni magumu yaani kifupi wamepigika.

Hizi Hapa ni Sababu Zitakazokufanya Wewe Binti Usiolewe Mapema

$
0
0
Hizi Hapa ni Sababu Zitakazokufanya Wewe Binti Usiolewe Mapema

★1. Kuvaa nguo za ajabu ajabu kama changudoa. Sijui ni nani aliyewaambia kuwa mkivaa hivyo mnapendeza!

★2. Kujipaka marangi ya ajabu ajabu usoni kama mwali wa kimakonde au kizaramo kwanza mnatutisha tu.

★3. Kupenda kujirahisisha au kujipendekeza pendekeza kwa wanaume, yani ukiguswa kidogo tu twende.

★4. Kuwa na picha karibia 500 Facebook, Twitter nk halafu picha zenyewe hazieleweki yani zimepigwa katika mavazi au mapozi ya ajabu ajabu, mara umebinua makalio, mara tumbo, mara mdomo, Haaaaa!

★5. Kila unachofanya basi unakimbilia kupost mfano kwenye Facebook account
yako au Instagram na nyinginezo hata ukienda haja basi lazima upost.

★6. Ni mtu wa maneno maneno yani we kila unachokiona unaongea na kuropoka ropoka tu hauna break! mwanamke gani?

★7. Huna mawazo ya malengo endelevu yani we kwenye bichwa lako kumejaa umbea tu sijui leo Wema Sepetu amefanya nini? Sijui Kim, Lupita amefanya vile na upuuzi mwingine.

★8. Mizinga. Yani siku ya pili tu baada ya kukutongoza unaanza " honey nataka galaxy" Htc" Huawei" mara baby nimeona nguo nzuri mara ooh baby yaani njaa inauma'' mimi babaako, utasindikiza harusi za wenzio hadi upigwe alama.

""Utaishia kunisonya lakini message sent""

Matikibokoyao: Wema Sepetu Rudisha Pesa za Nguo Unazodaiwa na Manyota

$
0
0
Aliyekuwa shabiki namba moja wa muigizaji wema sepetu(Team wema) , matilda au maarufu kama matikibokoyao ametoboa moja ya siri ya aliyekua boss wake kuwa huwa anakopa nguo kwa mfanyabiashara maarufu mjini aitwaye manyota, hivyo amemtaka msanii huyo mpenda kick mjini aende akalipe madeni ya watu.

Akiendelea kumwaga ubuyu, Yuda huyo hakumuacha nyuma muigizaji lulu michael na kudai kuwa na yeye pia ana madeni sugu kama ilivyo kwa boss wake(Wema).

Chanzo cha bifu hicho inasemekana ni mimba aliyokua nayo staa huyo(wema) ambapo inadaiwa mfuasi wake huyo nambari moja amekua akitembeza ubuyu kwa maadui zake(wema) kuhusu ujauzito wake ambapo boss huyo aliamua kumchana live kijakazi wake huyo na kumkana hadharani kuwa hamjui.

Bifu hilo liliendelea mbele zaidi ambapo shabiki huyo wa madame aliapa kutoboa siri kibao za boss wake huyo , hata hivyo baadae madame baada ya kuona mambo yake yanaanza kuanikwa alianza kujirudi taratibu kwa mfuasi wake huyo na kuyamaliza kiutu uzima

Chanzo: Jamii Forums

KIMENUKA...Mabilioni ya NSSF Yatafunwa

$
0
0
BODI ya Wakurugenzi ya Shirika la Tija la Taifa (NIP) imeishauri serikali kuunda tume ya kuchunguza matumizi mabaya ya fedha za serikali zaidi ya dola za Kimarekani 1.5 bilioni, anaandika Josephat Isango.

Kwa mujibu wa ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali ya mwaka 2012/13, imebaini kiasi cha dola za kimarekani 1,532,458.91 zilizotolewa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) zimetumika kinyume na taratibu za kisheria.

Akizungumza jijini Dar es Salaam hivi karibuni, Profesa Samweli Wangwe, Mwenyekiti wa NIP, amesema kuwa, fedha hizo zilikua za   mkopo kwa ajili ya uendelezaji wa jengo la Maarifa lililopo mtaa wa Ohio na Hollis jijini Dar es Salaam ambalo linamilikiwa na Shirika hilo zilipo.

Amesema, ripoti hiyo ilionyesha kuwa, kiasi cha dola za kimarekani 480,000 zilitumika kuilipa kampuni ya Zawadi Communication Limited ambayo inamilikiwa na Jamal Malinzi ambaye ni Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF), kama gharama za udalali wa kuitafutia NIP mbia wa ujenzi wa jengo hilo ambao ni NSSF.

Ameongeza kuwa, mashirika hayo mawili ni mali ya serikali, hivyo basi hakukuwa na ulazima wa kumtafuta dalali wakati makatibu wakuu wangeweza kukaa pamoja na kujadiliana namna ya kuweza kuingia makubaliano ya mkopo huo.

Amesema, licha ya kufanyika kwa malipo hayo, lakini ripoti hiyo imeonyesha kuwa, NIP haikuitisha zabuni yoyote ya kutafuta kampuni‎ ya udalali ya kutafuta mbia, jambo ambalo ni kinyume na sheria.
Alisema Kutokana na hali hiyo, bodi hiyo ilipata mashaka juu ya malipo hayo na kuitaka serikali kuchunguza mwenendo mzima wa malipo hayo kama ulifuata taratibu za kisheria.

“NIP haikutangaza zabuni yoyote ya kutafuta kampuni ya udalali kwa ajili ya kutafuta mbia,lakini malipo yameonyesha kuwa, kampuni hiyo ililipwa kiasi hicho Juni16 mwaka 2011,jambo ambalo ni kinyume na sheria,” amesema Profesa Wangwe.

Amesema, licha ya malipo hayo kufanyika, lakini pia kiasi cha dola 831,214.48 zimebainika kutumika kinyume na sheria wakati ujenzi wa jengo hilo haujaanza kinyume na makubaliano ya mkataba wa mkopo huo.

Wangwe aiwambia waandishi kuwa bodi hiyo pia ilibaini kuwa, fedha zote ambazo ni dola 1,532,458,91 ziliingizwa Katika akaunti ya NIP kwa mkupuo moja wakati makubaliano yalikuwa ni kuingiza kwa awamu kulingana na mahitaji halisi.

“Kutokana na hali hiyo, NIP inatakiwa kulipa jumla ya dola 1,002,228.13 ambayo ni pamoja na riba ya asilimia 13.08 kwa kipindi chote cha miaka mitano, jambo ambalo linazidi kuitia hasara serikali,” amesema.

Alifafanua kuwa, mpaka sasa shirika hilo halina vyombo vya usafiri, badala yake viongozi wakuu akiwamo Mkurugenzi anakodisha gari lake binafsi kwa ajili ya matumizi ya ofisi.
Profesa Wangwe amesema kuwa, licha mkataba huo kuonyesha matumizi ya fedha hizo ambayo ni pamoja na kulipa gharama za wapangaji za kutafuta sehemu nyingine ili kupisha ujenzi huo pamoja na NIP kukodi ofisi wakati ujenzi huo unaendelea, lakini fedha hizo zimetumika kinyume na makusudio.

Amesema baada ya kubaini upungufu huo, bodi hiyo iliitisha kikao cha dharura kwa ajili ya kuzungumza na menejimenti kuhusu suala hilo ambao na wenyewe walikiri kukiukwa kwa makubaliano ya mkataba huo kwenye matumizi ya fedha hizo.

Wangwe amesema kutokana na hali hiyo, bodi hiyo iliwasilisha mapendekezo ya kuitaka serikali kumsimamisha kazi Mkurugenzi wa Shirika hilo, Joel Mlanzi ambaye tayari ameshasimamishwa kazi ili kupisha uchunguzi wa suala hilo.

Chanzo: Mwanahalisionline

Mwakyembe: Katiba Mpya sio Kipaumbele cha Rais Magufuli....Wanaofikiri Tutaanza Na Rasimu Ya Warioba Wanapoteza Muda

$
0
0
Dr. Harrison Mwakyembe, Waziri wa Katiba na Sheria amewataka Watanzania wanaoulizia hatima ya mchakato wa katiba mpya kutambua kuwa suala hilo si sehemu ya vipaumbele vya Dk. John Magufuli.

Mwakyembe amesema hayo jana usiku katika mahojiano maalum aliyofanya na Marin Hassan, mtangazaji wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC), juu ya utendaji wa wizara yake katika siku 100 za serikali ya awamu ya tano.

Waziri huyo alisema kuwa katiba mpya haina umuhimu mkubwa katika maisha ya kila siku ya watu na wala sio kipaumbele cha rais Magufuli kwani ni kiporo tu alichoachiwa na serikali ya awamu ya nne na atakifanyia kazi wakati atakapoona inafaa.

“Watu wanadhani katiba mpya ndiyo kila kitu, wanaona katiba ni muhimu kuliko kulipia watoto waende shule, wanafikiri katiba mpya ikishapitishwa tu basi kesho yake wataletewa mkate na chai kitandani jambo ambalo sio kweli,” amesema Dk. Mwakyembe.

Aliongeza kuwa: “Kwa sasa rais bado anafanyia kazi vipaumbele vyake kwanza ikiwemo kusimamia elimu bure, kuongeza kasi ya ukusanyaji mapato ya serikali na kusimamia uwajibikaji wa watumishi wa umma na hivyo kelele za katiba mpya hazina msingi.”

Katika hatua nyingine, Waziri Mwakyembe alisema Watanzania ambao bado wana ndoto kuwa mchakato wa katiba mpya unaweza kuanzia katika hatua ya kujadiliwa kwa rasimu ya katiba ya Jaji Joseph Warioba kuachana na wazo hilo kwani limepitwa na wakati.

Alisisitiza kuwa katiba iliyopendekezwa na kupitishwa na wajumbe wengi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ni halali kwani ilipatikana kwa mujibu wa sheria na taratibu licha ya kususiwa na wajumbe wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).

Ukawa unaoundwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Chama cha Wananchi (CUF), National League for Demokracy (NLD) na NCCR Mageuzi.

“Rais alishasema alipohutubia bunge, kwamba kuna kiporo nimeachiwa, sasa mimi nashangaa hawa watu! tena wengine wana shahada za sheria, wanaongea nini? Hatua ya rasimu ya Warioba ilishapitwa na wakati na tayari tunayo katiba pendekezwa,” aling’aka.

Mwakyembe alihitimisha kwamba utakapofika wakati wa kulifanyia kazi suala la katiba mpya, serikali ya awamu ya tano itaendelea na hatua ya kura ya maoni ya katiba pendekezwa na sio vinginevyo.

Bodi ya Mikopo Ya Wanafunzi Yatoa Utaratibu wa Kuwasilisha Malalamiko.

$
0
0
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imetoa  utaratibu wa kushughulikia  malalamiko ya wanafunzi wanaopata mikopo katika taasisi za elimu ya juu nchini.

Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es salaam na Meneja wa Habari, Elimu na Mawasiliano Omega Ngole alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kuhusu utaratibu wa kushughulikia malalamiko ya wanafunzi wa elimu ya juu nchini.

“Utaratibu huu ulioboreshwa, ni msisitizo na maelekezo ya Serikali ya mwezi Agosti 2011 kupitia iliyokuwa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ambayo ilielekeza Taasisi zote za Elimu ya Juu nchini zinazopata mikopo kutoka Bodi ya Mikopo kuanzisha Madawati ya Mikopo ili kuongeza ufanisi katika utoaji mikopo”,Alisema Ngole.

Ameongeza kuwa, dawati hilo linatakiwa kusimamiwa na mtumishi teule wa chuo husika mwenye sifa na uhusiano mzuri na jamii na linapaswa kuwa chini ya Makamu Mkuu wa chuo husika anayeshughulikia taaluma.

Meneja Ngole amesisitiza kuwa kwa sasa vyuo vyote vina Maofisa Mikopo ambao wanawajibika kutafuta suluhisho la suala linalowasilishwa na kulitolea majibu.

Akifafanua hatua zinazotakiwa kufuatwa na Maofisa hao katika kutafuta suluhisho la malalamiko ya wanafunzi amesema kuwa, baada ya malalamiko kufika kwa Ofisa Mikopo yanatakiwa yapate suluhisho ndani ya siku mbili tangu kuwasilishwa kwake,ikiwa hatakua na ufumbuzi atatakiwa kuwasiliana na uongozi  wa juu wa chuo husika.

Endapo uongozi  wa juu wa chuo hautokuwa na ufumbuzi, malalamiko hayo yatatakiwa kupelekwa kwenye Ofisi za Kanda ambazo zinapatikana katika Mikoa ya Mwanza, Dodoma, Arusha na Zanzibar au ofisi za makao ya makuu ya Bodi  zilizoko jijini Dar es Salaam.

Bodi ya Mikopo ilianzishwa kwa sheria ya Bunge namba 9 ya mwaka 2004 na kuanza rasmi mwezi Julai 2005 kwa majukumu ya kutoa mikopo kwa wanafunzi wahitaji waliodahiliwa katika Taasisi za Elimu ya Juu pamoja kukusanya marejesho ya mikopo yote iliyotolewa tangu mwaka 1994.
Viewing all 104799 articles
Browse latest View live




Latest Images