Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all articles
Browse latest Browse all 109519

Huu Ndio Mshahara Ambao Maximo Anataka Ili Kuja Kuifundisha Yanga

$
0
0
YANGA chini ya Mwenyekiti wake, Yusuf Manji inataka kuonyesha kwamba ina nguvu na jeuri ya kufanya chochote kile inachotaka kwa vitendo ndani na nje ya ardhi ya Tanzania.

Mbrazil Marcio Maximo, amewaambia kwamba wakimpa mkataba watafurahia wenyewe lakini akawapa na masharti matatu ambayo yanahitaji kuvunja benki ila wametikisa kichwa wakamwambia haina noma.

Manji amewaambia Yanga kwamba wako kwenye hatua nzuri ya mazungumzo na bosi huyo wa zamani wa Stars na atatua nchini kwavile ana hadhi ya Yanga.

Ujio wa kocha huyo unaonekana kuwashtua mastaa kadhaa wa Yanga hususani wazalendo kwani kocha huyo huwa hapendi masihara na ni mwepesi kufanya uamuzi mgumu kama kumsweka mtu benchi msimu mzima.

Habari za ndani ya Yanga zinasema kwamba kwanza, kocha huyo amewaambia viongozi anataka kuja na msaidizi wake ambaye ni mtaalam wa viungo lakini mabosi wa timu hiyo hajakubaliana na hilo wakitaka afanye kazi na mzalendo Boniface Mkwasa.

Kocha huyo aliwahi kufanya hivyo wakati akitua nchini miaka kadhaa iliyopita wakati aloipokabidhiwa Taifa Stars. Alikuja nchini na Itamar Amorim ambaye alikuwa mtalaam wa viungo kwa kikosi hicho.

Taarifa kutoka ndani ya kamati ambayo ipo chini ya Manji ikishugulikia ujio wa kocha huyo zinasema kwamba Maximo pia amependekeza msaidizi wake huyo alipwe mshahara wa Dola 4,000 ( Sh6.4milioni) kwa mwezi jambo ambalo viongozi hao wanadai utakuwa mzigo mkubwa Yanga.

Sharti jingine la kocha huyo ni kutaka alipwe mshahara wa dola 15000 (Sh24milioni) ambalo bado Yanga wanalifanyia kazi na unaeza kupungua kidogo. Lakini pia anataka apewe nyumba ya gharama kama ambayo alikuwa akilipiwa na serikali wakati akiifundisha Stars ambapo kidogo hapo Yanga wameona wanaweza kutafuta kutokana kuwa na chaguo la nyumba nyingi nzuri.

Lakini Maximo pia ametaka apewe gari nzuri ya kisasa atakayoitumia katika kazi zake ambapo tayari Yanga wamemwambia watampa Prado la kisasa.

“Msaidizi wake atakuwa na kazi ya kushughulikia mazoezi ya viungo ni jambo zuri lakini ni gharama sana ukijumlisha na gharama zake ambazo tutampa kocha mkuu, tunataka kumwambia amuache kwanza aje afanye kazi na Mkwasa,”alisema bosi huyo..

Viewing all articles
Browse latest Browse all 109519

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>