Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104809 articles
Browse latest View live

SERIKALI Yadaiwa Bil. 70/-. za Chakula ..!!!

$
0
0

SERIKALI inadaiwa kiasi cha Sh. bilioni 67.7 na wazabuni mbalimbali wanaotoa huduma za chakula, uchapishaji na usambazaji vitabu shuleni, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali(Tamisemi), Seleman Jafo amesema.

Jafo alibainisha jumla ya deni hilo alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Bernadeta Mushashu aliyetaka kujua serikali inadaiwa kiasi gani na kwa miaka ipi na wazabuni hao na ni lini madai yao yatalipwa.

Akijibu swali hilo, Jafo alikiri kuwa wapo wazabuni mbalimbali ambao wanaidai serikali baada ya kuipatia huduma.

“Wapo wazabuni waliotoa huduma za chakula katika shule zenye wanafunzi wenye mahitaji maalum za msingi na shule za bweni za sekondari, na wazabuni waliochapisha na kusambaza vitabu shuleni,” alisema Jafo.

Alifafanua kiasi cha Sh. bilioni 54.8 zinadaiwa na wazabuni waliotoa chakula na pia Sh. bilioni 9.9 ni wazabuni waliotoa huduma ya uchapishaji na kusambaza vitabu vya shule za msingi.

Jafo alisema madeni hayo ni yale yaliyojitokeza kabla ya serikali kuanza kutekeleza sera ya elimu ya msingi bila malipo.

“Kwa kutambua umuhimu wa kuwalipa wazabuni hawa, serikali kupitia Wizara ya Fedha imeshalipa jumla ya Sh. bilioni 13.2 hadi kufikia Mei mwaka 2016,”alisema.

Naibu Waziri huyo alisema wazabuni wengi ambao madai yao hayajalipwa hadi sasa wataendelea kulipwa kwa awamu kadri uwezo wa serikali na upatikanaji wa fedha utakavyokuwa.

Aliwaomba wazabuni hao kuwa wavumilivu kama ambavyo wamekuwa wakifanya wakati serikali ikiendelea kulipa madeni hayo ikiwa ni pamoja na madeni mengine ya ndani.

Akitoa jibu la nyongeza, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji alisema madeni hayo yanahakikiwa na mara baada ya uhakiki serikali hulipa.

Kufuatia kauli hiyo, Naibu Spika, Dk. Tulia Ackson aliagiza madeni yaliyohakikiwa yalipwe haraka ili kuwaondolea usumbufu wabunge ambao wamekuwa wakiandikiwa barua na wazabuni.

UTATA Zaidi Waibuka Baada ya Anayedaiwa Kuwa Jambazi Kuuawa na Polisi Katika Tukio la Kutaka Kupora Milioni 300..!!!

$
0
0

MENGINE mapya yamezidi kuibuka kuhusiana na kuuawa kwa tuhuma za ujambazi mwanafunzi Salum Almas (28) aliyekuwa akisoma stashahada ya Teknolojia ya Mawasiliano (IT) katika Chuo cha Kompyuta (UCC), Chuo Kikuu cha Dar es Salaam-

Baada ya ndugu kudai kuwa siku ya tukio alikuwa na Sh. 30,000 alizotumwa azifikishe nyumbani kwao.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na polisi kuhusiana na tukio hilo, Almasi aliuawa kwa kupigwa risasi katika eneo la Kurasini akituhumiwa kuwa mmoja wa majambazi waliokuwa katika mipango ya kupora zaidi ya Sh. milioni 300 za benki ya CRDB.

Hata hivyo, ndugu zake wamedai kuwa kadri wanavyomfahamu, Salum hakuwahi kujihusisha na vitendo vya aina hiyo na kuomba Serikali ichunguze zaidi kujua ukweli wa kifo chake.

Tukio lililohusisha kuuawa kwake lilitokea Jumapili iliyopita katika eneo la Kurasini, karibu na mahala pa mashine ya kutolea fedha (ATM) ya benki ya CRDB iliyopo jirani na Ofisi ya Uhamiaji.

Mjomba aliyekuwa akiishi na marehemu, Tulleyha Abdulrahman, aliisema kuwa wameshangazwa na madai kuwa kijana huyo alikuwa jambazi na kwamba, wanachoamini ni kuwa polisi walikosea kwa kumdhuru mtu asiyekuwa na hatia.

Alisema anachofahamu ni kwamba siku ya tukio, Salum alikuwa akikatiza maeneo ya benki kuelekea nyumbani kama raia wengine na wala siyo kujihusisha na ujambazi.

“Salum hakuwa kijana wa makundi. Muda mwingi aliutumia kusoma na kuswali. Tunashangaa anaitwa jambazi. Tunamuomba Rais Magufuli aingilie suala hili kwa sababu hiki kilichofanywa na polisi siyo sahihi.

“Wamekatisha uhai wa mtu asiye na hatia. Tunaomba hatua zichukuliwe,” alisema mjomba huyo wa marehemu.

Alisema kinachowaumiza zaidi ni kuona kuwa baada ya tukio hilo, Polisi wametoa kauli zenye utata kwa kudai kuwa marehemu alikuwa katika pikipiki na aliporuka ndipo polisi walipomfyatulia risasi.

Alisema kauli nyingine zilizotolewa ni kwamba wakati wa tukio alikuwa anatembea huku akitangulizwa mbele kama chambo na majambazi wenzake waliokuwa kwenye pikipiki na kwamba, mkanganyiko wa taarifa hiyo ni dalili kwamba kuna utata juu ya kifo cha mwanafunzi huyo na hivyo kuna kila sababu ya kufanyika kwa uchunguzi wa kina.

Mjomba huyo alisema kuwa yeye alielezwa na polisi kwamba Salum alipita kwenye eneo ambalo lilikuwa likishushwa fedha za kuwekwa kwenye ATM ya benki hiyo na alipoambiwa asimame na askari waliokuwapo na kukaidi, ndipo walipoanza kumpiga risasi.

“Kauli nyingine wanasema Salum alipopigwa risasi ya kwanza aliendelea kutembea akapigwa ya pili hakuonyesha dalili ya kuanguka na alipopigwa ya tatu alidondoka chini na kuanza kutambaa kuelekea eneo ambalo alikuwapo polisi aliyekuwa akimfyatulia risasi,” alisema na kuongeza:

“Wanasema Salum ni jambazi na ni sahihi kilichofanywa na polisi kumuua kwa sababu kama siyo jambazi, mbona aliweza kufanya matendo hayo mpaka kutambaa chini kumfuata polisi mwenye silaha akitaka kumpora,” alisema.

Abdulrahman alisema polisi waliwaeleza kuwa Salum alikuwa na majambazi wenzake waliokuwa kwenye pikipiki lakini jeshi hilo halijaonyesha dalili za kuwatafuta hao wenzake na hiyo ni ishara nyingine juu ya imani yao kuwa kijana wao hakuwa na hatia bali ameuawa kimakosa.

Pia alisema polisi hao waliwaeleza kuwa majambazi walikuwa wamevaa makoti meusi ingawa ndugu yao, siku hiyo alikuwa amevaa kanzu na hata picha zilizopigwa eneo la tukio zilithibitisha kuwa alivaa kanzu.

FEDHA 30,000/-
Abdulrahman alisema familia yake inaishi Kurasini Shimo la Udongo ambako ili mtu afike kituo cha daladala cha JKT, ni lazima apite eneo ilipo ATM ya CRDB.
Alisema kabla ya mauaji hayo majira ya saa 3:33 asubuhi, alizungumza na Salum na kumtaka amfuate kituo cha JKT Mgulani ili amkabidhi fedha na alifanya hivyo.

“Nilionana naye pale kituoni na nilimkabidhi Sh. 30,000 kwa ajili ya kupeleka nyumbani,” alisema.

Alisema baada ya kuachana naye, saa nane baadaye alipigiwa simu na mtu aliyemtaja kwa jina la Sheikh Athuman Juma, akimtaarifu juu ya kifo hicho cha Salum.

“Nilipofika nyumbani nilimuuliza mke wangu kama fedha nilizompa Salum zilifika, akaniambia hapana ndipo nilipobaini muda ambao niliachana naye pale kituoni ndipo alipokwenda kuuawa,” alisema.

Alisema cha kusikitisha ni kwamba alipokwenda kituo cha polisi Chang’ombe na kujitambulisha kuwa ni ndugu wa marehemu, aliambiwa kuwa wanafuga jambazi na hivyo mauaji hayo ni sahihi.

Alisema kuwa alisimuliwa jinsi Salum alivyopigwa risasi hadi alivyotambaa kwa madai kwamba alikuwa akitaka kumpora silaha askari.

Alisema baadaye alikwenda katika ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke na baada ya kusimulia historia ya Salum, ndipo alipojibiwa kuwa taarifa zake zitazifanyia kazi pamoja na zile za polisi.

Alisema kati ya saa 2:00 na saa 3:00 usiku siku hiyo, polisi walikwenda nyumbani kwake kufanya upekuzi na kuchukua kompyuta mbili, flash na daftari la marehemu la chuo.

Alisema vitu hivyo vilikuwa kwenye chumba kimoja ambacho amekitenga kama eneo la kujisomea watoto.

Alisema hivi sasa, maziko yake yatafanyika baada ya taratibu zote kukamilika.

Credit - Nipashe

UKWELI ni Kwamba ...Naona Future Nzuri kwa Lazaro Nyarando, Mbunge wa Singida Kaskazini..!!!

$
0
0

"SIASA HAINA ADUI WALA RAFIKI WA KUDUMU".
"SIASA HAINA MWENYEWE"

Mbunge wa Singida Kaskazini, Mh Lazaro Nyarandu amekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii kipindi cha awamu ya nne ya Mh Jakaya Kikwete. Aidha, hajabahatika kurudi kwenye Baraza la Mawaziri kipindi hiki cha awamu ya tano, awamu ya Dk John Pombe Magufuli.

Tukio la ajali ya wanafunzi wa shule ya Vicent Lucky ya jijini Arusha iliyopelekea vifo vya wanafunzi 33 na walimu 2 imemfanya Mh Nyarandu kupambana sana kuhakikisha majeruhi wanaenda kutibia Marekani kupitia mtandao wake wa marafiki alio nao huko ambao pia wapo hapa nchini kwa ajili yan utalii.

Mh Nyarandu ameonekana mstari wa mbele sana kuhakikisha anawalink majeruhi hawa, serikali ya Tz na hao wafadhiri ili kuhakikisha wanafunzi hao wanaenda kupatiwa matibabu nchini marekani kwa kiwango cha hali ya juu sana. hiki siyo kitu kidogo kwa mwanasiasa kufanya jitihada hizi.

Namwombea mema Mh Lazaro Nyarandu

ARUSHA: Meya, Wamiliki wa Shule, Paroko na Waandishi Walivyowekwa Chini ya ulinzi shuleni Lucky Vincent

$
0
0
Mstahiki Mayor wa Jiji , Paroko , Mchungaji , Waandishi wa habari 7 , wamekamatwa leo na Jeshi la Polisi wakiwa Shuleni Lucky Vicent ambako Mayor alialikwa na Umoja wa Shule binafsi Tanzania , waliopenda kutoa rambi rambi moja kwa moja kwa wafiwa badala ya kupitia ofisi ya Mkuu wa Mkoa .

Wazazi waliokuwa hapo wamepatwa na taharuki kubwa baada ya kuona viongozi hao wanachukuliwa bila sababu yoyote ya msingi , mpaka sasa wako Polisi wanaambiwa walikuwa na mikusanyiko isiyo halali .

Nafikiri tunachoka sana . Mungu mpaka lini mambo haya ?

UPDATES:Polisi Wasema Gambo Amewatuma Kuwakamata Walioenda Kutoa Rambirambi

$
0
0
Jeshi la Polisi limesema, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo ndiye aliyetoa amri ya kukamatwa kwa walioenda kutoa salamu za rambirambi katika Shule ya Msingi ya Lucky Vincent leo.

====
UPDATES:

Waandishi zaidi ya 8 waliokamatwa Arusha leo ktk utoaji rambirambi kwa Lucky Vicent wameachiwa, Polisi wawaambia waliwapa lift tu.

Source:Jamii Forums

RC Makonda atoa maelekezo 17 kwa Watendaji wa Sekta ya Ardhi na Ujenzi

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dsm, Paul Makonda leo Mei 18, 2017 amezungumza Na Watendaji wa Sekta ya Ardhi Na Ujenzi wanaohudumu katika Manispaa za Ubungo, Kigamboni, Kinondoni, Temeke, Ilala Na Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam na kutoa maelekezo 17 ya kuzingatia katika utendaji wao.

Pia ameahidi kutoa jumla ya pikipiki 25 kwa idara hizo,yaani pikipiki 5 kwa kila manispaa.

Maelekezo hapa:

1.Watendaji wa Sekta ya Ardhi Na Ujenzi Kushughulikia migogoro ya ardhi Na Ujenzi ili wananchi wasipeleke malalamiko yao ngazi za juu.

2.Watendaji wa Sekta ya Ardhi Na Ujenzi Wameagizwa kutoa vibali vya Ujenzi ndani ya mwezi mmoja Na zoezi hilo lianze Mwezi wa sita mwaka huu 2017. Mwanzoni mwa mwezi wa Saba kuzinduliwa teknolojia ambayo wananchi watapata taarifa zao za Ardhi kwenye mtandao Jambo ambalo litafanya Dar es salaam kuwa kiganjani mwa wananchi.

3.Wakuu wa Idara katika Sekta ya Ardhi Na Ujenzi kuhakikisha wanatoa taarifa kuhusu Mipango ya Idara kwenye vyombo vya habari kwa kuwatumia maafisa habari kwani tayari wana mahusiano Na waandishi mbalimbali katika vyombo vyombo vya habari.

4.Wakuu wa Idara ya Ardhi Na Ujenzi kutoa TAARIFA ya maeneo yote ya wazi yaliyotolewa Hati, Na kujitokeza haraka kwa wote waliotoa Hati za maeneo ya wazi kama wapo.

5.Wakuu wa Idara ya Ardhi Na Ujenzi kusimamia haraka upimaji wa maeneo yote ya Umma kama kama vile Shule, Hospitali, Na Masoko kama alivyoagiza Waziri wa TAMISEMI sambamba Na kutoa Mikakati wa Upimaji.

6.Wakuu wa Idara ya Ardhi Na Ujenzi kuhakikisha ufanisi Na bidii ya utendaji inaongezeka hususani mikakati ya kuhusisha wapimaji binafsi wanaotambulika kwani Mji ukipimwa vyema Madiwani watafurahi lakini pia itakuwa njia rahisi ya kuepuka migogoro ya Ardhi.

7.Kushughulikia changamoto za kisera unaofanya utaratibu wa Upimaji Na utoaji wa Hati kuchelewa kukamilka.

8.Mabaraza ya Kata kuangaliwa upya kwa mujibu wa Sheria ili kuwa Na utendaji imara unaoshabihiana Na Jambo la kisera.

9.Kila Mtumishi kufanya Kazi yake kwa Uaminifu kwani dhamani aliyopewa ni kubwa Na anapaswa kuitendea Haki. Watumishi wote kusimamia Na kutekeleza ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwani chama hicho ndicho kimeingia mkataba Na wananchi katika kipindi cha miaka mitano.

10.Kila Mkuu wa Idara kupitia ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya Mwaka 2015-2020 ili kutambua maelekezo yaliyobainishwa katika Sekta yake sambamba Na kuwaelekeza wasaidizi wao pia kuisoma Na kuielewa vyema ilani hiyo.

11.Kufatilia Na kufahamu upandaji wa madaraja Na stahiki zao kwani ni Haki zao za msingi kisheria ikiwa ni pamoja Na kwenda likizo.

12.Watumishi wote kuheshimu mamlaka walizonazo Na kutumia vikao halali kutoa taarifa sahihi kwa watu husika.

13.Kuwa Na ushirikiano wa watumishi katika Idara zote ili kukuza ufanisi wa Kazi.

14.Kujitokeza ndani ya wiki moja kwa watumishi wote wa Sekta ya Ardhi waliojihusisha Na utoaji wa Hati za Ardhi kinyume Na sheria. Na endapo wasipojitokeza Na wakabainika watachukuliwa hatua za kisheria.

15.Kufafanua baadhi ya mambo ili Madiwani waweze kuelewa. Sambamba Na kutoogopa maadhimio kama wanatenda Kazi kwa mujibu wa Sheria pasipo kupendelea.

16.Wakuu wa Idara kila mwisho wa wiki kutoa taarifa kwa Wakurugenzi inayoonyesha idadi ya Migogoro Na jinsi ilivyotatuliwa.

17.Katika kupunguza changamoto ya kuwafikia wananchi kwa Wakati RC Makonda Amesema atatoa Pikipiki 5 kwa kila manispaa ya jiji la Dar es salaam, yaani jumla ya pikipiki 25 kwa manispaa zote 5 za Sekta ya Ardhi kwa kila Manispaa.
Hapa kazi tu.

EXCLUSIVE..Huyu Hapa Ndiye Mrithi wa Kinana CCM..!!!

$
0
0

Kama haya niliyoyapata kutoka kwenye chungu ni kweli, basi naamini CCM itaanza kurejea katika misingi yake ya ujamaa...

Dr. Bashiru ni miongoni mwa wana~ujamaa waliobaki katika nchi hii. Ni mtu anayeamini katika siasa za kujitegemea na katika falsafa ya Mwalimu Nyerere...

Ni mwanafunzi na mwalimu mtiifu wa falsafa ya ujamaa. Naamini akipewa chama atakirudishia heshima aliyoiacha Mwalimu Nyerere. Na ataendana sana na Mjamaa mwenzake Dr. Magufuli

RAIS Zuma Ataka Ziwa Victoria Libadilishwe Jina..!!

$
0
0
.
 Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma ameitaka Uganda kubadili jina la Ziwa Victoria ili liendane na jina linalowakilisha uhalisia wa wananchi wa eneo hilo.

Kiongozi huyo anayekosolewa vikali nchini mwake amesema tayari amemfahamisha Rais Yoweri Museveni juu ya haja ya kubadilishwa jina hilo.

Jina la Ziwa Victoria lilitolewa na mtafiti mmoja wa Uingereza kama zawadi kwa Malkia wa Taifa hilo aliyetambulika kwa jina la Victoria.

Akizungumza katika ufunguzi wa maonyesho ya utalii mjini Kampala, Rais Zuma amesema  Ziwa hilo kuendelea kuitwa  Victoria kunawanyima fursa wananchi wa eneo hilo kujivunia uasili wao.

“Mnaweza kuweka bango kubwa linaloonyesha jina la jipya na kisha mkaweka bango  dogo litakalosomeka kama “ zamani eneo hili liliitwa Ziwa Victoria”. Lazima mbadilishe jina hili na kuweka jina litakaloelezea uzuri wa Taifa hili,” amesema Rais Zuma. 

CCM Arusha Wamjibu Lowassa Sakata la Msiba wa Wanafunzi Lucky Vicent..!!!

$
0
0

Chama cha Mapinduzi mkoa wa Arusha kimeishangaa kauli ya aliyekuwa Waziri Mkuu Edward Lowassa kusema kuwa Rais John Magufuli amemtuma ‘mtoto mdogo’ kwenda kuiwakilisha serikali kwenye mazishi ya wanafunzi wa  shule ya Lucky Vicent

 Akizungumza  na waandishi wa habari leo, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Arusha Michael Lekule ,amesema kauli ya Waziri huyo mstaafu ameitoa kwa kudanganya wananchi na kuonesha serikali ya Magufuli haishirikiani na wananchi ,wakati serikali iliubeba msiba huo mzito wa taifa.

 Amesema jitihada za serikali ya Magufuli zimeonekana kupitia kwa wawakilishi wake Makamu wa Rais Samia Suluhu pamoja na Mrisho Gambo pamoja na wanachama wa CCM ambao walijitokeza kwa wingi kwenye msiba huo mzito

 "Serikali ilijitoa kwa hali na mali kuwezesha  familia 35 kwenda kupumzisha wapendwa wao,na ilihakikisha kila mwili unapumzika mahala popote familia inapopata,tunajiuliza walitaka nini kama kote nafasi ilijazwa na serikali ya Magufuli," alisema Michael

 "CCM inakanusha kwanguvu upotoshaji huo,hata ukiangalia siku ile uwanja wa shekh Amri Abeid wanaccm walijaa uwanjani ,kikubwa CCM imeguswa na msiba uliotokea na Rais wetu amekuwa bega kwa bega juu ya tukio lililotokea,"amesema

 Pia amesema wamemshangaa kwa kusema Rais alimtuma mtoto mdogo wakati yeye mwaka 2007 ajali mbaya iliyotokea Monduli duka bovu na kuua watu 20 ambao 11 walikuwa ni askari wa JKT,rais Kikwete alimtuma aje kuiwakilisha serikali.

 Hata hivyo alimtaka kiongozi huyo, ajiulize kama yeye kipindi akiwa Waziri Mkuu aliweza kutumwa na Rais, amuwakilishe kwenye msiba wa watu 20, je yeye na Makamu wa Rais ni nani mdogo?

 "Tena ajali hiyo ilikuwa ya kitaifa,askari 11 walifariki kwenye ajali,mbona hajayasema ya kwake?," amesema Lekule

HALOTEL Waanika A - Z Sakata la Madai ya Kuhujumu Uchumi..Watupa Mzigo wa Lawama kwa ...!!!!

$
0
0

Kampuni ya mawasiliano ya  simu ya  Halotel imetoa ufafanuzi kuhusu madai ya kuhujumu uchumi na kutoa kueleza kuwa iliingia kwenye kesi hiyo kutokana na mteja wake kuwa mhusika mkuu.

 Mkurugenzi Mtendaji wa Halotel,  Le Van Dai ameeleza kuwa makosa pekee ambayo wamehusishwa nayo na kukiri, ni kushindwa kutoa taarifa za usajili wa kampuni ya Unex Company Ltd kwa ajili ya kusajili laini za simu 1000 zilizouzwa kwa kampuni hiyo.

 Kosa lingine ni kushindwa kitimiza majukumu yao vizuri kwa kuuza laini za simu kwa kampuni hiyo ambayo haikuwa haikuwa imesajiliwa kikamilifu.

 Inadaiwa kuwa bila kupata kibali cha Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), kampuni ya Unex Company Ltd ilisimika mitambo iliyowezesha laini hizo kutumika kwa mawasiliano ya nchi na kuisababishia Serikali hasara ya Sh459 milioni.

 Siku zote tunafanya kazi kwa kufuata taratibu za nchi. Mitambo ambayo ilikuwa inafanya kazi ya kuiba mawasiliano sio yetu na hatukufahamu kama wateja wetu Unex walitumia mitambo hiyo,"amesema

BAADA ya Kuukosa Ubingwa....Simba Wapanga Kuwatupia Virago Wachezaji Wakimataifa..!!!

$
0
0

Wanamsimbazi na hata baadhi ya viongozi mpaka sasa hawaamini kama timu yao ndio imeukosa ubingwa wa Ligi Kuu Vodacom Tanzania Bara msimu huu, lakini moja ya wajumbe wa Baraza la Wadhamini wa klabu hiyo, Hamis Kilomoni amefichua siri nzito kuwa kuna wachezaji watano wa kigeni watatemwa na klabu hiyo.

Kilomoni amesema kuna wachezaji watano wa kigeni watatemwa klabuni hapo ili kupisha wazawa kuipigania klabu hiyo kwani wanagharama ndogo na wanajitoa kuipigania timu kwa jasho na damu.

 Kilomoni aliyewahi kuwa mchezaji na kiongozi wa Simba kabla ya kuwa Mwenyekiti wa Baraza la wadhamini, alisema Simba haikupata huduma sahihi kwa nyota wake saba wa kigeni iliowasajili msimu huu kwa uwezo mdogo walionao, hivyo anaona ni bora idadi yao ipunguzwe ibaki wawili tu.

Alisema mabosi wa Simba walifanya kosa kubwa kuwadharau wachezaji wazawa na kuwakimbilia wageni ambao wamekuwa hawana msaada wowote zaidi ya kuitia gharama kubwa ya kuwahudumia.

“Tulikuwa na wachezaji wengi kutoka kikosi B, lakini sijui nini kilitokea wakatolewa, huko waliko wanafanya vyema na hata kuisumbua Simba, halafu sisi tukakimbilia wageni saba ambao ukiniuliza faida yake hata sijaiona, nafikiri tunapaswa kuangalia upya hili suala la wachezaji wa kigeni halisaidii soka letu, Simba kama kuna wachezaji wa kigeni wanaostahili kubaki na walioisaidia timu wako wawili tu hawa wengine sioni wanachokifanya.” Alisema Kilomoni.

Hata hivyo Kilomoni hajawataja nyota wanaostahili kusalia, japo Simba kwa sasa ina wachezaji wa kigeni ambao ni  Method Mwanjali, Juuko Murshid, Fredrick Blagnon, Janvier Bokungu, Laudit Mavugo, James Kotei na kipa Daniel Agyei.

Chanzo : Mwanaspoti

Harmorapa Alivyoumbuliwa na Diva Kwenye Ala za Roho

$
0
0
Bidada alikuwa akimhoji jamaa anachomekea na maneno ya kiingereza amabayo yalikuwa yakimpa wakati mgumu kijana mpenda Kiki Harmorapa

Tazama Hapa:

SEHEMU Tano za Mwili Wako Ambazo Hupaswi Kuzigusa kwa Mkono..!!!

$
0
0

Mikono yetu ni kiungo muhimu sana kinachoweza kupapasa karibu asilimia 99 ya miili yetu bila shida, lakini tafiti zimeonesha kuwa ni hatari zaidi kwa afya yetu kushika sehemu kadhaa hususan sehemu hizi tano.

Katika hali ya kushangaza, utafiti uliofanywa na jopo lililoongozwa na Profesa Kelly Reynolds wa Chuo cha Zuckerman College of Public Health kilichoko ndani ya Chuo Kikuu cha Arizona, unataja maeneo hayo ya mwili. Baadhi ya maeneo hayo ni haya yafuatayo:

Macho

Kama jicho lako halikulazimishi kulishika labda pale unatoa uchafu wa aina yoyote kwa namna inayofaa, hakikisha hauligusi kabisa. Hii ni kwa sababu mikono yetu inabeba mambo bakteria ambao wanaweza kudhuru macho yetu taratibu na kudhurika bila kufahamu haraka.

Uso

Uso ni sehemu ambayo ni rahisi sana kupeleka mkono mara kwa mara. Ni ngumu sana kuacha kufanya hivyo hususan kwa tunaofanya kazi za kutoa jasho au kutembea sehemu ambazo zinatoa jasho. Pamoja na mambo hayo, wataalam wamebaini kuwa ngozi ya uso ni ngozi ya kipekee na inapaswa kutunzwa kwa uangalifu zaidi. Mikono yetu ambayo hubeba mafuta mafuta pamoja na bakteria inaweza kudhuru ngozi zetu za uso.

Mdomoni (Nje na Ndani)

Utafiti zilizofanywa hivi karibuni nchini Uingereza umebaini kuwa mtu ambaye ameboreka (bored) kazini hushika maeneo ya mdomoni zaidi ya mara 23.6 kwa saa moj. Hali hii ni tatizo kubwa kwani utafiti umebaini kuwa robo tatu ya bakteria wabaya hupitia kwenye mdomo.

Ndani ya Pua

Kuna watu ambao kuchokonoa mapua yao ni sehemu ya tabia iliyojengeka. Kwa bahati mbaya, tafiti za kitabibu zimebaini kuwa watu wanaochokonoa pua zao kwa vidole wako katika hatari kubwa zaidi ya kushambuliwa na bakteria (staph bacteria) zaidi ya wale ambao hawafanyi hivyo.

Ngozi ya chini ya kucha

Ni kosa kubwa kutunza kucha zako kuwa ndefu kiafya. Kucha hubeba uchafu hata ule ambao huwezi kuuona kwa macho, bakteria wanaweza kujificha chini ya ngozi za kucha yako. Bakteria hao wanaweza kuwa chanzo kikubwa cha kuharibu afya yako. Hivyo, jitahidi kutofuga kucha, hakikisha kucha zako ni fupi kwa kiasi cha kutosha ili usiipe nafasi bakteria kuishi.

Lakini kama unafuga kama urembo, unapaswa kuwa na matunzo ya ziada ya namna ya kupambana na bakteria ambao huwaoni kwa macho.


Note: Sehemu za siri ni shemu ambazo kila unapotaka kuzigusa fahamu kuwa ni sehemu ambazo zikiguswa na bakteria uliowasomba na mikono yako zinaweza kukusababishia madhara makubwa.

MREMBO Alipia Bango Katikati ya Jiji Akitangaza Kuwa Bikira, Adai Anasaka ‘Tendo’ Kabla Hajafa..!!!

$
0
0

Katika hali isiyo ya kawaida, muigizaji wa vipindi vya TV mwenye umri wa miaka 40 amelipia ‘Bango’ kubwa katikati ya jiji akijitangaza kuwa ni bikira anayetafuta mwanaume wa kufanya naye tendo la ndoa ili asife bila kujua uhondo wake.

Kwa mujibu wa Daily Mirror, Aranya ‘Pui’ Pathumthong ambaye ni muigizaji wa Thailand, aliyeweka bango hilo katika jiji la Bankok, karibu na wilaya ya Lat Phrao amesisitiza kuwa yuko ‘serious’ na tangazo hilo ambalo ameliweka baada ya matangazo yake kupitia mitandao ya kijamii ya mahusiano nchini humo kushindwa kuzaa matunda.

Tangazo lake limeandikwa, “I Want You. “40 and a virgin. Pui Aranya is looking for a husband!”Let me get it once before I die.” Linaonesha namba ya simu pia.

Aranya ameviambia vyombo vya habari nchini humo kuwa ameamua kusaka mwanaume kwa mtindo huo ili aweze kuonja raha ya penzi kabla hayafa.

Hata hivyo, Polisi jijini humo wameamuru Bango hilo liondolewe ingawa limelipiwa na kuongeza kuwa wanahitaji kumhoji mwanamke huyo kuhusu uamuzi wake wa kuweka bango hilo.

ZINGATIA ..Haya ni Mambo Matatu Ambayo Hupaswi ‘Kuya-Google’ Kamwe..!!!

$
0
0

Google imerahisisha njia za kufahamu mambo mengi ambayo binadamu angepaswa kutumia muda mwingi kuyatafuta au hata kulipia ili aweze kuyafahamu.

Kupitia Google unaweza kuwa na shule ya ziada ya ufahamu wa mambo mbalimbali yakiambatana na picha za aina unazotafuta. Ili mradi tu kuna mtu duniani aliwahi kuweka kwenye mtandao kwa ajili ya umma. Unachopaswa kuwa nacho ni kifaa cha mfumo wa ‘computer’ chenye mtandao.

Naweza kusema kuwa Google ni kama kioo cha ubongo wako, chochote unachotaka kukiangalia ndicho kitakachojitokeza kwenye kioo cha computer au simu yako yenye mtandao.

Wengi tumepata elimu kubwa sana na ufahamu wa mambo mengi makubwa na muhimu kupitia Google. Tunapata habari, burudani na mengine mengi.

Lakini nakumbuka mwalimu wangu wa chuo aliwahi kuniambia kuwa google ni msaada mkubwa kwa masomo yako, lakini ni chanzo kikubwa cha ‘kukupumbaza’ (google will make you stupid).

Kauli hiyo ndiyo iliyonifanya niweze kufikiria, ni mambo gani ambayo sipaswi kuya-google ili yasinifanye kuwa mpumbavu au yanayoweza kunidhuru kwa kuyaangalia?

Kwa bahati mbaya, wataalam wa Saikolojia wanaeleza kwamba akili ya binadamu hutamani sana kuangalia mambo yaliyozuiliwa kuangalia, kuliko mambo yaliyowekwa bayana.

Tukumbuke kuwa Google ni kama soko huria la mawazo ambalo karibu kila utakacho utapata, lakini huwezi kununua usichotaka. Kila aina ya usafi na uchafu hutupwa Google.

Mambo ambayo hupaswi kuya-google ni mambo yote ambayo, kwanza yatakubadili saikolojia yako na kufuata mambo ambayo kabla ya kuyagoogle ulijua kabisa hayafai katika jamii uliyopo.

Pili, ni mambo yote ambayo ni haramu kuyatamka au kuyazungumzia katika jamii yako, jiulize unataka kuyafahamu ili upate faida gani? Je, unahisi ukiyaona yatakusaidia kuendeleza zaidi maisha yako au yatakuondoa kwenye reli ya maadili na imani yako?

Tatu, mambo yote ambayo yanaweza kukuharibia siku kisaikolojia, unaweza kuona mateso, uchafu na mambo kama hayo ambayo yatakugharimu na kuichafua akili yako. Usijaribu ku-google vitu unavyovichukia, kisaikolojia vitakugharimu… hususan kama hakuna sababu muhimu na chanya zaidi ya kuviona.

Baki salama, usi-google kila kitu. Google isikufanye kuwa mpumbavu, google kwa malengo chanya na matokeo yatarajie kukujenga zaidi badala ya kukubomoa.

PICHAZZ: Amuua Mpenzi Wake na Kuendelea Kufanya Mapenzi na ‘Maiti Yake’...!!!

$
0
0

Mwanaume mmoja aliyetajwa kwa jina la Timothy Johnson mwenye umri wa miaka 25, anashikiliwa na Jeshi la Polisi la Florida nchini Marekani kwa kosa la kumuua mpenzi wake Judith Therianos aliyekuwa na umri wa miaka 52, na kisha kuendelea kufanya naye mapenzi kwa muda.

Taarifa zilizotolewa na Mkuu wa kitengo cha polisi cha Florida, Chris Nocco zimeeleza kuwa tukio hilo lilitokea mwezi uliopita wakati wawili hao walipokuwa wanafanya mapenzi.

Nocco aliwaeleza waandishi wa habari kuwa uchunguzi wa polisi umebaini kuwa wakati wanaendelea kufanya mapenzi, mwanamke huyo alimtaka mtuhumiwa kutoendelea na ndipo alipomuua na kisha kuendelea na zoezi hilo kwa muda.

Kwa mujibu wa Polisi, Judith hakuonekana tangu Machi 14 mwaka huu kabla ya kubainika kuwa alikuwa ameuawa baada ya mwili wake kupatikana Aprili 7.

USITHUBUTU Kwenda Kwenye Usaili wa Kazi Bila Kufahamu Mambo Haya Manne..!!!

$
0
0

Usaili wa kazi ni hatua muhimu kwa kila mwenye ndoto ya kuajiriwa na kupata kazi ya ndoto yake. Lakini ni hatua yenye vikwazo vidogo vinavyogeuka kuwa mlima wa kikwazo pale ambapo msailiwa ataruka hatua hizi nne muhimu katika maandalizi yake.

Kutofahamu mambo haya muhimu kabla ya kuingia kwenye usaili, huwafanya wasailiwa wengi kujikuta wakijuta kuingia kwenye usaili husika au kufikiri kuwa hawana bahati ya kupata kazi wanayoitamani kwa kuwa wamejibu vizuri maswali mengi waliyoulizwa.

Lakini maswali unapaswa kufahamu kuwa mambo haya manne yatakupa asilimia zaidi ya 80 ya ushindi kwenye maswali yoyote utakayoulizwa na wasaili. Hata kama maswali utakayoulizwa unayafahamu vilivyo, lakini kushindwa kuyaunganisha na mambo haya kutakuangusha vibaya na huenda ukambilia kudhani ulinyimwa kazi kwa makusudi.\

Fahamu vizuri Kampuni/shirika husika

Hii ni hatua ya kwanza na muhimu sana katika ushindi wa usaili husika. Karibu kila swali utakaloulizwa litakuwa na uhusiano na hili.

Hivyo, unapaswa kufahamu vizuri kazi na huduma au bidhaa zinazotolewa na shirika husika,  dhima na dira na lengo kuu la kampuni/shirika hilo. Unapaswa pia kuhakikisha unafahamu washindani wa kampuni husika hususan kama inafanya biashara yoyote.

Tambua Udhaifu, Uimara, Fursa na Hatari/vitisho ambavyo kampuni husika inakutana navyo. Ni rahisi kufahamu mambo hayo endapo utatumia muda wako kufanya utafiti wenye mantiki kuhusu kampuni husika. Taarifa hizi zote unaweza kuzipata kwa kusoma tovuti ya kampuni husika pamoja na machapisho yao mbalimbali.

Hii itakuongezea hali ya kujiamini kwa kuwa unamfahamu vizuri mwajiri wako.

Fahamu kiundani majukumu yote ya nafasi unayowania

Hapa simaanishi tu kukariri majukumu uliyoandikiwa kwenye tangazo la nafasi ya kazi, bali kufahamu kwa kina kinachotegemewa kutoka kwako.

Muajiri wako anatarajia mtu atakayemuajiri awe anajitambua vizuri na amejiandaa kuyakabiri majukumu yake. Anatarajia kuona nia na uwezo wa mtu anayemhitaji kwenye usaili husika.

Ukiyafahamu vizuri majukumu yako na mipaka yake, utakuwa na uwanja mpana wa kujibu maswali yako kwa kumshawishi muajiri kuwa majumu husika unaweza kuyakabili kwa ufanisi zaidi. Kila swali litakaloelekezwa kwako, lijibu ukiwa na picha ya majukumu yako pamoja na kampuni yako.

Kwanini unahitaji kazi hiyo na kwanini unadhani wewe ndiye mhusika

Mwajiri anahitaji sana mtu anayejielewa kama nilivyosema awali, ‘self determined and focused’. Unapaswa kujiuliza vizuri kwanini unahitaji kazi husika, huku ukilizingatia pia swali kuwa unadhani kwanini wewe ndiye mtu unayefaa zaidi kuliko wote.

Kama hufahamu kwanini unahitaji nafasi hiyo, sio kwa sababu unahitaji pesa, hilo linajulikana na ni vyema usiligusie kabisa. Zungumzia upande wa pili wa ‘Career’ yako hasa na unavyotaka kuleta mabadiliko kwenye kazi husika. Ni muda mzuri wa kujinadi.

Ifahamu vizuri, imeze CV yako

Curriculum Vitae (CV), ni maandishi yanayokueleza wewe ulivyo na uhusiano wako na kazi husika. Isome vizuri CV yako baada ya kuandika mambo muhimu unayopaswa kuyaandika. Tutaelezea siku moja kipi hakipaswi kuwekwa lakini huwekwa na wengi.

Usiiache nukta iliyo kwenye CV yako ikupite bila kuielewa vizuri. Isome tena na tena na uelewe kwanini umeandika yote uliyoandika na namna ya kuyaelezea.

Kumbuka katika usaili, CV yako inaweza kuzaa maswali mengi na ikakuinua au kukuangusha. Kumbuka ku-update CV yako kila unapotaka kazi fulani, usiitupe tu kwa kazi yoyote, mengine yanaweza kuwa yanakuinua kwenye kazi A, lakini  yakawa chanzo cha kukukoseha kazi B.

AGIZO la Rais Magufuli la Tanesco Kukata Umeme kwa Wadiawa Sugu Latekelezwa Kwenye Ofisi za Makao Makuu ya Polisi..!!

$
0
0

Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco)  mkoani hapa limesitisha  huduma za umeme katika  mgodi wa makaa ya mawe wa Kiwira (Kiwira Coal mine) na ofisi za Jeshi la Polisi mkoani hapa baada ya taasisi hizo kushindwa kulipa madeni zinazodaiwa na shirika hilo.

 Meneja wa Tanesco Mkoa Mbeya, Benedict Bahati amesema mgodi wa Kiwira unadaiwa  Sh1.3 bilioni  na Jeshi la Polisi Mkoa  wa Mbeya linadaiwa Sh700 milioni. 

Bahati amesema wamefikia hatua hiyo kwa sababu wadaiwa hao hawajaonyesha nia ya kulipa madeni yao ambayo ni ya muda mrefu na hivyo kulisababishia shirika hilo kushindwa kujiendesha kwa ufanisi.

“Taasisi za Serikali  ambazo  madeni  yake ni makubwa na mwitikio wake wa ulipaji sio mzuri, tumesitisha huduma mpaka watakapolipa madeni hayo,”amesema. 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Dhahiri Kidavashari amekiri kudaiwa deni na Tanesco pamoja na kusitishiwa huduma hiyo kwenye baadhi ya vitengo na kwamba wao kama taasisi wanadaiwa kama ilivyo kwa taasisi nyingine.

STAA wa Filamu ya 'Kuch Kuch Hota Hai' Reema Lagoo Amefariki Dunia..!!!

$
0
0

Reema Lagoo, muigizaji mkongwe kutokea nchini India aliyekuwa akiishi katika mji wa Mumbai amefariki dunia kwa kuugua kifua.

Lagoo amefariki akiwa katika hospitali ya Dhirubhai Ambani, masaa machache baada ya kufikishwa hospitalini hapo. Marehemu amepata umaarufu kupitia filamu ya “Kuch Kuch Hota Hai”, Kabla ya umauti wake amekuwa akigiza mara nyingi kama mama kwenye filamu kama vile “Hum Aapke Hain Koun” na “Kal Ho Na Ho”.

Lagoo mwenye miaka 59 kabla mauti kumfika, alifikishwa hospitalini hapo lakini alikuwa akilalamika juu ya maumivu makali ya kifua, Alisema msemaji wa Hospitali hiyo Bw. Ram Naraian.

Kabla ya mauti kumfika, marehemu amewahi kuigiza filamu kama vile “Maine Pyar Kiya”, “Saajan”, “Vaastav, na “Hum Saath-Saath Hain”., pia alikuwa akionekana kwenye tamthilia iitwayo “Naamkaran”, inayooneshwa Star Plus.

TRUMP Ainyima Mabilioni ya Pesa Kenya na Kuipa Tanzania ..Yadaiwa Ameridhika na Usimamaizi wa Fedha za Marekani kwa Tanzania..!!!

$
0
0

Marekani imetangaza kuipatia Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ufadhili wa kukabilana na virisu vya ukimwi.

Taarifa hiyo iliyotolewa na Serikali ya Marekani kupitia ofisi ya Rais Donald Trump imeeleza kuwa imeipa Tanzania kitita cha dola milioni 526 kutoka mfuko wa PEPFAR, ili kufanikisha mpango wa kutoa huduma kwa zaidi ya watu milioni 1.2 wanaoishi na virusi hivyo.

Mwakilishi wa ubalozi wa Marekani nchini Tanzania, Virginia Blaser amesema kuwa wanalenga kufanikisha kizazi kilicho huru kutoka virusi nchini Tanzania. ”Kwa niaba ya raia wa Marekani, tunafurahia ushirikiano wetu na Tanzania na tunajitahidi kuhakikisha hakuna anyeachwa nje,” Amesema.

Ufadhili huo umelenga matibabu, ukaguzi, na kuzuia maambukizi mapya ya virusi hivyo kuanzia sasa hadi Septemba mwaka ujao, pia fedha hizo zitatumika kuimarisha maisha ya wajane na mayatima wa viurusi hivyo, kuzuia dhulma za kijinsia, pamoja na kuwafikia zaidi ya watu laki tatu walioambukizwa.

Aidha, Serikali ya Marekani itashirikiana na Serikali ya Tanzania kutekeleza huduma za kuwapima raia milioni 8.6 ili kuwawezesha kujua hali yao ya virusi, imeeleza taarifa hiyo ya BBC.

Fedha hizo zitapitia katika mashirika mbalimbali yanayoendesha miradi ya afya nchini Tanzania, kama vile (TACAIDS), na Benjamin Mkapa (Benjamin Mkapa HIV/AIDS Foundation (BMAF)) yanatarajiwa kushiriki kufanikisha mpango huo.

Marekani ilikatiza ufadhili wake wa miradi kama hiyo nchini Kenya pamoja na kuyazuia mashirika dhidi ya kufanikisha miradi yoyote na wizara ya afya ya taifa hilo kutokana na usimamizi mbaya wa fedha.
Viewing all 104809 articles
Browse latest View live




Latest Images