Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104803 articles
Browse latest View live

Siku Chache Baada ya Kuvuliwa Uwaziri..Professor Muhongo Aionya Serikali..!!!

$
0
0

Aliyekuwa waziri wa nishati na madini prof. Muhongo ameteta rekodi yake ya utendaji kazi na uwaminifu kwa taifa kuwa uko wazi nawala si wakutilia shaka.

Amesema kuwa pia kujiuzuru kwake si kwa lengo jingine Bali kutoa nafasi ili watu wapate nafasi ya kujua nini kinachoendelea juu yake.

" Watu wanasema Mimi Nina kiburi, lkn kinachofanya hivyo ni elimu yangu ambayo imenipa Tania ya kusema ukweli. Nikisema hiki ni kijiko na wala si koleo huwa namaanisha hivyo"

Pamoja na hayo ameandika kuwa Tanzania si kisiwa hivyo ijiandae kwa matatizo makubwa yatakayofwatia kutokana na makosa yetu tunayoyatenda na tunayoendelea kuyatenda hadi sasa na kuipata shubiri Kali itakayo fwatia kutoka kwa wawekezaji.

Hizi Ndizo Fedha Halisi Ambazo Tanzania Ingepata Kwenye Makontena 277 ya Mchanga wa Madini..!!!

$
0
0

Baada ya kamati ya uchunguzi wa makinikia ya madini kutoa ripoti yake juzi, wengi wanaona kuwa Tanzania imekuwa ikiibiwa kiasi kikubwa cha fedha tangu usafirishaji mchanga wa dhahabu ulipoanza takriban miaka 20 iliyopita.

Wako wanaosema kuwa kiwango hicho cha fedha kinachotokana na kati ya tani 7.8 hadi 15 za madini yaliyo katika makinikia hiyo, kingeweza hata kutosheleza mahitaji ya bajeti ya mwaka.

Lakini kwa mujibu wa kanuni za uchimbaji madini, stahiki ya nchi katika madini haiwezi kuzidi asilimia 10 ya mrabaha.

Kamati iliyoundwa na Rais ambayo iliongozwa na Profesa Abdulkarim Mruma, ilisema imebaini kuwa kampuni ya Acacia, ambayo inaendesha migodi mitatu nchini, haikutangaza madini yote yaliyomo kwenye mchanga huo uliozuiwa bandarini na kwamba kiwango cha dhahabu iliyomo ni kubwa zaidi ya kilichotangazwa.

Wachimbaji wa madini wenye leseni pamoja na kulipa kodi nyingine kwa Serikali kama za mapato na kampuni, hutakiwa na Sheria ya Madini ya Mwaka 2010 kulipa mrabaha.

Mrabaha ni malipo yanayofanywa na kampuni inayochimba madini kama fidia ya kiuchumi inayolipwa kwa Serikali kutokana na kuchimba rasilimali zake ambazo hazina mbadala.

Kwa mujibu wa kifungu 87(1) wachimbaji wa urani, almasi ghafi na vito ghafi wanatakiwa kulipa mrabaha wa asilimia tano huku kwa madini kama dhahabu, shaba, fedha na platina wakitoa asilimia nne ya thamani ya madini yote.

Madini mengine ya ujenzi kama mchanga, mawe, chokaa hutakiwa kulipiwa mrabaha wa asilimia tatu wakati vito vilivyokatwa na kuchongwa vikilipiwa asilimia moja.

Matokeo ya kamati yanaonyesha kuwa thamani ya madini yote yaliyopo kwenye makontena 277 ni kati ya Sh829.4 bilioni hadi Sh1.439 trilioni.

Iwapo hesabu ya asilimia nne ya mrabaha itapigwa kwa thamani ya chini iliyoanishwa na kamati ya Sh829.4 bilioni kwa kuzingatia dhahabu, fedha na shaba zina thamani kubwa kuliko madini mengine yaliyoanishwa, basi Serikali ilitakiwa ipate Sh33.17 bilioni.

Ripoti ya kamati ya Profesa Mruma ilijumuisha hesabu za madini yote yenye thamani katika makontena hayo yakiwemo yale ya kimkakati kama lithium inayotumika zaidi duniani kutengeneza betri za vifaa vya kielektroniki kama simu za mkononi.

Na iwapo asilimia hiyo nne itapigwa kwa kiwango cha juu cha thamani ya madini hayo cha Sh1.439 trilioni, Serikali ilitakiwa ipate mrabaha wa Sh57.56 bilioni.

Ripoti hiyo inaeleza kuwa nyaraka zilizotolewa na wazalishaji zilionyesha makontena hayo yalikuwa na dhahabu tani 1.1 yenye thamani ya Sh97.5 bilioni.

Lakini Acacia katika moja taarifa zao za hivi karibuni juu ya ufafanuzi kuhusu makinikia wanaeleza kuwa kontena moja la tani 20 lina thamani ya wastani wa Sh310 milioni. Hii ina maana kuwa mzigo wote uliomo kwenye makontena 277 una thamani ya Sh85.87 bilioni.

Kwa hesabu za Acacia ambazo zinajumuisha madini ya dhahabu, fedha na shaba pekee, Serikali ilitakiwa kupata mrabaha wa Sh3.43 bilioni. Kampuni hiyo inapinga kuwa madini mengine yaliyosalia yaliyoorodheshwa na kamati hayana thamani ya kibiashara.     

Mbunge Alia Kisa Wabunge wa Upinzani kuitwa Mabwege..!!!

$
0
0

Mbunge wa Tarime Mjini (Chadema), Ester Matiko juzi jioni alikerwa na ujumbe unaodaiwa kuandikwa na Mwenyekiti wa Bunge, Musa Zungu uliowataka wapinzani waache mambo ya kibwege.

Matiko ambaye pia ni Waziri Kivuli wa Maliasili na Utalii, aliomba mwongozo wa Spika mara baada ya Bunge kupitisha bajeti ya wizara hiyo.

Matiko aliomba mwongozo huo akitaka kupata ufafanuzi wa utaratibu unaotumika kuwachagua wabunge watakaohoji wakati Bunge linapokaa kama kamati.

Alisema katika Bunge la 11 umekuwa utaratibu wa kiti cha Spika kuchagua wabunge wengi wa CCM kuchangia hoja na hivyo muda kumalizika bila wapinzani kupata nafasi.

Mbunge huyo alisema jambo hilo limekuwa tofauti na mabunge mengine ambayo Bunge limekuwa likienda hadi saa nne usiku ili kuwapa nafasi wabunge kujadili bajeti kwa kina.

“Tukikulalamikia matokeo yake unatutumia kikaratasi kimeandikwa maneno, mambo yenu ya kibwege bwege. Yaani unawaambia wananchi wa Tarime wamechagua bwege?” alihoji Matiko.

Akijibu mwongozo huo, Zungu alisema kanuni zinatoa fursa ya kuingia katika kupitisha vifungu kwa utaratibu wa fungu. Alisema kanuni hiyo pia inatoa fursa ya vyama kupeleka majina ya wachangiaji katika kila kamati ya matumizi inapokaa kupitia bajeti.

Aliwataja waliowasishwa kwa ajili ya bajeti hiyo kuwa ni ni Matiko, Chacha Rioba (Serengeti) na mbunge mwingine wa tatu ambaye hakumtaja jina. “Unasema sijui kuna karatasi mimi nimesema, hiyo karatasi iangalie vizuri imetoka wapi? Sasa wewe unaweza ukaichukua hiyo karatasi ukaipeleka kwa katibu ili ifanyiwe kazi,” alisema Zungu.

Majibu hayo yalisababisha minong’ono miongoni mwa wabunge, lakini Zungu alisema kuwa mwongozo ni huo na kuliahirisha Bunge.

Akizungumza jana kuhusu suala hilo, Mbunge wa Bunda Mjini (Chadema), Ester Bulaya alisema inapofika Bunge linapokaa kama kamati ya matumizi kila chama kimekuwa kikitakiwa kupeleka majina ya wachangiaji.

Alisema kuna wakati hoja moja wanapewa wabunge hata 10 kuchangia na kwamba hata kama ni uamuzi wa kiti lakini ni lazima busara itumike.

“Wanafanya hivyo ili kuhakikisha kuwa upinzani unakosa nafasi na hiyo tumekuwa tukilalamika hata kwa Zungu,” alisema.     

Mzee Yusuph Awataka Mashabiki wa Taarabu Kufuta Nyimbo Zake Zote Kwenye Simu Zao Ili Waepukane na Dhambi..!!!

$
0
0

Aliyekuwa mfalme wa muziki wa taarab nchini, Mzee Yusuph amefunguka na kueleza kuwa watu wote walio na nyimbo zake kwenye simu zao wafute na kuacha kusikiliza ili kuepuka dhambi.

Katika mahojihano na kipindi cha Mitikisiko ya Pwani cha Times Fm, Mzee Yusuph ameelezea maisha yake ya ndoa, kidini na kiuchmi yalivyo kwa sasa ukilinganisha na hapo awali.

“Mimi nikikubali watu wacheze nyimbo zangu ina maana nimeruhusu dhambi tena ni bora nirudi kuimba muziki tena hivyo, watu wote waliokuwa na nyimbo zangu kwenye simu zao wafute na kuacha kusikiliza kuepuka dhambi,” amesema Mzee Yussufu.

Mzee Yussufu amesema yeye hayupo kwenye kundi lake la ‘Jahazi Modern Taarab’ kama baadhi ya watu wanavyodhani na wala hafuatilii kabisa kundi hilo.

“Nilitaka kulivunja Kundi la Jahazi lakini sheria za nchi haziruhusu nikaliacha na haya niliambiwa na Basata wenyewe. Vyombo vya bendi ya Jahazi havikuwa vya kwangu tulikuwa tunasaidiana na mabosi,” amesema.

Katika hatua nyingine Mzee Yusuph amesema maisha ya kiuchumi kwa sasa ni toufauti na kipindi alichokuwa anafanya muziki kwani hapo awali kwa wiki alikuwa anaweza kutengeneza milioni moja na nusu mpaka mbili ila sasa kushika laki tano au milioni inaweza kumchukua miezi miwili.

Ameongeza kuwa wake zake wanne bado anaendelea kuishi nao kama kawaida, na kuwa na wake ni jambo ambalo amehimizwa na sio amri, na kwa sasa wanamjua ni mtu wa namna gani na mambo yote yanaenda sawa hakuna hata mmoja anayefanya sivyo.

Majeruhi Wawili ya Lucky Vincent Waruhusiwa Kutoka Hospitali..!!!

$
0
0

Watoto wawili majeruhi wa ajali ya gari la Shule ya Lucky Vincent wameruhusiwa kutoka hopitalini.

Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu ameandika katika ukurasa wake wa Facebook kuwa watoto hao, Sadia Ismael na Wilson Tarimo waliokuwa wamelazwa katika hospitali ya Mercy ya Marekani wameruhusiwa na sasa wapo katika makazi mapya.

“Watoto Sadia na Wilson waruhusiwa rasmi kutoka hospitali ya Mercy  na wanaelekea kwenye makazi yao mapya mjini Sioux City IA. Mungu azidi kuwaangazia nuru ya uso wake. Amani iwe nawe na Nesi wetu mpendwa kwa huduma kubwa mmefanya kwa watoto hawa na Tanzania,”ameandika Nyalandu.

Jana Nyalandu aliandika kuwa mtoto Doreen ataendelea kuwepo hospitali katika wodi ya watoto akiendelea kupata huduma za karibu hadi itakapoamuliwa vinginevyo.

Irene Uwoya Alamba Shavu Nono...Ateuliwa Kuwa Balozi

$
0
0

KAMPUNI ya simu za mkononi ya itel mobile Tanzania leo imetiliana saini na msanii wa Bongo Muvi, Irene Uwoya kuwa balozi wake atakayeitangaza kampuni hiyo kwa kipindi cha mwaka mmoja.


Akizungumza katika hafla hiyo Hafla hiyo iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam katika Hoteli ya Hhyatty Regency, Ofisa Habari wa Kampuni hiyo, Zwolle Fernando


“Sisi Itel Mobile Tanzania tumefanya makubaliano ya kushirikiana na  msanii Irene Uwoya ambaye atazitangaza bidhaa zetu kwa muda wa mwaka mmoja kuanzia sasa. Tunaamini kupitia yeye ataweza kuuunganisha Itel Mobie na Watanzania kwa ujumla wao.”


Aidha alifafafanua kuwa wanaamini jamii itafaidika kwa kupata elimu kuhusu bidhaa zao kupitia kwake watasaidiana nae hasa kwenye matukio ya kuonesha ukarimu kwa baadhi ya makundi ya jamii ambayo watayaendesha kupitia mpango wao uitwao Charity Event Programs na mengineyo.


“Sote tunafaham mchango wa Uwoya kwenye jamii, amekuwa akielimisha kupitia muvi zake, kwa kutambua hilo sisi itel tutashirikiana nae kikamilifu kuhakikisha jamii inakipata kile inachotarajia kukipata kutoka kwetu na kwake pia.alisema Fernando.


Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Itel Mobile Tanzania, Cooper Chen alielezea kampuni yao kwamba inajishughulisha na masuala ya teknolojia na uvumbuzi wa simu ambayo mpaka sasa inakadiliwa kufikisha miaka kumi tangu kuanzishwa kwake.


Na karibu kipindi cha mlongo mmoja kampuni hiyo imekuwa ikitamba kwa kusambaza bidhaa zake kwenye zaidi ya nchi 45 duniani kote na kwa kipindi cha mwaka wa 2016 kampuni hiyo iliuza zaidi ya simu milioni 50 barani Afrika na kushika nafasi ya kwanza kwenye tatu bora ya kampuni za simu zenye idadi kubwa ya mauzo ya bidhaa zake.     


“Tunazalisha bidhaa bora kwa sababu tunaamini kwamba tunawapatia wateja wetu bidhaa za mawasiliano zenye viwango vya juu na huduma ya kuridhisha,tunaisaidia jamii kuungana na jamii nyingine za kimataifa katika kushirikiana kuleta maendeleo na maisha bora zaidi.

Mzee Yusuph anakutaka ufute nyimbo zake kwenye simu yako

$
0
0

Aliyekuwa mfalme wa muziki wa taarab nchini, Mzee Yusuph amefunguka na kueleza kuwa watu wote walio na nyimbo zake kwenye simu zao wafute na kuacha kusikiliza ili kuepuka dhambi.


Katika mahojihano na kipindi cha Mitikisiko ya Pwani cha Times Fm, Mzee Yusuph ameelezea maisha yake ya ndoa, kidini na kiuchmi yalivyo kwa sasa ukilinganisha na hapo awali.


“Mimi nikikubali watu wacheze nyimbo zangu ina maana nimeruhusu dhambi tena ni bora nirudi kuimba muziki tena hivyo, watu wote waliokuwa na nyimbo zangu kwenye simu zao wafute na kuacha kusikiliza kuepuka dhambi,” amesema Mzee Yussufu.


Mzee Yussufu amesema yeye hayupo kwenye kundi lake la ‘Jahazi Modern Taarab’ kama baadhi ya watu wanavyodhani na wala hafuatilii kabisa kundi hilo.


“Nilitaka kulivunja Kundi la Jahazi lakini sheria za nchi haziruhusu nikaliacha na haya niliambiwa na Basata wenyewe. Vyombo vya bendi ya Jahazi havikuwa vya kwangu tulikuwa tunasaidiana na mabosi,” amesema.


Katika hatua nyingine Mzee Yusuph amesema maisha ya kiuchumi kwa sasa ni toufauti na kipindi alichokuwa anafanya muziki kwani hapo awali kwa wiki alikuwa anaweza kutengeneza milioni moja na nusu mpaka mbili ila sasa kushika laki tano au milioni inaweza kumchukua miezi miwili.


Ameongeza kuwa wake zake wanne bado anaendelea kuishi nao kama kawaida, na kuwa na wake ni jambo ambalo amehimizwa na sio amri, na kwa sasa wanamjua ni mtu wa namna gani na mambo yote yanaenda sawa hakuna hata mmoja anayefanya sivyo.

Familia yakanusha, “Aliyelazwa Muhimbili siye aliyechora Nembo ya Taifa”

$
0
0


Ikiwa ni siku chache tangu taarifa ya mzee ambaye alidaiwa kubuni na kuchora Nembo ya Taifa kuripotiwa na Serikali kuamua kumpatia msaada wa matibabu, familia moja imeibuka na kudai mzee huyo anayetajwa kuhusika kubuni siyo, bali ni mzee wao na ameshafariki.

Serikali kupitia Wizara ya Afya iliamua kumsaidia kimatibabu mzee Francis Maige maarufu kama ‘Ngosha’ ambaye alilazwa Hospitali ya Amana na kuamua kumhamishia Hospitali ya Taifa Muhimbili ambapo baada ya tukio hilo familia nyingine imeibuka na kudai kuwa mzee wao ambaye sasa ni marehemu ndiye mchoraji wa Nembo hiyo.

familia hiyo ambayo imeamua kufunguka na kuelezea kila kitu ukiwepo ushahidi wa mzee wao kuchora Nembo hiyo.

“Ushahidi ambao tunao ni wale watu wa rika lake ndiyo walikuwa wanashuhudia kwamba yeye ndiye aliyechora.” – Yehoshaphat Jeremiah Kabati (Mtoto wa tatu wa anayedaiwa kuchora Nembo ya Taifa)

My Story: Nilivyojikuta Naupenda Ukimwi Alioupata Mpenzi Wangu na Kilio Chake (Sehemu ya Pili 2)..!!!

$
0
0

Inaendelea....!!!

Siku ya tatu iliwadia, nilijipanga sana kumshawishi ausikie moyo wangu. Lakini alisisitiza tena kwamba hahitaji nimpigie simu wala kumtumia meseji kwa sababu hayuko tayari kuwa katika mahusiano na mtu yeyote…na kweli zilipita siku mbili nikiwa bize kumtafuta katika simu bila majibu.

Nilipoendelea sana, niligeuka kuwa usumbufu kwake.

“We mwanaume… kwanini tunasumbuana hivi?? Unanimalizia chaji, nikwambie kwa lugha gani? Hivi huna kazi za kufanya au ndugu wa kuwapigia simu?” alinambia kwa ukali sana.

“Naomba nikwambie ukweli tu ndugu yangu…mimi nina mtu mwingine ambaye amekwisha nitolea mahari, sasa tayari unajua kinachofuata, tusiharibiane please.”

Kufikia hapo moyo ulishituka mithili ya sahani nzuri za udongo zilizodondoka kwenye vigae imara. Nilitaka kupiga kelele kwa sauti kama aliyeona jinamizi, Duuu!!! Kweli nilikubali kutoka jasho na kuhema sana sio lazima uwe umekimbia au kubeba mzigo.

Kipindi nikiwa bado nimepigwa ganzi ya maneno hayo.. nilimsikia akiendelea kuongea na kusema “tafadhali!! usipige simu yangu ovyo utaniharibia ndoa yangu……mimi sasa nina mume tena mpole kama huamini basi muulize mtu yeyote wa karibu yangu atakwambia…so jiheshimu” kisha akakata simu.

Hadi kufikia hapo kwa wale waliowahi kukutana na hali hiyo naamini wanayatambua maumivu hayo…kwahiyo wanaweza kuyahisi maumivu niliyokuwa nayo kwa wakati huo. Kiufupi tu ni kwamba inauma zaidi ya sana.

Machozi yalianza kunitiririka. Nilikunja sura na kulia kama mtoto aliyefinywa. Nikijiuliza, muda wote nimepigwa na vumbi la chaki, nimeamka asubuhi na mapema, nimejinyima kwa kila namna ili niweze kutimiza ndoto za mpenzi wangu katika elimu yake lakini hatua ya mwisho ananiambia tayari yeye ni mchumba wa mtu na tayari mahari kishatolewa!! Kwahiyo nilimsomeshea mwanaume mwingine!

Nilijiuliza kama amepata mchumba hata wa kufikia kumtolea mahari basi mahusiano yao yalianza kitambo kidogo. Sasa kwanini muda wote alikuwa akiomba pesa kutoka kwangu?? Hata hatua ya mwisho aliomba nauli kutoka kwangu akamalizie mitihani yake, kwanini asingemuomba huyo mchumba wake?

Basi… zilipita kama siku tatu pasipo kumtafuta huku nikiwa katika wimbi kubwa la mawazo hatimaye nilishindwa kujiuzuia na kuamua kumpigia simu….lakini maneno yaliyotoka hapo hadi nilijuta kupiga simu.

Baada ya simu kuita mara kadhaa bila majibu hatimaye alipokea na kusema kwa lugha ya ukali sana “hivi wewe!! unataka kunambia hata mama yako alishafariki umeshindwa kumpigia simu umekaa kunisumbua mimi? aliweka pozi kidogo kisha akaendelea

“Hivi vyalimu navyo sijui vipi……havielewi! Sijui huko darasani vinafundisha nini, We si nimekwambia sitaki unipigie simu wala kunitumia meseji au hadi nibadili hii namba kwa ajili yako ndio ujue namaanisha ninachokisema!? Alimaliza kwa kunisonya kisha akakata simu.

Daaaa!!!! kufikia hapo nilijihisi kama vile pakiti ya chumvi imesiginwa kwenye kidonda kibichi tena bila huruma.

Nikijiuliza huo ualimu wangu ulivyofanya kazi kubwa kumlipia ada na mahitaji mengine ya shule na awapo nyumbani..leo hii ualimu kwake ni kama tusi na ni kazi ya kudharaulika, kweli waswahili walisema bora umfadhili mbuzi unaweza kuambulia hata mchuzi kuliko binadamu asiye na shukrani.

Mtu ambaye alitakiwa anishukuru sana kwa juhudi zangu kwamba licha ya kuwa napokea mshahara kidogo niliweza kujinyima kwa kila hali ili niweze kumuandaa kuwa mke bora wa familia yangu hata wakati mwingine nashindwa kuwahudumia ndugu na rafiki zangu hatimaye naambulia matusi na dharau…inauma sana!!!!

Hakika uchawi binadamu wengine hawazaliwi nao ila machungu na maumivu wanayosababishiwa na binadamu wenzao huwafanya kuingia katika uchawi na ushirikina ili kutafuta faraja katika nafsi zao.
Kumbe inaweza isiwe zoezi gumu kubeba silaha na kutafuta uhai wa mtu au kumdhuru mtu, hii ni kutokana na binadamu kuwazamisha wenzao katika dimbwi la matatizo na majuto na wao wakakosa uwezo na hekima za kupambanua  Ukuu na Utukufu wa Mwenyezi Mungu katika kuchagua njia sahihi.

Lakini katika yote ushindi wa maamuzi unaweza kupatikana katika kile unachoamini hasa kufanya maamuzi ambayo hutojuta baadae . Hivyo, nilipiga moyo konde nikaomba hekima ya Mungu itawale katika maamuzi yangu na inipitishe kando katika mbigiri za kisasi zilizotanda moyo wangu nisahau yote.

Nashukuru kwa mapenzi ya Mungu niliweza kusahau na kusamehe yote yaliyopita nikawa bize na shughuli zangu za kutafuta maisha. Yaani tangu siku ile sikuwahi kumpigia simu wala meseji wala kumuulizia kwa jambo lolote yaani yeye na maisha yake na mume wake mimi bize na mambo yangu
Lakini cha ajabu hivi karibuni takribani miezi miwili iliyopita alinipigia simu na hii ni baada ya zaidi ya mwaka mmoja kupita pasipo kuwasiliana naye. Niliitazama simu nikaona ni namba ngeni lakini nilipopokea tu nilimtambua mapema kwa sauti yake.

Ambapo baada ya salamu alijikita moja kwa moja kuulizia maisha yangu…kabla sijamjibu chochote nilimuuliza, “Mbona bize na simu? Vipi huogopi kupoteza ndoa yako? Au sasa umeshaizoea?”
“Aaaaa!!! kawaida tu,” alinijibu kwa unyonge kabla hajaanza kuleta habari nyingine.

Niliongea naye kwa dakika kadhaa kisha nikakata simu na kuendelea na ratiba zangu..lakini tangia hapo amekuwa na mazoea ya kutaka kuongea nami hadi inafikia wakati analalamika kwa baadhi ya ndugu na rafiki zangu. Ndipo nilipopata taarifa zake kwamba ni kwa muda mrefu sasa wametengana na huyo mume wake…jamaa alimkimbia.

Itaendelea Kesho..!!!

Utunzi wa Edward Lucas; 0655 545 064

Zingatia Vyakula vya Aina Hii Ili Kuilinda Mimba Yako na Athari za Magonjwa..!!!

$
0
0

Mjamzito anapaswa kuepuka ulaji wa kupita kiasi ili asinenepe kupindukia (Obesity). Kulingana na kijarida kiitwacho Krause’s Food, Nutrition and Diet Therapy, mtoto anayezaliwa akiwa na uzito wa chini sana anakabiliwa na hatari ya kufa mara 40 zaidi kuliko yule aliyezaliwa akiwa na uzito wa kawaida.

Hatari ya kupinda uti wa mgongo inayoletwa na kutoziba kwa mrija wa neva wa kitoto kilicho tumboni, inaweza kuzuiwa iwapo mjamzito ana kiasi cha kutosha cha aina fulani ya vitamini C.

Kwa kuwa mrija huo huziba siku ya 24 hadi ya 28 baada ya mimba kutungwa, baadhi ya wanawake wanaopanga kupata mimba hula vyakula vyenye vitamini hiyo.

Aina hiyo ya vitamini C na madini ya chuma yanaweza kupatikana katika maini, maharage, mboga zenye majani mabichi, njugu na nafaka zilizoongezwa vitamini na madini mbalimbali. Kuchanganya chakula chenye vitamini C, kama matunda yaliyotoka shambani karibuni pamoja na chakula chenye madini ya chuma huongeza madini hayo mwilini.

Kila siku mjamzito anahitaji kula matunda, mboga hasa zilizo na majani ya rangi nzito ya kijani, na zenye rangi ya machungwa, au nyekundu, maharage, soya, dengu na njegere, nafaka kama ngano, mahindi na shayiri—hasa zile ambazo hazijatolewa maganda au zilizotiwa vitu vingine, chakula kinachotokana na wanyama kama samaki, nyama ya kuku, nyama ya ng’ombe, mayai, jibini na maziwa, hasa yale ambayo yametolewa mafuta.

Mafuta, sukari na chumvi vinapaswa kutumiwa kwa kiasi. Mjamzito anywe maji mengi. Aepuke vinywaji vyenye kafeini na vyakula vilivyotiwa dawa za kuhifadhi na kemikali nyinginezo kama za kutia rangi na ladha.

Kuna vitamini ambazo zinaweza kudhuru. Kwa mfano, kiasi kikubwa sana cha vitamini A chaweza kumlemaza mtoto aliye tumboni.

Chuma ni madini muhimu pia. Mwanamke huhitaji madini mengi zaidi ya chuma anapokuwa mjamzito. Asipokuwa na kiasi cha kutosha, damu yake inaweza kuwa na upungufu wa madini hayo. Hali hiyo inaweza kuwa mbaya zaidi mwanamke apatapo mimba moja baada ya nyingine, kwa kuwa hana nafasi ya kurudisha kiasi kinachohitajika cha madini ya chuma.

Wasichana wenye umri wa chini ya miaka 16 ambao ni wajawazito wanakabiliwa na hatari ya kufa ya asilimia 60 zaidi kuliko wale walio na umri wa miaka 20 na kitu. Kwa upande mwingine, wanawake wenye umri unaozidi miaka 35 wana uwezekano mkubwa zaidi wa kuzaa watoto wenye kasoro, kama vile ugonjwa wa down.

UTUNZAJI WA MIMBA

Utunzaji wa mimba kabla ya kujifungua unaweza kuwasaidia wataalamu kuona hali ambazo huenda zikahitaji utunzaji wa pekee. Hali hizo zinaashiria kuwepo kwa watoto zaidi ya mmoja tumboni, shinikizo la juu la damu, matatizo ya moyo na figo na ugonjwa wa kisukari.

Mwanamke anapaswa kuomba msaada wa kitiba mara moja ikiwa damu inatoka kupitia sehemu ya siri, uso wake unafura ghafla, ana maumivu makali yenye kuendelea kichwani au uchungu kwenye vidole, anapoteza uwezo wake wa kuona ghafla au haoni vizuri, anaumwa na tumbo sana, anatapika sana, anaugua homa, mtoto aliye tumboni anaruka isivyo kawaida, umajimaji unatoka kupitia sehemu ya siri, anasikia maumivu anapokojoa, au hapati mkojo kama kawaida.

Mama anayekunywa pombe na kutumia dawa za kulevya (kutia ndani tumbaku) huzidisha hatari ya kumzaa mtoto aliye na akili pungufu, mlemavu, na hata aliye na tabia yenye kasoro. Mara nyingi wataalamu hupendekeza wajawazito wasiinywe hata kidogo. Wanapaswa pia kuepuka moshi wa sigara.

Ongezeko la uzito linalopendekezwa kwa mwanamke mjamzito ni kilogramu 9 hadi 12 kufikia wakati wa kujifungua. Hata hivyo, wasichana au wanawake ambao hawakuwa wakila chakula cha kutosha wanapaswa kuongeza kati ya kilogramu 12 hadi 15.

Kimenuka..Wafanyakazi wa Mochuari Mwananyamala Wapasua Maiti na Kuiba Kete za Unga

$
0
0

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro amefunguka kuwa wahudumu wa mochwari ya Mwananyamala wameiba jumla ya kete 32 za dawa za kulevya zilizokuwa kwenye mwili wa Raia wa Ghana aliyefariki dunia akiwa katika nyumba ya wageni

Kamanda Sirro amesema wahudumu hao wanne wote wamekamatwa na kukiri kwamba  baada ya kifo cha raia huyo wa Ghana aliyefariki ndani ya 'Red Carpet' iliyopo Sinza Dar es Salaam walipasua mwili wa raia huyo na kutoa kete hizo kisha kuziuza, na kuongeza wametaja watu ambao wamewauzia ambao nao wamekamatwa na wapo chini ya ulinzi wa polisi

"Yule Mghana ambaye alikutwa amefariki dunia tarehe 14/ 03/ 2017 kwenye nyumba ya wageni ya 'Red Carpet' na alichukuliwa na kupelekwa mochwari Mwananyamala lakini inaonekana wale wahudumu wali[pata taarifa kuwa ule mwili una dawa za kulevya, kimsingi walikula njama wakampasua na kutoa kete 32 za madawa ya kulevya na baada ya kuyapata waliyauza hayo madawa"alisema Sirro 

Kamanda Sirro aliendelea kusema kuwa mpaka sasa wanawashikilia watu wanne ambayo wamehusika katika jambo hilo.

"Mpaka sasa tunawashikilia watu wanne ambao wanakiri kupasua mwili huo ambao ni wahusika wakuu na ni wahudumu wa mochwari ya Mwananyamala lakini tumekwenda mbali zaidi baada ya kufanya upasuaji wamemuuzia nani naye amekatwa pia na anaeleza kuwa alinunua hayo madawa, lakini pia naye alichukua na kumuuzia mtu mwingine anayefahamika kwa jina la Ally Nyundo, huyu Nyundo tulishamkataga na kumpeleka kwa Mkemia Mkuu yeye alionekana ni mtumiaji, kimsingi tuna hao watuhumiwa wanne na huyo wa tano aliyekamatwa sasa tunaandaa jalada" alisisitiza Sirro 

Njia Sita za Kumnasa Demu Mkali Ambaye Anatingisha Mtaa Mzima..!!!

$
0
0

KUNA watu wamezaliwa wakiwa na hofu kubwa ya kuwaogopa mademu wazuri. Kuna mwingine akimuona demu mzuri mtaani, anajisemea kabisa kwamba; yule si taipu yangu, eti kisa kapendeza, msafi na anaonekana matawi fulani ya juu. 

Mwanaume anatakiwa kujiamini, hakuna mwanamke duniani ambaye si saizi yako, kila demu unayemuona mtaani basi jua kwamba huyo ni saizi yako ndiyo maana Mungu kamuweka katika dunia hii na wewe kufanikiwa kumuona.

 Leo nataka nikufundishe namna ya kumpata demu mkali, hata kama wewe ni muoga, unahisi kwamba mademu wa aina hiyo si taipu yako lakini naamini njia hizi zitakufanya kumpata kiurahisi kabisa na kufanya mambo yako, kama ni kupanga naye maisha au la.

TAFUTA JINA LAKE KWANZA

Unapomtaka demu mkali mtaani kwako, kitu cha kwanza tafuta jina lake. Hii itakusaidia kumshangaza. Wanawake wapo hivi, huwa hawapendi sana kujulikana, inapotokea msichana huyo ukaonana naye na kumuita jina lake, kwanza atasimama, atakuuliza umenijuaje? Nani kakwambia jina langu? Usiogope, kwanza tabasamu, hilo litamfanya kuona kwamba wewe ni mtu mzuri, jibu utakalompa, hakikisha linakuwa lile la kukutafuta baadaye.

Kwa mfano unaweza kumwambia: “Mbona nakufahamu! Wewe ni staa sana hapa mtaani, kila mtu anakujua!” ukimwambia hivyo, atataka kujua zaidi na zaidi, ni akina nani wanaomjua halafu mbona yeye siyo staa! Unachotakiwa kufanya ni kujiweka bize, mwambie ‘nitakwambia nimekujuaje ila kwa sasa kuna sehemu nawahi.’

Ukifanya hivyo itamfanya yeye kuwa na hamu ya kukutafuta. Hata ukimwambia akutafute baadaye, atakutafuta kwa lengo la kutaka kujua imekuwaje. Ukiona ameelekea kidogo, mwambie niachie namba yako, nitakwambia, si hilo tu, kuna mengi kuhusu wewe.

Nakwambia hivi, kwa hatua hiyo, hakuna msichana ambaye atakukazia namba yake, lazima atakupa.

USIMLETEE SANA SHOBO

Akikupa namba, usijifanye kuwa na haraka ya kumtafuta. Unachotakiwa kufanya ni kucheza na akili yake kwanza. Najua atakuwa na hamu ya kupata simu yako, kwa siku hiyo mkaushie mpaka kesho yake ndipo umtafute. Kuwa makini, usimpigie, wewe mtumie meseji, mwambie “Upo poa staa wangu wa ukweli?” atakachokifanya ni kuuliza wewe nani! Inawezekana akawa anajua, ila kwa mapozi ya kike ni lazima ajidai kuuliza. Mwambie ni yule mshikaji wa jana! Ongezea kwa kumwambia kwamba utamtafuta ukirudi kutoka kazini, hata kama huna kazi, jiongeze kidogo.

MPIGIE SASA, ANZA KUMSIFIA

Wanawake wanapenda sifa, wanapenda kusifiwa. Kitu cha kwanza mwambie kwamba kuna siku uliwasikia washikaji wakimzungumzia, kwamba demu fulani mkali, anajua kuvaa, ananukia vizuri, ukataka kumjua ndipo wakasema kwamba ni yeye. Hilo litamfanya kujiona anakubalika sana, kumbe watu wanamsifia mtaani, kumbe wewe unamuweka kwenye saiti yako.

Ukiwa unazungumza naye, jifanye mcheshi sana, mchekeshe, mwambie na wewe ulivyokuwa na hamu ya kumjua msichana huyo msafi na mrembo ndiyo maana ukaamua kumtafuta. Mpaka kufika hatua hiyo, ataanza kukukubali, kwa ucheshi utakaomuonyesha atakuona wewe mtu mzuri na mtakuwa mnaanza kuchati. Usimtongoze lakini muonyeshee dalili za kumtaka. Chati naye hata kwa wiki moja halafu fanya njia ifuatayo;

MUOMBE MTOKO WA KIZUSHI

Hapa simaanishi mtoko wa kwenda klabu au ule mtoko siriazi sana, kwanza mwambie wewe siyo mtu wa klabu ila unataka kumpeleka sehemu fulani hivi kwenda kunywa kahawa au juisi. Kwenye kumuomba mwambie utajisikia furaha ukiwa unatembea na demu mkali kama yeye, mwambie kila mwanaume anajisikia fahari akitembea na msichana anayependeza na kunukia vizuri kama yeye. Kwa sifa hizo za mara kwa mara, atakwambia anayo nafasi hivyo atakukubalia.

KUWA MAKINI KWENYE MTOKO WAKO

Demu yeyote anapenda mwanaume mchangamfu, jinsi utakavyomuonyeshea uchangamfu kwenye simu iwe hivyohivyo hata ukionana naye na kutembea naye. Usimuonyeshee akahisi yule wa kwenye simu ni tofauti na huyu.

NENDENI MNAPOKWENDA

Usitake kutumia sana pesa, usitake kuingia gharama kubwa kwani mademu wana kawaida ya kumsoma mwanaume siku ya kwanza tu. Kama vipi mwambie wakati wa kurudi mtembee kwa miguu, hii itakupa nafasi ya kuzoeana sana, hata kama akitaka mpande usafiri, mwambie mtachukua mbele, kwanza omba kutembea naye hata nusu kilometa. Katika maongezi yote usijisifie ila mfanye ajue unajua mambo mengi sana.

Jaribu kumwambia mambo ambayo unaamini hata yeye hayajui na angefurahi kuyajua. Mwambie kuhusu hadithi ya Romeo And Juliet, mwambie kuhusu Malkia Cleopatra alivyotetemesha kwa uzuri wake, mwambie mambo mengi ambayo utaamini kwamba hayafahamu ila angependa ayafahamu.

MALIZIA KWA KUMWAMBIA HIVI…

Mkiachana na kurudi nyumbani, mpigie simu, mwambie unamisi uwepo wake, ungetamani uwe naye tena, unaimisi harufu yake, mwambie ulikuwa karibu na ua kwa hivyo ile harufu yake imekupata hata wewe. Mchekeshe kidogo, mwambie unamisi tabasamu lake, mwendo wake wa twiga, mwambie unamisi uzuri wake, yaani huo ndiyo muda wa kumsifia mpaka ajione duniani hakuna mwanamke kama yeye. Ukifanya hayo, jua kwamba huyo mwanamke lazima akukubali kwani atahisi yupo na mtu sahihi. Tukutane wiki ijayo kwa mada nyingine bomba zaidi.

Unashindwa Kuweka Akiba Ya Kipato Chako Kidogo? Tumia Njia Hizi..!!!

$
0
0

“Kweli natafuta na napata… lakini fedha hazitoshi kabisa…”. Hizo ni kawaida kuzisikia kauli hizi katika maisha ya kila siku ya watanzania wengi hususan huku uswahilini kwetu ambapo wengi tunafanya kazi za kipato cha chini.

Ingawa kuweka akiba ni mtihani mkubwa kwa watanzania wengi, lakini ni mtihani mgumu zaidi kwa wananchi wa kipato cha chini ambao maisha yao yanategemea sana kile wanachokipata, lakini hata wanapokipata huwa hakitoshi siku zote.

Kwa bahati mbaya utamaduni wa kuweka akiba kwa wananchi wengi nchini ni utamaduni mgumu kuuishi, hii inatokana na mtazamo wa wengi kuwa akiba ni fedha inayowekwa kutokana na ‘ziada katika kipato’ cha mtu fulani. Mtazamo huo ni kikwazo kikuu cha kwanza, kwa kuwa kama unataka kuweka akiba lazima ujenge tabia ambayo baadae itakuwa utamaduni wako (mtindo wa maisha) wa kuweka akiba.

Tunapaswa kufahamu kuwa kipato kinachoitwa cha ‘ziada’ hakina maana ya kuwa ‘kimezidi’, hivyo kutokuwa na pato la ziada kwenye pato kuu kisiwe kigezo cha kwanza cha kutoweka akiba. Lakini hili halitawezekana kama hautajenga utamaduni wa kuweka akiba na kuuishi utamaduni huo.  Yaani kuweka akiba kuwe sehemu ya maisha yako.

Ni muhimu sana kuweka akiba, hiyo nilijifunza kutoka kwa bibi yangu ambaye hivi sasa amepumzika (Apumzike kwa Amani), ambaye alikuwa akiweka kibubu kwa kufukia kwenye sakafu ya udongo ya nyumba yake ya nyasi. Alikuwa na kipato kidogo sana na kisichotabirika, lakini ilikubidi uwe na maelezo ya kutosha kumshawishi kukigusa kibubu chake.

Ingawa nilimuona kama bahili kwa kuwa nilikuwa najua kuna sarafu anapata kutokana na kilimo chake cha mihogo kupitia shamba lake dogo, kila alipokivunja kibubu chake tulitabasamu muda wote na kusahau machungu kwani alifanya vitu vya maendeleo na kutimiza lengo fulani.

Kwa maisha ya sasa, njia hiyo inaweza kuwa ‘kituko’ lakini unaweza kutumia njia mbadala kwa lengo lilelile.

Hii ni namna ya kujenga utamaduni wa kuishi na kuweka akiba kupitia kipato kidogo unachokipata. Kama kipato chako ni kidogo sana, ukizifuata hizi unaweza kuwa na uwezo wa kuweka akiba angalau kwa asilimia 10 ya pato lako kwa kila mwezi.

1. Kuwa na nidhamu ya fedha

Iheshimu kila sarafu unayoipata. Tengeneza bajeti yako na utafakari kwa kuweka vipaumbele vya mahitaji yako kulingana na kipato. Hakikisha hautumii fedha bila kuwa na sababu za msingi na kujiridhisha kuwa unahitaji kutumia kiasi hicho cha fedha.

Hii ndio maana ya kuwa na nidhamu katika matumizi ya fedha kwa kuwa ingawa unao uwezo wa kutumia chochote ulichonacho bila kuhojiwa, bado unaweza kutengeneza ‘bunge’ kichwani kwako na kujadili mantiki ya matumizi husika.

2. Weka Malengo yanayopimika, yategemeze na akiba yako

Ili uwe na nguvu ya kuweka akiba, unapaswa kuweka malengo muhimu unayotakiwa kuyafikia katika kipindi fulani. Hakikisha malengo hayo yanapimika na yanatekelezeka endapo utaweza kuweka akiba kwa kipindi hicho. Ukiweka lengo kubwa sana, unaweza kukata tamaa baada ya kugundua hautaweza kutekeleza bila kujitesa sana au kwa muda uliopanga.

Malengo yanayopimika yatakupa nguvu ya kuweka akiba yako ndogo kwa kuwa utakuwa unaona jinsi unavyoyasogelea malengo yako kwa kupima ongezeko la akiba husika. Kumbuka kila ongezeko katika akiba yako lina maana kubwa sana kuliko kile unachokitumia kikakwisha.

3. Jitenge na Kipato chako

Ingawa wewe ndiye msimamizi na mdhibiti wa fedha zako, unapaswa kujitenga na fedha zako na kuhakikisha kuwa unakuwa msimamizi unayezitendea haki fedha hizo. Usiishi kwa kufuata kile anachofanya mtu fulani. Kama unapenda kile anachokifanya, jaribu kutafakari, weka kwenye mpango wako, kipime na anza kukifanyia kazi.

Kumbuka kuwa fedha unazoweka akiba, usipojitenga nazo na kuzichukulia kama ni fedha unazodaiwa kwa ajili ya kukamilisha jukumu au lengo fulani muhimu, utazitumia aghalabu.

4. Jipunguzie Kipato kwa Asilimia

Kwa kipato chako kuwa kidogo hakimaanishi hupati kabisa, au ndio kipimo cha mwisho cha kipato chako. Kumbuka utatumia kulingana na kile unachoingiza. Hivyo, kuwa na utaratibu wa kujipunguzia kipato chako angalau kwa asilimia 10. Asilimia hizo uzihamishie kwenye kibubu chako cha muda mrefu cha malengo makubwa. Hata kama umechukua mkopo kwa ajili ya kitu fulani, tumia njia hii kuweka akiba. Wakati unamaliza kurejesha mkopo wako, kibubu chako kitakuwa mtaji mpya.

5. Kaa Mbali na Kibubu chako!

Kwa usili ya binadamu yoyote, tamaa ni sehemu ya maisha yetu, ila tunazidiana kiwango cha tamaa. Unapotamani kuwa na kitu fulani, mara nyingi unajiangalia mifukoni. Hivyo tamaa ya jambo fulani ikikuzidia, unaweza kujikuta ukivunja kibubu chako kabla ya muda muafaka kwa sababu tu kiko karibu na wewe.

Tafuta namna nzuri ambayo itakuwa rahisi zaidi kwako kuweka pesa hiyo lakini vigumu sana kwako kuichukua.

Kwa mfano wa kawaida tu, unaweza kufungua akaunti Benki, kisha ATM Card ukaiacha kwa mtu unaemuamini mkoa fulani, mtu huyo asifahamu ‘password yako’ lakini pia mwambie lengo lako. 
Wakati yeye hajui password ya ATM Card yako japo anayo (Hasa zile zenye picha), wewe pia unafahamu password lakini huna uwezo wa kuchukua pesa bila ATM Card yako. Ugumu huo unaweza kukusaidia wewe kwa hali ya kawaida kabisa.

Hata hivyo, hivi sasa kuna mifuko mingi ya kijamii pamoja na njia za kibenki ambazo ni salama zaidi ambazo zitakufanya kuweka pesa kwenye akaunti yako lakini huwezi kuichukua kwa muda fulani, na utakapofikisha muda muafaka unapata riba ya asilimia kadhaa.

Kumbuka usipoweka akiba huku unawaza maendeleo makubwa, ni kama unakimbiza upepo. ‘Akiba Haiozi’.

Unachopaswa Kufanya Katika Hatua Za Awali Za Uhusiano Na Msichana Unaempenda..!!!

$
0
0

Kwa kawaida Mwanaume unapohitaji kuanza uhusiano na msichana unaempenda sana, kiu na njaa ya kuwa naye huwa iko katika kiwango kisichopimika.

Hasa unapokuwa unaanza kuwasiliana nae na ukafanikiwa kumsogeza karibu na kumuonesha kwa vitendo kuwa unampenda na kwa bahati nzuri, akaanza kukuwashia ‘Taa ya Kijani’.

Hata hivyo, mwanzo huu unaweza kuwa mbaya kwako endapo hautazingatia kanuni moja muhimu sana kati ya kanuni nyingi za kuendeleza na kudumisha mapenzi yaliyochipua yanayohitaji mbolea na maji safi kutoka kwako ili yachanue.

Ingawa ukweli ni kwamba muonekano wake na mvuto alionao mwanamke unaempenda unaweza kuwa ndio chanzo kikubwa kilichokusukuma kumfuata na kuanzisha maongezi kwa mara ya kwanza, ni muhimu sana kutomuonesha dalili zozote kuwa ‘ngono’ ndio hitaji lako la kwanza au kitu ulichokipa kipaumbele.

Kabla hujamwambia kitu chochote, kumbuka yule ni mtu mzima, mrembo aliyewavutia wengi kabla yako. Jiulize maswali kadhaa, je, kwa makadirio ya haraka haraka unadhani kuna neno jipya utakalomwambia ili akuamini wewe tofauti na wanaume wengine waliowahi kuongoa naye?

Hapo ndipo utagundua kuwa maneno yako yana nafasi ndogo sana kwake hivyo unapaswa kuyachagua kwa umakini mkubwa ili yapenye masikio yake na kuyahifadhi kwa muda ili ayatafakari kabla hayauruhusu moyo wake kuyatafrisi.

Wataalam wa masuala ya mahusiano wanashauri kuwa lugha ya mwili (body language) inaongea kwa sauti zaidi ya sauti yako. Hivyo, unapaswa kujiweka vizuri tangu unapomuangalia, unapomsalimia, mwili wako unapaswa kuongea kitu.

Hii inakuwa rahisi sana kama moyo wako umempenda kweli, mwili huongea wenyewe bila kuulazimisha.

Wanawake wengi wanajua kuzisoma lugha za mwili hata kabla ya lugha ya sauti. Hata hivyo, mioyo yao huwa migumu kuamini kile wanachokiona au kukisikia hususan kama wameshawahi kuumizwa mara kadhaa (kitu ambacho kipo kwa wanawake wengi hasa warembo).

Hata hivyo, baadhi hujikuta wanakupa nafasi ya kukusikiliza baada ya kugundua kuwa wewe unaonesha kupenda kweli tangu machoni. Imani ambayo huwepo kwa muda tu huku wasiwasi wa kuwa huenda unadanganya unakuwa juu zaidi.

Maneno na vitendo vyako vitakusaidia sana katika kuuteka moyo wa msichana unaetaka kuanzisha nae uhusiano ‘serious’ hivyo yachague kwa umakini. Tumia muda fulani mdogo kumsoma anachopenda, story anazopenda kuongelea na sehemu anazopenda kutembelea. Fahamu pia aina ya filamu anazopendelea na mengine ili uweze kuwa aina ya mwanaume unayeweza kucheza kila ngoma atakayokupigia katika mtiririko wa maisha.

Utafiti huo utakurahisishia maisha, na endapo utakaa naye vizuri na uhusiano wenu unaweza kuanza hata bila kumwambia maneno mengi. Yaani vitendo vikaongea hata bila kutumia maneno yanayotafsirika kama ‘kutongoza’. Kitakachofuata ni kumwambia maneno machache ili asikie alichokuwa anataka kusikia kutoka kwako. Funguka, na mwambie kiunaga ubaka.

Kagame Atangaza Kuachia Madarka ya Urais Rwanda..Awataka Wanyarwanda Kufikiria Mtu Sahihi Ili Kuziba Nafasi Yake..!!!

$
0
0

Kuelekea uchaguzi mkuu nchini Rwanda unaotarajiwa kufanyika Agosti 3 mwaka huu, Rais wa Rwanda Paul Kagame ameeleza kinaga ubaga kuwa ukomo wake wa kutawala ni mwaka 2024.

Rais Kagame amethibitisha taarifa hizo kupitia mtandao wa Jeune Afrique kuwa awamu hii ya miaka saba ndiyo ya mwisho na Wanyarwanda wanatakiwa waanze kufikiria mtu mwingine atakayewaongoza baada ya mwaka 2024.

“Inawezekana natakiwa niliangazie suala hili katika siku chache zijazo nitakapoanza mbio za urais. Kuna aina ya makubaliano kati yangu mimi na RPF-Inkotanyi kwa upade mmoja, na raia wa Rwanda kwa upande mwingine“,alisema Kagame na kuendelea kuweka wazi kuwa

“Raia, kupitia kura ya maoni ya Disemba 2015, waliniomba niendelee kuwaongoza nikakubali, ila muda mwafaka wa kupumzika umewadia na waomba waanze kufikiri nje ya mimi baada ya miaka saba“,alisema Kagame kwenye mahojiano yake na mtandao wa Jean Afrique.

Kwa sasa hakuna shaka yoyote kuwa Rais Kagame atashinda uchaguzi wa urais mwaka huu na ni ushindi ambao umekuwa ukitabiriwa kwa muda mrefu na Wanyarwanda.

Mwaka 2015 Wanyarwanda wapatao milioni 4 ambao ni zaidi ya asilimia 70% ya wapiga kura, walipaza sauti zao kulitaka Bunge lirekebishe katiba ili Kagame apate nafasi ya kuendelea kutawala.

Bunge lilifanya hivyo ili limruhusu rais huyo ambaye ana umri wa miaka 59 kuwania awamu zingine mbili hadi mwaka 2024.

Klabu ya Everton Yathibitisha Kutua Tanzania Kucheza na Simba na Yanga..!!!

$
0
0

Kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter wa klabu ya soka ya Everton, umethibitisha kuwa klabu hiyo kuwasili nchini mwezi Julai na itakuwa ni timu ya kwanza inayoshiriki Ligi kuu nchini Uingereza kucheza na timu za Afrika mashariki.

Ujio wa Everton ni sehemu ya maandalizi ya msimu ujao wa ligi, Vilabu vinavyo tarajiwa kunufaika na ujio huo ni vile ambavyo vipo chini ya udhamini wa kampuni ya Michezo ya kubashiri ya SportPesa. Kwa hapa nchini mpaka sasa kampuni hii imeingia mkataba na klabu tatu ambazo ni Simba SC, Yanga SC pamoja na Singida United .

Kwa mujibu wa Kampuni ya SportPesa, wameandaa ligi ijulikanayo kama SportPesa  Super Cup , inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi tarehe 5  / 6 / 2017, kwa kushirikisha jumla ya timu 8  kutoka mataifa mawili, Tanzania na Kenya, na mshindi wa mashindano hayo atacheza na timu inayoshiriki ligi kuu nchini Uingereza.

Mshindi wa michuano hiyo mikubwa atapata kiasi cha Dola za kimarekani Elfu thelathini (USD 30,0000) na mshindi wa pili wa michuano hiyo anatarajia kupata kiasi cha Dola za kimarekani Elfu kumi (USD 10,000).

Kutokana na kuthibitisha kwa klabu ya Everton bilashaka mshindi wa mashindano hayo atacheza na klabu hiyo kongwe iliyoanzishwa  mwaka 1978.

JPM Kutikisa Tena Baraza la Mawaziri..Miongoni mwa Hawa Huenda Akamrithi Prof Muhongo Kwenye Wizara ya Nishati na Madini..!!!

$
0
0

UAMUZI wa Rais John Magufuli kutengua uteuzi wa rafiki yake, Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo ni wa tatu tangu aunde Serikali, sasa analazimika kukuna kichwa kuteua waziri mwingine kushika nafasi hiyo.

Wakati hilo likisubiriwa, wanasiasa na wasomi wameeleza kuwa hakuna waziri atakayeteuliwa na kusalimika katika wizara hiyo, kwa madai kwamba inazungukwa na rushwa kubwa za kimataifa, mikataba mibovu na kuingiliwa uamuzi na Ikulu.

“Ndiyo maana tumekuwa tukipendekeza kugawanywa kwa wizara hii kwa maana ya kuwa na wizara mbili; ya Nishati na ya Madini,” alisema Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema.

Mei 20 mwaka jana, kwa mara ya kwanza Rais alitengua uteuzi wa rafiki yake mwingine wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga na nafasi yake kuzibwa na Mwigulu Nchemba, ambaye awali alikuwa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, huku Mbunge wa Buchosa, Dk Charles Tizeba akiteuliwa kuchukua mikoba ya Mwigulu.

Mabadiliko ya pili ya Baraza la Mawaziri yalifanyika Machi 23, baada ya mkuu huyo wa nchi kumteua Dk Harrison Mwakyembe kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kuchukua nafasi na Nape Nnauye ambaye aliachwa.

Katika mabadiliko hayo, Profesa Palamagamba Kabudi ambaye awali aliteuliwa na Rais kuwa mbunge, alipewa Wizara ya Katiba na Sheria ambayo kabla ya mabadiliko hayo ilikuwa ikiongozwa na Dk Mwakyembe.

Rais hakusubiri Profesa Muhongo ajitathmini, baada ya kupokea taarifa ya uchunguzi wa sakata la kiwango cha madini kwenye kontena, alikiri kuwa na urafiki na Mbunge huyo wa Musoma Vijijini na hilo halikumfanya asite kumwajibisha, kwani baada ya kuisoma ripoti hiyo, Ikulu ilituma taarifa kwa vyombo vya habari ikieleza kuwa Rais ametengua uteuzi wa mtaalamu huyo wa miamba.

Mara zote mbili alizofanya mabadiliko ya Baraza la Mawaziri, Rais Magufuli amekuwa na utaratibu wa kuhamisha mawaziri kutoka wizara moja kwenda nyingine au kuteua wabunge na kuwapa wizara.

Katika mabadiliko hayo mawili aliyofanya, ni Dk Tizeba pekee ambaye aliteuliwa kuwa waziri kutoka miongoni mwa wabunge wa majimbo.

Iwapo Rais Magufuli atazingatia utaratibu wa mtangulizi wake Jakaya Kikwete kuteua waziri kutoka mkoa ambao waziri aliyeondoka anatoka, huenda nafasi iliyoachwa wazi na Profesa Muhongo ikajazwa na wabunge kutoka mkoa wa Mara.

Baadhi ya wabunge wa CCM kutoka mkoani Mara ni Boniface Getere (Bunda Vijijini), Nimrod Mkono (Butiama), Vedastus Mathayo (Musoma Mjini), Kangi Lugola (Mwibara) na Lameck Airo (Rorya).

Pia, kauli ya CCM jana kwamba imechoshwa na mauaji yanayotokea kila uchwao mkoani Pwani, ni sawa na kutuma ujumbe kwa Rais Magufuli kwamba kuna tatizo katika Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, kuchochea ukubwa wa mabadiliko.

Utaratibu

Miongoni mwa wateule wake ni Naibu Spika, Dk Tulia Ackson. Novemba mwaka 2015 Naibu Mwanasheria Mkuu huyo wa zamani alichukua fomu za kuwania uspika kupitia CCM kabla ya kujitoa dakika za lala salama kisha akateuliwa na Rais Magufuli kuwa mbunge wa viti maalumu.

Baada ya kujitoa, alijitosa kuwania unaibu Spika ambapo wabunge 250 walimpigia kura ya ndiyo.

Wengine walioteuliwa kuwa wabunge na akawapa wizara ni; Waziri wa Mambo ya Nje, Dk Augustino Mahiga, Profesa Makame Mbarawa (Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano), Profesa Joyce Ndalichako (Elimu), Dk Philip Mpango (Fedha) na Dk Abdallah Posi  ambaye alikuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu.

Hata hivyo, Posi aliteuliwa kuwa balozi kufuatia dosari ya kikatiba katika uteuzi wa wabunge 10 wa kuteuliwa na Rais ambapo Ibara ya 66 (1)(e) inaeleza katika nafasi hizo,  wabunge watano au zaidi wanapaswa kuwa wanawake. Baada ya kuondolewa Posi, Rais alimteua Anne Kilango kuwa Mbunge.

Hivi karibuni, Rais alimteua Salma Kikwete kuwa mbunge na kufanya idadi ya wabunge wanawake wa kuteuliwa na Rais kuwa wanne, kubaki nafasi moja ya uteuzi ambayo ni lazima awe mwanamke.

Mwingine aliyeteuliwa na Rais kuwa mbunge ni Abdlallah Bulembo na kufanya idadi ya wabunge walioteuliwa na kiongozi mkuu huyo wa nchi bila kupewa uwaziri kuwa watatu.

Kwa mantiki hiyo, kama Rais Magufuli atazingatia utaratibu wake wa kuteua mbunge na kumpa wizara, safari hii atalazimika kuteua mbunge mwingine mwanamke.

Iwapo hatateua na kuamua kubadili utaratibu wake, huenda Salma na Kilango wakakumbukwa, huku kukiwa na kila dalili ya baadhi ya mawaziri kuhamishiwa Wizara ya Nishati na Madini.

Wanasiasa, wasomi

Katika maelezo yake, Mbowe alisema madini yanahusisha mafuta, gesi na vito hivyo vikichanganywa na nishati ni mzigo mkubwa.

Alibainisha kuwa wizara hiyo inakabiliwa na vishawishi vingi kutokana na fedha zinazopatikana kwa wawekezaji, jambo ambalo huwa ni mtego kwa mawaziri.

Huku akikosoa mikataba ambayo Serikali imeingia na wawekezaji wa sekta ya nishati na madini, Mbowe alisema ikifuatiliwa kwa undani hakuna atakayebaki salama.

“Yupo Waziri Mkuu mmoja aliondoka kwa kashfa ya wizara hii. Kusema nani atatosha ni ngumu sana kwa wizara hii,” alisisitiza Mbowe.

Mwenyekiti wa Chama Cha Kijamii (CCK), Constatine Akitanda aliitaja wizara hiyo na ya Maliasili na Utalii, kukiri kuwa ni ngumu kuziongoza.

Alidai kuwa mambo mengi yanayoikumba nchi kwa sasa ni matokeo ya nchi kuingia mikataba mibovu, hasa katika utawala wa Serikali ya Awamu ya Tatu.

“Tunachopaswa kufanya ni kuangalia mfumo na mikataba iliyoingiwa. Imetawaliwa na nguvu ya pesa, hakuna waziri atakayekuwa salama,” alisema Akitanda.

Kwa upande wake, kada wa Chadema na mbunge wa zamani wa Kigoma Kusini, David Kafulila alisema:”Madini na nishati ni rasilimali zinazoongozwa kwa rushwa duniani, ni ngumu kutulia.”

Kafulila alisema nchi kadhaa duniani zinapigana kwa sababu ya nishati na madini, jambo alilodai kuwa linaakisi nchini.

Rais wa zamani wa Chama kilichofutwa cha APPT-Maendeleo, Peter Mziray alisema, “Kama Mkapa angeona mbali haya mambo yasingetokea hivi sasa. Alishiriki ubinafsishaji ambao umenufaisha wageni.”

Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Dk Frank Tilly alisema kinachoikumba wizara hiyo ni matokeo ya nchi kukosa muundo madhubuti wa uongozi, kusababisha viongozi kufanya mambo wanavyojisikia.

Credit - Jambo Leo

Kafulila na Lissu Watoa Ushauri Kuhusu Sakata la Mchanga wa Madini..Watahdharisha Nchi Kuingia Katika Kesi Nzito ya Uvunjifu wa Mikataba ya Kimataifa..!!!

$
0
0

ALIYEKUWA Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila, amemtaka Rais John Magufuli kuchunguza baadhi ya watumishi wa Idara ya Usalama wa Taifa (TISS) na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kwa alichodai walijenga uhusiano na baadhi ya watendaji kufanikisha wizi wa madini.

Kafulila alisema hayo jana siku moja baada ya Rais Magufuli kupokea taarifa ya Kamati ya Kuchunguza Mchanga wenye Madini ya Dhahabu iliyokuwa chini ya Profesa Abdulkarim Mruma.

Kamati hiyo ilibainisha kuwa katika kontena 277 kuna tani 7.8 za dhahabu zenye thamani ya Sh bilioni 676.

“Namshauri Rais aboreshe TISS kwa kuwa na kitengo cha ujasusi wa kiuchumi kitakachomudu kukabiliana na uharamia wa utoroshaji utajiri wa Taifa,” alisema.

Alisema ipo haja ya kutazama upya Katiba ili ikibainika kuwa Rais yeyote aliyepita alihusika na ufisadi afikishwe kwenye mkondo wa sheria.

Kafulila alisema katika ofisi za viongozi wakuu - Ikulu ndipo vinapotoka vimemo kuruhusu uharamia wa namna hiyo.

“Ni ushauri wangu kwa Rais aruhusu mchakato wa Katiba ili pamoja na mambo mengine, tuangalie mfumo wa ofisi yake kama moja ya vyanzo vya   uozo na uharamia huu,” alisema.

Alisema kampuni hizo za kimataifa zinaiba duniani kote ikiwamo Ulaya na Marekani, isipokuwa huku kwetu zinaiba zaidi kutokana na sera duni, sheria dhaifu, mifumo ya usimamizi dhaifu na udhaifu wa wanaopewa nafasi kwa ujumla.

Aidha, alisema pamoja na changamoto hizo, bado hatua hiyo ya Rais Magufuli inapaswa kuungwa mkono na kila mzalendo huku akisisitiza kuwa ni moja ya malalamiko ya vyama vya upinzani.

 “Naipongeza Kamati kwa kazi iliyotukuka iliyojaa majaribu ya rushwa kubwa, kwani kampuni za madini, mafuta na gesi duniani zina sifa hiyo kama alivyopata kusisitiza Profesa Joseph Stirglitz gwiji wa uchumi na utandawazi duniani,” alisema.

Kafulila alimshauri Rais kuchukua hatua za kisheria za ndani, kwa kuzifikisha kampuni hizo kwenye mahakama za kimataifa kama inavyotamkwa kwenye mikataba ili kuzidai fidia kwa miaka yote ya mikataba yao.

Hali kadhalika alipendekeza mitambo na mali za wawekezaji zishikiliwe mpaka kesi zitapomalizika. “Na hili lisisomeke kwamba ni kukimbiza wawekezaji bali ni kukabili uharamia wa utoroshaji rasilimali ambao hata sheria za kimataifa zinapiga vita,” alisema.

Wakati Kafulila akisema hayo, Mbunge wa Singida Mashariki na Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu alisema hotuba ya Rais Magufuli ni ushahidi mwingine, kama bado kuna shaka, ya mamlaka ya kisheria kwa nchi ambayo anatuingiza kama Taifa.

“Natumia marufuku yake ya kusafirisha mchanga wenye madini nje ya nchi kama mfano,” alisema.

Alisema zaidi ya dhahabu, mgodi wa Bulyanhulu unazalisha pia madini ya fedha, cobalt, shaba na cadmium na ni mgodi pekee nchini wenye madini yote hayo.

Alisema madini hayo kwa mujibu wa Sheria ya Madini na Mikataba ya Uendelezaji Madini (MDAs) waliyopewa na Rais Benjamin Mkapa na kurudiwa na Jakaya Kikwete, ni mali ya wawekezaji.

Mgodi wa Bulyanhulu unachenjua dhahabu kwa asilimia 70 na asilimia 30 iliyobaki inafanyikia Japan ambayo ina mtambo wa hayo madini mengine.

“Ndiyo maana mchanga huo umekuwa unasafirishwa kwenda Japan tangu mwakan 2001. Sasa Rais angewaelekeza wawekezaji wajenge kwanza hicho kiwanda nchini, kabla ya kupiga marufuku usafirishaji mchanga,” alisema.

“Kwa kuzingatia kwamba wawekezaji hawa wanalindwa kisheria na kimkataba, Rais angejadiliana na MDAs ili kufanya mchakato wote ndani kwa ndani,” alisema.

Lissu alisema uamuzi wa Rais unaweza kusababisha agombane na wawekezaji na serikali zao na mabwana wakubwa wa kifedha duniani, ambao ndio wamiliki halisi wa rasilimali hizo.

Watampeleka kwenye mahakama za kimataifa ambazo Mkapa na Kikwete walizikubali kuwa ndizo za migogoro kati yetu na tuliowapa rasilimali zetu.

“Tukipelekwa huko hatuponi, kwa sababu tutakuwa tumevunja mikataba na sheria zinazolinda wawekezaji na hatapata anachokifikiria,” alisema.

Mwanasheria huyo alisema Rais wa Bolivia, Evo Morales alikuta nchi ikiwa na mikataba kama hiyo alipochaguliwa Desemba 2006, cha kwanza alichofanya ni kuiondoa nchi hiyo kwenye makubaliano ya MIGA na kwenye Mikataba ya Uwekezaji (BITs) zilizokuwa zinalazimisha Mahakama ya Kimataifa kwenye migogoro ya uwezekaji.

Kwa upande wake, Venant Rugabela alisema: “Ripoti ni ripoti, uhakika wake ni uhakika wake na utekelezaji ni utekelezaji.” Lakini hoja inarejea kuwa “ni kwa nini wahusika ambao ni wazalishaji hawakuunganishwa katika kamati?”

Mariam Chimile alisema kilichotokea katika taarifa, ni kuonesha dhahiri kuwa nchi imekuwa ikipoteza fedha nyingi ambazo zingepaswa kutoa huduma za kijamii.

“Tumeshuhudia hudumia za afya, miundombinu na nyingine nyingi ambazo zingekuwa nzuri kama madini hayo yamejulikana,” alisema.

Chimile alisema ni wakati mwafaka kwa Serikali kuangalia upya Sheria ya Madini ya Mwaka 2010 ili kuondoa mkanganyiko.

Ofisa Utawala wa NCCR-Mageuzi, Florian Mbeo alisema ripoti ni nzuri ila suala la msingi ni kutekeleza aliyoyaagiza bila kupepesa macho.

Mbeo alisema pamoja na ripoti hiyo kuwa nzuri, bado kuna changamoto hasa kwenye mikataba ambayo inaoneshwa kukosewa tangu awali na sheria kuwa na ukakasi.

“Tungefurahi kama mikataba ingejulikana kwa kila mwanajamii ili tuweze kutoa maoni, lakini mikataba ile ni siri. Hatujui kilichomo. Wanachukua rasilimali zetu kwa makubaliano ya siri,” alisema.

Alisema haya yote yanayoikuta Serikali lawama zinapaswa kuelekezwa kwao, wabunge na Baraza la Mawaziri.

Aidha, inasemekana taarifa hiyo ambayo alikabidhiwa jana kwa ilisababisha kushuka kwa hisa za kampuni ya uchimbaji madini ya Acacia kwenye Soko la Hisa la London, Uingereza.

Benki ya Dunia Yaunga Mkono Sera ya Elimu Bure kwa Kutoa Bilioni 181 ...!!!

$
0
0

BENKI ya Dunia (WB) imekubali kusaidia utekelezaji wa sera ya elimu bila malipo kwa Serikali ambapo imetoa dola milioni 80 sawa na Sh bilioni 181.

WB imefikia uamuzi huo baada ya kuona mwitikio mkubwa wa wanafunzi kujiunga na shule za msingi, hali inayoonesha kuanza kuilemea Serikali kutoa elimu hiyo kuanzia shule ya msingi hadi kidato cha nne.

Mkurugenzi Mkaazi wa WB kwa Tanzania, Somalia, Malawi na Burundi, Bella Bird alibainisha jana kwamba fedha hizo zimetolewa na taasisi ya International Development Association (IDA) inayokwenda na mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN).

“Lengo ni kusaidia Serikali kukabiliana na changamoto inazokutana nazo katika mpango huo wa kutoa elimu bila malipo,” alisema.

Alisema pia lengo la lingine la kutoa fedha hizo ni kusaidia kuhudumia ongezeko la watoto wanaoijunga na shule pamoja na elimu bora itakayosaidia Taifa baadaye.

“Mpango wa elimu bila malipo ni jambo la kusaidia Serikali kufikia malengo ya kuwapa watoto wa kitanzania elimu, hivyo sisi WB tumeamua kuongeza nguvu ili Serikali isikwame,” alisema.

Bird aliipongeza Serikali kuondoa vikwazo katika utoaji elimu, hivyo kusababisha makundi yote kupata elimu bila tatizo lolote.

Mkurugenzi huyo alisema ni dhahiri uamuzi huo utasababisha ubora wa elimu huku dhana ya utekelezaji lengo la elimu kwa wote ikikamilika, kwa kuwa hakuna atakayeachwa nyuma.

“Tunaamini kuwa kupitia msaada huu, ni matumaini yetu kuwa Mamlaka itahakikisha kuwa watoto wanapata elimu hasa ambao wanaishi katika mazingira magumu,” alisema.

Alisema mpango huu ulianza mwaka 2014 ambapo WB ilipitisha dola milioni 122 ili kuhakikisha kuna elimu bora kwa shule za msingi na sekondari.

Msaada huo wa WB ni mwendelezo wa benki hiyo kutoa misaada kwa nchi ambapo hivi karibuni Rais wake, Dk Jim Yong Kim alizuru nchini na kuweka jiwe la msingi la daraja la juu Ubungo, Dar es Salaam ambao utagharimu zaidi ya Sh bilioni 188.71 msaada kutoka benki hiyo.

Aidha, WB hadi sasa inafadhili miradi zaidi ya 28 nchini ukiwamo ujenzi wa barabara ya mwendo kasi kwa gharama ya zaidi ya dola bilioni 4.2 ambapo Tanzania itarudisha kwa riba ndogo ya asilimia 0.5.

Sakata la Mchanga wa Madini..Chenge Amchana Live Rais Magufuli..Habari Vichwa vya Magazeti ya Leo Jumamosi 27/5/2017..!!!

Viewing all 104803 articles
Browse latest View live


Latest Images