Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104799 articles
Browse latest View live

MAFURIKO KITU GANI BWANA....BIA NDIO MPANGO MZIMA

$
0
0
Kifo cha Imamu sio mwisho wa Ibada.... Hata mafuriko si sababu ya kuacha kunywa pombe kwa hawa jamaa

EXCLUSIVE DOWNLOAD WIMBO MPYA WA LADY JAY DEE-NASIMAMA

$
0
0

Wimbo mpya wa Lady Jay Dee Alio uachia leo hii ... Sikiliza ama Download hapo chini:

AJALI YA HELKOPTA..MAGUFULI, BILAL, KOVA NA MKUU WA MKOA WA DAR WANUSURIKA

$
0
0
Katika kukagua uharibifu wa miundombinu uliosababishwa na mvua kubwa katika Jiji la Dsm, Makamu wa Rais Dk. Mohamed Gharib Bilal, Dk.John Magufuli, Mkuu wa Mkoa wa Dar, Meck Sadiki na Afande Kova wamenusurika ajali ya helikopita iliyotokea leo Jijini Dsm. 

Jamani tumuombe mwenyezi Mungu awalinde hawa viongozi wetu wapendwa waliokuwa katika kuwatumikia watanzania. Natoa baadhi ya picha za helikopita hiyo ikizimwa moto:

walio nusurika ni

1. Makamu wa Rais, Dr. Bilal

2. Mkuu wa mkoa wa Dar, Sadik

3. Mkuu wa polisi Kanda Maalum, Kova

Wamepata majeraha kidogo walikuwa wakikaguwa athari za mvua jijini

TAARIFA YA POLISI KUHUSU IDADI YA WATU WALIOFARIKI KUTOKANA NA MAFURIKO

$
0
0
Kutokana na mvua zinazonyesha hivi sasa kwenye jiji la Dar es salaam pamoja na kusababisha mambo mengi kusimama, miundombinu kuharibika hasa madaraja yanayounganisha njia kuu, pia zimesababisha vifo vya watu 10.
Nyumba nyingi zimeingia maji hasa maeneo ya mabondeni na kulazimisha familia kuhama kutoka kwenye makazi yao ambapo mpaka sasa Polisi Dar es salaam inasema  watu kumi waliofariki, wamo watoto watano na watu wazima watano.
Kamanda Suleiman Kova wa kanda maalum ya Dar es salaam amesisitiza hali sio nzuri hivyo wananchi wanatakiwa wachuke tahadhari kwenye makazi yao na hata wanaotembea na magari barabarani kwa sababu njia nyingi zina mashimo na pia watu wapunguze mizunguko isiyo lazima barabarani.

TWEET YA JERRY SILAA YAONYESHA ZARAU KWA WAHANGA WA MAFURIKO DAR

$
0
0
Huu ni mtizamo wangu, na nilimfahamisha Mstahiki meya Jerry Silaa pia: huyu mtu ana bahati sana kwamba ni Meya wa manispaa nchini Tanzania, ambapo ukisahapata uongozi upo huru kufanya lolote lile- baya au zuri, la busara au la kipuuzi- pasi kuchelea matokeo. Laiti huyu mtu angekuwa Meya wa eneo lolote lile hapa Uingereza, basi Jumatatu angekumbana na wito wa kumtaka aachie ngazi. Ndio, uwepo wake Dar (Ilala) usingezuwia mafuriko, lakini sote twatambua kuwa nyakati za majanga zinahitaji viongozi kuonyesha uongozi kwa dhati (showing leadership). Kilichompeleka Mwanza ni shughuli za kichama, ambazo ninaamini zingeweza kusubiri hadi janga linalowasibu anaowaongoza limeshughulikiwa. 

Japo mwanzoni alileta majibu ya dharau baada ya kusoma 'tweets' hizo mbili za mwanzo hapo juu, lakini akakumbana na hasira za wananchi wengi ambao hawakupendezwa na majibu yake. Lakini kwa vile neno 'samahani' halipo kwenye kamusi za wengi wa viongozi wetu, Mstahiki Meya 'aliingia mitini' kimyakimya...na hajaonekana tena huko twitter hadi wakati ninaposti bandiko hili.

Swali la msingi: Hivi Katiba Mpya tunayohangaika kuipata huko Dodoma itaweza kweli kutengeneza mazingira yatakayowawezesha wananchi kuwashughulikia 'wahuni wa kisiasa' (political thugs)? Jeuri kubwa inayowafanya watawala wetu kufanya (including kusema) chochote ni kutochelea matokeo. Na japo Katiba tuliyo nayo sasa ina sheria nzuri tu za kumpatia mwananchi kile anachostahili (kwa maana ya haki zake), tatizo limebaki katika usimamizi wa sheria hizo, na pengine kubwa zaidi, sheria hizo kubaki kama maandiko tu yasiyoheshimiwa. Je Katiba Mpya (laiti ikipatikana) itaheshimiwa?

Finally, ninaamini Mstahiki Meya Silaa nafsi itamsuta na atakatisha ziara yake huko Mwanza na kuungana na wananchi katika harakati za kukabiliana na athari za mafuriko Dar (kwa yeye ni Manisapaa ya Ilala). See, kwenda kumwona mgonjwa hakumaanishi kutamfanya aopone bali kwaonyesha kuwa flani anajali. Kadhalika, tunapokwenda kwenye misiba haimaanishi kuwa tutamfufua marehemu, lakini ile tu kuwafariji wafiwa kunaonyesha kuwa tunajali. Nam ,Meya Slaa akiwa Illa/Dar hatozuiwa athari za mafuriko (au kama alivyosema mwenyewe "hawezi kzuwia mvua") lakini kibanadamu tu anapaswa kuwa na wahanga wa mafuriko (japo yeye ana-pick and choose nani anastahili kuitwa mhanga)

By Kibo10 

Source: JF

NOW HAKUNA KUINGIA / KUTOKA DAR....MTU RUVU WAFUNIKA DARAJA LA RUVU...TAZAMA PICHA HAPA

$
0
0


Maji yaliojaa pande zote za Barabara ya Morogoro Chalinze Eneo la Ruvu darajani muda huu.Maji ni Mengi Mto haujulikani unapoanzia na kuishia maji yamejaa pande zote za barabara,Magari yamesimama na hakuna Gari linalovuka daraja la Ruvu kwa sasa.

Msururu Mkubwa wa Magari barabara ya Chalinze Mlanzidi Eneo la Ruvu Darajani,Hali hii anatokana na Mvua Zinazozidi Kunyesha hali iliyopelekea Maji kujaa na Kukatiza Juu ya Barabara,Kwa usalama magari yote yamesimama kusubiri hali kutengemaa.

MUHIDIN GURUMO (ALIYEKUWA MSONDO NGOMA) AFARIKI DUNIA

$
0
0
Muhidin Gurumo (aliyekuwa Msondo Ngoma) afariki dunia!

Habari za hivi punde zinasema kuwa Nguli wa mziki wa bance Mzee wetu Muhidim Ngurumo amefariki dunia mchana siku hii ya leo.

Pole ziwafikie wapenzi wote na mashabiki!!


R.I.P Gurumo.
Chanzo.Uhuru Fm

YAHISIWA KUNA MTU AMEFARIKI DARAJA LA MATUMBI (MANDELA ROAD) MWILI WATOA HARUFU KALI

$
0
0
Daraja la Matumbi (Mandela Rd): Utafutaji wa mwili unaotoa harufu kali unaendelea muda huu!
Habari Kamili Baadae

MAPYA YAIBUKA NDEGE ILIYOPOTEA, RUBANI ALIPIGA SIMU ANGANI

$
0
0
Rubani msaidizi wa ndege iliyopotea namba MH370 alipiga simu yake ya mkononi wakati ndege ikiruka chini chini kupita pwani ya magharibi mwa Malaysia.

Wachunguzi wamegundua kwamba simu hiyo ilipigwa kutoka kwenye simu ya mkononi ya Fariq Abdul Hamid wakati Boeing 777 ikiruka chini chini karibu na kisiwa cha Penang, kaskazini mwa pwani ya magharibi ya Malaysia.
Gazeti la The New Straits Times limeripoti leo kwamba ilifahamika ndege hiyo, ilikiwa na watu 239 ndani yake, ilikuwa ikiruka chini chini kiasi cha minara ya mawasiliano iliyokuwa karibu kuweza kunasa ishara za Fariq.
Simu hiyo ilikatika ghafla, hata hivyo imefahamika kwamba mawasiliano yalirushwa na kituo kidogo cha mawasiliano kilichopo kwenye jimbo la Penang.
Gazeti hilo lilisemwa kwamba haikuweza kujulikana mara moja Fariq alikuwa akimpigia nani 'kutokana na chanzo cha habari kutotaka kuweka bayana taarifa zaidi za uchunguzi.'

Liliongeza: "Mnara wa kampuni ya mawasiliano ulinasa simu hiyo aliyokuwa akijaribu kupiga.
"Kuhusu kwanini simu hiyo ilikatika, inawezekana sababu ndege hiyo ilikuwa ikienda kwa kasi mbali na mnara huo na haikuweza kupata mawasiliano kwenye mnara unaofuatia," gazeti hilo lilisema, likinukuu vyanzo vya habari.
Gazeti hilo liliongeza kwamba imebainika pia kwamba mawasiliano ya mwisho ya Fariq yalikuwa kupitia WhatsApp na kwamba yalifanyika majira ya Saa 5:30 usiku wa Machi 7, muda mfupi kabla hajapanda ndege hiyo kuanza safari ya masaa sita kwenda Beijing, China.
The New Straits Times lilisema lilielezwa kwamba ukaguzi wa kumbukumbu kwenye simu ya Fariq ulionesha kwamba mtu wa mwisho kabisa kuongea naye ilikuwa 'mtu wake wa kawaida (namba iliyokuwa ikijirudia rudia katika orodha ya simu zake alizopiga).'
Simu hiyo ya mwisho, lilisema gazeti hilo, ilipigwa sio zaidi ya masaa mawili kabla ya ndege hiyo kuruka saa 6:41 usiku wa Machi8 kutoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kuala Lumpur.
Vyanzo tofauti vililieleza gazeti hilo kwamba ukaguzi kwenye simu ya Fariq ulionesha kwamba mahusiano na simu hiyo aliyopiga simu hiyo ya mwisho kabla ya kupanda ndege hiyo yalikuwa 'adilifu'.
"Hii ni matokeo ya kawaida kwa simu hiyo kuwa imezimwa.
"Wakati fulani, hatahivyo, wakati ndege hiyo ikiwa angani, kati ya Igari na eneo hilo karibu na Penang (muda mfupi kabla ya ndege hiyo kupotea kwenye rada), laini hiyo 'iliunganishwa tena'."
Gazeti hilo lilisema kwamba uunganishwaji haumaanishi kwamba lazima simu hiyo kwamba ilipigwa. Inawezekana pia ni matokeo ya simu hiyo kuwa imewashwa tena.
Jana ilionekana kama kisanduku cheusi kinaweza kuwa kimepatikana chini katika Bahari ya Hindi.
Kituo cha redio cha 6PR kilituma ujumbe katika twitter ugunduzi huo, kikimnukuu mtaalamu wa anga Geoffrey Thomas, ambaye alibainisha kinasa taarifa hicho cha ndege hiyo hatimaye kimepatikana zaidi ya mwezi mmoja baada ya Boeing 777 kupotea.
Waziri Mkuu wa Australia Tony Abbott, ambaye yuko nchini China, alisema watafutaji wana 'uhakika' ishara hizo zilizopatikana zilikuwa kutoka kwenye kisanduku cheusi kutoka kwenye ndege ya MH370.
"Hakika sitaki kusema taarifa zaidi ya hapo kwa wakati huu... kama ishara ya heshima kwa watu wa China na familia zao."

VIDEO IKIONESHA JINSI DARAJA LA BARABARA YA BAGAMOYO LILIVYOKUWA LINAVUNJIKA

$
0
0
Angalia Video Hapa Chini Jinsi Daraja la Mpiji hapa Maeneo ya Bunju Mpakani mwa Dar na Bagamoyo lilivyokuwa linavunjika...... Watu 10 wamepoteza maisha jijini Dar es Salaam,huku mawasiliano kati ya jiji la Dar-Es-Salaam na wilaya ya Bagamoyo mkoa wa Pwani yakisimama kwa zaidi ya siku tatu,mara baada ya tuta la barabara pembezoni mwa daraja la mto Mpiji kusombwa na maji umbali wa mita arobani na kuleta adha kwa wananchi wanao tumia barabara hiyo.

HATIMAYE AZAM FC WACHUKUA UBINGWA WA LIGI KUU YA TANZANIA SIMBA NA YANGA TUPA KULE

$
0
0
Ni baada ya kuilaza Mbeya City bao 2-1 katika Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya hivi punde na kufikisha jumla ya pointi 59 ambazo haziwezi kufikiwa na timu nyingine yoyote! Hivyo Azam Ndio Mabingwa wapya wa Ligi kuu ya Tanzania 2014

HAYA MAVAZI YA NYAKATI ZA USIKU NI MATATIZO. HUYU DADA YUPO MTUPU KABISAAAA

$
0
0
Hivi Huyu Dada Akitokea kabakwa na Huyu Bado bado Mbele ya Safari Atamlaumu nani ? Yani Hapo Kavaa Kichupi tu kwa Madai anaenda Club.....Mweeee Dareva wa Bado Bado Full Kushawishika....Majaribu Mengine Si Mazuri Dada Zetu......

BINTI WA KIBONGO MWANA CHUO ASABABISHA MZUNGU KUFUKUZWA KAZI

$
0
0
Raia mmoja wa nchini Finland amejikuta katika wakati mgumu sana baada ya kushindwa kufanya lolote kazini alipoajiriwa baada ya kutaka kuwa katika mahusiano na mwanadada huyu wa chuo kikuu cha Dar es salaam ambaye alimteka akili kiasi cha kumfanya Mzungu huyo kuwa anashinda chuoni kutwa nzima kubembeleza akubaliwe jambo lililomsababishia aache kuhudhuria kazini kwa muda wa miezi mine mfululizo kutokana na kupagawishwa na uzuri wa mwanadada huyu ambao umemfanya awe gumzo chuo kizima. Mzungu huyo  ambaye ni muajiriwa wa kampuni moja ya simu za mkononi (Jina limehifadhiwa) hapa jijini alikuja Tanzania mwaka jana kwa dhumuni la kufanya kazi kwa mkataba amejitia matatizoni baada ya kumtaka kimapenzi mrembo huyu ambaye alikutananae kwa mara ya kwanza katika coffe bar moja iliyopo Mlimani city na kwakushindwa kuzuia hisia zake alijikuta akiomba mawasiliano ya mrembo huyu jambo ambalo ndio hasa limemsababishia matatizo kutokana na ukweli kwamba Mzungu huyo amekuwa akimbembeleza sana mrembo huyu bila mafanikio  kiasi cha kumfanya aweanashinda Chuoni kwa huyu dada huyu Mlimani main campas. 

Utoro sugu wa Mzungu huyo umemuweka katika wakati mgumu kwani amepewa barua mbili za onyo mpaka sasa na amebakiza barua ya mwisho aachishwe kazi jambo ambalo mwenyewe anasema kuwa yuko katika wakati mgumu sana kwani hayuko tayari kumkosa dada huyo licha ya ukweli kwamba nchini kwao ameacha mke na watoto. 
Nilipomfanyia mahojiano dada huyo alidai hawezi kuwa na mtu ambaye hana m,alengo nae ya muda mrefu kwani uwepo wake hapa nchini ni wa muda mfupi tu hivyo yeye hayuko tayari kuwa kama chombo cha starehe kwa kila mpita njia. Licha ya kumpongeza dada huyo nilitaka nifahamu kama ameshamwambia ukweli Mzungu huyo ambapo dada alieleza kuwa ukweli ameshamwambia lakini jamaa huyo amekuwa king’ang’anizi kiasi cha kumnyima mpaka muda wa kujisomea jambo linalomfanya akate shauri la kwenda kumripoti katika kituo cha polisi kilichopo chuoni hapo endapo kesho siku ya kesho atathubutu kumfata tena

JUX AFANYE VIDEO YAKE MPYA CHINI AKIWA NA JACK CLIFF

$
0
0
Kuna Habari zinazozagaa kuwa Video Mpya ya Jux ya wimbo Nitasubiri amefanya na Jack Cliff Ambae ilisemekana yupo Jela huko Macau Chini....Habari hizi zimekuja baada ya Jux Kupost picha ya Mrembo kwenye hiyo Video Bila Kumuonesha Sura......Je Tutegemee Suprise ya Nguvu ama?

MADUKA YA WATANZANIA SOUTH AFRICA YACHOMWA MOTO-WADAIWA KUUZA UNGA

$
0
0
Afrika Kusini ni nchi yenye uchumi mkubwa Afrika ambao umevutia Waafrika wengi kukimbilia huko kwa ajili ya kufanya kazi kama za Udereva, uuzaji mafuta kwenye vituo vya mafuta pamoja na kazi nyingine mbalimbali.
Taarifa kutoka kwenye mji wa Pretoria ni kwamba Watanzania ambao wanamiliki na kufanya biashara mbalimbali zikiwemo za Maduka na wale wanaomiliki hoteli, wamevamiwa wakiwa kwenye mali zao na kufanyiwa uharibifu na nyingine kuchomwa moto.
Ni kundi la watu ambalo linaendeleza uvamizi huu ambapo linawashutumu Watanzania hawa kuhusika na biashara ya dawa za kulevya, yani kwa ufupi Watanzania wanasema hata kama kweli wangekua wanafanya hii biashara, walio na mamlaka ya kuwavamia ni Polisi na sio hao raia.

Inaaminika kundi hili lina sehemu kubwa ya madereva Taxi wazawa wa nchi hiyo ambao wamekua wakiumizwa na jitihada za raia wa kigeni wa Nigeria na Watanzania ambao wamejazana kwenye mtaa wao wakimiliki maduka mbalimbali yakiwemo ya nguo pamoja na hoteli.
Tayari balozi wa Tanzania amekutana na Watanzania hao na kuahidi kulifatilia ambapo ni Watanzania watano wamejeruhiwa wakiwemo watatu ambao bado wako hospitali na mmoja wao kavunjika mkono, mmoja kapigwa kichwani.
Kabla ya Watanzania wengine kuwahi kufunga maduka yao, maduka matatu ya Watanzania pamoja na hoteli mbili zinazomilikiwa na Watanzania zilivamiwa na wakachuchukuliwa simu na watu kupigwa ambapo polisi walipokuja hakuna chochote kilichofanyika zaidi ya maelezo.
Picha hizi zote zilipigwa na Mtanzania akiwa anakimbia baada ya kufanikiwa kufunga duka lake.

ALICHOSEMA JUX BAADA YA UMBEA KUZAGAA KUWA AMEFANYA VIDEO NA JACK CLIFF

$
0
0
December 2013 zilitoka stori kwamba Mtanzania Jackie Cliff ambae ni mrembo aliewahi kutokea kwenye video kadhaa za wasanii wa bongofleva amekamatwa na dawa za kulevya huko China.
Jackie Cliff ni mpenzi wa msanii wa bongofleva aitwae Jux ambae amehojiwa na Gossip Cop Soudy Brown baada ya picha kadhaa kusambaa akitengeneza video yake mpya huko China na mrembo ambae hajaonekana sura, ishu ambayo imefanya wengi wahisi kwamba ni Jackie Cliff.
Jux amekanusha stori kwamba hivyo video amefanya na Jackie Cliff na kusisitiza kwamba kutomuweka Jack kwenye hiyo video ni kutokana na sababu zake binafsi na wala hataki kuzungumza zaidi kuhusu hizo ishu.
Namkariri akisema ‘siwezi kusema ila kama atakuepo kwenye video au hatokuepo… ni watu wenyewe wataona’
Kwenye sentensi nyingine Jux amekanusha stori za kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Vanessa Mdee ‘V money’ kwamba ni rafiki yake tu ila hakuna kingine cha zaidi’

WAPI ZITTO KABWE BUNGE LA KATIBA...?

$
0
0
Wadakuz napenda kujua wapi ndugu zitto kabwe mbona haonekani katika mjadala wa katiba bungeni? Hasikiki Kabisa ...Yale Machachari yake Nimeyamiss ...naomba mwenye data zake atuwekee humu...

AJALI MBAYA ENEO LA LUGALO JIJINI DAR

$
0
0

AJALI hii imetokea leo asubuhi baada ya magari kusimamishwa ghafla eneo la Lugalo, Makongo ili kuruhusu wanafunzi wavuke ndipo lori liliposhindwa kusimama na kuparamia kingo za barabarani kisha kuiangukia gari dogo aina ya Toyota Cresta 'GX 100'.

BONGO MUVI KWAWAKA MOTO

$
0
0
Stori: Gladness Mallya na Hamida Hassan

PENYE wengi pana mengi! Lile kundi la mastaa waigizaji wa Kibongo, Bongo Movie Unity, linadaiwa kuparanganyika baada ya kuwaka moto kufuatia mwenyekiti wao, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ kudaiwa kuwa na upendeleo kwa baadhi ya wanachama wa jinsia ya kike.

Habari za uhakika kutoka kwa chanzo makini ndani ya kundi hilo zilieleza kuwa mwenyekiti wao huyo amekuwa na tabia ya kuwaburuza wanachama wake kama magari mabovu huku wakishindwa kubishana naye kwa lolote hivyo kila kitu anapanga mwenyewe kwa akili zake na anataka kiende kama anavyotaka.

Chanzo hicho kilidai kwamba mfano halisi ni hivi karibuni ambapo wasanii hao walikuwa wakisherehekea miaka mitatu tangu kuanzishwa kwake, Steve alipanga kila kitu mwenyewe pamoja na kwamba walichagua kamati lakini hazikufanya kazi yoyote.

“Jamaa anaamua vitu mwenyewe, halafu anatupeleka sisi wanachama kama gari bovu, sasa angalia ndani ya kundi hakuna maelewano, wanachama wengine wameamua kujitoa kama Ray (Vincent Kigosi), ameshajitoa pia mmoja wa waanzilishi Jimmy Mafufu amejitoa, sijui ataishia wapi huyu mwenyekiti na uamuzi wake,” kilisema chanzo hicho.

Wanachama mbalimbali wamekuwa wakilalamikia kitendo cha mwenyekiti wao kutoa tuzo kwa wanawake anaodaiwa kuwa nao, badala ya kutoa kwa wale wanaofanya vizuri kweli.

“Eti kama yule msanii aliyempa tuzo ya kwamba anajiheshimu anayeitwa Mille ana heshima gani, ameacha kumpa mwanzilishi wa kundi hilo hata kumpongeza tu na kwenda kuwapa hao huku wakimweka nyuma kabisa mwanzilishi ambaye ni Jimmy Mafufu jamani tunaenda wapi,” kilisema chanzo.

Akizungumza kwa masikitiko juu ya sakata hilo, Mafufu alisema anaumizwa na tabia ya viongozi kuonesha roho mbaya na ubinafsi kwani siku ya ‘bethidei’ ya Bongo Movie Unity hata hawakumkumbuka kwenye tuzo yoyote hata pongezi ya mdomo haikuwepo.

“Mimi ndiye niliyeanzisha Bongo Movies Unity, hakuna kundi ambalo limeshawahi kudumu kama hili hivyo haikuwa kazi rahisi kwangu lakini viongozi hawalioni hili wanaingiza roho mbaya na ubinafsi.
“Roho inaniuma sana mimi ndiye niliyewapa fomu wanachama wote na vitambulisho vyote vina saini yangu lakini leo naonekana sijafanya la maana, niko kwenye hatua za kujitoa kwa sababu sioni faida ya kukaa na watu wasionisapoti.

Ili kupata mzani wa habari hiyo, gazeti hili lilimmwagia ‘upupu’ wote Steve Nyerere ambapo alikuwa na haya ya kusema: “Tuhuma hizo siyo za kweli, tuzo nilitoa kwa wasanii wachanga ili kuwapa moyo wa kufanya vizuri zaidi.

“Kuhusu Jimmy Mafufu, nautambua sana mchango wake sema tu ana haraka na hao wanaosema nawapeleka kama gari bovu, wanakosea kwani najitoa sana, natumia muda mwingi kuwatumikia wao lakini hawaridhiki, wananiona kama jalala, wanasubiri nife ndiyo waanze kunisifia, inauma sana pia inakera.”
GPL

MTU ALIYE ANGUKIWA NA ROLI LA MCHANGA JANA AKIWA NDANI YA GARI MZIMA AMEUMIA KIDOLO TU

$
0
0


Huyu Jamaaa Ana Bahati Sana Aliangukiwa na Roli likiwa na mchanga kama picha inavyoonyesha hapo juuu ..lakini jamaa katoka mzima kabisa..kidolo tu ndio kimeumia..Nilivyoona hii picha ya Ajali kwa mara ya kwanza sikudhani kama driver atakuwa kasalimika....Mungu Mkubwa
Viewing all 104799 articles
Browse latest View live




Latest Images