Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all articles
Browse latest Browse all 109475

KENYA AIRWAYS WAMENUNUA DREAMLINER 6, ATC WANAKODI KANDEGE KA MOJA KA KWENDA MIKOANI KWA MBWEMBWE

$
0
0
Ndugu zanguni,

Jana wenzetu wakenya wameshuhudia historia mpya katika sekta ya biashara ya anga nchini mwao pale Rais wao alipozindua ramsi ndege ya Boeing 787 DREAMLINER. Ndege hii ni moja kati ya ndege sita ambazo wameagiza kutoka marekani. Na sasa jumla wana ndege kubwa 45.

Wakati huo huo, Air Tanzania wamekuja kwa mbwembwe na matangazo kibao kuwa wamekodi ka ndege ka abiria hamsini ka kwenda mikoani.

Tuweke siasa pembeni tuongelee uhalisia, ni kwa nini ATC wanashindwa hata kuungana ubia na mashirika makubwa ili na sisi tuonekane? Ni aibu kuona tundege twetu hatuwezi hata kwenda Zimbabwe tu. 

Hawa wenzetu hawanunui bali wanakopa, kwa nini na sisi tusikope? au hatukopesheki? hata used? 

BA wamekatisha safari za moja kwa moja Dar hivyo KQ na Swis Air ndio wamechukua soko ambalo kama tungekuwa na uwezo hilo lingekuwa soko letu kubwa. 

Inawezaje Precision air iwe na ndege nyingi kuliko ATC ya serikali? Watalii wote wanaokuja nyumbani wanapanda ndege za kuunga unga tu wakati kama tukiamua tuna uwezo wa kuwa na direct flights from US na Europe kuja home.

Kama mjuavyo, kwa sasa tumekuwa tunapendwa na kila mtu kwa sababu tuna gesi ya kumwaga, hivyo inabidi tutumie mwanya huu kuongea na hao marafiki wa sasa kutusaida na sisi tuwe na mapipa makubwa ya kwenda nje ya nchi sio hutu tu debe twa kwenda mwanza tu. Tuwaombe watukodishe kama hawataki kutuuzia. Hata tukiwa na jumbo mbili tu za kwenda masafa marefu tutakuwa tumemaliza kila kitu

Wivu sina, ila karoho kanauma sana...

Viewing all articles
Browse latest Browse all 109475

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>