Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104793 articles
Browse latest View live

Waandaa Siku Maalumu ya Kumuombea Dua Rais Magufuli..!!!

$
0
0

UMOJA wa madhehebu ya Kikristo mkoani Dodoma umesema utaandaa siku maalum ya kumpongeza na kumuombea Rais John Magufuli kutokana na kazi anazofanya zinazoleta tumaini jipya kwa wananchi wa kawaida.

Mwenyekiti wa umoja huo, Dk Damas Mukasa alisema hayo juzi kwenye makao makuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambapo wanachama, wazee wa mkoa wa Dodoma na viongozi wa chama ngazi ya mkoa na wilaya ya Dodoma Mjini walipojitokeza kumpongeza Rais Magufuli kutokana uamuzi mgumu anaochukua wa kulinda rasilimali za nchi.

Dk Mukasa alisema kazi anazofanya Rais Magufuli zinaleta msisimko kwa wananchi wa kawaida hasa kwa kubaini ufisadi mkubwa kwenye raslimali za nchi. “Anaondoa mafisadi anahakikisha rasilimali za nchi hazinufaishi watu wachache, ameondoa watu wasiostahili serikalini, tumeona kwa macho yetu na kushuhudia alivyoiondoa Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu (CDA),” alisema.

Alisema hata mwanzoni mwa wiki hii, Rais Magufuli alipotoa ripoti kuhusu ufisadi mkubwa unaofanyika kwenye madini wananchi wameshangilia. “Wakristo wa Dodoma wamefurahishwa sana na uamuzi huo tutaandaa ibada maalumu ya kumpongeza Rais Magufuli kwa uamuzi mgumu anaochukua wa kulinda maslahi ya nchi kwa manufaa ya taifa,” alisema.

Kwa upande wake kada wa CCM, Emmanuel Kamara alisema ripoti ya pili kuhusu madini rais Magufuli ameipokea kwa weledi na upeo mkubwa. “Rais alichogundua waliotuangusha ni ni watanzania wenzetu tena ni wasomi ni viongozi wetu na tena na cha kusikitisha zaidi walifanya kama makusudi katika kutekeleza jambo hilo,” alisema.

Naye Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa CCM, mkoa wa Dodoma Balozi Job Lusinde alisema sasa ni wakati wa kuunga mkono juhudi za Rais ili nchi ikae kwenye mstari. Katibu wa baraza la wazee mkoa wa Dodoma, Mohamed Makbel alisema watanzania wana kila sababu ya kumshukuru Mungu kutokana na madudu yanayoibuliwa ambayo yalifanya taifa lipate hasara kubwa kutokana na tamaa za watu wachache.

Lowassa Aeleza Anachoamini ni Mwarobaini wa Wizi Kwenye Madini..!!!

$
0
0

Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa ameeleza kile anachoamini kuwa ndio tiba halisi ya matatizo ya wizi katika sekta ya madini nchini. Amesema hayo siku chache baada ya Rais Magufuli kupokea ripoti ya pili ya mchanga wenye madini, uliokuwa ukisafirishwa kwenda nje ya nchi na kampuni ya Acacia.

Akizungumza na waandishi wa habari, Lowassa ambaye ni mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, alisema kuwa ili matatizo ya unyonyaji kwenye sekta hiyo yakabiliwe kikamilifu, Tanzania inapaswa kuandika katiba mpya.

Alisema kuwa mapungufu katika mikataba na sheria ya madini yamekuwa yakilalamikiwa na wapinzani kwa miaka mingi ndani ya Bunge lakini maoni yao hayakukubalika.

“Wapinzani wameshasema sana, wakasema mikataba hii iletwe tuitazame upya kwenye Bunge, lakini walikataliwa,” alisema akiwataja baadhi ya makada wa vyama vya upinzani kama Tundu Lissu, John Mnyika na Zitto Kabwe waliowahi kuwasilisha ombi hilo.

“Walikataliwa kwa sababu siri yake, jambo hili haliko kwenye katiba. Ndio maana mimi nasema tiba yangu moja kubwa ni kuhakikisha tunapata katiba mpya. Katiba ambayo itazitangatia maslahi ya wananchi katika kugawanya rasilimali zake,” aliongeza.

Exclusivee...Alichokisema Irine Uwoya Baada ya Dogo Janja Kumtaka Awe Mpenzi Wake..!!!

$
0
0

Wiki kadhaa baada ya Dogo Janja aka Janjaro kuweka wazi kwenye vyombo vya habari kuwa muigizaji Irine Uwoya ndiye anayemkosesha usingizi na angependa siku moja awe barafu wa moyo wake, Uwoya amemfungukia.

Janjaro aliwahi kusema kuwa, “Irene Uwoya nampenda tangu nikiwa mtoto, nimeshabandika sana picha yake maghetoni. Nampendaga sana na ni mtu ambaye nammezeaga mate.”

Muigizaji huyo ambaye amekuwa akitajwa mara kwa mara kwenye nyimbo za wasanii wa Bongo Flava akihusishwa na mfano wa uzuri na mvuto, amekejeli ombi la Janjaro ambaye amedai ni mdogo wake mwenye matatizo yake binafsi.

“Yaani kale jamani… ni mdogo wangu, naongeaga naye tunapiga story. Kananifurahisha lakini, hivyo tu,” Uwoya alisema

Hata hivyo, Uwoya aliweka wazi kuwa katika kumchagua mwandani yake, umri sio kigezo cha kumpima mwanaume anayetaka kuwa naye.

Mtoto Afariki Ndani ya Gari Baada ya Mama Yake Kwenda Kula Raha na Mpenzi Wake..!!!

$
0
0

MTOTO wa miaka nane alifariki jana Jumapili huko Bumula, katika Kaunti ya Bungoma nchini Kenya, wakati mama yake alipomwacha katika gari lililofungwa.

Mwanamke huyo na mpenzi wake wanasemekana walikwenda katika chumba cha nyumba ya wageni karibu na soko la Mateka na kumwacha mwanawe ndani ya gari likiwa limezimwa na kufungwa kabisa madirisha.

Mkuu wa Polisi wa Mateka Julius Barasa alisema mwanamke huyo alitambuliwa kama Christine Nasimivu.

“Walimwachia chupa tatu za soda lakini mtoto alifariki kutokana na kukosa hewa safi,” alisema afisa huyo wa polisi.

Polisi waliwaokoa wawili hao kutoka kwa wananchi wenye hasira ambao walikuwa wanataka kuwanyonga.

Wawili hao walikamatwa na kufikishwa katika kituo cha polisi cha Bumula wakati mwili wa mtoto ulipelekwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha hospitali ya rufaa ya Bungoma.

Joseph Lupao, afisa mwangalizi wa watoto, aliwashutumu wawili hao kwa kumwacha mtoto peke yake ndani ya gari.

“Hii ni ajabu na jambo bay asana – mtoto amefariki kutokana na uzembe. Wanapaswa kushitakiwa mahakamani,” alisema.

Kulingana na tovuti ya Kidsandcars.com, watoto ambao huachwa ndani ya magari hufariki kutokana na joto la gari.

Tovuti hiyo inaeleza kwamba ndani ya gari joto huongezeka kwa haraka linapokuwa limefungwa, na linaweza kufika hata nyuzi joto 125 ndani ya dakika chache.

Joto hilo linasababisha joto la mwili wa mtoto kupanda na kufika zaidi ya nyuzi joto 40, na kusababisha kifo. Tovuti hiyo inasema kwamba mwili wa mtoto hupata joto kwa haraka mara tatu hadi tano zaidi ya ule wa mtu mzima.

Dkt Bana - JPM Amewafungua Macho Viongozi Wengi wa Afrika na Dunia ..!!!

$
0
0

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dkt. Benson Bana amesema kuwa kitendo kilichofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kimewafungua macho viongozi wengi wa Afrika na dunia na kitakuwa ni mfano wa kuigwa kwa Serikali nyingi za Afrika na dunia kwa ujumla.

Dkt. Benson Bana amesema hayo wakati akiongea na Idara ya Habari (Maelezo), ambapo ameeleza kuwa kitendo cha kutafuta ukweli katika makinikia na biashara ya madini na kuweka wazi taarifa hiyo kwa umma na kusema wahusika wa sakata hilo wachukuliwe hatua za kisheria kimeonyesha uzalendo wa dhati kwa nchi yake.

“Ningefurahi kama tungetenga siku maalumu kuandamana kwa nia ya kuunga mkono nia njema ya Rais ya kuhakikisha kuwa rasilimali za nchi hii hazitumiwi hovyo hovyo” amesema Dk Bana.

Pia, Dkt. Benson Bana ameunga mkono kitendo cha Rais kukubali kufanyia kazi mapendekezo yote 21 yaliyotolewa na Tume ya Uchunguzi, kwani yataweka wazi mwenendo mzima wa biashara ya madini na kuziba mianya ya wizi wa madini.

Aidha, Amempongeza Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba kwa kuchukua uamuzi wa haraka wa kuwazuia kusafiri nje ya nchi watuhumiwa wa sakata hilo.

Dkt. Benson Bana ameongeza kuwa wale wote waliotajwa kuhusika na suala hilo kukaa nje ya utumishi wa umma kwa muda wakati uchunguzi dhidi yao ukiendelea na endapo watabainika kuwa hawana hatia warudishwe kazini na ikibainika kuwa walihusika wachukuliwe hatua stahiki, huku akitoa wito kwa Watanzania kuuunga mkono  nia njema ya Rais Magufuli kwa sababu hatua hiyo ni harakati za kuweka sawa uchumi wa nchi ili kuboresha maisha ya Watanzania.

Kufuatia uamuzi huo wa Rais Magufuli kuhusu Makinikia, baadhi ya wasomi wameonyesha kuridhishwa na kuunga mkono hatua ya Rais kuagiza wahusika wote wachukuliwe hatua za kisheria baada ya kupokea ripoti ya pili ya Kamati ya Wachumi na Wanasheria aliyoiunda kwa ajili ya kuchunguza Mchanga wa Madini unaosafirishwa kwenda nje ya nchi.

MAGAZETI YA LEO 15/6/2017

Sakata la Mchanga wa Madini..Siri Mpya Yafichuka Ikulu..Habari Vichwa vya Magazeti ya Leo 15/6/2017..!!!

Wanafunzi Shule za Msingi Wagoma, Wafunga Barabara ya Jiji Kushinikiza Wajengewe Matuta ya Marabara..!!!

$
0
0

Mamia ya wanafunzi wa shule ya msingi ya St. Anne wameandamana na kufunga barabara ya Jogoo jijini Nairobi nchini Kenya, baada ya basi la abiria maarufu kama ‘Matatu’kumgonga na mtu aliyekuwa akiwasaidia kuvuka barabara.

Kwa mujibu wa Daily Nation, wanafunzi hao wamefunga barabara kuu katika mji mkuu wa nchi hiyo ikiwa pia ni siku chache baada ya kuripotiwa kuwa gari moja lilimgonga na kumuua mwanafunzi mwenzao na kisha kutokomea.

Imeelezwa kuwa wanafunzi hao wameweka mgomo kwa kulala na kukaa barabarani huku wakiweka mawe katika maeneo mengine ya barabara hiyo, wakidai kuwekwa matuta barabarani hapo. 

“Tunataka haki itendeke kwa mwenzetu, hakuna matuta hakuna kusoma,” wanasikika wanafunzi hao.

Mashuhuda wa tukio la ajali wameeleza kuwa gari hilo lilikuwa likijaribu kulipita kwa kasi gari lingine kabla ya kumgonga mtu huyo aliyekuwa anajitolea kuwavusha wanafunzi.

Vyombo vya usalama vimeingilia tukio hilo na kuahidi kufanyia kazi maombi ya wanafunzi hao, baada ya magari mengi kulazimika kurudi yalipotoka kwa muda mrefu.

Tundu Lissu Kuwaponza Lowassa na Sumaye Sakata la Madini

$
0
0
Tundu Lissu Bungeni
Siku moja baada ya Rais Dkt John Pombe Magufuli kukabidhiwa ripoti ya pili ya uchunguzi wa makinikia yaliyozuiwa kwenye makontena bandarini na kuagiza viongozi wote walioshiriki katika kulisababishia taifa hasara kupitia sekta ya madini wahojiwe, Wabunge wa upinzani wameibuka na kutaka kinga za marais wastaafu ziondolewe.

Wabunge hao wametaka kinga za Rais wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa na Rais wa awamu ya nne, Dkt. Jakaya Kikwete ziondolewe kupitia marekebisho ya katiba ili nao waweze kushtakiwa kwa kulisababishia taifa hasara ya matrilioni ya fedha kupitia mikataba mibovu ya madini.

Akizungumza jana Bunge, Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu alisema kuwa kama serikali imeamua kuwashughulikia wote waliohusika katika sakata la madini, isifanye kwa kubagua badala yake hata marais wastaafu washtakiwe kwani nao ni sehemu ya walioshiriki katika kusainiwa mikataba hiyo.

Wakati wakiyasema hayo, Spika wa Bunge, Job Ndugai (Mb) aliwatahadharisha upinzani kwa kutaka Marais hao washtakiwe kwamba na wao wajue wana Mawaziri Wakuu wawili wastaafu ambao mmoja alihudumu katika serikali ya tatu, na mwengine serikali ya nne.

Mawaziri Wakuu wastaafu walipo katika kambi ya upinzani ni Frederick Sumaye aliyekaa madarakani tangu 1995-2005 chini ya Rais Mzee Mkapa na Edward Lowassa aliyekaa madarakani tangu 2005-2008 alipojiuzulu akiwa chini ya Rais Dkt Kikwete.

Hii ina maana kuwa, kama marekebisho yatafanyika kama ambavyo upinzani wanataka ili kinga ya marais hao iondolewe, ni dhahiri kuwa Lowassa na Sumaye nao watashtakiwa kwani wakati huo ndio walikuwa wasimamizi wakuu wa shughuli za serikali.

Swali lililobaki kwa watu wengi ni kama upinzani watakuwa tayari kuwatoa kafari wanachama wake hao wawili wakubwa ili wakajibu tuhuma zinazowakabili mahakamani za kusimamia mikataba mibovu wakiwa madaraka. Au, Je! CHADEMA wakijua kuwa mabadiliko ya katiba yatawaathiri pia wanachama wao, Sumaye na Lowassa wataendelea kusisitiza yafanyike?

Jana akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Edward Lowassa alisema alipoingia madarakani alikuta kweli mikataba ya madini ni mibovu na alijitahadi kwa kiasi fulani kuirekebisha. Lakini Waziri Mkuu aliyekuwepo kabla yake ni Sumaye, hivyo kwa namna nyingine anasema kuwa Sumaye alisimamia nchi kusaini mikataba mibovu.

Kwa mujibu wa kamati iliyowasilisha ripoti ya uchunguzi mbele ya Rais juzi, ilipendekeza waliokuwa Mawaziri wa Wizara ya Nushati na Madini, Makatibu Wakuu, Wanashaeria Wakuu wa Serikali, Maafisa wa TRA na watumishi wote pamoja na makampuni yaliyoshiriki kuingia mikataba ya madini tangu mwana 1998 wahojiwe, pendekezo ambalo Rais alilikubali.

Chenge Kuvuliwa Uenyekiti wa Bunge? Spika Ndungai Aeleza Utaratibu wa Kumvua

$
0
0
Andrew Chenge
Katika ripoti ya pili ya Kamati ya kutathmini mchanga wa madini Mbunge wa Bariadi, Andrew Chenge ametajwa na Mwenyekiti wa kamati hiyo kuwa alikuwa na mchango mkubwa wa kulisababishia Taifa hasara kubwa kutokana na kuandaa au kusaini mkataba mbovu wa madini unaoyaruhusu makampuni ya uchimbani kusafirisha mchanga huo kwenda nje ya nchi pamoja na kukubali viwango vidogo vya mrabaha kwa Taifa katika sekta ya madini.

Miongoni mwa mapendekezo yaliyotolewa kwa Rais na Mwenyekiti wa kamati hiyo ni pamoja na kuwashughulikia viongozi na watendaji wote wa Serikali walioshiriki kusababisha hasara hii kwa zaidi ya miaka 19.

Rais Dkt. Magufuli akiongelea pendekezo hili aliagiza vyombo vinavyohusika viwaite watu wote waliotajwa ili wahojiwe.

Baada ya kauli hiyo ya Rais, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amesema kuwa Chenge ataendelea kuwa Mwenyekiti wa Bunge mpaka atakapoitwa na kuhojiwa kuhusu mchanga wa madini (makinikia). Spika Ndugai alisema hakuna kanuni inayomzuia Chenge kuendelea kuwa Mwenyekiti wa Bunge kwa sasa.


Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai
“Kwa sasa hapana. Ataachia nafasi hiyo atakapoitwa kuhojiwa; akishathibitika ndio atatoka kwenye nafasi ya Uenyekiti,” alisema.

Utaratibu unaeleza kwamba Ofisi ya Spika ikishapata taarifa ya Mbunge au kiongozi fulani wa Bunge kuhitajiwa na chombo cha dola na Spika akatoa ruhusa hiyo, Mbunge huyo ataachia madaraka yake na kubaki na ubunge tu.

Mwenyekiti wa kamati ya pili ya kuchunguza hasara iliyoletwa na kusafirisha mchanga wa madini, Profesa Nehemiah Osoro alisema kuwa wakati Taifa linapitisha Sheria na mikataba ya hovyo, Mwanasheria Mkuu wa Serikali alikuwa ni Andrew Chenge.

Watanzania, Tuweke Siasa Pembeni Tumuunge Mkono Raisi Wetu

$
0
0
Rais Magufuli
Wananchi,
Salaam za upendo ziwafikie popote mlipo. Aidha baada ya salaam, nawasilisha mada tajwa hapo juu.
Sintoandika sana kwani, mengi sana yameshaandikwa kwenye nyuzi nyingi sana kuhusiana na suala zima la rasilimali zetu sanasana makinikia(maboso?! ).

Sasa watanzania wenzangu, tunakubaliana kwamba kitendo alichokifanya rais wetu ni kwa ajili ya manufaa yetu. Tumuunge mkono rais kwa vitendo, tuweke siasa na vyama pembeni. Wote kwa pamoja tupaze sauti kupitia maandamano nchi nzima hao mabepari watulipe chetu. Tuache unaa na ujuaji mwingi wa kuandika tuu mitaondi..

Raisi anahitaji msaada wetu kwani hii vita sio rahisi jamani. Pia tumtie moyo huyu kwa hili jema na kubwa alilofanya. Kwa kufanya hivo, tutawapa ujasiri mkuu hata viongozi wanaokuja wa kufanya maamuzi magumu kijasiri zaidi.

Namalizia kwa kusema, hatua aliyofikia raisi wetu pamoja na kamati zote na serikali kwa ujumla ni kubwa ila sio kamilifu kama watanzania tumekaa kimya. Nawahimiza tupige kelele tulipwe na dunia ijue kwamba tupo bega bega na raisi kwa maslahi yetu. Nna hakika mataifa mengine wanatushangaa sana wallahi!

Natoa wito kwa wabunge, madiwani na serikali za mikoa yote tanzania ku-organize maandamano nchi nzima ili ku-support hii move.

Utaifa mbele!
Good morning TZ...

JISAJILI USHINDE GARI LA BUREEEEE KABISA

$
0
0
Umeshawahi Kufikiria Kupata Gari la Bure bila Kulipa Chochote... Basi hii Kampuni ya Cars From Japan Wanakupa Nafasi Hiyo ...

CHAKUFANYA NI Fuata Maelekezo hapa chini Jinsi ya Kuweza Kuwa Mshindi wa Gari hilo..

Bonyeza Hapa >>> SHINDA GARI YA BURE <<< Kujisajili ni Bure tu...

Kisha Jisajili kwa Kuweka Jina na Email Yako

VIDEO: Wema Sepetu na Gabo Walivyozindua Filamu Yao Mpya – KISOGO

$
0
0
Wasanii wa filamu, Gabo Zigamba na Wema Sepetu, wamezindua filamu mpya ya kisasa iitwayo Kisogo, itakayoweza kuonekana na mtu yeyote mwenye simu ya mkononi ya kisasa (smartphone) kupitia application iitwayo Uhondo.

Wakizungumza kwenye uzinduzi wa filamu hiyo ndani ya Ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo jijini Dar es Salaam, waandaaji wa filamu hiyo, Kampuni ya Sarafu Media inayomilikiwa na Gabo Zigamba, wamesema filamu hiyo ipo tofauti na filamu nyingi zilizozoeleka Bongo na hata namna ya kupatikana kwake kwa urahisi.

Kwa mujibu wa waandaaji hao, mtumiaji wa simu akishadownload  app ya Uhondo, anaiona kwenye orodha ya filamu zilizopo ambapo itakuwa na dakika thelathini. Kwa kuanzia, Sarafu Media wamesema kuwa dakika kumi na tano za kwanza zitatolewa bure ili kila mtu ajionee ambapo sehemu ya pili yenye dakika kumi na tano pia, itauzwa kwa shilingi mia tano tu.

Alipopata nafasi ya kuzungumza, Gabo alisema haikuwa kazi nyepesi kukamilisha filamu hiyo, hasa katika kipindi hiki chenye changamoto kubwa kwamba Bongo Movie hazina ubora.

Kutana na Mtabibu Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH Maalim HUSSEIN Mtabibu wa Nyota za Binadamu na Dawa za Asili ya Africa...Anatibu Magonjwa Yafuatayo

$
0
0
Kutana  na Mtabibu Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH Maalim HUSSEIN Mtabibu wa Nyota za Binadamu na Dawa za Asili ya Africa Mwenye UWEZO Kubaini tatizo lako Pindi tu Utakapo Fanya Mawasilino Kupitia Wasaa Husika

Anatibu kwa Njia ya Simu Ukiwa Nchi Yoyote / Mkoa wowote
..JE UNASUMBULIWA NA Mapenzi? (Umeachwa na Umpendae,Awe Mume,Mke na Bado unampenda?Na  Umejaribu Sehemu nyingi Bila Mafanikio?Wasilina na Maalim Hussein Ujione muujiza wa Papo kwa Papo.. anauwezo WA KURUDISHA MAHUSIANO NA KUIMARISHA NDOA YAKO NDANI YA SAA 12 TU(LIMBWATA). Umekimbiwa na Mumeo,mkeo au Mpenzi na anaishi na mtu mwingine?Una Mpenzi wako ana Pesa na Unataka kumkamata? Muone akutatulie Anauwezo wa Hali ya Juu wa Kusambalatisha Mahusiano yao Endapo utafata Atakacho kuelekeza.
Atamfanya Atimize Ahadi zote kwa Muda Mfupi.
Maalim Hussein Anatumia Jina la Muhusika au Picha Kumaliza Tatizo lako..
Anatibu kwa Kutumia  Vitabu vya QUR-AN Dawa za Asili za Africa,Dawa za Kiarabu na Majini.Anatafsiri Ndoto. Kushinda BAHATI NASIBU, KUSAFISHA NYOTA,Hutoa  PETE ZA BAHATI inayoendana na NYOTA YAKO. Mvuto wa Mwili na BIASHARA, Kinga ya Mwili,ZINDIKO za Nyumba.HUZUIA CHUMA ULETE NA KUKUPA DAWA YA KUONGEZA FAIDA KWENYE BIASHARA. HURUDISHA MALI ZILIZOPOTEA AU KUDHULUMIWA.MIGUU Kufa GANZI.Kufungua KIZAZI kwa wale walio fungwa kwa njia za KISHIRIKINA. Anakupa Jini la Mali kwa yule anaehitaji Utajiri BILA MASHARTI.
Humaliza Kabisa Tatizo la Nguvu za KIUME na Kurefusha Uume kwa Saizi Unayotaka,

HUMALIZA KESI YA AINA YOYOTE NDANI YA SIKU 14. na mengi zaidi

Whatsapp: +255 674 835107 
Calls: +255746757102

Tiba ni kwa Watu wenye Imani na Dini zote..

JPM Avionya Vyombo vya Habari Vinavyowataja Kikwete, Mkapa Sakata la Makinikia

$
0
0

Magufuli
 
Rais John Magufuli amevionya vyombo vya habari vinavyowataja marais wastaafu, Benjamin Mkapa na Jakaya Kikwete wakiwahusisha na sakata la mchanga wa madini.

 Rais Magufuli ameyasema hayo leo (Jumatano) Ikulu baada ya kukutana na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Barrick ya nchini Canada, Profesa John Thornton.

Barrick Gold Corporation ni kampuni mama ya kampuni ya uchimbaji wa madini ya Acacia.

“Nimesoma ripoti zote mbili hakuna mahali ambapo Mzee Mkapa na Mzee Kikwete wametajwa, vyombo vya habari viache kuwachafua hawa wazee, wamefanya kazi kubwa ya kulitumikia Taifa letu, viwaache wapumzike,” amesema  Rais.

Ameonya viongozi hao kuhusishwa katika taarifa za kamati mbili za uchunguzi wa madini yaliyo katika makontena yenye mchanga wa madini (makinikia).


Je Wajua Kuwa Mazoea ni Sumu ya Penzi-Soma Hapa Ujue

$
0
0
mAPENZI
Unaweza usijue mtu uliyenaye anakupenda kiasi gani kwa sababu ya mazoea,unachukulia Mapenzi yake,I love you zake,Chakula anachokupikia,Kukufulia nguo,na Zawadi anazokupa,kama mazoea...Ukawa busy kutompa haki yake na penzi analostahili kwa Penzi lake juu yako,ukawa bize na Kokoto zingine na kuiacha dhahabu yako nyumbani imejaa vumbi...Dhahabu hata ijae vumbi vipi haiwezi kuwa na thamani sawa na Kokoto ya Tegeta!Siku atakayoondoka utajikuta una lori zima la kokoto lakini halina thamani,utakuwa umepoteza Dhahabu ya thamani kwa sababu tu hukuijali ilivyopaswa na wengine waliotambua thamani yake waliijali on ur behalf!
Mapenzi hayana Mazoea,hata muwe na miaka H kwenye Mapenzi msiishi kama wazee,hakikisha Mapenzi yenu yananukia upya kama mmeanza jana,kila anayewaona awatamani...Mazoea yataua penzi lenu,Once ukiingiza Mazoea utaona dhabau ni kama bati wakati majirani wanaona jinsi inavyong'aa na wanaitamani...Respect your Lover,Value even the small things he/she does to you,hata akileta boxer ya 800 ya Karume mwambie asante maana atleast ulicross kwenye mind yake akanunua...Mazoea ni adui wa Mapenzi,Kill it!

By Seth De Jesus Giovanni

Sakata la Deni la Zanzibar kwa Tanesco Lachukua Sura Mpya..Zanzibar Waja na Madai Haya Mengine..!!!

$
0
0

Serikali ya Zanzibar imesema ni matarajio yake kuwa ifikapo Juni 2018, deni lote la Sh65.6 bilioni wanalodaiwa na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), litakuwa limekamilika kulipwa.

Waziri wa Fedha na Mipango wa Zanzibar, Dk Khalid Salum Mohamed alisema hayo juzi katika kikao cha Baraza la Wawakilishi alipowasilisha Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2017/18.

Alisema katika hatua za awali, Serikali italipatia Shirika la Umeme Zanzibar (Zeco) Sh1 bilioni kila mwezi ili nao waongeze Sh2 bilioni na kuzipeleka Tanesco hivyo kufanya malipo kwa mwezi kuwa Sh3 bilioni.

Juhudi hizo alisema zinaweza kufanikiwa kwa mujibu wa utaratibu waliojiwekea wa kulipa deni hilo ambalo ni lazima lilipwe.

Alisema katika mwaka wa fedha wa 2017/18 wanatarajia pia kutumia Sh57.2 bilioni katika uanzishaji wa miradi ya jamii na ya kitaifa.

Alisema kati ya fedha hizo, Sh1.58 bilioni zitatumika kuvuta umeme katika kisiwa cha Kokota baada ya kukamilika kwa kazi kama hiyo katika kisiwa cha Fundo kilichopo Pemba.

Katika hatua nyingine, Dk Khalid alisema Serikali imedhamiria kufuta ada ya biashara katika uingizaji wa malighafi na pembejeo za viwandani ili kuvutia uwekezaji na kuongeza uwezo wa ushindani.

Alisema hatua hiyo inatarajiwa kuendeleza sekta ya viwanda na kuwavutia wawekezaji walio nje.

Waziri alisema Serikali inapendekeza kutoza kodi kwenye ada au kamisheni inayotozwa na benki katika huduma zake za fedha.

Dk Khalid alisema hilo linatokana na kubaini benki zimekuwa zikitoza kodi kwa huduma za benki zinazotolewa Zanzibar bila Serikali kufaidika. Alisema ili kuzuia ukwepaji huo wa kodi kwenye mishahara unaotokana na malipo ya fedha taslim, malipo ya mishahara ya wafanyakazi wa kudumu wakiwamo wa sekta binafsi, italipiwa benki. Alisema Serikali inatarajia kukusanya Sh600 milioni kutokana na kodi hiyo.

Inasikitisha ...Binti Aelezea A- Z Jinsi Dereva na kondakta Wake Walivyombaka kwa Zamu Ndani ya Basi Lao..!!!

$
0
0

Dereva na kondakta wa daladala zinazofanya safari ndani ya Manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro, Soweto–Mbuyuni wanatuhumiwa kumbaka abiria wao kwa zamu na kumuumiza sehemu za siri.

Tukio hilo lililotokea Juni 12 saa moja jioni maeneo ya Veta katika uchochoro uliopo karibu na shule ya Northen Highland iliyo umbali wa mita 400 kutoka barabara ya lami.

Akielezea tukio hilo, binti huyo mwenye umri wa miaka 20 alisema alitumwa na bosi wake kwenda kununua mahitaji ya nyumbani Soko la Mbuyuni na kumuelekeza kuwa akimaliza apande basi la Soweto sokoni hapo na ashukie mwisho ambako angechukua bodaboda ya kumfikisha nyumbani.

“Nilipomuuliza konda akaniambia ndiyo na nikampigia bodaboda ambaye nilipewa namba na bosi wangu ili ampe maelekezo huyo kondakta sehemu ambayo watanishusha ili yeye anichukue hapo na wakazungumza na baadaye akanirejeshea simu yangu,” alisema msichana huyo.

Alisema baada ya hapo safari ya kutoka Mbuyuni kwenda Soweto ilianza.

“Kwa kuwa nilikuwa mgeni, sikuelewa hata kituo kipi cha kushukia. Niliendelea kukaa hadi nilipoona watu wote wameisha kwenye (Toyota) Hiace, ndipo nikamuuliza konda kwa nini hanishushi akasema bado sijafika,” alisema.

Anasema alishangaa kuona dereva anaenda kuegesha gari uchochoroni na aliposimama, kondakta akashuka, akidai anaenda kujisaidia. “Aliporudi kwanye gari alifunga mlango na wakazima taa na kuanza kuniambia kuwa wamenipenda kama ninataka kuwa hai nikubaliane na wanachokitaka na nikikataa wataniua,” alisema binti huyo.

Alisema baadaye dereva alitoka kwenye usukani na kumfuata alipokaa na kuanza kumpapasa.

Alisema alipoona hivyo alijaribu kutoka nje kupitia dirishani, lakini walimvuta ndani huku wakimfunga mdomo asipige kelele na kumtishia kumuua.

“Nilikubali yaishe na nikatulia. Akaanza dereva huku kondakta akinishika mikono na baada ya kumaliza alichofanya, konda naye akaja akafanya hivyohivyo. Nilisikia maumivu, lakini nilishindwa kupiga kelele kwa kuwa walinitisha kuwa wangeniua,” alisema dada huyo.

“Walipomaliza kufanya ukatili huo, konda alimwambia dereva kuwa waniue kwa kuwa nimeshawatambua, lakini dereva akasema hakuna haja.”

Alisema katika mabishano hayo alijikaza na kuwaambia kuwa yeye ni mgeni na hajui popote kwa hiyo hatamwambia mtu kwa kuwa hilo ni tukio la aibu.

“Walikubaliana na mimi na wakaniambia kuwa ni kweli kubakwa ni kitendo cha aibu kwa hiyo nikimwambia mtu nitatengwa na jamii. Nikawaomba wanisaidie sehemu ya kupata msaada niweze kufika nyumbani,” alisema.

Alisema baadaye aliwaomba aende kuchukua kiatu chake kilichokuwa kimedondoka dirishani wakati akitaka kuruka, na walipomruhusu akatumia nafasi hiyo kusoma namba za gari.

Mlezi wake, Abdi Massawe alisema baada ya kufika nyumbani akiwa na bodaboda, binti huyo alimweleza tukio hilo na akatoa taarifa polisi ambako alipewa fomu ya matibabu aliyoitumia Hospitali ya Mawenzi, ambako vipimo vilithibitisha kuwa alibakwa.

“Huyu binti ni mgeni kutoka mkoani Singida. Hapa Moshi ana mwezi mmoja tu,” alisema Masssawe.

Massawe alisema baada ya hapo alianza kusaka daladala hilo kwa kutumia namba alizopewa na binti huyo na kufanikiwa kuikuta maeneo ya Soweto. Baadaye aliwapigia simu polisi ambao walifika na kushusha abiria waliokuwamo na kuipeleka kituoni.

Alisema wakati dereva akiendelea na mahojiano kondakta alitoroka.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Koka Moita alisema derava wa gari hilo aliyemtaja kuwa ni Salimu Abdalla (30) anashikiliwa na polisi ambao wanaendelea kumtafuta kondakta ambaye alitoroka akiwa katika kituo cha polisi.

Kwa sasa binti huyo anatibiwa Hospitali ya Mawenzi.

CCM na Ukawa Wabishana Bungeni Kuhusu Nani Aliyekuwa Wakwanza Kulifichua Sakata la Wizi wa Madini Nchini..!!!

$
0
0

Wakati Bunge likipitisha azimio la kumpongeza Rais John Magufuli kuhusu hatua alizochukua kwenye sakata la mchanga wa madini, wabunge wanaounda Umoja wa Katiba Tanzania (Ukawa), wamesema hakuna jipya na kwamba kinachotokea sasa kilishafanywa na viongozi wengine.

Jana, Bunge lilipitisha maazimio matatu ambayo ni kumpongeza na kuunga mkono hatua zilizochukuliwa na Rais Magufuli kukabiliana na udanganyifu unaofanywa kwenye sekta ya madini na kumhakikishia ushirikiano wakati wowote atakapohitaji.

Pia, Bunge limeishauri Serikali kuwachukulia hatua kali za kisheria wote watakaobainika kushiriki kulitia Taifa hasara kutokana na kuidhinisha mikataba mibovu na wizi uliofanywa.

Maazimio hayo yalitolewa jana baada ya kipindi cha maswali na majibu ikiwa ni siku moja tangu, Mbunge wa Vwawa (CCM), Japhet Hasunga kulitaka Bunge kuunga mkono juhudi za Rais na kufanikisha kuipitisha hoja hiyo iliyoundiwa kamati na Spika Job Ndugai.

Mbunge wa Newala (CCM), George Mkuchika ndiye aliyewasilisha maazimio hayo ambayo yaliwagawa wabunge waliochangia hoja hiyo kabla haijapitishwa.

“Bunge linamuunga mkono Rais John Magufuli na lipo tayari kutoa ushirikiano wa dhati kadri itakavyohitajika kuhakikisha juhudi hizi hazipotei bure na sekta ya madini inachangia maendeleo ya wananchi na Taifa kwa ujumla,” alisema Mkuchika ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Haki, Kinga, Maadili na Madaraka ya Bunge.

Lakini, aliposimama akiwa wa kwanza kuchangia hoja ya maazimio hayo, Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu alipinga akisema ni kinyume na majukumu ya Bunge hivyo kulitaka lisiendelee na taratibu za kumpongeza Rais akisema alichokifanya si kipya.

“Kazi ya Bunge ni kuishauri Serikali, siyo kuipongeza au kuiimbia mapambio. Hili siyo azimio la Bunge, bali wana-CCM kumpongeza mwenyekiti wao,” alisema mnadhimu huyo wa Kambi ya Upinzani Bungeni.

Alisema kinachofanywa na Rais Magufuli kilifanywa pia na watangulizi wake waliounda tume kadhaa na kwamba mpaka azimio hilo linajadiliwa, bado usafirishaji wa dhahabu inayochimbwa kwenye migodi mbalimbali nchini unaendelea.

“Dhahabu na madini mengine yanaendelea kusafirishwa hivi sasa. Ripoti za Profesa Mruma na Profesa Osoro ni professorial rubbish. Ni uongo, uongo, uongo,” alisema Lissu.

Ingawa alitakiwa kufuta neno rubbish kwenye mchango wake, Lissu alifafanua kwamba ripoti za wenyeviti hao wa kamati mbili za Rais za kuchunguza makontena 277 ya mchanga wa dhahabu, hazina taarifa sahihi.

Kuhusu azimio hilo kutokuwa na jipya, alisema Rais mstaafu, Benjamin Mkapa aliunda kamati ya Jenerali (Robert) Mboma mwaka 2002, ya Dk (Jonas) Kipokola mwaka 2004 kisha ya Dk (Enos) Bukuku mwaka 2005. Alisema hata Rais wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete naye aliunda mbili za Lawrence Masha na Jaji Mark Bomani.

Alisema kama Bunge linataka kupongeza kuhusiana na kamati zilizoundwa na Rais Magufuli, basi halina budi kuanza na watangulizi hao ambao walifanya kama anachokifanya sasa kwa masilahi ya Taifa huku akipendekeza semina itolewe kwa wabunge ili kuwaongezea uelewa wa masuala ya madini na kuwafanya wachangie wakiwa na ufahamu wa kutosha kuhusu sekta hiyo.

Lissu alipingwa na Mbunge wa Mtera (CCM), Livingstone Lusinde ambaye alitoa sababu za kumpongeza Rais Magufuli akisema kuna tofauti kati ya kamati alizoziunda na zile za watangulizi wake.

“Rais ameenda mbali zaidi. Ripoti imepokewa hadharani na wananchi wote wameisikia. Hii ni hatua ya mbele. Haiwezekani Taifa lisimpongeze Rais anapofanya mambo yanayoonekana,” alisema.

Alisema ameona clip (video fupi) za mawaziri wakuu wastaafu waliohamia upinzani; Edward Lowassa na Frederick Sumaye wakimpongeza Rais kwa hatua zake.

Lakini, Mbunge wa Temeke (CUF), Abdallah Mtolea alionekana kuungana na Lissu akiongeza kwamba maazimio hayo hayakuwa sawa kwa maelezo kwamba kilichofanywa na Rais Magufuli mpaka sasa hakijapiga hatua kubwa zaidi ya kilichofanywa na watangulizi wake.

Alisema suala la msingi ni kudhibiti wizi wa rasilimali nchini akikumbusha kwamba Kikwete pia aliunda tume lakini hata baada ya kupelekewa ripoti, hakufanya chochote hatua ambayo Rais Magufuli amefikia mpaka sasa kwenye vita aliyoianzisha.

Alisema hoja ya wizi wa madini ilianzishwa siku nyingi na wabunge ambao walionekana kuwa si wazalendo. “Kama Mkapa na Kikwete tungewapongeza kwa kuunda tume leo ingekuwaje? Bunge tusiwe washangiliaji,” alisema.

Alikumbusha pia kwamba Mbunge wa Kigoma Kaskazini (CCM), Peter Serukamba alipiga kelele, Dk Hamis Kigwangallah wa Nzega Vijijini (CCM) aliteswa, Tundu Lissu, Zitto Kabwe wa Kigoma Mjini (ACT Wazalendo) na John Mnyika wa Kibamba (Chadema) walilizungumza suala hilo lakini walibezwa.

Alisema kwa kuwa suala hilo sasa linazungumzwa na mtu anayependwa, linaungwa mkono.

Katika mchango wake, Hasunga ambaye ndiye aliyekuwa mtoa hoja alisema hatua ya Rais kuzuia usafirishaji wa mchanga nje ni muhimu inayopaswa kuungwa mkono na Watanzania wote.

“Jimboni na mkoani kwangu kuna madini mengi, hatustahili kuwa maskini,” alisema.

Akiunga mkono hoja hiyo, Mbunge wa Mwibara (CCM), Kangi Lugola alisema anachokifanya Rais Magufuli ndicho alichoahidi hata kabla hajashika wadhifa huo,

“Aliahidi watu watalima kwa meno, tunaona mafisadi wakilima kwa meno. Namuomba hata watu wanaowatetea wezi hawa awalimishe kwa meno pia.”

Mbunge huyo ambaye aghalabu huzungumza kwa mbwembwe aliungwa mkono na Mbunge wa Rufiji (CCM), Mohamed Mchengerwa ambaye alitaka neno uzalendo liondolewe kwenye kamusi ya Kiswahili endapo kuna mtu atapinga yanayofanywa na Rais Magufuli.

“Tunaamini mambo haya yakitekelezwa vyema tutakuwa na barabara za lami na hatutakuwa na deni la Taifa,” alisema Mchengerwa.

Ajali ya Moto London: Watu 12 Wafariki, 18 Wamo Katika Hali Mahututi Hospitali

$
0
0
London

Watu 12 wamethibitishwa kufariki na wengine 18 wamo katika hali mahututi hospitalini baada ya moto kuteketeza jumba la ghorofa 24 la makazi magharibi mwa London.


Moto huo ulizuka katika jumba hilo usiku wa kuamkia Jumatano. Jengo hilo bado linawaka moto na watu wengi hawajulikani walipo.

Taarifa za kwanza za kuzuka kwa moto jumba hilo la Grenfell Tower, kaskazini mwa Kensington ziliripotiwa saa, 00:54 BST (saa tisa kasoro dakika tisa Afrika Mashariki).

Watu 12 wamefariki kwa mujibu wa polisi, na idadi hiyo inatarajiwa kuongezeka.

Kuna watu 78 ambao wamepokea matibabu hospitalini. Hospitali sita – St Mary’s, Chelsea and Westminster, Royal Free, St Thomas’, Charing Cross Hospital na King’s College Hospital – zilipokea majeruhi.

Kamishna wa wazima moto wa London Dany Cotton anasema wazima moto kadha walipata majeraha madogo.

Walioshuhudia wanasema huenda kuna watu waliokwama kwenye jengo hilo, lililokuwa na nyumba 120 za makazi.

Diwani wa Notting Dale Judith Blakeman, anayeishi hapo karibu, anasema kumekuwa na watu kati ya 400 na 600 ambao wamekuwa wakiishi katika jumba hilo.

Meya wa London Sadiq Khan amesema wazimamoto walifanikiwa kufikia ghorofa ya 12 pekee.

Polisi wa jiji wametoa nambari ya dharura kwa watu wanaotafuta habari kuhusu jamaa na marafiki – 0800 0961 233.

Source:BBC
Viewing all 104793 articles
Browse latest View live




Latest Images