1.Ukiona umejipiga ‘selfie’ au hata picha yoyote ukaiweka kwenye facebook na
kutag watu mia ukapata ‘likes’ mbili tu ni dalili ya wazi kuwa we mbayaaa.
2.Ukiona wakaka wanapenda sana kampani yako lakini kila mara wanakuuliza ushauri juu ya kuwapata wadada wengine , ujue wewe ni mbaya, maana wanajiona kama vile wanaongea na mwanaume mwenzao
3.Ukiwa na wasichana wenzio halafu
mnataka kupiga picha ya pamoja ukona wanang’ang’ania wewe ndio uwapige
picha ni dalili ya wazi hawataki uwaharibie picha yao kwa sura yako mbaya.
4.Jina lako instagram na facebook pia ni dalili tosha kuwa na wewe unajijua ni mbaya, majina kama sexydiva, sweetylicious, cutebaby na kadhalika, ni nja ya kisaikolojia ya wabaya kutaka kuonekana wazuri.
5.Ukiona utafiti huu umekuudhi na una ulaani hiyo ndio dalili ya ukweli kuwa wewe mbayaaaaa