Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all articles
Browse latest Browse all 109519

Hongera Mheshimiwa James Mbatia kwa kuwafundisha CHADEMA jinsi ya Kuandika Maoni ya Upinzani

$
0
0

Wadau, 

Natumai kuwa wengi wetu tumemsikiliza Mheshimiwa James Mbatia, Mwenyekiti wa NCCR MAGEUZI na Waziri Kivuli wa Wizara ya Fedha wakati akitoa maoni ya Kambi ya Upinzani kuhusu Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Fedha kwa mwaka 2014/2015. 

Kwa wale waliosikiliza, kusoma au kuona maoni hayo ya Upinzani, watakubaliana nami kuwa yapo tofauti kabisa na maoni tuliyokuwa tumezoea kuyasikia kutoka Kambi ya Upinzani wakati huo ikiwa na wabunge wa CHADEMA pekee.

Hakika Mbatia amejitahidi kujenga hoja na kutoa ushauri stahiki kwa mustakabali mwema wa nchi hii.

Wengi walitegemea kuwa Mbatia atajikita kueleza au kulalamika juu ya masuala mbalimbali kama vile ESCROW Acount au hili sakata la UDA. Mbatia hakugusia kabisa masuala hayo kwa vile hayana tija katika ukuaji uchumi wa nchi yetu.

Pia Mbatia anajua kuwa kama kulikuwa na udhaifu wowote kwa siku za nyuma, hawezi kuwabebesha mzigo huo hawa vijana wachapakazi waliochaguliwa kuongoza wizara hiyo. 

Alichokifanya Mbatia ni kuwaonesha njia na si kuwakatisha tamaa kama walivyozoea kufanya CHADEMA.

Hebu tujiulize, hivi ile taarifa ya John Mnyika kwenye Wizara ya Nishati na madini ina tija gani kwa taifa?

Katumia dakika 25 kusoma introduction tu wakati James Mbatia katumia chini ya dakika 30 kuwasilisha maoni yake. 

Hakika Mbatia kawaonesha njia CHADEMA na hii inadhihirisha kuwa uwepo wake kwenye kambi ya upinzani utasaidia kuokoa Jahazi la CHADEMA lisizame japo uwezo huo najua hana. 

Atakachokifanya Mbatia ni kuokoa jahazi lake tu. kwani mpaka sasa Watanzania wenye akili timamu wanajua kuwa ndani ya CHADEMA hakuna upinzani wa dhati bali wamejaa walalamikaji na wanung'unikaji.

CHADEMA, alichokifanya Mbatia leo iwe fundisho kwenu katika kujitathmini upya juu ya mustakabali wenu kisiasa.

Mawaziri vivuli karibu wote ambao si wabunge wa CHADEMA wameandaa taarifa nzuri sana na zenye tija kwa taifa hii tofauti na za wabunge wa CHADEMA.

Huwezi kulinganisha taarifa za Sugu, Lema, Wenje, Msigwa na Mnyika na zile zilizoandaliwa na akina Mkosamali, Kafulila, Mbatia na Machali. 

Hakika kuna utofauti mkubwa na Watanzania wenye akili zao hawahitaji mikutano ya hadhara kupima juu ya jambo hilo. 

Nawashauri CHADEMA. Kujifunza si ujinga. Japo mmekaa miaka 3 kama kambi rasmi ya upinzani, mjifunze hiki kipindi cha miezi miwili mlichofanya kazi pamoja na akina Mbatia. Mnapojifunza hakika mnaangamia.

Najua kuna mizengwe inasukwa na baadhi yenu kwa kutaka kuwaandalia kashfa nzito akina Mbatia ili hatimaye kambi yenu ivunjike. Huo si ushindani wa kisiasa. Anayejua anajua tu. cha kufanya ni wewe kujifunza kutoka kwake

Nawasilisha.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 109519

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>