Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all articles
Browse latest Browse all 109450

Arnold Kayanda 'Siku Hizi Vipindi vya Jioni Redioni Vimepungua Utamu, Huwezi Linganisha Tulivyokuwa Mimi na G-Habash

$
0
0
"Huyu ni ndugu yangu Captain Gardner G Habash. Juzi kati tulikutana kwenye radio mpya mjini , walituomba maoni mawili matatu kuboresha. Nimemkumbuka! Gardner nilipojiunga Clouds FM yeye alishakuwa maarufu sana. Tofauti na watu maarufu wa wakati huo, alinipa nafasi sana na hata akafikia kuwa ananifanya Co-captain mara moja moja. Siku moja aliniambia, "nataka kuondoka nitakuachia 'Kipindi'". Alipoondoka hawakunipa 'kipindi'. Baada ya miezi kadhaa waliniita 'niokoe Jahazi'. Watu wanasema nilivaa vizuri viatu vya G. Habash (Sidhani kama nilimfikia hata nusu). Ingawa kila mtu ana mtazamo wake lakini pengine utaniunga mkono kuwa siku hizi vipindi vingi vya jioni vimepungua utamu. Hakuna tena uchambuzi wa kina wa masuala nyeti unaofanyika kiburudani, hakuna tena Maelezo juu ya muziki yaliyokuwa matamu kuliko muziki wenyewe unaozungumziwa. I publicly #ThankYou Captain Gardner G Habash" 
Anold Kayanda

Viewing all articles
Browse latest Browse all 109450

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>