Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104793 articles
Browse latest View live

MAMBO Matatu Makubwa Ambayo Unaweza Kuyapata kwa Kunywa Chai Tu..!!!

$
0
0

Je, ni mara ngapi umekuwa ukiondoka kwako asubuhi bila kunywa chai? naamini inaweza kuwa ni mara kadhaa lakini wengine ikawa ndio desturi yao kabisa kutokunywa chai asubuhi wanapotoka nyumbani kuelekea kwenye mishughuliko au masomo yao.

Sasa leo ninazo hizi faidia kadhaa za kunywa chai wakati wa asubuhi kabla hujatoka kwako.

1. Husaidia kuongeza uwezo wako wa kufikiri  zaidi ya vile ambavyo utatoka bila kunywa chai asubuhi. Hivyo kama wewe ni mwanafunzi au mfanyakazi ni vyema kuzingatia unywaji wa chai kabla ya kuanza shughuli zako za siku husika.

2. Unapokunywa chai unajipunguzia hatari ya kuzongwa na magonjwa mbalimbali hususani yale ambayo si ya kuambukiza.

3.Pia unapokunywa chai asubuhi husaidia kuboresha mahusiano mazuri kati yako na familia yako. Kwa sababu unapoamka na kukaa meza moja na watoto au mke au ndugu na kunywa chai huwezesha wanafamilia kujuzana machache kuhusu siku hiyo kabla ya upilika 'ubuys' wa siku hiyo kuanza.

HALI ya Sukari Nchini Kizingumkuti..Bei Yapaa Hadi 2800 kwa Kilo Moja,,!!!

$
0
0

LICHA ya kuwepo kwa wafanyabiashara wachache wa sukari wasio waaminifu mkoani Mwanza kupandisha bei ya bidhaa hiyo kwa asilimia 22 kutoka Shilingi 2,300 hadi 2,800 kwa kilo moja, uzalishaji wa sukari umepanda hadi kufikia tani 326,000 kwa mwaka 2016/2017.

Kupanda kwa kiwango hicho cha uzalishaji sukari nchini kumebainishwa na Mwenyekiti wa mfuko wa maendeleo wa sekta ya sukari Tanzania (SIDTF), Deo Lyatto, wakati wa kikao cha wataalamu wa sukari cha kujadili changamoto zinazoikabili sekta hiyo.

Kwa upande wa wazalishaji wa sukari na wakulima wa miwa nchini na nje wameishauri serikali kutoa ushirikiano wa kutosha katika sekta hiyo ili kujenga uchumi na kuwezesha adhima ya serikali kuwa na nchi ya viwanda.

Naye Mkurungenzi wa bodi ya sukari nchini, Henry Semwanza, alisema huu ni muda muafaka kwa wazalishaji wa sukari kuongeza jitihada katika kuzalisha bidhaa zenye ubora na kuuza kwa bei ya chini ambayo wanachi wa hali ya chini waweze kumudu bei hiyo.

SERIKALI Yaumwa Sikio Ripoti CAG..!!!

$
0
0

PROFESA wa Uchumi katika Chuo Kikuu Mzumbe, Honest Ngowi, amesema kuna haja ya kuimarisha mifumo ya usimamizi wa fedha, kuongeza matumizi ya mashine za kieletroniki (EFD) na kutoa elimu sahihi kwa walipa kodi ili kuinua mapato.

Pia amesema kuwa mifumo ya usimamizi na utawala wa fedha iimarishwe pia na utaratibu wa misamaha ya kodi iangaliwe upya kuongeza ufanisi.

Prof. Ngowi aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam kwenye mkutano wa wadau wa haki na watetezi wa wananchi kutoka asasi mbalimbali ulioandaliwa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kujadili ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), kwenye ripoti ya mwaka 2015/16.

Alisema kwenye ripoti ambazo hutolewa mara kwa mara na CAG, pamoja na mapendekezo na maelekezo kutolewa na Kamati za Kudumu ya Hesabu za Serikali, hatua zinazochukuliwa bado hazijaleta mabadiliko kwa kiwango kikubwa.

“Kodi ikikusanywa ipasavyo huduma za jamii kama elimu, afya, miundombinu zitaboreka na hapa nidhamu katika matumizi ya fedha ni lazima,” alisema Prof. Ngowi na kuongeza:

“Ripoti inaonyesha kuna matumizi mabaya ya misamaha ya kodi. Mfano kuna magari 200 yamepewa msamaha kampuni mbili bila utaratibu. Haya ni matumizi mabaya ya misamaha na hivyo sheria ziangaliwe upya.”

Mkuu wa kitengo cha Utetezi na Maboresho wa LHRC, Anna Henga, alisema uchelewaji wa fedha za miradi ya maendeleo inasababisha ufujaji wa fedha na mianya ya rushwa.

Alisema masuala yaliyojitokeza kwenye ripoti ya CAG, ikiwamo kukua kwa deni la taifa, kuwapo kwa watumishi hewa ambao walilipwa zaidi ya Sh. trilioni 1.4 pamoja na vyama vya siasa nchini kupata hati isiyoridhisha, yaangaliwe na kuchukuliwa hatua.

Nape Nnauye Atumia Maneno ya Mwalimu Nyerere Kutupa Dongo Gizani..!!!

$
0
0

Mbunge wa jimbo la Mtama, Mh Nape Nnauye amemkumbuka marehemu baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na kuamua kutumia maneno yake katika kufikisha ujumbe wake kwa wananchi kupitia ukurasa wake wa twitter 

Mhe Nape Nnauye alikuwa akitoa ujumbe kuwa maana ya ubinadamu na heshima ya binadamu ni kutokaa kimya pale jambo la uovu linapokuwa likitokea, akiwataka wananchi kutokaa kimya wanapoona kuna jambo la uovu linatendeka.

Ili kufikisha ujumbe huo vizuri Mhe. Nape Nnauye ilibidi atumie clip ya video ya marehemu baba wa taifa, Julius Kambarage Nyerere wakati akihotubia kwa mara ya mwisho katika Mkutano Mkuu. Ambapo mwalimu alisema maneno haya kwa lugha ya kiingerza  

"Hotuba yangu ya mwisho kwenye huu mkutano mkuu, nimeelezea matukio na mienendo na mahitaji kwa namna ambavyo sisi Watanzania tuonavyo, kukaa kimya pale tuonapo hatari, kutulia tu pale tuonapo sera hatari ambazo ziko kinyume na kulinda amani na haki, kufanya hivyo itakuwa tunaachia uhuru wetu na utu wetu kamwe hatutafanya hivyo" Mwalimu Nyerere 

Baada ya kuweka video hiyo ya Mwalimu Nyerere Nape Nnauye naye aliweka ujumbe wake ambao ulisomeka hivi 

"Heshima ya binadamu na maana ya kweli ya ubinadamu ni kutokaa kimya pale uovu unapotendeka" aliandika Nape Nnauye   

LISSU Akomalia Vyeti vya Bashite Mahakamani..Habari Vichwa vya Magazeti ya Leo 1/5/2017..!!!

RAYVANNY Azitaja Kolabo Zake za Kimataifa Zilizokuwa Tayari...!!!

$
0
0

Msanii Rayvanny ametaja kolabo zake na wasanii wa nje ambazo zipo tayari.

Muimbaji huyo, ambaye yupo nchini Sweden kwa ziara yake ya muziki, amemuambia mmoja wa watangazaji wa nchi hiyo kua, tayari ameshafanya kolabo na msanii mkubwa kutoka Nigeria, Afrika Kusini na Kenya.

“Nina kolabo na msanii mkubwa kutoka Nigeria, ingawa kwa sasa siwezi kutaja jina lake. Lakini pia kuna kolabo Afrika Kusini, na Kenya ukiacha Bahati, kuna mwingine Khaligraph Jones kutoka Nairobi,” amesema Ray.

Kwa msanii wa Afrika Kusini tayari muimbaji huyo kutoka WCB ameshafanya kolabo na Dj Maphorisa tangu mwezi Disemba mwaka jana.

UKWELI Mchungu..Serikali Imepigwa Changa la Macho Kwenye Ununuzi wa Boeing 787- 8.Hivi Ndivyo Ilivyo A -Z ..!!!

$
0
0

Disemba 12, 2016 ilikuwa siku ya furaha  baada ya taarifa kutoka serikali kuwa imeweka oda Boeing, ili kununua ndege ya kisasa kabisa 787-8.

Na yakwamba serikali itatoa $224.6Millioni ili kupata ndege hiyo. 

Kumekuwa na taarifa mbali mbali, kwamba manunuzi haya yana chembe chembe za ufisadi. Na kwakuwa sipendi kuamini vitu bila kufanya utafiti nami nimeona nizame kwenye websites mbali mbali kutafuta ukweli. 

Kwa ufupi kama wengine wasemavyo ni kweli hata Mimi nimeshaamini "SERIKALI IMEPIGWA"
lakini hadi kufikia hii Conclusion kuna mambo ya msingi unatakiwa kuyajua. 

1. SERIAL NUMBER(SN) NA LINE NUMBER.
-Kila ndege huwa na serial number yake kama yalivyo magari. Ndege tulioagiza serial number yake ni 35508
-Line number ni ndege ya ngapi kutengenezwa. Kwa mfano kama zimetengenezwa ndege 10. Ndege ya kwanza itakuwa LN1, ya pili LN2 nakuendelea. 

2. TERRIBLE TEENS NI NINI? 
Terrible teens ni zile ndege za mwanzo kutengenezwa za Boeing 787-8. Hizi ndege zilikuwa 20. Kwahiyo hiyo ni Line number 1-20 (Kuwa makini hapa). Na hizi ndege zilifanyiwa majaribio mengi na matengenezo mengi mapya ili kupata ndege bora zaidi. 

Kwa kifupi tunaweza sema zilikuwa sample ya kutengenezea ndege zingine. Kutokana na kufanyiwa modification za mara kwa mara hizi ndege zilipitiliza uzito uliotakiwa. Kutokana na kuongezeka uzito ndege hizi hata uwezo wake wa Masafa ukawa Umepungua kwa Maili 1000 au KM 1609.344

Kutokana na hili makampuni yaliotaka order za mwanzo kama All Nippon, Maroc etc. yaligoma kuchukua hizi ndege bali yalichukua ndege zilizotengenezwa baada ya zile 20 za mwanzo yaani Line number 21 na kuendelea. 

Terrible teens zingine ziliwekwa kwenye majumba ya kumbukumbu na baadhi ya kampuni walizichukua. Zikabaki 12 uwanjani miaka mitano bila mnunuzi toka 2009 zilipoanza tengenezwa. 

Kutokana na aibu iliyokuwa inaipata Boeing ya kukaa na mindege isiyo uzika. Ikaamua yafuatayo 

(a) Kutafuta Wateja ambao hawatajali issues ya kikomo cha masafa ya ndege 

(b) Kuziuza hizi ndege kwa bei rahisi ( karibu nusu bei kutoka $224M hadi $99M) 

CONCLUSION 
Kutoka katika websites ya Boeing na na web zingine za usafiri wa anga zimeweka wazi Ndege tulio iwekea order ni Boeing 787-8, serial number 35508, Line number 19.

Sasa kwa maelezo niliyotoa Line number 19 IPO ndani ya Line number 1-20. Kwa kifupi ndege tuliogiza ndio zile ndege za mwanzo 20 zilizopachikwa jina la Terrible Teens. 

Swali lingine la kujiuliza kwanini tumeuziwa ndege iliyo doda ,iliyoshushwa bei hadi kufikia $99M kwa bei ya ndege mpya yaani $224.6M? 

Bila kupepesa macho hapa tumepigwa $124M na ushee ambazo tungeweza nunua Boeing 737-800 Next Generation mpyaaaa ya 2016.

Kama nilivyokwisha sema Nina imani na Rais Magufuli ni mtu makini anayeipenda Tanzania. Na imani hili litatolewa maelekezo na kufanyiwa kazi. 

PATA Tiba ya Asili Kutoka Kwa Mtabibu wa Nyota Maalim Hussein...Una Shida na Mapenzi Au Pesa Hazikai?

$
0
0

Kutana  na Mtabibu Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH Maalim HUSSEIN Mtabibu wa Nyota za Binadamu na Dawa za Asili ya Africa Mwenye UWEZO Kubaini tatizo lako Pindi tu Utakapo Fanya Mawasilino Kupitia Wasaa Husika..

JE UNASUMBULIWA NA Mapenzi? (Umeachwa na Umpendae,Awe Mume,Mke na Bado unampenda?Na  Umejaribu Sehemu nyingi Bila Mafanikio?Wasilina na Maalim Hussein Ujione muujiza wa Papo kwa Papo.. 

Anauwezo WA KURUDISHA MAHUSIANO NA KUIMARISHA NDOA YAKO NDANI YA SAA 12 TU. 

Umekimbiwa na Mumeo,mkeo au Mpenzi na anaishi na mtu mwingine? Muone akutatulie Anauwezo wa Hali ya Juu wa Kusambalatisha Mahusiano yao Endapo utafata Atakacho kuelekeza, Atamfanya Atimize Ahadi zote kwa Muda Mfupi.

Maalim Hussein Anatumia Jina la Muhusika au Picha Kumaliza Tatizo lako..

Anatibu kwa Kutumia  Vitabu vya QUR-AN Dawa za Asili za Africa,Dawa za Kiarabu na Majini.Anatafsiri Ndoto. Kushinda BAHATI NASIBU, KUSAFISHA NYOTA. Mvuto wa Mwili na BIASHARA, Kinga ya Mwili,ZINDIKO za Nyumba, MIGUU Kufa GANZI, Kufungua KIZAZI kwa wale walio fungwa kwa njia za KISHIRIKINA, Anakupa Jini la Mali kwa yule anaehitaji Utajiri BILA MASHARTI, Nguvu za KIUME, Humaliza Kesi zilishindika ndani ya siku 14 tu..na mengi 

ZaidiWhatsapp +255 674 835107  Au Piga +255746757102

NB: TIBA KWA DINI ZOTE NA IMANI ZOTE...

LISSU Akomalia Vyeti vya Bashite Kortini...Aungana na Wanasheria Wenzake TLS Kutaka Aliyefoji Jina Atupwe Gerezani..!!!

$
0
0

WAWKILI Tundu Lissu na wenzake wa Chama Cha Wanasheria Tanganyika (TLS) wamelikomalia vilivyo sakata maarufu la Bashite linalohusiana na tuhuma za kughushi vyeti vya kielimu linalomkabili mmoja wa wakuu wa mikoa kwa kulifikisha kortini ili lipatiwe ufumbuzi.

Aidha, Lissu na wenzake hao wamedhamiria kuona kuwa kigogo huyo anayetuhumiwa kuliacha jina lake halisi la Daudi Albert Bashite kutokana na matokeo mabovu ya sekondari na kutumia jina la mtu mwingine, achukuliwe hatua za kisheria ikiwamo kufungwa jela kwa kosa la kughushi ikiwa itathibitika kuwa ana hatia.

Akizungumza jana na waandishi wa habari mjini Dodoma jana, Lissu ambaye ni Rais wa TLS, alisema uamuzi huo wa kulifikisha mahakamani suala la Bashite umetokana na maazimio ya baraza la uongozi la chama hicho, lengo likiwa ni kulinda utawala wa sheria na uwajibikaji nchini.

Tofauti na matarajio ya baadhi ya watu, sakata hilo la Bashite halikupatiwa jibu kutokana na ripoti ya uhakiki wa vyeti vya watumishi wote wa umma iliyokabidhiwa kwa Rais John Magufuli Ijumaa kutowagusa viongozi wa kisiasa wakiwamo mawaziri, wakuu wa mikoa, wabunge na madiwani.

Katika kufanikisha nia hiyo ya TLS, Lissu aliyekuwa na viongozi wengine wa chama hicho wakiwamo Makamu Rais, Godwin Ngwilimi na Wakili Stephen Kuwayawaya, alisema miongoni mwa hatua walizochukua ni pamoja na TLS kufungua mashtaka binafsi ya jinai dhidi ya mkuu huyo anayedaiwa kuitwa Bashite.

Aliongeza kuwa mkuu huyo wa mkoa, anatuhumiwa kwa makosa mbalimbali ya jinai likiwamo hilo la kutumia vyeti feki na kwamba, kazi ya kumshtaki haitachukua miezi bali ni wiki mbili au tatu.

“Kifungu cha 128(2) cha sheria ya Mwenendo wa jinai, sura ya 20 ya sheria za Tanzania kinaruhusu mtu binafsi (pamoja na taasisi, kampuni au mashirika kama TLS) kupeleka malalamiko kwa hakimu mwenye mamlaka pale anapoamini kuna sababu za msingi zinazoonyesha kuwa kosa la jinai limetendwa,”alisema Lissu, akielezea vifungu wanavyotumia kufikisha suala hilo kortini.

Alisema dhana ya utawala wa sheria ina maana pana na kwamba, pamoja na mambo mengine, siyo tu kwamba hakuna mtu aliyeko juu ya sheria, bali pia kila mtu bila kujali cheo au nasaba na hali yake kiuchumi na jamii, yuko chini ya udhibiti wa sheria za kawaida za nchi na hivyo yuko pia chini ya mamlaka ya mahakama za kawaida.

“Kuna tuhuma za muda mrefu sasa kwamba Mkuu huyo wa mkoa ametumia vyeti vya shule ya sekondari visivyokuwa vyake. Yeye… ni Daudi (Albert) Bashite,” alisema Lissu, akiongeza kuwa jina linalotumiwa sasa na mkuu huyo linadaiwa kuwa mwenyewe yupo na ndiye mwenye vyeti halisi, na kitendo hicho ni kosa la jinai.

Akifafanua zaidi, Lissu alisema kifungu cha 120 cha Kanuni ya Adhabu, Sura ya 16 ya Sheria za Tanzania, kinasema “Mtu yeyote aliye kwenye utumishi wa umma ambaye, wakati akitekeleza majukumu ya ofisi yake akifanya kitendo cha udanganyifu au ukiukaji dhamana huo ungekuwa ni kosa la jinai kama ungefanywa na mtu binafsi au la, anafanya kosa na endapo atapatikana na hatia atapata adhabu ya kifungo cha miaka saba jela.”

Lissu alisema kwa kutumia vyeti vya shule visivyokuwa vyake, na kwa kutumia majina ya mtu mwingine wakati akiwa mtumishi wa umma, mkuu huyo mwenye jina halisi la Daudi Bashite ameathiri imani ya wananchi kwa serikali yao kwa kuajiri na kulinda watu wadanganyifu na wasiokuwa na vyeti halali.

“Mtu huyu amefanya kosa la jinai ambalo kwalo anastahili kushtakiwa mahakamani na endapo atapatikana na hatia anastahili kuadhibiwa kwa mujibu wa sheria za kawaida za nchi yetu,” alisema Lissu ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema).

Lissu aliongeza kuwa endapo Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) atakataa kutoa ridhaa, TLS itamfungulia mkuu huyo wa mkoa mashataka ya rejea ya kimahakama katika Mahakama Kuu ili alazimishwe kutoa ridhaa hiyo.

Kabla ya kumkabidhi Rais Magufuli ripoti ya uhakiki wa vyeti vya elimu na kitaluma kwa watumishi wa umma nchini, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Uatawala Bora, Angela Kairuki, alisema watumishi 9,932 walikutwa na vyeti vya kughushi na kwamba, ripoti hiyo haikuwagusa viongozi wa kisiasa wakiwamo mawaziri, wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya, wabunge na madiuwani.

Hata hivyo, Makamu Rais wa TLS, Ngwilimi, alisema kuwa kwa mujibu wa kifungu cha Sheria ya Utumishi wa Umma namba 3 na 5, tafsiri ya mtumishi wa umma inawahusisha pia Wakuu wa mikoa na Wakuu wa Wilaya na hivyo kina Bashite walipaswa pia kuhusishwa katika uhakiki huo.

JPM - Naomba Mniombee Ili Urais Usinipe Kiburi..Maisha Haya ni ya Mpito Tu..!!

$
0
0

RAIS John Magufuli maetoa ombi zito kwa viongozi wa dini nchini wakiwamo maaskofu baada ya kuwataka wamwombee ili kazi yake ya urais isimpe kiburi bali aendelee kuwa mtumishi mwema wa watu.

Rais Magufuli alitoa ombi hilo kwa nyakati tofauti jana wakati aliposhiriki ibada ya Jumapili kwenye Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Moshi Mjini na Kanisa Kuu la Kiaskofu la Parokia ya Kristo Mfalme (la katoliki), pia la Moshi Mjini, mkoani Kilimanjaro.

Magufuli aliomba maaskofu na viongozi wengine wa dini wamuombee wakati akiwa katika kanisa la Usharika wa Moshi, kwenye ibada iliyoongozwa na Mkuu wa Kanisa la KKKT Tanzania, Askofu Dk. Fedrick Shoo na baadaye katika Kanisa la Kristo Mfalme ambako ibada iliongozwa na Askofu wa Jimbo Katoliki la Moshi, Mhashamu Isaac Amani.

Awali, akiwa katika kanisa la KKKT, Askofu Shoo alimuomba Rais Magufuli kujitenga na washauri wanaojikomba na badala yake apokee ushauri unaotolewa na washauri wema na wenye nia njema kwake na kwa taifa.

“Tunamuomba Mungu akupe washauri wazuri wasio na hila na wasiojikomba kwako….na ambao hawatakuwa na ajenda za kujinufaisha binafsi. Pale unapoona mambo hayaendi na umepungukiwa, sisi kama kanisa na Watanzania wenye nia njema tunasema tupo tayari kukushauri na kukuombea,”alisema Askofu huyo ambaye pia ni Askofu wa Dayosisi ya Kaskazini.

Aidha, Askofu Shoo alisema pamoja na jitihada mbalimbali za maendeleo zinazoendelea kufanywa na serikali ya awamu ya tano, bado kumekuwa na baadhi ya watu ambao wamekuwa wakiona mabaya tofauti na yale mazuri ambayo yamekuwa yakifanywa na serikali, jambo ambalo sio sahihi.

“Tunamuomba Mungu atupe Watanzania ambao wana uwezo wa kuona mema ambayo umekuwa ukiyatenda  na umekuwa ukiyafanya katika kipindi hiki kifupi cha utawala wako,” alisema Dk. Shoo

Dk. Shoo aliongeza kuwa kanisa lake litaendelea kuunga mkono jitihada zinazochukuliwa na serikali katika utumbuaji majipu na kuwashughulikia wale wote ambao wamekuwa wakiishi kwa kutegemea shughuli za magendo na rushwa.

Alimwomba pia Rais Magufuli kuangalia uwezekano wa kuzipunguzia taasisi za dini mzigo wa kodi ambazo wanatozwa pale wanapoingiza mali ambazo zimekuwa zikitumika kutoa huduma za kijamii.

Wakati alipoitwa na Dk. Shoo ili kutoa salamu kwa waumini wa kanisa hilo, ndipo Rais Magufuli alipoomba viongozi wa dini wamuombee ili madaraka aliyo nayo yasimpe kiburi.

Alisema mtu anaweza akapata madaraka na kuwa kiburi, na akafanya mambo ya ajabu wakati maisha yenyewe ni ya temporary (muda), jambo ambalo yeye anaomba lisimtokee.

“Mheshimiwa Baba Askofu, ombi lako kuhusu kodi kwa taasisi za dini nitalibeba na nitalifanyia kazi. Haiwezekani mtu unaagiza X - Ray machine kwa ajili ya huduma halafu ulipe kodi. Nitazungumza na viongozi wa Wizara ya Fedha wajadili na kuona namna ya kulishughulikia,”alisema Rais Magufuli.

Rais Magufuli alilichangia kanisa hilo (KKKT) mifuko 150 ya saruji kwa ajili ya shughuli za ujenzi na pia kuizawadia kwaya ya Usharika wa Moshi Mjini Sh. milioni moja.

IBADA KANISA KRISTO MFALME

Katika Kanisa Kuu la Kiaskofu la Parokia ya Kristo Mfalme, Askofu Amani alisema ni vyema wananchi wakaendelea kulinda amani na umoja wa taifa kwani ni dhahiri kuwa amani iliyopo inalindwa pia na wananchi na siyo majeshi peke yake kama inavyodhaniwa na baadhi ya watu.

Baada ya kumaliza mahubiri yake, Askofu Amani alimpa nafasi Rais Magufuli kutoa salamu zake ambapo alisema: “Najua urais mnao ninyi na mliamua niwe mtumishi wa watu. Naomba muendelee kuniweka kwenye maombi ili kazi hii ya urais isinipe kiburi… niwe mtumishi wa watu.”

Akieleza zaidi, Rais Magufuli alisema amekuwa mtu wa kufikiriwa vibaya  na baadhi ya watu kwamba ni mtu mkali, lakini ukweli ni kwamba yeye ni mkali kwa watu wanaofanya maovu.

Alisema ni vyema Watanzania wakaendelea kumuombea ili asiwe na kiburi cha madaraka na kuendelea kutekeleza kazi aliyopewa na Mungu na kwamba, amekuwa akifanya mabadiliko makubwa kutokana na ukweli kwamba nchi ilikuwa inaelekea pabaya.

Rais Magufuli alichangia pia Kanisa la Kristo Mfalme mifuko 100 ya saruji pamoja na kwaya ya kanisa hilo kiasi cha Sh. milioni moja.

MAMA Samia Aungana na Magufuli Kuutikisa Mji wa Moshi na Vitongoji Vyake Leo Siku ya Wafanyakazi Duniani..!!!

$
0
0

MAKAMU wa Rais, Samia Suluhu Hassan ameungana na Rais John Magufuli na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa katika sherehe za maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi) ambazo kitaifa zinafanyika leo mjini Moshi

Samia aliwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) jana jioni, wakati Rais Magufuli na Waziri Mkuu waliwasili tangu juzi wakitokea mkoani Dodoma.

Rais Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika sherehe hizo zinazofanyika katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MoCU), ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kikazi ya siku tatu mkoani hapa iliyoanza juzi.

Kwa mujibu wa Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Said Meck Sadiki, Rais Magufuli atazungumza na wafanyakazi wote nchini kupitia sherehe hizo kwenye uwanja huo.

Aidha, inatarajiwa kuwa pamoja na mambo mengine, Rais Magufuli atatoa maelekezo kuhusu kilio cha vyama vya wafanyakazi ambacho ni pamoja na kukosekana kwa mikataba ya hali bora kazini.

"Nawasihi wananchi wajitokeze kwa wingi katika kilele cha sherehe za wafanyakazi (Mei Mosi) ambazo kwa mwaka huu zinafanyika kitaifa mkoani Kilimanjaro.

Pia nashauri wafanyabiashara watumie fursa hii kufanya biashara zako kwa ukarimu na uaminifu mkubwa ili kuwavutia wageni wanaoingia Moshi na watakaoendelea kuja," alisema Sadiki

ZITTO Aendelea Kupalilia Sakata la Serikali Kununua Ndege Mbovu....Adai Tumepigwa

$
0
0
MOROGORO WA NDEGE ILIYONUNULIWA AINA YA BOEING 787-8

Disemba 12, 2016 ilikuwa siku ya furaha baada ya taarifa kutoka serikali kuwa imeweka oda Boeing, ili kununua ndege ya kisasa kabisa 787-8.

Na ya kwamba serikali itatoa $224.6Millioni ili kupata ndege hiyo.
Kumekuwa na taarifa mbalimbali, kwamba manunuzi haya yana chembe chembe za ufisadi.

Na kwakuwa sipendi kuamini vitu bila kufanya utafiti nami nimeona nizame kwenye websites mbalimbali kutafuta ukweli.

Kwa ufupi kama wengine wasemavyo ni kweli hata Mimi (Zitto Kabwe) nimeshaamini "SERIKALI IMEPIGWA"
lakini hadi kufikia hii Conclusion kuna mambo ya msingi unatakiwa kuyajua.

1. SERIAL NUMBER(SN) NA LINE NUMBER.
-Kila ndege huwa na serial number yake kama yalivyo magari. Ndege tulioagiza serial number yake ni 35508

-Line number ni ndege ya ngapi kutengenezwa. Kwa mfano kama zimetengenezwa ndege 10. Ndege ya kwanza itakuwa LN1, ya pili LN2 nakuendelea.

2. TERRIBLE TEENS NI NINI?
Terrible teens ni zile ndege z a mwanzo kutengenezwa zp

a Boeing 787-8. Hizi ndege zilikuwa 20. Kwa hiyo hiyo ni Line number 1-20 (Kuwa makini hapa). Na hizi ndege zilifanyiwa majaribio mengi na matengenezo mengi mapya ili kupata ndege bora zaidi.
Kwa kifupi tunaweza sema zilikuwa sample ya kutengenezea ndege zingine. Kutokana na kufanyiwa modification za mara kwa mara hizi ndege zilipitiliza uzito uliotakiwa.

Kutokana na kuongezeka uzito ndege hizi hata uwezo wake wa Masafa ukawa Umepungua kwa Maili 1000 au Km 1609.344
Kutokana na hili makampuni yaliyotaka order za mwanzo kama All Nippon, Maroc etc. yaligoma kuchukua hizi ndege bali yalichukua ndege zilizotengenezwa baada ya zile 20 za mwanzo yaani Line number 21 na kuendelea.
Terrible teens zingine ziliwekwa kwenye majumba ya kumbukumbu na baadhi ya kampuni walizichukua. Zikabaki 12 uwanjani miaka mitano bila mnunuzi toka 2009 zilipoanza tengenezwa.

Kutokana na aibu iliyokuwa indicate Kampuni ya Boeing ya kukaa na mindege isiyo uzika. Ikaamua yafuatayo:-

(a) Kutafuta Wateja ambao hawatajali issues ya kikomo cha masafa ya ndege,

(b) Kuziuza hizi ndege kwa bei rahisi (karibu nusu bei kutoka $224M hadi $99M).

CONCLUSION
Kutoka katika websites ya Boeing na web zingine za usafiri wa anga zimeweka wazi Ndege tuliyo iwekea order ni Boeing 787-8, serial number 35508, Line number 19.

Sasa kwa maelezo niliyotoa Line number 19 IPO ndani ya Line number 1-20. Kwa kifupi ndege tuliyoagiza ndiyo moja ya zile ndege za mwanzo 20 zilizopachikwa jina la Terrible Teens.

Swali lingine la kujiuliza kwa nini tumeuziwa ndege iliyo doda ,iliyoshushwa bei hadi kufikia $99M kwa bei ya ndege mpya yaani $224.6M?

Bila kupepesa macho hapa tumepigwa $124M na ushee ambazo tungeweza nunua Boeing 737-800 Next Generation mpyaaaa ya 2016.

Kama nilivyokwisha sema Nina imani na Rais Magufuli ni mtu makini anayeipenda Tanzania. Na imani hili litatolewa maelekezo na kufanyiwa kazi.

My take:
Iwapo humu tuna wataalamu wa ndege tupeni maoni yenu ili tupanue uelewa juu ya ndege hizi.

WEMA Sepetu, Jokate Wapigwa ‘Stop’ Wanaume

$
0
0
Mikakati ya kusaka nafasi ya kuingia bungeni mwaka 2020 kwa walimbwende wa Bongo, Wema Isaac Sepetu na Jokate Mwegelo ‘Kidoti’, imenoga baada ya mastaa hao kutakiwa kutengeneza sifa ‘CV’ nzuri kwa kupigwa ‘stop’ kuhusishwa na skendo za wanaume kama walivyozoeleka, Wikienda limedokezwa.

WEMA

Habari kutoka ndani ya chama chake kipya cha Chadema baada ya kuhama CCM zilieleza kuwa, Wema anatarajia kukabidhiwa majukumu ya uhamasishaji kama ilivyokuwa kwa mama yake, Mariam Sepetu ambaye alipewa cheo hicho kwa mtaa wake wa Sinza-Mori jijini Dar.

“Ameshaelezwa nini cha kufanya. Cha muhimu ni kuhakikisha anakuwa mbali na skendo za wanaume na kutengeneza CV kwa kufanya kazi za kijamii.

“Kama mtakumbuka hivi karibuni Wema alikuwa Morogoro kuhamasisha upandaji wa miti akiwa na Mbunge wa Viti Maalum wa Chadema, Devotha Minja. Sasa mwendo ni huohuo na ubunge kwake siyo jambo la kuuliza ifikapo 2020.

“Mbali na kufanya uhamasishaji kupitia shughuli za kijamii, pia anatengenezwa namna ya kuzungumza kwa kujenga hoja kwenye siasa ngumu, tofauti na alipokuwa CCM ambapo huko kuna siasa laini ukilinganisha na Chadema,” kilifunguka chanzo hicho.

Wikienda lilimtafuta Wema ili kupata ukweli wa ishu hiyo ambapo alikuwa akikata simu na kuomba ampigie mwandishi wetu baadaye.

Hata hivyo, alipotumiwa ujumbe mfupi kuelezewa kuhusu ishu hiyo ulionesha kupokelewa lakini hakujibu.

JOKATE

Wakati hali ikiwa hivyo kwa upande wa Wema, Wikienda pia lilidokezwa juu ya Jokate ambaye hivi karibuni alipewa cheo cha Kaimu Katibu wa Uhamasishaji wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) ikidadavuliwa kwamba huo ni mwendelezo wa harakati zake za muda mrefu za kutaka kuingia bungeni.

“Unajua, kama ilivyo kwa Wema, Jokate ana mvuto wake kwa vijana. Hicho cheo alichopewa ni ili kuzidi kumuweka karibu na viongozi wa chama na kuona utendaji wake. Suala la bungeni 2020 ni lazima, lakini pia amepigwa stop mambo ya sk¬endo za wanaume. Ndiyo maana baada ya kudaiwa kuachana na Ali Kiba hajasikika kuwa na mwanaume mwingine,” kilisema chanzo chetu.

Akizungumza na gazeti hili juu ya ishu hiyo, Jokate alisema kuwa, ndiyo kwanza ameanza kutekeleza majukumu yake hivyo ni mapema mno kuzungumzia ishu hiyo.

“Kwanza mimi namshukuru Mungu kwa nafasi niliyopewa, naamini sitawaangusha vijana,” alisema Jokate kwa mkato.

Hivi karibuni Jokate alikuwa miongoni mwa wanachama 450 wa CCM walioji¬tokeza kuchukua fomu za kuwania ubunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) lakini hakupata nafasi hiyo.

IMEJULIKANA ..Ray C Ataka Kujiua Mara 10

$
0
0
MWANAMUZIKI ambaye miaka kadhaa iliyopita alipotea kwenye anga la muziki baada ya kujitumbukiza kwenye matumizi ya madawa ya kulevya, Rehema Chalamila ‘Ray C’, amefunguka jinsi alivyotaka kujiua zaidi ya mara 10 kutokana na kujichukia.

Akizungumza na Wikienda katika mahojiano maalum wikiendi iliyopita, Ray C au Kiuno Bila Mfupa alisema kuwa, alifikia uamuzi huo mara kwa mara baada ya kujichukia kupita kiasi huku akiona kuwa hana thamani tena duniani wala hajui atatokaje kwenye dimbwi alilojiingiza akiwa bado msichana mdogo.

“Kujiua kwangu lilikuwa ni wazo la mara kwa mara, inaweza ikawa hata zaidi ya mara kumi kutokana na kukata tamaa kabisa ya maisha huku nikijitazama nilivyokuwa msichana mwenye ndoto nyingi lakini nateketea nikijiona,” alisema Ray C.

Mwanamuziki huyo ambaye amerejea kwenye gemu kwa kishindo alisema kuwa, nia ya kujitoa uhai ilikuwa ikitokana hasa na kuamini kwamba hawezi tena kujinasua sehemu aliyokwama kutokana na kujaa vizingiti vya kushindwa hivyo kufikiria hakuna njia nyingine zaidi ya kifo.


“Kuna wakati nilikata kabisa tamaa kuwa hakuna njia nyingine ya kunifanya nipumzike na tabu niliyokuwa nikipata zaidi ya kujitoa uhai ambao kwangu haukuwa na thamani na wala sikuwa ninajipenda tena hata kidogo,” alisema Ray C ambaye anatamba na wimbo wake mpya wa Unanimaliza.

By Imelda

ROMA Mkatoliki Yamfika Hapaa! Amtolea Uvivu Mbunge Kessy

$
0
0

Katika kipindi cha #Clouds360 kinachoendelea muda huu, msanii #RomaMkatoliki ameonyesha kukasirishwa na kitendo cha Mh Kessy ( Mbunge wa Jimbo la Nkasi ) kutaja jina lake Bungeni na kudai kwamba Roma aliimba wimbo kumhusu Rais. Hivi karibuni Mh Kessy aliongelea ' sakata la kutekwa kwa Roma ' na kudai kwamba hayo yalitokea baada ya Roma kuimba wimbo unaomkashifu Rais.
.
.
#RomaMkatoliki ameeleza kwamba alisikitishwa na kitendo hicho kwani Mbunge huyo alichokisema kilikuwa kitu cha uongo. " Tena alitaha kabisa jina langu. Akitoka nje ya Bunge yule ukimuuliza hana uhakika. Lakini ameongea vile kwa sababu yeye ana mahali pa kusemea. Je mimi mimi nitasemea wapi ? " - #RomaMkatoliki
.
TOA MAONI YAKO HAPA

RAIS Magufuli Afunguka Mambo Yanayomfanya Awe Mkali Kupita Maelezo..!!!

$
0
0

Rais John Magufuli ambaye yuko mkoani Kilimanjaro kwa ziara ya siku tatu, jana alisali kwenye makanisa mawili; akianza na Kanisa Katoliki la Kristo Mfalme na baadaye kwenye Usharika wa Moshi Mjini wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT).

Hata hivyo, licha ya kuwaomba viongozi wa makanisa na wananchi wamuombee katika awamu ya uongozi wake, pia aliwataka waelewe mambo kadhaa yanayomfanya awe mkali, ingawa hana tabia hiyo.

“Nafikiri mnaweza kuona sura yangu nilipo hapa. Ni tofauti sana na inavyotafsiriwa. Inawezekana inatafsiriwa ni mtu katili, wa ajabu mkali, siko hivyo. Mimi ni mpole na mnyenyekevu,” alisema Dk Magufuli akiwa katika kabisa la Kristo Mfalme.

Kisha, Dk Magufuli aliainisha mambo yanayomweka katika hali ya ukali kuwa ni pamoja na rushwa, watumishi hewa serikalini, wizi, dawa za kulevya na maovu yote yaliyomo serikalini.

 “Haya ninayoyafanya mimi na Serikali ni kwa sababu ya maovu makubwa yaliyokuwa yamejengeka ndani ya jamii na watu kutoogopa maovu,” alisisitiza huku akipigiwa makofi na waumini.

Mkuu wa KKKT, Dk Fredrick Shoo akamsifu kwa moyo wa kuthubutu kuyaanika majibu anayoyatumbua.

“Tunakuomba pale ambapo unatolewa ushauri kwa nia njema na washauri wema, Mungu akupe sikio la kusikia,” alisema Dk Shoo kauli ambayo iliamsha hisia za waumini wengi kanisani hapo.

Askofu Isaac Amani wa Kanisa Katoliki la Kristo Mfalme

Aliwataka Watanzania kuwa walinzi wa Taifa lao badala ya kuiachia jukumu hilo Serikali.

Leo, Rais Magufuli; Makamu wake, Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa watawaongoza wananchi katika maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani ambayo kitaifa itafanyika mjini Moshi.


KIMENUKAA..Jaji Mkuu Ampeleka Lissu Mahakamani..!!!

$
0
0

Chama Cha Wanasheria Tanganyika (TLS), kimepanga kwenda mahakamani kupata ufafanuzi wa kisheria kuhusu nafasi ya Jaji Mkuu.

Rais wa TLS, Tundu Lissu alisema Baraza la Uongozi la chama hicho katika kikao chao kilichofanyika kwa siku mbili mjini Dodoma, wameamua kuwa na kauli moja ya kurudisha utawala wa sheria na hawawezi kukaa kimya wakati mambo yanakwenda ndivyo sivyo.

“TLS tumeamua kufungua mashauri Mahakama Kuu ya Tanzania kuhoji uhalali wa kikatiba wa Rais John Magufuli kushindwa hadi sasa kuteua kiongozi mkuu wa Mahakama ya Tanzania yaani Jaji Mkuu,” alisema Lissu.

Alisema kuwa baraza lao linaamini kuwa, Rais Magufuli anakiuka Katiba ya nchi ijapokuwa ana mamlaka kwa mujibu wa ibara ya 118 (4) inayomruhusu kuteua Jaji Mkuu iwapo itatokea nafasi hiyo kuwa wazi.

Alisema Kaimu Jaji Mkuu ni nafasi ya muda inayoshikiliwa na mtu mwenye sifa za kuwa Jaji Mkuu kabla haijajazwa na Jaji Mkuu kamili, lakini wanashangazwa na kauli aliyoitoa Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi bungeni hivi karibuni kuwa mamlaka ya kukaimu hayana kikomo cha muda.

Pia, alisema wamepanga kuitisha mdahalo wa nchi nzima ambao utashirikisha viongozi wa Serikali, vyama vya siasa, wasomi, wanataaluma na waliokuwa wajumbe wa Tume ya Katiba ili kujua mustakabali wa suala hilo.


MBUNGE Meya Waeleza Walivyozuiwa Kuingia Ikulu...!!!

$
0
0

Mbunge wa Moshi Mjini, Jaffar Michael na Meya wa Mji wa Moshi, Raymond Mboya wameeleza namna walivyozuiwa kuingia Ikulu ya mjini Moshi kuzungumza na Rais John Magufuli.

Viongozi hao ambao wanatokana na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), walikumbana na kadhia hiyo saa 6:00 mchana wakati wakiwa katika foleni ya ukaguzi wa maofisa usalama.

Mbunge Michael alisema aliamriwa kuondoka akiwa katika foleni Ikulu, lakini akasema awali alijulishwa na Meya Mboya kuwa walihitajika katika kikao hicho.

“Ni kweli nikiwa kwenye foleni alikuja ofisa usalama mmoja akaniambia kistaarabu tu kuwa mimi sikuwa natakiwa nilijaribu kumwambia mimi ni Mbunge lakini akasisitiza siruhusiwi,” alisema Mbunge huyo.

Mstahiki Meya Mboya alisema alijulishwa na viongozi wa halmashauri na ofisi ya mkuu wa mkoa kuwa wangehitajika.

“Niliambiwa Mkurugenzi wangu alifanya mawasiliano na Ras (Katibu Tawala wa mkoa) na wote wakaona ipo haja ya sisi kama wenye mji kuwapo lakini ndio hivyo tulizuiwa,” alisema.


BAADA ya Kuichapa Yanga Kimoja cha Uchungu..Mbao Waitia Presha Simba Sc..!!!

$
0
0

Simba italazimika kukaza msuli ili kupata nafasi ya kushiriki mashindano ya kimataifa mwakani baada ya Mbao FC kuitoa Yanga kwa kuifunga bao 1-0 katika mchezo mkali wa nusu fainali uliofanyika kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

Ushindi wa Mbao, umeivua Yanga ubingwa wa mashindano hayo na sasa kombe linabakia kumpata bingwa mpya iwe Mbao ama Simba katika mechi ya fainali itakayopigwa mwishoni mwa mwezi huu baada ya kumalizika kwa mechi za Ligi Kuu. Simba iliingia fainali baada ya kuitoa Azam kwa bao 1-0.

Ushindi wa Mbao ni kama umevuruga mipango ya Simba na kuamsha upya presha yao ya kusaka tiketi ya kuiwakilisha nchi kwenye mashindano ya kimataifa.

Hali hiyo iko vipi, Simba ilikuwa ikitarajia mteremko wa Yanga ambayo ina nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa wa Tanzania Bara, kwani hata kama ingeifunga katika fainali ya FA na huku imetwaa ubingwa wa Bara, ni wazi Simba ingepanda ndege kuwakilisha Kombe la Shirikisho.

Simba sasa wanatakiwa kutumia nguvu zao wenyewe kusaka tiketi hiyo mwakani kwa kuhakikisha wanaifunga Mbao FC kwenye mchezo wa fainali.

Ikiwa hali haitakuwa hivyo, salama ya Simba ni kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu na kukata tiketi ya Ligi ya Mabingwa Afrika na kuacha Mbao ambayo ishinde ama ifungwe na Simba, itacheza Kombe la Shirikisho kwa mara ya kwanza.

Hata hivyo, Simba inaweza vilevile kukosa yote kwani, pamoja na kujipa matumaini makubwa, inaweza isitwae ubingwa wa Ligi Kuu na pia ikapoteza mchezo wake wa fainali na Mbao na kuwaacha wauza mbao hao wakiweka rekodi ya kuingia Ligi Kuu na moja kwa moja kuiwakilisha Tanzania kimataifa.

Dk Shein Alivyowajibu Waliosusia Fomu CCM

$
0
0

Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar), Dk Ali Mohamed Shein amewaambia vijana na makada  waliosusia kuchukua fomu za kugombea nafasi mbalimbali ndani ya chama hicho kuwa, ni aibu kutoa kauli ya namna hiyo kwa nchi yao.

Kauli hiyo ya Dk Shein imefuatia ile ya Katibu wa CCM Mkoa wa Kusini Unguja, Sauda Mbamba aliyesoma taarifa ya mkoa huo mbele ya Dk Shein katika hafla maalumu ya kukabidhi vifaa vya michezo kwa vijana wa Jimbo la Uzini akisema vijana wengi hawachukui fomu hizo.

Ikiwa ni kama majibu kwa vijana hao, Dk Shein amesema suala la msingi ni kuwa na uzalendo ambao ndiyo mwongozo sahihi katika kulinda heshima na nidhamu ya mtu kwenye jamii na Taifa kwa ujumla.

“Kilio kikubwa cha vijana hao inawezekana ikawa ni suala la ajira, lakini suala hilo ni gumu kwani haiwezekani kila mtu kuajiriwa na Serikali kama wengi wanavyotaka,” amesema.

Makamu huyo wa mwenyekiti wa CCM amesisitiza ajira ni changamoto kubwa kutokana na kuwa kwa sasa idadi ya watu visiwani humo ni kubwa hali inayosababishwa na Wazanzibari kuzaliana kwa wingi ikilinganishwa na nchi nyingine.

“Hivi sasa Zanzibar tumeongezeka sana na hili linachangiwa na sisi wenyewe kwa kuzaa sana, hivyo ni vigumu kila mmoja kupata ajira serikalini kwa kuwa utaratibu wa ajira hauko hivyo,” amesema.

Awali, Sauda alimwambia Dk Dhein kuwa pamoja na chama kutangaza uchukuaji wa fomu za uongozi, bado zimedoda matawini jambo linalohitaji nguvu ya pamoja ya viongozi wakuu kuwashawishi ili wazichukue.
Viewing all 104793 articles
Browse latest View live




Latest Images