Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all articles
Browse latest Browse all 109519

Niko Njia Panda Nikubali Kuolewa na EX Boy Au Nimsubiri Niliyenae sasa Japo Bado Hajajipanga..Ushauri Please

$
0
0
Mimi ni msichana mwenye umri wa miaka 23.niliwahi kuwa na mpenzi wangu wa kwanza tangu mwaka 2010 ambae ndie aliyekuwa wa kwanza kimapendi kwa upande wangu tulikuwa tunapendana sana,mimi binafsi nilikuwa nampenda sana sababu sijawahi mapenzi kabla yake.nikawa nawafahamu baadhi ya ndugu zake na pia tuliahidiana kuoana na mambo mengi tu mazuri sasa ilipofika mwezi wa  kwanza mwaka huu 2014 kutakorofishana,nikajaribu kumbembeleza bila mafanikio  basi ikawa kila mtu na ishu zake.sasa baada miezi kadhaa kupita mimi binafsi nikapata mpenzi mwingine sijajua kwa upande wake ilikuwaje,nikawa na mahusiano mapya na mpenzi wangu huyo mpya,akanitambulisha marafiki zake wadogo zake na tumeahidana kuoana ananipenda sana kiukweli.sasa juzi yule mpenzi wangu wa kwanza aliniambia anaomba tuonane nikamkubalia baada ya kuonana akaniambia tuachane na yote yaliyopita kwani kwa mda wote huo alikuwa anahangaika tu kila msichana aliyempata alikuwa anamzingua amenikumbuka sana hivyo anaomba turudiane kwani kila akikaa moyo wake unahisi amenikosea na anahitaji msamaha wangu ili mambo yake yakae vizuri na msamaha wangu ni kumkubalia apeleke barua kwetu anioe kabisa.sasa tatizo ni huyu mpenzi wangu wa sasa ameniahidi kunioa ila kiupande wake maisha bado kabisa hayajakaa sawa na sijui ni lini yakataa vizuri ila mwenyewe ameniambia nimvumilie tu ipo siku sasa najiuliza nilini?.yani nina wakati mgumu sababu yule mvulana wangu wa kwanza ana historia kwenye maisha yangu ya mapenzi sababu ndie alienianza kimapenzi.sasa naombeni ushauri wenu nifanye nini?

Viewing all articles
Browse latest Browse all 109519

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>