Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104809 articles
Browse latest View live

SOMA Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumatatu Ya March 21

$
0
0

SOMA Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumatatu Ya March 21

Idadi Ndogo ya Wapiga Kura Wajitokeza Uchaguzi wa Marudio Zanzibar.....

$
0
0
Zanzibar Uchaguzi Mkuu wa marudio wa Zanzibar umefanyika kwa amani na utulivu huku kukiwa na idadi ndogo ya wapiga kura, ikilinganishwa na idadi ya waliojitokeza katika uchaguzi uliofutwa wa Oktoba 25, mwaka jana.

Takwimu za Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), zinaonyesha kuwa waliojiandikisha kwenye Daftari la wapiga kura kwa Unguja na Pemba ni 503,860, na sehemu zote hizo zilikuwa na jumla ya vituo vya kupigia kura 1,580, na  kila kituo kina wastani wa wapiga kura 350.  

Katika uchaguzi huo vyama vya CCM, AFP,  ADC  na CCK vimeshiriki katika uchaguzi huo na kuweka mawakala wake vituoni huku chama cha CUF kikiwa hakina wakala yeyote kwenye vituo  vyote vya kupiga kura vya kisiwani Unguja.

Pamoja na kuwepo kwa hali ya taharuki katika siku za karibuni visiwani hapa, hali hiyo imekuwa tofauti ambapo leo  maeneo mengi yalionekana kuwa na amani, pia vikosi vya ulinzi havikujitokeza barabarani kama ilivyozoeleka.

Maduka mengi yalionekana kufungwa na katika vituo vya kupiga kura ambavyo inadaiwa  ni ngome ya CUF, watu walijitokeza kwa idadi ndogo ikilinganishwa na wale waliojitokeza kwenye maeneo ambayo ni ngome ya CCM.

Katika Kituo  cha Shule ya Sekondari Bububu pamoja na msimamizi wa kituo hicho Mohammed Zamani,  kusema kuwa watu walijitokeza kwa wingi kupiga kura, wakala wa chama cha AFP, Fumo Machano Fumo alieleza kuwa tokea kufunguliwa kwa kituo hadi sita mchana watu waliokuwa wamepiga kura katika chumba chake walikuwa 25.

Mtoto Afariki Kwa Kukosa Matibabu..Wazazi Waliamini Maombi Pekee

$
0
0
Mwanafunzi wa darasa la saba Shule ya Msingi Laela A, Ruti Sikapitaamefariki dunia baada ya wazazi wake kukataa kumpeleka hospitali  kwamadai kuwa imani ya dhehebu lao haliruhusu waumini wake  kutibiwa hospitali.

 Tukio hilo lilitokea Machi 17 baada ya mtoto huyo kuugua kwa siku tatu
huku akiwa anafungiwa ndani na  baba yake Cossam Sikapita, akidai kuwa
hawataki aende hospitali kupatiwa matibabu kwani kwa kufanya hivyo angekuwa ametenda dhambi kwani dini hairuhusu kutibiwa na  dawa za hospitali.

Mwenyekiti wa Kitongoji cha Laela, Didas Simtengui,alisema kuwa mtoto
huyo alikuwa anaumwa kwa siku tatu na hawakumpeleka hospitali badala
yake walikuwa wanazidisha maombi wakiamini kuwa atapona.

 Mmoja wa majirani, Musa Mwanakulya  alisema kuwa wao walikuwa hawamuoni
mtoto huyo akienda shuleni na wenzake na walijua anaumwa na ametibiwa
isipo kuwa maombi ni kitu cha kawaida na walikuwa wakisikia wanaomba
kila siku katika nyumba hiyo.

‘’tulikuwa tunasikia wakisali sana huku wakiwa wamejifungia ndani,
tulipo uliza walidai kuwa wanamuombea Ruti anaumwa lakini hawataki
kumpeleka hospitali wakidai kuwa mafundisho ya dini yao haya ruhusu
kutibiwa hospitali….waliendelea kumuombea mpaka akafariki
dunia’’…alisema.

Majirani walipopata taarifa kuwa mtoto huyo amefariki kutokana na wazazi wake kugoma kumpeleka hospitali, walikwenda kuvamia katika nyumba hiyo
wakitaka wawakamate wazazi hao ili nao wawaue.

 Kutokana na vurugu kubwa kuibuka ililazimu polisi wa kituo cha Laela
wafike katika eneo hilo na kuwatawanya watu waliokuwa na hasira kali
na kuuchukua mwili wa marehemu kwenda kuuhifadhi katika chumba cha
kuhifadhia maiti kilichopo katika kituo cha afya cha Laela na wazazi
wa mtoto huyo kuwaweka rumande ili kuwaokoa na wananchi wenye hasira
kali.


Kuteleza si Kuanguka, Chidi Benz Asaidiwe...Nape Moses Nnauye Upo Wapi?

$
0
0
Katika mitandao ya kijamii Jumamosi iliyopita kulisambaa picha za rapa Chidi Benz ambazo zinamuonyesha jinsi alivyokonda na kupoteza ule mwili wake wa kuvutia aliokuwa nao zamani.

Mkali huyo wa wimbo Dar es Salaam Stand Up, anakubalika na vijana wengi kutokana na uwezo wake wa kuandika pamoja na kuchana. Lakini miaka ya hivi karibuni alianza kubadilika baada ya kujiingiza kwenye matumizi ya madawa ya kulevya.

Oktoba 24 mwaka 2014, Chidi alikamatwa na madawa ya kulevya katika Uwanja wa Ndege wa JK Nyerere wakati akielekea jijini Mbeya kwa ajili ya show. Lakini kesi hiyo ilimalizika miezi michache baadaye baada ya kuamriwa na mahakama kulipa faini.

Tukio hilo liliwafanya wasanii mbalimbali kuzungumzia hali hiyo huku wakimshauri kuachana na matumizi ya madawa ya kulevya. Ray C ambaye ni mmoja kati ya waathirika janga hilo ambaye kwa sasa yupo kwenye tiba ya methadone, aliamua kumshauri Chid Benz.

“Pole kaka yangu Chidi Benz. Naumia kuona tatizo uliokuwa nalo bado haujalitafutia jibu la kutatua tatizo lako. Mimi ni dada yako natumeshafanya kazi pamoja, tatizo ulilonalo na mimi nilishakuwa nalo na niliweza kulitatua sababu nilijitambua na kutafuta suluhu, nimejaribu kila njia kukushauri badala yake ukaja na rungu la kimasai na kunitandika nalo nyumbani,” aliandika Ray C kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Hata hivyo Chidi Benz aliendelea na harakati zake huku akijinadi katika vyombo vya bahari kwamba tayari ameshaachana na matumizi ya madawa ya kulevya. Lakini watu wake wa karibu pamoja na marafiki zake walikuwa wanadai kwamba bado hajaacha. Lakini Jumamosi hii akiwa katika kipindi cha Da Weekend Chart Show cha Clouds TV, Chidi amelionekana amechoka zaidi huku akiowamba wadau mbalimbali kumsaidia.

“Matatizo yangu na stress zangu ambazo niko nazo zinanisababishia mwili wangu unapungua kwasababu siko okay, siko poa, siko sawa yaani,” alisema.

Mmoja kati ya wasanii wakongwe wa muziki wa Hip Hop, Afande Selle, alionyesha kusikitishwa na jinsi madawa ya kulevya yanavyomaliza nguvu kazi ya taifa. 
“Yanapita kwa njia gani madawa ya kulevya hapa nchini? Anayasambaza nani mitaaani kote mitaani? Madawa ya kulevya hayaleti maendeleoooo,madawa ya kulevya yanaua masela leooooo,” alisema Afande Selle.

Pia wadau mbalimbali wamewataka watu pamoja na wasanii wenzake kumsaidia huku Arnold Kayanda, mtangazaji wa BBC Swahili akisema amelipokea kwa masikitiko suala hilo.

“Kama picha hii ni rafiki yangu Chidi Benz kama nilivyotaarifiwa, kwa hisani yenu wote naomba kila mtu kwa nafasi yake amsaidie. Mimi niko mbali lakini nikirudi nitakutana naye,” alisema.

Licha ya wadau mbalimbali kutaka asaidiwe lakini bado tunaona hakuna msaada wa haraka ambao mpaka sasa umechukuliwa ili kumuokoa Chidi Benz. Serikali ya Magufuli ni sikivu sana, bila shaka kupitia Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo inayoongozwa na Waziri kijana mpenda sanaa, Nape Moses Nnauye ataliangalia suala hili.

Salim Jecha Aendesha Uchaguzi Kutoka Mafichoni Zanzibar.....

$
0
0
Hatimaye  uchaguzi mkuu wa marudio Zanzibar Umefanyika Jana huku Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (ZEC), Jecha Salim Jecha akishindwa kuonekana hadharani kuzungumzia uchaguzi huo.

Kwa kawaida, kama ilivyokuwa katika uchaguzi wa awali uliofanyika Oktoba 25 kabla ya kufutwa siku tatu baadaye, Jecha alitarajiwa kuwa mstari wa mbele na kuzungumza na waandishi wa habari kwa nia ya kutoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali kuhusiana na uchaguzi huo.

Hata hivyo, katika tukio nadra kuwahi kutokea hapo kabla, Jecha aliendelea kuadimika na hadi kufikia jana jioni, taarifa zake kwa umma zilitolewa kupitia taarifa iliyosambazwa kwa vyombo vya habari na wasaidizi wake tu huku yeye mwenyewe akiendelea kutoonekana hadharani.


Kichanga Mwingine Adaiwa Kufariki Dunia Kwa Uzembe Mkoani Mwanza

$
0
0
Matukio ya wajawazito kupoteza watoto kwa madai ya uzembe wa wahudumu wa afya yameendelea kuugubika Mkoa wa Mwanza baada ya mkazi wa Nyarawambo wilayani Sengerema Tatu Muhangwa, kujifungua na mtoto wake kufariki kwa kukosa huduma.

Mama mzazi wa Tatu, Vumilia Nailon alisema mjukuu wake alifariki baada ya wahudumu wa afya katika Zahanati ya Ngoma ‘B’ iliyopo Kata ya Nyamatongo wilayani Sengerema, kuchelewa kumhudumia.

Mhudumu wa afya aliyekuwa zamu, Helena Mulwisha alisema alishindwa kumhudumia mjamzito huyo kutokana na kubaini kuwa mtoto alikuwa kakaa vibaya tumboni na kuwashauri kumpeleka hospitali ya wilaya kwa msaada zaidi.

Nailon alisema: “Nilimfikisha mgonjwa wangu zahanati juzi, saa kumi na moja alfajiri, lakini hadi saa tatu hakuwa amepatiwa huduma yoyote hadi alipojifungua mwenyewe bila msaada na mtoto kufariki.

“Mmoja wa wahudumu wa afya aliyekuwapo alishindwa kumhudumia baada ya kugundua mtoto amekaa vibaya tumboni na yeye hana utaalamu wa kumsaidia.”

Alisema Mulwisha aliwashauri kumpeleka mgonjwa hospitali ya wilaya kwa sababu wauguzi na madaktari walikuwa wakihudhuria semina.

“Baada ya kukosa gari ya kumuwaisha hospitali, tuliamua kutembea kwa miguu umbali wa kilomita mbili, lakini hatukufika baada ya magonjwa wangu kujifungulia njia kwa msaada wa wasamaria wema na mtoto kufariki,” alisema Vumilia.

Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya ya Sengerema, Dk Henry Nyamete alisema ofisi yake inachunguza tukio hilo na kwamba itachukua hatua za kinidhamu dhidi ya mhudumu wa afya aliyekuwa zamu siku hiyo kwa kushindwa kuwajibika kwa kuita gari la wagonjwa ili kumuwahisha mjamzito huyo hospitali kwa matibabu zaidi.

Maalim Seif Afunguka wakati Wazanzibar wakipiga Kura........"Kilichotokea Zanzibar ni mipango iliyopangwa na CCM"

$
0
0

Aliyekuwa Mgombea Urais kupitia Chama cha Wananchi (CUF), Oktoba 25, mwaka jana, ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, amesema hatma ya Wazanzibar iko mikononi mwa Chama Cha Mapinduzi (CCM).



Maalim Seif alitoa kauli hiyo baada ya kuulizwa ni nini hatma ya Zanzibar baada ya uchaguzi wa marudio uliofanyika jana.


“Mimi sijui, waulizeni CCM wao ndiyo wametengeneza hali hii, wao ndiyo wamekusudia na wanajua wanaipeleka wapi nchi hii, watasema wao,” alisisitiza Maalim Seif.


Aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutembelewa na Vijana wa Baraza la Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema-Bavicha jijini Dar es Salaam jana kumjulia hali.


Baada ya kufutwa kwa uchaguzi wa Oktoba 25, mwaka jana, hali ya kisiasa ya Zanzibar imedaiwa kuwa tete haswa kutokana na CUF kudai hawatambui kufutwa kwa uchaguzi huo msimamo wao wakitaka mshindi atangazwe.


Maalim Seif alisema CCM wanafahamu wazi kwamba mshindi aliyeshinda katika uchaguzi wa wa Okotoba 25, ni nani, lakini wameamua kufanya hivyo na kuifikisha Zanzibar hapo ilipo sasa.


Alisema miaka mitano iliyopita kulikuwa kumepatikana maridhiano Zanzibar na walikuwa wameanza kwenda vizuri, lakini kinachoonekana hivi sasa wameanza kuwarudisha nyuma kwa kuvuruga tena maridhiano hayo na kuanza kuleta uhasama.


“Hapo nyuma kulikuwa na uhasama wa kisiasa Zanzibar halafu ukaisha, lakini hivi sasa wanaurudisha, CCM ndiyo wameamua iwe hivyo,” alisema Maalim Seif.


Kadhalika, Maalim Seif alisema anaamini Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (Zec), Jecha Salim Jecha, ametumwa kuitafutia kura CCM.


“Jecha ametumwa kuitafutia kura CCM, lakini ijulikane kwamba hata wafanye vyovyote watakavyofanya, Wanzanzibari ndani ya mioyo yao, wanafahamu Rais wao ni mimi,” alisema Maalim Seif na kuongeza:


“Kinachotokea Zanzibar ni mipango iliyopangwa na CCM ambao pamoja na kwamba wanamfahamu mshindi ni nani katika uchaguzi wa mwaka jana, lakini wameamua kufanya hicho wanachofanya hivi sasa.”


Aidha, alisema kwa sasa hataki kusema chochote, isipokuwa anasubiri Rais atangazwe.


Maalim Seif yuko jijini Dar es Saalam kwa mapumziko mafupi baada ya kuugua na kuruhusiwa kutoka hospitali zaidi ya wiki moja iliyopita.

Breaking News: Tume ya Uchaguzi Zanzibar Yamtangaza Dr. Ali Mohammed Shein Kuwa Rais wa Zanzibar

$
0
0
Breaking News: Tume ya Uchaguzi Zanzibar Yamtangaza Dr Shein Kuwa Rais wa Zanzibar
DR SHEIN ASHINDA URAIS ZANZIBAR, KURA ALIZOPATA 299, 982 SAWA NA 91% YA KURA ZOTE ZILIZOPIGWA.

Breaking News: Ajali Mbaya Yatokea Msafara wa Wabunge Kamati ya Tamisemi Bagamoyo...Lori Laparamia Msafara Vifo Vitano Vimeripotiwa

$
0
0
Msafara wa Wabunge wa kamati ya Tamisemi wapata ajali katika eneo ya mteremko wa kerege. Watumishi 5 wa Halmashauri ya Bagamoyo na dereva wamefariki ila wabunge wamepona wote. Hii ni baada ya Lori kuparamia msafara wao. Mungu azilaze roho za marehemu mahala pema peponi.

Hivi Ndivyo Rais Magufuli Alivyosalimisha Silaha zake Polisi Baada ya Paul Makonda Kutoa Maagizo Kwa Wenye Silaha Wote

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amekuwa mtu kwanza kutekeleza agizo la Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam la kuhakiki silaha, ambapo bunduki zake mbili aina ya Shortgun na Pistol zimehakikiwa nyumbani kwake Ikulu Jijini Dar es salaam.

Uhakiki huo umefanywa na maafisa wa Jeshi la Polisi wakiongozwa na Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es salaam, Kamishna Simon Sirro.

Akizungumza baada ya kukamilika kwa zoezi hilo, Rais Magufuli amempongeza Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam na Jeshi la Polisi kwa kuendesha zoezi la uhakiki wa Silaha, na ametoa wito kwa watu wote wanaomiliki silaha nchi nzima kuhakikisha zinahakikiwa.

Dkt. Magufuli pia amelitaka Jeshi la Polisi kuongeza juhudi za kukabiliana na watu wanaojihusisha na vitendo vya uharifu ili kutokomeza kabisa vitendo hivyo.

"Ni aibu kumuona askari polisi mwenye silaha ananyang'anywa silaha, ni aibu, na nasema hiyo ni aibu, mpaka jambazi akunyang'anye silaha na wewe una silaha?" Amehoji Rais Magufuli

Kwa upande wake Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es salaam Kamishna Simon Sirro, amemshukuru Rais Magufuli kwa kuunga mkono zoezi hilo na amesema Jeshi la Polisi limejipanga kuhakikisha zoezi hilo linafanyika kwa mafanikio.

Katika hatua nyingine, Rais Magufuli ametaka pande zinazogombea kiti cha Umeya katika Jiji la Dar es salaam, kukamilisha mchakato wa kumpata Meya katika uchaguzi uliopangwa kufanyika kesho tarehe 22 Machi, 2016 badala ya kuendelea kurumbana.

Dkt. Magufuli amesema upande wowote uwe tayari kupokea matokeo ya uchaguzi huo, ili Meya apatikane na Jiji liweze kuendelea na mipango yake ya kuwahudumia wananchi bila vikwazo.

"Mahali tunapostahili kushinda kama tumeshinda tushinde kweli, lakini mahali tunaposhindwa napo tukubali kushindwa, na hiyo ndio demokrasia ya kweli" ameongeza Rais Magufuli

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiiweka silaha yake vizuri mara baada ya kuhakikiwa Ikulu jijini Dar es Salaam.

Waziri Mkuu Amwagiza CAG Kukagua Bandari na Benki ya CRDB......Makampuni 150 ya Uwakala Yafunguliwa

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali aende Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) ili akague taarifa za mapato ambazo zilikuwa zikilipwa na mawakala wa forodha na bandari kupitia benki ya CRDB lakini hazionekani kwenye mifumo ya benki.

Ametoa agizo hilo leo jioni (Jumatatu, Machi 17, 2016) wakati akizungumza na mamia ya mawakala wa forodha na bandari waliohudhuria mkutano aliouitisha ili kusikiliza kero zinazowapata katika utendaji kazi wao.

Akizungumza na mawakala hao kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam, Waziri Mkuu alisema kuna dalili za kutupiana lawama baina TPA na CRDB kuhusu malipo yaliyikuwa yakifanyika benki halafu fedha hazionekana na wakala anaidaiwa kuwa hajalipia mzigo wakati alishaulipia.

“Kimsingi bado liko tatizo baina ya Mamlaka ya Bandari pamoja na Benki ya CRDB. Naona kila mmoja hapa anamkana mwenzake. Nitamtuma CAG ili akafanye ukaguzi wa kina ili tujue ni nani kati yao amehusika na upotevu wa fedha,” alisema huku akishangiliwa na mawakala hao.

Alimwagiza pia Kaimu Mkurugenzi wa Bandari, Eng. Aloyce Matei aandae dispatch zote walizotumia kupokelea malipo za kuanzia mwaka 2015 na ikibidi aandae za kuanzia mwaka 2014 ili CAG anapozopitia aweze kupata picha halisi.

Vilevile, Waziri Mkuu alimwagiza Eng. Matei kuhakikisha wananunua mashine ya photocopy ili iwekwe kwenye chumba cha kupokelea stakabadhi za malipo ya benki (bank pay in slip) ili mteja anapoleta nakala ya benki aweze kutolewa photocopy na kubakia na nakala ya malipo aliyofanya,

Waziri Mkuu alisema Serikali inatambua bandari ni eneo nyeti katika kuinua uchumi na mapato ya nchi lakini pia ni eneo muhimu katika kutengeneza ajira. 

“Ninapenda niwahakikishie kuwa bado tutaendelea kukagua bandari hadi pawe safi. Hii bandari ni yenu na mtafanya kazi kama kawaida,” alisema.

Mapema, akizumgumza kwa niaba ya mawakala hao, Rais wa Chama cha Mawakala wa Forodha nchini (TAFFA), Bw. Stephen Ngatunga alieleza matatizo mbalimbali ambayo wao kama mawakala wa forodha wamekuwa wakikumbana nayo kuanzia ulipaji, utoaji wa mizigo na kuitaka Serikali iongeze nguvu katika kuikabilia sekta hiyo.

Alizikosoa baadhi ya sheria ambazo zinaruhusu wamiliki wa bandari kavu kumiliki pia makampuni ya uwakala wa forodha, sheria kadhaa zinazochangia kukwamisha utoaji wa mizigo bandarini, ukaguzi hafifu wa kwenye scanner na uwepo wa vituo vinane vya mizani kuanzia Dar es Salaam hadi Tunduma ambavyo vimegeuka kuwa kero kwa wasafirishaji wa mizigo kwenda nchi jirani.

Wakati huohuo, Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Eng. Edwin Ngonyani amesema Serikali imeamua kuyafungulia makampuni zaidi ya 150 ambayo yalikuwa yamefungiwa kufanya kazi za uwakala wa forodha kutokana na madai ya kuhusishwa na ukwepaji wa kodi.

“Hapa tumegundua kuwa wote siyo wasafi iwe ni mawakala, benki ama bandari. Mkurugenzi wa Bandari, kuanzia leo watu hawa waruhusiwe waanze kufanya biashara lakini nyaraka za nyuma zisiguswe hadi CAG atakapokamilisha uchunguzi wake,” alisema kuibua kelele za shangwe kwenye ukumbi huo.

(mwisho)

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU2 MTAA WA MAGOGONI,
S. L. P. 3021,11410 DAR ES SALAAM
JUMATATU, MACHI 21, 2016.

Diva Loveness Akiri Kukumbwa na Misukosuko ya Mapenzi na Kuumia Sana...Kurudi Kwenye Muziki Kwa Kumshirikisha Chid Benz

$
0
0
Mtangazaji wa Clouds FM, Diva amesema Chidi Benz atamsaidia kuandika mashairi ya wimbo wake mpya alioupa jina ‘Kosa Langu.’

Kupitia Instagram, Diva amedai kuwa Mr Blue pia atahusika kwenye wimbo huo mpya unaovunja kimya chake cha zaidi ya miaka miwili kwenye muziki.

“@lamarfishcrab vibin this weekend , Nilikutana na Chid Benz Juzi, akaniahidi kuniandikia wimbo na Kusisitiza ndani ya Mwezi huu nifanye RNB Moja amazing,” ameandika Diva.

“Sometimes kuimba inahitaji hisia sana, hapa kati nimekubwa na misukosuko ya Mapenzi nikaumia sana , and i said why nat Put this into a love song … yes nikapata melody and the verse and chorus Paw jus like that .. called Lamar like YOH ‘ ts about time .. lets jus do the hook up, am very comfy when it comes to studio session with Lamar , matter fact ts been a while and me and blue this year tulikaa and discuss the return,” ameongeza.
“Then nikaanza andika , wimbo wangu verse ya Kwanza nimeandika Mwenyewe , Verse ya Pili itaandikwa na Chidi Benzi and Mr Blue Bayser atamalizia Na Rap Music , strictly RNB ‘ Leo usiku tunaanza kazi ya Kurekodi wimbo Unaitwa ‘ Kosa Langu ‘ saa 6:15 usiku , Production ya Fishcrab Cook Out. Utakuwa ni wa Kiswahili kilichounganika na kiingereza, a very beautiful song wish muuskize and Utatoka week 2 Mbele, after a week itakuja video then … kuusambaza All over Africa , so stay Tuned, always been a fan of Chidi and Mr. Blue, Very Talented…. But Kosa Langu is jus tooo emotional , huwezi amini i crieeed wakati naandika , trials and tribulations , love this and that but sucha happy song , Extremely.”
“I believe in Chiddi Benz Chuma, I believe in his Talent as well , amenisisitiza sana Kufanya this song .. and y’all kno me i live it to the fullest and always givin a shot .. i live to Please My heart … And wanna Be Happy man, Music is the way forward ya Happiness , This time hits me to the core .. and i can’t deny it ama go with The flow YO… lemme.”

Kabla ya hapo Diva aliwahi kuachia wimbo Piga Simu aliomshirikisha Diamond na Mgonjwa kwa raha zako aliomshirikisha Mr Blue.

Mwandishi wa Mwananchi na Sauti ya Ujerumani Salma Said Aelezea Jinsi Alivyotekwa na Wanaume Wawili....

$
0
0
Mwandishi wa habari wa Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL) na DW, Salma Said amedai alitekwa na wanaume wawili baada ya kumkamata na kumuingiza kwenye gari lao kisha kuondoka naye na kumpeleka kusikojulikana.

Salma aliyetekwa Ijumaa iliyopita na watu hao katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) akitokea Zanzibar kwa ajili ya kuchunguzwa afya yake kwenye moja ya hospitali za jijini Dar, alisimulia mkasa huo jana mbele ya waandishi wa habari huku akimwaga machozi.

Alisema alipoteremka uwanjani hapo, alimpigia simu dereva wake amfuate na wakati akimsubiri, ndipo wakatokea watu hao.

Salma alisema watu hao walimfunga mtandio wake mweusi usoni ili asibaini mahali walikokuwa wakimpeleka na kumfungia chumbani .Alisema ndani ya chumba hicho kulikuwa na vitambaa.

“Waliponiingiza ndani ya chumba kile siku ya kwanza, wakanifungua tambala usoni kwa hivyo nikawaona nyuso zao, mmoja alikuwa na kovu shavuni, mrefu na mwingine mweupe kidogo, waliniweka kule ndani bila kupata chakula chochote,” alisema.

Salma alisema alitakiwa kurudi Zanzibar kwa ajili ya kuripoti marudio ya Uchaguzi Mkuu wa marudio uliofanyika juzi, lakini alishindwa baada ya watu hao kumteka na kumfungia kwenye chumba hicho.

Alidai kuwa watu hao walimwambia watamuachia baada ya uchaguzi huo kufanyika na mgombea wa CCM kutangazwa kuwa mshindi.

Katika mkutano huo na waandishi wa habari uliofanyika katika ofisi za Baraza la Habari Tanzania(MCT), Salma aliongozana na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Theophil Makunga, Katibu Mtendaji wa MCT, Kajubi Mukajanga na Mratibu wa Kitaifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Bara (THRDC), Onesmo Ole Ngurumwa, ambao kwa pamoja walieleza kupinga ukatili huo huku wakiliomba Jeshi la Polisi kuwasaka wahalifu waliohusika.

“Walinisababishia maumivu makali, walinipiga mabuti na makofi huku wakiniambia maneno ya vitisho kama ilivyokuwa kwa Dk Ulimboka na Kibanda,” alidai Salma.

Kabla ya watekaji hao kumrudisha katika eneo walilokuwa wamemteka, Salma alidai kuwa watu hao walimpiga kila walipoingia na kutoka nje ya chumba alichowekwa na kumsababishia apumue kwa tabu.

Akijibu swali la mwandishi wa habari aliyetaka kupata ufafanuzi wa taarifa za uvumi wa kujiteka mwenyewe, Salma alijibu swali hilo huku akidondosha machozi: “Hakuna sababu ya kusema uongo, mimi ni Mwislamu na dini yangu inakemea kufanya hivyo.”

Pia, alisema amefanya kazi kwa miaka zaidi ya 20 na matukio ya vitisho yalianza alianza kuyapata muda mrefu kwa kupigiwa simu, kutumiwa meseji na kufuatwa nyumbani kwake.

Salma ambaye alizungumza huku akionyesha ushahidi wa meseji za makundi ya mitandao yanayojadili kufurahishwa na kutekwa kwake, alisema kujiteka ni kauli zisizokuwa na uhusiano wowote na ukweli, kwani alijitambulisha kuwa mwandishi mtetezi wa haki za binadamu na siasa ambazo zinazokinzana na maslahi ya wachache.

Wakati huohuo; Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Siro alisema ni mapema kuzungumzia tukio la kutekwa kwa Salma kwa madai kuwa bado wanaendelea kufanya uchunguzi.

Pendeza na Kessy Products..Pata Dawa za Asili Zisizo na Madhara Wala Kemikali Yoyote

$
0
0

PENDEZA NA KESSY PRODUCT.
PATA DAWA ZA ASILI ZISIZO NA MADHARA WALA KEMIKALI YOYOTE,
NA MATOKEO KUANZIA WEEK (2) ADI (4) NAKUENDELEA

1) KUTOA MVI SUGU 80,000/
2) KUREFUSH NYWELE NA UKATIKAJI 80,000/
3) TENGENEZA SHEPU YAKO FIGA UMBO (8) KWA DAW...
@ KUPAK 70,000/
@ KUNYWA NA VIDONGE 130,000/
4) TENGENEZA MGUU KAMA CHUP YA BIA 60,000/
5) PUNGUZA KITAMBI NA MANYAMA UZEMBE
@) KUNYWAA 90,000/
@) KUPAKA 70,000/
6) PUNGUZA MWILI MZIMA PAMOJA NA KILO
@) MAJAN 130,000/
@) VIDONGE 150,000/
7) PUNGUZA MAZIWA NA YASIMAME 60,000/
8) ENGEZA MAZIWA NA SAIZ UNAYOPEND 60,000/
9) ONGEZA MWILI MZIMA NA KUKUPA HAMU YAKULA (WEMBAMB) 80,000/
10) TOA MICHIRIZI SUGU PIA NA ILE YAKUJIFUMGUA, 70,000/
11) TOA MAKOVU, CHUNUSI, WEUSI KATIKATI YA MAPAJA 50,000/
12) TOA NGIRI YA AINA ZOTE 70,000/
13) KUWA MWEUP MWILI MZIMA KUPAKA 80,000/PIA VIDONGE VIDONGE.
14) TOA VINYWELEO NA NDEVU 80,000/
15/ ONGEZA NGUVU ZA KIUME
@) JEL KUPAKA 60,000/
@) VIDONGE 80,000/
16) ONGEZA MAUMBIL KWA
@) HANDSM UP MASHIN 170,000/
@) JELI YAKUPAKA 100,000/
17) RUDISHA HAM YA TENDO 60,000/
18) RUDISHA USICHAN(BIKRA) 70,000/

TUPO DAR, K/KOO SINZA, MAPAMBAN, KWA MIKOAN T UTATUMA KWA MABAS, KWA ZENJ PIA KWA BOT ZA AZAM
CHAKUFANYA PIGA CM
0719955558.
0756259180.
0785371237.
AMA TU FOLLOW
@dr_kessy_product
@dr_kessy_product

Delivery kwa DAR ipo utaletewa popote ulipo

SOMA Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumanne ya March 22, Magufuli Atia Mguu Umeya Dar

$
0
0

SOMA Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumanne ya March 22, Magufuli Atia Mguu Umeya Dar

Mkuu wa Wilaya Lucy Mayenga Aihofia Kasi ya Magufuli..Ajisalimisha na Kumuomba Rais Asimchague Tena Ukuu wa Wiliya

$
0
0
Wakati Taifa likisubiri uteuzi wa wakuu wa wilaya huku wanaoshikilia nafasi hizo wakiwa katika chekeche kwa kuzingatia vigezo vitano, Mkuu wa Wilaya Iramba, mkoani Singida, Lucy Mayenga amemuomba Rais John Magufuli asimjumuishe kwenye orodha ya wakuu hao anayotarajia kuitangaza wakati wowote.

Rais Magufuli ameweka bayana vigezo atakavyotumia kufanya uteuzi wa wakuu hao wa wilaya ambavyo ni pamoja na suala la migogoro ya ardhi, tatizo la elimu hasa upungufu wa madawati, njaa na mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu alivyovitangaza wakati akizungumza na wazee wa Dar es Salaam na katika uteuzi wa wakuu wa mikoa, alizungumzia pia suala la wafanyakazi hewa ambao wamekuwa wakilipwa mishahara bila ya wahusika kuchukua hatua kudhibiti.

Akizungumza kwenye kikao cha UWT, Mkoa wa Shinyanga mwishoni mwa wiki, Mayenga ambaye pia ni mbunge wa Viti Maalumu alisema aliwasilisha ombi hilo binafsi kwa Rais Magufuli ili apate fursa ya kusimamia biashara zake alizosema zinazodorora kutokana na kubanwa na majukumu ya ukuu wa wilaya.

“Pamoja na ukuu wa wilaya, mimi pia ni mbunge na wakati huohuo ni mfanyabiashara; haya ni majukumu mengi kutekelezwa na mtu mmoja kwa wakati moja,”alisema Mayenga 

Aliwaambia wajumbe waliohudhuria mkutano huo uliofanyika katika Kata ya Nyamilangano, wilayani Ushetu kuwa biashara zake nyingi zilizopo mkoani Shinyanga zimedorora kutokana na kukosa usimamizi wake.

“Ombi hili nililitoa binafsi kwa Waziri Mkuu ambaye alinishauri kusubiri uteuzi; isitafsiriwe kwamba nimeogopa kasi ya utendaji ya Serikali ya Awamu ya Tano.Hapana! Nimeona ni vyema nibaki na ubunge na biashara zangu,” alisema Mayenga ambaye kitaaluma ni mwandishi wa habari.

Baadhi ya wanachama wa UWT waliohudhuria mkutano huo walimpongeza kwa uamuzi huo wakisema unapaswa kuigwa na viongozi wengine wenye majukumu mengi kwa kuachia watu wengine nafasi za kutumikia umma badala ya kung’ang’ania nafasi zote.

“Nampongeza Mheshimiwa Mayenga kwa uamuzi wake wa kuomba asiteuliwe tena kwenye nafasi ya ukuu wa wilaya kwa sababu itatoa fursa kwa watu wengine kutumikia nafasi hiyo,” alisema Selina Mkula.

Katika mkutano huo ambao Mbunge wa Ushetu, Elias Kwandikwa alitoa msaada wa mifuko 60 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa madarasa katika shule za msingi Nyamilangano na Mitonga pamoja na Shule ya Sekondari Kisuke, wanachama wapya 55 walijiunga na UWT.

Mbunge huyo pia aliahidi kutoa vyerehani 20 kwa makatibu kata wa UWT ili kusaidia harakati za maendeleo ya wananchi kwa kuanzisha vikundi vya kiuchumi katika kata zao.

Mahakama Yatupilia Mbali Maombi ya Kuzuia Uchaguzi wa Meya wa Jiji la Dar Es Salaam...

$
0
0
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imeamuru uchaguzi wa meya na naibu meya wa Jiji la Dar es Salaam, kufanyika leo kama ilivyopangwa.

Hakimu Mkazi Mkuu, Warialwande Lema alitoa uamuzi huo jana akijibu maombi yaliyokuwa yamewasilishwa na walalamikaji, Suzan Massawe na Saad Mohammed Kimji kupitia wakili wao, Elias Nawela dhidi ya Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam.

Wakati Mahakama ikitoa uamuzi huo, Rais John Magufuli amezitaka pande zinazogombea kiti cha umeya Dar es Salaam, kukamilisha mchakato huo katika uchaguzi uliopangwa kufanyika leo, badala ya kuendeleza malumbano.

Rais alitoa kauli hiyo jana Ikulu wakati akihakiki silaha zake. Alisema pande zote ziwe tayari kupokea matokeo ya uchaguzi huo, ili meya apatikane na jiji liweze kuendelea na mipango yake ya kuwahudumia wananchi bila vikwazo.

“Mahali tunapostahili kushinda kama tumeshinda tushinde kweli, lakini mahali tunaposhindwa napo tukubali kushindwa, hiyo ndiyo demokrasia ya kweli,” alisema Rais Magufuli.

Akitoa uamuzi wa Mahakama uliokuwa ukisubiriwa kwa hamu na walalamikaji na walalamikiwa, Hakimu Lema alisema Mahakama haikuona sababu za msingi kati ya zilizowasilishwa na walalamikaji kuishawishi kuzuia kufanyika kwa uchaguzi huo.

“Siyo busara kuendelea na sababu ambazo hazijathibitishwa,” alisema Hakimu Lema alipokuwa akitoa uamuzi huo na kuongeza kwamba kwa kukosekana orodha inayoonyesha majina ya wapigakura, haijulikani kama waleta maombi ni miongoni mwa wapigakura au la.

Hakimu Lema alisema walalamikaji hawakuwa makini tangu awali walipofungua shauri hilo, Februari 5 kwani hawakutokea mahakamani hadi Februari 14, wakili wao Nawela alipojitokeza na kuomba nakala ili awapelekee wajibu maombi jambo linalofanya washindwe kuishawishi Mahakama kuwapa haki yoyote kwa kuwa hawakufuatilia shauri lao tangu awali.

Mapema jana mchana, wakili Nawela aliiomba Mahakama itoe zuio la kufanyika uchaguzi huo na iamuru hali ibaki kama ilivyo hadi pale kesi ya msingi itakaposikilizwa na kutolewa uamuzi kwa madai ya kwamba walalamikaji katika shauri hilo, hawajapewa haki yao ya kualikwa kushiriki katika uchaguzi huo.

Alidai kuwa iwapo uchaguzi huo utafanyika, basi maombi yao na kesi ya msingi yatakuwa hayana maana.

Akijibu hoja hizo, wakili Jumanne Mtinange kwa niaba ya Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, aliiomba Mahakama kuyaondoa maombi hayo kwa madai kuwa hayana msingi wowote.

Mtinange alidai hakuna uthibitisho wowote au orodha ya wapigakura kuonyesha kwamba waleta maombi wamekosekana, hivyo maombi ya kutaka hali ibaki kama ilivyo hayana uzito wowote.

Alisema maandalizi ya uchaguzi yana gharama na kwamba ni mara ya tatu umeahirishwa, hivyo kuomba uchaguzi wa leo uendelee kama kawaida.

Timu ya mawakili wa Chadema wakiongozwa na Wakili Peter Kibatala, Omary Msemo na John Mallya walikuwa muda wote wakifuatilia kesi hiyo mahakamani hapo.

Kwa uamuzi huo, kinyang’anyiro cha kugombea umeya sasa kimebaki kwa Isaya Mwita wa Chadema na Omary Yenga wa CCM wanaowania nafasi hiyo katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika leo katika Ukumbi wa Karimjee baada ya kuahirishwa mara tatu kwa sababu mbalimbali ikiwamo zuio batili la Mahakama kabla ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Tamisemi), George Simbachawene kuiagiza uchaguzi huo ufanyike kabla ya Machi 25.

Baadaye, Kaimu Mkurugenzi wa Jiji, Sarah Yohana alitangaza na kutoa barua kwa wajumbe husika juu ya wito wa kikao cha Baraza la Madiwani kitakachokuwa na ajenda ya uchaguzi akisema wajumbe 163 watashiriki kupiga kura, kati yao 87 ni kutoka Ukawa na 76 CCM.

Mwanamuziki Diamond Platnumz Ateketeza Sh.Mil 100 Ulaya Akiwa na Familia yake

$
0
0
Kufuru! Ndilo neno pekee linaloweza kuakisi takriban Sh. milioni 100 ambazo Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ ameziteketeza akiwa na msururu mrefu wa wanafamilia wa Wasafi Classic Baby (WCB) barani Ulaya, akianzia nchini Ujerumani kufanya shoo sambamba na kula bata, Wikienda linakupa habari kamili.

Diamond aliyeambatana na wanafamilia kama 14 wakiwemo Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’, mama yake mzazi, Sanura Kassim ‘Sandra’, Tiffah (mwanaye), Romy Jons (DJ wake), Kifesi (mpigapicha), meneja (Salam), mke wa Tale (meneja Tale), madansa wanne na dada mmoja ambaye ni ndugu wa Zari, walikwea pipa na kufikia Frankfurt, Ujerumani.

TUJIUNGE NA CHANZO
Chanzo kilicho karibu na familia ya Diamond kilichoambatana na msafara huo kilipenyeza ‘ubuyu’ kuwa, kwa kushirikiana na uongozi wake, Diamond alitenga si chini ya Sh. milioni 100 ili kufanikisha ziara hiyo aliyoipa jina la Europe Tour ambapo inatarajiwa kuchukua takriban wiki tatu.
“Diamond ni noma, ameandaa mkwanja usiopungua milioni 100 kwa ajili ya msafara wake. Fedha hizo zitatumika kuanzia usafiri wa ndege kwenda na kurudi, chakula, shopping na malazi kwa kipindi chote cha wiki tatu atakachokuwa Ulaya,” kilisema chanzo hicho na kuongeza:

WATUA FRANKFURT
“Walitua kwenye Uwanja wa Ndege wa Frankfurt, Ijumaa (iliyopita), walichelewa kutoka uwanja wa ndege kwa sababu walikuwa na mizigo mingi lakini pia bahati mbaya kitoroli cha kumbebea Tiffah kilipotea hivyo uongozi ulichukua muda mrefu kukitafuta hadi walipokipata.”

AMEFUATA NINI NCHINI HUMO?
Chanzo hicho kiling’amua kuwa, Diamond alikuwa na ziara ya kimuziki barani Ulaya lakini kwa kuwa imeangukia wakati wa Sikukuu ya Pasaka, aliamua kuambatana na mama yake, mpenzi wake (Zari) na mwanaye ili wakainjoi.
“Ameona aitumie ziara hii ya kimuziki pia kuinjoi. Kila atakapokuwa anapita atakuwa anapata muda wa kula bata za nguvu, kufanya shopping za hapa na pale ambapo kama unavyojua tena huyu Diamond ndiyo Rais wa Wasafi, kila anapotua na msafara mzima unalala kwenye hoteli ya kifahari ambayo si chini ya nyota tatu.

SHOO ZOTE HIZI HAPA
“Jumamosi (iliyopita) ndiyo ataanza kupiga shoo Franfurt, Machi 25, atakuwa Oslo (Norway), Machi 26, atakuwa Bergen (Norway), Machi 27, atakuwa Stockholm (Sweden), Aprili 1, atakuwa Bruxelles (Belgium), Aprili 2 ni Stuttgart (Ujerumani), Aprili 8 ni Helsink (Finland) na Aprili 9 atamalizia Copenhagen (Denmark),” kilisema chanzo hicho.


SHOO ZITAFIDIA MATUMIZI?
Ijumaa Wikienda lilipokibana chanzo hicho kutaka kujua Diamond ataingiza shilingi ngapi kama malipo ya shoo hizo ili kufidia au kuzidi matumizi ya shilingi milioni 100, kilisema hakina uhakika wa malipo ya shoo kama yatafidia gharama lakini kikashauri aulizwe Diamond mwenyewe.
“Dah! Kuhusu malipo ya shoo, mimi kwa kweli sijui japo naamini lazima itamlipa, Diamond siyo mpuuzi aje huku atumie hela nyingi kuliko fedha atakazolipwa kwenye shoo. Wote atupandishe ndege daraja la kati. Atakuwa ameshafanya hesabu na kuona anabaki na faida katika ziara ndiyo maana akakubali kuja na msafara mkubwa, ila kama vipi muulize mwenyewe,” kilisema chanzo hicho.

DIAMOND HUYU HAPA
Wikienda lilimtafuta Diamond kupitia Mtandao wa WhatsApp ili kutaka alithibitishe ukweli wa yeye kuteketeza shilingi milioni 100 katika ziara hiyo ambapo alikataa kuzungumzia malipo aliyoyapata kwa shoo hizo lakini akadai kuwa zinaweza kufika au hata zaidi kulingana na starehe watakazoamua kuzifanya.

“Siwezi kusema moja kwa moja kama inafika au la lakini inaweza kufika na hata zaidi. Wewe chukulia mimi tu na familia yangu (yeye, Tiffah, Zari na ndugu zake) nimetenga kama dola 30,000 (zaidi ya Sh. milioni 65) kwa ajili ya usafiri, malazi na shopping za hapa na pale sasa vipi kuhusu timu nzima ya madansa, meneja na wengine?” alihoji Diamond.

UCHUNGUZI WA WIKIENDA
Gazeti hili lilifanya uchunguzi wa wastani wa bei ya nauli pekee kutoka Bongo hadi Ujerumani kwa daraja la chini (Economy Class) si chini ya shilingi milioni 3 kwa mtu mmoja. Daraja la kati (Business Class) si chini ya shilingi milioni 5 kwa mtu mmoja kwa maana ya kwenda na kurudi Bongo.

MCHANGANUO ZAIDI
Kama wamepanda watu wote (14) kwenye Economy Class maana yake watakuwa wametumia si chini ya Sh. milioni 42 kwa usafiri pekee. Lakini endapo watakuwa wamepanda Business Class watakuwa wametumia si chini ya Sh. milioni 70.

INAWEZEKANA!
Kama familia ya Diamond imetumia Sh. milioni 65 kwa malazi, usafiri na shopping ni zaidi ya robo tatu ya Sh. milioni 100 hivyo ni dhahiri timu iliyosalia inaweza kuwa imetumia zaidi ya Sh. milioni 30 kwa nauli, malazi na chakula, jambo ambalo halijawahi kutokea Bongo kwa staa yeyote.

Chanzo: Global Publishers

Breaking News: Milipuko ya Mabomu yatokea uwanja wa ndege Brussels

$
0
0

Milipuko miwili imetokea katika uwanja wa ndege wa Zaventem mjini Brussels.

Moshi umeonekana ukitanda angani kutoka kwa moja ya majengo katika uwanja huo.

Serikali ya Ubelgiji imethibitisha kwamba kunao watu waliojeruhiwa lakini haijasema idadi.

Watu wameondolewa kutoka kwenye uwanja huo na safari za ndege kutua au kupaa kutoka uwanja huo kukatiz

Vyombo vya habari nchini humo vinaripoti kwamba kuna watu wamejeruhiwa katika ukumbi wa kuhudumia watu wa safari za kuondoka nchini na kwamba milipuko ilitokea karibu na meza ya shirika la ndege la American Airlines.

Haijabainika ni nini chanzo cha milipuko hiyo.

Milipuko hiyo imetokea siku nne tu baada ya kukamatwa kwa mshukiwa mkuu wa mashambulio ya Paris ya mwaka jana ambayo yalisababisha vifo vya watu 130.

TUHUMA za Rushwa Kamati ya Bunge..Mbunge Zitto Kabwe Amejiuzulu Ujumbe wa Kamati ya Huduma ya Jamii

$
0
0

TUHUMA ZA RUSHWA KAMATI ZA BUNGE: Mbunge Zitto amejiuzulu ujumbe wa Kamati ya Huduma za Jamii.

Amwandikia Spika kumuomba achunguze na achukue hatua kali dhidi ya yeyote atakayekutwa kuhusika na vitendo vya rushwa.
Viewing all 104809 articles
Browse latest View live




Latest Images

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596344.js" async> </script>