Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104799 articles
Browse latest View live

Watoto wawili wafariki dunia kwa kula boga

$
0
0

WATOTO wawili wa familia moja, wilayani Kiteto, Mkoa wa Manyara, wamefariki dunia baada ya kula boga.

Wakati huo huo, watoto wengine watatu wamelazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma, baada ya kula boga hilo linalodaiwa kuwa na sumu.


Waliopoteza maisha wametajwa kuwa ni Leiyoo Birikaa (6) na Nanyori Birikaa (12), wote wakazi wa Kijiji cha Partimbo, wakati waliolazwa hospitalini hapo ni Kitwaini Birikaa (12) Orkiang Birikaa (7) na Taleck Birikaa (6)

Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Partimbo, Kimirey Mesiaya, aliliambia MTANZANIA jana kwamba aina ya boga lililosababisha madhara hayo, imekuwa ikitumiwa na wananchi wa kijiji hicho.

Kutokana na hali hiyo, aliitaka Serikali ifanye uchunguzi wa maboga hayo kwa sababu yamekuwa yakiliwa na wananchi wengi kama sehemu ya vyakula vyao vya kawaida.

Akizungumzia tukio hilo, mmoja wa madaktari wanaowatibu wagonjwa hao, Dk. Sarah Magoma, alithibitisha kupokewa kwa watoto hao na kusema walikuwa na matatizo katika maini kwa sababu yalikuwa hayafanyi kazi vizuri.

“Dalili za matatizo hayo ni kuumwa tumbo na kutapika, macho kubadilika rangi na kuwa ya njano na kutokwa damu puani na mdomoni.

“Pamoja na hayo, matatizo ya aina hiyo yamewahi kutokea wilayani Chemba na Kondoa. Kwa hiyo, tunaendelea kufuatilia chanzo chake kwa sababu watu wamekuwa wakipoteza maisha pamoja na jitihada zinazofanywa na madaktari,” alisema Dk. Magoma.

Si Kwa Hii Enzi ya Magufuli...Adai Wanaopata Mimba Mashuleni Hakuna Kuendelea na Shule

$
0
0
Rais John Magufuli amesema wakati wa utawala wake hakuna mwanafunzi atakayepata mimba na kuruhusiwa kurudi shule.

 Ameyasema hayo leo (Alhamisi) wakati wa ziara yake ya siku tatu mkoani Pwani ambako amezindua viwanda saba.

“Azae halafu aende kuwahubiria wenzake, unajua ilikuwa hivi, halafu nilifanya hivi,”amesema.

Amesema waliozaa shuleni wanaweza kwenda kupata elimu nyingine kama vyuo vya ufundi stadi (Veta) na kilimo badala ya kurudi shule na kuanza kuwafundisha wenzao yale waliyoyafanya.

“Mnataka niwaambie warudi shule halafu, ni bora wakalime ili ile nguvu waliyoitumia kujifungua waitumie kulima,” amesema.

Amesema; “Ni rahisi zaidi kuzalia chuo kikuu, ule mwaka wa kwanza, wa pili lakini sekondari, darasa la kwanza  kupeleka walio na watoto, tunapoteza maadili yetu, watazaa mno.”

 “Mtajikuta darasa la kwanza wote wanawahi nyumbani kwenda kunyonyesha. Hii tutalipeleka Taifa pabaya,” amesema.

Dawa Za Nywele Zinazosababisha Uvimbe Wa Kizazi Kwa Wanawake

$
0
0
Dawa za kulainisha nywele (relaxer) zimekuwa zinapendwa na wanawake wengi wa Afrika kwa kuwa zina uwezo wa kulainisha nywele na kumfanya apendeze na awe wa kuvutia.

Hata hivyo, wataalamu wa afya wanadai kuwa dawa hizo zinasababisha uvimbe kwenye kizazi kutokana na kemikali za dawa hizo ambazo huingia mwilini kupitia majeraha au ngozi wakati wa kupaka.

Daktari wa Manispaa ya Ilala, Laurent Chipata alifanya utafiti na kubaini kuwa dawa za nywele na vipodozi zina kemikali ambazo husababisha uzalishwaji wa vichocheo kwa kiasi kikubwa na kusababisha uvimbe kwenye kizazi uitwao fibroids au leimyoma.

“Kemikali hizi hupenya kwenye ngozi na wakati mwingine hata kwa harufu tu, husababisha kuzalishwa kwa wingi wa vichocheo aina ya estrogen ambavyo huchangia kuota kwa uvimbe wa fibroids,” anasema.

Dk Chipata anasema kukua kwa uvimbe kwenye kizazi hutokea katika kipindi ambacho mama yupo kwenye uzazi yaani kabla hajakoma hedhi.

Utafiti wa Dk Chipata ulifanywa nchini na kujumuisha wanawake wa kada tofauti tofauti wanaotumia dawa za nywele na wale wasiotumia na ukubwa wa tatizo hili ulibainika.

“Zipo kemikali tofauti tofauti zinazosababisha uvinbe kwenye kizazi, zipo za kwenye dawa za kilimo kama DDT na za kwenye mafuta ya ngozi kama vile mercury na hydroquionone,” anasema.

Dk Chipata anasema madhara yanayopatikana katika kemikali za vipodozi ni makubwa siyo tu kwenye kizazi bali nyingine husababisha saratani au kufeli kwa figo. Anatoa mfano wa kemikali ya zebaki (mercury).

“Dawa za nywele zina madhara si lazima zipenye kwenye ngozi baada ya mtu kupata jeraha la kuungua bali zinaweza kupenya zenyewe kwenye ngozi kutokana na mfumo wa ngozi,” anasema.

Anashauri kuwa ni vyema watu wakasoma kipodozi kimetengenezwa kwa nini kabla ya kukitumia na kuongeza kuwa ni salama zaidi kubaki na ngozi au nywele halisi badala ya kujibadilisha.

Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) imekataza vipodozi vyenye kemikali kama biothionol, hexachlorophene, mercury, vinyl chloride, zirconium na bidhaa zenye aerosol, chloroquionone, steroids, methylene na chloroform.

Utafiti mwingine uliofanywa mwaka 2012 na Dk Lauren Wise na wenzake nchini Marekani na kuchapishwa kwenye jarida la afya la nchini Marekani ulibaini kuwa vipodozi vingi vina kemikali zenye vichocheo vya estrogen ambavyo kwa kawaida huchochea kasi ya kuota kwa uvimbe kwenye kizazi cha mwanamke na wakati mwingine kwenye mji wa mimba. Kitaalamu uvimbe au vivimbe hivi hujulikana kama fibroids au myoma.

Dk Wise anasema aliwafanyia uchunguzi wanawake wanaotumia dawa za kulainisha nywele na kuangali umri walioanza kutumia dawa hizo, mara ngapi, waliungua kiasi gani na walikaa na dawa hizo kichwani kwa kipindi gani.

Aliwafuatilia wanawake 23,580 wanaotumia dawa za kulainisha nywele na baada ya kipindi fulani walipimwa. Kati yao, 7146 waligundulika kuwa na uvimbe kwenye kizazi baada ya kupimwa kwa mionzi na wengine kufanyiwa upasuaji.

Kwa nini relaxer ni hatari kwa wanawake?
Dk Wise anasema mchanganyiko ulio kenye dawa za nywele hasa zilizoandikwa “Lye Relaxer” ni sodium hydroxide wakati makopo ya dawa yaliyoandikwa “No Lye Relaxer” yana calcium hydroxide na guanidine carbonate.

Bidhaa za kulainishwa nywele zilizoandikwa ‘no lye relaxer’ zinadaiwa kusababisha majeraha kwa kiasi kidogo ukilinganisha na zile zilizoandikwa “Lye Relaxer”.

“Tale Alitakiwa Kunipenda…Nilikuwa Msanii Mkubwa Kabla yake” – Chid Benz

$
0
0
Kupitia XXL ya Clouds FM rapa mkongwe Bongo Chid Benzi amefunguka na kueleza kilichotokea kipindi ambacho Babu Tale alijitolea kumsaidia ili arudi kwenye hali ya zamani na kuendelea na maisha yake kama awali.

Chid Benzi amesema kuwa Babu Tale angemvumilia na hali yake aliyokuwa nayo kabla ya kukata tamaa ingawa anampenda na kumuheshimu kama kaka yake na hana maana kuwa alikosea kumuacha kipindi kile.

“Nilikuwa na game yangu kitambo na Tale alitakiwa kunipenda. Angevumilia tu maana nilikuwa msanii mkubwa kabla yake kwenye game. Kipindi nipo zangu Sober ilikuja list ya Magezeti wapo watu wanavuta Unga, niligundua tupo wengi kumbe sipo peke yangu.

“Tale asinitangaze kwenye Media mimi nimerudia Madawa, yeye ni kaka yangu napenda tuishi kama ndugu siku zote. Sikuwepo Wasafi, nilienda pale kama La Familia ila Tale alikuwa ananisimamia kama mdogo wake tu. Nahangaika sana kupambana ili nitoke kwenye hili janga, now am okay.” – Chid Benzi.

Shilole Amlipia Kodi ya Nyumba Nuh Mziwanda....Mke Afunguka

$
0
0
June 22, 2017 kupitia XXL ya Clouds FM mtangazaji Soudy Brown ametusogezea U HEARD ambayo inamuhusu mwimbaji wa Bongofleva Nuh Mziwanda ambaye inadaiwa kodi ya nyumba anayoishi na familia yake amelipiwa na aliyekuwa mpenzi wake Shilole.

Kufuatia kusambaa kwa taarifa hizo Soudy Brown alipiga story na Nawal ambaye ni mke wa Nuh Mziwanda na kusema haimuhusu akidai kitendo hiko ni vizuri kwa kuwa kinampunguzia mumewe majukumu na haimuumizi bali anaangalia maisha yake.

Kwangu mimi naona vizuri inampungumzia mume wangu majukumu kwa sababu ana majukumu mengi; amuangalie mtoto wake, mkewe, familia, bado yeye mwenyewe. Kwa hiyo hata kama yeye akilipa kodi hainiumi hata kidogo. Mimi naangalia maisha yangu.” – Nawal.

Hii Ndio Historia ya Muuza Madawa ya Kulevya Nguli Duniani PABLO ESCOBAR Aliyejijengea Gereza

$
0
0

Katika milima inayotazamana na mji wa Medellín nchini Colombia, yapo majengo ya kifahari kabisa ndani ya milima hiyo ambayo kwa sasa majengo haya yanatumika kama nyumba ya watawa wa Kanisa Katoliki lakini kabla ya watawa hawa kupewa majengo haya mwaka 2007, majengo haya yalikuwa ni gereza ambalo lilijengwa mwaka 1991 kumuhifadhi mfungwa maalumu raia wa Colombia.

Gereza hili lilikuwa ni tofauti kabisa na magereza yote ambayo umewahi kuyasikia kwani gereza hili licha ya kuwa mali ya serikali lakini michoro yake ilichorwa na kubuniwa na mfungwa mwenyewe.
Si hivyo tu, bali hata maaskari magereza ambao walikuwa wanalinda gereza hili walichaguliwa na mfungwa mwenyewe na hata polisi wa nchi ya Colombia walikuwa hawaruhusiwi kusogolea gereza hilo hata umbali wa maili 12. Kama hiyo haitoshi gereza hili lilikuwa na uwanja wa mpira wa miguu, lilikuwa na bafu lenye Jaccuzi, lilikuwa na bar, lilikuwa na maporomoko ya maji (water falls) yaliyobuniwa kiustadi, na pia chumba (selo) alicholala mfungwa huyu kilikuwa na kitanda kikubwa cha duara chenye kuzunguka pamoja na televisheni kubwa.

Kama hii haitoshi kwenye gereza hilo pia kulikuwa na chumba maalumu cha michezo ya watoto maalumu kwa ajili ya watoto wa mfungwa huyo pindi akitembelewa na familia yake. Na pia ndani ya gereza kuliwekwa darubini kali (Telescope) ya kumuwezesha mfungwa huyo kuangalia katika mji wa Medellín ambako familia ya mfungwa huyu iliishi na kila siku jioni walitoka nje kibarazani kuongea naye kwenye simu huku akiwatazama kwa darubini.

Gereza hili lilijulikana kama La Catedral (the cathedral) na lilimuhifadhi mfungwa muhimu zaidi duniani na binadamu aliyeifinyanga na kuifanya biashara ya mihadarati iwe jinsi ilivyo hivi leo. Marafiki zake wa karibu walipenda kumuita El Patrón (The Boss) au El Zar de la Cocaína (The Tsar of Cocaine) lakini alipozaliwa wazazi wake walimuita Pablo Emilio Escober Gaviria au kwa kifupi Pablo Escobar kama ulimwengu wote ulivyomtambua.
The Boss
Akiwa mtoto wa tatu kwenye familia ya watoto saba ambapo baba yake alikuwa ni mkulima na mama yeke mwalimu wa shule ya chekechea, Pablo Escobar alikuwa ni mwenye kutamani mambo mazito na mwenye maono makubwa tangu angali mtoto.
Akiwa bado kwenye umri wa makumi (teenage) Pablo mara kwa mara aliwaambia ndugu zake na marafiki zake kuwa anataka awe na utajiri wa kiasi cha Peso Milioni 1 za Colombia (COL$ 1 Million) atakapofikisha umri wa miaka 22.
Ndoto hizi zilimfanya ashindwe kumaliza Chuo kikuu alipokuwa anasoma (Universidad Autónoma LatinoAmericana of Madellín) na kujiingiza katika biashara za halali na haramu na hatimaye aliacha masomo chuoni. Moja ya biashara zake haramu za kwanza kabisa akiwa kijana chini ya miaka 21 ilikuwa ni kutengeneza vyeti bandia vya stashahada vya chuo alichokuwa anasoma na kuwauzia watu waliohitaji kwa ajili ya kwenda kupata ajira.
Pamoja na biashara hiyo pia Pablo alijihusisha na kusambaza mizigo ya sigara zilizokuwa haziruhusiwi nchini Colombia (Marlboro), pia alifanya kazi kama mlinzi binafsi (bodyguard) pamoja na wizi wa magari.

Moja ya matukio muhimu ya ujana wa Pablo yaliyochangia kuamsha ari ndani yake na kumfanya atamani kuwa moja wa manguli wa biashara haramu lilikuwa ni tukio ambalo alipofikisha miaka 26 alifanikiwa kuweka benki (Cash Deposit) kiasi cha Peso Millioni 100 za Colombia (COL$ 100 Million).
Mafanikio haya yaliwasha taa ndani yake na kuamsha ari ya kutaka kuwa 'Papa' katika 'Dunia' ya siri ya ulimwengu wa biashara haramu.
Katika miaka ya 1970 mamlaka ya kupambana na matumizi mabaya ya madawa nchini marekani (US Drug Enforcement Agency) waliwahi kutangaza kuwa wamewekeza zaidi rasilimali zao kupambana na matumizi na uingizaji wa dawa aina ya Heroin nchini marekani na kwa maoni yao walisema kuwa wanadhani madawa aina ya Cocaine hayakuwa na uwezo wa kuleta uteja (addiction) au kufanya mtumiaji kuwa muhalifu tofauti na dawa aina ya Heroin. Hivyo basi walielekeza nguvu zao zote na rasilimali kupambana na biashara ya usafirishaji wa Heroin kama kipaumbele cha kazi zao.
Hili lilikuwa ni kosa kubwa sana kwa upande wao. Kwani kijana Pablo aliona mwanya huu na udhaifu huu upande wa DEA au pengine tusema kwamba Pablo alifahamu zaidi kuhusu ulimwengu wa mihadarati kuliko DEA.

Kitu kikubwa ambacho Pablo alikiona na watu wakiwemo DEA hawakukiona ilikuwa ni uwezekano (potential) ya kuifanya Cocaine kuwa moja ya madawa yenye soko zaidi Amerika ya Kaskazini. Katika kipindi hiki kulikuwa na watumiaji wachache sana wa Cocaine nchini marekani lakini Pablo aliona fursa ya kuifanya mihadarati hiyo kuwa moja ya madawa yenye kuhitajika sana nchini marekani na ulimwenguni kiujumla.
Kutokana na uzoefu wake wa ulimwengu wa kihalifu, Pablo aligundua kuwa zao la Coca linalimwa nchini Bolivia ambalo linatumika kutengeneza Cocaine ni bora zaidi kuliko Coca inayolimwa nchini kwake Colombia. Hivyo basi Pablo akadhamiria kuwa kama anaingia kwenye biashara hii ya kusafirisha Cocaine ni lazima mihadarati yake iwe tofauti na bora zaidi kuliko Cocaine nyingine watu waliyozoea kutumia. Akadhamiria kufanya Cocaine yake iwe daraja la kwanza ili kuvutia watumiaji na kufanya soko likue kwa haraka.

Kama sehemu ya mkakati wake wa kuingia rasmi kwenye biashara ya kusafirisha mihadarati aina ya Cocaine, mwaka 1975 kijana Pablo alisafiri mpaka nchini Bolivia kukutana na Roberto Suaréz Goméz ambaye marafiki zake walipenda kumuita El Padrino (The Godfather) kiongozi wa Genge lililoitwa La Corparacíon (The Corporation). Suaréz alikuwa ndiye mtu pekee anayeendesha na kuratibu uzalishaji wa zao la Coca katika nchi ya Bolivia na Peru. Kipindi hiki Suaréz tayari alikuwa na mtandao mkubwa katika America ya kusini na alikuwa na jina kubwa, ushawishi na nguvu ya kijeshi hivyo haikuwa kazi rahisi kwa kijana Pablo kumshawishi Suaréz akubali kufanya naye biashara.
Huyu bwana Suaréz alikuwa na nguvu kiasi kwamba alikuwa na jeshi lake binafsi la anga (Air force) na wanajeshi wa miguu 1,500 ambao walipatiwa mafunzo nchini libya.

Pablo alitumia uwezo wake wa kujieleza na uzoefu wake wa ulimwengu wa kihalifu kumshawishi Suaréz na kumueleza kuhusu mkakati wake wa kuiteka biashara ya mihadarati ya Cocaine nchini marekani na akamdadavulia jinsi ambavyo yeye Suaréz atapata utajiri wa kupindukia kama atakubali kufanya nae biashara.
Pia Pablo alimpa wazo Suaréz kuwa atumie ushawishi wake alionao serikalini (Suaréz alikuwa amefanikiwa kumpenyeza Mdogo wake serikalini na kuwa Waziri wa mambo ya ndani) ahakikishe wanakutana na kiongozi wa Cuba Fidel Castro ili wamuombe kuwa mshirika wao katika mambo kadhaa.
Suala hili lilifanikiwa kwani Pablo na Suaréz walipata fursa adhimu na wakakutana na Fidel Castro na ombi lao kubwa kwake lilikuwa ni kuwaruhusu kupitisha mizigo yao nchini kwake Cuba na nchi za jirani pasipo bugudha. Pia walimuomba aruhusu ndege zao za mizigo zitue kwenye viwanja vya ndege vya Cuba na kujaza mafuta pale inapobidi kufanya hivyo.
Castro akawakubalia kwa masharti mawili, moja ni kwamba atakuwa anawachaji mamilioni ya dola za marekani kwa huduma hizo na pili mihadarati hiyo isiuzwe ndani ya Amerika ya Kusini bali isafirishwe na kuuzwa Marekani ambapo Fidel Castro alisisitiza kuwa atafurahi akiona vijana wa Mabepari wakiharibika na mihadarati.

Masharti yote mawili haya yakakubaliwa na Pablo na Suaréz kisha wakarejea Bolivia. Baada ya kufanya mazungumzo juu ya namna watakavyo fanya biashara hatimae Pablo na Suaréz walifikia muafaka na kwa mzigo wake wa kwanza alioununua nchini Bolivia kutoka kwa Suaréz ulikuwa ni kilo 14 za unga gafi za Cocaine.
Baada ya unga gafi kufikishwa nchini Colombia kwenye mji wa Medellín, Pablo alikuwa ameandaa jengo maalum la ghorofa mbili ambalo alilitengeneza kuwa maabara maalumu ambapo Cocaine gafi kutoka Bolivia ilichanganywa na maligafi nyingine na kuboreshwa zaidi kikemia na hatimaye kupata Cocaine daraja la kwanza aliyoihitaji tayari kusafirishwa nchini Marekani kwa 'walaji'.

Baada ya Cocaine kutoka kwa Pablo kuingia kwenye soko la Marekani uhitaji na biashara ya mihadarati ya Cocaine ilipaa kwa kasi ya ajabu na Pablo Escobar akaanzisha rasmi genge lake la biashara ya mihadarati na akaliita Medellíne Cartel.
Pablo akatengeneza mtandao madhubuti wa wasambazaji wa mihadarati yake katika miji ya Florida na California pamoja na majimbo mengine ya Marekani.
Pia akabuni njia mpya ya kupitisha mihadarati kupitia Bahamasi katika kisiwa cha Norman's Cay takribani kilomita 350 kusini mashariki mwa pwani ya Florida.
Ili kufanikisha zaidi azma yake Pablo Escobar alinunua nusu ya ardhi ya kisiwa cha Norman's Cay na nusu nyingine ikanunuliwa na swahiba wake wa kimarekani aliyeitwa Robert Vesco ambaye pia alikuwa ndiye anashughulikia masuala yake ya kibenki na uhasibu.

Katika Kisiwa hiki Pablo alitengeneza uwanja wa ndege, bandari, hoteli, nyumba za kuishi pamoja na ghala kubwa la jokofu maalumu kwa ajili ya kuhifadhi mizigo ya Cocaine kabla ya kuisafirisha kwenda marekani. Kwa kifupi hapa ndipo kilikuwa kitovu cha kibiashara cha Genge lake la Medellíne Cartel.
Pablo Escobar alikuwa amepania haswa kuliteka soko la Cocaine Amerika ya Kaskazini na hii ilijidhihirisha kutokana na juhudi zake alizozifanya kibiashara ili mda wote awe hatua kadhaa mbele tofauti na washindani wenzake kibiashara.

Pablo Escobar alikuwa amepania haswa kuliteka soko la Cocaine Amerika ya Kaskazini na hii ilijidhihirisha kutokana na juhudi zake alizozifanya kibiashara ili mda wote awe hatua kadhaa mbele tofauti na washindani wenzake kibiashara.
Ili kufanikisha usafirishaji wa mizigo yake kwa ufasaha na uhakika Pablo alinunua ndege za mizigo 15 za ukubwa wa kati na helikopta 6. Pia alinunua Nyambizi ndogo mbili (submarines) kwa ajili ya kusafirisha mizigo mikubwa ya mihadarati.
Hadi kufikia mwaka 1985 Pablo alikuwa anasafirisha takribani tani 70 mpaka 80 za Cocaine kwa mwezi na alikuwa ameshikilia asilimia 80 (80%) ya soko la mihadarati la Marekani.
Na katika kipindi hiki Genge lake la Medellíne Cartel lilikuwa linaingiza kipato cha cha Dola Milioni 70 kwa siku (Shilingi Bilioni 140 za Kitanzania) na mapato yao kwa mwaka mzima yalifikia Dola Bilioni 21.9. (Shilingi Trilioni 46 za Kitanzania).
Katika miaka ya 1990 utajiri wake binafsi ulifikia kiasi cha Dola za kimarekani Bilioni 30 ambazo ni sawa na Dola Bilioni 54 kwa hesabu za sasa (Shilingi Trilioni 110 za kitanzania)
Ni katika kipindi hiki ambacho Jarida maarufu la Forbes lilimuorodhesha Pablo Escobar kama mtu namba 5 tajiri zaidi ulimwenguni na muhalifu tajiri zaidi katika historia ya Ulimwengu.
Kutokana na nguvu na ushawishi alionao, Pablo aliteuliwa na serikali kama mjumbe wa baraza la wawakilishi la Colombia (Chamber of Representatives of Colombia) kupitia chama cha Kiliberali Cha Colombia (Colombia Liberal Party).

Moja ya majukumu muhimu aliyoyafanya akiwa kama Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi kilikuwa ni kwenda kuiwakilisha Serikali ya Colombia katika sherehe za kuapishwa kwa Waziri Mkuu mpya wa Uhispania Bw. Felipe González mwaka 1982 ambapo Pablo alitumia nafasi hii ya Safari ya kiserikali nchini Uhispania kuanzisha tawi jipya la Genge lake la Medellíne Cartel katika nchi ya Uhispania.
Hacienda Nápoles: Pepo Juu ya Uso wa Dunia
Kutokana na utajiri uliopitiliza wa Pablo Escobar alithubutu kutengeneza makazi ya kuishi ambayo namna pekee ya kuyaelezea ni kana kwamba alijitengenezea 'pepo' akiwa duniani.
Katika mji mdogo wa Puerto Triunfo, takribani kilomita 150 kutoka katika mji wa Medellín, Pablo alinunua eneo lenye ukubwa wa Kilomita za mraba 20 na kujenga makazi yake na familia yake na akayaita makazi haya Hacienda Nápoles (Naples Estate).

Licha ya majengo ya kifahari ya kuishi yeye na familia yake pia makazi haya yaliwekwa anasa lukuki zisizomothirika. Ndani ya makazi haya kulikuwa na Uwanja wa ndege binafsi (private airport), bustani maalumu ya sanamu za kuchonga na kufinyanga (Sculpture Park), kulikuwa na sehemu maalumu ya kuhifadhi magari ya kifahari na pikipiki za kifahari kwa ajili ya kutazama tu (collection), kulikuwa na uwanja wa mbio za magari magogo (kart racing track), kulikuwa na uwanja wa mapigano ya ng'ombe (Bullring), na pia ndani ya makazi haya kulikuwa na mbuga ya wanyama ya kutengeneza (Zoo) ambapo Pablo alikusanya aina mbali mbali za wanyama kutoka kila kona ya dunia na kuwaweka humo.
Katika geti la kuingia kwenye 'pepo' ya Pablo sehemu ya juu ya geti ilininginizwa ndege (ndege halisi) kama urembo. Ndege hii aina ya Piper PA-18 Super Cub yenye namba ya mkia HK-617-P hii ndio ilikuwa ndege ya kwanza aliyoitumia Pablo kuingiza mzigo wake wa kwanza wa Cocaine nchini Marekani.
Hapa katika 'pepo' hii ndipo ambapo Pablo Escobar aliishi yeye na familia yake.
Plata o Plomo
Moja ya vitu muhimu vya kihalifu alivyovifanya Pablo na kufanikiwa kuibuka kama kinara wa uhalifu Amerika ya kusini ilikuwa ni kutekeleza sera yake aliyoianzisha yeye mwenyewe ili kuidhibiti serikali na vyombo vya ulinzi ambapo sera hii aliita "Plata o Plomo" (silver of lead (fedha au risasi)). Akiwa na maana kwamba kama wewe ni mtu wa serikali na ikitokea mmesigana basi atakupa fedha (rushwa) kama ukikataa kupokea fedha basi anakupiga risasi.

Sera hii ilimfanya Pablo aogopwe na watendaji wa serikali pamoja na vyombo vya usalama na ikapelekea wengi kukubali 'Plata' (silver (fedha)) wakihofia kupoteza maisha endapo wangekataa fedha kutoka kwa Pablo. Hii ilimsaidia Pablo Escobar kuwa na vibaraka wengi katika serikali na vyombo vya ulinzi na usalama.
Lakini sera hii iligharimu maisha ya watu wengi sana wale ambao walikataa kupokea fedha kutoka kwa Pablo na mojawapo ya matukio mawili yanayokumbukwa sana ya utekelezaji wa sera ya 'Plata o Plomo' ni haya:-
Mosi; Uvamizi wa Mahakama Kuu ya Colombia 1985.
Mwaka 1985 baada ya mabishano ya muda mrefu bungeni kuhusu vifungu vya kikatiba vinavyokataza raia wa nchi ya Colombia kukabidhiwa kwa nchi ya kigeni akiwa kama muhalifu hatimae serikali ikafungua kesi ya kikatiba mahakama kuu ya Colombia ikitaka ruhusu ya kukabidhi baadhi ya wahalifu kwa serikali ya Marekani ikitokea wakikamatwa.
Suala hili lilikuwa linamlenga moja kwa moja Pablo Escobar kwani serikali ya Colombia ilikuwa inapewa shinikizo kubwa na Marekani kuwa wafanye marekebisho ya katiba ili iruhusu raia wa nchi hiyo ambaye ni muhalifu kukabidhiwa kwa nchi ya kigeni. Haya yalikuwa ni maandalizi endapo ikitokea Pablo Escobar akikamatwa.

Pablo akajitahidi kwa juhudi zake zote kuhonga serikalini na hata kutoa onyo kuwa mabadiliko hayo ya kikatiba yasifanyike lakini serikali iliendelea na mchakato kutokana na shinikizo walikuwa wanapata kutoka kwa marekani.
Inajulikana kwamba Pablo mara kwa mara alikuwa akiapa mbele za watu wake wa karibu kuwa kamwe hatokubali kufungwa katika nchi ya marekani na alikuwa na msemo anaoupenda kuusema kwamba "ni heri kuwa kaburini Colombia kuliko kuwa hai kwenye gereza la Marekani".
Baada ya juhudi zake zote za kuionya serikali kutobadili katiba kushindikana hatimaye Pablo akakodi kikundi cha wapiganaji wa msituni kilichoitwa M-19 ili wasaidie kumaliza tatizo lake.
Siku ya Novemba 6, 1985 majaji 25 wa mahakama kuu walikuwa katika vikao vya mwisho kujadili na hatimae waweze kuridhia mabadiliko hayo ya katiba lakini kabla ya kumaliza vikao vyao na kuridhia mabadiliko hayo walivamiwa na wapiganaji wa kikundi cha M-19.
Wapiganaji hawa walivamia na kuteka mahakama kuu kwa muda wa siku mbili na zaidi ya nusu ya majaji waliuwawa na waliosalia walichukuliwa mateka.
Majaji hawa waliochukuliwa mateka walikuja kutumiaka kama sharti muhimu la kuibana serikali waache kurekebisha katiba ili waweze kuachiwa. Baada ya serikali kukubali kuacha kubadili katiba hasa kipengele cha kukabidhi wahalifu kwa nchi ya kigeni, majaji wote waliotekwa wakaachiwa.
Pili; Mauaji Mgombea Urais Luis Carlos Galán
Tukio la pili linalokumbukwa sana la utekelezaji wa sera ya 'Plata o Plomo' lilikuwa ni mauaji ya mgombea Urais wa Colombia aliyeitwa Luis Carlos Galán. Galán alikuwa anaongoza kwenye kura za maoni nchi nzima na alikuwa anatarajiwa kushinda kwenye uchaguzi mkuu wa urais wa Colombia wa mwaka 1990.
Moja ya sera kubwa aliyokuwa anaihubiri kila kona ya nchi ilikuwa ni kupambaa na Magenge ya Mihadarati hasa hasa akililenga Genge la Medellíne Cartel na kiongozi wake Pablo Escobar.

Pablo alimtumia barua kadhaa ambazo ziliwekwa nje ya nyumba yake kwenye kisanduku cha barua akimuonya na kumtaka aachane na sera hiyo ya kumsakama yeye pamoja na washirika wake wa Medellíne Cartel lakini Bwana Galán alionekana dhahiri amezamilia kutekeleza sera hiyo endapo angechaguliwa kuwa rais wa Colombia.
Akiwa katika kampeni Bwana Galán alifanikiwa kufika kwenye mji wa Madellín ambapo Pablo alikuwa na ushawishi mkubwa na wapo wananchi waliojaribu kumuua Galán kwa kumrushia guruneti la kutupa kwa roketi (Rocket Propelled grenade) lakini kwa bahati nzuri Bwana Galán akisalimika.
Baada ya hapo Pablo akakodi wadunguaji maalumu kufatilia nyendo za Galán na akawapa amri ya kumpiga risasi mara tu wakipata upenyo wa kufanya hivyo.
Wiki kadhaa baadae akiwa kwenye kampeni katika mji wa Saocho Kiranga alipokwenda kuhutubia wafuasi wake wapatao 10,000 waliokusanyika wakisubiri kumsikia na mara baada ya kuwasili na kupanda jukwaani kuhutubia kabla hajatoa hata salamu kwa wafuasi wake alidunguliwa na risasi na kupoteza maisha papo hapo.

Tukio hili lilizua taharuki nchi nzima na imekuwa skendali yenye utata mpaka leo hii nchini Colombia kwani kuna tetesi kuwa viongozi wa serikali, polisi, pamoja na mashushushu walishirikiana na Pablo Escobar kutekeleza mauaji haya.
Licha ya Pablo kuonekana kama adui namba moja nchini marekani na baadhi wa watendaji wa serikali ya Colombia hali ili kuwa tofauti kwa raia masikini wa Colombia ambao wengi wao walimuona kama shujaa wao na katika mji aliozaliwa na kushi wa Medellín anaonekana zaidi ya shujaa kwani mpaka leo hii wanamuona kama ni aina fulani hivi ya masihi walipewa.
Hii inatokana na umahiri wa Pablo Escobar katika mahusiano na jamii iliyokuwa inamzunguka.
Pablo alikuwa ni mtu mwenye kusaidia masikini nchini Colombia pengine kuliko hata serikali yenyewe.
Pablo alijitolea kweli kweli katika kuboresha huduma za jamii kama vile kujenga mahospitali, shule, nyumba za wazee, nyumba za kuishi kwa ajili ya masikini na akawekeza fedha nyungi kujenga miundo mbinu ya Kanisa Katoliki na nyumba za kuabudia. Pia Pablo alijenga vya kuendeleza watoto katika mpira wa miguu, alifadhili klabu mbali mbali za wakubwa za mpira wa miguu na alijenga viwanja vya kisasa kabisa vya mpira na michezo mingine.

Ilifikia hatua mpaka Pablo alikuwa anawapa fedha taslimu wananchi wa Madellíne ili waweze kujikimu kimaisha.
Mambo haya yote yalifanya wananchi wampende na kufumbia macho uhalifu wote aliokuwa anaufanya.
Kwa mfano katika mji wa Madellín ilifikia hatua kana kwamba wananchi wote walikuwa ni walinzi wake binafsi kwani walikuwa wakimtonya kila walipoona polisi wageni wakiingia hata kwa siri kwenye mji huo. Au wakati mwingine walikuwa wakitoa taarifa za uongo au kukataa kusema chochote pindi wakiulizwa na vyombo vya ulinzi kuhusu nyendo za Pablo.
Hii ilimfanya Pablo azidi kujizatiti na kuongeza mahaba kwa wakazi wa Medellín na raia wa Colombia kwa ujumla.Pablo ataendelea kua na mahusuano mazuri na wananchi.



VITA KUU YA KWANZA YA MAGENGE YA MIHADARATI.

Kuna msemo wanasema 'adui wa adui yako ni rafiki yako'! Swali: je, inakuwaje pale adui wa adui yako akitishia maslahi yako??
Adui wa Adui yako (Kikao cha Kwanza)
Hapo baadae nitaeleza kwa kifupi kuhusu kuibuka kwa genge lingine ambalo nalo lilishamiri katika biashara ya Cocaine lililoitwa Cali Cartel hivyo kufanya kuwe na uwepo wa magenge mawili yanayoshindana kibiashara yaani Medellín Cartel chini ya Pablo Escobar na Cali Cartel.
Licha ya ushindani wao wa kibiashara mwaka 1983 iliwabidi washirikiane kwa sababu za msingi kabisa. kuliibuka kikundi cha wahuni waliokuwa wanateka watu na kudai fedha kutoka kwa ndugu ili wawaachie. Baada ya kuteka ndugu kadhaa wa viongozi wa serikali wahuni hawa wakaanza kuteka ndugu wa mabosi wa Cartels na kudai pesa.
Moja ya watu muhimu waliowateka alikuwa ni Marta Nieves Ochoa dada wa moja ya mabosi wa Cali Cartel na watekaji walikuwa wanataka wapewe dila milioni 10 ili wamuachie. Hii ndio ilikuwa sababu kubwa ya mabosi wa Cali Cartel na Medellín Cartel kukutana ili kuweka mkakati maalumu ambao utapeleka ujumbe kwa wahuni na watekaji wote kuwa familia za mabosi wa Magenge ya mihadarati ni mwiko kuzigusa.
Katika kikao hiki cha kwanza Medellín Cartel na Cali Cartel waliunda kikosi kazi maalumu walichokiita Muerte a Secuestradores (Death to kidnappers (Kifo kwa Watekaji)) au kama kilivyojulikana kwa kifupi MAS.

Kila Genge lilichangia fedha, vifaa (silaha), na askari kwa ajili ya kikosi kazi cha MAS.
Kesho yake baada ya kikundi hiki kuundwa ndege ilipita juu ya uwanja wa mpira wa miguu kuliko kuwa na mechi kubwa ikifanyika na kumwaga vipeperushi kuhusu kutangaza zawadi nono kwa yeyeto atakayetoa taarifa kuhusu kufahamu lolote juu ya wahuni wanaoteka watu na kushinikiza wapewe hela. Jioni ya siku hiyo taarifa muhimu kutoka kwa wananchi zikaanza kuletwa na kikosi kazi cha MAS mara moja kikaanza kukamata wahuni wa vikundi vya utekaji na kuwatesa huku wakiwarekodi na kuwatumia wenzao wanaoshikilia dada wa bosi wa Cali Cartel.
Ndani ya siku tatu Marta Naives dada wa bosi wa Cali Cartel aliachiwa akiwa salama salimini na huo ndio ukawa mwisho wa magenge ya wahuni kuteka wanafamilia wa mabosi wa magenge ya mihadarati.
Kama ni rafiki yako, anaweza kuwa mshirika wako: Kikao cha Pili
Licha ya ushindani wa kibiashara kuendelea kuwepo kati ya Medellin Cartel ya Pablo Escobar na Cali Cartel lakini kufanikiwa kwa mkakati wa MAS kuliwapa moyo kuwa yako maeneo mengine mengi wanayoweza kufanya kwa kushirikiana na yakawa na faida kwa pande zote mbili.
Sehemu ya kwanza ambayo waliona inaweza kuwa na faida kwa pande zote mbili ilikuwa ni Cali Cartel kukubali Pablo Escobar aweze kupitisha fedha zake haramu katika benki ya First InterAmericans Bank ambayo ilikuwa inamilikiwa na maswahiba wa mabosi wa Cali Cartel. Hii ilikuwa na faida kwa kubwa kwa Pablo kwani ilikuwa ni njia rahisi na salama kwake kuweza kusafisha fedha zake haramu lakini pia ilikuwa na faida upande wa wamiliki wa benki maswahiba wa mabosi wa Cali Cartel kwani nao wangepata faida kwa kutoa huduma hiyo kwa Pablo kutokana mabilioni ya dola ya dola ambayo atakuwa anayapitisha kwenye benki yao.

Sehemu ya pili waliyokubaliana kushirikiana ilikuwa ni namna ya kuratibu bei ya Cocaine mtaani, kuratibu viwango vya ubora wa uzalishaji na njia salama za kusafirisha mizigo.
Sehemu ya tatu walikubaliana kuhusu kugawana soko. Cali Cartel wakakubaliwa kuendesha biashara kwenye jiji la New York na Medellín Cartel ya Pablo Escobar wakapewa Florida na Miami. Jiji la Los Angels likaachwa kama sehemu huru ambayo yeyote anaweza kufanya biashara.
Kwa pamoja wakasonga na biashara ikashamiri.
Rafiki yako anapotishia maslahi yako: Vita Kuu ya Kwanza (Pablo Escobar VS Cali Cartel).
Biashara ya madawa ya kulevya katika America ya Kusini na duniani kote kwa miaka yote imetawaliwa na vita kati ya magenge yanayopambana ili kumiliki na kujipatia ushawishi zaidi katika soko. Lakini katika historia hakuna vita ya magenge ya mihadarati iliyotisha na kuitikisa Marekani na Amerika ya Kusini kama vita kati Medellín Cartel ya Pablo Escobar dhidi ya Cali Cartel.
Vita hii ilitishia hata usalama wa uwepo wa Taifa la Colombia na kuleta aibu kubwa kwa serikali za Colombia na Marekani.
Lakini kabla sijaeleza chochote kuhusu vita hii, nieleze kwa ufupi tu kuhusu Cali Cartel.
The Cali Cartel
Cali Catel ilianzishwa mwishoni mwa miaka ya 1970 kikiwa kama kikundi maalumu cha wapiganaji kilichokuwa kinatumiwa na Pablo Escobar na kilijulikana kama Las Chemas.
Moja wapo ya kazi walizozifanya kwa mafanikio ilikuwa ni utekaji wa raia wawili wa nchi wa uswisi na wakalipwa kiasi cha dola laki saba.
Baada ya malipo haya washirika wa kikundi cha Las Chemas wakajitenga na Pablo Escobar na kukimbilia kusini mwa nchi ya Colombia katika mji wa Cali na wakatumia fedha hiyo kuanzisha biashara yao ya mihadarati na wakafahamika kama The Cali Cartel.
Baada ya biashara yao kuanza kukua wakafanikiwa kuwashawishi wanajeshi kadhaa waasi na kujiunga nao katika biashara na wakafanikiwa kuwapata wengi.

Uwepo wa wanajeshi katika Cali Cartel unadhihirishwa na mfumo wao wa kibiashara pamoja na uwezo wao wa kufanya upelelezi na ushushushu (counterintelligence).
Kwa mfano mfumo wao wa kibiashara ulikuwa tofauti na Medellín Cartel ya Pablo Escobar ambayo yenyewe ilikuwa ni genge linalomilikiwa na mtu mmoja (Pablo) ambapo Cali Cartel wenyewe walikuwa ni muunganiko wa wafanyabiashara wanaojitegemea wanaounda genge/mtandao mmoja wa mihadarati (Cali Cartel).
Kwa upande wa ushushushu na upelelezi walikuwa mahili kiasi kwamba katika baadhi ya ripoti za CIA walikuwa wanawaita kwa jina la utani "Cali the KGB", wakiwafananisha na shirika la upelelezi la Urusi ya kipindi hicho.
Turejee kwenye...'Vita Kuu'
Ushindani mkubwa wa kibiashara kati ya magenge haya mawili unaweza kuwa sababu kubwa ya wao kuingia vitani lakini hii iliepushwa kutokana na vikao vya makubaliano walivyokaa awalinkuhusu kugawana soko.
Sababu kubwa zaidi na ya msingi iliyochochea vita hii ilikuwa ni Pablo kuamua kuacha kuheshimu makubaliano akiyoingia na Cali Cartel kutokana na genge hili kujihusisha na vitendo ambavyo Pablo alivipinga kwa nguvu zote.
Haijulikani ni kichaa gani kiliwapata viongozi wa ngazi za juu wa Cali Cartel lakini ilipofika miaka ya kati kati ya 1980 Cali Carteli wakaanza kujihusisha na imani zenye utata za "Kusafisha Kizazi/jamii" (Social Cleansing). Cali Cartel walisimamia mauaji ya mamia ya watu kwenye mji wa Cali pasipo sababu ya msingi wakidai kuwa watu hao wanaichafua Cali.

Mauaji yao yaliwalenga walemavu, machangudoa, watu wanajihusisha na mapenzi ya jinsia moja, watoto wa mitaani, na watu wasio kuwa na makazi.
Baada ya kuwaua waliwaandika maandishi kifuania "Cali limpia, Cali linda" (Clean Cali, beautiful Cali (Cali nadhifu, Cali inayopendeza)
Vitendo hivi vilimkera Pablo na ikampa sababu ya kutokuheshimu makubaliano yake na Cali Cartel kuhusu kugawana soko na akaamuru watu wake wafanye biashara nchini marekani katika mji wowote ule wanaojisikia.
Kitu hiki kikiwakera viongozi wa Cali Cartel na ili kumuonyesha kuwa wamechukizwa wakaanza kutoa ufadhili kwa kikundi cha wapiganaji kilichokuwa kinajiita Los Pepes amacho ni kifupi cha Los Perseguidos por Pablo Escobar (People Persecuted by Pablo Escobar (watu walioumizwa na Pablo Escobar)).
Kikundi hiki kilikuwa kinaundwa na ndugu za watu waliouawa na Pablo au Wapambe wake na walikuwa wamejiapiza kumsaka na kumuua Pablo popote alipo. Kitendo cha mabosi wa Cali Cartel kuanza kukipa ufadhili kikundi hiki kilichochea moto wa vita ya magenge amabao haukuwahi kuonekana hapo kabla.
Katika kipindi hiki Colombia ilishuhudia mauaji ya kutisha ambapo wafuasi wa magenge yote mawili walikuwa wakitafutana usiku na mchana. Mauaji haya yaliwahusu mpaka marafiki, ndugu na wanafamilia wa makundi yote mawili. Katika mwaka 1988 pekee idadi ya vifo ilifikia zaidi ya watu 21,000 na mwaka 1989 idadi iliongezeka mpaka vifo zaidi ya 28,000.

Hiki kilikuwa ni moja ya vipindi vigumu zaidi kiusalama kwa Pablo kwani alikuwa na lundo la maadui waliokuwa wakimtafuta. Kulikuwa na serikali ya marekani inamtafuta, serikali ya Colombia inamtafuta, Kikundi cha Los Pepes kinamtafuta, na genge la Cali Cartel linamtafuta. Kutokana na suala la usalama kuwa tete mno ilimlazimu aame kutoka katika 'pepo' yake ya Hacienda Napolés na kwenda kujificha katika nyumba za maficho juu ya milima ya mji wa Madellín.
Ilikuwa inambidi abadili makazi mpaka mara nne kwa siku moja. Nyumba zake nyingi hizi za juu ya milima alikuwa anazitumia kuhifadhi pesa na silaha na ilitokea siku walienda kwenye nyumba yake iliyopo karibia kabisa na kilele cha mlima na ilikuwa iko ndani ya msitu mnene.
Siku hii kulikuwa na baridi lisilomithirika na kutokana na nyumba hii kujengwa maalumu kwa ajili ya kuhifadhi fedha na silaha haikuwa na mfumo wa joto wala umeme. Ilifikia kipindi cha usiku baridi lilizidi na kupitiliza kiwangi cha kawaida mpaka ikaanza kutishia afya ya mtoto wake wa kike aliyekuwa naye pamoja na familia yake.

Kutokana na kutokuwepo na namna nyingine yeyote ya kupasha moto nyumba hiyo ili kupunguza baridi, ili mbidi Pablo achome moto maburungutu ya fedha usiku kucha ili kuipatia joto familia yake na hasa mtoto wake wa kike ambaye alionekana kuathiriwa zaidi na baridi. Mpaka asubuhi kunakucha na baridi kupungua kufikia kiwango cha kawaida Pablo alikuwa ameteketeza maburungutu ya hela ya kiasi cha dola milioni mbili za kimarekani.
Baada ya Juhudi za Cali Cartel kumpata Pablo kutozaa matunda, walitoa kandarasi kwa Jorge Selcado ambaye alikuwa ni muhandisi na Mwanajeshi. Jorge alikuwa maarufu kwa kuandaa timu maalumu za mauaji ya kuratibiwa kiumakini (assassination teams) na mara zote mipango yake inakuwa ya mafanikio.

Baada ya Jorge kupewa 'ofa' hii na mabosi wa Cali Cartel aliwasiliana na watu wake ambao walikuwa ni wanajeshi wa kukodi (mercenaries) kutoka nchini uingereza ambao walikuwa wamewahi kutumikia katika jeshi la Uingereza kitengo maalumu cha Anga (SAS - Special Air Services).
Timu hii ilikuwa na watu kumi mbili na iliwasili Colombia na kufanya mazoezi kwa miezi kadhaa ili kujiandaa na zoezi lililopo mbele yao. Walifahamu kuwa kwa kipindi hicho Pablo alikuwa amejificha mahali kusiko julikana kwenye milima, hivyo walisubiri wapate taarifa kuwa amerejea kwenye 'pepo' yake ya Hacienda ili wafanye shambulio la kushitukiza.
Siku hiyo haikuchelewa sana kwani timu ya Mpira ambayo Pablo alikuwa anaishabikia na kuifadhili ilifanikiwa kuchukua ubingwa wa ligi kuu ya Colombia. Hivyo Pablo alirejea jijini Medellín ili ajumuike kusherehekea ushindi huo.
Kikosi hiki kilichotumwa kumuua Pablo walijiandaa na Chopa mbili za kivita zilizobeba silaha nzito na mpango wao ulikuwa wamshitukize Pablo nyakati za asubuhi na kufanya shambulizi nyumbani kwake Hacienda Napolés.
Ili mpango huu uwe na ufanisi walikubaliana kuwa washambulie kutokea nyuma ya milima na chopa ziruke katika mfumo maalumu wa kijeshi wa usawa wa chini chini kabisa (nap-to-earth) ili wasiweze kuonekana kutokea mbali.
Keshi yake chopa ziliruka kuelekea Hacienda Napolés kama walivyopanga wapitie nyuma ya milima huku zikiruka chini chini, lakini wakiwa kwenye milima hiyo kwa bahati mbaya chopa moja ilimshinda rubani kutokana na kuruka chini chini na ikagonga kwenye mlima na kudondoka.
Zoezi ambalo kilipangwa kuwa la kwenda kushambulia na kumuua Pablo likageka kuwa ni zoezi la uokoaji na mpango huu ukaishia hapo hapo.



Zoezi ambalo kilipangwa kuwa la kwenda kushambulia na kumuua Pablo likageka kuwa ni zoezi la uokoaji na mpango huu ukaishia hapo hapo.
Baada ya kufeli kwa zoezi hili serikali ya Colombia iliwasiliana na Pablo kujaribu kumuomba ajisalimishe.
Waliharibu kumbembeleza kwa kila namna ambayo waliweza na kumuahidi watakubaliana na masharti yoyote atakayoyasema. Serikali ilifikia kipindi walikuwa 'desperate' kutokana na aibu waliyokuwa wanaipata kimataifa kwa kushindwa kumdhibiti muhalifu mmoja aliyeifanya nchi yao ya Colombia mpaka kubatizwa jina la 'Capital of death' (mji wa kifo). Hivyo matamanio yao ilikuwa tu kuutangazia ulimwengu kuwa wamemkamata Pablo.
Baada ya Pablo kutafakari kwa kina na kuona jinsi usalama wake na familia yake kuwa ni mdogo kutokana na maadui wanaomzunguka kila kona akakubali ombi la serikali kujisalimisha lakini akawapa masharti matatu.

Moja, kipindi hicho serikali ilikuwa imefanya mchakato na kubadili kifungu cha katiba kuruhusu kukabithi raia wake kwa nchi za kigeni (extradition). Pablo akawaeleza waitishe kikao maalumu cha Bunge na kurudisha kifungu cha zamani kinachokataza raia wa nchi hiyo kukabidhiwa kwa nchi za kigeni. Serikali ikakubaliana na sharti hili. Kikaitishwa kikao maalumu cha bunge na kifungu hicho cha katiba kikarejebishwa.
Pili, Pablo aliwapa sharti kuwa anataka atengenezewe gereza maalumu katika sehemu atakayoichagua yeye na yeye na wahandisi wake ndio watakaochora michoro ya namna gereza hilo anavyotaka liwe. Serikali wakakubaliana na sharti hili na gereza kikajengwa kama ambavyo Pablo aliamuru.
(Tafadhali rejea aya ya kwanza ya makala hii kuhusu namna ambavyo gereza hili likikuwa tofauti na gereza lingine lolote duniani).
Gereza hili lilipo malizika Pablo mwenyewe alilipa jina La Catedral (The Cathedral) lakini watu wengi walilipa jina la utani 'Club Escobar' na wengine waliliita 'Hotel Cathedral'.
Sharti la tatu aliwaambia serikali yeye ndiye atakaye chagua askari wa kumlinda. Serikali ikakubali pia sharti hili.
Baada ya masharti yote kukamilika yakafanyika makubakiano maalumu ya kisheria ambapo Pablo Escobar licha ya uhalifu wa kutisha alioufanya kwa miaka karibia ishirini alipewa adhabu ya kifungo cha miaka mitano pekee.
Baada ya makubaliano. Pablo alijisalimisha na kupelekwa kwenye makazi yake mapya, gereza la La Catedral.

Baada ya Pablo kujisalimisha mwaka 1991 serikali ilitangazia ulimwengu kwa mbwembwe zote kuwa wamemkamata Pablo Escobar na amehifadhiwa katiba gereza la siri.
Ikikuwa ni kweli kuwa Pablo alikuwa gerezani lakini ulimwengu mzima walifichwa ukweli halisi kwani katika gereza hilo Pablo aliishi kama mfalme na aliendelea kutoa maagizo kwa wafuasi wake na kuendesha biashara yake ya miahadarati akiwa ndani ya La Catedral. Tena kwa sasa Pablo inawezekana alifurahi zaidi kwani alikuwa uhakika wa usalama wake kutokana na kulindwa na jeshi la serikali ambao wao walimuona kama mfungwa huku yeye akiwaona kama walinzi wake binafsi.
Kitendo hiki kiliwaumiza sana Cali Cartel ambao walihangaika usiku na mchana wafahamu hili gereza lilipo. Baada ya mwaka mkoja wakapata taarifa kuhusu mahala ambapo gereza anahifadhiwa Pablo. Kutokana na ulinzi mkali wa kijeshi waling'amua fika kuwa hawataweza kuvamia gereza hilo na kumuua Pablo hivyo mshauri wao wa masuala ya kijeshi akawashauri Jorge Selcado akawashauri kuwa namna pekee ya kumuua Pablo ndani ya La Cathedral ni kulipua gereza hilo kwa mabomu mazito kwa kutumia ndege maalumu ya kivita.

Cali Cartel wakanunua ndege ya kivita aina ya A-37 Dragonfly na wakaweza kupata dili la magendo kuuziwa mabomu mazito ya kivita ya uzito wa paundi 500 kutoka kwa generali wa jeshi ka El Salvador.
Hivyo Jorge akarusha ndege na kuelekea El Salvador katika uwanja wa ndege wa kiraia asubuhi alfajiri ili kuchukua mabomu.
Kwa bahati mbaya mabomu hayo yalikuwa kwenye maboksi makubwa manne na ndege aliyoenda nayo Jorge ilikuwa ndogo isingeweza kubeba maboksi yote hayo. Wakahangaika kunga'aniza maboksi yaenee ndani ya ndege lakini maboksi matatu pekee ndiyo yalienea. Zoezi hilo la magendo lililopaswa kuchukua dakika chache tu likatumia zaidi ya dakika ishirini ambapo palianza kupambazuka na watu kufika uwanjani hivyo ikambidi Jorge aruke na maboksi matatu na kulitelekeza boksi moja uwanjani hapo.
Baada ya raia kushikwa na butwaa kuhusu walichokiona hatimae polisi walifika na baada ya masaa machache walipewa taarifa za siri kuhusu mpango huo wa Cali Cartel kununua mabomu hayo ili kulipua La Catedral. Skandali hii iliteka vyombo vya habari siku hiyo na ikapekekea Cali Cartel kuachana na mpango huo wa kulipua La Catedral waliamini kuwa taarifa hiyo itakuwa imemfikia Escobar na ameshachukua tahadhali.

KIFO CHA PABLO El Mágico

Licha ya serikali kufahamu kuwa Pablo alikuwa anaendelea na biashara zake licha ya kuwa ndani ya gereza serikali ilifumfumbia macho kadiri ambavyo ulimwengu ulivyo amini kuwa Pablo Escobar yuko gerezani anajutia.
Lakini uvumilivu huu uliisha mara baada ya kuzuka skendali katika vyombo vya habari kwamba Pablo aliwaita marafiki zake wa kibiashara wanne walioko uraiani waende akawape maelekezo, walipofika huko aliamuru walinzi wanaomlinda wawapigwe risasi marafiki zake hao kwa madai kuwa wamemdhulumu hela na ilisemekana miili yao ilifukiwa ndani ya gereza.
Skandali hii ilikuwa kubwa kiasi kwamba ilitishia kurudisha tena upya zama za serikali kuumiza kichwa kuhusu Pablo. Ili kuepusha mambo yasiharibike kabisa serikali ikaamua kuwa Pablo inabidi afungwe kwenye gereza maalumu la kijeshi na aishi maisha ya kifungwa kama mfungwa mwingine yeyote.
Kutikana ma makubaliano kuwa polisi wengine isipokuwa wanajeshi wanaomlinda hawaruhusiwi kusogea hata maili 12 karibu na La Catedral, hivyo serikali ikatuma waziri muandamizi na maafisa wengine watatu wa ngazi za juu serikalini kumpelekea taarifa hiyo Pablo kuwa anaamishwa gereza.

Baada ya kupewa taarifa hii Pablo akiwageuzia kibao na kuamuru wanajeshi wanaomlinda waweke chini ya ulinzi vuongozi hao wa serikali. (Kumbuka wanajeshi hawa wanaomlinda aliwachagua yeye hivyo ni dhahiri walikuwa maswahiba wake wakikuwa tayari kumtii Pablo kuliko rais wa nchi)
Baada ya taarifa kufika serikalini kuwa Pablo amewaweka chini ya ulinzi viongozi wa serikali waliotumwa kufanya nae mazungumzo juu kuhamishwa gereza. Serikali ikatuma kikosi cha wanajeshi 600 kulizunguka gereza hilo na kumtaka Pablo ajisalimishe.
Pablo akawajibu kuwa wakithubutu hata kukanyaga hatua moja ndani ya uzio wa La Catedral basi ataamuru viongozi hao aliowashikilia mateka wapigwe risasi.
Mabishano haya yalidumu kwa takribani masaa kumi mpaka ambapo giza lilipoingia kikosi cha wanajeshi waliokuwa wamelizunguka gereza walivamia ndani ya La Catedral lakini jambo la ajabu waliwakuta viongozi hao wa serikali wamefugwa kwenye viti na kuzibwa midomo lakini walikuwa salama salimini ila Pablo na wapambe wake hawakuwepo. Na watu waliokutwa ndani ya La Catedral walidai Pablo na wapambe wake hajaonekana/ameondoka kwa taribani masaa manne yaliyopiata.

Ni kwa jinsi gani Pablo aliwatoroka wanajeshi amabo walikuwa wamelizunguka gereza kila kona kitendawili hiki mpaka leo hakuna aliyekitegea. Hakukuwa na njia yoyote ya chini kwa chini wala handaki, hivyo huu utata wa jinsi alivyowatoroka haujapata jibu la kuridhisha mpaka leo.
Kufumba na kufumbua jinamizi la aibu kwa serikali ya Colombia na Marekani kilikuwa limerudi. Na serikali zote mbili ziliapa kwamba sasa imetosha ni lazima walizike jinamizi hili.
Kamandi ya Oparesheni maalumu za kijeshi za marekani (Joint Special Operations Command) kikaunda kikosi kazi maalumu cha kijeshi kilichoelekea nchini Colombia kuungana na kikosi maalumu cha jeshi la Colombia kikichoundwa maakumu kwa ajili ya kumsaka Pablo kilichoitwa 'Search Block' na kwa pamoja wakaanza msako mkali wa kumtafuta Pablo. Pia walishirikiana na kikundi cha Los Pepes kilichoapa kumteketeza Pablo na ukoo wake wote ambao walitumia mwanya wa msako huu kuua watu 300 waliokuwa na uhusiano na Pablo, yaani ndugu zake, marafiki na wafanyabiashara wenza.

Baada ya mwaka mzima wa msako mkali hatimae siku ya desemba 2, 1993 jeshi la Colombia lilifanikiwa kunasa mawasiliano ya simu kati ya Pablo na wasaidizi wake. Wakatumia 'triangulation technology' kung'amua mahali alipo ambapo alikuwa katika mtaa wa Los Olivos katika mji wa Madellín. Baada ya kufanikiwa kufahamu nyumba aliyojihifadhi pasipo kupoteza mda wakafanya shambulio la kushitukiza.
Wakati wanawafanyia shambulio hili la kushitukiza Pablo alikuwa yupo na mlinzi wake binafsi mmoja tu Alvaro de Jesús.
Baada ya kuanza kushambuliwa nao wakarudisha mashambulio ya risasi kwa vikosi vya jeshi la serikali. Majibizano haya ya risadi yalidumu kwa dakika kadhaa ndipo Pablo na mlinzi wake wakakubali kuwa hakuna namna wao watu wawili wataweza kuwashinda kikosi kizima cha kijeshi chenye silaha nzito. Hivyo wakaamua warushe risasi huku wakiwa wanakinbilia juu ya paa la nyumba. Lakini kabla hawajafika juu kabisa ya paa la nyumba mlinzi wa Pablo alidunguliwa na risasi na kufariki papo hapo na Pablo mwenyewe alipigwa risasi mguuni na akajikongoja mpaka juu ya paa.
Baada ya wanajeshi wa serikali kuvamia nyumba na kufika juu ya paa walimkuta Pablo amelala chini amefariki akiwa na tundu la risasi aliyopigwa kwenye sikio kwenda ndani ya kichwa.

Haijulikani ni nani alimpiga hii risasi lakini marafiki zake wa karibu pamoja na kaka yake wa kuzaliwa wanasema kwamba siku zote Pablo akikuwa anasema kuwa hatokubali kupigwa risasi ya mwisho na adui yake. Kama ikitokea ameshambukiwa na adui na hana namna ya kujiokoa basi atajipiga risasi sikioni itokee upande wa pili. Serikali haijawahi kupinga au kuthibitisha suala hili la Pablo kujipiga risasi mwenyewe lakini huo ndio ulikuwa mwisho wa Pablo juu ya uso wa dunia.
Mpaka leo hii nchini Colombia hasa katika mji wa Madellín kila mwaka wanafanya kumbu kumbu ya kifo cha Pablo kama shujaa wao lakini kwa watu wengi duniani Pablo amebakia kama muhalifu aliyeitesa na kuisumbua dunia kadiri atakavyo.
Binafsi nadhani namna nzuri ya kumkumbuka Pablo ni sentesi moja maridhawa iliyotolewa na Virginia Vallejo aliposema; Amando a Pablo, Odiando a Escobar.! Akimaanisha kuwa lazima kuna upande fulani wa nafsi yako utampenda Pablo kama mtu mwenyenye jitihada, umahiri na uthubutu lakini upande wa pili wa nafsi lazima utamchukia Escobar kutokana na uhalifu wake.
Lakini kwa namna yeyote ile historia ya Dunia itaendelea kumkumbuka Pablo kama binadamu aliyeufinyanga ulimwengu wa siri na hatari wa biashara haramu na kuufanya uwe jinsi ulivyo leo hii. Vizazi vyote vijavyo vitaendelea kusimulia historia ya kusisimua ya Pablo El Mágico. Pablo El Zar de la Cocaína. Pablo Emilio Escobar

Siri ya Herufi ya Mwanzo ya Jina Lako

$
0
0

HERUFI A
Mwenye jina linaloanziana na herufi A ni mtu anayependa mambo makubwa, anajiamini na mwenye uwezo wa kutimiza malengo yake. Ni mtu mwenye tahadhari, mchangamfu na mpenda matukio. Anapenda Kuheshimiwa, anapenda Mamlaka, na ana kiburi, na hasira.

HERUFI B
wenye jina linaloanziana na herufi B ni mtu, mkarimu, muaminifu, na hupenda kazi. Ni Jasiri, shujaa na mkatili katika vita au pale anapotaka kulinda vilivyo katika himaya yake.

HERUFI C
Mwenye jina linaloanziana na herufi C ni mtu wa kukubadilika badilika, mshindani na hupenda kupigania malengo yao wanayopenda. Ni watu wa wabunifu na wanaopenda mawasiliano.

HERUFI D
Mwenye jina linaloanziana na herufi D ni mtu anayependa usawa, Biashara. Ni watu wanaopenda kuamrisha na mwenye kupenda usafi. Ni jeuri na wenye msimamo.

HERUFI E
Mwenye jina linaloanzia na herufi E ni mtu mwenye roho nzuri ,yenye mapenzi na huruma. mwenye kupenda uhuru katika mapenzi na mchangamfu. Kinyume na hivyo atakuwa ni mtu asiotegemewa na kigeugeu.

HERUFI F
Mwenye jina linaloanzia na herufi F ni mtu mwenye mapenzi,huruma , roho nzuri na ana uwezo wa kuwafariji watu. Ni mtetezi wa watu na mwenye huzuni lakini ni mzito wa kufanya maamuzi.

HERUFI G
mwenye jina linaloanzia na herufi G ni mtu mwenye mwenye imani ya kidini na nguvu za kiroho. Ana kipaji cha kubuni na uwezo wa kutatua matatizo ya watu. ni mtu mwenye hisia kali,msomi, mpweke na mkaidi wa kukubali ushauri wa kutoka kwa watu.

HERUFI H
Mwenye jina linaloanzia na herufi H ni mtu mwenye ubunifu na nguvu katika biashara, hupata faida kubwa kutokana na jitihada na bidii zake. ni mwenye mawazo mengi, mchoyo na mbinafsi.

HERUFI I
Mwenye jina linaloanzia na herufi I ni mtu mwenye kupenda sheria, ana huruma na utu. Wakati mwingi hajiamini na ni mwenye hasira za haraka.

HERUFI J
Mwenye jina linaloanzia na herufi J ni mtu mwenye matamanio,mkweli, mkarimu na muerevu. asiyekubali kushindwa na hupata mafanikio makubwa. Wakati mwingine anakuwa ni mtu mvivu na aliyekosa mwelekeo.

HERUFI K
Mwenye jina linaloanzia na herufi K ni mtu mwenye jeuri. mwenye msimamo thabiti,mashuhuri na mwenye uwezo wa kushawishi na kuamsha hisia za watu wana uwezo wa utambuzi ambao watu wengi hawana. ni mtu asioridhika na hali ya kimaisha.

HERUFI L
Mwenye jina linaloanzia na herufi L ni mtu wa vitendo, mwenye hisani na aliyejipanga vizuri kimaisha. Huwa wanapata ajali mara kwa mara.

HERUFI M
Mwenye jina linaloanzia na herufi M ni mtu mwenye kujiamini sana, mchapakazi na hupata mafanikio. ni mtu mropokaji,mwenye haraka na mwepesi kukasirika.

HERUFI N
Mwenye jina linaloanzia na herufi N ni mtu mwenye ubunifu, hisia kali na hupenda kuwasiliana lakini ana wivu sana.

HERUFI O
Mwenye jina linaloanzia na herufi O ni mtu mwenye subra, mvumilivu na mwenye bidii ya kusoma. Ni mtu mwenye kupenda kutumikia jamii na mwenye uwezo mkubwa wa kudhibiti hisia.

HERUFI P
Mwenye jina linaloanzia na herufi P ni mtu mwenye uwezo wa kuamrisha na hekima kubwa. Ana nguvu za kiroho lakini anapenda sana kujitumbukiza kwenye mambo ya watu.

HERUFI Q
Mwenye jina linaloanzia na herufi Q ni mtu mwenye kupenda mambo ya asili. Ni watu wasiyoelezeka nawana uwezo wa kuonyesha vitu visivyojulikana hata hivyo ni mtu aliyepooza sana.

HERUFI R
Mwenye jina linaloanzia na herufi R ni mtu mwenye uvumilivu, wenye huruma lakini ana hasira za haraka. Muda wote anakuwa mpenda amani.

HERUFI S
Mwenye jina linaloanzia na herufi S ni mtu mwenye mvuto mkali wa kuleta utajiri. Ni watu wenye maamuzi ya ghafla na hupenda mageuzi makubwa.

HERUFI T
Mwenye jina linaloanzia na herufi T ni mtu mwenye kupenda ushauri wa kiroho, anatumia nguvu za ziada kusaidia watu na hupata mafanikio baada ya muda mrefu. Ni watu wenye hisia kali sana na ni wepesi kushawishika.

HERUFI U
Mwenye jina linaloanzia na herufi U ni mtu mwenye bahati kubwa kwa ujumla. Anapenda uhuru katika mapenzi. Lakini ni mtu mbinafsi, mwenye tamaa na aliyekosa maamuzi.

HERUFI V
Mwenye jina linaloanzia na herufi V ni mtu Mchapakazi, wenye bidii na asie choka. Hata hivyo ni watu wasiotabirika.

HERUFI W
Mwenye jina linaloanzia na herufi W ni mtu muwazi, wachangamfuu kupita kiasi na mwenye uwezo wa kutambua mtu mwema na mbaya. Ni watu wenye tamaa na hufanya mambo ya hatari.

HERUFI X
Mwenye jina linaloanzia na herufi X ni mtu asiyependa kuwekewa vizuizi katika kwenye anasa na ni rahisi kujiingiza kwenye uzinzi na kujitoa uaminifu.

HERUFI Y
Mwenye jina linaloanzia na herufi Y ni mtu mwenye kupenda Uhuru na hawapendi kupingwa jambo lao lolote. Ni watu wanaokosa uamuzi na husababishia kupoteza bahati katika maisha.

HERUFI Z
Mwenye jina linaloanzia na herufi Z ni mtu mwenye kupenda matumaini na amani. Ni wenye msimamo mkali ila wanashauriwa kufikiria kabla ya kuamua jambo,
je na jina lako lina maana gani? Jibu usione aibu!Sambazaaa hii
Usisahau Ku #LIKE_PAGE

Simon Msuva Amlilia Niyonzima

$
0
0

Mshambuliaji wa Yanga SC Simon Msuva amesema japo kiungo Haruna Niyonzima ameacha pengo ndani ya timu, wachezaji waliobaki wataendelea kuipigana kwa juhudi ili kuziba huku mashabiki wakiamini hakuna pengo linaloonekana.

Msuva amesema, kuondoka kwa Haruna kumemuachia pengo kubwa ndani ya Yanga kutokana na ushirikiano waliokuwa nao ndani na nje ya Timu lakini atajitahidi kuendeleza ushirikiano na wachezaji waliobakia ili kuhakikisha timu inaendelea kufanya vizuri.

“Katika timu lazima kuwe na mazoea, mimi Haruna nilimzoea kupitiliza na hii habari kuwa amesaini Simba SC mimi sifahamu lakini kwaupande wangu kama amesaini kweli mimi nimeumia lakini ni maisha yake yeye na familia yake lakini mimi kwa upande wangu nitajitahidi kwa sababu kuna watu wengine nipo nao pale kama wa kina Kamusoko wapo wengi tu, kwahiyo nitashirikiana nao kama nilivyoshirikiana na Haruna lakini kwaupande wangu imeniuma, ” amesema Msuva.

Msuva amesema, atamkumbuka Haruna hususani ndani ya uwanja kwani walishirikiana kwa kiasi kikubwa kuhakikisha wanaipa timu ubingwa misimu mitatu mfululizo.

“Haruna nitakumbuka vitu vingikutoka kwake kwani licha ya Uwanjani pia ni mtani wangu na hata yeye huko alipo anajua kabisa ameniacha mchezaji mwenzake sina raha kwani tumekuwa na ushirikiano mkubwa ndani ya timu hususani katika suala la ushauri, ni mchezaji wa kimataifa ambaye na mkubali katika soka, ” Msuva aliongeza.

Hivi Ndivyo Rais Magufuli Alivyotengua Kauli ya Waziri Wake Ummy Mwalimu....

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli amesema kuwa chini ya utawala wake, haitotokea mwanafunzi aliyepata mimba akaruhusiwa kurudi shuleni kuendelea na masomo baada ya kujifungua.

Rais Magufuli amesema kuwa kwa kufanya hivyo itapelekea wanafunzi wengi kupata mimba wakiwa bado wapo shuleni kwa sababu wanajua wataruhusiwa kuendelea na masomo kitu ambacho yeye hawezi kukivumilia.

Rais Magufuli ameyasema hayo leo alipokuwa akifungua barabara ya Bagamoyo – Msata yenye urefu wa kilomita 64 ambayo itasaidia kupunguza msongamano wa magari katika barabara ya Morogoro kwani ndiyo pekee iliyokuwa ikitumika kuingia na kutoka jijini Dar es Salaam.

Kwa kauli hiyo ya Rais Magufuli, ni dhahiri kuwa ametengua kauli iliyokuwa imetolewa na Waziri wa Afya, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu Aprili 27 mwaka huu ambapo alisema kuwa, mwanafunzi hawezi kunyimwa haki yake ya elimu kwa vile tu amepata mimba akiwa shule.

Waziri Ummy Mwalimu alisisitiza kuwa wanafunzi wa kike wanaopata mimba wakiwa mashuleni waendelee na masomo yao ili kufikia malengo walioyanayo nchini.

Aliyasema hayo wakati wa ufunguzi wa mkutano wa kwanza wa maswala ya kijinsia ulioandiliwa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Kitivo cha Ualimu (DUCE) alipomuwakilisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.

“Tunapokataza watoto wa kike wasiendelee na masomo pindi wanapopata ujauzito wakiwa mashuleni tunawaadhibu watoto wa masikini washindwe kutimiza malengo yao kwa wakati waliotarajia,” alisema Waziri Ummy.

Aidha, Rais Dkt Magufuli amezita Asasi za Kiraia (NGOs) zinazotaka wanafunzi wenye watoto waendelee na masomo, zijenge shule zao za kuwapeleka hao watoto lakini serikali yake haiwezi kutoa fedha kwa ajili ya elimu bure halafu mwanafunzi apate mimba bado serikali hiyo hiyo ichukue jukumu la kumsomesha mzazi.

Katika kutoa mbadala wa hilo, Rais Magufuli amesema wanafunzi hao wanaweza kujiunga na vyuo vya ufundi pindi wanapopata ujauzito ambapo vyuo hivyo vitawakubali lakini sio kuendelea na masomo tena.

Akizungumzia upande wa wanaowapa wanafunzi mimba, Rais Magufuli alisema kuwa sheria ipo wazi kwamba ni miaka 30.

Kauli hii ya kiongozi wa nchi imepokelewa kwa mtanzamo tofauti ndani na nje ya nchi, ambapo baadhi wamemuunga mkono kuwa wanafunzi wakijifungua wasirudi shule huku wengine, hasa wale watetezi wa haki za wanawake wakipinga kauli hiyo na kusema, huko ni kuwabagua baadhi ya watu kupata haki yao ya msingi.

Asikudanganye Mtu..Hawa NDIO Mashujaa wa Kweli Waliokuwa Nyuma ya Vita vya ESCROW

$
0
0


HAWA ndio vinara wa kupinga malipo ya zaidi ya Sh bilioni 300 zilizolipwa kwa Kampuni ya kufua umeme ya Independent Power Limited (IPTL) kwa kuhakikisha hoja hiyo inasimamiwa imara na Bunge ili kupinga malipo hayo ya fedha.

Viongozi hao waliosimama na kupinga malipo hayo ni aliyekuwa Mkurungezi wa Takukuru, Dk. Edward Hoseah, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh, aliyekuwa Kamishna wa TRA, Rished Bade, Spika Mstaafu wa Bunge la 10, Anne Makinda na Spika wa sasa Job Ndugai ambao kila mmoja alitumia nafasi yake kuhakikisha suala hilo linafika bungeni na wahusika wanachukuliwa hatua

 Kusimama kwao imara kumekuja siku chache baada ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (Takukuru), kuwafikisha mahakamani vinara wawili wa sakata hilo kuwaburuza mahakamani, Mwenyekiti wa Mtendaji IPTL/Pan Africa Power (PAP), Harbinder Sethi Singh na mwenzake wa Kampuni ya VIP Engineering and Marketing Ltd,  James Rugemalira.
Vigogo hao hao walifikishwa   katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam Juni 19, mwaka huu na kusomewa mashtaka sita yakiwamo ya uhujumu uchumi.

Watuhumiwa hao pia wanadaiwa kula njama, kughushi, kujihusisha na mtandao wa uhalifu, kutoa nyaraka za kughushi, kujipatia fedha kwa udanganyifu na kuisababisha Serikali hasara ya Dola za Marekani 22,198,544.60  (Sh bilioni 309.5).

Washtakiwa hao walisomewa mashtaka yao na Mwendesha Mashtaka, Wakili wa Serikali, Paul Kadushi mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi na kupelekwa rumande hadi Julai 3 kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza wala kutoa dhamana kwa kesi ya uhujumu uchumi.

Inadaiwa kuwa kati ya Oktoba 18, mwaka 2011 na Machi 19, 2014 jijini Dar es Salaam, watuhumiwa walikula njama katika nchi za Afrika Kusini, Kenya na India ya kujipatia fedha kwa udanganyifu.

VINARA

Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe (ACT-Wazalendo), amewataja vinara waliofanikisha vita dhidi ya uchotwaji wa fedha hizo kutoka katika akaunti ya Tegeta Escrow.

Akaunti hiyo ilifunguliwa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ili kuhifadhi fedha za malipo ya tozo ya ufuaji wa umeme baada ya Tanesco kuingia kwenye mgogoro na IPTL kuhusu kiwango kinachopaswa kulipwa na baadaye suala hilo kupelekwa mahakamani.

Fedha hizo zilitakiwa zitolewe baada ya mahakama kutoa uamuzi wa mgogoro huo, lakini zilitolewa na kulipwa kwa mmiliki mpya wa Kampuni ya PAP na kusababisha kuibuka kashfa hiyo.

Baadaye ilionekana fedha hizo zikiingia katika akaunti za mawaziri, majaji, watendaji waandamizi wa Serikali, wabunge na watumishi wengine wa umma.

Kutokana na wabunge wengi kusimamia kidete suala hilo, baadaye Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema alijiuzulu huku viongozi wengine wakiwamo mawaziri nao wakiachia nafasi zao.

Awali, kabla watuhumiwa hao kufikishwa mahakamani, Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Valentino Mlowola, aliwaeleza waandishi wa habari jinsi alivyochukua muda kuchunguza suala hilo hadi kuamua kulipeleka mahakamani.

Kutokana na hali hiyo Zitto, amelazimika kuandika waraka mzito baada ya watuhumiwa hao kufikishwa mahakamani na kusema suala lao limeleta msisimko mkubwa kwa jamii.

“Navuta picha ya mahakamani, namwona pia James Rugemalira mmiliki wa hisa asilimia 30 za IPTL na aliyeuza hisa hizo kwa Sethi kwa malipo yaliyotokana na fedha zilizoporwa kutoka BoT.

“Kisaikolojia picha ile ina maana kubwa sana kwenye vita dhidi ya ufisadi nchini. Rais Magufuli amefanya jambo la kiukombozi (psychological liberation),” alisema Zitto.

 VINARA VITA YA ESCROW

Alisema ni wazi kwamba mtu kama David Kafulila (aliyekuwa Mbunge Kigoma Kusini), siku watuhumiwa hao walipofikishwa mahakamani alikuwa na furaha sana kuona matunda ya kazi yake kwa sababu alisimamia kidete sakata hilo.

Zitto ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), alisema wajumbe wote waliokuwamo katika kamati hiyo mwaka 2013-2015 wanastahili pongezi kwani wangekubali kugawanywa wangepoteza ajenda.

“Mshikamano tulioonyesha ilikuwa silaha kubwa. Wapo mashujaa ambao siwezi kutaja majina yao (Unsung Heroes), hawa ni wengi mno, wengine ni watumishi wa Bunge. Sitaki kuwataja, lakini vijana wale na mama yule chini ya Katibu wa Bunge walipata majaribu makubwa sana. Walisimama kidete,” alisema.

Katika waraka huo, pia aliwataja aliyekuwa Mkurungezi wa Takukuru, Dk. Edward Hoseah, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh na watumishi wengine wa ofisi hiyo kwa namna walivyoisaidia kamati kwa kiwango cha juu.

“Mpaka leo nikimuwaza Hoseah kwenye sakata hili kama nimevaa kofia ninaivua kwa heshima kubwa sana kwake,” alisema Zitto.

Wengine aliowapongeza ni Kamishna wa TRA, Rished Bade akisema ndiye aliyekata mzizi wa fitina kwa kuithibitishia Kamati ya PAC ushahidi nyeti kuhusu masuala ya kodi.

Alisema ushahidi huo muhimu wangeukosa, pengine wasingekuwa na taarifa hiyo.

Pia alisema Bunge lilifanya kazi yake kwa ufahari kwa kulisaidia taifa kwa kuleta maazimio yaliyolipa heshima na kwamba anajivunia kuhudumu kwenye Bunge hilo la kumi.

Aidha alimkumbuka pia Makamu Mwenyekiti wake, marehemu Deo Filkunjombe (aliyekuwa Mbunge wa Ludewa), akisema suala hilo la Escrow limemuonyesha kuwa watu wema hawafi.

“Jambo hili la Tegeta Escrow limenionyesha kuwa ‘watu wema hawafi, hata kama miili yao iko mchangani tayari (kaburini)’, na hili ndilo linalojidhihirisha kwa ndugu na rafiki yangu wa karibu mno, aliyekuwa makamu wangu wa uenyekiti wa PAC, Deo Fulikunjombe. Miaka miwili tangu afariki sasa, bado taifa linakumbushwa juu ya uzalendo wake.

“Sijui Deo angekuwa hai angekuwa katika hali gani. Ninamlilia ndugu yangu. Kitu kimoja ambacho watu wengi hawajui ni kwamba muda wote wa kuandaa taarifa maalumu ya PAC kuhusu Tegeta Escrow, yeye ndiye aliandaa ulinzi wangu kuhakikisha sidhuriwi.

“Alimwambia dada yangu aje Dodoma kuhakikisha ninakula kile tu kilichopikwa na dada yangu. Shujaa wa kazi hii ni yeye,” alisema Zitto.

Alisema funzo kubwa muhimu katika kadhia hiyo ni umuhimu wa uhuru wa kiutendaji wa taasisi mbalimbali nchini.

“Taasisi huru husaidia uwajibikaji mahali penye makosa, husaidia kufichua ufisadi na huleta uwazi. Yawezekana bila uhuru wa Takukuru, CAG, BoT, TRA, vyombo vya habari pamoja na Bunge, leo nisingekuwa nazungumza haya, ni muhimu sana tupiganie na kulinda uhuru huu wa taasisi,” alisema Zitto.

Akielezea namna walivyopambana awali, alisema alishauriana na Filikunjombe ili ukaguzi ufanywe na CAG kuhusu suala hilo.

“Baada ya siku mbili tukamwita Gavana wa BoT, Benno Ndulu mjini Dodoma. Baada ya kikao kifupi PAC ikaagiza rasmi ukaguzi maalumu kuhusu akaunti ya Tegeta Escrow. Tukaagiza taarifa iletwe bungeni na si wizarani.

“Mkakati huu ulitusaidia mno mbeleni kwani juhudi za Serikali kuzuia ukaguzi ziligonga mwamba maana mchezo wa wizara tuliushtukia na kuuzuia. PAC ilitoa taarifa kwa umma juu ya ukaguzi husika,” alisema Zitto.

Alisema katika mapambano hayo ambayo yalikuwa na vikwazo vingi, Kafulila akajitokeza kubeba jukumu la kuweka shinikizo kwa Serikali.

Mbali na hilo, alisema naye aliyekuwa Mbunge wa Simanjiro, Christopher ole Sendeka, alitoa msaada mkubwa kwa kamati na baadaye akatukanwa kuwa hakuwa msomi na kwamba kidato cha sita alipata sifuri.

“Mtindo huu wa kuvunjia watu heshima pia ulitumika dhidi yangu, kwa kutengeneza kijitabu cha propaganda kilichogawanywa kwa ustadi na mafanikio makubwa kwa kila mbunge nyumbani kwake mjini Dodoma,” alisema.

Zitto alisema baada ya kuona jamii haielewi kuhusu ufisadi huo, aliamua kutafuta fedha ili Kafulila azunguke mikoani kuwaelimisha wananchi kwa kugawa kitabu alichokiandaa kuhusu sakata hilo.

Alisema wakati huo PAP na IPTL nao waliongeza nguvu, huku sauti dhidi ya ukwapuaji ule ikiwa ni ya Kafulila na PAC tu jambo ambalo liliwafanya wavunjike moyo kwa sababu viongozi wengine wa vyama vya upinzani walikuwa kimya.

“Tulikuwa tunajiuliza nini hasa kimetokea? Tulipata nguvu ya pamoja baada ya hoja kufikishwa kwenye kamati na kwa makusudi kabisa kuvujisha baadhi ya taarifa kwenye vyombo vya habari ili kupata uungwaji mkono wa wananchi.

“Watu wa PAP/IPTL pia walikuwa na mikakati yao ya vyombo vya habari. Kwanza walicheza na taarifa ya CAG na kuisambaza kwa nguvu kabla ya taarifa rasmi kutolewa. Hawakujua kuwa sisi PAC tulikuwa na taarifa ya kwanza kabisa ya CAG ambayo ilikuwa na ukweli wote kabla ya taarifa yao iliyochezewa.

“Ndiyo maana kulikuwa na mchanganyiko mkubwa kwa umma kuhusu fedha ni za umma au si za umma, kwani ilikuwa ni mkakati maalumu wa wakwapuaji wa fedha zile,” alisema Zitto.

Alisema ili kujenga umoja ndani ya Bunge, alimwomba Spika Makinda kumwongezea wajumbe wa kamati, ombi ambalo alilikubali kwa kuwaongezea Kangi Lugola, Suleiman Zedi na Dk. Hamis Kigwangala.

Alisema wakati wakiendelea na harakati hizo, wakwapuaji hao nao walijipanga kwa kuwagawia fedha kila mbunge anayechangia.

“Sisi tuliamua kuwachezea mchezo wa kupanga wachangiaji wetu wazuri siku ya mwisho na wao wakaja kuchangia siku ya pili ya uwasilishaji wa taarifa bungeni, Filikunjombe alifanya kazi hiyo ya mkakati,” alisema Zitto.

Alisema Spika Makinda na kabla yake Naibu wake, Job Ndugai walitoa ushirikiano mkubwa.

“Ndugai alituambia wakati wa kukabidhiwa ripoti, namnukuu ‘waelezeni Watanzania ukweli. Nipo nanyi’. Kweli alikuwa nasi na ili kutupunguza nguvu akapewa safari ya ghafla kwenda Paris.

“Lakini Spika Makinda alikuwa ameelewa jambo hili vizuri sana. Alitupa mwongozo kama mzazi, kutoka mwanzo mpaka mwisho. Naushukuru sana uongozi wa Bunge.

“Pia tulijua kuwa wabunge wa CCM wakiweka msimamo wa kupinga, taarifa yetu itakwama. Siasa za kibunge uamuliwa kwa msingi wa demokrasia ya ‘wengi wape’. Wabunge wa CCM ndio wengi bungeni, ukitaka jambo lako ni lazima ujenge ushawishi kwao,” alisema.

Kutokana na ugumu wa vita hiyo, Zitto alisema ilimlazimu azungumze na aliyekuwa Katibu NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akiwa kwenye ziara mikoa ya kusini na kumwambia amwombe Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana kuwa kusiwe na msimamo wa chama chao kwenye jambo hilo kwa kuwaacha wabunge wao wawe huru kuzungumza jambo ambalo lilikubaliwa na kiongozi huyo.

“Filikunjombe akazungumza na mzee Philip Mangula (Makamu Mwenyekiti wa CCM) ambaye alikuwapo Dodoma kumwomba hivyo hivyo. Mzee Mangula alimwuliza ‘kwa nini maazimio umesoma wewe na si mwenyekiti wako? Sio mtego kuwa wewe ndio unyonge CCM wenzako?’. Bahati nzuri jambo tulilipanga vizuri kabla,” alisema Zitto.

Alisema wakati huo alikuwa kwenye ugomvi mkubwa na chama chake Chadema, hivyo ikabidi ajisogeze kwao ili taarifa isipate mkwamo.

“Hata kamati ya kuandika maazimio tukawaweka watu kama Tundu Lissu na Freeman Mbowe na upande wa CCM, Anna Kilango Malecela ambaye mwanzoni hakuwa upande wetu. Tulifanikiwa kujenga mwafaka wa kibunge,” alisema.

Pamoja na hali hiyo pia aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Kazi Maalumu), Profesa Mark Mwandosya, alipinga hatua ya fedha hizo kuitwa ni mali ya IPTL na kuhoji inakuwaje kama fedha hizo zingekuwa mali ya mtu binafsi kwa nini ilikaguliwa katika vitabu vya BoT.

Profesa Mwandosya alimpa pole Zitto kutokana na makombora alitokuwa akirushiwa huku akimtaka kutokata tamaa na asimame imara kwani Taifa litakumbuka mchango wake siku moja.

Wakati akisema hayo Lissu, alisema watu waliopewa fedha hizo ni wezi na hawastahili kutetewa kwani baada ya kuona kuna hatari ya suala lao kugeuka waliamua kugawa fedha kwa baadhi ya wabunge na watendaji wa Serikali.

Mbali na hao pia aliyekuwa Mbunge wa Nzega, Dk. Hamis Kigwangalla, alisema kuwa Profesa Muhongo, alikuwa muongo kwani imekuwa ni kawaida yake kutetea uongo mara kila wakati.

WALIOTETEA UCHOTWAJI FEDHA

Pamoja na Kamati ya PAC kuwasilisha ripoti yake juu ya suala hilo ambapo ilijiridhisha kuwa sehemu ya fedha hizo ni za Serikali, baadhi ya wabunge na mawaziri walipinga hatua hiyo na kusema kuwa fedha hizo hazikuwa za umma bali ni mali za IPTL.

Mmoja wa mawaziri waliosimama bungeni kutetea suala hilo ni aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo ambaye alizungumza kwa kujiamini kuwa fedha hizo si mali ya umma.

 LUSINDE

Mbunge wa Mtera, Livingstone Lusinde (CCM), akichangia ripoti hiyo ya PAC bungeni, alisema hata Zitto ambaye ni mwenyekiti wa kamati alipokea fedha kutoka kwa Sethi.

“Zitto ni rafiki yangu mkubwa na aliwahi kunisaidia nilipokuwa na tatizo, lakini katika hili lazima niseme kwamba ulipokea fedha kutoka kwa Sethi, atupe jibu isije kuwa tunakaa hapa kumbe walaji wako wengi. Kwa nini Tibaijuka anapopewa inakuwa fedha haramu, lakini kwa Zitto ni halali?

“Na Zitto anahusika, Kafulila naye anakuja hapa ohh eti taarifa ya siri imevuja tujadili, tujadili kwani ninyi Mungu?” alihoji Lusinde.

 MOHAMED CHOMBO

Mbunge wa Magomeni, Zanzibar, Mohamed Chombo (CCM) alisema: “Nimesikiliza ripoti ya PAC na Serikali, lakini jambo hili lipo wazi kwamba hizi fedha hazikuwa za umma, zilikuwa za IPTL zimelipwa na Tanesco.”

 RICHARD NDASA

Mbunge wa Sumve, Richard Ndassa (CCM), alisema kumezuka mtindo wa kusingiziana na kwamba wabunge wa aina wamwogope Mungu.

“Tusiwavunje moyo wizara, wamefanya kazi kubwa, tushauri pale kwenye tatizo tuseme sasa fukuza huyu halafu nini kinafuata?

“Tukiwa na utaratibu wa kufukuzana itaendelea hivyo hivyo, tumwogope Mungu, lakini nafsi zetu zitatusuta kwa sababu ya matendo yetu. Hivi sasa kamezuka mtindo wa kusingizia mtu huyu kala, huyu kapewa mtu akipewa asimame hapa aseme amepewa, lakini tusiwasingizie,” alisema Ndassa.

 MARIAM KISANGI

Mbunge wa Viti Maalumu, Mariam Kisangi (CCM), alisema upinzani baada ya kuona kwamba chama tawala kinapeta wakaamua kuwakoroga na Escrow.

“Tuangalie utendaji wa watu na ninawaambia hatoki Muhongo wala Maswi, CCM kitapita na hiyo ndiyo njama zenu upinzani kutukoroga. Mmekaa mkao na CCM inapeta, mkajisemea hawa tuwakoroge na nini ndio mkaja na Escrow mara EPA, nawaambia njama zenu hazisaidii.

“Zile fedha si za umma. Tanesco ina madeni mengi, inadaiwa Sh bilioni 700. Waziri ameeleza vizuri, kwa hiyo tusipotezeane muda hapa,” alisema mbunge huyo.

SIMBACHAWENE

Aliyekuwa Naibu Waziri wa Nishati na Madini na Mbunge wa Kibakwe, George Simbachawene, naye alitumia mbinu zote kutetea ufisadi huo na wakati mwingine alijenga hoja ili watuhumiwa waweze kupenya.

Chanzo: MTANZANIA

Kimenuka:Meya, Madiwani wa Chadema ARUSHA Wakamatwa

$
0
0
Naibu Meya wa Jiji la Arusha, Viola Likindikoki, pamoja na madiwani wengine wawili wa Chadema wamekamatwa na Jeshi la Polisi mkoani humo kwa sababu ambazo mpaka sasa hazijafahamika.

Meya wa Jiji la Arusha, Kalist Lazaro amesema Viola pamoja na madiwani hao wawili wamekamatwa leo (Alhamisi) wakiwa katika mkutano wa ndani uliokuwa ukisikiliza kero za wananchi.

“Nipo Tanga kikazi na nilimkaimisha nafasi yangu Viola, kwa kawaida Alhamisi tunasikiliza kero za wananchi, wakati wakiendelea kusikiliza kero ndipo walipokamatwa,” amesema.

Wengine waliokamatwa katika tukio hilo ni diwani wa viti maalumu (Chadema), Kata ya Ngarenaro Happiness Charles na diwani wa Viti Maalumu kata ya Olorieni, Sabrina Francis.

Kamanda wa Polisi mkoani Arusha, Charles Mkumbo amesema kwa kifupi kwamba jeshi lake linawashikilia kwa uchunguzi.

Akizungumza na gazeti hili, diwani wa viti maalumu (Chadema), Jenipher Lomayan  amesema madiwani hao wamekamatwa  leo saa 9 alasiri  wakiwa ndani ya ofisi ya Meya wa Jiji la Arusha wakisikiliza kero za wananchi.

Lomayan, amesema  wakiwa ndani ya ofisi hizo polisi waliovalia nguo za kiraia waliingia na kuwaeleza kwamba wako chini ya ulinzi na wanatakiwa kufika mbele ya makao maku ya jeshi hilo kwa uchunguzi zaidi.

“Wale polisi walitaka kuichukua simu ya Naibu Meya na ndipo madiwani wawili (Sabrina na Happiness) wanaoshikiliwa waliingilia kati na kuwazuia polisi wasimnyanganye simu hiyo na ndipo na wao wakaunganishwa katika tukio hilo,” amesema.

Dogo Janja KUTOKA Kimapenzi na Muna Love Yawa GUMZO Mjini...Mwenyewe Afunguka

$
0
0
Msanii wa hip hop Dogo Janja amekanusha tetesi za kujihusisha kimapenzi na muigizaji wa zamani na mfanyabiashara Muna Love kwa kusema hajawahi kuwa na mahusiano na habari hizo zinamuweka sehemu mbaya katika mahusiano lakini pia kifamilia.


Janjaro amelazimika kufunguka hayo baada ya tetesi kuenea muda mrefu kujihusisha na Mwanadada huyo huku wengine wakienda mbali zaidi kwa kusema kwamba analelewa na mfanyabiashara huyo.

"Hakuna kitu kibaya kama utandawazi, yaani kila mtu ana simu na bando lake kwa hiyo akiamka asubuhi anajisikia kufanya  chochote au kutunga vitu kama hivyo lakini siyo kitu kizuri, maana yananiumiza mimi na familia yangu, Uongozi wangu lakini pia vinamuumiza mpenzi wangu kwa sababu tuna malengo makubwa hivyo haya yanapoendelea yanazidi kumuumiza au kumchanganya", Dogo Janja alifunguka.

Aidha Janjaro ameongeza kwamba "Mimi siyo mtu wa kuonesha maisha yangu binafsi kwenye mitandao ndio maana hata mpenzi wangu sijawahi kumuweka mitandaoni, maisha yangu binafsi ni ya kwangu na siyo ya kila mtu hata huyo dada wa watu anaumizwa na hili na anafamilia pia kwa hioyo hizi habari zinazidi kumuweka pabaya.

Pamoja na hayo Dogo Janja amewataka watu kutoamini chochote kinachoanzishwa kwenye mitandao ya kijamii mpaka atakapozungumza mwenyewe

PROF. Muhongo Afunguka Uhusika Wake Katika Mikataba ya MADINI, Kutokuwapo Kwake Bungeni Kipindi Cha BUNGE la Bajeti

$
0
0
Aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo amesema hahusiki na mikataba ya yote ya madini.

Muhongo alitoa maelezo hayo jana, ikiwa si siku moja baada ya Nipashe kuripoti kutoonekana kwake bungeni bila ruhusa ya Spika.

Aidha, Prof. Muhongo alidokeza Nipashe chanzo cha kutokuwapo kwake katika chombo hicho cha kutunga sheria kwa wiki tano sasa.

Gazeti hili jana liliripoti kuhusu kutoonekana bungeni kwa mbunge huyo wa Musoma Vijijini (CCM) bila ruhusa ya Spika tangu uteuzi wake katika baraza la mawaziri utenguliwe wiki tano zilizopita.

Katika ripoti hiyo ya jana, Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashililah, alisema ofisi yake haina taarifa za mtaalamu huyo wa kimataifa wa Jiolojia na haijui aliko tangu alipoachishwa nafasi ya uwaziri, muda mfupi baada ya Rais John Magufuli kukabidhiwa ripoti ya Kamati ya kwanza ya uchunguzi wa mchanga wa dhahabu (Makinikia) Mei 24, mwaka huu.

Hata hivyo jana asubuhi Prof. Muhongo kupitia simu yake ya mkononi ambayo kwa siku tofauti amekuwa akipigiwa bila kupokea, alituma ujumbe mfupi wa maandishi kwa Nipashe akikana kuhusika na mkataba wowote wa madini na kutolea ufafanuzi kutokuwapo kwake bungeni kipindi hiki muhimu cha Bunge la bajeti.

Katika maelezo yake Prof. Muhongo alisema hahudhurii vikao vya Bunge kwa kuwa yuko mapumziko.

Aliongeza kuwa kipindi hiki hataki malumbano na hahusiki na mikataba mibovu ya madini ambayo kwa sasa 'imeteka' vinywa vya watanzania wengi wakiwamo wabunge.

"Muhongo yuko mapumzikoni. Hataki malumbano na hahusiki na mikataba yote hiyo", aliandika.

Nipashe ilipotaka kujua mahali ambapo Prof. Muhongo ameamua kupatumia kupumzika, msomi huyo alijibu kwa ufupi " It is my private life''(ni maisha yangu binafsi).

Nipashe pia ilitaka kujua kauli ya Prof. Muhongo kuhusu kutenguliwa kwa uwaziri wake na sababu za kuamua kwenda mapumzikoni kipindi hiki ambacho Bunge linajadili bajeti ya Serikali kwa mwaka ujao wa fedha.

Hata hivyo, msomi huyo hakuwa tayari kueleza kwa kina. Katika majibu yake Prof. Muhongo aliandika: " Tuheshimu taratibu za malezi, utamaduni, uzoefu na tabia ya kila mmoja wetu".

Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashililah aliiambia Nipashe juzi kuwa ofisi yake haina taarifa za Muhongo jambo ambalo ni kinyume na utaratibu.

Chanzo: Nipashe

Gonjwa La ZARI Hofu Yatanda, Siku Chache Mumewe KUFARIKI Dunia

$
0
0
PRETORIA: Takriban siku 25 baada ya kifo cha aliyekuwa mumewe, Ivan Ssemwanga ‘Don Ivan’, staa wa Afrika Mashariki, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’, ameibua hofu kubwa kwa ndugu, jamaa na marafi ki baada ya kupata gonjwa la ghafla lililosababisha kukimbizwa hospitalini akiwa hoi.

Kwa mujibu wa mpenzi wake ambaye ni msanii wa Bongo Fleva, mapema wiki hii, Zari alikimbizwa hospitalini huko Pretoria nchini Afrika Kusini na kulazwa kutokana na hali yake kuwa mbaya. Ilifahamika kwamba, Zari alikutwa na hali hiyo siku moja tu tangu mama yake mzazi, Halima Hassan naye alazwe jijini Kampala, Uganda kwa matatizo ya moyo kushindwa kufanya kazi hivyo kupishana kwa saa kadhaa za kukimbizwa hospitalini.

NI SIKU CHACHE TANGU AKABIDHIWE OFISI YA IVAN
Ilielezwa kwamba, Zari ambaye ni mfanyabiashara wa Uganda mwenye makazi Afrika Kusini alikutwa na hali hiyo ikiwa ni siku chache tangu alipoanza kufanya kazi kwenye ofi si ya Ivan aliyokabidhiwa hivi karibuni huko Pretoria, Juni 15, mwaka huu. Hata hivyo, habari hizo hazikueleza ni nini hasa kinachomsumbua Zari hadi kuwa katika hali hiyo hivyo ndugu, jamaa na marafi ki kupata hofu kubwa.

Katika hofu hiyo, baadhi ya ndugu hao walikaririwa wakisema kwamba, kutokana na mbilingembilinge za msiba wa Ivan ambapo Zari alikuwa ndiye kila kitu, ilikuwa ni lazima aumwe kwa kuwa alichoka mno. “Ukiacha uchovu lakini pia maumivu ya majonzi ya kufi wa na baba watoto wake vinaweza vikawa vimechangia kupata gonjwa ambalo hadi  hivi sasa halijajulikana,” alikaririwa mmoja wa ndugu wa mpenzi wake wa sasa wa jijini Dar.

KUHUSU MAMA YAKE
Habari kutoka Kampala zilieleza kuwa, wakati Zari akiwa bado mambo hayajakaa sawa, mama yake huyo aliugua ghafl a hivyo kulazimika kukimbizwa hospitali usiku.

“Ndiyo, mama Zari alikimbizwa hospitalini usiku lakini Zari hakuposti chochote kuhusu hilo.

NDUGU WA KARIBU ATOA HABARI
“Lakini ndugu wa karibu wa Zari ndiye aliyetoa habari kuhusu mama yake akisema kuwa, alikimbizwa hospitalini na kubainika kuwa ana tatizo la moyo kushindwa kufanya kazi,” kilikaririwa chanzo cha habari nchini Uganda na kuongeza: “Mama yetu amelazwa hospitali kutokana na tatizo hilo, anahitaji maombi yako.
Insha’allah atapona…” Hadi gazeti hili linakwenda mitamboni, hakukuwa na taarifa za wawili hao kuruhusiwa kutoka hospitalini hivyo bado ndugu, jamaa na marafi ki wana hofu juu ya mwanamama huyo na mama yake.
Zari ambaye ndiye msimamizi wa biashara kibao alizoziacha Ivan, ameachiwa watoto watatu wa kiume aliozaa na Ivan, Pinto, Raphael na Quincy ambapo ana wengine wawili, Tiffah na Nilan aliozaa na mpenzi wake wa sasa hivyo kuwa na jumla ya watoto watano.

NA MWANDISHI WETU, AMANI
GPL

Sikiliza WIMBO Mpya wa Nay wa Mitego ‘MOTO’, Alikiba, Ruby, Young Killer na Wengine Watajwa

$
0
0
Msanii wa muziki wa hip hop, Nay wa Mitego ameachia wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la ‘Moto’. Rapa huyo ameendelea na nyimbo zake za kuwachana baadhi ya wasanii ambapo ndani ya wimbo huu uliotayarishwa na producer Awasome ametajwa, Alikiba, Baraka The Prince, Nandy, Ruby pamoja na wengine. SIKILIZA HAPA CHINI:

Diamond Amtolea Uvivu Q-BOY Msafi, ‘Nikiamua Nitamnyoosha’

$
0
0
Baada ya maneno mengi kuzunguzwa na QBoy Msafi kuhusu kupigwa chini na Lebo ya WCB, hatimae Diamond Platnumz amefunguka kwa mara ya kwanza akidai kuwa amemsikia kwenye mahojiano yake karibia yote akilalamika huku akitoa lawama kwa uongozi wa WCB kitu ambacho sio kizuri kwenye jamii.



Diamond Platnumz amesema Q-Boy Msafi alipewa adhabu ya kinidhamu na Uongozi wa WCB kama Ofisi zingine zilivyo akasimamishwa kwa wiki moja lakini yeye akaona kama ameonewa akaendelea kufanya vitu ambavyo vile vile alivyokuwa anakosea tena zaidi.

“Unajua Ofisi kama Ofisi ina kanuni na taratibu zake na binadamu mnapokaa kwa pamoja haiwezekani mkawa perfect siku zote mimi mwenyewe sometimes nakosea Ofisi kama Ofisi inanipa adhabu zangu za kiofisi, inanikemea …aaahhh tulivyokaa na QBoy kwa takribani muda mrefu kuna vitu fulani fulani alikuwa anakosea lakini kama binadamu tunamuelewa na mimi nilikuwa mtu wa kwanza kumkingia kifua..

Kuna time akaja kuwa anapitiliza kwenye kukosea so kama ofisi ikiwa kuna watu wengine wanapewa adhabu wewe usipopewa adhabu inaonekana kama unapendelewa kwa hiyo nikampa adhabu ya kumsimamisha kama wiki mbili ili watu wengine wasione  labda kama yeye anapendelewa sasa yeye alivyopewa zile wiki mbili akaenda kufanya vitu vingine tofauti zaidi ndiyo suala limetokea hivyo,”alisema Diamond Platnumz huku akiendelea kusisitiza kuwa endapo ataamua kuchukua maamuzi kwa kivuli cha jina lake la Nassib basi atamnyoosha QBoy ndiyo maana akaamua kukaa kimya

“Kwahiyo suala hilo yeye akalichukulia tofauti na kuanza kuongea vitu vyote hivyo vingine tuu naamua kukaa kimya kwasababu mikiamua kusema sasa natumia Naseeb acha Diamond nikiamua kutumia Naseeb….ntamnyoosha“alisema Diamond Platnumz kwenye mahojiano yake na Clouds FM.

Hata hivyo Diamond Platnumz amesema kila binadamu anakosea na ili mtu aweze kujifunza kwani hakuna mtu aliyefanikiwa bila kukosea akitolea mfano kwa Kifesi ambaye nae alipewa adhabu kwa ya kusimamishwa kwa miezi sita lakini hakuwahi kuzungumza chochote nje ya WCB .

Diamond Platnumz jana aliachia video za nyimbo mbili mpya mmoja akiwa amemshirikisha Tiwa Savage kutoka Nigeria wimbo unaitwa ‘Fire’ na mwingine ‘I miss U’ akiwa peke yake unaweza ukazitazama video ya wimbo wake wa Fire hapa chini

Kutana na Maalim Fadhil Rashid Kutoka Komoro ni Mtaalam wa Tiba za Asili Anayetibu Magonjwa Yafuatayo

$
0
0
KUTANA NA MAALIM FADHIL RASHID KUTOKA KOMORO NI MTAALAM WA TIBA ZA ASILI

UNASHIDA NA MCHUMBA UNATATIZO PESA HAIKAI KURUDISHA MUME AU MKE KWA MUDA MFUPI MVUTO WA MAPENZI

MVUTO WA BIASHARA KUMSHIKA MUME AU MKE ASIKUSUMBUE

DAWA YA ( LIMBWATA )KUMTAWALA MPENZI WAKO KWA SABABU MAALUM

KUSAFISHA NYOTA ILI UWE NA MUONEKANO

NA PIA ANATOA PETE YA BAHATI INAYO ENDANA NA NYOTA YAKO ITAKAYO KULETEA PESA BILA MASHARTI

NA KUMILIKI MALI DAWA YA KUONGEZA UUME SAIZ UIPENDAYO

DAWA YA NGUVU ZA KIUME INAPATIKANA PIA ANAYO DAWA YA KUONGEZA HIPSI SHEP KUA NA UMBO BOMBA UMEIBIWA AU KUDHURUMIWA UTARUDISHIWA MALI YAKO NDANI YA MASAA 24 ANAFUNGA KESI NA KUPATA HAKI YAKO

DAWA YA MVUTO WA BIASHARA KUUZA MALI YAKO KWA HARAKA KUZUIA CHUMA ULETE

NA KUONDOA MIKOSI NA KUPANDISHWA CHEO KAZINI ACHA KUTESEKA ACHA KUHANGAIKA MAALIM FADHIL RASHID

YUPO TANZANIA KWA AJIALI YAKO. CALL...+255719362806/
+255763276239

WhatsApp IMO +255785786436

ACT Wamkana Aliyejitangaza Kuhamia CCM Mbele ya Rais Magufuli..WADAI ni Mchezo Mchafu wa Humphfrey Pole Pole

$
0
0

Chama cha ACT-Wazalendo wamtolea nje aliyetangazwa kwenye mkutano wa Rais John Magufuli kuwa ni Mwenyekiti wa ACT mkoa wa Pwani aliyeamua kurejea CCM mbele ya Rais Magufuli.

Taarifa Kamili Hii Hapa chini:

Mume WANGU Hanitoshelezi Kitandani-Now I’m Sleeping With My ex'' - lady

$
0
0
Hello, please post this as you might just be helping me save my future.

My name is Daisy. I’m 25 and might be getting married in December, if only I will say yes to my man.

He’s 31 by the way, but I told him I was going to think about it. To cut the story short, I’m really scared of getting married to him because I wouldn’t want to cheat on my husband. This guy is not even a one minute man when it comes to scx. He is a 5 seconds person. I’ve complained severally and he has tried to take all kinds of drugs to make him last but they don’t work.

Whenever we are ready to get down and he is inside me, he just thrusts for 5 seconds and that’s it. Then he leaves me wanting and he can’t go a second round because his body can’t do it. There was a time I was so horny, I had to go meet my ex and yes he made me feel like a woman. But with my soon to be hubby I don’t feel that way. He does not smooch me, he just goes straight in and then everything is over in a blink. I’m just frustrated and I need advice because he has tried basically every solution including Viagra, but the after effect was bad.

How can I be a faithful wife after I get married to this guy when he can’t even satisfy my urge? What should I do?

Install APP ya Blog Hii ya UDAKU SPECIAL Kwenye Simu yako Kutoka Google Play Kusoma Habari Kirahisi

$
0
0

Download  Application ya Udaku Special Blog Kwenye Simu yako Kutoka Play Store Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi

Bonyeza Hapa CLICK HERE 


Au Kama Unayotayari Bonyeza HAPA Ku Update Uweze Kupata Ikiwa na Muonekano Mpya
Viewing all 104799 articles
Browse latest View live




Latest Images