Kutokana na trend ya maendeleo ya chama ya siku za hivi karibuni, kuanzia kwenye uchaguzi wa madiwani, nashawishika kwamba huu ni wakati mzuri sasa wa Mbowe kuondoka. Ni dhahiri kwamba Mbowe ameshindwa kukiongoza chama au anazeeka kama mwenzake Lipumba kiasi cha kukifanya chama kianze kupoteza mwelekeo na watu wengi kuanza kurudisha imani kwa CCM. Sikutegemea kabisa kwamba Kalenga tungeshindwa vibaya kiasi hiki, despite resources tulizotumia kwenye kampeni. Na kwa matokeo haya ya Kalenga, ni dhahiri kule Chalinze hata kura 5000 hatutafikisha.
Hata NCCR na CUF walianza kuporomoka polepole hivi hivi na mwisho wa siku wakapotea kabisa. Naanza kuona dalili za CHADEMA kupoteza mwelekeo siku za hivi karibuni. Chini ya utawala wa Mbowe naona hatuwezi kuwa na jipya kwa sasa kama chama. Amefanya kazi kubwa na nzuri sana ya kukiwezesha CHADEMA kukuwa na kufikia kuwa chama kikuu cha upinzani, lakini kwa sasa mbinu zake zimeexpire! Matumizi makubwa ya fedha za chama yasiyokuwa na matunda mazuri kwa kweli yafikie mwisho.
Tunataka kuona returns za kile tunachospend. Naamini Mbowe atajitathimini na kuamua kwa nia njema kabisa kutogombea katika kinyang'anyiro cha mwenyekiti wa chama kwenye uchaguzi wa chama ujao.
By Lokolo From JF