Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all articles
Browse latest Browse all 109623

Walio Muua Sista wa Kanisa la Roma Walipora Kiasi Hichi cha Fedha..Soma Mchezo Mzima Ulivyokuwa

$
0
0
Polisi Kanda Maalumu Dar es Salaam imesema majambazi waliohusika na mauaji ya Sista wa Kanisa Katoliki, Clencensia Kapuli wamepora kiasi cha Sh20 milioni na nyaraka mbalimbali.

Tukio la kupigwa risasi sista huyo lilitokea juzi saa 8 mchana eneo la Riverside Ubungo, Dar es Salaam na dereva , Patrick Mwarabu alikatwa kidole gumba kwa risasi.

Sista Kapuli wa Shirika la Mtakatifu Maria wa Parokia ya Mtakatifu Gaudence Makoka jijini hapa alikuwa Mhasibu wa Parokia hiyo ambayo inamiliki Shule ya Sekondari Mwenyeheri Anwarite na Chuo cha Ufundi Stadi Makoka.

Kamanda wa Kanda hiyo alisema Kamishna Suleiman Kova alisema jeshi hilo limetangaza msako wa kuwatafuta na kuwakamata wote waliohusika na tukio hilo.

Kova alisema marehemu akiwa ameongozana na wenzake ambaye ni Sista Brigita Mbaga na dereva aliyekuwa akiendesha gari aina ya Toyota Hilux walikuwa wakitoka Benki ya CRDB, Tawi la Mlimani City kuchukua fedha.

Alisema walipofika eneo la Ubungo Kibangu ili kulipa deni la chakula katika duka la Thomas Francis ndipo walitokea majambazi wawili wakiwa na pikipiki ambayo haikusomeka namba.

Alisema kati ya majambazi hao mmoja alikuwa na bunduki aina ya SMG wakampiga risasi ya kidole gumba cha mkono wa kulia dereva wa gari hilo kisha sista huyo alipigwa risasi ya kifua na kuporwa fedha hizo Sh20 milioni.

Kova alisema jeshi hilo limebaini kuwa matukio ya ujambazi hasa unaohusiana na wananchi kuporwa kiasi kikubwa cha fedha unaanzia benki na huwafuatilia wanapoingia na kutoka.

“Ni muhimu kwa benki kuwahimiza wateja wao kutochukua kiasi kikubwa cha pesa kiholela kwani ni rahisi kuporwa na watu wasio na nia njema,” alisema Kova.

Alisema benki ziwahimize wateja wao kutumia njia mbadala za kusafirisha pesa nyingi kama vile kwa hundi, kufanya miamala bila kadi na matumizi ya kadi za ATM.

Kova alizishauri benki nchini zianzishe vitengo vya ushauri kwa wateja ili wanapokuwa na fedha nyingi wasindikizwe na polisi.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 109623