Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104808 articles
Browse latest View live

Nuh Mziwanda: Haikuwa rahisi kumshirikisha Alikiba, ni heshima kubwa kwangu

$
0
0


Nuh Mziwanda amesema kumpata Alikiba na kumshirikisha kwenye wimbo wake halikuwa jambo rahisi na kwamba kwake hiyo ni heshima kubwa.



Anadai kawa wimbo huo ulichukua muda kuurekodi kutokana na ratiba ngumu ya Alikiba.

“Nimegundua kwamba nina uwezo, yeye ana uwezo mkubwa ambao kumbe hata msanii kama Alikiba anaanza kutoka mimi namsikia bado mdogo, ameweza kufanya collabo na mimi kiroho safi sababu ni msanii mgumu sana kufanya naye collabo,” Nuh ameiambia Bongo5.

“Kwahiyo imenipa moyo na kuona kwamba kumbe mimi ni mwanamuziki sio mbabaishaji. Kuna credit kubwa sana ambazo nimezipata na ushauri mkubwa pia anaokuwa ananipa,” ameongeza.

Nuh alimshirikisha Alikiba kwenye wimbo wake Jike Shupa.



Serikali ya Tanzania yasifika kwa kuwa na uongozi unaozingatia Sheria na Utawala Bora.

$
0
0


Serikali ya Tanzania yasifika kwa kuwa na uongozi unaozingatia Sheria na Utawala Bora.


Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Waziri wa Nchi,

Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angella Kairuki alipokuwa akifungua Mkutano wa siku mbili  wa Kimataifa kuhusu Utawala wa Sheria na Utawala bora.

 

Lengo la mkutano huo ilikuwa ni  kujadili masuala ya Afrika katika kukuza utawala wa sheria katika utekelezaji wa agenda ya maendeleo endelevu ya mwaka 2030 na agenda ya Umoja wa Afrika ya 2063.


“Mkutano huu wa kistoria nchini Tanzania utasaidia kuleta mageuzi katika Taasisi zinazosimamia masuala ya Sera na Sheria ambayo yatachochea maendeleo mazuri katika nchi za Afrika”, alisema Waziri Kairuki.


Akiendelea kuzungumza Waziri Kairuki alisema uwepo wa Marais wastaafu kama Mhe.Benjamin Mkapa na Dkt. Jakaya Kikwete, katika mkutano huo ni ushahidi tosha wakuwepo na mafanikio ya utawala wa sheria na utawala bora nchini Tanzania.


Kwa upande wa Rais Mstaafu Mhe.Benjamin Mkapa, amesema ili Bara la Afrika liendelee Kiuchumi ni lazima watu wake wapate elimu ya uraia ili waweze kushiriki zaidi katika masuala mbalimbali yanayohusu maendeleo yao pamoja na kuwepo na uongozi utakaoleta mabadiliko “transformative leadership”.


Naye, Waziri wa Haki Sudani ya Kusini Mhe. Pwanauwilla Unango amesema pamoja na kuwa Bara la Afrika lina matatizo mengi kama vita, njaa, magonjwa na ndoa za utotoni, dunia isiitazame Afrika kwa mtazamo huo pekee, bali inahitaji msaada kutoka Jumuiya za Kimataifa.


Mkutano huo wenye kauli mbiu “Kufikia agenda ya 2030 na agenda ya 2063:Utawala wa Sheria kwa Maendeleo Endelevu ya Afrika”, (Achieving the 2030 agenda and agenda 2063:The rule of law as a driver of Africa’s suistainable development) , umeandaliwa na  Shirika la Kimataifa la Maendeleo ya Sheria (IDLO) la nchini Italia, kwa Ushirikiano wa Serikali ya Tanzania  umehusisha wadau mbalimbali wakiwemo Mawaziri, kutoka nchi mbalimbali za Afrika, Mabalozi kutoka ndani na nje ya Afrika pamoja na wawakilishi wa Mashirika ya kutetea Haki za Binadamu.


Wanao Uza Wasichana Nje ya Nchi kwa Kisingizio cha Kuwatafutia Ajira Watajwa

$
0
0

SERIKALI imepata majina ya baadhi ya wahusika wa mtandao wa kimataifa unaohusika kusafirisha na kuuza nje ya nchi wasichana wa Kitanzania wa miaka kati ya 16 na 24, kwa kisingizio cha kuwatafutia ajira.

Aidha, imesema tayari mawasiliano na serikali za nchi wanakopelekwa wasichana hao yamefanyika kuhakikisha wanakamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria kwa sababu wanachokifanya ni biashara haramu.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Augustine Mahiga alieleza Bunge jana akiwasilisha Makadirio ya Bajeti ya Mapato na Matumizi kwa mwaka wa fedha 2016/2017.

Balozi Mahiga aliweka wazi kuwa katika orodha wamo Watanzania wanaoishi nchini na wengine nje ya Tanzania wanaoshirikiana na wageni. Kwa mujibu wa Balozi Mahiga, kufanikiwa kupata majina hayo kumetokana na ushirikiano kutoka kwa Jumuiya za Watanzania waishio nchini Thailand na India pamoja na waathirika wa biashara hiyo haramu.

“Kwa hapa nyumbani uchunguzi unaendelea kwa kushirikiana na balozi za nchi ambazo wasichana wetu wanapelekwa ili kubaini watu wote walio sehemu ya mtandao huo, hususan wanaowezesha upatikanaji wa vibali vya kusafiria kwenye balozi hizo ili kuwakamata na kuwachukulia hatua kali za kisheria,” alisema Balozi Mahiga.

Alisema tayari serikali imeziomba balozi hizo ziwe makini zaidi kudhibiti uombaji wa vibali vya kusafiria kwa shughuli mbalimbali na kuwataka wahusika kuthibitisha uwezo wa kifedha walionao kufanya utalii, kufanya shughuli au kuishi kwenye nchi wanazokwenda ili kuudhibiti mtandao huo.

Alisema, wanamtandao hao wanaojihusisha zaidi kuuza watu ili washiriki ukahaba, huwanyang’anya, kushikilia pasipoti za wasichana wanaowarubuni na kuwadai Dola za Marekani 5,000 hadi 6,000, baada ya kuwafikisha wanakowapeleka, jambo linalokuwa gumu kutekelezwa na wasichana hao kwa kukosa fedha, hivyo kujikuta wakikubali kufanya biashara ya ukahaba.

“Ninatoa mwito kwa Watanzania wote tuwe makini pale tunapopata fursa za kazi nje ya nchi. Ni muhimu kuzingatia na kujiridhisha kuhusu masuala ya msingi yanayohusu ajira za nje ikiwa ni pamoja na kuwepo mkataba rasmi wa ajira unaotambuliwa na mamlaka husika zilizopo nchini na za nchi ambayo mtu anataka kwenda,” alisema.

Alitoa rai pia kwa Watanzania wanaokwenda nje kufanya kazi kujisajili kwenye ofisi za ubalozi wa Tanzania uliopo katika nchi hizo na kutokubali kuweka hati za kusafiria rehani. Balozi Mahiga aliwataka wananchi waelewe kuwa ahadi nyingi za ajira kwa nchi za Thailand, Malaysia na China zinatolewa na watu wasio waaminifu wanaoshiriki katika mtandao wa biashara haramu ya watu.

Aidha, alisema bado kuna Watanzania kadhaa wanatumikia vifungo na adhabu ya kifo katika magereza ya nchi mbalimbali duniani baada ya kukutwa na hatia ya makosa ya kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya. Alitaja nchi waliko na idadi yao kwenye mabano kuwa ni Brazil (41), China (266), Iran (68), Thailand (14) na Umoja wa Falme za Kiarabu (3).


Wapinzani Wawasilisha Hoja ya Kumwondoa Madarakani Naibu Spika, Dr Tulia Ackson

$
0
0


Wabunge wa upinzani wamewasilisha kwa Spika wa Bunge hoja ya kumwondoa madarakani Naibu Spika, Dk Tulia Ackson kwa kutokuwa na imani naye.


Hatua hiyo imefikiwa na wabunge hao kufuatia kutoridhishwa na mwenendo wa uongozi wa Dk Tulia anapokalia kiti cha Spika.


Tangu Jumanne wiki hii, wabunge hao wamekuwa wakisusa vikao vinavyoongozwa na kiongozi huyo kwa madai anaminya demokrasia.


Walifikia uamuzi huo baada ya Dk Tulia kuzuia kujadiliwa hoja ya kufukuzwa kwa wanafunzi zaidi ya 7,000 wa Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom) iliyowasilishwa na Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari na kukatisha mjadala wa bajeti ya maji.


Kitendo hicho kiliwafanya wabunge wote wa upinzani kupingana na maamuzi ya Dk Tulia, jambo lililosababisha watolewe bungeni.


Kutokana na hali hiyo wabunge hao kupitia Mbunge wa Simanjiro, James Ole Millya akisindikizwa na Mbunge wa Kibamba, John Myika wa Chadema na Mbunge wa Konde wa CUF, Khatibu Said Haji waliwasilisha hoja hiyo kwa Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashilillah baada ya Spika, Job Ndugai kutokuwapo bungeni.


Hoja hiyo iliwasilishwa kwa mujibu wa Kanuni ya 138 (1) ambayo inaeleza utaratibu wa jinsi ya kumwondoa Naibu Spika.


Kanuni hiyo inasema, “Utaratibu wa kumwondoa Naibu Spika madarakani chini ya Ibara ya 85(4)(c) ya Katiba utakuwa kama ule wa kumwondoa Spika, isipokuwa tu taarifa ya kusudio la kumwondoa Naibu Spika madarakani inayoeleza sababu kamili za kuleta hoja hiyo, itapelekwa kwa Spika ambaye ataiwasilisha kwenye Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kwa ajili ya kuijadili.”


Fasili ya pili ya Kanuni hiyo inasema:“Endapo Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge itaridhika kuwa zipo tuhuma mahususi dhidi ya Naibu Spika zinazohusu uvunjaji wa Katiba, Sheria au Kanuni zinazoongoza Shughuli za Bunge, basi Kamati hiyo itaidhinisha kuwa hoja hiyo ipelekwe bungeni ili iamuliwe.”


Kwa mujibu wa Ibara ya 85(4)(c), Naibu Spika atakoma kuwa Naibu Spika na ataacha kiti cha Naibu Spika endapo ataondolewa kwenye madaraka ya Naibu Spika kwa azimio la Bunge.


Akizungumzia uwasilishwaji wa hoja hiyo, Millya alisema taarifa zaidi watatoa leo kuhusu msimamo wao huo.


Dk Tulia aliwataka wabunge wenye malalamiko juu ya utaratibu wa uendeshaji wa shughuli za Bunge kukata rufaa kwa kufuata Kanuni za Bunge.


Alisema kanuni ndogo ya 5(2) inasema Spika atawajibika kutilia nguvu kanuni zote za Bunge na 5(3) inasema Spika anaweza kumtaka mbunge yeyote anayekiuka kanuni hizi kujirekebisha mara moja.


Alisema kwa hiyo mbunge yoyote asiyeridhika, kanuni za Bunge zinamruhusu kukata rufaa na zinamweleza nini cha kufanya.


Kikwete: Nchi za Afrika Haziwezi Kukwepa Misaada ya Wazungu

$
0
0

Rais mstaafu wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete amesema nchi za Afrika haziwezi kukwepa misaada kutoka nchi za Ulaya kwa kuwa misaada hiyo ni jukumu lao la kihistoria.


Kikwete alisema hayo jana wakati wa ufunguzi wa mkutano wa siku mbili unaojadili malengo mapya 17 ya Umoja wa Mataifa yanayohusu ‘Maendeleo Endelevu kwa mwaka 2030’.


Mkutano huo umejikita kujadili lengo namba 16 linalohimiza haki, amani na jamii shirikishi, hasa katika masuala ya utawala wa sheria kama chachu ya maendeleo endelevu.


Kikwete alisema jukumu hilo linapaswa kuendelezwa kwa kuwa maendeleo ya nchi za Ulaya yalitokana na rasilimali walizozitoa Afrika kipindi cha ukoloni.


Alisema nchi za Afrika zina rasilimali za kutosha hivyo, ili zifanye kazi bado kunahitajika uwekezaji ambao utaweza kuinua viwanda na kukuza uchumi wa nchi za Afrika, kwani bila hivyo itachukua muda mrefu kufika mbali kiuchumi.


Hata hivyo, alisema nchi za Afrika lazima zijiwekee utaratibu wa namna ya kupokea misaada hiyo, lakini lengo liwe ni kunufaisha wazawa na kwa kufuata sheria za nchi husika na zile za kimataifa.


“Misaada tunayoizungumzia siyo lazima iwe fedha, bali tunahitaji wawekeze zaidi kwetu kwa mikataba ya kisheria inayolinda wazawa, kwa mfano Tanzania tuna rasilimali za kutosha kama gesi, madini na vinginevyo, lakini hivi vyote vinahitaji kuibuliwa na kutayarishwa. Lazima tuwape nafasi ili kufanikisha lakini kwa sheria zitakazowalinda Watanzania,”alisema Kikwete.


Kauli hiyo ya Kikwete imekuja wakati Rais wa Awamu ya Tano, John Magufuli amekwisha kuweka msimamo katika hotuba zake kadhaa akitaka Tanzania ijitegemee kwa asilimia kubwa badala ya kutegemea misaada ya nje.


Wakati akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa barabara ya kwanza ya juu (flyover) katika makutano ya Barabara za Mandela na Nyerere eneo la Tazara, Rais Magufuli aliita misaada ya wahisani ‘mkate wa masimango’ na kusema kuliko kula mkate huo ni bora kushindia muhogo.


Ingawa hakufafanua wala kuzungumza kwa undani juu ya kauli hiyo, lakini aliitoa ikiwa zimepita siku chache tangu Shirika la Maendeleo la Milenia (MCC) la Mareka ni kusitisha msaada wa Dola za Marekani milioni 472.8 karibu Sh1 trilioni kwa madai kuwa Tanzania ilikiuka misingi ya kidemokrasia kwa kurudia uchaguzi wa Zanzibar na kushindwa kusimamia She ria ya Makosa ya Mtandao.


Pia, Rais Magufuli Machi 29, akiwa katika kijiji cha Mlimani, Wilaya ya Chato mkoani Geita alisema jukumu kubwa lililo mbele ya Watanzania kwa sasa ni kushikamana na kujisimamia katika maendeleo ili kila mmoja ahakikishe anaongeza uzalishaji na utendaji kazi mahali pake pa kazi.


“Kwa hiyo ni lazima tujisimamie sisi wenyewe, na tukijisimama sisi wenyewe kwa kila mmoja kuwajibika mahali alipo, kama ni mfanyakazi afanye kazi kwelikweli, kama ni mkulima afanye ukulima wake kwelikweli, kama ni mfanyabiashara afanye biashara kwelikweli, kama ni mfugaji afuge kwelikweli, kama ni mvuvi avue kwelikweli, Tanzania hii tutavuka,”alisema.


Mkutano huo ulioandaliwa na Taasisi ya Kimataifa ya Maendeleo ya Sheria (IDLO) yenye makao makuu yake nchini Italia, ambayo kwa Tanzania mlezi wake ni Rais mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa.


Akizungumza kwenye mkutano huo, Mkapa alisema katika nchi yeyote ili kupata maendeleo ni lazima kuwe na Katiba ya wananchi ambayo haitalenga kundi moja.


“Awali nchi nyingi za Afrika hazikuwa na Katiba ya wananchi, bali kulikuwa na Katiba ya chama ambayo kwa sasa ni nchi za kidikteta pekee zimebaki na mfumo huo, kwa sasa tulilenga kuweka sera, mikakati thabiti ili tuweze kutekeleza malengo mapya ya dunia chini ya dira mpya ya Umoja wa mataifa ya maendeleo ya dunia,” alisema Mkapa.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora, Angela Kairuki alisema kama ilivyo ajenda ya nchi za Afrika, nchi haiwezi kuwa na utawala wa sheria kama hakuna upatikanaji mzuri wa sheria.


“Lazima uweke mifumo mizuri ya kutatua migogoro pia, utoaji wa vibali bila kutoa rushwa, hata katika uwekezaji utakapokuwa huna sheria nzuri inayolinda upande huo ni vigumu wawekezaji kuwepo,” alisema Kairuki.


Mkurugenzi Mkuu wa IDLO, Irene Khan alisema mkutano huo umejikita katika kujadili haki, amani na jamii shirikishi.


“Lengo ni kuwa na dira mpya ya maendeleo ya dunia inayolenga kutokomeza umaskini, kulinda mazingira, kupambana na mabadiliko ya tabianchi na kushirikisha makundi yote kwenye jamii katika masuala ya maendeleo,” alisema Khan.


Nuh Mziwanda atoboa Siri ya ‘Jike Shupa’

$
0
0



Nuh Mziwanda amefunguka kile kilichojificha kwenye wimbo wake wa ‘Jike shupa’ ambao kwa sasa unafanya poa, aliomshirikisha Alikiba, na jinsi alivyoupokea kwa mara ya kwanza.

Akiongea kwenye kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio, Nuh Mziwanda amesema Alikiba alimtaka Nuhu autoe wimbo huo bila yeye kutia sauti yake, kwani aliuona umekamilika na mzuri pia.

“Kiukweli nilikuwa nishaurekodi ushaisha, na nilikuwa nina plan ya kuuachia mimi mwenyewe, baadae nikaona mbona nimekaa kimya muda mrefu alafu nahitaji kuja kitofauti, ndio nikamfuata Alikiba nikamsikilizisha, nashukuru Mungu mwenyewe aliupenda kwa muda mfupi, akaniambia Nuh mbona wimbo umekamilika? uachie tu hivi hivi, nikamwambia hapana nahitaji sauti yako, ndio maana Kiba kaimba kidogo sana lakini kafanya kitu kikubwa”, alisema Nuhu Mziwanda.

Pia Nuhu Mziwanda amesema anaamini wimbo huo utakuja kubadilisha status yake na kuwa kubwa zaidi kuliko alipo sasa , kwenye kazi zake za muziki.


Mzee Majuto Akanusha Kustaafu Kuigiza

$
0
0



Msanii wa filamu za kuchekesha, King Majuto amekanusha taarifa ambazo zilizagaa katika mitandao ya kijamii kwamba amestaafu kuigiza.

Akiongea katika kipindi cha Clouds E cha Clouds TV Jumatano hii, Mzee Majuto amedai sio kweli kwamba amestaafu kuigiza ila kuna baadhi ya filamu ambazo hatafanya tena.

“Watu wameniwekea maneno mdomoni, sijasema nimeacha kuigiza,” alisema Majuto.“Wakati nipo Hija mwaka jana nilikuwa nafikiria niache kabisa kuigiza, lakini baada ya kurudi nikaona nalazimika kuendelea kuigiza ili nipate pesa za kuendesha maisha yangu, kwa sababu bila filamu nitakufa njaa,”

Pia muigizaji huyo amesema hafanyi tena stand up comedy kwa kuwa wakati anafanya kuna matukio ambayo yatakuwa yanaendelea katika ukumbi ambayo dini yake hayaruhusiwi.

Pia Majuto amewataka mashabiki wa filamu zake kuendelea kusubiria kazi zake ambazo atakuwa anaandaa mwenyewe.

Bongo5


Tulia Akson Aendelea Kususiwa Bunge na Wabunge wa Upinzani..Hichi ndo Kilichotokea leo

$
0
0


Wabunge wote wa vyama vya upinzani leo tena  wametoka nje kupinga Naibu Spika wa Bunge  Dk. Tulia Ackson kuendesha vikao vya Bunge na kumwachia Bunge yeye na wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).


Taarifa kutoka Bungeni zinaeleza kuwa, wabunge wote wa upinzani wametoka nje kususia kikao cha Bunge ikiwa ni kutekeleza azimio lao la kutokuwa na imani na Dk Tulia.


Baada tu ya kusomwa dua ya kufungua Bunge, wabunge hao wametoka nje  majira ya saa 3:00 asubuhi na kumwacha Dk. Tulia akiwa na wabunge wa CCM pekee.


Kambi  upinzani  ilianza utaratibu huo juzi kwa kutoka ndani ya ukumbi wa Bunge baada ya Dk. Ackson kuingia ukumbini.


Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, juzi alisema wataendelea kutoshiriki vikao vinavyoongozwa na Naibu Spika hadi pale "haki itakapopatikana."



Wema Sepetu Afunguka na Kuwapa Makavu Laivu Wanaomchagulia vya Kupost Instagram

$
0
0

By  @wemasepetu -  Quick Question..... Is there a book of rules Ya Instagram inayosema kuna vitu tufanye na tusifanye....!? I dont think so... And kitu ambacho nakiona kutoka Instagram, Watu wanapenda sana fujo fujo, Purukushani, mara huyu na huyu hawaongei, flani kamchukulia flani bwana, yule kafumaniwa... Hicho ndo mnachokiona kina kick... Ila mwisho wa siku ukija kuangalia , IT is TRUE... Maana the world ya leo Only Gossip sells... Ila jamani ifike tym tukue... Mi binafsi kuna vitu vinanichosha... Actually Vimenichosha... Ifike tym kila mtu aangalie maisha yake na afanye kile kinachomridhisha nafsi yake.... Y'all can Judge me mnavyotaka ila mi  kwangu naangalia wat God has to say bout wat im doin... Imekuwa too much tokea nilivyopost uzalendo ikaonekana all sorts of Crazy, But u know wat, I dont care... Sasa basi, nitapost ninachotaka nyie endeleeni kujudge na kuleta conclusion zenu mnazojua... Iwe nataka attention, iwe natafuta kick, iwe nitokeje, iwe najipendekeza, iwe vyovyote It all comes down to me.... Kupost Lipstick vepee...??? Kuna msemo unasemaga Tenda Wema uende zako... Dats how I roll... Na nimekuwa nikifanya hivyo siku zote... Sitegemei na wala sitaki mtu ninae msupport au kumuunga mkono na yeye afanye the same.... Na wala sina haja na kupostiwa....Niwe sipindui au napindua It doesnt make A difference... Kwanza haya mambo ya kupinduana yameanzaga lini Mungu wangu... Ila instagram mna majungu sana... Mi siwezi jamani... Mniachage basi sometimes... Sina amani... Imekuwa kama nimeua... Sio poa bana.... Haiya basi tuishie hapo... Atleast nimeyatoa yangu... Sijakataza mtu kusema anachotaka... Uwanja wenu.... Have a Blessed TBT Wapendwa.....!!!! 💋💋💋 But another quick question before I share this post, Have y'all ever wondered if tungekuwaga hatuna mambo ya majungu majungu tungefika wapi...? Au tungefanya vitu vingapi...? Mambo mangapi mazuri yanatupita jus because of kuendekeza upuuzi usio kuwa na faida... Im Just saying...


Wivu wa Mapenzi: Ateketeza Nyumba Kwa Moto Kutaka Kumuua Mtalaka Wake Akizania Yupo Ndani ya Nyumba

$
0
0


MTU na mkewe wamenusurika kifo, baada ya nyumba yao walimokuwa wamelala kuchomwa moto na kuteketea yote.

Aliyeteketeza nyumba hiyo ni mwanamume mmoja, akidhani kuwa mke wake waliyetengana miezi kadhaa iliyopita amelala ndani ya nyumba hiyo, ili aweze kumuua.

Kamanda wa Polisi mkoani Mara, Ramadhani Ng’anzi, alisema jana kuwa tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia juzi katika kitongoji cha Mlimani eneo la Balili kona, mjini Bunda.

Alisema kuwa wazee walionusurika kifo baada ya nyumba yao kuchomwa moto ni Malenya Maduhu Suba (68) pamoja na mke Kabula (52), ambao wote ni wakazi wa kitongoji hicho.

Ng’anzi alisema siku ya tukio mwanamume huyo aliambiwa na mama mkwe wake kuwa mke wake waliyeachana naye miezi sita iliyopita na kuolewa na mwanamume mwingine yuko nyumbani kwa wazee hao amekuja kuwasalimia hao wakwe zake, ambao kwa sasa kijana wao ndiye amemuoa mwanamke huyo.

Baada ya mwanamume huyo kupata taarifa hiyo usiku wa manane aliamka na kwenda hadi nyumbani hapo na kisha kuichoma moto nyumba hiyo, akidhani kuwa mke wake ambaye tayari wameshaachana naye pia amelala ndani ya nyumba hiyo.

Aidha, alisema ndani ya nyumba hiyo kulikuwa na hao wazee wawili tu, kwani huyo mwanamke alikuwa amelala katika mji mwingine. Alisema hao wazee walinusurika baada ya kukimbilia nje, lakini wakiwa wamejeruhiwa na moto huo na kwamba kila kitu kilichokuwa ndani ya nyumba hiyo zikiwemo samani zote za ndani pamoja na kuku wakubwa 17 na vifaranga 18 vyote viliteketezwa na moto huo.

Mwenyekiti wa kitongoji hicho, Francis Paul alisema wananchi walifanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo Mathias Masalu (26) na kumpeleka polisi. Mzee ambaye nyumba yake ilichomwa moto alisema kuwa thamani ya vitu vyote ni Sh milioni 2.5.


Tumbua Tumbua Majipu Uchungu Yawakuta Watumishi Watano Nzega

$
0
0



BARAZA la madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Nzega, mkoani Tabora limewasimamisha kazi watumishi watano kwa tuhuma za ubadhirifu wa zaidi ya Sh milioni 190, ambazo ni fedha za Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) pamoja na fedha za chanjo.

Watumishi hao wanatuhumiwa kughushi nyaraka, kukosekana kwa baadhi ya nyaraka za fedha, kuidhinisha malipo hewa pamoja na kukiuka taratibu na kanuni za utumishi wa umma na kukiuka matumizi ya fedha za umma.

Kikao hicho kilihudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri na Mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Kiwelle Bundala. Kiwelle aliwataja watumishi waliosimamishwa kazi kupisha uchunguzi kuwa ni Katibu wa Afya Wilaya, Kisasu Sikalwanda, Mhasibu wa Halmashauri ya Wilaya, Denins Gombeye, Mratibu wa Chanjo wa Wilaya, Joel Mjondela, Mganga Mkuu Hospitali ya Wilaya, Emmanuel Mihayo na Mweka Hazina, Stanslaus Kalokola.

Alisema uchunguzi utakapofanyika na kubaini watumishi hao hawana hatia wataendelea na kazi na ikiwa tofauti hatua nyingine za kinidhamu zitachukuliwa.

Mwanri alilipongeza baraza hilo kwa kuchukua maamuzi magumu ya kulinda maslahi ya wananchi na kuongeza kuwa ataendelea kusimamia sheria na taratibu za utumishi wa umma. Aliwataka watumishi wa Serikali kuhakikisha wanasimama katika nafasi zao za kufanya kazi kwa uandilifu na kuepuka ubadhirifu ambao hauna faida ndani yake.

Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Mkoa wa Tabora, Mohamed Msangi alisema sababu za watumishi hao kusimamishwa kazi ni kughushi nyaraka za malipo, kukosekana kwa baadhi ya nyaraka pamoja na kufanya malipo hewa.

Alisema taarifa ya CAG inaonesha kukiuka taratibu nyingi za matumizi ya fedha za umma..


Bunge Latoa Msimamo Wake Kuhusu Naibu Spika Tulia Ackson Kukataliwa na Kambi ya Upinzania

$
0
0
Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashililah

Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashililah, amesema msimamo wa wabunge wa upinzani kutohudhuria vikao vinavyoongozwa na Dk. Tulia hauwezi kuathiri shughuli za Bunge na uongozi wa Bunge hauoni tatizo la Dk. Tulia kwani ni kiongozi mahiri anayesimamia kanuni wakati wa kuliongoza Bunge.
Neno moja kwa Katibu wa Bunge

Baada ya Kumwagana na Shilole Nuhu Mziwanda Amtambulisha Mpenzi Wake Mpya Hapa

$
0
0
Pichani Nuhu na Mpenzi Mpya
Mwanamuziki Nuhu Mziwanda amemtambulisha mpenzi wake mpya kupitia mitandao siku ya jana baada ya kuachia picha kadhaa akiwa na mrembo huyo ambae mkononi amejichora Tatooo ya jina lake 'Nuhu Mziwanda'

Nuhu Mziwanda kabla ya hapo alikuwa na Mwanamuziki Shilole ambae walimwagana baada ya kushindwa kuelewa na kugombana mara kwa mara na muda mwingine Nuhu Kuishia Kupigwa makofi ......

Video : Huyu Ndio Mtoto wa Aunti Ezekeil, Angalia Jinsi Alivyofanana Sana na Baba Yake

$
0
0
Moses Iyobo na Aunty Ezekiel 
Kama kuna habari ilimake headline sana wiki iliyopita basi hutaacha kuitaja ya Birthday ya mtoto wa mwigizaji Anti Ezekiel na Dansa wa Diamond anaefahamika kama Mose Iyobo. Mastar hao walikua wakisherehekea mwaka mmoja wa kuzaliwa wa mtoto wao Cookie katika sherehe iliyohudhuriwa na mastar mbalimbali.

Itakumbukwa kua ni watu wachache sana waliokua wakiifahamu sura ya mtoto wa Anti kwani amekua akificha sura ya mwanae hasa kwenye mitandao ya jamii. Ila watu wengi baada ya kuona picha za mtoto huyo kwa mara ya kwanza walisema kafanana sana na baba yake kuliko mama. Unaweza tazama video ya Mose akicheza na mwanae na uone jinsi walivyofanana.

Video : Ali Kiba Ajibu kwa nini Hamsaidii Abdu Kiba Afanikiwe Kimuziki

$
0
0
Abdu Kiba na Ali Kiba Katika Pozi
Baada ya kupata dili la kujiunga na label kubwa sana duniani ya Sony, watu wengi walimpongeza kwa hatua kubwa aliyofikia. Kwani Kiba ndio msanii wa kwanza Tanzani ambae kazi zake zitakua zikisimamiwa na kampuni hiyo kubwa.

Ni ukweli usiofichika kua Kiba ni msanii mkubwa sio tu Tanzania bali Afrika nzima. Watu wengi wamekua wakijiuliza ni kwa nini Kiba hamsaidii mdogo wake Abdu Kiba ili na yeye awe maarufu na mwenye mafanikio kama yeye?? Kiba amejibu swali hilo,

Unaweza tazama video hapa chini kumskia....


Diamond Platnumz Ategua Kitendawili..Amsainisha Rasmi Rich Mavoko Kwenye Lebo yake ya WCB

$
0
0
Mwanamuziki Diamond amemchukua rasmi mwanamuziki Rich Mavoko na sasa atakuwa chini ya lebo yake ya Wasafi ..

Baada ya tetesi nyingi sasa leo rasmi amemtangaza mwanamuziki huyu kuwa chini ya lebo yake

Ameandika haya katika ukurasa wake wa Instagram

From @diamondplatnumz  -  Wolcome to the Family @richmavoko Let's take Bongo fleva to the world!

Mahakama Yatengua Kifungo cha Siwema wa Nay wa Mitego

$
0
0
Mahakama Kuu ya Mkoa wa Mwanza imetengua kifungo kwa mzazi mwenzake na Nay Wamitego, Siwema kwa kumhukumu kifungo cha nje cha miaka miwili.

Siwema-akilia-kwa-uchungu-baada-ya-kuona-nyumba-mpya-ya-mume-wake

Mwezi April mahakama kuu ya Mkoa wa Mwanza ilimhukumu Siwema kifungo cha miaka miwili jela baada ya kukutwa na kesi kumtukana matusi kwa njia ya mtandao mlalamikaji ambaye anafahamika kwa jina la Deo.

Nay Wamitego amesema, “Ndiyo ana kifungo cha nje, nimemsaidia kama mzazi mwenzangu sijawahi kufikiria kurudiana naye. Nimefight mimi na ndugu zake ilimradi nitimiza kile ambacho niliwaahidi watu kile ambacho nilizungumza.”

Aidha Nay wa Mitego ameongeza kuwa ameonana na mzazi mwenzake huyo siku ya mwisho tangu amefungwa na wala hana mawasiliano naye tena kwa kukwepa kuanzisha mambo mengine yasiyokuwa na msingi.

Ndoa ya Diamond Platnumz na Zari Hassan inanukia?

$
0
0
Diamond Platnumz ameidhihirishia Dunia kuwa Mpenzi wake wa Sasa Zari Hassan si wa Kupita tu

Na ndio maana ujumbe alioandika Diamond kwenye Instagram unaashiria kuwa huenda siku za wao kuwa Mr and Mrs Chibu rasmi zimekaribia.

“A Morning Convo with My Beautiful Wife to be…. taking Blessings on what we about to do today…She always makes me Smile….Love you so Much Mama tee @ZaritheBossLady Nkwagara Nyo,” ameandika Diamond kwenye picha ya mazungumzo kwenye app ya Facetime.

Baraka anazozizungumzia Diamond kwenye ujumbe huo ni za utambulisho wa kitu kikubwa kutoka WCB ambacho licha ya mimi kuwa najua ni nini, kwa heshima na taadhima nawaachia wao wenyewe waumwage mchele muda ukifika.

“Blessed to see another day,
Stay tuned @wcb_wasafi is dropping a new hit today, you surely don’t wana miss this one,” ameandika Zari.

Daktari: Mwanamuziki Diamond Platnumz Anamuua Baba’ke

$
0
0
Baba Mzazi wa Diamond Platnumz

“Msongo wa mawazo ni tatizo kubwa duniani linalotokana na kusheheni kwa mawazo ya kila wakati, husasan kuhusu maisha au afya. Kwa hiyo anachofanya Diamond kwa baba yake ni sawa na kumuua kwa sababu ya kumsababishia msongo,” ndivyo alivyosema daktari Rweyemamu wa hospitali moja ya jijini Dar.
Daktari Rweyemamu alizungumza na Amani hivi karibuni kufuatia habari zinazoandikwa na Magazeti Pendwa ya Global Publishers kuhusu nyota wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ kwamba amemtelekeza baba yake, Abdul Juma.

AZUNGUMZIA HISTORIA

“Nimekuwa nikisoma habari mbalimbali kwenye Magazeti Pendwa ya Global, lakini hili la Diamond kumtelekeza baba yake mimi naona lina mapana yake. Najua utetezi wa Diamond ni kwamba, baba alimtelekeza mama yake (Sanura Kasim) yeye akiwa mtoto.
“Kwa hiyo malezi yote, ameyapata kwa mama mpaka kufika kwenye kiwango cha mafanikio. Lakini pia nimewahi kusoma kwamba, baba aliomba msamaha yaishe, atambulike kama baba lakini mtoto akagoma.”

MAGONJWA YA BABA
“Kuna wakati nikasoma kwamba, yule mzee anasumbuliwa na miguu, mara sijui ugonjwa wa kansa ya ngozi. Pia amekuwa mtu wa kuumwa mara kwa mara.”

MSONGO WA MAWAZO NI CHANZO 
“Yule mzee atakuwa na magonjwa mengi, hasa yanayotokana na msongo wa mawazo. Mawazo yake kwa sasa ni kitendo cha kuona mafanikio ya mwanaye akilinganisha na maisha yake magumu bila msaada.
“Binadamu yeyote, anapomwona mtu wake wa karibu amefanikiwa na yeye hali duni lakini huyo aliyefanikiwa anaweza kumsaidia yeye akaondokana na hali duni, lazima asumbuliwe na msongo.”

MIGOGORO, UGUMU WA MAISHA

“Lakini pia migogoro inayotokea katika familia, ni moja kati ya sababu zinazoweza kumpa mtu msongo wa mawazo, hasa pale ambapo utaichukulia ‘serious’ kwa kuwa inagusa moja kwa moja maisha yake. Ugumu wa maisha unachangia pia.”

MWILI UNAVYOATHIRIWA NA MSONGO

“Moja ya sababu ambazo zinachangia kwa kiasi kikubwa kuzorota kwa afya na kusababisha vifo vingi ni msongo wa mawazo. Mwili unavyokutana na hali tofauti aidha kitu cha kutisha au kinacholeta mawazo ndani ya muda mfupi na tofauti hiyo ikashindwa kutambuliwa haraka na ubongo mfano pale unapokutana na jambo usilolitegemea,  basi mwili hutoa kichocheo kinachoitwa cortisol ambacho kinamwagwa kwenye damu ili kuuandaa mwili aidha kupigana au kukikimbia kitu hicho.
“Mapigo ya moyo huongezeka, mapafu huchukua kiwango kikubwa cha hewa na mzunguko wa damu pia huongezeka na baadhi ya sehemu za kinga huzidiwa na mzigo mkubwa hivyo kutoa nafasi kwa viumbe adui kuushambulia mwili kirahisi.
“Msongo wa mawazo unapokuwa mkubwa siku hadi siku ndipo kinga ya mwili inavyozidi kushindwa kubaini uwepo wa kichocheo cha cortisol, msongo unapunguza makali ya kinga ya mwili, hivyo matatizo ya afya huongezeka.”

UTAFITI
“Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na World Health Organization, Shirika la Afya Duniani ‘WHO’, maradhi ya moyo, akili, ugumba, ukosefu wa nguvu za kiume na vidonda vya tumbo, pia yanacha-ngiwa na msongo wa mawazo.”

LAZIMA BABA DIAMOND AWE HIVI

Kwa mujibu wa daktari huyo, lazima baba Diamond wa sasa atakuwa amebadilika tabia, kwamba atakuwa mpole na siyo mwenye furaha kwa muda mwingi.
“Kuishi kwa kubangaiza pesa za kula huku akiwa anajua mwanaye anazo, tena mpaka zinamzidia, baba Diamond atakuwa anamalizika polepole. Lazima kila akiamka, anasema; ‘mateso yote haya, mwanangu yupo lakini hataki kunisaidia.”

WITO WAKE  KWA DIAMOND
Daktari huyo alisema kuwa, anamtaka Diamond kurejesha moyo wake nyuma, amtunze baba yake ili amuokoe na kumalizika.
“Namtaka Diamond ajue kuwa, anachomfanyia baba yake ni kumuua bila yeye kujua. Ukuta anaomuwekea katika usaidizi unamfanya mzee huyo kunyemelewa na magonjwa ya moyo na vidonda vya tumbo ambavyo kwa mazingira ya maisha yake yanaweza kumsumbua kwani yanahitaji kipato kizuri.

Chanzo:Global Publishers

Video ya Aje ya Alikiba imehit 1 Million views over one week

$
0
0
Ali Kiba
Hongera Alikiba #kingkiba Uzuri wa kazi yako ya Aje ndio uliofanikisha leo kupata views Million 1 just only over 1 week tangu iachiwe YouTube.

Umesimama mwenyewe bila collabo na umetoboa mwenyewe bila kubebwa na collabo,

#BigUpKiba
Viewing all 104808 articles
Browse latest View live


Latest Images

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596344.js" async> </script>