Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104799 articles
Browse latest View live

Ted Cruz ajitoa mbio za urais Marekani..Donald Trump Azidi Kupeta

$
0
0
Muwania urais wa Marekani Ted Cruz ametangaza kuachana na kampeni za urais kwa tiketi ya chama cha Republican, baada ya kushindwa vibaya na Donald Trump katika kura za Indiana.

Bw. Trump ambaye ni mfanyabiashara wa Jijini New York, ambaye si maarufu kwa wengi kwenye chama chake, sasa ni kama amejihakikishia kuteuliwa kuwania urais wa Marekani.

Mapema Bw. Cruz alimuiita Bw. Trump kuwa ni mtu muongo ambaye hastahili kuwa rais wa Marekani.

Katika mbio za kuwani urais kwa chama cha Democratic, Bw. Bernie Sanders anatarajiwa kumshinda Bi. Hillary Clinton, Indiana.

Maelfu Wajitokeza Kumuaga na Kumzika Marehemu Papa Wemba

$
0
0
Mwanamuziki Papa Wemba aliyefariki wiki iliyopita nchini Ivory Coast amefanyiwa ibada ya mazishi katika kanisa la kanisa kuu la Notre Dame Kinshasa ili kuweza kuhifadhiwa katika nyumba yake ya milele leo.

Ibada hiyo imefanyika baada ya wananchi kupewa fursa ya kuuaga mwili wa nguli huyo wa muziki kwa muda wa siku tatu baada ya kufikishwa nchini humo kutokea Ivory Coast.
Gwiji huyo wa muziki wa lingala alizaliwa mnamo Juni 14 mwaka 1949, katika eneo la Lubefu, Wilaya ya Sankuru nchini DR Congo.

Baadhi ya nyimbo zake ambazo ziliwika sana ni pamoja na Mwasi, Show me the way, Yolele, Mama, P na Rail On.

Aidha Papa Wemba alifariki baada ya kuzirai wakati akiendelea na tamasha mjini Abidjan Ivory Coast April 24 2016.


EDWARD Lowassa Achomoza Kamati Kuu ya CCM Dodoma..

$
0
0
Ukimya wa aliyekuwa mgombea wa Urais wa UKAWA,Edward Lowassa umezua mjadala kwenye mkutano wa Kamati Kuu ya CCM.Kikao cha Kamati Kuu kimefanyika jana hapa Dodoma. 

Mjadala ulianza pale Mwenyekiti Kikwete alipochagiza maelezo yake ya chama kuendelea kufanya maandalizi ya chaguzi zijazo na kutobweteka. Mwenyekiti alisema kuwa Lowassa bado ana uungwaji mkono na nguvu ya kisiasa na hutumia ukimya kujijenga zaidi.

Mwenyekiti alionya kuwa Lowassa hakufika mwisho na chama chapaswa kuutazama ukimya wake wa kuchangia na kutoa hoja juu ya Serikali ya Rais Magufuli kwa jicho la tatu. Wajumbe wote wa KK walikubaliana na Mwenyekiti Kikwete.

Wakati huohuo,Rais Magufuli ameaswa kuwa 'mpole kiasi' atakapoukwaa uenyekiti wa taifa wa CCM mnamo mwezi Juni mwaka huu. Imesemwa kuwa wanachama wa chama cha siasa hutendewa mambo kwa upole ili wabaki chamani na kukijenga chama. KK imeunga mkono hatua za Rais na Serikali yake kutumbua majipu!

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Dodoma)

Vuai Nahodha: Serikali ya Muungano na Serikali ya Zanzibar zapaswa Kugawana Mapato

$
0
0
Kwenye video anaongea anasema ''Hali ya mtafaruku wa kisiasa Zanzibar unatokana na ukosefu wa rasilimali na hali duni ya kiuchumi , hivyo uchumi mkubwa ni sharti usaide uchumi mdogo, serikali ya muungano na serikali ya mapinduzi zapaswa kugawana mapato, amani ya Tanzania inategemea sana mustakabali wa uchumi wa Zanzibar''

Msikilize Hapa Chini:

Breaking News:Asha-Rose Migiro ateuliwa kuwa Balozi wa Uingereza

$
0
0
Dkt. Asha-Rose Migiro anakwenda kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Balozi Peter Kalaghe ambaye amerudishwa nyumbani.
Dkt. Asha-Rose Migiro ataapishwa kesho Alhamisi tarehe 05 Mei, 2016 katika Ikulu ndogo ya Chamwino Mkoani Dodoma.

DUDU Baya Achoka Maisha ya Umaarufu..'Nashindwa Hata Kununua Vitumbua'

$
0
0
Dudubaya kupitia kipindi cha Planetbongo amekiri kuwa kuna wakati anajutia maamuzi yake ya kutaka kuwa maarufu na kuwa maarufu kwani yanamfanya aishi maisha ambayo si yake kwani akifanya vitu vingine baadaye vinageuka stori mitaani na mitandaoni.

"Kuna wakati huwa nasema kwanini nilitaka kuwa star na nikawa star kwa sababu kuna wakati mwingine unatamani kufanya jambo fulani lakini unashindwa kufanya kutokana na umaarufu wako, maisha ya umaarufu magumu sana haya mambo yanatukuta hata mtaani mfano unaweza kuwa unakaa uswahilini unakaa Manzese, Tegeta, Mwananyamala mtu mwingine anaweza kukudharua kumbe ni maisha ya kawaida kama watu wengine. Mfano mzuri mimi napenda sana mihogo na vitumbua lakini nashindwa kwenda kununua mtaani kwani nikisema niende tayari watu wanaleta skendo mtaani," alisema Dudubaya.

Dudubaya anaonyesha kuwa maisha ya kuwa maarufu ni mzigo mzito kama ambavyo Fid Q alishawahi kusema kuwa 'u Superstar' ni mzigo wa mwiba ukiubeba utaumia

Millen Magese Afunguka 'Watanzania Tupende vya Kwetu'

$
0
0
Mwanamitindo wa Kimataifa kutoka Tanzania anayefanyia shughuli zake nchini Afrika Kusini na Amerika, ametoa witoa kwa watanzania, akiwataka kuwa wazalendo.

Kwenye ukurasa wake wa Instagram Millen Magese ambaye kwa sasa yupo mapumzikoni Jijini Dar es Salaam, amendika ujumbe kwa watanzania akiwaambia kuwa na upendo na kuthamini vya kwao, pamoja na kuvitangaza, huku akielezea matamanio yake ya kwenda mbuga ya wanyama ya Serengeti na Saadani.

“Tuwe na utamaduni wa kupenda vya kwetu na kusifia vya kwetu, na kutangaza vya kwetu......Tanzania is beautiful ..... Tutembelee vya kwetu .#SmallVacayInTanzania, next....wish to go to Serengeti and Saadani, #TakingTimeOff”, aliandika Millen Magese.

Kwa sasa mwanamitindo huyo yupo kwenye kampeni kubwa ya kutafuta tiba ya ugonjwa wa endometriosis, ambao umemsumbua kwa miaka 13 mpaka sasa, uliopelekea kufanyiwa upasuaji mara 13 kupata matibabu yake.

Vodacom South Africa yaamriwa imlipe mfanyakazi aliyebuni huduma ya ‘Tafadhali Nipigie’

$
0
0
Nkosana Makate ndiye aliyebuni huduma ya Please Call Me
Mahakama nchini Afrika Kusini jana iliiagiza kampuni ya Vodacom kumlipa fidia mfanyakazi wa zamani wa kampuni hiyo aliyebuni mfumo wa messaga za bure, baada ya kesi hiyo kudumu kwa miaka minane.

Hukumu hiyo imeipa kampuni hiyo kubwa nchini Afrika Kusini siku 30 za kuanza majadiliano ya jinsi ya kujua kiasi gani cha kumlipa Nkosana Makate.

Makate aliwasiliana na Philip Geissler, aliyekuwa mkurugenzi wa zamani wa maendeleo ya bidhaa na utawala wa kampuni hiyo kuhusu wazo lake la huduma ya “Please Call Me.”

Geissler alikubali kwa mdomo kuijaribu huduma hiyo, zinasema nyaraka za mahakama. Makate aliambiwa na kampuni hiyo kwamba atalipwa share yake kutoka kwenye mapato yatakayotokana na huduma hiyo lakini haikufanyika hivyo.

Baada ya kushindwa kulipwa fidia yake miaka minne baada ya huduma hiyo kuanzishwa, Makate alifungua kesi mahakamani ambayo sasa ameshinda.

“It’s just a relief for me you know, eight years in trial. I’m just happy we are now at the end of this journey,” Makate alisema kwenye mahojiano na kituo cha runinga cha serikali, SABC.

“I never really lost faith that I’ll win this case, I think that really kept me going even in times when I lost hope or felt a bit despondent,” aliongeza.

Huu ni Udhaifu wa Instagram Uliogunduliwa na Mtoto wa Miaka 10

$
0
0
Mtoto mwenye umri wa miaka 10 nchini Finland amewashangaza watu wengi baada ya kugundua udhaifu katika mtandao wa kijamii wa Instagram.

Mvulana huyo kwa jina Jani ametunukiwa $10,000 (£7,000) baada ya kugundua udhaifu huo uliowezesha mtu kuingia kwenye mtandao huo wa kusambaza picha na kufuta maoni ya watu.

Jambo la kushangaza zaidi ni kwamba kisheria haruhusiwi kutumia mtandao huo hadi atimize umri wa miaka 13. Kampuni ya Facebook ambayo inamiliki Instagram, ilichukua hatua upesi na kuondoa udhaifu huo.

Sasa, ndiye mtu mchanga zaidi kutunukiwa pesa kwa kugundua udhaifu katika mitandao ya kampuni hiyo. Aliandikia wasimamizi wa mtandao huo barua pepe Februari kuwafahamisha kuhusu ugunduzi wake.

Wataalamu wa mtandao huo walimfungulia akaunti ndipo aweze kuthibitisha madai yake na akafanikiwa. Mvulana huyo kutoka Helsinki, ameambia gazeti la Iltalehti la Finland kwamba atatumia pesa hizo kununua baiskeli, mpira na mavazi ya kuchezea kandanda na kompyuta za kutumiwa na ndugu zake.

Facebook imeambia BBC kwamba imelipa jumla ya $4.3m kwa watu waliogundua udhaifu kwenye mitandao yake. Malipo hayo hutolewa kama kishawishi kuzuia watu kuuzia wahalifu ugunduzi wao na hivyo kusaidia kampuni husika.

Rais wa zamani wa Burundi Jean-Baptiste Bagaza afariki dunia

$
0
0
Rais wa zamani wa Burundi Kanali Jean-Baptiste Bagaza amefariki akitibiwa nchini Ubelgiji.

Kanali Bagaza amekuwa akitibiwa kwa muda katika hospitali ya Sainte Elisabeth mjini Brussels.

"Imethibitishwa, rais wa zamani Jean Baptiste Bagaza amefariki dunia akiwa nchini Ubelgiji,2 ameandika mshauri wa rais wa Burundi Willy Nyamitwe kwenye Twitter.

"Alikuwa seneta maisha.”

Kanali Bagaza aliingia madarakani Novemba 1976 kupitia mapinduzi ya kijeshi.

Aliondolewa madarakani kupitia mapinduzi mengine yaliyoongozwa na binamu wake Meja Pierre Buyoya Septemba 1987.

Hospitali ya Amana Wameweka wazi Chanzo cha Binti Aliyejifungua Chooni….

$
0
0
Ni Mei 4 2016 ambapo hospitali ya rufaa ya mkoa ‘Amana’ leo iliitisha mkutano na waandishi wa habari na kuzungumzia tuhuma za kutotoa huduma sahihi kwa wananchi  wanaofika hospitali hapo kupata matibabu.

Akizungumza mbele ya waandishi wa habari kaimu Afisa Uhusiano wa Manispaa ya Ilala David Langa alisema.

‘Kumekuwa na malalamiko mbalimbali kutoka kwa wagonjwa kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii juu ya huduma zinazotolewa hospitali moja ni lile lililotokea mnamo tarehe 23/03/2016 lililotolewa kwenye gazeti la Mwananchi la Bi Asha Soudy mwenye umri wa miaka 17  aliyejifungulia chooni‘ –  David Langa

‘Yule binti alipoambiwa aende kubadilisha nguo maana utararibu wetu kabla ya kutoa huduma zetu kwanza tunamtaka mtu anayepatiwa huduma zetu kwenda sehemu husika, sasa yule binti baada ya kupewa ruhusa alijikuta anajifungulia chooni ndipo taarifa zikaenea kuwa ni uzembe wetu ambapo si kweli’- David Langa

‘Na tukio la tarehe 30/03/2016 lililotolewa na mitandao ya kijamii kuhusu hospitali ya Amana kuhusika na kifo cha Mtoto kilichotokana na kucheleshwa kupata huduma Bi. Mariam Hassan, Malalamiko haya yameshafanyiwa kazi na watumishi waliohusika wameshachuliwa hatua za kinidhamu’ – David Langaa

Majibu ya Snura baada ya Chura wake Kupigwa Nyundo na Serikali

$
0
0
Baada ya wizara ya habari, utamaduni, sanaa na michezo kuufungia wimbo wa Snura, Chura jana, muimbaji huyo anaonesha kutoshtushwa na hatua hiyo hasa kutokana na support anaiyopata kutoka kwa mashabiki wake.

Kwa ufupi haoneshi stress, walau kwa kile alichokiandika kwenye Instagram. “Ingekua ndio hela leo ningekua bilionea lo!!! Nawapenda sana kwakweli na nawatakia usiku mwema,” aliandika Snura kwenye Instagram.

Aliongeza hashtag: #utaipenda2_ndimuimekolea_malimao_kama__210_habarizetuwanazo_ilazaohatuna.”

Pamoja na wimbo huo kufungiwa kuchezwa kwenye redio na TV, Snura aliagizwa kuhakikisha amefuta video zake zote mtandaoni.

Mitandao yaharibu soko la magazeti, takwimu zaonyesha magazeti yanapitwa na wasomaji wa mitandao

$
0
0
Vyombo vya habari vya asilia hususani magazeti vinakufa. Hivi sasa vvyombo hivyo vinajikongoja kutokana na mauzo hafifu  na mdororo wa mapato kutoka matangazo na kupunguza wafanyakazi.

Ila wakati idadi ya wasomaji wa habari mtandaoni ikizidi kukua, wanaoperuzi mtandaoni  humo hawatumii muda mwingi kwenye magazeti tando, utafiti wa Pew Research Centre unaeleza.

Katika utafiti wake wa hali ya vyombo vya habari 2015 (“State of the News Media 2015,”) imeonesha kwamba katika vyombo vya habari vya karatasi (print media), Digitali na TV, imeonesha Dhahiri kwamba magazeti yanaelekea kuzimu.

Utafiti huo umetolea mfano magazeti makubwa ambapo wasomaji wake wa mtandaoni wamewashinda kwa mbali kwa idadi ya wasomaji wa makaratasini, ambapo gazeti kubwa sana la New York Times la Marekani limetangaza kuwa nakala zake zipatazo 650,000 kwa wiki zimepitwa kwa mbali sana na wa mitandaoni
Hivi sasa kuna mjadala mitandaoni endapo kama Tanzania iko ama itafika huko. Mabishano ni makali ambapo wa makaratasini wanashikilia msimamo wao kuwa nchini hapa tasni ya habari mtandaoni bado ni change sana kuweza kutishia amani ya magazeti.

Upande wa digitali unajibu kwamba endapo kama kuna wahariri viburi wanaobeza kasi ya mitandao, basi wakae mkao wa kulala njaa muda si mrefu ujao, maana ni wachache wanaoendelea kupata habari kwa njia asili ya magazeti.

Upande wa digitali umeyasifia magazeti ya Global Publishers na la Mwananchi  anbayo ni dhahiri yana wahariri wanaokwenda na wakati na wanaojua nini wanachokifanya kwa kuanza na mapema kuogelea bahari ya maendeleo ya tasnia kwa vitendo kwa kuwa na vitengo vya mtandao vinavyopelekesha mbio magazeti yanayobeza technolojia hio kwa kubuni.

“Ni kweli kwamba Tanzania  bado sana kiteknolojia na miundombini kiasi cha habari za mtandaoni zikatishia uhai wa habari za makaratasini, lakini si uongo kwamba ukizingatia uharaka na gharama pamoja na kwenda na wakati muda si mrefu print media itakwenda na maji”, amesema blogger mmoja ambaye pia ni mwanahabari kwenye moja ya magazeti makubwa nchini.
 Chanzo BOFYA HAPA

P Diddy Aongoza Orodha ya Forbes ya Wana Hip Hop Watano Wenye Mkwanja zaidi

$
0
0

Forbes wametoa orodha mpya ya wasanii wa hip hop wenye fedha zaidi, The Forbes Five.
Diddy ameongoza orodha hiyo mwaka huu kwa kuwa na utajiri ufikao dola milioni 750. Nafasi ya pili imekamatwa na Dr Dre mwenye dola milioni 710 huku Jay Z akifuatia kwa dola milioni 610.

Mwanzilishi wa Cash Money, Birdman amefuatia katika nafasi ya nne akiwa na dola milioni 110. Drake amechukua nafasi ya 50 Cent na kukamata nafasi ya tano kwa utajiri wa dola milioni 60.

Kampuni yatozwa Sh118 Bilioni Poda yake Kusababisha Saratani

$
0
0
Poda ya Johnson, iliyodhaniwa kuwa ni kipodozi na tiba mujarabu kwa watoto na watu wazima duniani kote imebainika kusababisha saratani.

Jana, Mahakama ya St Louis ya Marekani, iliiamuru kampuni inayotengeneza poda hizo, Johnson & Johnson kumlipa Deane Berg wa Sioux Falls, South Dakota, Dola za Marekani 55 milioni (Sh118 bilioni ) baada ya kujiridhisha kuwa kipodozi hicho kilimsababishia saratani ya mayai ya uzazi (ovarian cancer).

Mpaka sasa, zaidi ya wanawake 1,000 wameshafungua kesi kuishtaki kampuni hiyo kwa madai ya kuwasababishia saratani hiyo baada ya kutumia poda ya Johnson kwa miaka mingi.

Ofisa Uhusiano wa Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania, (TFDA), Gaudensia Simwanza alisema wanazo taarifa juu ya madhara ya poda hizo ingawa bado hawajathibitisha kitaalamu kwa poda zilizopo nchini.

“Tuliwaandikia (Mamlaka ya Chakula na Dawa Marekani) FDA ambako kuna kampuni mama inayotengeneza Johnson Powder, lakini mpaka sasa hawajatujibu, tunawasubiri,” alisema.

Alisema TFDA ilishafanya uchunguzi wa kimaabara kuhusu poda hizo lakini haikuona madhara yoyote.

“Lakini labda ni kwa poda zilizoletwa kwa awamu hii, tunaendelea na uchunguzi zaidi wa kimaabara,” alisema.

Simwanza alisema FDA ilitakiwa pia kuwapa taarifa watumiaji wa bidhaa hizo duniani kuhusu madhara ya poda hizo.

Mwaka 2013, Berg alikuwa mwanamke wa kwanza kuishtaki kampuni hiyo baada ya kugundulika na saratani.

Baada ya kuridhishwa na malalamiko ya Berg, Mahakama iliamuru kampuni ya Johnson & Johnson kutoa onyo kuwa poda hizo, Johnson Baby Powder na sabuni ya Shower to Shower, zinasababisha saratani. Hata hivyo, kampuni hiyo haikufanya hivyo.

Baada ya mwaka mmoja, Berg alifungua tena kesi hiyo na Mahakama iliamuru alipwe kiasi hicho cha fedha.

Daktari wa Hospitali ya Wanawake, Brigham, Daniel Cramer alitoa ushahidi mbele ya Mahakama na kueleza kuwa zaidi ya wanawake 10,000 wamegundulika kuwa na saratani ya mayai ya uzazi kwenye hospitali hiyo.

Kadhalika, wanawake hao walibainika kuwa na chembechembe za ‘talcum’ kwenye kizazi.

Daktari wa Saratani wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, Herry Tungaraza alisema kuna uwezekano wa kemikali ya ‘talcum’ kupenya kwenye ngozi, hadi kwenye damu na kuingia kwenye mayai ya uzazi na kisha kusababisha saratani.

“Hata hivyo, hili suala linahitaji uchunguzi zaidi na pia hadi mtu adhurike, ni lazima awe ametumia poda hizi kwa muda mrefu,” alisema.

Alisema si lazima poda hizi zimuathiri mtu kwa kuzitumia sehemu za siri tu, hata kama akizitumia kwa kupaka usoni, zinaweza kusafiri na kuathiri mayai ya uzazi. “Kama ingekuwa zinadhuru kwa kuzipaka sehemu za siri tu, basi zingeathiri zaidi shingo ya kizazi au nyumba ya uzazi, lakini mayai yapo mbali na ndiyo yaliyoathiriwa na saratani,” alisema.

Shahidi mwingine wa katika kesi ya Berg alithibitisha kuwa aliona chembechembe za ‘talcum kwenye uvimbe ulioko kwenye mayai ya Berg.

Mwathirika mwingine

Mei mwaka jana, Gloria Ristesund (62), alifungua kesi dhidi ya Johnson & Johnson kwa kushindwa kuwaonya wateja wake kuhusu poda hiyo kusababisha saratani.

Ristesund aligundulika na saratani, mwaka 2011 baada ya kutumia poda hiyo kwa kuipaka sehemu za siri kwa miaka kadhaa hasa. Mahakama iliamuru Ristesund pia kulipwa Dola 55 milioni.

Tovuti ya CNN inaeleza kuwa utafiti kuhusu kemikali za ‘talcum’ kusababisha saratani ulitolewa miaka mingi nyuma lakini Johnson & Johnson hawakutaka kuweka wazi ukweli huo kwa wateja wao.

“Ni kama kampuni zinazotengeneza sigara, wanajua kuwa imeshathibitishwa kuwa uvutaji wa sigara unasababisha saratani ya mapafu lakini wanauficha umma kuhusu hili,” ilisema taarifa ya CNN.


Ripoti: Jay Z Kuja na Album yake Atakayousema Ukweli Wake Kama Alivyofanya Beyonce Kwenye Lemonade

$
0
0
Jay Z analikamua limao lake mwenyewe pia.
Mtu wa karibu na familia hiyo, ameliambia jarida la US Weekly kuwa rapper huyo, 46, anarekodi nyimbo zitakazoeleza upande wake wa kilichotokea kwenye ndoa yake na Beyonce.

April 23, Queen Bey, 34, aliwashangaza mashabiki kwa video maalum iliyorushwa na HBO pamoja na album ya Lemonade, inayoelezea tetesi za muda mrefu za kusalitiwa na mume wake kwa mashairi kama: This is your final warning / You know I give you life / If you try this s‑‑t again / You gon’ lose your wife.”

Watu wanadai kuwa wawili hao walikuwa mbioni kuachana kabisa mwaka 2014 baada ya tukio maarufu kwenye lifti. May 2014, TMZ walivujisha video inayomuonesha mdogo wake Beyoncé, Solange Knowles, akimshambulia Jay Z wakiwa kwenye lifti baada ya kuhudhuria hafla ya Met Gala.

Vyanzo vinadai kuwa wanandoa hao waliweza kumaliza tofauti zao na sasa wako imara tena.


Wabunge Warushiana Makonde Afrika Kusini

$
0
0
Wabunge nchini Afrika Kusini wamepigana bungeni baada ya spika kuamuru maafisa wa usalama kuwaondoa kwa lazima wabunge wa upinzani ambao walimbeza rais Jacob Zuma alipoingia bungeni tayari kulihutubia kikao.

Rais Zuma ambaye ameshindwa katika kesi mbili kuu zinazomhusisha na ubadhirifu wa mali ya umma na usimamizi mbaya alikuwa amefika bungeni kwa mara ya kwanza tangu kushindwa mahakamani.

Hata hivyo ujio wake uliwakera sana wabunge wa chama cha upinzani Economic Freedom Fighters (EFF).

Wabunge hao chini ya kiongozi wao Julius Malema walipiga mayowe na kumtupia matusi bw Zuma jambo lililomlazimu spika wa bunge kuamuru wabunge hao wa EFF kuondolewa nje.

Ijumaa iliyopita mahakama ya juu ya Afrika Kusini iliamua kuwa rais Zuma anapaswa kufikishwa kizimbani kufuatia kesi za ufisadi dhidi yake.


Kesi hiyo inahusiana na ufisadi uliotokea katika ununuzi wa silaha zenye thamani ya mabilioni ya dola mwaka wa 1999.

Zuma amekanusha madai yote dhidi yake, Anatarajiwa kukamilisha hatamu yake mwaka wa 2019.
Uamuzi huo wa mahakama ulikuwa msumari wa moto kwa kidonda cha Zuma ambaye mwezi uliopita alipatikana na hatia ya matumizi mabaya ya madaraka yake alipokaidi amri yakulipa pesa za umma zilizotumiwa kukarabati nyumba yake ya Nkandla.

Mauaji ya Kutisha Kaole Bagamoyo Jana Jioni..Mama na Mtoto Wachinjwa Kama Kuku

$
0
0
Samahani kwa Kuficha Picha , Sio Nzuri
Watu wawili mama na mtoto wamenyongwa hadi kufa kisha kuchinjwa kama kuku maeneo ya kaole jion ya jana

Habari kutoka Kaole; Majira ya saa 12 jioni jana, ilipita pikipiki eneo hilo ikiwa imepakiza watu watatu, dereva wa nne! Wanaume wawili, mwanamke na mtoto.
Walipofika eneo la darajani, porini kidogo, pikipiki ilipaki, watu wote wakashuka ndipo hatua za utekelezaji mauaji hayo zilianza.

Inadaiwa kwamba, Mama na mtoto wake walinyongwa Kwanza kabla ya kuchinjwa shingoni mithili ya kuku!
Lakini wakati mauaji hayo yakitekelezwa kulisikika makelele porini ambapo baadhi ya wananchi waliyoyasikia walielekea huko ndipo walipokutana na wauaji hao wakiwa na majambia yaliyoloa damu wakitokea porini.

Walipowaona watu hao walikimbia na kuacha pikipiki yao ambayo inashikiliwa Polisi. Katika eneo la tukio, mbali na pikipiki pia kulikutwa simu tatu za mkononi na mkoba wa mwanamke aliyeuawa.
Kwa mujibu wa taarifa, watu hao ni wageni Kaole na mpaka sasa bado miili yao haijatambuliwa!

Picha zinatish mno ndo maana hazijatumwa humu kama una ndugu yako mwenye mtoto wa kiume umri miaka 3-5 halafu kapotea mazingira ya kutatanisha jitahidi kufwatilia

SOMA Nafasi za Kazi Zilizotangazwa Leo Katika Mitandao Mbali Mbali

Baada ya Bunge Kukatazwa Kuonyeshwa Live..Baadhi Waamua Kujirekodi Kwa Kutumia Simu

$
0
0

From @mangekimambi_ - Omg this is sooooo sad jamani... Eti nchi yetu ndo imefikia hapa, Mbunge akiwa anachangia bungeni mwenzie inabidi amrekodi Kwa simu then waposti kwenye social media ndo wananchi wajue michango Yao.... This is really sad! Hivi Kweli Raisi wetu asiependa uonevu wa watanzania anayaona haya???
Viewing all 104799 articles
Browse latest View live




Latest Images