Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all articles
Browse latest Browse all 109446

AJALI: Mwanamke Aanguka Kwenye Bodaboda, Akanyagwa na Lori na Kufariki Dunia Papo Hapo

$
0
0

Mwanamke anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 25 amekufa papo hapo baada ya kudondoka kwenye pikipiki aliyokuwa amepanda na kisha kukanyagwa na gari.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camillius Wambura amesema kuwa ajali hiyo ilitokea jana  mchana katika barabara ya Bagamoyo eneo la Tangibovu ambapo gari likiendeshwa na dereva asiyefahamika akitoka kwa Alysykes kuingia barabara ya Bagamoyo, aliigonga pikipiki namba T 505 CTJ Fekon ikiendeshwa na dereva asiyefahamika.
Alisema pikipiki hiyo iliyokuwa ikitokea Mbezi Makonde kwenda Mwenge ilikuwa imempakia mwanamke huyo ambaye baada ya pikipiki kugongwa alianguka chini na kisha kukanyagwa na lori namba T 277 CIL aina ya Tata likiwa na trela namba T 339 CYB lililokuwa katika uelekeo mmoja na pikipiki.

Kamanda alisema mwanamke huyo alikufa papo hapo na mwili wake umehifadhiwa katika Hospitali ya Mwananyamala huku Polisi wakiendelea kuwasaka madereva waliohusika katika ajali hiyo.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 109446

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>