Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all articles
Browse latest Browse all 109439

OKWI "NIPANGENI MECHI YA SIMBA NA YANGA NIWAONESHE SIMBA MIMI NI NANI"

$
0
0
 Uwanja wa Bora uliopo Kijitonyama jana ‘ulifurika’ mashabiki wa Yanga waliokuwa na shauku ya kumwona mshambuliaji wao mpya Emmanuel Okwi akifanya mazoezi na timu hiyo.

Okwi alitua nchini juzi Alhamisi tayari kuitumikia klabu hiyo ya Mtaa wa Twiga na Jangwani baada ya kutokea sintofahamu kuhusu uhamisho wake wa kutoka SC Villa kuja Yanga.

Si bajaji, pikipiki achilia mbali magari yaliyofurika kwenye uwanja huo huku Okwi mwenyewe akisema, “Nimefurahi sana na mapokezi niliyopewa na viongozi na mashabiki wa Yanga, nitafurahi kama nitacheza mechi ya kesho,” alisema Okwi ambaye jana alifanya mazoezi kwa mara ya kwanza na Yanga.

Akisisitiza umuhimu wa yeye kucheza alisema, “Mrisho Ngassa nimecheza naye Simba, Hamis Kiiza tunacheza naye timu ya taifa (Uganda), hakuna wasiwasi, mimi nikipangwa nao tutacheza kwa uelewano sana pale mbele  na nitafunga.”

Alisema kwa jumla anaijua Yanga vizuri na anajua uchezaji wa wachezaji wake wengi, hivyo anaweza kucheza vizuri katika mfumo wa timu hiyo.

“Unaweza kuitwa timu ya taifa, siku mbili kabla ya mechi na wakati mwingine unakuta wachezaji wengi hujawahi kucheza nao kabisa, lakini mnafanya mazoezi siku moja mnaelewana na mnacheza vizuri,” alisema Okwi.

Kwa upande wa kocha wa timu hiyo Ernie Brandts alisema Okwi ni mwepesi na anakasi na anajua kutengeneza nafasi za kufunga mabao na atampanga katika mchezo wa leo wa Nani Mtani Jembe dhidi ya mahasimu wao.

Jezi za Yanga zenye jina la Okwi zimetapakaa na zimekuwa zikigombewa kama njugu na mashabiki wa klabu hiyo ambayo mara zote walisikika wakiimba Okwi... Okwi...

Na kabla ya kuanza mazoezi, Brandts alimtambulisha, Okwi kwa wachezaji wenzake na benchi la ufundi.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 109439

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>