Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all articles
Browse latest Browse all 109519

Kajala: Watu Wanaamini Sana Magazeti, Sina Utajiri Huo Wanaousema na Siwezi Kumwajiri Wema Sepetu

$
0
0
Kajala Masanja amedai kuwa maisha yake hayajabadilika sana kama ambavyo magazeti ya udaku yamekuwa yakiandika.

Muigizaji huyo wa filamu alisema kuwa tetesi kuwa ana fedha nyingi kiasi cha kuwa na mpango wa kumwajiri Wema Sepetu ni uzushi mtupu. “Mbona maisha yangu ni ya kawaida sana,” Kajala aliiambia Bongo5.

“Mimi naona nipo vilevile hakuna kubwa sana lililongezeka. Nafanya shughuli zangu tu. Tatizo watu wanaamini sana magazeti. Mimi i sina utajiri huo wanaouzungumzia, Kajala ni yule yule,” alisisitiza.

Hivi karibuni Kajala alizindua filamu yake fupi iitwayo ‘Mbwa Mwitu’.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 109519

Trending Articles