Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all articles
Browse latest Browse all 109519

Wema Sepetu Aanika Ugomvi wake na Mama Yake Mzazi, Kisa Kumbe ni Diamond

$
0
0
STAA wa filamu Bongo, Wema Sepetu ametaja sababu zinazomfanya aingie katika mgogoro na mama yake mzazi, Miriam Sepetu kuwa ni suala la uchumba wake na Nasibu Abdul ‘Diamond’ ambao alikuwa akiupinga mara kwa mara.

Akipiga stori na mapaparazi, Wema alisema kwa muda mrefu alikuwa akitofautiana kauli na mama yake katika suala zima la uhusiano wake na Diamond lakini anamshukuru Mungu amemuelewa na sasa kila kitu kinakwenda sawa.

“Mama nilikuwa nikimsihi sana juu ya uchumba wangu na Diamond lakini sasa tumefikia hatua nzuri namshukuru Mungu amekubali, maana siku hizi nikionana naye ananiuliza vipi mwenzako mzima, anaendeleaje, wakati mwanzoni haikuwa hivyo,” alisema Wema huku akiahidi kumkutanisha Diamond na mama yake. Imeandikwa na Mayasa Mariwata na Shani Ramadhani

Viewing all articles
Browse latest Browse all 109519

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>