Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104795 articles
Browse latest View live

Kutana na Mama aliyejifanya mwanaume ili afanye kazi mgodini Tanzania

$
0
0

Pili Hussein alitamani kujiimarisha kimaisha na mawe ya thamani yanayosemekana kuwa nadra mara elfu mia moja kuliko almasi, lakini kwa kuwa wanawake hawakuwa wanaruhusiwa kwenye migodi hiyo alivalia mavazi kama mwanamume na kuwadanganya wafanyikazi wenzake kwa zaidi ya mwongo mmoja.


Pili alilelewa katika familia kubwa mjini Tanzania. Mtoto wa mchugaji ambaye aliyekuwa na mashamba makubwa, babake Pili alikuwa na wake sita na alikuwa miongoni mwa watoto 38.


Licha ya hayo yote alilelewa vyema kwa njia tofauti.


''Babangu alinichukulia kama mwanamume na nilikuwa nikichunga mifugo yake, lakini sikuyapenda maisha hayo kabisa'', alisema.


Hata ndoa yake haikuwa ya furaha, akiwa na umri wa miaka 31 Pili aliikimbia ndoa yake iliyokumbwa na migogoro ya kinyumbani.


Alipokuwa akitafuta ajira alijipata katika mji mdogo wa Mererani, Tanzania, uliopo chini ya mlima mkuu wa Kilimanjaro.


Eneo hilo ni maarufu sana duniani kwa kuwa na madini nadra ya rangi ya samawati ya tanzanite.


''Sikwenda shule , kwa hivyo sikuwa na mambo mechi kuchagua,'' Pili alisema.


''Wanawake wahakuruhusiwa kwenye maeneo ya migodi hiyo, nikajitosa kama mwanamume shupavu na mwenye nguvu. Nilichukua suruali ndefu na kuzikata zikawa kama kaputula ili kufanana na mwanamume. Hivyo ndivyo nilivyofanya.''


Ili kukamilisha mabadiliko yake , alibadilisha pia jina lake.


''Niliitwa Uncle Hussein {akimaanisha mjomba Hussein}, sikumwambia yoyote kuhusiana na jina langu halisi la Pili.


Hata leo ukija katika kambi hiyo utanitafuta kwa jina hilo la Uncle Hussein.''


Kwenye migodi hiyo yenye joto ,uchafu mwingi na wenye kina cha mita mia moja chini ya ardhi Pili angefanya kazi kwa saa 10-12 kwa siku , akilima na kuchunga akiwa na matumaini ya kupata mawe hayo ya thamani kwenye mishipa ya mawe hayo ya grafiti.


''Ningeenda hadi mita 600 chini ya mgodi, mara kwa mara nikiwa shupavu kuliko wanaume wengine.

Nilikuwa na nguvu nyingi na niliweza kufanya kazi kama matarajio ya wanaume wengine wangefanya.''


Pili amesema hakuna aliyemshuku alikuwa mwanamke.


''Nilijifanya kama nyani aina ya Gorilla'' alisema, Nilipigana, lugha yangu ilikuwa mbaya , nilibeba kisu kikubwa kama Maasai.


Hakuna mtu alifahamu kwamba mimi ni mwanamke kwa sababu kile nilichokuwa nikifanya nilikifanya kama mwanamume.''


Baada ya mwaka mmoja, alipata utajiri , alipopata mawe mawili makubwa ya Tanzanite. Kutokana na pesa alizozipata alimjengea babake, mama na pacha wake nyumba mpya na akajinunulia vifaa zaidi na akaanza kuajiri wachimba migodi kumfanyia kazi.


Na kujificha kwake kuliwashawishi kwamba alichukua hatua zisizo za kawaida kwa utambulisho wake kujulikana.


Mwanamke mmoja aliripoti kwamba alikuwa amebakwa na wachimba migodi Pili akiwa miongoni mwa washukiwa.


''Polisi walipokuja, wanaume waliotekeleza ubakaji huo wakasema: 'Huyu ndio mwanamume aliyetekeleza hilo'' na nilipopelekwa katika kituo cha polisi , Pili akasema alikuwa hana namna bali kutoboa siri yake.''


''Aliwauliza polisi kumleta polisi mwanamke ili amchunguze kwamba yeye hakutekeleza kitendo hicho na baadaye aliachiliwa huru. Hata baada ya hilo wachimba migodi wenzake waliona vigumu kuamini walikuwa wamedanganyika kwa siku nyingi''.


''Hawakuamini hata polisi waliposema kwamba alikuwa mwanamke," alisema, ''haikuwa rahisi kwao kukubali hadi mwaka 2001 nilipoolewa na nikaanza familia.''


Kutafuta bwana wakati kila mtu amenizoea kama mwanamume haikuwa rahisi, Pili alipata bwana na akafanikiwa.


Swali lililokuwa akilini mwake lilikuwa,'je ni mwanamke kweli?'' anakumbuka. ''ilimchukua miaka mitano ndipo aliponikaribia.''


Pili aliikuza taaluma yake na hivi leo anamiliki kampuni yake ya migodi ambayo ameajiri wachimba migodi 70 , watatu kati yao ni wanawake, lakini wanafanya kazi ya upishi.


Pili amesema licha ya kwamba kuna wanawake wengi katika makampuni ya migodi kuliko wakati wake, hata leo ni wanawake wachache wanaofanya kazi kwenye migodi hiyo.


''Wanawake wengine huyaosha mawe hayo , wengine ni wakala na wengine ni wapishi'' , alisema, ''lakini hawaingii ndani ya migodi , si rahisi kumpata mwanamke akifanya nilichofanya wakati wangu.''


Mafanikio ya pili yamemuezesha kuwalipia karo watoto wa ndungu zake 30 na wajukuu. Licha ya hayo amesema hawezi kumrai mwanawe kufuata nyayo zake.


''Najivunia kwa kile nilichokifanya, imenifanya tajiri lakini ilikuwa vigumu kwangu'', amesema.


''Nataka kuhakikisha mtoto wangu ataenda shule apate elimu na ataweza kujiendeleza kimaisha kwa njia tofauti mbali na nilivyopitia.''

TAFITI: Instagram ndiyo mtandao hatari zaidi kiafya

$
0
0

Mtandao wa Instagram umeorodheshwa kuwa mtandao wa kijamii ambao una madhara zaidi kwa afya ya kiakili ya vijana.

Katika tafiti zilizofanywa nchini Uingereza, vijana 1,479 wa miaka kati ya 14 na 24 waliombwa kueleza utathmini wao kuhusu mitandao mbalimbali ya kijamii kwa kuzingatia wasiwasi, mfadhaiko, upweke, dhuluma na sifa za kimwili.

Mtandao wa Instagram ndiyo uliongoza kwa kuwa na madhara zaidi kwa vijana ukilinganisha na mitandao mingine ya kijamii

Mashirika ya hisani kuhusu afya ya kiakili yametoa wito kwa makampuni kuimarisha usalama wa watu wanaotumia mitandao ya kijamii.

Utafiti huo uliofanywa na taasisi ya Royal Society for Public Health unasema mitandao ya kijamii inafaa kutambua watu wanaotumia mitandao ya kijamii kwa kupitiliza na pia wale wenye matatizo ya kiakili.

Inakadiriwa kuwa 90% ya vijana hutumia mitandao ya kijamii, na hivyo ndio huathirika zaidi.

Utafiti huo uliwauliza washiriki maswali kuhusu iwapo YouTube, Instagram, Snapchat, Facebook na Twitter zina madhara kuhusu afya yao na hali yao.

Washiriki walitakiwa waipe alama mitandao ya kijamii kuhusu masuala 14 ya afya na hali yao.

Kwa kufuata vipimo vyao, YouTube ilichukuliwa kuwa yenye manufaa mengi zaidi katika afya ya kiakili, ikifuatwa na Twitter na kisha Facebook.

Snapchat na Instagram zilikuwa na alama za chini kabisa kwa jumla.

Shirley Cramer, afisa mkuu mtendaji wa RSPH, alisema: “Inashangaza kuona Instagram na Snapchat zikiorodheshwa kuwa na madhara zaidi kwa afya ya kiakili na hali nzuri ya vijana – majukwaa haya mawili sana huangazia sura na sifa nzuri na mtu. Mitandao hii miwili inaonekana kuwafanya vijana wengi wajihisi kwamba hawatoshi au wana mapungufu fulani na hivyo kuwaongezea wasiwasi.“.

By Godfrey Mgallah

Meya wa Arusha na wenzake kufikishwa Mahakamani

$
0
0

MEYA wa Jiji la Arusha, Kalist Lazaro na pia baadhi ya madiwani na viongozi wa dini waliokamatwa katika tukio la kutoa misaada kwenye shule ya Lucky Vincent iliyopo mjini Arusha sasa wako katika hatari ya kufikishwa mahakamani kukabiliana na mashtaka.


Hata hivyo, hatua hiyo ya kushtakiwa kwa viongozi hao itatokana na matokeo ya uchunguzi unaoendelea kufanywa na jeshi la polisi na hivyo, bado haijawekwa wazi ni makosa gani watakabiliana nayo pindi wakifikishwa kortini.

Viongozi hao na ujumbe wao wenye jumla ya watu 13 walikamatwa juzi wakati wakiwa katika Shule ya Awali na Msingi ya Lucky Vincent na hadi kufikia jana jioni, bado walikuwa wakishikiliwa katika mahabusu ya polisi.

Wengine wanaotajwa kuwamo katika kundi hilo ni pamoja na viongozi wa Shirikisho la Wamiliki na Mameneja wa Shule na Vyuo Binafsi (Tamongsco), Kanda ya Kaskazini. Walikwenda shuleni hapo kutoa rambirambi kutokana na tukio lililohuzunisha taifa hivi karibuni la ajali ya basi la shule hiyo, iliyopoteza maisha ya watu 35, wakiwamo wanafunzi 32.

Aliyeashiria kuwapo kwa uwezekano wa kushtakiwa kwa viongozi hao ni Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Yusuph Ilembu, aliyeiambia Nipashe jana kuwa bado wanawashikilia watu 13 waliowakamata juzi.

Kamanda Ilembu aliongeza kuwa hadi kufikia jana, bado walikuwa wakiendelea kuwahoji masuala kadhaa wahusika ili baadaye taratibu zingine zifuate, ikiwa ni pamoja na kuwafikisha mahakamani au vinginevyo.

Aidha, Kamanda Ilembu alikataa kuwataja majina watuhumiwa wanaowashikilia kwa maelezo kuwa bado wanaendelea kuwahoji.

Hata hivyo, waliokuwapo katika tukio la kutoa rambirambi juzi kwenye shule hiyo ya Lucky Vincent walifahamika kuwa ni pamoja na Meya Lazaro na viongozi kadhaa wa dini.

Rambirambi iliyotarajiwa kutolewa ilifuatia ajali hiyo ya gari ya Mei 6, mwaka huu na kuwaua wanafunzi 32, walimu wawili na dereva waliokuwa wakienda kufanya mitihani ya ujirani mwema na wanafunzi wenzao wa darasa la saba wa Shule ya Tumaini Junior iliyoko wilayani Karatu.

Hata hivyo, rambirambi hiyo haikuweza kutolewa baada ya polisi kuwakamata kwa kile kilichoelezwa na Kamanda Ilembu kuwa wahusika walifanya mkusanyiko/mkutano usio na kibali katika eneo hilo.

Pia katika tukio hilo, waandishi wa habari 10 walikamatwa pia na kuachiwa muda mfupi baada ya kufikishwa kituo kikuu cha polisi cha mkoa.

Ushauri: Nilizaa na Dada Yangu, JE Nitapata Laana au Ni Sawa Tu ?

$
0
0

Kwetu tumezaliwa wawili tu mapacha , Mimi na Dada yangu, baba yetu alikua mkali na mkoloni sana hatukuruhusiwa kutoka nje kabisa labda shule tu na tulienda na Gari la nyumbani Tulikua tukiishi mkoani na ilikua ni mwishoni mwa miaka ya tisini Tukiwa form six, nadhan tulikua tumefunga shule tukiwa home, Dada yangu aliletewa mkanda Wa kikubwa na Rafiki yake baada ya Rafiki kuondoka tukawa tunauangalia sielewi ni nini kilitupata tukajikuta tumezini, mm kwangu ilikua ni Mara ya kwanza ila nadhan mwenzangu alikua tayari keshafanya huko nyuma Ikawa kila siku tunafanya wazazi wakiondoka. 

Kuja kustuka haoni siku zake akamwambia mama naye akamwambia baba Sijui niwaeleza lugha gani muweze kuelewa kilichotokea Ilikua ni mtiti akaambiwa aeleze ni nani aliempa mimba akawa anasingizia wanafunzi wenzie shuleni, wakifika shule anababaika anashindwa kutaja basi akafukuzwa shule hata mtihani Wa mwisho hakufanya Wakati hilo halijaisha biashara za Mzee zikaanza kuyumba vibaya vibaya na alikua na deni kubwa sana benki wakaja kuuza nyumba tunayokaa bado haikutosha Nyumba tuliyohamia ikapigwa mnada pia Mzee akapata stroke, tukaanza kuhangaika nae kila hospital, Mtihani Wa mwisho ulipofika sikuweza kufanya kitu nilikua naangalia tu makaratasi maana tulitoka maisha ya juu ghafla tukaporomoka hadi chini ndani ya miezi 9-12. 

Mzee akawa amefariki tukaenda kuzika kijijini Hakukua na chochote kilichobaki mjini si nyumba nini Tumezika kama Leo wiki moja mbele Dada akajifungua mapacha Wa kiume kama sisi tulivyo mapacha Baada ya ndugu kutawanyika na miezi minne kupita tukiwa bado kijijni maana tulipanga tuishi huko huko mjini hatukua na chochote mama aliniita akaniambia niende mjini nikaangalie matokeo yangu ndipo tunaweza kupanga tufanye nn Matokeo yalikua mabaya Usiku mmoja mama na babu wakaniita babu akaniambia chukua hawa ngombe ukauze wote utuachie watano tu Hii ndio mali pekee Mzee wako alioacha, walikua ngombe 200 Nikapewa baba zangu wadogo tukaenda mnadani tukauza nikapata pesa nyingi mno Nikaja dar kutafuta maisha na kiasi hicho cha pesa 

Nikawa nanunua ngombe mkoani naleta dar hadi mtaji ukaongezeka mara tatu Nikafungua biashara zingine na nikanunua kiwanja boko na nikajenga Nikarudi kijijini nikamchukua Dada yangu na watoto had I mkoani wakiwa na miaka mitano nikampangia nyumba na kumfungulia biashara lengo ni watoto waanze la kwanza hivyo walitakiwa maandalizi ya nursery Mama tulimwacha kijijini alikataa kabisa kuja mjini Siku moja tuliagiza pombe walau tusherehekee mafanikio maana hatukumini kama tungefika hapo Baada ya kunywa sana nikaona nikalale akanifuata chumbani na kuanza romance nikamzuia nikamwambia hatupaswi kurudia kosa hili, tushukuru huenda ni mpango Wa mungu Mzee kufariki kabla hajajua mm ndio nilikupa mimba Na bado hatujui siku mama akijua itakuaje Akaniambia yeye hataki mwanaume mwingine zadi yangu na kwamba ananipenda mm tu Nakuja kustuka hivi na boxer na vest ameshavitoa huku akiendelea na zoezi moyo wangu ulishakataa ila mwili ukawa dhaif tukawa tumezini. 

Tangu hapo huwa anakuja dar tunafanya nashindwa kuresist ile pressure Nikapata msichana mmoja dar alipokuja dar akatukuta nae kwangu alifanya fujo na kumpiga vibaya yule binti hadi majirani wakaniambia kumbe ulishaoa husemi, mi nashindwa kuwajibu Nikapata demu mwingine Dada yangu alipokuja akakagua simu akaona SMS za mapenzi akampigia akamtukana sana akamwambia yule demu eti nimeoa na nna watoto wawili demu akakimbia kimoja Nimepata Dada mmoja Wa benki tunapendana sana na tumepanga kuishi pamoja lakini kikwazo ni Dada yangu Akigundua tu ni balaa Sijui nimwambie huyu banker in advance kuhusu ili tatizo? Marafiki naombeni ushauri Maana mama mwenyewe anataka nioe nitulie 

Dada anasema nisijidanganye kuoa ni kazi bure Nikimwambia tafuta mtu wako na wewe uolewe hanielewi. 

Nifanye nini ? Naogopa laana, naomba mnishauri.

GAMBO Azungumzia Siasa Tukio la Ajali ya Basi la Wanafunzi wa Lucky Vincent..!!!

$
0
0

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo amesema kuwa tukio la msiba wa wanafunzi wa Lucky Vincent uliotokea hivi karibuni halikutegemewa na halipaswi kutumika kujinufaisha kisiasa, huku Meya wa Jiji la Arusha akiendelea kushikiliwa na polisi.

Meya huyo, Kalist Lazaro; viongozi wa dini na baadhi ya viongozi wa Shirikisho la Umoja wa Wamiliki wa Shule Binafsi Kanda ya Kaskazini (Tamongsco) wanashikiliwa na polisi baada ya juzi kukamatwa walipokwenda kutoa rambirambi katika shule hiyo.

Akipokea rambirambi kutoka kwa wadau mbalimbali wakiwamo taasisi ya Wezesha Sasa walitoa Sh4.4 milioni, Umoja wa Wauza Mafuta Rejareja (Tapsoa) na Shule ya Dar es Salaam Independent (DIS), Gambo alisema jana kuwa kila mchango uliopokelewa utatumika kwa malengo yaliyokusudiwa na hakuna pesa itakayopotea.

“Tusiangalie waliofiwa tu lakini tunapaswa tuangalie na hawa wanafunzi watatu walionusurika Mungu ana mipango nao na lazima tufanye jambo kwao kwa sababu nao ni sehemu ya waliohusika katika ajali iliyopoteza maisha ya watu 35,” alisema.

Alisema kelele zinaendelea juu ya matumizi yasiyo sahihi ya fedha zote zilizochangwa hazina msingi kwa sababu wakati kuna watu waliahidi, lakini hawakutoa kwa wakati na shughuli zisingeweza kusimama na Serikali ilitumia busara kutafuta fedha ili shughuli za kusafirisha miili na mazishi inafanikiwa.

POLISI Waua Majambazi Matatu Katika Vita ya Majibizano ya Risasi Iliyoshangaza Watu Mwanza..!!!

$
0
0
WATU watatu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi wameuawa kwa risasi jijini Mwanza jana katika kile kinachoelezwa kuwa ni matokeo ya vita kali ya kurushiana risasi baina ya watuhumiwa hao na askari wa Jeshi la Polisi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi, alisema tukio hilo limetokea katika eneo la viwanja vya ST. Mary’s Mtaa wa Ndofe wilaya ya Nyamagana, ambako polisi walikuwa wameweka mtego baada ya kupata taarifa kuwa watuhumiwa walipanga kufanya uhalifu.

Ilielezwa zaidi kuwa polisi waliwafikia watuhumiwa baada ya kumkamata mganga wa kienyeji aitwaye Ayubu Nyamweru (45), mkazi wa Katoro mkoani Geita, ambaye alikutwa akiwa na kompyuta mpakato tatu na simu moja aina ya Sumsung vilivyokuwa imeibwa katika tukio la kuvunja nyumba maeneo ya Nyamanoro.

Tukio la kuporwa kwa vitu hivyo lilihusisha pia kuporwa kwa bastola aina ya Duty CZ 75P-07 na fedha, siku ya Mei 13 mwaka huu na kufunguliwa jalada lenye namba NY/IR/3773/2017.


Ilielezwa na polisi kuwa baada ya mganga Nyamweru kuhojiwa, alitaja wenzake anaoshirikiana nao katika kufanya matukio mbalimbali ya uvunjaji na unyanga’anyi jijini Mwanza na maeneo ya jirani.

Ilielezwa kuwa kufuatia maelezo ya mganga huyo, ndipo polisi walipofuatilia na kumkamata mtuhumiwa mwingine (Benedicto Thobias) kabla ya kuweka mtego uliosababisha kutokea kwa majibizano ya risasi baina yao na majambazi hao.

Akizungumza jana, Kamanda Msangi aliwataja watuhumiwa wlaiofariki kwa kupigwa risasi katika mapambano hayo kuwa ni Benedicto Thobias ambaye ni mkazi wa Nyamatara Buhongwa na wengine waishio pia Mwanza ni Mabula Segeja na Charles Thomas.

 “Mnamo Mei 19 mwaka huu, katika viwanja vya ST. Mary’s mtaa wa Ndofe wilaya ya Nyamagana walifika watu watano ambao walikuwa ni wenzake na mtuhumiwa Benedicto. Askari walipowaamuru wajisalimishe walikaidi amri hiyo na kuanza kufyatua risasi uelekeo wa askari,” alisema Msangi na kuongeza:

“Ndipo askari wakajibu mapigo na kuwajeruhi majambazi wawili na zile risasi walizozipiga ziliweza kumjeruhi mwenzao (Benedicto) aliyekuwa amewapeleka askari kwenye eneo lile… wote watatu walifariki dunia wakati wanapelekwa hospitali kwa matibabu.”

Aidha, Kamanda Msangi alisema kuwa katika tukio hilo, polisi walifanikiwa kukamata silaha mbili ambazo ni bastola aina ya Duty CZ 75P -07 yenye namba B.512637 ikiwa na risasi 15 na magazini mbili na short gun iliyofutika namba ikiwa na risasi mbili na maganda mawili ya risasi, mali ya Suleimani Waziri aliyekuwa akiimiliki kihalali.

Kwa mujibu wa Kamanda Msangi, miili ya watuhumiwa hao imehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando kwa ajili ya uchunguzi na utambuzi zaidi wakati msako wa kuwasaka wenzao waliotoroka na wengine waliokuwa wakishirikiana nao bado ukiendelea.

Credit - Nipashe

UTATA Waibuka Wakili Aliyefia Sebuleni Dar..Maiti Yake Yakutwa na Damu Kichwani...!!!

$
0
0

WAKILI wa kujitegemea, Noel Ndalu, amekutwa amefariki sebuleni nyumbani kwake Sinza jijini Dar es salaam, kifo ambacho kimeacha maswali kadhaa kutokana na mazingira yake.

Jana, Nipashe ilifika nyumbani kwa wakili huyo aliyekuwa akiishi Sinza kwa Remmy wilayani Kinondoni na kupata simulizi zenye kuibua maswali juu ya kifo hicho.

Baadhi ya maswali hayo ni pamoja na sababu za kifo chake kilichoonekena kuwa cha ghafla, hasa kwa kutambua kuwa kazi zake huhusisha kesi zitokanazo na masuala mbalimbali ya migogoro ya kisheria wanayokumbana nayo wateja wake.

“Inasikitisha sana…kifo chake ni cha ghafla na kwakweli hatujui ni kitu gani kimemkuta…labda alikuwa akisumbuliwa na maradhi kama ya kifafa ambayo wakati mwingine huwafanya watu wanaoishi peke yao wapoteze maisha kwa namna hii. Hakuna anayejua kwakweli,” mmoja wa majirani aliiambia Nipashe kuhusiana na taarifa za kifo cha wakili huyo.

Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, Suzan Kaganda, hakuweza kuzungumzia tukio hilo jana baada ya kueleza kuwa ametingwa na kikao, lakini baadhi ya majirani wameeleza kushangazwa na kile kilichomtokea mwenzao huyo.

Akizungumza na Nipashe, mama mwenye nyumba aliyokuwa amepanga wakili huyo, iliyopo katika Mtaa wa Mtendaji, Salama Shaaban (50), alisema Wakili Noel alikutwa amefariki sebuleni kwake juzi majira ya saa 4:00 asubuhi.

Alisema mara ya mwisho kuonana na mpangaji wake huyo ilikuwa ni Jumanne, saa 12:00 jioni wakati wakili huyo akimkabidhi stakabadhi ya uniti za umeme wa Luku aliokuwa amenunua.

“Jumanne alikuja hapa akaniambia mama nimekuletea umeme, nikamwambia ahsante mwanangu na alikuwa ni mzima wa afya...na tangu siku hiyo nikawa sijamuona kwa sababu anaishi upande wa pili wa nyumba yangu na ana geti lake,” alisema Salama.

Alieleza kuwa, hawakuwa na kawaida ya kuonana mara kwa mara na ndiyo sababu hakushtuka kutomuona kwa siku zote hizo.

“Hapa wako wapangaji wawili, marehemu na mwingine. Sasa jana asubuhi, nikiwa ndani kwangu, alikuja mpangaji mwenzake, akaniambia mama simu inaita muda mrefu ndani kwa Noel na hakuna anayepokea na yeye hajamuona akitoka,” alisema.

Alisema baada ya kupewa taarifa hizo, alitoka yeye na kijana wake kwenda hadi kwenye mlango mkubwa wa wakili Noel na kuanza kugonga. Walifanya hivyo kwa muda mrefu bila majibu na ndipo nao wakingiwa na wasiwasi.

“Chini ya mlango kuna uwazi hivyo mwanangu aliamua kuchungulia, akaniambia mama sioni kitu lakini nasikia harufu ya kitu kilichooza inatoka ndani,” alisema Salama.

Alisema mtoto wake huyo alichukua fimbo ndefu na kuipitisha chini ya mlango ambao upo karibu na dirisha kwa ajili ya kusukuma pazia ili waweze kuchungulia dirishani.

“Tulifanikiwa kusogeza pazia na tukachungulia ndani… tukamuona Noel akiwa amelala chali chini ya sakafu kuelekea mlango wa chumbani na kwenye paji lake la uso kulikuwa na damu zimechuruzikia kwa chini,” alisema.

Alisema baada ya kuona hali hiyo, waliamua kwenda kuwaita wajumbe wa mtaa wao ambao walifika na kushuhudia tukio lile kabla ya kutoa taarifa katika Kituo cha Polisi Mabatini.

“Baadaye Polisi walikuja na gari. Waliamuru mlango uvunjwe, wakaingia ndani na kuuchunguza mwili. Wakakuta amechanika kwenye paji la uso wake,” alisimulia Mama Salama.

Alisema pia alikutwa amevaa kaptura na hawakukuta silaha ya aina yoyote. Baada ya hapo polisi waliuchukua mwili huo na kwenda kuuhifadhi katika Hospitali ya Mwananyala.

Akisimulia namna anavyomfahamu, Salama alisema wakili huyo binafsi ambaye alikuwa na ofisi yake Temeke jijini Dar es Salaam, ameishi kwenye nyumba yake kwa miaka mitatu.

Alisema awali alikuwa akiishi na mwanamke ambaye aliondoka miaka miwili iliyopita, na hivyo hadi umauti ukimkuta alikuwa akiishi peke yake.

“Mke wake aliondoka na mtoto wa miezi miwili. Kwa hiyo alikuwa akiishi peke yake,” alisema Salama.

Alisema baada ya kifo hicho, mjomba wake alifungasha mali za wakili huyo na kuondoka nazo na kwamba jana, waliuaga mwili wake katika Hospitali ya Mwananyamala na kusafirisha kwenda Dodoma kwa maziko.

“Baba yake anaishi Dodoma hivyo leo (jana) walienda Mwananyamala saa 4:00 kwa ajili ya kuuchukua mwili kuusafirisha,” alisema.

MAWAKILI WAMLILIA
Aidha, Chama cha Wanasheria Tanganyika(TLC), kilitoa taarifa ya kifo cha aliyekuwa mwanachama wao mwenye namba ya usajili 4644, Noel Ndalu .

Taarifa iliyotolewa na uongozi wa TLC kwa wanachama wake, ilieleza kuwa, mwanachama huyo alifariki Jumanne ya wiki hii, Mei 16 na kwamba aliagwa jana katika Kanisa la Kaloloni Chang’ombe na baadae kusafirishwa kuelekea mkoani Dodoma kwa maziko

ALIYEKUWA Mkuu wa Mkoa Katika Serikali ya Kikwete Aionyooshea Serikali ya JPM Kidole..Aitahadharisha Juu ya Machafuko Kutokea..!!!

$
0
0

Wakati watu wasiojulikana wakiendelea kuua viongozi wa vijiji licha ya Jeshi la Polisi kuweka kambi, aliyekuwa mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Stephen Mashishanga ameitaka Serikali ijitathmini akisema matukio hayo ya mkoani Pwani yanaitia doa.

Amesema vyombo vya ulinzi na usalama havina budi kufanya uchunguzi wa kina na kuhakikisha mauaji hayo yanakomeshwa mara moja ili shughuli za uzalishaji mali ziendelee kama kawaida, badala ya wananchi kuishi kwa hofu ya kutofahamu nani atafuata katika orodha ya wanaosakwa kuuawa.

Watu 31 wameshauawa katika kipindi cha kuanzia Mei mwaka jana na mauaji ya viongozi wa vijiji yamekuwa yakishabihiana, huku askari wa Jeshi la Polisi wakiuawa katika mashambulizi.

Viongozi 15 wa serikali za vijiji na vitongoji vya wilaya za Mkuranga, Rufiji na Kibiti, polisi kumi, watumishi wawili wa Idara ya Maliasili, mwanachama mmoja wa CCM na watu watatu waliokuwa wamevaa nguo za kike wameshauawa katika kipindi hicho.

Hadi sasa, Jeshi la Polisi halijaeleza kama wanaofanya mauaji hayo katika vijiji hivyo, ambavyo baadhi vinapakana na hifadhi za taifa, ni majambazi, magaidi au majangili.

“Hatupendi kuona haya yanayotokea yakitendekea na kuendelea kusikika kila siku kana kwamba hatuna vyombo imara vya ulinzi na usalama,” alisema Mashishanga alipozungumza na gazeti hili katika Mkutano Mkuu wa 22 wa Wanahisa wa Benki ya CRDB unaomalizika leo jijini Arusha.

Jeshi la Polisi limeweka kambi katika Kijiji cha Jaribu katika jitihada za kukabiliana na mauaji hayo na Wizara ya Mambo ya Ndani imetangaza katika bajeti yake ya mwaka 2017/18 kuwa itaunda mkoa maalumu wa kipolisi utakaojumuisha wilaya hizo tatu, lakini watu hao wameshaua makada wawili wa CCM na kujeruhi watu wawili tangu Waziri Mwigulu Nchemba atangaze uamuzi huo.

Katika tukio la wiki hii, watu wasiojulikana walimuua kwa risasi mwenyekiti wa CCM wa Tawi la NjiaNne, Iddy Kirungi aliyekuwa akijaribu kukimbia baada ya kuwaona wauaji waliokuwa wamemjeruhi mtoto wake.

Mtoto huyo alikuwa akielekea bafuni na inaonekana wauaji walidhani kuwa ni mwenyekiti huyo na kumrushia risasi. Siku tano kabla ya tukio hilo, watu hao walimuua kwa risasi aliyekuwa katibu wa CCM wa Kata ya Bungu, Alife Mtulia wakati akielekea bafuni kuoga.

“Ni aibu kwa kinachoendelea. Serikali iangalie imekosea wapi au wananchi wake wamefanya nini hadi hali hiyo ikatokea na ikomeshe matukio hayo,” alisema Mashishanga, ambaye kwa nafasi ya ukuu wa mkoa alikuwa mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama.

Kwa uzoefu wake, alisema huenda dhuluma ikawa chanzo hivyo uchunguzi ufanywe haraka na kurekebisha kasoro zitakazobainika ili wananchi wa mkoani humo waishi kama ilivyo maeneo mengine.

“Wakati mwingine viongozi wanajisahau katika maamuzi yao. Bila kujua wanaweza wakawa wanapandikiza chuki na kusababisha kisasi ambacho kinaweza kuhusisha vifo vya namna hii,” Mashishanga alieleza shaka yake.

Maeneo yenye shaka, alisema mkuu huyo wa zamani, ni masuala ya uhusiano hasa wa ndoa, mchakato wa uteuzi wa wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya vyama kwa ngazi za wilaya au uporaji mali kwa kutumia mamlaka ndiyo yanaweza kusababisha mauaji hayo.

Mashishanga pia aliipongeza Serikali ya Awamu ya Tano kwa kurudisha imani ya wananchi katika masuala mbalimbali.

“Ni kazi ngumu kuondoa wasiwasi na shaka ya wananchi kwa muda mfupi, lakini Serikali ya awamu hii imeweza. Hata mwananchi wa kawaida ana uhakika wa kufanikisha akitakacho bila kusumbuliwa kama ilivyokuwa awali,” alisema kiongozi huyo aliyehudumu kwenye Serikali ya Awamu ya Tatu na Nne.

Mashishanga pia alizungumzia kuacha kazi kwa aliyekuwa mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Saidi Meck Sadiki akisema kumetokana na tathmini binafsi iliyofanywa na kiongozi huyo na kuona hawezi kuendana na kasi iliyopo.

Credit - Mwanachi

HIZI Hapa Ajenda Tano Kuu Zitakazowasha Moto Kikao cha Wakuu wa Nchi za Afrika Mashariki Leo..!!!

$
0
0

Baada ya kuahirishwa mara tatu, hatimaye Mkutano wa 18 wa wakuu wa nchi zinazounda Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), leo unaanza kwa kujadili ajenda tano kubwa, ikiwamo inayosababisha nyufa mpya katika ujenzi wa jumuiya hiyo.

Ni mwelekeo gani jumuiya hiyo inapaswa kuchukua, hasa baada ya kushuhudia kusuasua kwa miradi mikubwa katika umoja huo, ni moja ya masuala makubwa yatakayoibua mijadala mizito katika mkutano huo.

Kuna minong’ono kuwa suala la mwelekeo mpya ambao jumuiya inapaswa kuchukua, limesababisha mvutano kiasi cha kutoelewana kwa baadhi ya wakuu wa nchi wanachama wa EAC, ambayo miaka ya hivi karibuni imekuwa ikishindwa kutosheleza bajeti yake.

Mkutano huo unafanyika wakati nchi wanachama zikiwa zimegawanyika kuhusu Mkataba wa Ushirikiano wa Kiuchumi na Umoja wa Nchi za Ulaya (Epa).

Wakati Kenya na Uganda, kwa upande mmoja, zinasukuma kwa nguvu zote jitihada za kuridhiwa kwa mkataba wa Epa, Tanzania inaongoza kundi linalopinga mkataba huo.

Tanzania imeshatamka rasmi kwamba haitasaini mkataba huo ambao unaruhusu, pamoja na mambo mengine, bidhaa kutoka nchi za Afrika Mashariki kuingia Ulaya bila kodi.

Katika utaratibu huo pia, baadhi ya bidhaa kutoka Tanzania zitaweza kuingia katika ukanda huo bila kutozwa kodi huku baadhi ya bidhaa kodi ikiondolewa taratibu kwa muda wa miaka 25.

Tanzania inauona mkataba huo kuwa unaigawa jumuiya kwa ukoloni mamboleo na kwamba utaua kabisa ubunifu, viwanda vya ndani na kugeuza ukanda huu kuwa wa kuzalishaji malighafi. Tanzania inaamini kwa sasa hakuna mwanachama wa EAC aliye tayari kushindana kiuchumi na nchi za Ulaya.

Septemba mwaka jana, wakuu wa EAC walikutana wakati Tanzania ikionyesha upinzani mkali kwa mkataba huo. Ni katika mkutano huo wa 17 ndipo walikubaliana kuwapa wataalamu wa uchumi kutoka serikali za nchi wanachama muda zaidi wa kuwasiliana ili kuangalia upya misimamo yao na kukutana tena Januari.

Hadi sasa hakuna dalili kwamba nchi hizo zitafikia makubaliano ya pamoja, na tayari Bunge la Tanzania, ambalo kiutaratibu ndilo linaloridhia mikataba yote ya kimataifa, limeshapiga kura kuizuia Serikali kusaini mkataba huo.

Habari kutoka ndani ya vikao vya matayarisho ya mkutano huo wa 18, zinadai kuwa suala la Epa halitarajiwi kupewa kipaumbele. Tanzania imeendelea kusisitiza kwamba nchi za EAC zisisaini Epa mpaka faida na hasara zake zitakapowekwa wazi.

Sudan Kusini

Suala jingine linalotarajiwa kuibua mjadala ni taarifa ya maendeleo yaliyofikiwa katika kuiingiza Sudan Kusini katika EAC. Wakuu hao wataamua kama wakati mwafaka umefika wa kuikubali moja kwa moja nchi hiyo ifikapo Julai mwaka huu.

Tayari Sudan Kusini imeteua wanachama wake wa kujiunga na Bunge la Afrika Mashariki (Eala) na Mahakama ya Afrika Mashariki kama inavyoelekezwa katika mchakato wa kuikubali nchi hiyo.

Marais hao wanatakiwa kutoa mwelekeo kama nchi hiyo inaweza ikateua makamishna wa EAC na kutoa majina ya watakaoiwakilisha katika nafasi za kiutendaji ndani ya sekretarieti na jumuiya.

Bajeti ya Jumuiya

Jambo jingine muhimu ni mfumo mahususi wa ugharamiaji bajeti ya Jumuiya. Mawaziri wa jumuiya, isipokuwa Burundi, wamekubaliana kuendelea kwa mfumo wa sasa wa uchangiaji sawa na kuweka vikwazo kwa watakaoshindwa kulipa.

Nguo na viatu vya mitumba

Pia, katika meza ya mkutano wa leo utajadili suala la uzuiaji kwa awamu wa uagizaji wa nguo na viatu vya mitumba, ambao unafanyika kwa miaka mitatu mfululizo kuanzia mwaka 2016.

Marais pia wanatarajiwa kuipitisha kuwa sheria miswaada mbalimbali iliyojadiliwa na kupitishwa na Bunge la Afrika Mashariki kama wa Mfumo wa Usimamizi wa Forodha, wa Sheria ya Matumizi ya EAC na wa Sheria ya Matumizi ya Ziada ya EAC.

Soko la Pamoja

Wakuu hao wa nchi pia wanatarajiwa kujadili ripoti ya hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa Soko la Pamoja, moja kati ya hayo ni kuzitambua kwa pamoja hati za biashara kutoka kila nchi na suala la kuzuia kabisa utozaji kodi mara mbili kwa kampuni zinazofanya biashara kati ya nchi hizo.

Katika mkutano wa hivi karibuni wa Baraza la Mawaziri wa EAC liliiomba Tanzania kuharakisha mchakato wa kupitia upya mfumo wake wa kisheria na kumaliza mawasiliano ya ndani kuhusu ulinganishaji wa ada za vibali vya kazi ifikapo Septemba.

Ombi hilo limekuja kufuatia uamuzi wa hivi karibuni wa Serikali ya Tanzania kupunguza ada ya vibali vya ukaazi hadi dola 500 za Kimarekani kutoka dola 2,000 kwa raia wa Afrika Mashariki wanaotaka kukaa na kufanyakazi nchini.

Kenya, Uganda na Rwanda wamefuta kabisa ada ya vibali vya kazi, lakini Tanzania na Burundi hawajaridhia suala hilo.

AVEVA - Bado Tunanafasi ya Kuwa Mabingwa wa Ligi Kuu Kupitia FIFA..!!!

$
0
0

WAKATI Ligi Kuu Tanzania Bara inatarajia kumalizika leo, Klabu ya Simba rasmi imepeleka malalamiko yake katika Shirikisho la Soka Duniani (Fifa) ya kudai pointi tatu baada ya Kagera Sugar kumchezesha beki wake Mohammed Fakhi ambaye alikuwa na kadi tatu.

Katika mechi hiyo ya Ligi Kuu Tanzania Bara iliyofanyika Aprili 2 mwaka huu kwenye Uwanja wa Kaitaba Bukoba, wenyeji walipata ushindi wa mabao 2-1.

Baada ya mechi hiyo kufanyika, Simba iliwasilisha malalamiko katika Bodi ya Ligi Kuu na kupewa pointi tatu na mabao matatu lakini uamuzi huo utatenguliwa na Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji ndani ya muda mfupi.

Akizungumza na gazeti hili jana, Rais wa Simba, Evans Aveva, alisema katika barua yao hiyo wameieleza Fifa wanataka haki itumike kwa kuzingatia kanuni za ligi baada ya Kagera Sugar kumtumia mchezahi huyo ambaye alikuwa na kadi tatu za njano.

Aveva alisema kuwa wameamua kulifikisha suala hilo Fifa baada ya kuona vyombo vya hapa nyumbani vimewanyima haki yao.

"Ni kweli tumeshatuma malalamiko yetu rasmi tangu juzi (Jumatano) kwa njia ya nukushi na barua pepe, tukiwa tumepeleka vielelezo vyote muhimu," Fakhi katika mechi hiyo.

Rais huyo aliongeza kuwa wameamua kuwasilisha shtaka hilo la kadi tatu za njano na wakiweka kiporo usajili wa Mbaraka Yusuph ili kuepuka kujichanganya na hapo baadaye watawasilisha pia suala hilo katika chombo hicho cha juu duniani.

"Tunaamini hatujachelewa hata kama ligi inamalizika kesho (leo), tutaiangalia hiyo hukumu ya Fifa na tusiporidhika nayo tutakwenda CAS (Mahakama ya Usuluhishi ya Michezo," Aveva aliongeza.

Endapo Simba itashinda katika mchezo wake wa leo dhidi ya Mwadui FC utakaofanyika kwenye Uwanja wa Taifa na kushinda malalamiko yake huku ikiwaombea Yanga kufungwa dhidi ya Mbao FC leo itafanikiwa kutwaa ubingwa huo walioukosa kwa muda mrefu.

MAWAZIRI Watano Washikamana kwa Hoja Moja..!!!

$
0
0

Mshikamano, ndivyo unavyoweza kusema baada ya vichwa vinne kusimama bungeni kuokoa jahazi lisizame kufuatia wabunge kutaka kukwamisha bajeti ya Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji.

Ukiondoa waziri wa wizara hiyo, Charles Mwijage mawaziri waliomuokoa baada ya wabunge kumkomalia kutokana na mianya ya uingiaji wa biadhaa feki nchini kuwachwa bila udhibiti ipasavyo ni Mwigulu Nchemba, ambaye ni Waziri wa Mambo ya Ndani, Edwin Ngonyani (Naibu Waziri Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano), Seleman Jafo (Naibu Waziri wa Tamisemi) na Luhaga Mpina (Naibu Waziri Muungano na Mazingira).

Hoja ya bidhaa zisizo na ubora iliibuliwa na mbunge wa Wawi (CUF), Ahmed Juma Ngwali na kushika kasi wakati Bunge lilipoketi kama kamati chini ya Naibu Spika, Dk Tulia Ackson kupitia vifungu vya bajeti hiyo.

Kutokana na kubanwa huko, Mwijage alitishia kumuomba Rais John Magufuli na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ampe meli aina ya nyambizi ili azizamishe mashua zitakazoingiza bidhaa bandia.

Hata hivyo, majibu ya mawaziri wenzake yalimuokoa maana walishambulia kutoa ufafanuzi uliosababishwa Ngwali aliyekuwa ameshikilia shilingi mpaka ahakikishiwe majibu ya maana, akaamua kukubaliana na hoja zao.

ZANZIBAR: Watakaokula Mchana Hadharani Ramadhani Kukiona..!!!

$
0
0

SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar(SMZ) imetoa onyo kwa wananchi watakaokula hadharani katika kipindi cha mchana wakati wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

Hayo yalisemwa na Naibu Waziri wa Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma, Khamis Juma Maalim wakati akijibu swali la mwakilishi wa jimbo la Paje, Jaku Hashim Ayoub aliyetaka kujua serikali inatoa tahadhari gani kwa watu watakaobainika kula mchana wakati wa Mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Alisema utamaduni wa wananchi wa Zanzibar ni kuheshimu kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadhani kwa makundi yote ikiwemo wa dini tofauti. Alifahamisha kwamba utamaduni huo upo hata kabla ya Mapinduzi ya Januari 12 mwaka 1964 wa dini tofauti kuheshimu dini za watu wengine.

Alisema kazi ya kutoa elimu kuhusu ujio wa mwezi mtukufu wa Ramadhani imeanza kutolewa na Ofisi ya mufti ambayo ndiyo yenye jukumu la kushughulikia masuala ya mambo ya dini ya Kiislamu.

Alisema kazi kama hiyo imeanza kutolewa na maimamu wakuu wa misikiti mbalimbali Unguja na Pemba ikiwemo katika sala za Ijumaa ambazo hukusanya idadi kubwa ya Waislamu kwa wakati mmoja.

Alikiri kuwepo vijana wengi wanaoacha kufunga katika kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadhani na kula hovyo pamoja na kuvuta sigara. Maalim alisema zipo taarifa kwamba hoteli nyingi hufanya kazi wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhani ambapo wateja wake wakubwa ni vijana wa Kiislamu. Waislamu nchini wanatazamiwa kuanza mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani wiki ijayo ambapo ibada ya funga ni moja ya nguzo tano za dini ya Kiislamu

FEDHA za Lembeli Zilivyowavuruga Viongozi wa CCM..!!!

$
0
0

Wakati Rais John Magufuli akisisitiza kila mara kuwa maendeleo hayana itikadi za vyama huku akiwahimiza Watanzania kushiriki na kusaidia miradi ya maendeleo, hali inaonekana tofauti kwa baadhi ya viongozi na watendaji wilayani hapa.

Hii ni baada ya baadhi ya viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na idara za Serikali kumweka kiti moto Diwani wa Sabasabini, Emmanuel Makashi wakimhoji sababu za kusimamia ujenzi wa barabara kwa fedha zilizotolewa na Mbunge wa zamani wa Kahama, James Lembeli aliyehamia Chadema.

Barabara hiyo yenye urefu wa kilomita moja kutoka Kijiji cha Mseki, Kata ya Burugwa hadi Kituo cha Afya Burungwa, imejengwa kwa gharama ya Sh1.5 milioni, kati ya hizo Sh800,000 zikiwa zimetolewa na Lembeli.

Kiwango kingine kilitokana na michango ya wakazi wa kijiji hicho na wafanyabiashara waliokuwa wakiathirika kwa ubovu wa barabara hiyo, ambao kwa hiari walichangisha Sh500,000 kwa ajili ya mafuta ya greda ili kuunga mkono juhudi za Lembeli.

Miongoni mwa waliomweka kiti moto Diwani Makashi ambaye pia ni mfanyabiashara wa eneo la Mseki, ni Diwani mwenzake wa Burungwa ilipo barabara husika, Joseph Masaluta (CCM).

Waliochukizwa

Katika orodha ya waliochukizwa na kitendo cha diwani wa CCM kusaidia na kusimamia ujenzi wa barabara kwa fedha zilizotolewa na Lembeli, wamo baadhi ya watendaji wa Serikali na mbunge mmoja wilayani Kahama.

Akizungumzia sakata hilo, Masaluta ambaye barabara hiyo ipo ndani ya kata yake, alisema kitendo cha mwenzake kusimamia ujenzi huo kwa fedha zilizotolewa na mpinzanim siyo tu usaliti dhidi yake, bali hata kwa CCM.

“Tayari nimewasilisha jambo hilo ngazi za juu za chama na Serikali. Lazima hatua zichukuliwe,” alisema Masaluta.

Hata hivyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Ushetu, Michael Matomola alionekana kupingana na wanaohoji sababu za diwani huyo kusimamia mradi huo unaohusisha michango ya wananchi, akiwamo Lembeli ambaye ni mkazi wa Kijiji cha Mseki.

“Sioni tatizo kwa Lembeli kama mkazi wa Mseki kuungana na wenzake kujichangisha fedha kujenga barabara hiyo, kwa sababu ni rai ya Serikali kila mwananchi kushiriki kuchangia miradi ya maendeleo eneo lake,” alisema Matomola.

Akijibu tuhuma dhidi yake, Makashi alisema huo ulikuwa uamuzi wa wakazi na wafanyabiashara wa eneo hilo ambao baada ya kuchanga fedha walimuamini na kumkabidhi dhamana ya usimamizi.

“Lembeli ni mkazi wa Mseki, anawajibika kushirikiana na wananchi wenzake kuchangia miradi ya maendeleo. Tofauti zetu kiitikadi hazipaswi kuwa kikwazo cha maendeleo ya wananchi,” alisema Makashi.

Hoja hiyo iliungwa mkono na Mwenyekiti wa Serikali ya kijiji hicho, Paulina Ndutu aliyempongeza Lembeli kwa kuwa tayari kushirikiana na wanakijiji wenzake kutatua kero ya barabara.

Akizungumzia sakata hilo, Mbunge wa Ushetu, Elias Kwandikwa aliunga mkono kitendo cha Lembeli kuunganisha nguvu na wananchi kujenga barabara hiyo, lakini akasema fedha hizo zingewasilishwa ofisi ya mkurugenzi wa halmashauri ambaye ndiye angesimamia utekelezaji wa mradi huo.

Credit - Mwananchi

KUTANA na Watu wa Kabila la Hamar..Ambapo Mwanamke Hupenda Kuchapwa Kikatili na Mwanaume Anayetaka Kumuoa..!!!

$
0
0

Leo hii kwa mara nyingine tunakuja na utamaduni mwingine wa ajabu ambao bado ungalipo hadi sasa.

Kutoka hapa tulipo tunasafiri kwa ndege umbali wa maili 1,139 hadi kusini mwa Ethiopia, katika Bonde la Mto Ommo, linalopakana na mataifa ya Kenya na Sudan Kusini.

Katika eneo hilo lililotanda kutoka mji mkuu wa Ethiopia kuelekea Ziwa Turkana linalopakana na Kenya zinaishi jamii mbalimbali, ambazo nyingi bado zipo katika vijiji vya kienyeji vya zama zile za kale hata kabla ya kuingia kwa ustaarabu.

Hata hivyo, katika eneo hilo wengine wamehamia maeneo ya mijini ikiwamo Addis Ababa katika kile kinachoonekana kufumbuka macho kuhusu uwapo wa dunia nyingine mbali ya hiyo yao ya gizani pamoja na kusaka malisho bora zaidi.

Miongoni mwa jamii hizo ni Kabila la Hamar lenye wakazi 20,000 katika ukanda huo wenye utajiri wa rutuba na wingi wa mifugo, ambayo inaabudiwa mno hasa ng’ombe.

Kikubwa cha ajabu katika kabila hili ni kitendo cha wanawake kuruhusu kuchapwa fimbo au mijeredi kikatili mno na wanaume.

Wakati kichapo kikiendelea, badala ya wanawake hawa kukimbia ndio bado huchochea moto zaidi kwa kuwabembeleza wachapaji wao kuendelea kuwatandika tena na tena.

Hilo hutokea katika maisha ya kila siku na kuonekana hadharani wakati wa sherehe za jando, ambazo wanawake wenye umri mdogo hushuhudiwa wakichapwa ili kuonesha walivyo tayari kujitoa muhanga kwa wanaume.

Ng’ombe ni kitu muhimu mno kwa jamii ya Hamar, ushahidi ni uwapo wa maneno tofauti 27 yanayoeleza rangi ya ng’ombe kwa lugha ya kabila hilo.

Kabila hilo linaamini kuwa alama za makovu yanayotokana na vichapo hivyo ni ishara ya uwezo wa mwanamke kutoa pendo lote kwa waume zao.

Na humhakikishia ‘bima’ wanawake watakaojikuta katika matatizo ikiwamo ujane au njaa katika siku za usoni.

Kwamba hilo likitokea katika siku hizo za mbeleni watawageukia wale wanaume waliowachapa zama zile za ujana huko nyuma wajaribu kukumbuka makovu hayo na hivyo wawasaidie utatuzi wa shida zao.

Hivyo, inakuwa ngumu mno kwa mwanamume kukataa kumsaidia mwanamke huyo aliye katika uhitaji, shida au dharura.

Wanawake wanachapwa kama sehemu ya kutoka ujana kwenda utu uzima kwa wavulana, wakati wanafamilia wanawake wanapotangaza penzi lao kwa kijana wa kiume aliye katikati ya sherehe hizo. 

Baada ya sherehe, mvulana anakuwa mwanamume kamili, na anaruhusiwa kuoa. 

Utamaduni huo wa kikatili hujulikana kama Ukuli Bula na ulikutwa na mpiga picha wa Daily Mail, Jeremy Hunter.

Badala ya kukimbia, wanawake huwaomba wanaume kuwachapa tena na tena wakati wa sherehe hizo zinazofanyika katika bonde hilo la Mto Omo. 

Wanawake wa Hamar huvaa mitindo ya namna nyingi ikiwamo mavazi kutokana na ngozi ya mbuzi zilizonakishiwa kwa shanga zinazotokana na majani, huku nywele zao zikifunikwa kwa mchanganyiko wa grisi na udongo mwekundu.

Kwa wanaume, mitindo ya uvaaji wao ni ya kawaida isipokuwa upakaji rangi katika nyuso zao ambazo alama huonesha hadhi zao au upandaji wa ngazi ya kijamii.

Kufikia uanaume, wavulana wa Hamar hupitia taratibu mbili za sherehe za jadi: jando na kuwaruka ng’ombe dume.

Wakati wa mchakato wa kutoka ujana kwenda utu uzima. Wanawake huimba kwa vigeregere na shangwe, wakitangaza penzi lao kwa kijana huyo na nia yao ya kutaka wapate makovu kwa kutandikwa naye.

Huipaka miili yao kwa jibini kupunguza makali ya kichapo, ambacho huendeshwa tu na Maza – yaani wale wavulana waliopitia tayari jando.

Baadhi ya utandikaji huwa wa wenye huba lakini mwingineo huwa wa kikatili.

Lakini mara wanapochapwa, wasichana hawa ambao hawaruhusiwi kupiga kelele au kulia, katika hali ya kujivunia huonesha makovu yao kwa ufahari mkubwa– kama ushahidi wa ushupavu na uadilifu wao.

Hii ni aina ya sera ya bima ya kuja kuwasaidia hapo baadaye.

Hilo linalenga kubaini iwapo mvulana wa Hamar yu tayari kwa mruko wa kijamii kutoka ujana kwenda utu uzima.

Baada ya kufanikiwa kumruka ng’ombe dume – daima wakiwa watupu – mvulana wa Hamar, sasa anakuwa mwana jamii aliyepevuka – anaweza kuoa. Wakati wa hilo, anatarajiwa kukabidhi zaidi ya ngombe 17.

Breaking: Waziri Mkuu Mstaafu Frederick Sumaye Ajiuzulu Ujumbe wa Bodi CRDB

$
0
0

Arusha. Waziri Mkuu mstaafu na Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Mashariki, Frederick Sumaye, amejiuzulu ujumbe wa bodi ya Benki ya CRDB ili atekeleze zaidi majukumu yake ya kisiasa.

"Nina shughuli nyingi za kisiasa ambazo zitaninyima nafasi ya kuhudhuria vikao vya bodi.  Sipendi pia kuona CRDB ikihusishwa na msimamo wangu kisiasa. Hii ni taasisi huru ambayo ina wanahisa wengi ambao sitapenda kuona maslahi yao yakiingiliwa kutokana na siasa,"  amesema Sumaye.

Wastara Awaburuza Wasambaza Filamu Bongo Kortini

$
0
0

STEPS Entertainments, ambayo ni kampuni ya kusambaza filamu Tanzania, imepelekwa mahakamani na Wastara Juma, anayeidai kiasi kikubwa cha fedha baada ya kukataa kumlipa, Risasi Jumamosi limeambiwa.

Kwa mujibu wa chanzo, muigizaji huyo alipeleka kazi yake kwa kampuni hiyo ili asambaziwe kama wanavyofanya waigizaji wengi nchini, lakini licha ya kusubiri kwa muda mrefu, kampuni hiyo imeshindwa kumlipa na hivyo kumfanya kuamua kuipeleka kortini.

Akizungumza na Risasi Jumamosi, Wastara alikiri kuchukua hatua hiyo akidai amewapeleka katika Mahakama ya Mwanzo Ilala akitaka apewe fedha zake alizokataa kutaja kiasi chake, lakini akisema licha ya kupewa barua mbili za kuitwa mahakamani, hawajawahi kufika.

“Hapa ninavyoongea napewa barua ya tatu kwa ajili ya kuwapelekea, wasipofika tena mahakamani mali zao zitakamatwa na kupigwa mnada ili wanilipe,” alisema.

Juhudi za kuwatafuta wahusika wa Steps ziligonga mwamba baada ya msemaji wao, aliyejulikana kwa jina moja la Moses kutokuwepo ofisini, ingawa ofisa mmoja wa kampuni hiyo aliyeomba hifadhi ya jina lake, alikiri kampuni hiyo kudaiwa na kupokelewa kwa barua za Wastara.

“Mimi si msemaji, mwenyewe yupo lakini habari za Wastara kuleta barua nimezisikia, -ila jitahidi umuone hata mwanasheria wetu Cloud atakupa ukweli ulivyo,” alisema ofisa huyo.

Niliachana na Harmonize miezi 3 iliyopita lakini…- Wolper

$
0
0

Malkia wa filamu Jacqueline Wolper amedai aliachana na aliyekuwa mpenzi wake Harmonize miezi 3 iliyopita lakini waliamua kuficha kwaajili ya shughuli zao za kibiashara.

Muigizaji huyo ambaye alicheza vitendo kwenye video ya wimbo ‘Niambie’ wa Harmonize, amedai wakati kazi hiyo inatoka walikuwa tayari  wameachana lakini waliamua kushirikiana katika promo ya wimbo huo ambao unafanya vizuri.

“Nyie mnajua sisi tumeachana juzi? Tumeacha miezi mitatu iliyopita kabla hata ya wimbo wake Niambie haujatoka,” Wolper alikiambia kipindi cha Shilawadu cha Clouds TV.

Aliongeza ,“Sisi wenyewe tuliamua kukaa kimya kwa sababu kuachana sio kugombana kuna kesho mnaweza kushirikiana katika mambo mengine ya kibiashara,”

Hata hivyo muigizaji huyo aligoma kueleza sababu ya kuachana na muimbaji huyo anayefanya vizuri na wimbo ‘Happy Birthday’.

Mpenzi wa Rayvanny arudisha mwili wake wiki kadhaa baada ya kujifungua mtoto wa Kiume

$
0
0

Fahyma ambaye ni mpenzi na mama ya mtoto wa Rayvanny amekuwa akiwaekea mashabiki wake picha huku akionesha umbo lake ambalo limerudi wiki kadhaa baada ya kujifungua mtoto wake wa kwanza, Jaydan.

Mrembo huyu ambaye amejitambulisha kama teen mom amewapa wengi nafasi ya kufikiria kuwa bado hajafikisha miaka 20 na ikiwa ni ukweli basi inaonekana kuwa ameharakisha maisha yake.

Hata hivyo Rayvanny bado anampenda kulingana na mambo ambayo huyaweka kwenye mtandao wake wa Instagram. Tukiyaacha hayo, picha ambazo Fahyma ameziweka zinamuonesha kama amevalia nguo za kuogelea na kwa kweli amependeza sana.

Aliyofunguka Meya wa Arusha Baada ya Kuachiwa Huru Leo

$
0
0

Gumzo jingine la Arusha lilikua ni Meya wa Arusha, Madiwani, kiongozi wa Umoja wa wenye shule binafsi Arusha pamoja na viongozi wa dini kukamatwa na Polisi May 18 baada ya kufanya mkutano/kusanyiko kutoa rambirambi kwenye shule ya Lucy Vicent bila kibali.

Baada ya kuachiwa leo May 20 2017, Meya wa Arusha Kalist Lazaro ameongea na Waandishi wa habari na kusema >> ‘Nilikamatwa nikiwa kwenye majukumu yangu ya kawaida kabisa kama Meya wa Jiji, majukumu ya kijamii kwenye shule ya Lucky Vicent ambayo hivi karibuni ilipoteza Wanafunzi 32 kwenye ajali’

‘Tarehe 16 mimi kama Meya wa Jiji nilipewa taarifa na umoja wa shule binafsi Tanzania (TAMOSCO) na NewLIFEambayo ni NGO kutoka Ngaramtoni na baadhi ya watu wengine ambao walitaka kuhakikisha wanafikisha rambirambi zao kwa wafiwa’


‘Mimi ni Diwani wa Sokoni One, Wazazi waliofiwa wako 6 kwenye kata yangu, Diwani wa Olasiti ana familia 11 zilizofiwa… na Diwani mwingine Credo ana familia 6 zilizopoteza watoto, kwahiyo nikawaambia Madiwani wangu wahakikishe hizo familia zinakuwepo pale shuleni na mwenye shule akaandaa darasa moja ili tukio hilo lifanikiwe’

‘Moja ya vitu Wadau hao walitaka kuwe na maombi na nilimuandaa Padri waKanisa Katoliki, Mchungaji wa KKKT na kiongozi wa BAKWATA kutoka Olasiti, kabla ya zoezi la kukabidhi rambirambi mkononi kwa Wafiwa Polisi walivamia’



‘Mswali tulikua tunahojiwa ni kwanini fedha hizi hatujazipitisha kwa mkuu wa mkoa? nataka Watanzania wajue kwamba hakuna Kiongozi wa Serikali aliyefariki, walifiwa Wananchi wa kata zetu… mimi Meya wa jiji nimefiwa na Wananchi wangu’

‘Rambirambi za Wananchi zinatakiwa zipelekwe kwa waliofiwa na ndio maana siku nne zilizopita nilimtaka Mkuu wa mkoa aje hadharani awape rambirambi wale waliofiwa’ – Meya Kalist Lazaro

Habari Mpya Kuhusu Watoto Majeruhi Walioko Marekani Kwa Matibabu

$
0
0

Tunakumbuka watoto watatu waliojeruhiwa kwenye ajali ya basi la Wanafunzi Karatu, Arusha wako Marekani katika Hospitali ya Mercy, Sioux City Iowa kwa matibabu ambapo mtoto wa mwisho kufanyiwa upasuaji ni Doreenaliyefanyiwa upasuaji wa uti wa mgongo.

Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu ambaye amekuwa mstari wa mbele kwenye harakati za kuwasaidia watoto hawa amesema tayari amekwenda Lucky Vicent kuchukua mitaala maana watoto hao wataendelea kufundishwa wakiwa Hospitali Marekani ambapo kuna Walimu wa Marekani waliojitolea watashirikiana na Walimu wa Tanzania.

Nyalandu amesema :

  ‘Madaktari wanasema itachukua miezi kadhaa na kwa uhakika wanasema Doreen atachukua zaidi ya miezi sita akiwa katika uangalizi wa karibu Hospitalini”
Viewing all 104795 articles
Browse latest View live




Latest Images