Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104793 articles
Browse latest View live

Timu ya Ruvu Shooting Yapata Ajali

$
0
0

Msafara wa Timu ya Ruvu Shooting Umepata Ajali mbele Kidogo ya Singida wakiwa safarini kurejea Dar es Salaam.


Ruvu Shooting walikuwa njiani wakiokea Shinyanga walipocheza mchezo wao wa kumalizia msimu wa 2016/2017 wa Ligi Kuu soka Tanzania bara dhidi ya Stand United  


Taarifa kutoka kwa mmoja wa wachezaji waliokuwapo zinasema kwamba gari  hilo likiwa katika Mwendo, tairi lilipasuka na kusababisha gari kuhama Njia na kuparamia miti iliyokuwa jirani.

 

Hakuna mtu yoyote aliyeumia sana japo kuna mchezaji mmoja ambaye amepata Majeraha ya kawaida.

TFDA yakanusha soda ya Novida kuwa na virusi vya Ebola

$
0
0

Mamlaka ya Chakula na madawa (TFDA) imewataka wananchi kupuuza taarifa ambazo zimekuwa zikisambazwa kwa nyakati tofauti kwenye mitandao ya kijamii  kuwa kuna soda aina ya ‘Novida’ kutoka nchini Nigeria zimeingizwa nchini kinyemela na zina sumu ya virusi vya Ebola na tayari zimesababisha vifo vya watu 180 nchini humo.

Taarifa ya Mamlaka hiyo iliyotolewa mwishoni mwa wiki iliyopita ikiwa ni mwendelezo wa taarifa yake ya awali iliyotolewa mwezi Aprili 2017 inabainisha kuwa taarifa zinazosambazwa za kuingizwa soda zenye sumu ya Ebola haina ukweli na inapaswa kupuuzwa.

Kwenye taarifa hiyo, TFDA imeeleza kuwa inatambua uwepo wa soda ziitwazo Schweppes Novida zinazozalishwa na viwanda vya Coca-Cola Kwanza,Bonite na Nyanza Bottlers na soda hizo zinazalishwa kwa kuzingatia mifumo bora ya uzalishaji na zinakidhi vigezo vya usalama na ubora.

‘’Kama  ilivyo kwa bidhaa nyingize za chakula,vipodozi,vifaa vya tiba na vitendashi,soda za  Schweppes Novida ambazo zimesajiliwa na TFDA zimekuwa zikifuatiliwa katika soko kupitia mifumo liyopo ya udhibiti ili kujiridhisha kuwa zinaendelea kukidhi vigezo vya usalama na ubora kwa lengo la kulinda afya ya mlaji’’inabainisha sehemu ya taarifa ya TFDA .

Soda aina ya Schweppes Novida  kwa hapa nchini ilizinduliwa mwaka 2013, inatengenezwa na kusambazwa na viwanda vya Coca-Cola vilivyopo katika mikoa ya Dar es Salaam,Mwanza,Mbeya na Kilimanjaro.Soda hizi zinazopendwa na wateja zinatengenezwa kwa ujazo wa ml 300 na ml 500 zipo za aina ya Mandarin Cooler zenye ladha murua ya machenza na Pineapple Breeze zenye ladha ya Nanasi.

Baba Harmorapa afunguka kuhusu ndugu ‘feki’ aliyedai ana undugu na Harmorapa

$
0
0

Baada ya kijana aliyedai kusafiri kutoka Iringa kuja Dar es salaam kwaajili ya kumtafuta Harmorapa kwa madai ni ndugu yake na baadaye Harmorapa kumkataa, Baba wa Harmorapa amempigia simu mwanaye na kumuondoa shaka kuhusu kijana huyo.

Kijana huyo aitwae Frank Omary amedai aliamua kumtafuta Harmorapa baada ya mama yake kumwambia kwamba  rapa huyo ni ndugu yake ambaye wamechangia baba..

Akiongea na Bongo5 Jumamosi hii, Harmorapa amedai baada ya kuzagaa kwa taarifa hizo mtandaoni alipigiwa simu na baba yake mzazi.

“Nimetoka kuongea na baba yangu amesema siyo kweli, huyo mtu hamfahamu kabisa,” alisema Harmorapa ambaye yeye ni mtoto wa pili kwa upande wa baba yake. “Baba mwenyewe amemshangaa sana, hata jina la huyo jamaa halijui ndio maana akaniambia kwamba huyo sio ndugu yako,”

Harmorapa amemtaka kijana huyo kutafuta ishu nyingine ya kufanya na kuacha kupoteza muda katika mambo ambayo amedai hayawezi kumsaidia.

Askofu Gwajima Amjibu Mhubiri Aliyemtabiria Siku Atakayo Kufa

$
0
0

Dar es Salaam. Mchungaji wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima amesema hatakufa hadi pale atakapotimiza lile lililomleta duniani.  Ameyasema hayo leo wakati wa ibada ya Jumapili kanisani kwake ikiwa ni siku chache baada ya mhubiri mmoja wa kimataifa kutabiri kuwa Gwajima atakufa ifikapo 2018. “Mungu ndiye anajua siku saa na dakika ya kufa kwangu si mwanadamu,” amesema Gwajima.

Kama Unafanya Mambo Haya Lazima Utaishi Maisha Mafupi

$
0
0

Kwa kawaida maisha ya kibinadamu mwisho wake huwa ni kufa, hivyo kila mwenye pumzi hii leo mwisho wa maisha yake huishia kaburini.

Hata hivyo, kumekuwepo na viashiria fulani fulani ambavyo huweza kuashiria baadhi ya makundi fulani ya watu huenda wanaweza kuwa na muda mfupi wa kuishi duniani kutokana na sababu tofauti tofauti.

Miongoni mwa dalili ambazo huweza kuashiria mhusika anaweza kuwa na maisha mafupi duniani ni pamoja na hizi zifuatazo:


1. Watu wenye kupenda maisha ya anasa na starehe
Watu wa aina hii huwa katika hatari ya kupoteza maisha haraka hata kabla ya siku zao kutokana na kuwa na hatari kubwa ya kupatwa na magonjwa mbalimbali yakiwemo ya zinaa.

2. Wavutaji wa sigara.
Watu wanaovuta sigara huwa katika hatari ya kuishi maisha mafupi zaidi kuliko wale ambao hawatumii sigara kwani watu wa aina hii huwa katika hatari ya kukumbwa na saratani ambayo huweza kukatisha uhai wa mhusika hata kabla ya siku zake.

3. Kushinda umekaa siku nzima
Wale ambao huwa miili yao haina mazoezi kabisa nao huwa katika hatari ya kupoteza maisha mapema kutokana na kushambuliwa na magonjwa yasiyoambukiza kama vile shinikizo la damu, kisukari nk.

4. Unywaji wa pombe
Watumiaji wa vileo na huwa katika hatari ya kupoteza maisha yao mapema kutokana na mambo mawili makuu

a) Kupata ajali kutokana na kutumia vyombo vya moto wakati wakiwa wamelewa na baadaye kujikuta wanapoteza maisha.

b) Ugomvi ambao huweza kuibuka kutokana na mihemko ya vilevi wanavyokuwa wamekunywa na kuweza kusababisha ugomvi mkubwa. Mfano kupigana na chupa na baadaye kupoteza uhai.

5. Ulaji wa vyakula vya viwandani
Kuna wale ambao mara nyingi wamekuwa wakila vyakula vya makopo ambavyo vinapotumiwa mara kwa kwa mara huweza kuwa na madhara kadhaa likiwemo tatizo la saratani. Hivyo kundi hili nalo linaweza kuwa katika hatari ya kupoteza maisha kabla ya siku zao

Azam yamtema Boko

$
0
0

Tetesi za nahodha wa Azam FC na mshambulizi tegemeo John Bocco kuwa ametemwa na klabu yake ya Azam FC zinaendelea kuenea kwa kasi kila kona kwenye mitandao ya kijamii.

Kumekuwa na taarifa kwamba Azam FC wameamua kuachana na Bocco ambaye ameichezea klabu hiyo tokea ianzishwe.

Ambacho kinaonekana kuwashitua mashabiki ni Bocco kutupia maneno kadhaa ya mafumbo kwenye mitandao ya kijamii ambayo wengi wametafsiri kuwa huenda akawa anaaga.

Kesho ni Kesho: Macho na Masikio yetu yote ni Star TV! Je, Daudi Bashite Atajibu Maswali Haya?

$
0
0

By Pascal Mayalla

Wanabodi,

Hili ni bandiko la uhamasishaji, kesho make sure you don't miss this session!. Macho na masikio yetu yote ni Star TV, wakati kesho itakuwa ndio mara ya kwanza kwa Daudi Albert Bashite kujitokeza rasmi. Swali la msingi ni jee atajibu maswali haya, jee ungekuwa ni wewe ungependa kumuuliza swali gani?.

Kanuni ya kwanza ya haki kote duniani ni "No one is condemned un heard", yaani hakuna mtu anaweza kuhukumiwa bila kusikilizwa!, mtu yoyote mwenye tuhuma zozote, kabla hajahukumiwa, lazima kwanza apewe fursa ya kujieleza na kujitetea.

Wakati Tume ya Mwakyembe ilipomhukumu Edward Lowassa bila kumpa nafasi ya kusikilizwa, sisi wengine humu tuliilaani na kuishutumu kamati ile.

Ni kwa muda mrefu sana, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Daudi Albert Bashite, ametuhumiwa kwa tuhuma lukuki zikiwemo kughushi vyeti vya elimu, kutumia majina yasiyo ya kwake, kumiliki mali nyingi kuliko kipato chake kama mtumishi wa umma, kuvamia kituo cha Clouds TV akiwa na askari wenye silaha za moto na mavazi ya makirikiri etc. etc.

Hakuna hata wakati mmoja, mtuhumiwa huyu alipewa fursa ya kujieleza na kusikilizwa, bali alifikia hadi kuhukumiwa na Jukwaa la Wahariri TEF, bila kusikilizwa.

Lakini hatimaye kituo cha Televisheni cha Star TV, kwa busara kubwa, kesho siku ya Jumatatu, kimeamua kumpatia fursa na haki ya kusikilizwa tena akiwa live, mubashara moja kwa moja kutokea studio, kuanzia saa 1:30 asubuhi hadi saa 3:00 asubuhi.

Ni matumaini yangu, wapenzi wote wa haki za binaadamu, na wapenzi wa the right to information, wapenzi wa freedom of expression, wapenzi wa nothing but the truth, wataiunga mkono hatua hii nzuri ya Star TV, na wale wenye nafasi, watahakikisha, they never miss session, watasikiliza.

Mimi kwa upande wangu, kesho asubuhi nitasitisha shughuli zangu zote na kuelekeza macho na masikio yangu kule Star TV, ili nisikie mwenyewe kwa masikio yangu huku nikishuhudia kwa macho yangu, tone ya kujibu maswali, pulse ya adrenaline, na eye contacts,ili tukidanganywa, tuwaeleze members humu kipi amesema kweli na kipi amedangaya bila hata ya kutumia lie detectors.

Maswali ni mengi kumhusu Daudi Albert Bashite, swali ni jee maswali haya yatajibiwa?.
Muongozo kwa waulizaji maswali, wasiulize maswali kwa mtindo wa simple questions, bali wamuulize kwa mtindo wa interrogations, ili wauliza maswali kuonyesha, they did their homework well.

Mswali 10 ya mwanzo ni intro tuu kwa kumwambia ajitambulishe kwa simple questions na maswali kumi ya pili ni concrete questions zilizofungwa bila mlango wa kutokea, lazima mtu aseme ukweli.

1. Alizaliwa lini, wapi, na aliitwa kwa majina gani?.
2. Majina matatu ya Mzee Makonda ( baba) ni nani? .
3.Majina matatu ya Makonda (mtoto) aliyoandikishwa Primary pale Kolomije, alianza Shule ya msingi mwaka gani na kumaliza darasa la 7 mwaka gani?, shule gani na matokeo ni nini, alipasi au alifeli .
4. Baada ya kumaliza la 7 alijiunga na sekondari gani mwaka gani?.
5. Alitumia majina gani matatu sekondari, Pamba, alihitimu mwaka gani na alipata matokeo gani?
6. Alijiunga chuo cha Nyegezi kusomea nini, mwaka gani, kwa cheti gani na majina gani?.
7. Alijiunga Mbegani mwaka gani kwa cheti gani chenye majina gani? .
9. Alijiunga chuo cha Ushirika kusomea nini, mwaka gani kwa vyeti vipi, alihitimu lini?
Alizaliwa tar.15/02/1981 katika kijiji cha Koromije, wilaya ya Misungwi, mkoa wa Mwanza.
10. Alipoteuliwa alitumia majina gani.

Baada ya hapa, ndipo waje na interrogation questions

11. Uchunguzi wetu umeonyesha ulianza shule mwaka 1988 katika shule ya msingi Koromije ukitumia majina ya Daudi Albert Bashite, na mwaka 1991 ulirudia darasa la nne, kulitokea nini hadi akarudia darasa?.

12. Mwaka 1992 alifeli tena na hivyo akahamishiwa Mwanza mjini, ili aweze kusoma na kupata masomo ya jioni (tuition), na uliishi kwa Mama Kamese, jee ulifanya kosa gani hadi kufukuzwa kwa Mama Kamese na nguo zako kwenda kutupwa Stendi ya Kolomije, wasamaria wema wakaziokota na kuzipeleka kwa wazazi wako?.

13. Uchunguzi wetu umeonyesha Mwaka 1996 alihitimu darasa la 7 shule ya Nyanza, lakini hakuchaguliwa kuendelea na elimu ya sekondari katika shule ya serikali, uliwezaje kujiunga na Shule ya Sekondari ya Pamba mwaka 1997 kwa kidato cha kwanza wakati ulifeli Nyanza?.

14. Inasemekana Mwaka 2000 ulihitimu kidato cha 4 na kupata daraja sifuri (division zero) lakini mwaka 2001 akatumia cheti cha Ndg. Paul Christian Muyenge (chenye div.3 ya points 25) kujiunga na chuo cha uvuvi Nyegezi (Nyegezi Fisheries Training Institute) kwa masomo ya Certificate akahitimu mwaka 2002. Jee uliwezaje kupata cheti cha Paul Christian?, ulikiiba au alikupa mwenyewe?

15. Inasekana Mwaka huohuo 2002 ukitumia cheti cha Ndg. Paul Christian Muyenge, alijiunga na Chuo cha uvuvi Mbegani Bagamoyo kwa masomo ya Diploma ya uvuvi (ORDINARY DIPLOMA IN MASTER FISHERMAN, NTA LEV.6), na kuhitimu mwaka 2005, kwa nini uliendelea kutumia majina ya Paul Christian badala ya kubadili majina baada tuu ya kujiunga Nyegezi?.

16. Mwaka 2005 baada ya kuhitimu Stashahada yako ya uvuvi, kwa nini aliomba admission Chuo cha Kilimo Sokoine kusoma shahada kilimo bila kubadili majina ya watu?.

17. Baada ya kukosa nafasi kusoma Sokuone, uliwezaje kwenda kuishi nyumbani kwa Marehemu Sitta wakati hamna undungu wa aina yoyote?.

18. Mwaka 2006, alipopata udahili Chuo cha ushirika na biashara Moshi (wakati huo kikiwa chuo kikuu kishiriki cha SUA), kwa nini uliendelea kutumia vyeti vyako halali vya certificate (ya Nyegezi) na diploma (ya Mbegani) lakini kwa kutumia majina ya Paul Christian?.

19. Ulipojinga Chuo cha Ushirika, ulidahiliwa kwa course ya BA in Cooperate Management & Accounting na mwaka 2007 ulimaliza first year, kwa nini ulishindwa kuendelea na 2nd year?.

20. Mwaka huohuo 2007 kwa nini uliomba Admission upya? lakini mwaka uliofuata wa 2008 kulitokea nini hadi ukaamua kuacha chuo? na badala yake akaenda kuomba tena udahili chuo kikuu SUA kwa mara nyingine wakati mwanzo uliishajaribu lakini akakosa?.

21. Kwa nini mwaka 2009 ulirudi tena MUCcoBS kwa udahili mpya kwa kaachana na CMA ulisomea hapo mwanzo, na badala yake ukachukua Community & Economic Development (CED)?.

22. Mwaka 2012 alipohitimu shahada yako ya kwanza ya Community & Economic Development, kwa nini uliendelea kutumia jina la Paul C hristian badala ya majina yako halisi ya Daudi Albert Bashite?.

23. Ulipo kula kiapo mahakamani cha kubadili majina, kwa nini uliendelea kuapa kiapo cha uongo kwa kutumia majina ya wizi ya Paul Christian Muyenge na kuwa Paul Christian Makonda ya badala ya kutumia majina yako halisi ya Daudi Albert Bashite?. Jee unajua kula kiapo cha uongo mahakamani ni kosa la jinai?.

24. Kwa nini ulitumia jina la uongo kuolea mke, jee unajua kiapo cha uongo kwenye ndoa, kinaweza kuibatilisha ndoa?. Pia umetumia majina ya bandia kuombea hati ya kusafiria ya Tanzania, jee unajua ni kosa la jinai?.

Naomba niishie kwenye maswali kuhusu jina tuu, hayo mengine yote ya kumiliki mali ni wivu tuu wa maendeleo yake, na kule kuvamia Clouds ni uzushi tuu, the real game ni kwenye forgery, cheating, impersonation, na self pretense, ambayo yote ni makosa ya jinai.

Video ya Wakili Msando na Gigy Money Wakifanya Yao Yazua Gumzo Instagram

$
0
0
Video ikionyeza Wakili Maarufu Alberto Msando akimshika Gigy Money sehemu  imekuwa gumzo huku Instagram Kila mtu akiwa na maoni yake tofauti:

Video iliyopostiwa na mtu anayeitwa @carrymastory Itazame Hapa:



Baadhi ya Maoni Soma Hapa chini: 

45beyouKwani uanasheria na gigy unaingiliana vipi??

saumsaid10Huyu dda atakuja act x huko tunakoelekeaa

 cherry_wemasepetuNdio maana uchumi unashuka

tasha_boyDuh huyu demu hajielewi naeee


Ben Paul Amezungumzia Picha zake za 'Uchi'

$
0
0
Ben Pol amefunguka kwa mara ya kwanza tangu picha yake inayomuonyesha akiwa utupu kusababisha maneno mengi mitandaoni.

Muimbaji huyo amerudi tena kupitia mtandao wa Instagram kwa kuweka video ambayo inamuonyesha akiwa mtupu huku ukisikika wimbo ukiimba na kuandika, “Usi-judge kitabu kama hujakisoma ndani .”

Hata hivyo imeonyesha kuwa picha hizo zilizozua utata mkubwa mapema wiki hii ni ujio wa nyimbo yake mpya ya Ben ambayo imedaiwa kupewa jina la ‘Mateka’ na ndani yake amemshirikisha rapper Darassa.

Wimbo huo pia umetayarishwa na Tiddy Hotter ambaye alitengeneza wimbo mwingine wa Phone wa Ben.

Wazazi Waliyofiwa na Watoto Wao Ajalini Arusha Walijitoa Kwenye Kamati ya Gambo Ukweli Huu Hapa

$
0
0
Wazazi waliokuwepo kwenye kamati ya rambirambi ya msiba huo iliyoundwa na Mkuu wa mkoa wa Arusha wamejitoa rasmi katika kamati hiyo.

Kwa mujibu wa mzazi huyo ambaye hakutaka jina lake linukuliwe ameeleza Sababu kubwa ya wao kujitoa kwamba ni kitendo cha kutumika nguvu ya dola hasa wakati ambapo kulikuwa na ibada ya kupewa pole na rambirambi , ibada ambayo haikufanyika kutokana na kuvamiwa na Jeshi la Polisi na kukamatwa Meya wa jiji la Arusha mh. Kalisti Lazaro ,Katibu wa TAMONGSCO kanda ya Kaskazini Mh. Leonard Mao , Waandishi wa Habari 10 , pamoja na wamiliki wa shule binafsi waliokuwepo katika hafla hiyo.

KATIKA VIDEO HAPA CHINI MZAZI HUYU ANAELEZA SABABU YA WAO KUJITOA KWENYE KAMATI YA RC GAMBO

Zitto avipa "kibomu" Vyombo vya Habari

$
0
0
"Natamani vyombo vya Habari kufanya uchambuzi wa kina wa tozo ambazo Serikali imesema imeondoa kumsaidia mkulima. Hii ni Habari pekee ambayo inapigiwa debe mno na Serikali kiasi cha kuficha kabisa uhalisia kwamba Mwaka Jana Serikali ilitoa 3% tu ya fedha za Bajeti ya Maendeleo ya Kilimo.

Nataraji kuwa taasisi Kama MVIWATA zitatupatia uchambuzi wao" Amesema hayo kupitia ukurasa wake wa Facebook

HITIMISHO Makundi: Serengeti Boys Inahitaji Ushindi Mnono kwa Niger Kumuepuka Ghana..!!!

$
0
0

Mishale ya saa mbili na nusu za Tanzania, Serengeti Boys itashuka dimbani kupepetana na Niger kuhitimisha safari ya makundi huku ikihitaji ushindi ama sare ya aina yoyote kusonga mbele hatua ya nusu fainali.

Huku Tanzania ikihitimisha na Niger, Mali atahitimisha na Angola. Mpaka sasa Ghana ndio timu pekee ambayo goli lake halijatikishwa huku ikipachika wavuni mabao tisa, ni timu iliyo gumzo zaidi nchini Gabon. Aheri kukutana na Ghana fainali kupitia mgongo wa Guinea.

Ubingwa wa Yanga Waingia Kimavi...Sasa Wasubiria Neema ya Mungu

$
0
0
Baada ya kuenea kwa tetesi kuwa Klabu ya Simba imewasilisha malalamiko ya barua kwa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) kupinga kunyang'anywa pointi 3, hatimaye uthibitisho wapatikana.


Kitendo cha Simba kuwasilisha rufaa hiyo na kuenea kwa picha ikionyesha vielelezo hivyo, imeanza kuwakwaza mashabiki wa Yanga ambao walikuwa wameanza sherehe za ubingwa.

Baadhi ya mashabiki wa Yanga, wameonekana kukerwa na jambo hilo huku wakiwakejeli Simba kwa kuwaita “Wazee wa pointi za mezani”.

Simba imeamua kwenda Fifa kuhakikisha inapata pointi tatu ambazo kama itafanikiwa, basi moja kwa moja itatangazwa kuwa bingwa.

Haya ni baadhi ya maneno aliyoandika Msemaji wa Simba aliyefungiwa, Haji Manara;....."Last week nilipowapongeza Yanga kwa ushindi na kuwaambia mapambano yanaendelea,sijui kama tulielewana!! Bila shaka sasa mmenielewa, soon tutapewa haki yetu,MWANA KULITAKA,MWANA KULIPEWA"

Halafu akaendelea;........"Hivi unadhani FIFA wana figisu guys?kadi tatu za njano ni kukosa game inayofuata tu,no way out!!ukizingatia repoti za mwamuzi na kamisaa na bodi inayosimamia ligi, sasa mjiandae kisaikolojia kulileta kombe kwa magoti!SHUBAMIT"

Dada Tulia uolewe sasa miaka hairud nyuma. Wachawi wako ni hawa ndugu zako

$
0
0
Huyu dada ana miaka 32 kwa sasa kama tungekuwa tunaangalia saa kwa njia za kale tungesema sasa ni jioni kwake. Ana sura nzuri na umbo zuri pia.

Shida kubwa sasa amekuwa na hamu ya Kuolewa mpaka anaharibu sababu ya Kujirahisi yaani ukimzoea kidogo tu ukawa naye siku mbili tatu ukaomba issue anakupa. Ye anaamini akikupa na kukuonesha maujuzi haraka utatangaza ndoa. Ufundi wanasema anao si haba. Lakini wanaume wengi nadhan hawamwoni kama mke. Wanamwona zaidi kama ni mwanamke wa dharura.

Dada anavifaham viwanja vyote Dar na Mikoa Jirani. Ye ni wa kupost pich FB anakula Bata na Kunywa Machozi ya Simba kila wakati. Ukimwona ni mtu wa Kujirusha sana. Anasema kwa usiku anaweza tembelea Viwanja hata 10. Yaani anakunywa hapa kama vipi anahama anahamia pale napo akiona vipi anaondoka anelekea kule akina hajapenda anakuja huku.

Akija kazin Jumatatu amechoka kila sehem ya mwili. Na bado analalamika kuwa hapati mume. Najiuliza atapaje Mume kwa style hiyo?

Na umri nao unaenda anaelekea Usiku. Sasa anazunguka kwa waganga anadai amerogwa asiolewe. Lakini ukiangalia mfumo anaotumia kucheza katika maisha ni mfumo ambayo unakaribisha Mashambulizi kwake.

Huyu dada amejiroga mwenyewe. Mtu gani pombe yeye, kuachia kupigwa mabao yeye, Umjini mjini mwingi na maneno ya shombo.bado analalamika kuwa amerogwa.

GuDume

KIMENUKAA..Baada ya Video Kusambaa Mitandaoni Ikumonyesha Gigy Money Akichezewa Sehemu za Siri na Wakili Maarufu Nchini Albert Msando..Gigy Money Kaanika Yote Aliyofanyiwa..!!!


IMEFICHUKA..Hii Hapa Siri ya Makonda Kwenda Kufanya Interview Staa Tv..Inasemekana Amemtisha Mmiliki wa Star Tv Ili Akubali Kumruhusu Kujisafisha Tuhuma Zinazomganda..!!

$
0
0

Baada ya Paul Makonda hali yake kisiasa kuchafuka kutokana na matendo yake hivi karibuni alikuja Mwanza na kubaini kuwa kwa sasa amepoteza mvuto Kabisa kutokana na kukosa kiki kwenye vyombo vya habari na baadhi ya marafiki zake kuanza kumkimbia. 


Inasemekana ujio wa Makonda Mwanza ilikuwa ni Kwa ajili ya kuweka mambo sawa na Mkurugenzi wa Star Tv ndugu Antony Dialo, ambaye walikutana Kwa siri na Mkurugenzi huyo. 

Imebainika kuwa Makonda alikuja Kwa malengo matatu la kwanza ni kujaribu kuweka mambo sawa na Dialo ambaye pia ni mwenyekiti wa chama mkoa wa Mwanza ambaye anaunga mkono tamko la Jukwaa la wahariri kutokurusha habari za Makonda. 

Imefahamika katika lengo la kwanza walimtisha mzee Dialo kama atashindwa kufanya kazi pamoja na Makonda watamuondoa mara moja ndani ya chama Kwa kumvua nyadhifa zote za uongozi. 

Jambo la pili tulilodokezwa ni kwamba Hali ya uchumi ni mbaya katika kampuni ya Sahara iliyopelekea MD wake ndugu Sammy Nyala kuondoka kutokana kushuka sana kibiashara katika kampuni hiyo inayomilikiwa na Mzee Dialo siku hizi hawafanyi vizuri kibiashara na ukichangia na Deni la zaidi ya shilingi bilioni nne kutoka TRA. 

Makonda alimuhaidi atamsaidia kuongea na mamlaka za juu kumpatia TAX HOLIDAY endapo atakubali kufanya naye kazi na kurusha taarifa zake Yeye Makonda. 

Makonda katika safari ya Mwanza aliambatana na Ray pamoja JB ambaye hivi karibuni amemteua kuwa mhamasishaji wa wasanii katika kusambaza taarifa za Makonda mitandaoni. 

Katika Siku ya Pili pale Malaika Resort Makonda alisikika akiongea kwenye simu na mtu ambaye alionekana kumtii sana ndani ya chama na kumpatia taarifa juu ya adhima ya Antony Dialo kuifikiria zaidi nafasi ya Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi. 

Jioni walipokutana Katika hotel ya Malaika Resort Majira ya Jioni Gari ya mzee Dialo ilifika, Makonda na Dialo walizungumza tena Kwa kirefu na kupanga jinsi gani wataweza kufanya kazi pamoja mojawapo ni kujisafisha kuhusu uvamizi wa Clouds Media ili kuizima ishu ya Uvamizi mipango ipangwe haikuwa ishu ya Gwajima bali tetesi za uwepo wa Dawa za kulevya rejea tamko aliloliandika Mzee Dialo. 

Pia wakati wanazungumza na Mzee Dialo, Makonda alimjulisha kuwa tayari mipango ya kumuandalia nafasi ya Ukatibu mkuu ndani ya chama CCM Taifa imekwishaiva hivyo asiwe na wasiwasi pale Mkutano Mkuu Taifa utakapoitishwa muda wowote kuanzia sasa kumjadili Nape Nnauye basi ndiyo utakuwa muda muafaka wa jambo lake kuingizwa kwenye ajenda ya Mkutano Mkuu. 

Chanzo kilidokeza kuwa Makonda alimuhaidi kumpatia Dialo Kiasi cha fedha ambacho atachukua kutoka kwa Wafanyabiashara marafiki zake wa Dar kwa ajili ya kumsaidia kulipa madeni na Mishahara kwa wafanyakazi wake Kwa mwezi wa 3 hadi wa 6 kwani inasemeka wafanyakazi hao wengi wao bado hawajalipwa Mishahara yao isipokuwa posho ndogo zilizopo Kwa ajili ya kujikimu kwa kuwa hali ya Uchumi kwenye kampuni hiyo ni Mbaya sana. 

Kingine Makonda amehaidi kumsaidia Anthony Dialo kwa kumpatia ulinzi kwa kipindi Chote watakachokuwa wanafanya kazi pamoja kumlinda na hasira kutoka Kwa waandishi wasio unga mkono harakati za Makonda. 

Baada ya kumaliza Maongezi na na Makonda inasemekana Dialo aliwaita wafanyakazi wake na kujadiliana wajipange jinsi gani ya kufanya kazi na Makonda kitu ambacho Wafanyakazi wametafsiri kuwa ni ishara mbaya kwa kituo hicho cha habari hasa ikichangiwa na uhusiano mbovu na dharau alizozionyesha Makonda kipindi cha nyuma kwa wafanyakazi wa kituo hicho. 

Unaambiwa Baada ya Antony Dialo kumaliza kile kikao aliwashinikiza wafanyakazi wake kuwa asiyetaka aondoke akatafute kazi sehemu nyingine Kwa kuwa tayari ajenda pekee alizobaki nazo kwa siri kichwani ni Ukatibu Mkuu wa chama na kusamehewa madeni anayodaiwa. 

Kwa Taarifa zilizopo mzee Dialo alikwenda South Africa haijulikani alikwenda kufanya nini, nitaendelea kuwajuza kwa kadri iwezekanavyo juu ya ziara hiyo na kila kitu kitakuwa wazi. 

Hii sasa ni kufuru kama Paul Makonda ataendelea kutumia ukaribu wake na Mamlaka za juu ili tu aendelee kujinufaisha Kwa maslahi yake binafsi.

Chanzo - Jamii forum

Namna ya Kumjengea Mtoto Mazingira Mazuri ya Kujifunza Nyumbani

$
0
0
Utakubaliana nasi kuwa shule ya kwanza katika maisha ya mtoto ni nyumbani – wazazi, ndugu wa familia, majirani na marafiki wa familia husika. Jukumu la malezi linatoka kwa Mungu na mzazi hana budi kulitekeleza maadam ameamua kumleta mtoto duniani. Kupitia mzazi/mlezi mtoto anapata nyenzo zitakazoongoza maisha yake yote – heshima, utii, unyenyekevu na nidhamu. Yaani wema au ubaya wa mtu mara nyingi ni matokeo ya aliyojifunza nyumbani.

Nyumbani ndiko msingi hujengwa. Bahati mbaya ‘ualimu’ wa nyumbani unatokana na matendo zaidi ya maneno. Mtoto uko naye kila uchao hivyo badala ya kutumia muda mwingi kutoa ‘maelekezo ya tabia njema’. Ishi kwa mfano. Unamwambia mtoto sala na ibada ni muhimu katika maisha – wewe unasali? Je, mnahudhuria ibada pamoja? Kupitia maisha unayoishi utamjengea mtoto misingi ya kiakili na kiimani ili kama ilivyo kwa chakula bora awe na uwiano sawia katika maisha. Bahati mbaya wazazi/walezi wengi huingia katika shughuli hii wakiwa ndiyo kwanza bado vijana. Lugha za ujana na misemo iliyo mingi huwa bado inazo chembe za utovu wa nidhamu. Ukiwa mzazi – mtoto anakusikia, anakuiga. Chagua maneno.

Fursa ya kujenga tabia/kukuza vipaji. Anapotoka tumboni mwa mama, mtoto huwa na kurasa zilizo wazi pasi na tabia za aina iwayo­yote. Isipokuwa kwa vipaji na tabia za kurithi – mzazi/mlezi wewe unalo­jukumu la ‘kuumba’ tabia na kukuza vipaji vya mtoto. Ukiwa kama mwalimu wa kwanza wa mtoto, mwandae kwa ajili ya elimu ya shule (awali, msingi, sekondari, nk.) na stadi za maisha. Muache mtoto ajifunze shughuli tofauti kutoka kwako kulingana na kipaji ulichojaaliwa, shiriki shughuli za jamii ili ajifunze uwajibikaji kutoka kwako.

Umoja wa wazazi/walezi ni wa lazima. Baba na mama wawe wamoja katika kulea. Pale inapotokea tofauti baina yao kuhusu namna ya kutoa maelekezo kwa mtoto – basi na wasibishane mbele ya mtoto. Ikiwa kwa mfano, mama anamwadhibu mtoto na baba hakubaliani na adhabu inayotolewa – muombe mama faraghani na mzungumze juu ya hili. Ukomavu namna hii utasaidia kutomchanganya mtoto na ujumbe unaokinzana. Kamwe msikwaruzane mbele za watoto. Tofauti zenu zivumiliwe mpaka mpatapo faragha mbali na watoto.

Elimu ianze umri gani hasa? Elimu inaanza akiwa tumboni – kupitia mazungumzo ya mama mtoto anaandaliwa kuzijua sauti za watu wake wa karibu kama baba, mashangazi nk. Hii inakwambia kwamba malezi yanaanza mara tu uwapo mjamzito. Punguza ugomvi usio­lazima na ikiwezekana jenga mazingira rafiki kwa kuwa mwenye furaha wakati mwingi. Mara tu unapomtia mikononi mwako kichanga wako – anza kumsemesha. Elimu ya lugha unayotumia ndiyo lugha atakayoanza kuifahamu. Jenga msamiati wenye lugha za staha ili mtoto naye ajifunze hivyo.

Jifunze miongozo ya malezi. Sote tunafahamu kuwa malezi hayana shule eti ukajifunze upate kujua mbivu au mbichi. Nyakati nazo zimebadilika na watu hasa waishio mijini hawakai pamoja na familia tandaa. Hii inamnyima mzazi mpya fursa ya kupata maelekezo ya namna bora ya kulea toka kwa wazazi wazoefu. Pamoja na changamoto hizi, zipo fursa za kujielimisha kupitia vitabu, majarida na makala mfano wa haya. Fursa nyingine adhimu ni mtandao wa intaneti wenye maandiko ya kitaalamu na toka kwa wazazi wa matabaka, makabila na lugha mbalimbali kote ulimwenguni.

Yafahamu Mambo Kumi Muhimu Kuhusu Ugonjwa wa Kisukari

$
0
0
Tarehe 07 Aprili 2016 ilikuwa ni siku ya Afya Duniani. Na kaulimbiu ya mwaka huu ilikuwa imelenga kupunguza ukuaji ya Ugonjwa wa kisukari. Taarifa zilizotolewa na shirika la afya (WHO) mwaka huu, jumla ya watu milioni 422 walikuwa wameathirika na Kisukari 2014. Kutokana na idadi hiyo kubwa shirika hilo lilieza mambo gani mtu anaweza kufanya kupunguza uwezekano wa kupata ugonjwa huu.

Udaku Special tunakuwekea hapa mambo 10 yakuzingatia.

1.    Kila siku hakikisha kuwa umetembea hatua 10,000, punguza kula vyakula vya kusindika, hakikisha uzito wako ni sahihi, lala kwa saa 6 hadi 8 kwa siku, na pima kiwango cha sukari katika damu ukifikisha miaka 30 kama una ndugu yeyote mwenye Kisukari.

2.    Ulaji wa Nyama kwa kiwango kikubwa ni hatari kwa afya yetu. Hivyo punguza ulaji wa nyama hasa nyama nyekundu (Ng’ombe, Mbuzi)

3.    Kifungua kinywa ni mlo muhimu sana kwa afya ya mwili na akili kwani mwili hupata nguvu ya kufanya kazi kwa siku nzima. Kupata kifungua kinywa ni kitu muhimu sana kila mara kwani husaidia mmeng’enyo kufanya kazi kwa usahihi.

4.    Hakikisha mtoto anapata maziwa ya mama akiwa mdogo kwani maziwa ya mama yana kinga ya kumuwezesha mtoto kupambana na magonjwa. Huduma bora za hosipitali pia ni muhimu.

5.    Mshtuko wa Moyo huua watu wengi sana duniani. Watu 3 kati ya 10 duniani hufariki kwa sababu ya Mshtuko wa Moyo. Tunaweza kuzuia ugonjwa huu kwa kupata mlo kamili kila mara, mazoezi ya mwili na pia kuto vuta sigara.

6.    Takribani asilimia 10 ya watu wazima duniani wanaugonjwa wa Kisukari. Watu wenye kisukari wanahatari ya kupata magonjwa Moyo. Vifo vinavyosababishwa na Kisukari vimeongozeka tangu mwaka 2000, mwaka 2012 watu milioni 1.5 walifariki kurokana na Kisukari.

7.    Ulaji wa vyakula vyenye Sukari husababisha ugonjwa wa Kisukari. Mtu huugua Kisukari pindi mwili unaposhindwa kuzalisha Insulin kuishughuikia sukari kwenye damu. Kuto kufanya mazoezi, kuwa na uzito uliopitiliza kunakufanya kwenye hatari ya kuugua kisukari kadiri unavyoelekea uzeeni.

8.    Kiini cha yai hua na Cholestrol kubwa. Hivyo kama kiwango cha Cholestro mwilini kipo chini unashauri kula viini vya mayai mara kadhaa kw wiki.

9.    Kunywa maji ya kutosha kila siku, usisubiri hadi uwe na kiu ndipo unywe maji. Maji husaidia kuondoa sumu mwilini.

10.    Unashauriwa kula vyakula kama MTAMA; ambavyo huwa na Protein, Vitamins na madini kama Chuma, Calcium, Phosphorus na Pottasium, SAMAKI, VYAKULA JAMII YA KUNDE ambavyo huwa na Fibre na Protein, VIAZI VITAMU ambavyo huwa na Vitamin A na C ambayo husaidia kukuza kinga ya mwili.

Jinsi ya Kuanzisha Salon Yenye Faida

$
0
0
Utunzaji wa nywele ni kitu cha kila siku kwenye maisha yetu.Kwenye jamii yetu kila mtu anajali anavyoonekana.Nywele zinaongezea muonekano wa kuvutia.Kuanzia mtoto mpaka mtu mzima wanataka huduma ya kutunza nywele.

Kama unaweza kuhesabu gharama ulizotumia kwa mwaka mzima kutunza nywele utashangaa kwa kiwango kikubwa.Biashara ya salon zipo kila mahali lakini leo tutajifunza jinsi gani unaweza kukabiliana na ushindani huo na kumiliki idadi kubwa ya wateja.

Kabla ya yote kwanini nakushawishi uanzishe biashara ya saloni.
Biashara ya salon unaweza kutenga muda wakufanya huku ukiwa na shughuli nyingine labda jioni tu na weekend(part time job).
Biashara hii unaweza kuiendesha ukiwa nyumbani.
Biashara unaweza kuifanya na biashara nyingine kama kuuza bidhaa za nywele, mafuta ya nywele n.k.
Hauhitaji kubuni bidhaa yako binafsi.

Jinsi ya kufanikiwa katika biashara ya salon.

Unatakiwa uwe na ujuzi mzuri wa salon.Kama wewe ni kinyozi ama msusi utakiwa uwe na utaalamu wa nywele hivyo utakiwa uwaone watu wenye uzoefu katika maswala haya.
Uwe na ukarimu kwa wateja.
Siku macho yako yawaangalie washindani wako.Unatakiwa kuwatawala washindani wako.Unatakiwa ujue mapungufu ya saloni zao na pia nini kinawaimarisha katika saloni zao na ndio utafaidika zaidi.
Huduma nzuri kwa wateja.
Chagua sehemu sahihi.Watu wenye hukosea kuchagua sehemu sahihi, Sehemu sahihi si sehemu isiyo na saloni tu bali sehemu yenye watu wengi na inafikika kwa urahisi.Sehemu yenye wapitaji wengi inayoonekana kwa urahisi.Kuanzisha biashara mpya sehemu isiyo na biashara kama yako ninaweza kuwa hatari ama faida.


Mahitaji.
Kabla ya kuanzisha biashara hii hakikisha una vitu vya msingi kama,


    Curlers
    Hair Brush
    Chana
    Hair Dryer
    Hair Rollers
    Hair Wand
    Hair Waver
    Mkasi
    Straighteners
    Vibanio
     Kioo
     Kiti
    TV kuburudisha  wateja
    Barber Chairs

Kumbuka vifaa vya biashara ya salon inategemea salon ni mahususa kwa jinsia gani.

Biashara nyingine unazoweza kuzifanya pamoja na hii ni:-

Kupaka nywele rangi.(Hair Colouring)
Shampooing.
Kuuza mafuta ya nywele.

Njia nyingine kuvutia wateja ni.

Ukarimu kwa wateja.
Usafi na huduma nzuri.
Punguzo la bei kwa mwezi wa mwanzo.

SERIKALI Yawatumia Mamilioni Wazazi wa Majeruhi wa Ajali ya Bus la Wanafunzi wa Lucky Vicent..!!!

$
0
0

Serikali kupitia ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Arusha,imetuma  Sh  44.9 milioni kwa wazazi wa majeruhi ya ajali ya Lucky Vicent wanaotibiwa hospitali ya Mercy iliyopo Marekani

Watoto wanaotibiwa Marekani ni Saidia Ismail, Wilson Tarimo na Doreen Mshana.

Akizungumza na waandishi  wa habari , Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo  amesema  kuna sababu ya kuelekeza nguvu kubwa kwa kuwasaidia majeruhi hao watatu walioponea chupuchupu kwenye ajali ya gari huko Karatu.

Pia alisema pesa hizo walizotuma zitaenda kusaidia familia zilizoondoka na majeruhi kwenda nchini Marekani na kwamba kila mzazi atapata Sh 11 milioni ,huku daktari aliyeondoka na majeruhi hao pamoja na muuguzi  watapata  Sh 5.5 milioni kila mmoja

"Tumetoa pesa hizo kwa familia zilizopo huko nchini Marekani ili ziweze kuwasaidia waliko huko ugenini," amesema Gambo

Kwa mujibu wa Mkuu huyo wa Mkoa alisema fedha hizo zilizotolewa zinatokana na rambirambi zinazoendelea kuchangwa na wadau mbalimbali na ambako mpaka Mei 20 , Sh 67.99milioni  zilipatikana.

Amesema pamoja na kutoa Sh 44.72 milioni,fedha zilizobaki ofisini kwake ni Sh 23.27 milioni na akasema   fedha hizo zitaendelea kuwekwa huku timu ya wawazi wanne walioteuliwa na wafiwa wakiendelea kushirikiana na Serikali kuhakiki mapato na matumizi wa rambirambi hizo

"Kuna tuhuma nyingi ambazo zinadai rambirambi za wafiwa hazijawafikia wafiwa,taarifa hizo hazina ukweli,ofisi yangu imeratibu zoezi hilo kwa uaminifu wa hali ya juu na taarifa ya jumla imetolewa kwa umma juu ya mapato na matuzi yote," amesema Gambo
Viewing all 104793 articles
Browse latest View live




Latest Images