Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104789 articles
Browse latest View live

Picha: Young Dee apatana na Max Rioba?, washare picha wakiwa pamoja

$
0
0
Jumatano hii litapatikana jibu la kama ni kweli rapper Young Dee amepatana na boss wake wa zamani Max Rioba baada ya wawili hao kugombana miezi kadhaa iliyopita na kila mmoja kufanya kazi kivyake.

Jumapili hii wawili hao walishare picha katika mtandao wa kijamii na kila mmoja kuandika ujumbe wa ‘Happyfathersday#tuongeejumatano’ kauli ambayo imefurahiwa na mashabiki wengi.

Ugomvi wa Young Dee na bosi wake Max Rioba uliibua mambo mengi likiwemo la madai ya rapper huyo kuhusishwa na matumizi ya Madawa ya kulevya.

Haya ni maoni ya baadhi ya mashabiki wa kwenye mitandao baada ya kuona ujumbe huyo.

Alfredmbuya.
Am Gud kam humejitambua xamtimes kampan mbaya huchangia kukupoteza mdogo wang!

Saidmashua
Nimefurah sana mwanangu kurudi kwa max…………hope kila kitu kitaenda saana….!!!

Vituko vya uswazi
Nafulai kama utakua umejitambua kwasababu kati ya wanakuziki wote wenye umri mdogo wwe ndo unapendwa sana sasa tumia iyo Chans vizur usiipoteze tunakupnda xna achana na makundi yakixhenzi yanakuludixha nyuma.

Hellenkazimoto
Maximilian Rioba na Youngdaresalama u two made ma day..im impressed.empire for life

Bravepivot
Hatimaye umerudi kwenye mikono salama, respect kwa @maximilianrioba kweli we ni brother, angepotea uyo chalii

Hemedi20D
umetisha sana hapa nakuelewa sana ww na Max tena sana nmefurah mno kuona hivi I hope mangoma makali yatarudi upya kama enzi zile nmemiss flw zako kali bro

Basi la NBS kutoka Dar Kwenda Tabora na Basi la Kisbo, Yamepata ajali Morogoro, Watu Watano Wafariki, 27 Wajeruhiwa

$
0
0
Basi la NBS linalotoka Dar es salaam  kwenda Tabora  limepata ajali mbaya maeneo ya Chakwale wilayani Gairo  mkoani Morogoro.

Taarifa kutoka eneo la tukio zinaarifu kuwa watu 5 wamefariki na 27  wamejeruhiwa katika ajali hiyo.


Kwanini makampuni makubwa ya mafuta SHELL na BP yalijiondoa kufanya biashara Tanzania ?

$
0
0
Kampuni ya SHELL japo ilikuwa ama bado mpaka sasa iko kama NEMBO HALISI ya biashara ya mafuta nchini , lakini miaka mingi iliyopita ilijiondoa kufanya biashara nchini mwetu .

Juzi juzi miaka michache iliyopita tumeshuhudia kampuni lingine kubwa la BP , kampuni pekee lililoaminika kutochakachua mafuta nalo likifunga virago vyake.

Nilikuwa nawaomba wadau waliozifahamu sababu za makampuni haya kutukimbia watuwekee hapa tuzijadili na kujifunza , na ikibidi tujirekebishe ili tusije kukimbiwa na makampuni mengine .

By Erythrocyte/JF

Familia Yaingilia ishu ya Mwanaume Shoga Kumtaka Mwanamuziki Juma Jux...

$
0
0
 Familia ya staa wa Bongo Fleva, Juma Musa ‘Jux’ imeingilia kati ishu ya mwanaume ‘tata’, mkazi wa Dar, James Delicious aliyetangaza kumtaka kimapenzi msanii huyo ambaye ni mpenzi wa Mwanamuziki Vanessa Mdee ‘V-Money’.

Akizungumza na Wikienda kwa niaba ya familia, dada wa Jux, Fatu-ma Juma alisema kuwa hakuna kitu kinachowaudhi kama kijana huyo kutwa kutangaza kumpenda na kumtaka mdogo wao huyo wakati wote ni wanaume na ni kinyume cha maadili ya kidini (familia ya Kiislam), Kitanzania na Kiafrika kwa jumla.

“Kiukweli familia inachukizwa sana na tabia ya huyo kijana ambaye haoni aibu, tunamtaka kuacha mara moja kusumbua watu akitaka namba ya Jux la sivyo tutachukua hatua za kisheria kwani anatukera sana,” alisema Fatuma.

Hivi karibuni kijana huyo alitangaza kwenye mitandao ya kijamii kuwa lazima ampindue Vanessa kwa Jux kwani anampenda jamaa huyo kupita kiasi.


JWTZ Yakanusha Taarifa za Kuibwa Kwa Kifaru

$
0
0
Jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ)  limekanusha taarifa za kuibiwa kwa kifaru  cha jeshi zilizoripotiwa leo na gazeti la Dira  na kusema kuwa taarifa hizo hazina ukweli wowowte huku  likisisitiza ulinzi katika maeneo ya jeshi uko imara.

Akiongea na  waandishi wa habari leo  kukanusha habari hizo, msemaji wa jeshi hilo, Kanali Ngemela Lubinga amesema jeshi limesikitishwa sana na habari hizo za upotoshaji kwa kuwa zinachafua taswira ya jeshi na taifa kwa ujumla.

Amelitaka Gazeti la Dira kuomba radhi mara moja na wakishindwa kufanya hivyo hatua Kali na za kinidhamu zitachukuliwa dhidi yao

Irene Uwoya na Kajala Waingia Vitani

$
0
0

Ubuyu mzito! Mastaa wakubwa kunako Bongo Muvi, Irene Pancras Uwoya ‘mama Krish’ na Kajala Masanja ‘Kay’ wanadaiwa kuingia vitani, kisa mapenzi ya wasanii wa Bongo Fleva, Msami Giovani na Abbott Charles ‘Quick Racka’ Wikienda limeng’atwa sikio.

Chanzo kilicho karibu na wawili hao kilipenyeza ishu kuwa aliyeanza yote ni Uwoya baada ya kumchukua mpenzi wa Kajala ambaye ni kigogo serikalini jambo lililomkera na kulipiza kisasi kwa kumchukua Msami.

“Siku zote Kay (Kajala) si mzungumzaji sana zaidi ya vitendo, sasa baada ya kuona kigogo wake anatoka na Uwoya aliamua kulipiza kwa kutoka na Msami,” kilisema chanzo.

Chanzo hicho kiliendelea kutiririka kuwa baada ya Uwoya kuona Kajala amemchukua Msami alihamishia ‘majeshi’ kwa mpenzi wa zamani wa Kajala, Quick Racka. “Ni mwendo wa kulipiziana tu na unaambiwa kwa sasa wawili hao hawazungumzi yaani ni chui na paka,” kiliweka nukta chanzo hicho.

Ili kuweka ubuyu huo sawa, Wikienda lilimtafuta Msami ambaye alifunguka: “Ni kweli mimi na Kajala tuko karibu na mara ya mwisho alitumika na meneja wangu kunikabidhi gari kama sehemu ya jasho langu na hakuninunulia yeye, lakini hata kama kuna vitu vingine vinaendelea siyo mbaya kwani mimi ni mwanaume na yeye mwanamke.”

Alipotafutwa Quick Racka naye alisema: “Ujue kwanza mimi na Kajala mapenzi yetu yalikuwa ya kishkaji sana yaani naweza kutoka na mtu mwingine na yeye hivyohivyo ila hili la kuhusu kutoka na Uwoya si kweli na haijawahi kutokea.”

Kwa upande wa Uwoya alipotafutwa kulizungumzia hili alionesha hali ya kushangaa kisha akasema: “Duh! Sijawahi kuwa na mazoea na Quick Racka hata siku moja na wala mimi na Kajala hatuna tatizo lolote yaani hatujawahi kugombana.”

Alipotafutwa Kajala alipokea simu lakini hakusikilizana vizuri na mwandishi kutokana na kelele lakini alipopigiwa mara ya pili alipokea na kukaa kimya.

Jitihada ziliendelea kwa kumuandikia ‘waraka’ mrefu wenye madai hayo na kumtumia kwenye simu yake ambapo licha ya meseji kuonesha imemfikia napo hakujibu.

Video Queen Tunda Akwaa Aibu Kali...Adai Huwa Anakojoa Kwenye Swimming Pool

$
0
0

Video queen matata Bongo ambaye ni mpenzi wa msanii wa Bongo Fleva, David Genzi, Tunda Sabasita hivi karibuni alitupia video kwenye ukurasa wake wa Instagram, akitamka maneno ambayo watu walimshangaa na kudai kuwa anatia aibu.

Mrembo huyo ambaye alitupia video hiyo akiwa kwenye jakuzi na Mtangazaji wa Radio Choice FM, Gifty Stanford ‘Gigy Money’ wakati akiogelea, alitoa kichwa kwenye maji na kuanza kuelezea kuwa hakuna kitu kilichomkera kama jakuzi hilo kuwa na maji meupe badala ya bluu ambayo huwa akitoa haja ndogo haionekani.

Baada ya kupewa za uso na watu walioiona video hiyo, Wikienda lilimwendea hewani Tunda ambapo alisisitiza kuwa alichoongea ni kweli kabisa na hata siyo yeye peke yake bali ni watu wengi wanapenda kufanya hivyo kwa hiyo wasimshangae

Al Shabaab Waua Polisi Watano Kenya

$
0
0
MAOFISA watano wa Jeshi la Polisi nchini Kenya wameuawa leo mjini Mandera katika shambulizi lililotekelezwa na wapiganaji wa Kundi la Wanamgambo la Al Shabab kutoka Somalia.

Kamishna wa jimbo hilo la kaskazini Mashariki mwa Kenya, Bw. Job Borongo ameithibitishia kuwa wapiganaji hao walifanya shambulizi la kuvizia dhidi ya msafara wa magari ya polisi uliokuwa ukienda El Wak wakitumia guruneti. Maafisa hao tano waliangamia papo hapo huku gari walimokuwa wakisafiria likiharibiwa kabisa. Maafisa wengine wanne wamejeruhiwa vibaya.
Msafara huo wa polisi ulikuwa ukitoa ulinzi kwa msafara wa mabasi ya uchukuzi wa umma, desturi iliyoanzishwa baada ya wapiganaji hao kuteka basi moja na kuua abiria 28 wakristu.

Gavana wa Mandera, Bw. Ali Roba aliwalaumu maofisa wa polisi katika eneo hilo kwa kupuuza tahadhari iliyotolewa na wenyeji kuhusiana na mashambulio ya kigaidi. Roba anasema walipuuza vyanzo vya kiintelijensia vilivyotolewa kuhusiana na kuonekana kwa wapiganaji hao waliojihami.

Hii si mara ya kwanza Mandera kushuhudia mashambulizi ya Al Shabaab. Shambulizi hilo la Novemba, 2014 liliwaacha wasafiri wengi wasiokuwa waislamu na hofu ya kusafiri na hivyo kuilazimu serikali kutoa usalama kwa mabasi ya uchukuzi wa umma. Mwezi mmoja baadaye wapiganaji hao waliwaua wachimba migodi 36 katika eneo hilo la Mandera.

Kundi hilo la wapiganaji wa kiislamu limekuwa likitekeleza mashambulizi katika maeneo ya kaskazini mwa Kenya likitaka kuishinikiza taifa hilo jirani kuondoa majeshi yake nchini Somalia. Kenya ilipeleka vikosi vyake vya jeshi nchini Somalia mwaka wa 2011 ikitaka kuzima mashambulizi ya mara kwa mara.

Hata hivyo kundi hilo limeongeza mashambulizi nchini kenya ikiwemo mauaji ya watu 67 katika maduka ya Westgate mjini Nairobi mwaka 2013. Mwaka uliopita Al Shabab ilitekeleza mashambulizi katika chuo kikuu cha Garissa na kusababisha vifo vya wanafunzi 148

Kugomea Vikao Vya Bunge Sio Suluhisho Kwa Matatizo Ya Mwananchi Aliyekuchagua

$
0
0
Wabunge Wa UKAWA Wamekua Na Desturi Ya Kutoka Nje Ya Bunge Wakisingizia Kunyanyaswa Na Naibu Spika Jambo Ambalo Si La Kweli, Kwanza Wao Ndio Chanzo Cha Vurugu, Wanaomba Muongozo Kwa Jazba, Wanazomea Kama Watoto Na Kufanya Vurugu Zisizo Na Tija. Asante Genius Tulia Kwa Kuwaondoa Hawa Watu.

Naomba Serikali Izuie Mikutano Yao Kwani Muda Huu Si Wakufanya Siasa, Wasubiri 2020 Kampeni Zitakapoanza.

Huu Ni Muda Wakujenga Nchi Upya Hatutaki Siasa Mikutanoni, Siasa Tumeshamaliza 2015..

SOMA Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumanne ya June 21, Ikiwemo ya Rais Kukubali Kukatwa Kodi Kwenye Mafao yake

$
0
0


SOMA Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumanne ya June 21, Ikiwemo ya Rais Kukubali Kukatwa Kodi Kwenye Mafao yake

NAPE Nhauye Awashukia CCM...Adai Kumejaa Majipu

$
0
0
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye amesema ndani ya chama hicho tawala kuna majipu mengi yanayohitaji kutumbuliwa.

Kwa mujibu wa katibu huyo wa uenezi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mtama mkoani Lindi, hatua hiyo ndiyo njia pekee ya kuleta mapinduzi na mageuzi ndani ya chama hicho.

Amesema chama hicho kilishaingiliwa na makolokolo, hivyo yanahitaji kusafishwa yote kwa mustakabali wake.

Kauli ya Nape ni sawa na ile iliyowahi kutolewa na viongozi wakuu wa nchi. Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan mwanzoni mwa mwaka huu akiwa mkoani Tanga alisema ndani ya CCM kuna watu majipu ambao wameficha makucha ili wasijulikane uovu wao.

Siku ambayo Rais John Magufuli alipewa cheti na Tume ya Uchaguzi (NEC) baada ya kushinda uchaguzi alikwenda kwenye ofisi ndogo za CCM Lumumba na kuhutubia huku akisisitiza kuwa ndani ya chama hicho kuna watu wanafiki.

Nape anasema pamoja na kutumbua majipu, chama hicho pia kinahitaji kujitathimini muundo wake kwa kuwa uliopo sasa ni mkubwa na hauendani na hali halisi ya kipato cha chama.

“Muundo wetu ni mzigo mzito unaongeza urasimu. Kwa mfano wajumbe wa NEC hivi sasa wapo zaidi ya 400 ni mzigo mkubwa kwa chama matokeo yake walitumia fursa kutafuta ubunge, inahitaji marekebisho makubwa kwa kuwa uchumi wa chama ni mdogo kwa sasa, tunategemea ruzuku tu. "- Nape

Alisema hata katika upande wa watumishi wa chama wapo wengi sana na wote si wanasiasa, robo tu ndiyo wanasiasa.

Kwa mujibu wa Nape, kwa sasa kinachohitajika ni kutengeneza chama kidogo ili gharama ya kuendesha iwe ndogo.

Alisema sababu nyingine ya kusafisha chama kutokana na urasimu uliopo; “Lazima tupunguze mlolongo wa vikao vya kutoa maamuzi lakini pia tuangalie upya sera na taratibu zetu.”


 Akizungumzia watu wenye tabia ya kuhama vyama kama ilivyotokea kwa Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa na kundi lake, Nape alisema yeye si muumini wa hilo.

“Mimi siamini katika kuhama  vyama ni sawa na kumsilimisha Papa. Kwangu kuchukua watu kutoka upinzani ni sawa na gari zima kuwekewa vifaa chakavu. Watanzania waliopo katika vyama vya siasa hawazidi milioni 10 kwa nini tunyang’anyane wakati kuna zaidi ya watu milioni 45."- Nape


Akizungumzia utendaji wa Rais John Magufuli, Katibu huyo wa uenezi wa chama hicho anayetarajia kustaafu hivi karibuni katika mkutano mkuu alisema ameanza vizuri na kwamba mtindo wake wa kutumbua majipu ndiyo hasa ulikuwa ufanyike baada ya wananchi kukosa imani na Serikali kwa muda mrefu.

 “Yanayotekelezwa hivi sasa na Rais Magufuli ni ripoti yetu. Baada ya kuzunguka nchi nzima tuligundua mambo mengi na ili kukiweka salama chama hatuna budi kuhakikisha tunasafisha uozo wote.

“Ilifika wakati wawekezaji wamechukua ardhi hawaitumii, wananchi hawana ardhi tena matokeo yake ni migogoro kila kukicha, walimu wanadai haki yao watu wenye mamlaka hawatimizi wajibu wao matokeo yake kukaanza kujengeka hisia kwamba walimu ni wapinzani.

 "Hivi mtu anakuwaje mpinzani kama anadai haki yake? Mlipe kwanza haki yake uone kama ataendelea na malalamiko,” alisisitiza Nape ambaye aliingia rasmi katika siasa akiwa kijana mdogo wa miaka 20 tu.

Alisema Rais Magufuli amerejesha heshima kwani nchi ilifika mahali ambapo wezi wa mali ya umma walionekana ndiyo wajanja na wale ambao walikuwa wana maadili walionekana legelege.

Alisema jamii ilipotea na Taifa lilikuwa likijenga jamii ya ajabu ya watu mafisadi, wezi na wasioogopa mali ya umma na hawakuwa na wa kuwazuia kufanya wanavyotaka.

 Akizungumzia mchakato wa kumpata mgombea urais ndani ya chama chake uliofanyika mkoani Dodoma mwishoni mwa mwaka jana Nape alisema vikao vilikuwa vya moto sana.

“Wakati mwingine tulikaa katika mkutano mpaka saa tisa usiku na hata mkitoka hamtazamani usoni kila mmoja anaingia katika gari na kuondoka, palichemka sana.”

Hata hivyo, Nape alisema anashukuru Mwenyekiti wa chama hicho Taifa, Jakaya Kikwete kwa kuwa na kifua na hiyo ndiyo siri ya kufanikisha mchakato huo.

Alisema Kikwete ni mtoto wa CCM hivyo ilikuwa rahisi kumkata yeyote kwani uzoefu wake ndani ya chama ulisaidia na kwamba itachukua muda mrefu kupata kiongozi kama yeye lakini pia hawawezi kupuuza kazi iliyofanywa na Katibu Mkuu wa chama hicho Abdulrahman Kinana.

“Ukongwe ulituvusha lakini pia wazee wakarekebisha mambo tukavuka salama, hali ilikuwa mbaya lakini ndiyo demokrasia,” alisisitiza Nape ambaye ni mtoto wa mwanasiasa mkongwe, marehemu Moses Nnauye. CCM itafanya mkutano mkuu Julai 23 mwaka huu.

Msamaha wa Kodi ya Kiinua Mgongo kwa Wabunge, Mawaziri, Rais, Wakuu wa Mikoa na Wilaya Wafutwa

$
0
0
Waziri wa fedha akijibu hoja zilizotolewa na wabunge leo ametangaza rasmi viongozi wote wakuu wa serikali kuanzia Rais, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, na Wakuu wa Mikoa na Wilaya pamoja na wabunge wote viiunua mgongo vyao kukatwa kodi!

Hii ni baada ya wabunge kulalamika iweje wao wakatwe kodi na kuwwacha viongozi wengine wa kisiasa kukatwa kodi.

Babu Tale Anaweza Kuwa Kikwazo Chid Benz Kupona!

$
0
0
JUKWAA la burudani linafahamu kuhusu hali aliyonayo Mbongo Fleva, Rashid Makwiro ‘Chid Benz, ‘unga’ unamtesa na kumfanya kuporomoka kwa kiwango kikubwa kutoka kileleni kwa ubora hadi kuwa mtu anayeonewa huruma, kwa sababu hali yake kiafya imetetereka kiasi cha kuhitaji msaada, Wikienda linakupa zaidi.

Ingawa kipindi cha nyuma aliwahi kukana kwa nguvu zote juu ya matumizi ya unga (madawa ya kulevya), lakini siku zote maradhi hayajifichi na hatimaye, Chid Benz aliibuka hadharani na kuomba msaada kutoka kwa wadau, ili angalau awezeshwe kuachana na utumiaji wa unga, kitendo ambacho kilipokelewa kwa mikono miwili na wadau wa burudani.

Chid anakuwa msanii mwingine mkubwa, anayesukumwa nje ya ‘game’ kutokana na kuathirika na madawa hayo, akifuata nyazo za Rehema Chalamila ‘Ray C’ na aliyekuwa mwandani wake, Lord Eyez.

Kati ya watu waliojitokeza kumpa msaada ni pamoja na Hamis Taletale ‘Babu Tale’ ambaye ni meneja wa muda mrefu wa Kundi la Tip Top Connection lakini kwa sasa pia yupo katika benchi la viongozi ndani ya Lebo ya Wasafi (WCB).

Tale na Mbongo Fleva, Kalama Masoud ‘Kalapina’ walimpeleka Chid katika kituo cha kuwasaidia waathirika wa madawa ya kulevya ‘Sober House’ kilichopo Bagamoyo, Pwani ambako alipokelewa na uongozi katikati ya Machi, mwaka huu na akawa tayari kukabiliana na changamoto zilizopo mbele yake ili mradi aachane na ‘ujinga’ huo unaowapoteza vijana wengi.

Tale aliuambia umma kupitia baadhi ya vyombo vya habari kwamba, atakuwa tayari kuhakikisha Chid anarejea katika ubora wake. Lakini kule Sober House, msanii huyo alikaa siku 28 tu, akang’ang’ania kuondoka siku ambayo meneja huyo alikwenda kumtembelea.

Waandishi wa makala haya walidokezwa kuhusu kutokuwepo kwa Chid kule Sober, wakafunga safari hadi huko ambako uongozi wa kituo hicho ulikiri kuondoka kwa msanii huyo kabla ya muda aliostahili. Meneja wa kituo hicho, Tumaini Majira alisema angalau angekaa miezi mitatu ingesaidia.
Baada ya habari ile kutoka, takriban wiki mbili baada ya Chid kuondoka katika kituo hicho, Babu Tale alikuja juu akikanusha kuhusu msanii huyo kutoroka matibabu licha ya ukweli kuwa kabla ya habari hiyo kuandikwa, yeye kama mtu aliyempeleka, alipigiwa simu na kuombwa maoni yake,
lakini alikataa kusema lolote akidai kwa sasa hataki kusema, muda muafaka ukifika atafunguka.
Kuna vitu viwili hapa, kwanza Babu Tale alikaa kimya bila kuwataarifu Watanzania ambao awali alikuwa ‘laini’ ya mbele kupitia ‘media’ kusema juu ya nia yake ya kumsaidia Chid.
Kabla ya habari ya kutoroka Sober kuripotiwa na Global Publishers, wadau walikuwa wakijua msanii huyo anaendelea na matibabu.

Sijui ni kwa nini Tale alificha juu ya Chid kuondoka Bagamoyo kabla ya wakati? Kibaya zaidi, akatumia nguvu kubwa kukanusha kuhusu kutoroka, akipingana na meneja wa kituo hicho, aliyeongea kitaalam. Babu Tale aliuambia umma kuwa, msanii huyo hakutoroka, isipokuwa muda aliokaa ndiyo aliotakiwa!
Shame on him! Hakuna mwathirika wa unga wa kiwango cha Chid aliyewahi kutumia dawa za kumsaidia kuwa fiti kwa siku 28 kisha akawa sawa.

Lakini achana na hilo, habari mpya ni kwamba, baadhi ya wasomaji wetu walitaka kujua hali ya Chid kwa sasa baada ya kuwepo kwa madai kwamba, amerejea katika matumizi ya unga. Hivyo, ili kupata ukweli, gazeti hili lilitaka kujua, likatumia mbinu zote kumtafuta ili kuzungumza naye, lakini Babu Tale alifanikisha kwa kiwango kikubwa Chid Benz kutokupatikana!

Wikienda linaamini katika nguvu ya media, linajua endapo wadau watajulishwa kuhusu kinachoendelea kwa msanii wao, wapo ambao wangeweza kumsaidia kama kweli amerejea katika matumizi, kama Babu Tale ameshindwa.

Meneja huyo wa Tip Top, hataki Chid Benz ahojiwe, hataki msanii huyo ajieleze kwa sababu hata ukimpata ‘mkorofi’ huyo kwenye simu yake ya mkononi, anakwambia Babu Tale amemkataza kuongea chochote na media.

Baadhi ya wasanii waliozungumza na Wikienda juu ya nyendo za Babu Tale, walisema jamaa anataka kumtumia Chid ili kujinufaisha. Kwamba, kwa kuwa msanii huyo kwa sasa hajiwezi, anatumia udhaifu wake ili amuongoze, atengeneze wimbo, amfanyie ‘kavareji’ katika media anazozijua yeye, arudi upya halafu yeye ‘apige’ hela.

“Jamaa anajifanya ameukamata huu muziki kwa sasa, anataka kila mtu amnyenyekee. Awafanyie haohao sisi wengine tupo katika muziki kabla yeye hajaja mjini, tunakomaa na kitaeleweka,” alisema msanii mmoja mkongwe wa Hip Hop akimzungumzia Tale huku akiomba jina lake lihifadhiwe.
Alhamisi iliyopita, Wikienda lilimsaka Chid kwa siku nzima lakini hakupatikana licha ya kufika kwenye saluni moja iliyopo Magomeni ambayo gazeti lilitonywa kuwa, huwa anapatikana hapo.
Baadhi ya watu kwenye eneo hilo la saluni, walisema Chid hupatikana hapo na Tale hivyo wa kutafutwa zaidi ni meneja huyo.

Wikienda lilimpigia Babu Tale ambaye alitoa mwongozo atafutwe kesho yake, Ijumaa mchana. Kesho hiyo ilipofika, alipigiwa simu lakini akaomba apigiwe baadaye.

Wikienda lilimpigia hiyo baadaye, akaomba muda tena akisema atakuwa amekutana na Chid. Baada ya muda alioomba, akapigiwa, sasa hakupokea simu na wala hakujibu meseji.
Cha ajabu, mmoja wa vyanzo vya Wikienda kwenye saluni hiyo alipiga simu na kusema, Chid na Babu Tale wapo kwenye saluni hiyo lakini wanajiandaa kutimka.

Mpaka Ijumaa inakatika, Tale hakuwa ametoa ushirikiano wowote kwa Wikienda. Hakusema kwamba hajaonana na Chid na wala hakusema kwamba hataki Chid azungumze na vyombo vya habari.

Chanzo:Global Publishers

CHADEMA Wataka Mkutano Mkuu wa CCM Kumkabidhi Uenyekiti Magufuli Nao Uzuiliwe

$
0
0
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetoa tamko zito kikitaka Polisi kuzuia Mkutano Mkuu wa CCM utakaofanyika mwezi ujao, vinginevyo watatumia nguvu ya umma kuuzuia.

CCM kimeitisha mkutano mkuu maalumu unaotarajiwa kufanyika Julai 23 mjini Dodoma, kwa lengo la Mwenyekiti wa chama hicho, Jakaya Kikwete kumkabidhi uongozi wa chama, Rais John Magufuli.

Kauli ya kutaka Polisi kuzuia mkutano huo kama inavyofanya kwa vyama vingine vya siasa, ilitolewa juzi mjini Moshi na Katibu Mkuu wa Baraza la Vijana wa Chadema (Bavicha), Julius Mwita.

Msimamo huo wa Chadema ambao uliungwa mkono na Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Zanzibar, Salum Mwalim unafuatia Polisi kuzuia mahafali ya wahitimu wa vyuo vikuu ambao ni wanachama wao.

Akizungumza na wanahabari, Mwita alikwenda mbali na kudai kuwa, Chadema watalifungulia Jeshi la Polisi kesi ya madai ya fidia kwa kuvuruga mahafali ya Chaso mjini Dodoma mwishoni mwa wiki iliyopita.

“Ukisoma barua yao wamesema wamezuia mikutano ya hadhara sasa kama wanakuja hadi kwenye vikao vya ndani, hatuwezi kuendelea kukubali jambo hili.Tumetumia busara sana,” alisema Mwita na kuongeza:

“Msipouzuia Mkutano Mkuu wa CCM Dodoma Julai 23 tunakuja kuuzuia sisi... yaani muwe tayari kusafiri kwenda Dodoma tukauzuie ule mkutano la sivyo, wauzuie kama walivyouzuia mikutano yetu.”

Mwita alimgeukia Mwalimu na kumweleza kuwa hiyo ni lugha ya ujana na inatekelezeka, akawahoji vijana wa Chaso waliokuwapo: “Wangapi mko tayari kuja Dodoma?” Wote wakaafiki.

“Intelijensia ya polisi ni ya kiumbea, inayoweza kujua tu Chadema wanakwenda kwenye mkutano, haiwezi kujua watu wamejificha wana bunduki na risasi 300 kwenye mawe kule Mwanza,” alidai.

Mwalimu alisema utaratibu wa Polisi na Serikali lazima ukome na kwamba wao ni viongozi.

Mambo Matano ya Kufahamu Baada ya Kadi za UDART Kuanza Kutumika

$
0
0
Abiria wa mabasi yaendayo haraka Jijini Dar es salaam leo June 20 2016 wameanza kutumia kadi maalumu za kielektroniki badala ya tiketi. Mfumo huu ambao utamuwezesha abiria kuweka fedha katika kadi hio kwa kutumia mitandao ya simu na utasaidia kupunguza msongamao katika vituo vya ukataji tiketi.

HAYA NI MAMBO MATANO YA KUFAHAMU

1.Unapokwenda kununua kadi utapewa maelekezo ya namna ya kujisajili, kuna namba ya *152*22# ukipiga namba itakupa maelekezo, utachagua kwenye menu litatokea neno DART itakupa maelekezo kama unajisajili utatakiwa kujaza namba ya kadi, utajaza majina yako na utaweka namba yako ya siri.

2.Ukipoteza kadi hatua ya kwanza unaweza kuifunga isitumike na mtu mwingine kwa kubonyeza *152*22# unachagua DART itakuja option ya kuifunga.

3.Kadi ikinunuliwa tayari ina muda wa kusafiri, kwamba hutalazimika kufanya Top up  baada ya kuinunua, kadi utainunua 500 lakini utakuwa na muda wa kusafiri wa sh 4500, baada ya kuwa umeshainunua unaweza kusafiri muda huohuo.

4.Ukipoteza kadi na ukitaka kupata mpya, kama iliyopotea ina muda wako wa kusafiri taarifa zako zitasaidia kupata kadi mpya na utarudisha pia salio lako ambalo litakuwa limebaki.

5.Wanafunzi wataendelea kutumia tiketi kwa sababu mfumo wa tiketi pia bado utatumika sanjari na matumizi ya kadi, usajili wa mwanafunzi ili wapate kadi zao utachukua muda.

AUDIO: Wananchi Wamempeleka Polisi Mama wa Mtoto Kisa Mtoto ni Mwarabu

$
0
0
June 20 2016  Geah Habib kupitia Hekaheka ya Clouds FM  ametuletea Hekaheka kutokea Buguruni Dar es salam ambapo mama amepelekwa polisi na wananchi kisa mtoto anayedaiwa kuwa ni wa kwake ni mwarabu.

Mama alifika maeneo hayo nyakati za usiku na watu wakawa na mashaka naye wakamwambia aende kwa mjumbe……..

’Shida yake yeye ni kwamba anamuhitaji ndugu yake alikuwa bungoni lakini alipofika alikuwa ameshahama na kuna ndugu zake wengine akaomba kulala kwa sababu hawezi kufika mbezi kwa usiku huo, nikamwambia twende kituo cha polisi hapo zogo ndio likaanza’:-Mjumbe

kwa nini mnakuwa washamba hapa Dar es salaam hamna watu waliozaa na wahindi au waarabu mpaka mnakuja kunishangaa mimi, hapa nishaadhalilishwa sana kwa hiyo twende polisi nikamshtaki aliyenidhalilisha‘:-Mama wa mtoto

Unaweza kusikiliza kwa kubonyeza play hapa chini:

New Video Alert:Diamond Platnumz ft P Square

$
0
0
Hii imekuwa video iliyosambaa zaidi mitandaoni baad aya kutolewa kama tangazo kuwa msanii Diamond Playnumz anatoa kazi yake mpya aliyofanya na wasanii wa kimataifa kutoka Nigeria P Square.

Leo Diamond ameandika haya Katika Ukurasa wake wa Instagram:
"My People!!!!!!!!! Subscribe to my Youtube Channel now so that you can be the first one to watch the HIT from SIMBA ft P-SQUARE!!!! (Najua unakiu kias gani....haya Jiunge na Channel yangu ya YOUTUBE sasa ili uwe mtu wa kwanza kushuhudia Mshine yangu Mpya Nilowashirikisha P-SQUARE! ) Cc @peterpsquare @rudeboypsquare #SimbaKaseMa"

Hii ni miongoni mwa collabo zilizosubiriwa kwa shauku kubwa na mashabiki wa bongo fleva,nyingini ni pamoja na collabo yake na Neyo na WizKid.

Nuh Mziwanda Ajichora Tatooo ya Mpenzi Wake Mpya...Adai Huyu wa Sasa Amekuja Kwa Gia Kubwa....

$
0
0
Nuh Mziwanda Baada ya Kumpata mpenzi mpya amejikuta amerudia alilofanya kwa Shilole la Kujichora Tatoo Mkononi ya jina la mpenzi wake huyo mpya..

Nuh Amesema huyu wa sasa amekuja na gia kubwa sana kiasa anaamini anampenda kwa dhati, amempa sifa kuwa ni mwanamke anayependa marafiki zake sana tofauti alivyokuwa shilole...

Wataalamu wa Prescion Air na TCAA Waelekea Zanziba r Kuchunguza Tukio la Ndege Kuwaka Moto

$
0
0
Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), wakishirikiana na mafundi wa Kampuni ya Ndege ya Prescion Air wameelekea Zanzibar kuchunguza tukio la ndege ya kampuni hiyo kupata hitilafu na kuwaka moto na kusitisha safari.

Tukio hilo lilitokea Juni 16 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Karume mjini Zanzibar.

Taarifa iliyotolewa jana na Mkuu wa Mawasiliano wa Prescion Air, Azda Mkullo inasema wamepeleka injini mbadala kwa ajili ya kufungwa.

Inaongeza kuwa baada ya tukio hilo ilimlazimu rubani kuchukua hatua za kuuzima moto na kuirudisha ndege kwenye eneo la maegesho.

Ndege hiyo wakati ikipata hitilafu ilikuwa imefanya safari zake kati ya Kilimanjaro na Dar es Salaam.Ndege hiyo PW432 ilikuwa na abiria 34 na wahudumu wanne wote walitoka salama.

Wabunge wa Ukawa Waendelea na Mgomo...Wametoka Leo Tena nje Bunge

$
0
0

Wabunge wa Ukawa wameendelea kususia vikao vinavyoongozwa na Dk Tulia Ackson, lakini leo wametoka kimyakimya bila mbwembwe kama za jana.


Kwa sasa kamati ya uongozi ya umoja huo imeingia kufanya kikao kujadili mustakabali wao.


Mbunge wa Vunjo (NCCR-Mageuzi), James Mbatia amesema watatoa taarifa kamili baada ya kumaliza kikao hicho.
Viewing all 104789 articles
Browse latest View live




Latest Images