Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all articles
Browse latest Browse all 109519

Chaz Baba:Simwelewi Sajent Amegoma Kunipa Mwanangu Niliye zaa Naye

$
0
0
Na Musa Mateja
PREZIDAA wa Bendi ya Mashujaa Musica, Charles Gabriel ‘Chaz Baba’ amefunguka kuwa anatamani kuishi na mwanaye aliyezaa na mwigizaji Husna Idd ‘Sajent’ lakini mzazi mwenziye huyo amekuwa akimgomea.

Akizungumza na paparazi wetu, Chaz Baba alisema kabla hajaoa alikuwa akimg’ang’ania akae naye lakini alipooa, amegeuka na kukataa katakata.

“Kiukweli simuelewi kabisa Sajent maana katika hali na akili ya kawaida tu, sijaona mantiki ya kumkatalia mtoto wangu labda angeniambia kama mwanangu amekataa mwenyewe hapo kidogo nisingekuwa na swali,” alisema Chaz Baba.
Chaz Baba ambaye alikuwa akibanjuka na Sajent miaka ya nyuma, kwa sasa ni mume halali wa ndoa na bi dada anayefahamika kwa jina la Rehema.
GPL

Viewing all articles
Browse latest Browse all 109519

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>