Kama mjuavyo, majirani zetu wanasumbuliwa na magaidi wa alshabaab ambao wako bize kulipua mabomu kila sehemu Kenya na kuifanya nchi hiyo kutokuwa salama tena.
Inasikitisha sana, lakini nadhani ni wakati sasa tutumie mwanya huu kudumisha amani yetu na kujitangaza kwa nguvu zote kwenye sekta ya utalii.
Tanzania ina vivutio vingi na vikubwa vya utalii zaidi ya Kenya, na kwa sasa nchi zote za magharibi zinawaonya raia wake wasiende Kenya. Kipindi cha holidays kwa nchi za magharibi ni kuanzia july, badala ya kwenda Kenya tuwavute kwetu.
Lakini serikali ibabidi idhibiti vidumu vya tindikali kule kwa wazee wa urojo...