Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all articles
Browse latest Browse all 109482

Tundu Lissu: Wachungaji, Maaskofu na Masheikh ni Wala Rushwa.

$
0
0
Wakati akichangia katika mdahalo wa ‘Nani anataka kuwazuia Watanzania kupata katiba mpya, jijini Dar es Salaam na kurushwa na kituo cha ITV, Gazeti la Nipashe limemnukuu Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu, akisema baadhi ya Maaskofu na Masheik nchini ni viongozi wanaopewa chakula, vinywaji na pesa kama rushwa. 

Lissu alinukuliwa akisema, “Akina Sheikh Jongo (Thabit Norman) na Jongo mwenzake (Hamid Masoud), Askofu Muhagachi (Amos), Askofu Mtetemela (Donald) na Mchungaji Mgimwa wapo 166 wote hawa ni wana CCM na wameteuliwa na Mwenyekiti wa CCM, wanaitwa kwa Waziri Mkuu, kwa mawaziri wanapewa hela, wanapewa chakula, vinywaji maana yake ni wala rushwa …”.

Ukiyasikiliza na kusoma madai ya Tundu Lissu bila kuyachambua kimantiki unaweza ukadhani ni mambo ya kawaida kisiasa lakini kiuhalisia ni madai ambayo yanagusa taasisi na viongozi ambao uongozi wao unagusa misingi ya kiroho kwa wananchi ambayo hukumu yake haifanywi na binadamu bali na Mwenyezi Mungu. Viongozi wa Taasisi za kiroho ni wajumbe wa Mwenyezi Mungu.

Heshima na utu wa taasisi za kidini nchini ambazo zilipeleka viongozi wake kwenye Bunge la Katiba ambao leo wanaodaiwa na Tundu Lissu kuwa ni wala rushwa, lazima ziheshimiwe kwa njia ya kumtaka Tundu Lissu atoe pia ushahidi wa madai yake.

Kwa lugha nyingine, Tundu Lissu anadai taasisi za kidini (kiroho) zimejaa wala rushwa!. Really? 

I believe these are extremely serious allegations and needs solid evidence. Madai ya Tundu Lissu hayawezi yakapita bila kupata majibu ya uhakika.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 109482

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>