
FikraPevu ilikuwapo wakati Maswi akitumia maneno makali kwa kuyarudia, akikejeli nyaraka zinazotajwa kuwa ni ushahidi wa jinsi IPTL ilivyouza hisa zake na fedha kutolewa kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT) katika akaunti maalumu ya pamoja (Escrow), akisema nyaraka hizo ni karatasi za kufungia vitumbua zinazosambazwa na wabunge hao aliowaita “washenzi”.