Watu wengi wanachukulia single momz kama hawana umuhimu tena na hawafai katika mahusiano. Siku hizi wanaume wengi ambao hawajakuwa na watoto utasikia wakisema "Mimi mwanamke wenye mtoto simtaki amechoka na amekongoroka kabisa huyo"
Kumbuka hapa kuna wanawake wengine hata ukikutana nae na asipokuambia ana mtoto huwezi jua, anajipenda na ni mrembo wa kuvutia na mwenye maendeleo.
Wanaume wengi sana wanaona hana thamani, na wengine kusema ni wameshindikana walikotoka yaani na jaamaa aliyezaa nae.Tukumbuke NOT EVERYMAN MEANT TO BE A DADY, kuna wengine ni waharibifu tu, pengine pia tofauti za maisha zinazotokea zinapelekea yote hayo kutokea, Watu hawaelewi...
Single moms haimaanishi hawatakiwi kuwa na mahusano mengine mapya labda na mwanaume ambaye hana mtoto, wengi hudhani ukijitumbukiza hapo basi utalea mtoto.
Jamani kuna watu wanauwezo wa kutake care ya watoto wao bila msaada, jiulize kabla yako nani alikuwa anamsaidia kama sie mwenyewe. Ni faraja na upendo tu anahitaji kutoka sehemu nyingne.
Hawa watu haimaanishi waolewe au wawe na mahusiano na wanaume ambao nao wanawatoto...eti sababu wasaidane kulea... Tena na zile familia zikisikia kijana anasema "nina mwanamke ila ana mtoto" moto unawaka, jamani jamani? Huu si ubaguzi lakini?
Mwenye mawazo hayo wewe ni katili na mbinafsi kabisa. Na ndo maana inafikia hatua wanaume mnafichwa mnakuja kutambua kwamba ana mtoto imepita hata miaka 10, halafu unalaumu oooh hakuniambia. Hakukuambia kwasababu anajua mtazamo wenu kwao...
Mimi naomba tu niwaambie ndugu Kaka zangu, wadogo zangu, Mwanamke aliyezaa ni sawa na wengine tu, tena bora yeye kazaaa anajua ana kizazi, kuliko hao wasiozaa na wanaokesha kila siku kutafuta watoto kwa waganga..
Mimi mwenyewe ni mfano mzuri, nimepata unyanyasaji sana na wanaume, pale nilipokuwa nawaambia nina mtoto, wengine walishia kimya kimya, wakidai eti tuna kawaida ya kupasha kiporo na mzazi mwenza HIYO NI UONGO NA FIKRA MBOVU ZA WATU
Na kamwe sikuweza kuficha kama sina mtoto kwasababu najua nini maana ya mtoto. Mtoto ni zaidi ya thamani ya vitu ulivyonavyo ndani...
Tena wanawake ambao mmekutana na haya wala msifiche ukweli, Mwanaume akikimbia ujue mungu kakuepushia jambo.
WANAUME HEBU TOENI NA MBADILIKE NA HIZO IMANI AMBAZO SIO...
Swali lolote linakaribishwa... Asanteni