Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104799 articles
Browse latest View live

Fahamu Sababu 3 za Mbu Kutosambaza VVU/ UKIMWI

$
0
0

1. Kwanza mdomo wa mbu haupo kama sindano za kawaida zinazotumika, mlija wa mbu ambao hutumika kuingizia mate yenye vimelea vya malaria ni tofauti na ule unaotumika kufyonza damu kutoka kwa

binadamu, kutokana na hili kwaiyo damu tu ndio huingia kwenye mwili wa mbu kutoka kwa binadamu alieng`atwa na mbu, na mate tu ya mbu ndio huingizwa kwenye mwili wa binadamu.

2. Pili magonjwa yote ambayo huambukizwa na insekta kama, matende na malaria aya magonjwa yanaweza kusambazwa na mbu kwa sababu vimelea vya aya magonjwa huweza kujizalisha(multiply) katika mwili wa mbu, ambapo hivi vimelea huweza kusambaa hadi kwenye mate ya mbu baada ya hapo huweza kuingizwa kwa kung`atwa binadamu. Tofauti ni kwamba vimelea yani virusi vya ukimwi(vvu) vinapoingia kwenye mfumo mzima wa mmeng`enyo wa mbu humeng`enywa kama chakula cha kawaida kisha hutoka kama uchafu, ili virusi vya ukimwi viweze kujizalisha(multiply) ni lazima viingie kwenye seli maalumu za binadamu.

3. Tatu, virusi vinavyosabisha ukimwi huzunguka taratibu kwenye damu ukilingansha na vimelea vinavyosababisha magonjwa yatokanayo na insekta(mbu), hii inamaanisha ata mbu anaponyonya damu kwa binadamu ambaye tayari virusi vya ukimwi hawezi kunyonya idadi kubwa ya virusi. Tafiti zaidi zinaonyesha kwamba ili mbu aweze kueneza virusi vya ukimwi kwa binadamu mtu huyo ina bidi ang`atwe na mbu million kumi(10) idadi hii ya mbu ndio inaweza kutengeneza uniti moja(1) ya kirusi apo ndipo huenda kikasababisha kueneza vvu, hii inamaanisha ata ikatokea kwa bahati mbaya uka mmeza mbu aliye mng`ata binadamu ambaye ana virusi vinavyosabisha ukimwi huwezi kupata maambukizi.

UHIMU
Achana na ngono zembe kwani
huchangia kwa asilimia kubwa maambukizi
ya VVU ambavyo usababisha UKIMWI…

Jinsi Ya Kuapproach Mwanamke Ambaye Humjui..!!!

$
0
0

Unataka kuzungumza na mwanamke ambaye humfahamu?

Kuongea na mwanamke ambaye humjui ni kama vile kujaribu kuoga na maji baridi.
Inakuwa vigumu na inakufanya kuingiwa na kibaridi. Kila wakati unapochukua hatua ya mbele unaskia kama tumbo linakukoroga vile.

Lakini kama mwanamume, jinsi ya kuapproach mwanamke ni jambo muhimu la kujua ikija maswala na kudate.

Kile ambacho kinachohitaji kwanza kabisa ni kumfanya mwanamke kama huyo akutambue...yaani upate attention kutoka kwake. Hii inakuwa rahisi kwa kutumia mbinu hizi:

1. Mwangalie
Tuseme sahizi uko na marafiki zako ama uko pekeako katika sehemu ambayo ina watu wengi halafu huyo mwanamke unataka kumuaproach yuko karibu na wewe ama sehemu mbali kidogo na wewe. Kile unachohitajika sasa ni umuangalie ili ufanye kumuonyesha kama unajaribu kumuangalia yeye. Jaribu kujifanya unamwuangalia kisirisiri, halafu akijaribu kukuangalia tu unajifanya unashughli nyingine ama unaongea na marafiki zako. Hii itamsisimua kutaka kujua kwa nini unamuangalia hivyo itamfanya na yeye kukuangalia mara kwa mara kama utakuwa ukimwangalia

2. Mwangalie machoni
Kila wakati akikuangalia, wewe muangalie halafu papo hapo uangalie kando kikondoo. Endelea kumuangalia kimtindo huo mara kwa mara, na wakati mwingine, mwangalie nusu sekunde, uangalie kando halafu hapo hapo muangalie tena (nadhani hapo umenipata). Ukifanya hivyo utakuwa automatiacally unamsisimua kihisia. Lakini kama umejaribu njia hii yote halafu hakuonyesha dalili ya kuingiliana basi itakuwa hajakupenda ama kuridhika na wewe.

3. Jifanye kutoeleweka
Kama uko na marafiki zako, muangalie mara kwa mara, lakini jifanye kama unasumbuliwa na jambo fulani ambalo linakufanya wewe usielewe kile ambacho marafiki zako wanaongea. Hii itamfanya yule mwanamke kufikiria kuwa ameingia kwa akili yako hivyo ataona ya kuwa yeye ndiye chanzo kikuu kinachokuzuia wewe kumakinika na yale ambayo marafiki zako wanaongea. 

4. Mwonyeshe tabasamu
Bila kupoteza wakati, hii itakuwa ufunguo wa kwako kufungua mlango wako wa kuongea naye kwani atenshen yote yake itakuwa imekuja kwako hivyo lile unalohitajika la kufanya ni kumwonyesha tabasamu. Fanya kusmile kiasi tu ili kuonyesha kuwa wewe umekuwa intrested na yeye muda huyu wote.

ONYO: Usijaribu kuweka smile kubwa kwani itaweza kuleta maana nyingine haswa kwa mwanamke ambaye humfahamu kabisa.
Hatua hizi hapa juu lazima zote ziwiiane, yaani lazima zifanye kazi. Iwapo katika hatua yoyote hapo juu utamwona mwanamke anakupotezea, basi jua na mapema kuwa hujamridhisha na kile unachohitaji kufanya ni kukimbia tu.

Rapa Rosa Ree Amjibu Rapa Chemical Kiaina

$
0
0

Rapa Chemical siku mbili hizi amekuwa midomoni mwa watu baada ya kusema kuwa hataki kushindanishwa na watoto kitu ambacho kinaonekana kimemlenga moja kwa moja Rapa wa kike mpya ambaye amekuja juu sana ghafla kwa nyimbo zake mbili tu....

Msanii Rosa ree Leo amepost picha na maneno haya hapa chini na yanayoonyesha kuwa amemjibu Chemical kiana:

"How I be chilling when I think of my next HIT then some blasphemous mofo think they can beat the GODDESS 👑😎👑 " Rosa Ree

AFANDE Sele Amrushia Dongo Kitila " Kitila Ulikuwa Unaongea Sana Kabla Hujakaribishwa Mezani"

$
0
0

Kupitia ukurasa wa Facebook Afande Sele ameandika haya:

"Hongera Profesa Kitila Japo Kwa Shingo Upande Lkn Kupitia Wewe Nimejifunza Maana Ya Kuweka Akiba Ya Maneno Ili Elimu na Uungwana VIthibitishe Umuhimu Wake Ulimwenguni....Dah''Kitila Alikuwa Anaongee Saaana Kabla Hajakaribishwa Mezani...Sasa Na Yeye Yupo Mezani Kapewa Madikodiko Anakula....Mila Za Kikwetu Zinakataza Mtu Kuongea Wkt Wa KULA....Nasubiri Kuona Kama Kitila Atakiuka Mila Hiyo Kwa Kuendelea Kuongea Wkt Wa Kula Au Nae Atafuata Mkumbo Kwa Kukaa Kimya.....Dunia RangiRangile...." Afande Sele

Breaking News..Zitto Kabwe Aungana Rasmi na Ukawa..Asema 2020 Lao ni Moja Watamsimamisha Mgombea Mmoja..!!

$
0
0

Kiongozi mkuu wa chama cha ACT wazalendo katika mahojiano maalum amesema mwaka 2020 kuwa hajapiga hesabu zakugombea urais amesema atakaa na vyama vya upinzani na kumsimamisha mgombea mmoja, mgombea huyo anaweza akatoka chama chochote kati ya Chadema, CUF,NCCR Mageuzi au ACT

Alipoulizwa kama anaukubali UKAWA kama muungano thabiti amesema wataunda umoja mwingine kwa sababu ule ulikuwa nikwa ajili ya mambo ya katiba

Kwa Nini Wanawake Wanapenda Wanaume Masharobaro aka Bad Boys

$
0
0

Wanawake kuchagua wanaume masharobaro aka badboys kuwaliko wanaume wa kawaida si jambo geni na hutokea mara kwa mara. -aidha katika vyuo, vilabuni, sinema, maktabani ama sehemu yeyote ile. Wanaume masharobaro, kama wanaume wengine, wao pia wanamaumbo ya kila aina, shepu na mvutio wa kijinsia. Kama wewe ni mwanamume wa kawaida ambaye humaliza wa mwisho ama ushawahi kupoteza mpenzi wako kwa sharobaro fulani, hapo chini kuna nadharia ambazo zitasaidia kueleza kwa nini  wanawake wanapenda sana kuvutiwa na wanaume masharobaro.

1. Hamu ya kufuata
Kufuata kitu ambacho unakipenda huwa kuna msisimko fulani mtu hupata. Lakini msisimko zaidi hutokea wakati ambapo mtu anajaribu kufuata mtu ambaye hataki kujulikana mienendo yake ya kimaisha, kufuatwa ama kueleweka kimaisha. Haya ndio maisha anayoishi mwanamume sharobaro. Wanawake wanapenda sana wanaume ambao hawaeleweki kimaisha (yaani hawatambuliki) ama kutaka kujua maisha yao. Na wewe kama mwanamume unataka kutumia huu udhaifu kwa manufaa yako, wakati mwingine unafaa kumfanya mwanamke abaki na maswali chungu nzima kutaka kukujua zaidi. Kama unampenda, jaribu kadri iwezavyo kutojaribu kumuonyesha.  Badala yake mpe pia yeye changa moto kwa kuweka ujanja wa kutoeleweka mara kwa mara. Hii ni njia moja murua ya kuhakikisha utaingia katika akili yake.

2. Kutaka kuwafunga fundo
Kitu kingine ambacho wanawake huvutiwa kwa sharobaro ni kutaka nafasi ya kuwafunga fundo ama kuwajeuza tabia zao. Mwanamke, amezaliwa naturally na hisia za uzazi, yaani kutaka kujeuza mtu mwenye tabia ovyo kuwa na tabia nzuri. Hii huibua hisia halizi za uzazi ndio maana kama mwanamume unapaswa wakati mwingine kumsumbua mwanamke hikisia, kimawazo na kadhalika. Unafaa kuwa mpinzani lakini usiwe mhalifu. Unafaa kuwa hatari lakini usipitishe kiwango ambacho kitamwogopesha. Kimtazamo, unafaa kumfanya mwanamke auonyeshe uke wake wote ili kujaribu kukubadilisha, mpe nafasi ajaribu kuubadilisha upande wako wa kiza na mwishowe kukufanya uwe mwanamume thabiti katika mchakato mzima.

3.Uanaume uliothabiti
Wanaume masharobaro (na si wale feki) karibu nyakati zote huwashinda wanaume wa kawaida kwa sababu ya mambo mawili makuu. Kwanza ni kuwa ni wanaume majasiri na pili wanaudhibiti uanaume wao kwa kuwa ngangari kimaisha. Kutoogopa kwao kwa jambo lolote ndiko kunawafanya wanawake kuvutiwa nao. Wanawake wengi wanavutiwa na wanaume ambao ni hatari, ngangari na wenye nguvu kwa sababu si rahisi kuchezewa au kufanyiwa masihara. Ukismama  kumtetea mwanamke kuhusu mahitaji yake na uovu, hii inamaana ya kuwa una uwezo wa kusimama kando yake na jambo lolote lile.  Kuweza kuonyesha level ya kuwa wewe ni mtu usiekuwa na woga wowote, unafaa kumwonyesha mwanamke wako kuwa una uwezo wa kuwa ngangari mahali popote pale ili mradi kumlinda yeye tu.

4. Uoga wa kujitwika majukumu
Wanaume masharobaro hupenda kuhepa majukumu yanayohusiana na mahusiano. Kwa wanawake ambao wana uoga huo huo wa kuwa na majukumu, masharobaro huwavutia sana na kuwaona kama hakuna wanaume wazuri kama hao. Kwa kuwa wanawake hawatajitweka majukumu, huwa hawana haja ya kujishughulisha na hisia za kipenzi ambazo ni stress. Pia ni habari njema kwa wanawake ambao wako tayari kwa uhusiano wa kimapenzi wa muda mfupi pekee. Lakini kama kawaida, mwisho wa siku lazima mwanamume sharobaro au mwanamke mtundu lazima kuna sehemu fulani ndani ya mawazo yake anatamani kuwa na mahusiano ya kudumu na pia kupendwa. Hivyo siri hapa ni kuipima miondoko yake na uangalie level yake ya kujitwika majukumu katika mapenzi halafu sasa uanze na hapo.


Upende usipende, wanaume masharobaro watakuwa na nafasi kubwa katika moyo wa mwanamke. Kuna kitu ndani yao ambacho kinawasababisha wanawake kuangua mwili mzima kihisia na kimapenzi kwao. Lakini hii haimaanishi kuwa lazima kila mwanamume ajeuke na kuwa sharobaro ili aweze kuwa na nafasi rahisi ya kutongoza mwanamke aliye kwa ndoto zako. Kile unachotakiwa kufanya ni kucheza mchezo mzima kiwastani. Daima unafaa kuwa vile ulivyo huku ukiingiza tabia flani za usharobaro hivi katika miondoko yako. Kama kuna kitu nzuri kati yenu wawili, basi pia kuna sehemu mbaya ambayo unaweza kuitumia ili ukajinufaisha nayo

Wolper Aapa Kuacha Kunywa Pombe,Adai Zimemuharibu Vibaya..!!!!

$
0
0

NYOTA wa filamu nchini, Jackline Wolper, amesema yupo mbioni kuachana na unywaji wa pombe kama sehemu ya mkakati wake wa kuzuia unene uliopiga kambi kwake.

Wolper ameliambia DIMBA Jumatano kwamba, anachukizwa na unene alionao kwa sasa ambao kwa kiasi kikubwa umechangiwa na unywaji wa pombe.

Alisema, amekusudia kuanza mazoezi ya gym yatakayomsaidia kurudisha mwili wake wa wembamba ambao ulikuwa unampa mwonekano mzuri zaidi.

“Unajua mimi sikuwa mnywaji kabisa wa pombe na nilikuwa siipendi kabisa, huu mwili unaouona umesababishwa na pombe kwa sababu nikinywa ndio napata hamu zaidi ya kula chakula, kwa sasa nimeanza harakati za kuhakikisha narudisha mwili wangu wa mwanzo ambao ulinifanya nionekane vizuri zaidi ya hapa,” alisema Wolper.

Ccm ,Cuf A na Cuf B Zilivyoichanganya Chadema Kwenye Ubunge wa Afrika Mashariki..!!!

$
0
0

Wakati wabunge saba kati ya tisa watakaoiwakilisha Tanzania katika Bunge la Afrika Mashariki (Eala) wakipatikana juzi usiku, suala la wawakilishi wa upinzani limetawaliwa na hali ya kutoeleweka, huku ikibainika rasmi kuwapo kwa CUF  ‘A’ na CUF ‘B’.

Kikao cha juzi kilichotawaliwa na mjadala wa kikanuni kuhusu wawakilishi wa Chadema na CUF, kiliweka rekodi ya kuchukua muda mrefu baada ya kumalizika saa 7:00 usiku kikikipiku kikao kilichojadili sakata la uchotwaji fedha kutoka Akaunti ya Tegeta Escrow.

Waliopitishwa ni Fancy Nkuhi, Happines Legiko, Maryam Ussi Yahya, Dk Abdullah Makame, Dk Ngawaru Maghembe na Alhaji Adam Kimbisa kutoka CCM, wakati Habib Mnyaa, aliyekuwa amevuliwa uanachama na CUF, alichaguliwa pia kuingia kwenye chombo hicho.

Hata hivyo, wanachama wawili walioteuliwa na Chadema kuwania ubunge wa Eala, Ezekiah Wenje, aliyepata kura 124 za ndiyo na 174 za hapana, na Lawrence Masha, aliyepata kura 124 za ndiyo na 198 za hapana, hawajaingia kwenye chombo hicho, kitu ambacho kimeifanya Chadema kwenda mahakamani.

Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Tundu Lissu alisema jana kuwa uchaguzi huo ulikuwa ni batili kutokana na taratibu kutofuatwa.

Huu Ndio Ukweli Halisi..Profesa Mkumbo ‘Amevishwa Bomu’..!!!

$
0
0

Hatua ya Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliagi, Profesa Kitila Mkumbo kutwishwa mzigo wa ‘kumtua mama ndoo’, ni sawa na kuvishwa mabomu.

Profesa Mkumbo aliapishwa jana na Rais John Magufuli, na kupewa mzigo mzito wa “kumtua mama ndoo” katika wizara hiyo yenye mzigo mkubwa wa kuhakikisha miradi ya maji inatekelezwa.

Profesa Kitila, ambaye ni mwanachama wa ACT-Wazalendo aliteuliwa juzi kushika nafasi hiyo, ambayo ameikubali licha ya awali kukaririwa akimtaka Rais Magufuli aache kuwateua wasomi katika nafasi za kisiasa ili wafanye kazi zao za utafiti na kuzalisha wasomi wengine.

“Ukipewa kazi na mkuu wa nchi ni kushukuru Mungu na jukumu lako ni kufanya kazi kwa bidii. Na mimi niahidi Mheshimiwa Rais, nitakusaidia wewe na Mheshimiwa Waziri wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji kuhakikisha kwamba ajenda yako ya kuwafikia Watanzania na kuboresha maisha tunaifanikisha,” alisema Profesa Kitila mara baada ya kuapishwa Ikulu jijini Dar es Salaam jana.

“Maji ni tatizo namba moja kwa Watanzania. Tafiti zinaonyesha kuwa kweli Watanzania wanataja maji kuwa ni tatizo namba moja. Kwa hiyo tuna jukumu kubwa la kumsaidia Mheshimiwa Rais kadri iwezekanavyo (ili kuhakikisha) Watanzania wengi wanapata maji safi na salama,” alisema.


Kimenukaa..Mwakyemba Kumbana Makonda kwa Maswali 9.. Asema Tukio la Uvamizi Clouds ni la Jinai Hivyo Haliwezi Kuachwa Lipite Tu...

$
0
0

WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe, amesema kuna mambo tisa ambayo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, atatakiwa kuyatolea ufafanuzi kuhusiana na tuhuma zinazomkabili za kuvamia kituo cha televisheni cha kampuni ya habari ya Clouds Media.

Dk. Mwakyembe aliyasema hayo wakati wa mahojiano na Nipashe kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma jana, muda mfupi baada ya Spika wa Bunge kusitisha shughuli za chombo hicho cha kutunga sheria hadi leo saa 3:00 asubuhi.

Nipashe ilitaka kujua kinachoendelea kuhusu uchunguzi dhidi ya Makonda ambaye kamati ya watu watano iliyoundwa na aliyekuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, ilitoa ripoti ikidai Mkuu wa Mkoa huyo alivamia kituo cha TV cha Clouds akiwa na askari wenye bunduki na kutoa vitisho kwa wafanyakazi wa kituo hicho.

Kamati hiyo ilidai kubaini Makonda alifanya hivyo ili kulazimisha video ya mwanamke anayedai kuzaa na Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima, irushwe hewani.

Katika majibu yake, Dk. Mwakyembe alisema suala hilo ni “zito” na haliwezi kuachwa lipite bila kuchunguzwa na kuchukuliwa hatua stahiki.

Huku akiendelea kuikosoa ripoti ya kamati ya Nape ambayo amekuwa akisisitiza haijakidhi matakwa ya kikatiba na kisheria kwa kushindwa kumhoji Makonda, Dk. Mwakyembe alisema Mkuu wa Mkoa huyo atahojiwa kwa mambo tisa yanayohusiana na tukio hilo.

“Hili ni suala zito maana linahusisha uvamizi ambao ni kesi ya jinai,” alisema Mwakyembe ambaye ni daktari wa sheria na Waziri wa Katiba na Sheria mpaka wiki mbili zilizopita.

“Kuna vitu tisa ambavyo upande wa pili (Makonda) utaulizwa.”

Dk. Mwakyembe hata hivyo, alikataa kuvitaja vitu hivyo tisa huku akisita pia kutaja tarehe ambayo Makonda atahojiwa.

“Upande wa kwanza (Clouds TV) tayari umeshahojiwa na ripoti tunayo. Upande wa pili nao tutauhoji na wenyewe pengine una hoja,” alisema Dk. Mwakyembe.

“Ili kukidhi matakwa ya kikatiba na kisheria, ni lazima tuuhoji upande wa pili. Hili suala kama nilivyotangulia kusema ni la jinai. Lazima mtuhumiwa apate haki ya kujitetea.
“Ukifika mahakamani, hata yule mwenye kesi ya mauaji lazima tumpatie wakili, hata kama tunao uthibitisho kwamba ameua.”

Machi 29, wakati akijibu maswali ya waandishi wa habari alipokaribishwa ofisi kwake mjini Dodoma, Dk. Mwakyembe alisema hawezi kuikabidhi kwa wakubwa wake ripoti hiyo ya kamati ya Nape bila kuwapo na maelezo ya Makonda.

“Taaluma yangu ni sheria, hivyo siwezi kufanya jambo hilo la kupeleka malalamiko ya upande mmoja kwa mabosi zangu bila kusikiliza ule mwingine,” alisema Mwakyembe siku hiyo.

Alisema hatateua kamati nyingine ya kufuatilia jambo hilo, bali yeye na viongozi wenzake watakuwa kamati hiyo ili kuuhoji upande wa pili kisha kupeleka taarifa kwa wakuu wake ambao ni Waziri Mkuu, Makamu wa Rais na Rais mwenyewe.

JELA MIEZI SITA

Kamati ya watu watano iliyoundwa na Nape kuchunguza tukio la uvamizi wa televisheni ya Clouds ilibaini kuwa kiongozi huyo aliwatishia kuwafunga jela miezi sita wafanyakazi wake endapo wasingerusha kipindi alichokitaka.

Pia Kamati hiyo ilibaini Makonda aliwatisha kuwa angewaingiza wafanyakazi hao kwenye tuhuma za matumizi ya dawa za kulevya kama wasingerusha kipindi chake.

Aidha, kamati ilibaini kuwa Makonda aliwatisha wafanyakazi wa kituo hicho ili wasitoe taarifa za uvamizi wake, kwa mujibu wa taarifa iliyosomwa na Katibu wa Kamati hiyo, Deodatus Balile.

Wajumbe wengine wa kamati hiyo iliyokuwa chini ya uenyekiti wa Dk. Hassan Abass, ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari - MAELEZO, ni Mhariri Mkuu wa Magazeti ya The Guardian, Jesse Kwayu, Nengida Johannes wa Upendo Media na Mabel Masasi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).

Ilidaiwa Makonda akiwa na askari kadhaa wenye bunduki, alivamia kituo hicho na kuwalazimisha watangazaji wa kipindi cha ‘Da Wikend Show’ kurusha taarifa ya mama anayedai kuzaa na askofu Gwajima, bila ya kiongozi huyo wa kidini kupewa nafasi ya kusikilizwa.

Ingawa taarifa ni ya upande mmoja, kwa mujibu wa Balile mtuhumiwa alikubali kuwaona, lakini wakati wakipanda ngazi kwenda ghorofani iliko ofisi ya Mkuu wa Mkoa Ilala jijini, Makonda aliteremka kwa kutokea mlango wa nyuma.

Credit - Nipashe

Ukweli Mchungu...Kapu la JPM Latoa Lulu...!!!

$
0
0

Akiwa kwenye kapu la Rais John Magufuli linalosubiri kupangiwa kazi nyingine, Dk Mwele Malecela, mwana wa Waziri Mkuu mstaafu, John Malecela, amenyofolewa na Shirika la Afya Duniani (WHO) na kupewa ulaji. 

Wakati Dk Mwele aliyekuwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Magonjwa ya Binadamu (Nimr), Dk Mwele Malecela akipata kazi katika Shirika la Afya Duniani (WHO), baadhi ya wachambuzi wa masuala ya siasa na utawala wametofautiana kuhusu hatua za uwajibishaji zinazochukuliwa na Rais Magufuli.

Dk Mwele, aliyeteuliwa na WHO kuwa Mkurugenzi wa Vituo vya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa Afrika, alivuliwa ukurugenzi wa Nimr na Rais Magufuli Desemba 16, mwaka jana. Taarifa ya Ikulu haikueleza sababu ya kuondolewa, lakini hatua hiyo ilifanyika siku moja baada ya Dk Mwele kutangaza uwapo wa ugonjwa wa Zika nchini.

 Akizungumzia suala hilo kwa simu, Mhadhiri wa Sayansi ya Siasa wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam UDSM), Dk Benson Bana alisema Rais Magufuli hakurupuki kutengua uteuzi wa mtendaji yeyote bali huangalia rekodi zinazoonyesha udhaifu unaosababisha waondolewe.

Hata hivyo, Mhadhiri wa Sayansi ya Siasa wa Chuo Kikuu cha Mt. Augustine, Profesa Mwesiga Baregu alisema Rais Magufuli anakiuka taratibu za uwajibishaji wa watumishi wa umma.

“Rais yuko mbali kabisa na uwajibishaji, kwa sababu una misingi na kanuni zake. Huwezi kumwajibisha tu mtu kwa matukio kwa sababu anatekeleza taaluma yake. Huenda Rais anajiona yuko sahihi kwa kila jambo, lakini haitamsaidia kupata watendaji bora wa kumsaidia,” alisema.

 Akizungumzia suala hilo, Mhadhiri wa Sayansi ya Siasa wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Richard Mbunda alisema japo kuna watendaji waliokosea, lakini kuna uwajibishaji wenye utata.


Spika Ndugai Awatisha CHADEMA

$
0
0
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limetoa nafasi ya pili na ya mwisho kwa ajili ya mchakato wa kuwapata wawakilishi wawili wa Tanzania katika Bunge la Afrika Mashariki kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo.

Akitoa taarifa yake bungeni leo , Spika wa Bunge hilo Job Ndugai amesema hadi sasa nafasi hizo bado ni za CHADEMA na atahakikisha haki hiyo wanaipata na kwamba Katibu wa Bunge atatoa taarifa ni lini mchakato huo utafanyika.

Katika hatua nyingine, Ndugai ametoa tahadhari kwa chama hicho kuwa yeye ndiye mwenye mamlaka ya kutoa utaratibu wa kupatikana kwa wawakilishi wa Tanzania kupitia vyama vya upinzani, hivyo endapo wasipotumia nafasi hiyo, atatumia mamlaka aliyonayo kutangaza utaratibu mwingine ili Tanzania isikose wawakilishi katika nafasi hizo.

“Ikumbukwe kuwa maamuzi haya ya kuwatenganisha wabunge wa upinzani kwa  kuangalia vyama vyao ni maamuzi ya Spika, tukumbuke mabunge yaliyopita maspika wenzangu hawakufanya hivyo, waliwaweka wabunge wote wa upinzani kwenye kundi moja, mimi nikasema twende na demokrasia hii ya wawili, ambayo katika kufanya hivyo, mimi yuleyule,....tuendelee....... Hatuwezi kukubali nchi yetu ikose uwakilishi nchi yetu ikatekwa nyara kwa sababu fulani fulani". Amesema Ndugai

Pia Ndugai amewatoa hofu watanzania kuwa hawatakosa uwakilishi kwa kuwa anajua cha kufanya. "Tutatoa nafasi ya pili, lakini baada ya nafasi ya pili, tunajua hatua itakayofuata, nawahakikishia watanzania kwamba hawatakosa nafasi katika bunge hilo”

Katika uchaguzi uliofanyika juzi, Bunge hilo liliwachagua wajumbe 7 kati ya 9 waliohitajika, huku wagombea wawili wa CHADEMA  Ezekiah Wenje na Lawrence Masha wakikataliwa kwa kupigiwa kura za hapana.

Nafasi za Ajira/Kazi Zilizotangazwa Siku ya Leo Magazetini

Huwa napata shida sana nikikutana na Wanawake wenye hii tabia..

$
0
0
Huwa napata shida sana nikikutana na Wanawake wenye hii tabia...Unampenda Mwanamke kabisa from ur heart,unajipanga unampiga saundi..anakujibu,''How old are you kaka'' unamwambia am 29 years..utamsikia,''Oh my Ghosh,ur still a kid,mi nadate guys who are 45 years above...Wanajua kupenda,they are so caring,yaani nyie vijana mnasumbua sana''.Sio tunasumbua,anajua kabisa miaka 29 bado ndo unasaka hela,ndo umeanza maisha huna cha kumhonga,ukijitahidi sanaaa utampeleka shopping Karume na hiyo hela itakuuma kishenzi!

Anakuita Kid bila aibu wakati yeye ana miaka 23 tu halafu eti ana mahaba na jitu la miaka 47..Uongo mtupu!Ina maana mtu hawezi kupenda na kucare hadi afike miaka 45??Nyie semeni tu mnawalia timing coz mnajua mtu mwenye miaka 45 anakuwa ameshajipanga,amefanya kazi ana hela,unajifanya unampenda kumbe Parasite tu unataka kumnyonyoa mafao yake ya uzeeni,hamna hata aibu..Mnapenda sana vitu ready made,tengenezeni vya kwenu,ukiona mtu ana miaka 45 jua kuna Mwanamke mwenzio amefanya kazi kumfikisha hapo alipo,we unakuja unadandia tu,,,Kama kweli una mahaba tafuta mwanaume wako,panda nae daladala za Buguruni mrukie wote dirishani,msotee maisha kwa kutembelea TZ 11 hadi siku apate gari mfaidi wote halafu akifika miaka 45 uone kimwanamke cha IFM kinamsogelea eti hes caring uone inavyouma,utatamani umpige patasi ya kisogo...Gold diggers,waone kwanza,msione gesi mtwara mshaanza kuandamana!45years guy waiting for u student of 23 years,ina maana miaka yote hiyo alikuwa Stevie Wonder au??

By  Seth De Jesus Giovanni

Je..Sababu Mojawapo ya Makamanda wa CHADEMA 'Kummiss' Kikwete ni Hii Hapa..!!!?

$
0
0

Juzi Rais wa zamani JK alipoenda Bungeni inasemekana alishangiliwa zaidi na Makamanda wa Chadema, kuliko hata Wabunge wa CCM tafsiri nyingi sana zimetolewa ku justify kitendo hicho na hii ya kuitwa itwa Ikulu kupata Chai na Juice, inatajwa kuwa ni mojawapo ukizingatia kwamba Rais wa sasa ameshasema kwamba ni wakati wa kazi tu sio kukaa kaa na kucheka cheka na kunywa Juice ikiwa ni pamoja na kubana matumizi,

By Lemutuz

Mungu Atupe Nini: Neema Zaendelea Kumiminika Umoja wa Ulaya Wamuahidi Magufuli Bilioni 500...!!!

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 06 Aprili, 2017 amefanya mazungumzo na Balozi wa Umoja wa Ulaya hapa nchini Mhe. Roeland Van de Geer na kuushukuru umoja wa nchi hizo kwa kutoa msaada wa Euro Milioni 205 sawa na takribani Shilingi Bilioni 500 kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za maendeleo hapa nchini kwa kipindi cha miaka 4 kuanzia mwaka huu.

Mhe. Rais Magufuli amesema kutolewa kwa fedha hizo kumethibitisha uhusiano na ushirikiano mzuri uliopo kati ya Tanzania na Umoja wa Ulaya na kwamba pamoja na kutoa fedha hizo umoja huo unatarajia kutoa fedha nyingine kiasi cha Euro Bilioni 1.2 kwa ajili ya kuendeleza viwanda, kilimo na uzalishaji wa nishati.

“Nimefurahi sana kwamba uhusiano na ushirikiano wetu unajikita kushughulikia mambo ya msingi kwa Watanzania, nakuhakikishia kuwa fedha mnazotoa zitatumika vizuri na zitatoa mchango mkubwa katika maendeleo yetu” amesema Mhe. Dkt. Magufuli.

Nae Mhe. Balozi Roeland Van de Geer amempongeza Mhe. Rais Magufuli kwa uongozi wake mzuri na dhamira yake ya kujenga uchumi na kusimamia utawala bora ikiwemo mapambano dhidi ya rushwa, na pia amemuahidi kuwa nchi wanachama wa umoja huo zitaendeleza na kuimarisha zaidi ushirikiano wake na Tanzania.

Wakati huo huo, Mhe. Rais Magufuli amefanya mazungumzo na Balozi wa Israel hapa nchini Mhe. Yahel Vilan na kumhakikishia kuwa Tanzania imedhamiria kuimarisha na kukuza zaidi uhusiano na ushirikiano wake na Israel hususani katika masuala ya uwekezaji, biashara, utalii na uboreshaji wa huduma za kijamii.

Mhe. Rais Magufuli amesema ili kufanikisha dhamira hiyo Tanzania imefungua ubalozi nchini Israel na amemuomba Mhe. Yahel Vilan kupeleka ujumbe kwa Waziri Mkuu wa Israel Mhe. Benjamin Netanyahu kuwa Tanzania itafurahi kuona Israel inafungua ubalozi wake hapa nchini.

“Naamini uhusiano na ushirikiano wetu utaongeza manufaa zaidi kwa nchi zetu na watu wake, nimefurahishwa sana na taarifa kuwa watalii wataanza kuja kwa ndege moja kwa moja kutoka Tel Aviv Israel na hivi karibuni ndege yenye watalii zaidi ya 200 itakuja nchini kwetu, nawakaribisha sana watalii na wawekezaji kutoka Israel” amesema Rais Magufuli.

Kwa upande wake Mhe. Balozi Yahel Vilan pamoja na ujumbe wake amemueleza Mhe. Rais Magufuli kuwa wamefurahishwa na ziara waliyoifanya hapa nchini iliyowawezesha kukutana na viongozi mbalimbali na ameahidi kuwa Serikali ya Israel itajenga jengo la wagonjwa mahututi (ICU) katika Hospitali ya Benjamin Mkapa Mkoani Dodoma kuanzia mwishoni mwa mwaka huu.

Mhe. Balozi Yahel Vilan amemhakikishia Mhe. Rais Magufuli kuwa Israel itaendelea kushirikiana kwa karibu na Tanzania kwa kuunga mkono juhudi mbalimbali za maendeleo ikiwemo ujenzi wa viwanda, kilimo na kuimarisha huduma za matibabu kwa wananchi.

MC Algiers Yaja na Nyota 18..Watoa Neno Hii Moja Tu kwa Yanga..!!!

$
0
0

MC Algiers itawasili leo usiku jijini Dar es Salaam tayari kwa mchezo wake wa kwanza wa kufuzu kwa hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Yanga.

MC Algiers imesafiri na wachezaji 18 huku ikilazimika kuwaacha majeruhi mabeki Azzi na Boudebouda, ambao wanategemea kurejea katika mechi ya marudiano jijini Algiers.

Kocha Kamel Mouassa ambaye hajashinda katika mechi zake mbili za kwanza alizocheza ugenini dhidi ya Bechem United na FC Renaissance amesema wanataka kufanya mabadiliko suala hilo "Ni ukweli kwamba hatujashinda mechi mbili tulizocheza  Ghana na DR Congo; Siwezi kulificha hilo kwa wakati huu kwenu sababu tumekuwa tukishinda mechi za nyumbani.

"Tunajua haitakuwa kazi nyepesi kushindi ugenini, lakini tutafanya kila kitu kuhakikisha tunashinda nyumban. Kama tukishindwa kuwafunga kwao tunatakiwa kufunga japo bao moja ugenini litatusaidia katika mechi ya marudiano, "alisema Mouassa.

Naye nahodha Hachoud alisema: "Tuna mechi mbili za kutufikisha hatua ya makundi, tunatakiwa kupata matokeo mazuro Dar es Salaam ili kufuzu kwa hatua ya makundi. Hatupaswi kufanya makosa katika mechi hizo mbili, iwe Jumamosi au hapa Algiers. "

Kikosi cha MC Algiers: Chaouchi, Chaal, Hachoud, Karaoui, Bouhenna, Mebarakou, Demou, Kacem,  Chita, Derrardja, Seguer, Aouedj, Bouguèche, Nekkache, Djemaouni , Zerdab, Gourmi.


Mwanamuziki wa Ubelgiji Atua Nchini Kufanya Kolabo na Harmorapa..!!!

$
0
0

Mwanamuziki Kriticos kutoka Ubelgiji amewasili nchini kwa ajili ya kutengeneza wimbo wa pamoja na mwanamuziki  Harmorapa.

Kriticos ambaye anaimba miondoko ya kufokafoka, (rap) amesema ameupenda uimbaji wa Harmorapa  na ndiyo sababu ya kuamua kufanya naye kazi.

Aliyazungumza hayo muda mfupi baada ya kutua uwanja wa ndege wa Julius Nyerere leo mchana.

Kwa upande wake Harmorapa anayetamba na wimbo wa Kiboko ya Mabishoo alisema ujio huo ni heshima kubwa kwake.

Harmorapa amewataka mashabiki wake kukaa tayari kupokea ngoma hiyo itakayotengenezwa na mtayarishaji wa muziki, P-Funk Majani.

Imethibitika..Hivi Ndivyo Mbwana Samatta Alivyoibeba Tanzania Mikononi Mwake..FIFA Watoa Ripoti Hii..!!!!

$
0
0

MABAO ya mastraika Mbwana Samatta, Saimon Msuva na Mbaraka Yusuf waliyofunga wakati Taifa Stars ikizitambia Botswana na Burundi, imesaidia kuitoa Tanzania shimoni katika orodha ya viwango vya soka vya Shirikisho la Sola la FIFA.

Katika orodha iliyotolewa jana mchana, Tanzania imechupa kwa nafasi 22 kutoka 157 mpaka 135, ikiwa siku chache tangu nyota hao waliotupia kambani kuipa Stars ushindi wa mechi mbili mfululizo wa mechi za kirafiki za kimataifa.

Wakati Tanzania ikipanda kwa nafasi hiyo, majirani wa Kenya wamesogea kwa nafasi 10 juu kutoka ile ya 88 hadi ya 78 kidunia, matokeo ambayo yamechangiwa na ushindi kwenye mechi ya kirafiki dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na sare dhidi ya Uganda.

Uganda wenyewe wamezidi kuonyesha utemi wao kwenye ukanda wa Afrika Mashariki na Kati baada ya kupanda kwa nafasi mbili kutoka ya 74 hadi ya 72 jambo linalowafanya wawe vinara kwa nchi zilipo kwenye ukanda huu.

Kwa mujibu wa viwango hivyo, Misri inaongoza kwa ubora kwa Afrika ikiwa nafasi ya 19 kidunia ambapo inafuatiwa na Senegal iliyopo nafasi ya 30 kwa viwango vya FIFA na Cameroon iliyotwaa ubingwa wa Afrika mwaka huu, ipo nafasi ya 33.

Brazili ndio vinara wa dunia kwa sasa ikiipiku mahasimu wao wa Argentina walishuka nafasi ya pili, huku Ujerumani ikifuatiwa katika nafasi ya tatu.

Nchi za Chile, Colombia, Ufaransa, Ubelgiji, Ureno, Uswisi na Hispania zimekamilisha 10 Bora ya orodha hiyo mpya ya Fifa.

Kuhusiana na Zile Nyasi Bandia za Simba Kutakiwa Kupigwa Mnada..Hiki Ndicho Kilichofanyika Leo..!!!

$
0
0

Klabu ya Simba SC imesha malizana na mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) baada ya kulipa zaidi ya Sh milioni 80, kodi ya nyasi bandia zilizo kuwa bandarini.

Baada ya hapo, kinachofanyika ni kumalizia masuala kadhaa yakiwepo ya kuzitoa nyasi hizo bandarini.

Uongozi wa klabu ya Simba umetoa taarifa hiyo kupitia mtandao wao wa wakijamii wa instagram

simbasctanzania Taarifa Rasmi kuhusiana na Nyasi Bandia, Mpaka sasa Tumeshalipia Kodi yote ya Nyasi Bandia, Kinachoendelea sasa ivi ni Wakala wetu kumalizia taratibu za Kutoa Container zenye nyasi hizo bandarini kwenda kuwekwa rasmi katika uwanja wetu wa Bunju.
Viewing all 104799 articles
Browse latest View live




Latest Images

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596344.js" async> </script>