Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104789 articles
Browse latest View live

Spika Ndugai Apokea Barua ya Kujiuzulu Ubunge ya Dk Abdallah Possi Aliyeteuliwa Kuwa Balozi..!!!

$
0
0

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bw. Job Ndugai amepokea barua ya kujiuzulu Ubunge iliyowasilishwa kwake na Dokta Abdallah Saleh Possi aliyeteuliwa kuwa Balozi katika kituo atakachopangiwa hapo baadae.

Taarifa ya Spika Ndugai ya kuwaarifu wabunge wote na wananchi kwa ujumla iliyotolewa jana imesema barua hiyo ya kujiuzulu Ubunge wa Dokta Possi imezingatia masharti ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, Ibara ya 67(1) (g) ikisomwa pamoja na ibara ya 149 (1) (d), hivyo Spika wa Bunge amemwandikia rasmi Rais kuwa hivi sasa wabunge wa kuteuliwa na Rais waliopo Bungeni ni saba (7) na hivyo nafasi zilizowazi ni tatu (3) baada ya Dk Possi kujiuzulu.

Taarifa hiyo imetolewa na kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano ofisi ya Bunge.

Mtoto wa Ray, Jaden afuata nyayo za Tiffah na Nillan wa Diamond...!!!

$
0
0

Tiffah ni mtoto maarufu zaidi kwenye mtandao wa Instagram Afrika akiwa na followers zaidi ya milioni moja. Mdogo wake, Nillan naye anafuata nyayo zake akiwa na followers zaidi ya 99k sasa. Akaunti zao husimamiwa na mama yao, Zari na hutumia Kimombo.

Na sasa mtoto mwingine wa mastaa wa Bongo, Jaden naye amejiunga kwenye kundi la watoto wa aina hiyo.

Jaden ni mtoto wa Ray Kigosi na Chuchu Hans aliyezaliwa wiki hii na tayari amefunguliwa akaunti kwenye mtandao huo. Yake inasimamiwa na mama yake na kama Tiffah na Nillan, amewafollow wazazi wake tu.

Katika kufurahia zawadi ya mtoto, Ray ameendelea kuweka wazi furaha yake kwa kuandika: Nikikuangalia Mwanangu Jaden Nakuwa Na Furaha Isiyo Kifani Na Kunipa Nguvu Ya Kupambana Na Maisha Ili Uishi Vizuri.. Mtoto ana Raha Yake Jamani asikwambie mtu Nyie Puyangeni Tu.

Steven Gerrard Aula Livepool..!!!

$
0
0


Nahodha wa zamani wa Liverpool na England Steven Gerrard atarejea katika klabu hiyo ya Ligi ya Premia kama kocha wa kikosi cha wachezaji chipukizi.

Gerrard, 36, ambaye alichezea Liverpool mara ya kwanza 1998, ataanza kazi Februari.

Kiungo huyo wa kati aliondoka Anfield mwishoni mwa msimu wa 2014-15 na kujiunga na klabu ya LA Galaxy inayocheza ligi kuu ya soka ya Marekani na Canada (MLS).

Alistaafu uchezaji soka Novemba baada ya kucheza kwa miaka 19.

“Ni kama kukamilisha mduara, kurejea pahala ambapo yote yalianzia,” Gerrard amesema.

“Nilipojua kwamba ningerejea, nilitaka kurejea katika nafasi muhimu. Hii inanipa fursa ya kujifunza na kujiboresha kama mkufunzi, na vile vile kutoa ujuzi wangu, mawazo na tajriba kwa wachezaji hawa chipukizi katika kipindi muhimu sana katika ukuaji wao,” amesema.

Gerrard alihusishwa na kazi ya meneja klabu ya MK Dons baada yake kuondoka LA Galaxy.

Amekuwa akisomea leseni yake ya ukufunzi ya Uefa, ambayo anahitajika kuwa nayo ndipo awe mkufunzi Ligi ya Premia.

Gerrard alichezea Liverpool mechi 710, na kushinda vikombe tisa.

Ndiye mchezaji wa nne kwa kuchezea England mechi nyingi zaidi za kimataifa, mechi 114.

Nyama Yaanza Kutengenezwa Maabara,Inafanana na Nyama ya Ng'ombe Hadi ladha..!!!

$
0
0

DUNIA inabadilika kwa haraka kutokana na maendeleo katika sekta mbalimbali. Teknalojia nayo inakua kwa kasi huku ikitoa mchango mkubwa katika maendeleo ya binadamu. Siku hizi Dunia inashuhudia uvumbuzi wa teknalojia za kisasa katika nyanja za kilimo, afya, nishati na nyingine nyingi.

Leo katika safu hii, nitajadili namna ambavyo wanasayansi walivyofanya jitihada za kutengeneza nyama katika maabara. Ndiyo, sasa si lazima kuhangaika kufuga na kupata usumbufu wa kutunza wanyama ili uweze kupata nyama.

Wote mtakubaliana na mimi kuwa, aina zote za vyakula vinavyotumiwa na binadamu inatokana na mimea na wanyama. Mamilioni ya wanyama huchinjwa kila siku duniani kwa ajili ya kupata kitoweo. 

Uchinjaji wa wanyama umekuwa mkubwa kuliko uzalishaji jambo ambalo limewafanya wanasayansi kufikiri namna ya kutengeneza kitoweo hiki muhimu pasipo kuhusisha kuchinja mnyama.

Rasilimali nyingi zimekuwa zikitumika kulisha wanyama, kuwachinja na kusafirisha, pia kumekuwapo upotevu mkubwa wa maji na nishati katika mzunguko mzima wa kupata kitoweo hiki. 

Ufugaji wa wanyama ambao hutupatia nyama unazalisha gesi ya methane ambayo inamchangio mkubwa katika mabadiliko ya tabianchi, wanasayansi wanataka kuondokana na haya yote kwa kutafuta mbinu mbadala ya kuzalisha nyama.

Kwa upande mwingine, wanyama hufungiwa ndani kwa maisha yao yote. Wanyama pia huchinjwa kikatili ili kuweza kupata nyama. Pamoja na haya yote, ni vigumu kufikiri maisha ya binadamu bila kula nyama. 

Utamaduni wa kula nyama ni mkongwe duniani na kwa vyovyote vile haitakuwa rahisi kuufuta. Kwa kutambua ukweli huu, wanasayansi wameaanza kutengeneza nyama maabara waliyoipa jina la nyama ya Vitro au Vitro meat kwa kimombo.

Nyama ya Vitro huzalishwa maabara. Kwa kawaida nyama hutengenezwa kutokana na kemikali ndogo inayojulikana kitaalamu atoms. Kama unaweza kutengeneza atoms kwa njia tofauti na ya kawaida, basi pia unaweza kutengeneza nyama. 

Ukipewa vipande viwili vya nyama kimoja kilichotokana na mnyama aliyechinjwa na nyingine aina ya Vitro ambayo hutengenezwa maabara ni vigumu kuelezea tofauti yake kutokana na kufanana kwa muonekano na hata ladha.

Maabara sasa inafanya kazi ya kutengeneza nyama ambayo ni sawa na nyama uliyozoea kununua buchani. Profesa wa Molecular Biology, katika Chuo Kikuu cha Stanford, alinukuliwa na gazeti la The Gurdian la Uingereza akisema inawezekana kuondokana na usumbufu wa kufuga na kuchinja wanyama kwa kuwa nyama sasa inaweza kutengenezwa maabara.

“Sina nia ya kutengeneza vyakula vipya kwa watu wasiokula nyama. Natengeneza chakula kwa ajili ya wanaokula nyama na ambao wana nia ya kula nyama. Hii itawasaidia kupata nyama bila shurba.

“Nyama ya Vitro haitokani na kiumbe hai hivyo haiwezi kufa na hii naletea tofauti kubwa katika upatikanaji wake. Kiuchumi, gharama za uzalishaji wake ni kubwa na hivyo kufanya uzalishaji mkubwa kuwa changamoto. 

Pia kutokana na ushawishi wa wafugaji wakubwa Marekani na sehemu nyingine duniani, inawezekana kuwa na vikwazo vya kisheria,” anasema Profesa huyo.

Gharama kubwa za uzalishaji wa nyama ya Vitro inaweza kuwa ndiyo kikwazo kikubwa katika uzalishaji wake. Hata hivyo, ugunduzi zaidi kwenye teknalojia ya uzalishaji wake itaweza kupunguza gharama. 

Kampuni kubwa ikiwamo New Harvest na Modern Meadow zinafanya kazi kuhakikisha kuwa nyama hii inazalishwa kwa wingi na kuwafikia walaji wengi.

Usichokijua Kwenye Remix ijayo ya Aje ya Alikiba

$
0
0

Aje ni wimbo wa Alikiba uliompa mafanikio makubwa mwaka jana ikiwemo tuzo kadhaa za video bora ya mwaka ikiwemo ile ya Soundcity MVP Awards.

Baada ya kuwepo version yenye verse toka kwa rapper Jude ‘M.I’ Abaga aka Mr Chairman wa Nigeria iliyovuja hata kabla ya official video, mashabiki walikuwa wamekaa tamaa kuwa hakutokuwepo na official remix yake.

Habari njema ni kuwa, Alikiba anaileta remix official ya Aje. Na tena itakuwa ni video.

“Ndio, remix inayokuja ndio ambayo yuko M.I na ina utofauti than the one that leaked,” meneja wa Alikiba, Seven ameyasema hayo. Seven amewataka mashabiki wawe tayari muda wote sababu remix hiyo itaachiwa kwa kushtukiza.

“He will just release it when it’s ready,” ameongeza. “Hatutoi official release date. It will drop unexpectedly.”

Je, Trump Ataweza Kuwatuliza Wamarekani? Hali Yaendelea Kuwa Mbaya Mitaani

$
0
0

Ikiwa ni muda mchache baada ya Rais Trump kuapishwa kuwa Rais wa 45 wa Marekani, bado wanaompiga wanaendelea na maandamano dhidi yake.

Je, Trump ataweza kuwatuliza na kuwaunganisha wamarekani kabla hali haijawa mbaya zaidi?

Breaking News ..!! Rais Magufuli Amteua Anne Kilango Malecela Kuwa Mbunge..!!!!

$
0
0

Rais John Magufuli amemteua Anne Kilango Malecela kuwa mbunge, huku akiwa mkuu wa mkoa pekee kwenye utawala wa awamu ya tano aliyedumu na wadhifa huo kwa muda mfupi wa siku 29.

Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Rais Ikulu, imeeleza kuwa Kilango ataapishwa kwa mujibu wa taratibu za Bunge.

Uteuzi huu unakuja siku chache kabla ya Rais Magufuli kumteua aliyekuwa  mbunge wa kuteuliwa ambaye pia alikuwa Naibu Waziri wa Kazi, Dk Abdallah Possi kuwa balozi. Tayari, Dk Possi amekabishi barua ya kujiuzulu ubunge.

Hata hivyo, Kilango anarudi katika ulingo wa siasa huku akiwa amepitia katika misukusuko kadhaa ikiwamo kupoteza kiti cha ubunge Same Mashariki, mkoani Kilimanjaro.

Kilango aliteuliwa Machi 13, 2016 na uteuzi wake kutenguliwa Aprili 11 mwaka huohuo, kutokana na kutoa taarifa kwamba Mkoa wa Shinyanga aliokuwa akiuongoza haukuwa na watumishi hewa.

Safari yake ya kisiasa

Mbunge huyo mteule alizaliwa Januari 9, 1956 Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro. Mwaka 1979-1983 alikuwa mwalimu Sekondari ya Kisutu jijini Dar es Salaam; 1983-1991 alikuwa Mhasibu Msaidizi Shirika la Ndege Tanzania (ATC); na 1991-1993 alikuwa Mdhibiti wa Fedha Shirika la Ndege la Gulf.

Pia, mwaka 1993-1994 alikuwa Mhasibu Shirika la Ndege la KLM; 1994-2000 alikuwa akijishughulisha na ujasiriamali kwenye kampuni yake ijulikanayo kama Ninna Bridal Centre; 2000-2005 aliteuliwa ubunge na Rais Benjamin Mkapa; na 2005-2015 alikuwa mbunge wa kuchaguliwa Same Mashariki.

Tanzania Yang'ara Afrika Kwa kuwa na Wanawake Wengi Kwenye Baraza la Mawaziri..!!!

$
0
0

TANZANIA imetajwa kuwa miongoni mwa nchi 20 bora duniani kwa kuwa na sehemu kubwa ya mawaziri wanawake kwenye Baraza la Mawaziri, huku ikishika nafasi ya tano Afrika.

Mtandao wa How Africa, The Rise of Africa, umeeleza hilo jana ukinukuu utafiti mpya ulioandaliwa na taasisi ya UN Women na Inter Parliamentary Union, ambazo zinaongoza duniani kwa kupigania ajenda ya kuongeza uwakilishi wa wanawake kwenye vyombo vya uamuzi.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Cape Verde ndiyo nchi inayoongoza kwa kuwa na sehemu kubwa ya wanawake kwenye Baraza la Mawaziri, inayoundwa na wanawake ambalo kati ya mawaziri wote 17, tisa ni wanawake.

Mbali na kuwa ya kwanza Afrika, Cape Verde imetajwa kuwa ya pili duniani kwa kigezo hicho, ikitanguliwa na Finland, ambayo ndiyo ya kwanza duniani kwani kati ya mawaziri wake 16, mawaziri 10 ni wanawake.

Nchi ya pili Afrika kwa kuwa na sehemu kubwa ya wanawake kwenye Baraza la Mawaziri ni Afrika Kusini, ambayo kati ya mawaziri 36, mawaziri 15 ni wanawake.

Rwanda inashika nafasi ya tatu Afrika, kwani kati ya mawaziri wake 31, mawaziri 11 ni wanawake na inafuatiwa na Burundi na Tanzania katika nafasi ya tano.

Tanzania

Baraza la Mawaziri Tanzania likijumuisha na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, lina mawaziri 36 na kati yao, tisa ni wanawake.

Mawaziri hao ni Jenista Mhagama (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu); Ummy Mwalimu (Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto); Anjela Kairuki (Utumishi na Utawala Bora); Profesa Joyce Ndalichako (Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi).

Wengine ni Dk Ashantu Kijaji (Naibu Fedha na Mipango); Dk Susan Kolimba (Naibu Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afika Mashariki); Angelina Mabula (Naibu Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi); Stella Manyanya (Naibu Elimu, Sayansi Teknolojia na Ufundi) na Anastasia Wambura (Naibu Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo).

Nchi zingine

Afrika sasa ina nchi saba ambazo angalau asilimia 30 ya mawaziri wao ni wanawake na katika nchi 30 duniani zinazofikia wingi huo wa mawaziri wanawake na kuzidi, robo ya nchi hizo zinatoka Afrika na kufanya Bara hilo kuwa la pili kwa kufikia kigezo hicho baada ya Ulaya.

Nchi yenye uchumi mkubwa zaidi Afrika; Nigeria kati ya mawaziri 29, saba ni wanawake uwiano sawa na Jamhuri ya Afrika ya Kati, ambayo kati ya mawaziri 22,  watano ni wanawake.

Djibouti ndiyo ya mwisho, ambayo kati ya mawaziri wake 19, waziri mmoja tu ndiye mwanamke, wakati Sierra Leone ina mawaziri wanawake wawili tu kati ya mawaziri 29.  

Bungeni

Rwanda inaongoza duniani katika uwakilishi wa wanawake bungeni ambapo kati ya viti 80 vya ubunge, viti 51 ni vya wanawake sawa na asilimia 63 ya wabunge wote.

Ushelisheli, Senegal na Afrika Kusini zinafuata na kuwa miongoni mwa nchi 10 bora duniani kwa kuwa na uwakilishi mkubwa wa wanawake bungeni.

Msumbiji, Angola, Tanzania, Algeria, Zimbabwe, Tunisia, Kameruni na Burundi, ni miongoni mwa nchi zingine za Afrika, zenye zaidi ya asilimia 30 ya wabunge wanawake kwenye mabunge yao.

Nchi zenye uwakilishi mbovu wa wanawake bungeni ni  Swaziland, Nigeria, Congo zote mbili, Ivory Coast, Gambia, Mali na Botswana, ambazo uwakilishi wa wanawake kwenye mabunge yao ni chini ya asilimia 10.

Wastani wa uwakilishi wa wanawake kwenye mabunge ya nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara, umetajwa kuwa asilimia 22.4 katika mataifa yenye mabunge yenye sehemu moja na asilimia 20 kwa mabunge yenye sehemu mbili; Bunge la Wawakilishi na Bunge la Seneti.

Hii Ni zaidi ya Hatari!! Hivi Ndivyo Maelfu ya Wamarekani Walivyoandamna Kumpinga Rais Trump Mitaani..!!!

$
0
0

DONALD Trump ameapishwa kuwa Rais wa 45 wa Marekani, na kurudia ahadi yake ya kuifanya nchi yake kuwa taifa lenye nguvu zaidi kuliko ilivyokuwa awali.

Hata hivyo, Trump ameapishwa wakati ambao nchi hiyo imegawanyika, ambapo jana maelfu ya wananchi waliandamana kupinga kuapishwa kwake. Kwa mujibu wa uchunguzi wa maoni, ni asilimia 40 ya Wamarekani ndio wanamuunga mkono.

Trump aliapishwa huku idadi ya wageni walioalikwa kuhudhuria sherehe hizo ikiwa ni nusu ya wale waliohudhuria wakati Rais aliyemaliza muda wake jana, Barack Obama alipoapishwa kwa mara ya kwanza mwaka 2009.

Takribani watu milioni 1.8 walihudhuria sherehe za kuapishwa kwa Obama wakiwamo watu maarufu na wanamuziki, lakini mambo yashindwa kwenda sawa kwa Trump kutokana na sherehe zake kuhudhuriwa na wageni takribani 800,000.

Jana Polisi walipambana na kundi kubwa la wananchi waliokuwa wakiandamana na kuziba mitaa na barabara za majimbo mbalimbali nchini humo wakipinga kuapishwa kwa Trump kuwa rais wa nchi hiyo.

Trump ambaye alimshinda mpinzani wake wa Chama cha Democratic, Hillary Clinton katika uchaguzi mkuu uliofanyika Novemba 8 mwaka jana, amekuwa akipingwa na kundi kubwa la raia wa nchi hiyo ambao wanasema hakuwa chaguo lao bali alishinda kutokana na mfumo mbovu wa upigaji kura unaotumiwa na Taifa hilo.

“Tutaandamana tu wala hatutaogopa kama Polisi watatupiga au kutukamata, lengo ni kumwonesha Trump kwamba hakubaliki miongoni mwa raia wengi wa Marekani, haijalishi ameshinda na anaapishwa, katu hatopata nafasi nyoyoni mwetu.

“Hajawahi kuwa na sera zinazoonesha kama ni kiongozi wa kutazamwa, kauli zake za kibaguzi kuanzia rangi na wanawake vinamfanya kuwa Rais wa ajabu kuwahi kutokea Marekani,” alisema mmoja wa waandamanaji katika eneo la San Diego, California.

Democrats

Sherehe hiyo iligubikwa na mabadiliko mengi mahsusi tofauti na ilivyozoeleka kwa watangulizi wake.
Jambo kubwa mbali na maandamano hayo yaliyoendeshwa na wafuasi wa chama cha Democrats, ni uchaguzi wa Trump wa Biblia ambayo alitumia kuapia, kwani alichagua aliyotumia utotoni, lakini pia kiutaratibu alitumia Biblia ya Lincoln ambayo ilitumiwa katika viapo vitatu vilivyotangulia.

Biblia hiyo ilitumiwa na Abraham Lincoln mwaka 1861 na Barack Obama mwaka 2009 na mwaka 2013.
Tofauti na viapo vya nyuma, idadi ya waburudishaji haikuwekwa wazi kutokana na wengi waliokuwa wamejulishwa kushiriki walijijitoa kutokana na upinzani wa kisiasa uliogubika sherehe hizo.

Mmoja wa waburudishaji waliothibitishwa tangu awali ni Jackie Evanco (16) ambaye ni maarufu kwa albamu yake ya ‘America’s Got Talent’ na ndiye aliyeimba Wimbo wa Taifa.

Jambo lingine lisilo la kawaida ni idadi kubwa ya wajumbe wa Baraza la Congress wa Democrats ambao walitangaza kususa hafla hiyo, huku idadi ikionesha kuwa theluthi tatu ya wajumbe wote wa Baraza hilo kutoka Democrats hawakushiriki.

Hata hivyo ratiba ya matukio ya jana haikutofautiana sana na ilivyozoeleka katika viapo vilivyotangulia vya marais, hata hivyo, Trump ambaye alilala na familia yake kwenye jengo la Blair House mkabala na Ikulu ya White House, alianzia kanisani asubuhi.

Baadaye akifuatana na mkewe, Melania, walikwenda White House kufungua kinywa pamoja na familia ya Rais Barack Obama kabla ya kwenda Capitol.

Baada ya kiapo, Obama aliondoka na kumwacha Trump akipata chakula cha mchana kabla ya matukio mengine kama vile gwaride na shamrashamra zingine ili kuhitimisha siku hiyo.

Wapinzani

Wapinzani wa Trump usiku wa kuamkia jana walipambana na polisi na kunyunyiziwa pilipili jijini hapa.
Kundi kubwa la waandamanaji wanaompinga Rais Trump lilikusanyika mapema nje ya Klabu ya Taifa ya Waandishi wa Habari, ambako kulikuwa na sherehe zijulikanazo kama ‘DeploraBall’ – tukio ambalo liliandaliwa na wafuasi wa Trump juzi usiku.

Mamia ya waandamanaji hao waliingia mitaani nje ya klabu hiyo, wengi wakiimba huku wakibeba mabango ya kumkataa Trump.

Mmoja wa wafuasi wa Trump ambaye alikuwa eneo hilo lakini hakuhudhuria hafla hiyo, alidai kuwa waandamanaji hao walifanya vurugu – wakimshutumu mmoja wao kwa kumshambulia kwa mlingoti wa bendera.

“Nilikuwa nimevalia kofia yangu yenye maandishi ya ‘Ifanye Marekani Taifa Kubwa tena’, na mwanamume mweupe akanifuata kwa nyuma na kunisukasuka kwa mlingoti wa bendera – nikapoteza fahamu kama dakika moja hivi,” Jones Allsup (21) aliiambia Fox News.

Wafuasi

Kambi ya Trump kwenye ghasia hizo nayo iliwakilishwa na waendesha mapikipiki waliotoka sehemu mbalimbali za nchi kuja hapa siku kadhaa kabla ya jana ambao walijiandaa kukabiliana na waandamanaji hao.

Kundi hilo linalojiita Bikers For Trump liliomba kibali cha watu 5,000 kukaa kwenye bustani ya John Marshall, huku wakipanga kufanya mkutano usio rasmi kati ya tukio la kula kiapo na kuanza kwa gwaride.

Muasisi wa kundi hilo, Chris Cox (48), aliiambia Fox & Friends: “Kwenye tukio hili ambalo tunahitajika, tutajenga ukuta wa nyama. Tutakuwa bega kwa bega na ndugu zetu na tutakuwa kidole kwa kidole na yeyote atakayethubutu kuvuka vizuizi vya Polisi,” alionya Cox.

Kabla ya kuapishwa Trump na Makamu wake, Mike Pence na familia zao walihudhuria ibada kwenye Kanisa la Mt John baadaye wakaenda Ikulu ya White House kufungua kinywa na familia ya Rais Barack 
Obama kabla ya kuelekea jengo la Capitol, kuapishwa na Jaji Mkuu, John Roberts Jr na kuhudhuriwa na wabunge wa Baraza la Congress.

Duh,Hii Noma Sana!! Mshitakiwa Ajipaka Kinyesi na Kutoroka Mahakamani Huku Polisi Wakimuangalia..!!!

$
0
0

MSHITAKIWA Emmanuel Mkenya aliyefikishwa kwenye Mahakama ya Mwanzo Kariakoo jana kusomewa mashitaka ya uzembe na uzururaji, ametoroka mikononi mwa polisi baada ya kujipaka kinyesi mwilini.

Mshitakiwa huyo alifikishwa asubuhi mahakamni hapo kujibu mashitaka yanayomkabili na kuwekwa mahabusu kusubiri kuitwa.

Muda wa kusomewa kesi ulipofika, askari alikwenda kumwita yeye na wenzake ili wapande kizimbani, lakini mshitakiwa huyo alitoka akiwa amejipaka kinyesi chake, alichojisaidia kwenye choo cha ndani ya mahabusu.

Huku akionekana kujiamini, mshitakiwa huyo badala ya kupanda kizimbani, aliondoka taratibu kupitia lango la kutoka nje ya Mahakama, huku polisi wakishindwa kumkamata kutokana na hali aliyokuwa nayo.

Baada ya kutoka nje, mshitakiwa mwenzake kwenye kesi hiyo ya uzembe na uzururaji, alipandishwa kizimbani mbele ya Hakimu Agnes Barasobian.

Hata hivyo, kabla ya Karani Hatanawe Kitogo kusoma mashitaka dhidi ya mshitakiwa wa pili, Hakimu Agnes aliuliza alikokuwa mshitakiwa namba moja.

Polisi aliyekuwa mahakamani hapo alimjibu Hakimu kuwa mshitakiwa huyo alitoroka baada ya kujipaka kinyesi mwili mzima.

Hakimu Agnes akionesha kukasirika, alimtaka askari huyo ahahakishe mshitakiwa anatafutwa na kukamatwa, kwani haiwezekani aondoke mahakamani huku akiwa na mashitaka yanayomkabili.

Alisema hakubaliani na sababu za askari huyo, kwa kuwa anatambua kuwa kwenye mafunzo ya kijeshi, hupewa mbinu za kukabiliana na washitakiwa.

Washitakiwa hao walikamatwa na Koplo Luseseko Januari 19 Msimbazi, Dar es Salaam wakituhumiwa kwa uzururaji. Kesi hiyo iliahirishwa jana hadi Januari 30 itakapotajwa.

Kudadeki!!! Trump Aaanza Kazi kwa Spidi 120,Afumuafumua Mifumo yote ya Obama Ikulu ya White House..!!!

$
0
0

Rais mpya wa Marekani, Donald Trump aanza kazi hiyo kwa kutia saini amri inayolenga kufanyia mabadiliko ya mfumo wa afya ulioasiliwa na mtangaulizi wake, Barack Obama.

Hatua hiyo inataka wakala mbalimbali kupunguza mzigo wa kiuchumi wa sheria unaotokana na mfumo wa afya unaojulikana kama Obamacare.

Katika hotuba yake ya uzinduzi Ijumaa mara baada ya kuapishwa kuwa Rais aliahidi kutoa kipaumbele katika utendaji wake ‘’kwa kuitanguliza Amerika kwanza’’ na kumaliza kile alichokiita ‘’ Mauaji ya Amerika’’ ya kutelekeza viwanda na uwepo uhalifu mkubwa.

Baadaye watu wapatao 200,000 walitarajiwa kujiunga katika maandamano ya wanawake jijini Washington.
Waandaaji wa maandamano hayo wanasema wanataka kutoa msisitizo juu ya uwepo wa ubaguzi wa rangi na kukosekana kwa usawa wa kijinsia na mambo mengine ambayo yanayoonekana kuwa hatarini kukiukwa na utawala wa Trump.

Maandamano kama hayo tayari yanafanyika Australia na New Zealand na maeneo mengine mengi yanayoandaliwa katika nchi mbalimbali duniani.

Mwandishi wa Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) Washington, Barbara Plett-Usher anasema Rais Trump ameapa kufanya kinachowezekana mara moja kwa kutumia madaraka aliyonayo kusukuma uhai viwanda kabla ya kurejea kuandaa muswada wa kupeleka bungeni.

Timu yake kwa haraka ilibadilisha mfumo wa wavuti wa Ikulu ya Marekani, White House,ukihusisha nia yake kuzuia mkakati wa Obama kuhusu mabadiliko ya tabia nchi. Muda mfupi baada ya kushika madaraka kama rais wa 45 wa Marekani, Trump asiwasilisha mapendekezo ya baraza lake la mawaziri kwenye Seneti.

Inasikitisha Mnoo!! Mama Atupa Kichanga Chake Chooni Kisa Eti Anaokoa Ndoa Yake Isivunjike..!!!

$
0
0

MATUKIO mawili ya mama kutupa vichanga chooni baada ya kujifungua, yametikisa katika wilaya za Sikonge na Shinyanga. Katika tukio la wilayani Sikonge, mama akichukua uamuzi huo ili kulinda ndoa isivunjike, baada ya kupata ujauzito nje ya ndoa.

Katika tukio jingine, mtoto wa siku moja mwenye jinsia ya kiume, amekutwa ametupwa kwenye tundu la choo la Kanisa la African Inland Tanzania (AICT) lililopo Kitangiri Manispaa ya Shinyanga na kutofahamika mara moja mtu aliyefanya kitendo hicho.

Kutoka Sikonge inaelezwa kuwa Polisi wilayani humo mkoani Tabora, inamshikilia mkazi wa kitongoji cha Ukanga katika kijiji cha Sikonge mjini, Paulina Mussa (21) kwa tuhuma ya kumtupa mtoto aliyejifungua kwenye shimo la choo.

Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Sikonge, Mselemi Maulidi akizungumza na waandishi wa habari, alisema kwamba tukio hilo ni la Januari 19, saa 10 usiku katika Kitongoji cha Ukanga wilayani Sikonge.

Maulidi alisema mtuhumiwa, Paulina Mussa alishikwa na uchungu majira ya usiku wa saa 10, ambapo alitoka nje na kumuacha mume wake akiwa amelala ndani, lakini baada ya muda alirudi ndani.

Mwenyekiti huyo alibainisha kuwa akiwa ndani, alimueleza mume wake, Saulo Kaombwe kuwa mimba aliyokuwa amebeba, imeharibika huku akimuomba ampeleke hospitali akatibiwe, ambapo mume wake alikubali kumpeleka.

Alisema akiwa Hospitali ya Wilaya, mama mmoja ambaye hakutaka jina lake liandikwe kwenye gazeti, alikwenda kujisaidia katika choo hicho cha jirani yake, ambapo alisikia kichanga kikiwa kwenye shimo la choo kikilia .

Kutokana na hali hiyo, alitoka haraka chooni na kuomba msaada kwa majirani, ambao walifika katika choo hicho na kuamua kukivunja na kukikuta kichanga hicho, kikiwa kimewekwa kwenye mfuko wa saruji uliokuwa tupu.

Baada ya kukitoa kichanga hicho, walikipeleka katika Hospitali ya Wilaya, alipokwenda kutibiwa mama wa kichanga hicho, na walipomhoji alikiri kujifungua na kukitupa kichanga kwenye shimo la choo, jambo ambalo baadhi ya akinamama liliwakera na kuanza kumtembezea kipigo mama huyo, huku baadhi ya wananchi wakituliza ghasia hizo.

Alipoulizwa kwa nini alifanya hivyo, alidai alikuwa anaokoa ndoa yake, kwa kuwa mimba aliyobeba, ilikuwa si ya mume aliyekuwa akiishi naye.

Mmoja wa majirani wa mama huyo, Lameck Benjamin alisema jambo hilo ni la aibu na kuiomba serikali ichukue hatua kali dhidi ya akinamama, wanaofanya tabia ya kutupa watoto huku akiwataka kuacha kubeba mimba, endapo hawataki kuzaa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Kamishna Msaidizi Hamisi Selemani Issa, alithibitisha kutupwa kwa kichanga hicho na kusema kuwa tayari mtoto huyo, anaendela kupatiwa huduma na mama yake huku wakisubiri kuchukua hatua za kisheria.

Kamanda Issa alitoa wito kwa akina mama, kuacha tabia hiyo ya kuwatupa watoto pasipo kuwa na sababu ya msingi kwani nao wana haki ya kuishi.

Mwingine atupwa kwenye choo cha kanisa Katika tukio jingine, mtoto wa siku moja mwenye jinsia ya kiume, amekutwa ametupwa kwenye tundu la choo la Kanisa la African Inland Tanzania (AICT) lililopo Kitangiri Manispaa ya Shinyanga na kutofahamika mara moja mtu aliyefanya kitendo hicho.

Mwenyekiti wa Mtaa wa Kitangiri, Habiba Jumanne aliwaeleza waandishi wa habari jana kuwa majira ya saa 11 jioni ya Januari 20, mwaka huu, alipigiwa simu na baadhi ya waumini wa kanisa hilo, kuwa kuna mtoto mchanga wanasikia sauti yake ndani ya tundu la choo.

Jumanne alisema kuwa mtoto huyo mwenye siku moja, alikutwa kweli kwenye tundu la choo akiwa hai, huku waumini wa kanisa hilo na askari walibomoa choo na kumtoa mtoto huyo, kisha kumpeleka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa.

“Tulifanya jitihada za kuvunja choo na kumtoa mtoto akiwa hai, tukamkimbiza Hospitali ya Rufaa ya Mkoa.
Chakusikitisha leo asubuhi tumekwenda kuona hali ya mtoto, daktari ametueleza mtoto amefariki dunia, hatuna jinsi aliyefanya kitendo hicho hafahamiki.

Tunachotaka ni kuomba kibali cha polisi na kwenda kumzika kwa kushirikiana na Kanisa la AICT,” alisema Jumanne.

Mzee wa Kanisa la AICT, David Madata alisema kuwa wakati alipokuwa akifundisha watoto somo la Injili, alimuona mwanamke mmoja akiwa amelala karibu na choo hicho, lakini hakumdhania kama alikuwa na nia ovu.

Alisema baada ya muda, mwanamke huyo aliondoka na kuelekea mahali kusikojulikana na baadaye watu waliokuwa wanaenda chooni, walianza kusikia sauti ya mtoto mchanga akilia chooni, hivyo waliamua kutoa taarifa kituo cha polisi na serikali ya mtaa.

Kaimu Kamanda Polisi Mkoa wa Shinyanga, Elias Mwita alithibitisha kutokea kwa tukio hilo, ambapo alieleza kuwa mtoto huyo alitupwa kwenye tundu la choo la Kanisa la AICT na mtu ambaye hajafahamika.

Alisema bado wanaendelea na uchunguzi kumbaini aliyehusika na kitendo hicho. Habari hii imeandikwa na Lucas Raphael, Sikonge na Kareny Masasy, Shinyanga.

Pitia Vichwa Vya Magazeti ya Leo Jumapili ya Tarehe 22/1/2017 ...!!!

Imefichuka,CUF ya Maalim Seif Waanza Kumchafua Msajili wa Vyama vya Siasa Baada ya Kuidhisha Pesa Kwa CUF ya Prof Lipumba..!!!

$
0
0

SIKU chache baada ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini Jaji Francis Mutungi kuidhinisha ruzuku ya CUF kwa Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba mikakati ya kumchafua imeanza chini kwa chini.

Mikakati hiyio inadaiwa kuratibiwa na Kamati ya Uongozi ya Chama hicho ambayo Msajili haitambui.

Taarifa  zinadai kwamba mbinu hizo zimeanza kutekelezwa na viongozi wa Kamati hiyo kwa kusambaza habari zinazomdhalilisha Msajili wa katika vyombo mbalimbali vya habari na mitandao ya kijamii.

Moja ya mikakati hiyo ni iliyosambazwa na Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano, Mbarala Maharagande iliyojaa kejeli, matusi, tuhuma na dhihaka kwa Msajili na kuacha kujibu hoja za msingi ambazo awali zilitolewa na Ofisi ya Msajili.

Taarifa za ndani ya mkakati huo zinadai kuwa pamoja na mitandao ya kijamii, pia magazeti kadhaa likiwamo maarufu la kila wiki linalomilikiwa na wabunge wawili wa chama cha upinzani nchini yatatumika kufanikisha azma hiyo.

Maharagande alizungumza na waandishi wa habari huku akidai kuwa Ofisi ya Msajili inasababisha mpasuko ndani ya chama hicho na ndiyo maana imetoa ruzuku kwa Lipumba.

Aidha, Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya CUF, Julius Mtatiro aliyesema Mutungi amevunja maadili ya kazi yake, hivyo hawawezi kumvumilia.

Alisema kwa sasa wanasheria wao wako kwenye mchakato wa kufungua kesi ili kushitaki wahusika wa wizi huo.

Akizungumzia taarifa hizo katika moja ya magazeti, Jaji Mutungi alisema haogopi kuchafuliwa vyovyote kwa kuzingatia ukweli kwamba yeye ni mtumishi wa umma na anafanya kazi zake kwa mujibu wa sheria za nchi na hawezi kuyumbishwa na matusi wala kejeli dhidi yake na ofisi yake.

"Na mimi nimezipata hizo taarifa, kwamba kuna baadhi ya watu wamepanga kupambana nami kwa kunichafua, japo naendelea kuzifanyia kazi, lakini kwa kifupi niwaambie waache wanichafue na wala siogopi lolote," alisema.

"Mimi ni mtumishi wa umma nafanya kazi kwa mujibu wa sharia, hivyo siwezi kuyumbishwa na mambo ya kitoto ya kuchafuana na kurushiana tuhuma zisizo na kichwa wala miguu. Sidhani kama kumshambulia Mutungi kunaweza kuleta tija ya wao kufikia malengo yao," alisema.

Aidha, alisema mjadala wa ruzuku ya CUF aliyoitoa kwa chama hicho ameshaufunga na anashangazwa na maneno ya uongo yanayozidi kusambazwa na watu wanaojiita viongozi wa CUF.

Jaji Mutungi alisema yeye ni muumini wa haki na sheria, na ndiyo maana mamlaka za uteuzi zilimwamini na kumpa ujaji.

"Natambua uadilifu wangu na sitaki niuelezee, ila nahisi tukiendelea kulizungumzia hili tutakuwa tunalikuza bila sababu za msingi.  Nasisitiza tena kuwa ofisi yangu inamtambua Profesa Lipumba kama Mwenyekiti wa CUF na Maalim Seif Sharif Hamad kama Katibu Mkuu,” alisema.

Kutokana na hali hiyo, alisema kinachoendelea kufanywa na kundi la watu wanaojiita viongozi wa CUF ni kuzungumza mambo mengi ya uongo na kumhusisha bila ukweli huku wakishindwa kusoma vyema Katiba yao wenyewe.

"Nasisitiza tena si Mutungi au Ofisi ya Msajili iliyoandika Katiba ya CUF, ni wao wenyewe. Ofisi ilichofanya ni kuitafsiri na kutoa mwongozo. Sasa tatizo liko wapi?” Alihoji.

Askofu Mokiwa Azidi Kupingwa,Waumini Wamzui Asiingie Ofisini Kakwe..!!!

$
0
0

. Askofu wa Dayosisi ya Dar es Salaam wa Kanisa la Anglikana, Dk valentino Mokiwa jana alishindwa kuendesha vikao viwili baada ya kundi la waumini kufika Usharika wa Ilala kwa lengo la kuzuia.

Askofu Mokiwa, ambaye anapinga uamuzi wa Askofu Mkuu wa Anglikana, Dk Jacob Chimeledya kumvua madaraka kutokana na tuhuma za matumizi mabaya ya fedha, alikuwa aendeshe vikao vya kamati ya fedha na halmashauri kuu, lakini alilazimika kuviahirisha baada ya kundi hilo kufika eneo hilo.

Wakati waumini hao wakizuia vikao hivyo kufanyika, mashemasi, mapadri, wainjilisti na waumini wa dayosisi hiyo wametoa tamko la kumuunga mkono Dk Mokiwa wakipinga uamuzi wa mkuu wa kanisa hilo kumvua madaraka.

Askofu Mokiwa anapinga uamuzi wa kumvua madaraka akisema hauwezi kufanywa na mkuu wa kanisa, bali na halmashauri kuu ya jimbo ambayo anasema haikushirikishwa zaidi ya kutaarifiwa uamuzi huo.

Tukio la jana la kumzuia Dk Mokiwa kufanya mkutano lilitokea saa mbili asubuhi katika Kanisa la Mtakatifu Nicolau wilayani Ilala, ambako kuna ofisi ya Askofu wa Dayosisi ya Dar es Salaam.

Dk Shein na Maali Seif Watambiana,Shein Adai Hakuna wa Kumng'oa Madarakani hata Yaje Majeshi ya UN ..!!!

$
0
0
.
 Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar), Dk Ali Mohammed Shein na Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad jana walihitimisha kampeni za vyama vyao za ubunge wa Dimani ambao uchaguzi wake unafanyika leo kila mmoja akitamba kushinda.

Dk Shein ambaye ni Rais wa Zanzibar, akihutubia mkutano wa hadhara katika viwanja vya Fuoni alirejea kauli yake kwamba hakuna umoja wa mataifa au nchi yoyote inayoweza kumuondosha madarakani.

Dk Shein alisema hayo akiendelea kujibu kauli ya Maalim Seif kwamba siku si nyingi kutatokea mabadiliko makubwa na kwamba wanachama wake wasifadhaike.

Dk Shein alisema CUF walikataa wenyewe kushiriki katika Uchaguzi Mkuu wa marudio uliofanyika Machi 20, 2016, hivyo wanabaki wakitangatanga, “...Wasahau kabisa kuipata nafasi ya urais wa Zanzibar. Hawana uwezo hata wa kuongoza udiwani sembuse urais.”

Mahaba Niue..!! Tazama Hapa Jinsi Trump na Mkewe Walivyoonyeshana Mahaba Ikulu Wakati Wakicheza Muziki..!!

$
0
0

Donald Trump na mkewe, Melania juzi walilionyesha jiji la Washington mvuto wa familia yao  wakati walipopanda kudansi kwenye jukwaa lililopambwa kwa taa za rangi nyekundu, nyeupe na bluu ambazo ni za bendera ya Marekani.

Wimbo wao wa kwanza kwa wawili hao kucheza ulikuwa “My Way (Kivyangu)” wa mwaka 1969 uliorekodiwa na gwiji wa muziki, Frank Sinatra. Lakini katika sherehe ya juzi, kibao hicho kiliimbwa na nyota wa muziki wa jazz, Erin Boheme.

Melania Trump alivutia waalikwa kwenye sherehe hiyo alipoibuka na gauni lake jeupe la kung’aa, lililoacha mabega wazi, lakini lenye mikono ya mchinjo, na refu hadi kufikia kifundo cha mguu, lakini likiwa na mpasuo unaofikia juu kidogo ya goti.

Hafla hiyo ilikuwa ya kusherehekea kukabidhiana madaraka kwa amani baada ya rais aliyemaliza muda wake, Barack Obama kumpisha Trump. Hafla hiyo ya burudani hufanyika kuzindua kipindi cha rais mpya ambaye huitumia kuonyesha mapenzi yake katika mavazi, muziki na dansi

Chadema Walianzisha ..!!!!

$
0
0

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko, Juma Maganga amepewa siku saba kueleza sababu ya kupitisha bajeti ya mwaka 2017/18 ikidaiwa ni  kinyume na utaratibu.

Wakizungumza na waandishi wa habari, madiwani kutoka Chadema walidai kuwa mwenyekiti huyo alitumia mabavu kupitisha bajeti ambayo haijakamilika.

Katibu wa madiwani hao, Medas Amosi alisema: “Mwenyekiti alienda kinyume na kifungu cha 183 cha Sheria namba 7, na kifungu 97 cha  Sheria namba 8 ya mwaka 1982  zinazotoa madaraka na mamlaka kwa Serikali za Mitaa.” 

Amosi alisema utaratibu unaotumika kupitisha bajeti ni theluthi ya wajumbe ambao huwa  12, lakini mwenyekiti huyo aliipitisha baada ya wajumbe 10 ambao ni wa CCM kuikubali, huku wanane wa Chadema wakiikataa.

Rais wa Uturuki Aleta Neema Tanzania...!!!

$
0
0

Wakati Rais wa Uturuki, Recep Erdogan akitua nchini leo, uhusiano kati ya nchi yake na Tanzania umesaidia kukua kwa biashara kutoka Dola66 milioni za Marekani (zaidi ya Sh 135 bilioni) hadi Dola180 milioni (zaidi ya Sh360 bilioni).

Taarifa iliyotolewa jana na Katibu wa Ofisi ya Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Mustafa Efe Uzman ilisema kushamiri huko kuliongezeka zaidi katika kipindi cha mwaka jana.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam juzi, Uzman alieleza kuwa Uturuki inaamini uhusiano huo utainua hadhi ya Watanzania ambao nchi yao ni miongoni mwa mataifa yanayokua kiuchumi katika Afrika Mashariki.

“Sehemu ya uhusiano wa kiuchumi kwa pande hizi inajumuisha safari za ndege za  moja kwa moja za kutoka Istanbul hadi Dar es Salaam,” alisema katibu huyo.

Baada ya Bilicanas na Shamba, Serikali ‘Yakamata’ Hoteli ya Mbowe Arusha

$
0
0

 Ikiwa ni takribani miezi mitano sasa tangu Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe alipoondolewa katika jengo la Bilicanas lililokuwa pia na ofisi za Free Media na siku moja tangu serikali imzuie kuendeleza shughuli za kilimo kwenye shamba lake, kiongozi huyo amepata pigo jingine katika hoteli yake anayoimiliki.

Mbowe ambaye ni kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni amepewa siku 14 na serikali awe amelipa kodi ya hoteli yake ya Aishi takribani TZS milioni 13.5 vingine vyo hoteli hiyo itafungwa.

Hoteli ya Aishi inayomilikiwa na Freeman Mbowe iliyopo Machame wilayani Hai mkoani Kilimanjaro.


Uamuzi huu wa serikali ya Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro umekuja siku moja tangu Mkuu wa Wilaya ya Hai, Gellasius Byakanwa alipotangaza kusitisha shughuli za kilimo katika shamba la Kilimanjaro Veggies linalomilikiwa na Mbowe kwa madai kuwa lipo katika eneo la chanzo cha maji cha Mto Weruweru.

Mkuu huyo wa wilaya alisema kuwa mujibu wa taarifa alizozipata kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri, Freeman Mbowe amekuwa akikwepa kulipa kodi kwa miaka mitano na kusababisha halmashauri kushindwa kufikia malengo ya ukusanyaji mapato.

Kwa miaka mitano imeelezwa kuwa Mbowe hakupeleka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) hali ya mauzo yake ambayo inapaswa kutumika kujua ni kodi kiasi gani anatakiwa kulipa.

Kuhusu shamba lake, DC alisema kuwa shughuli za kilimo katika eneo hilo limepeleka uharibifu wa mazingira huku kiongozi huyo akivuna miti ya asili bila kibali cha Mkuu wa Wilaya kinachotolewa baada ya uamuzi wa Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC).
Viewing all 104789 articles
Browse latest View live




Latest Images