Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all articles
Browse latest Browse all 109519

BREAKING NEWS: ASKARI WATANO WAFARIKI DUNIA

$
0
0
Na: Halima Kiondo

Kwa taarifa zilizotufikia HIVI PUNDE. Askari WATANO wafariki papo hapo baada ya bus aina ya Mohamed Trans, kugongana uso kwa uso na gari ndogo aina ya Toyota Corola iliyokuwa ikitokea Dodoma mjini ambayo lilikuwa na sakari hao kisha kupoteza maisha.

Akizungumza na Radio One, Kamanda wa polisi Mkoani Dodoma, David Misime, amesema kuwa ajali hiyo imetokea majira ya saa 9 usiku kuamkia leo katika kijiji cha Namtumba Mkoani Dodoma na abiria waliokuwemo kwenye Bus hilo hakuna aliyejeruhiwa.

"Hakuna aliyejeruhiwa kutoka kwenye Bus hili, lakini Dereva aliyekuwa anaendesha abiria hao anafahamika kwa jina la Juma Mohamed, amekimbia mpaka sasa haijafahamika yuko wapi, ameongeza kuwa gari ndogo aina ya Toyota Corola imeharibika vibaya na baadhi ya miili ya askari hao imeharibika. " Tumeipeleka miili hiyo hospital kwa ajili ya kuihifahi huku tukisubiri mipango ya mazishi," amesema David.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 109519

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>