Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all articles
Browse latest Browse all 109475

Rais Kikwete Iga Mfano wa Uhuru Kenyata Mapambano Dhidi ya Madawa ya Kulevya

$
0
0
Hakika raisi wa kenya ni mfano wa kuigwa:
Ni raisi ambaye awali sikufurahishwa na siasa zake lakini baada ya kuanza kuitumikia kenya anaonekana kuwa ni kiongozi makini na mwenye uzalendo wa kweli kwa taifa lake.
-hii ni kutokana na yeye kumwondoa mkuu wa idara ya usalama wa taifa wa nchi hiyo,ambapo licha ya kutambua umuhimu wake na uwezo wake lakini kutokana na matukio ya milipuko na mabomu ambavyo vililitikisa taifa hilo akaamua kumwajibisha mkuu huyo wa usalama bila kuangalia maslahi binafsi na kubebana kusiko na msingi wowote.
*=kubwa kuliko yote ni kitendo cha raisi huyu kuizamisha meli iliyokuwa imebeba madawa ya kulevya na kukamatwa bahari ya hindi ukanda wa mombasa.
Haya madawa yanakadiriwa kuwa na thamani ya trilioni 1.6 za kitanzania.
Huu ni ushujaa na ni ukomavu kama raisi kulitangazia taifa kuwa lazima hayo madawa yaharibiwe na meli husika izamishwe.
**jakaya kikwete iga mfano wa kiongozi huyu mwenzio.
-matukio kama haya yamekuwa yakijitokeza nchini lakini hatuoni hatua kali zikichuliwa.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 109475

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>