Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104793 articles
Browse latest View live

Sanchi Bila Mahari Ya Mil. 10 Siolewi

$
0
0
MWANAMITINDO na video queen mwenye umbo tata Bongo, Jane Rimoy ‘Sanchi’ amefunguka kuwa thamani yake ni kubwa hivyo mwanaume anayetaka kumuoa lazima ajipange kwa mahari ya milioni 10 za Kitanzania.

Akizung-umza na Star Mix, Sanchi mwenye figa matata alisema kuwa, siku zote wanaume wanaowaoa wanawake kwa mahari ndogo huwachukulia hivyohivyo lakini akilipa mahari kubwa hata heshima inakuwepo na uthamini pia.

“Unajua mwanaume wa kweli unampima kwenye vitu vidogo kama hivyo, mimi mahari nataka iwe ya heshima kabisa na kama mtu hana milioni hiyo 10 basi hana sifa ya kuwa mkewe na kunimiliki,” alisema Sanchi.

Rage Aifafanua Katiba ya Simba Kuhusu Hatma ya Aveva na Kaburu

$
0
0
Juni 29, 2017 viongozi wa juu wa klabu ya Simba Rais wa klabu Evans Aveva na makamu wake Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ walifikishwa mahakamani kujibu mashtaka yanayowakabili.

Hatua hiyo imefikiwa baada ya TAKUKURU kuwashikilia viongozi hao kwa siku kadhaa, viongozi hao wamesomewa mashtaka matano yakiwemo ya kughushi nyaraka ili kujilipa deni ambapo inadaiwa waliikopesha Simba dola za Marekani 300,000 huku makosa mengine yakiwa ni ya utakatishaji pesa.

Swali linakuja kwamba, inapotokea viongozi wa ngazi ya juu kama hao wa Simba kushikiliwa na mahakama jukumu la kuiongoza klabu linakuwa kwa nani?

Ismail Adden Rage ametoa ufafanuzi kuhusu suala hilo kwa mujibu wa katiba ya Simba anayoifahamu yeye kama haijabadilishwa.

“Katika ali kama hii viongozi wa kamati ya utendaji watakaa wajitathmini ni nani miongoni mwao ambaye ni senior anaweza akakaimu kwa uda lakini badae itabidi waitishe mkutano mkuu ili waweze kuamua lakini katiba haisemi itachukua muda gani kufanya hivyo lakini pia katiba hairuhusu sana kukaimu bila kupata baraka za mkutano mkuu.”

“Ni vyema kamati ya utendaji ikakaa na kusoma katiba vizuri, kama haijabadilishwa ninavyofahamu mimi, endapo Rais hayupo basi madaraka yote yatachukuliwa na makamu wa Rais endapo pia kakamu wa Rais hayupo, miongoni mwa wale wajumbe wa kamati ya utendaji ambaye ni senior kuliko wote ataongoza klabu hadi hapo mkutano mkuu utakapoamua vinginevyo kama haijabadilishwa.”

Kama ikitokea viongozi hao wakatiwa hatiani kwa makosa yanayo wakabili halafu wakatoka Rage ameendelea kufafanua kama viongozi hao watakuwa na sifa ya kuendelea kuongoza au ndio utakuwa mwisho wao.

“Huruhusiwi tena kuwa kiongozi katika klabu yoyote ile, vilabu vya mpira vyote vimesajiliwa kwa msajili wa vyama vya michezo, mimi binafsi nimewahi kupata matatizo lakini kwa bahati nzuri mahakama ya rufaa ilinisafisha. Kwa kuwa mahakama ya rufaa ilinisafisha, basi kwa maana hiyo katika maisha yangu bado sijawahi kutiwa doa mahali popote.”

“Kwa bahati mbaya ikitokea wakatiwa hatiani, lazima wakate rufaa waombe kusafishwa lakini kama wenyewe wataridhikabasi hawawezi kuwa viongozi tena wa michezo kwa sababu sheria za nchi wala za katiba ya Simba haziruhusu.”

VIDEO: Lema, Mnyika Waliamsha Tena Dude Bungeni

$
0
0
VIDEO: Godbless Lema, John Mnyika Waliamsha Tena Dude Bungeni, Tazama Video hiyo hapo chini ujionee mwenyewe

VIDEO: Rayvanny kafunguka kuhusu Zari kutompost mitandaoni

$
0
0
Moja ya issue kubwa inayoendelea kwenye mitandao ya kijamii ni maneno yanayosambazwa mitandaoni kuhusu uhusiano wa mwimbaji Rayvanny na Zari ambaye ni mpenzi wa Boss wa WCB Diamond Platnumz ikidaiwa kuwa wawili hao hawana uhusiano mzuri ndio sababu Zari huwa hampost Rayvanny kwenye page zake za kijamii.

Tazama Hapa:

Maskini:Mwanamke Asimulia Alivyobakwa Kwa Zamu Siku ya Harusi yake

$
0
0
Wakati Terry Gobanga, wakati huo akiitwa Terry Apudo alipotoweka katika harusi yake hakuna mtu aliyedhani kwamba alitekwa nyara, kubakwa na kutuwa kandakando ya barabara akipigania uhai.

Lilikuwa janga la kwanza kati ya mawili kumkabili muhubiri huyo kijana. Lakini ni manusura.

Harusi iliopangwa ilitarajiwa kuwa harusi kubwa.

Nilikuwa muhubiri hivyobasi wanachama wote wa kanisa walitarajiwa kuhudhuria.

Mchumba wangu Harry na mimi tulikuwa na furaha tulikuwa tunafunga ndoa katika Kanisa la All Saints Cathedral mjini Nairobi na nilikuwa nimekodisha rinda zuri sana la harusi. Lakini usiku kabla ya ndoa yetu, niligundua kwamba nina baadhi ya nguo za Harry .

Asingeweza kuja katika harusi bila tai kwa hivyo rafiki yangu mmoja ambaye alikuwa amekubali kubaki nami usiku wa kuamkia harusi alikubali kumpelekea mapema alfajiri.

Niliamka mapema na kumpeleka hadi katika kituo cha kupanda basi.

Nilipokuwa nikirudi nyumbani, nilipita karibu na mtu mmoja ambaye alikuwa ameketi kati boneti ya gari na akanishika kutoka nyuma na kuniingiza katika viti vya nyuma vya gari hilo na kuondoka mahali hapo.

Yote haya yalifanyika kwa sekunde moja. Nilifunguliwa mdomo na kuwekwa kipande cha nguo mdomoni.

Nilikuwa nikirusha mikono na miguu nikitaka kupiga kelele. Nilipofanikiwa kutoa kitambara hicho nilipiga kelele, ni siku yangu ya harusi! hapo ndipo nilipopigwa ngumi .

Mmoja ya wanaume hao wakaniambia nishirikiane nao ama niuwawe. Wanaume hao walinibaka kwa zamu .

Nilihisi nitafariki, lakini bado niliendelea kupigania uhai wangu, hivyo basi mtu mmoja alipotoa kitambara kilichokuwa mdomoni mwangu nilimuuma uume wake.

Alipiga kelele kwa uchungu na mmoja wao akanidunga kisu tumboni.

Baadaye walifungua mlango na kunitupa kando ya barabara huku gari likiendelea kwenda. Nilikuwa mbali na nyumbani, nje ya jiji la Nairobi .

Ilikuwa zaidi ya saa sita baada ya kutekwa. Mtoto mmoja aliniona nikirushwa nje ya gari na akamweleza bibiye.

Watu walikuja mbio. Wakati maafisa wa polisi walipokuja walijaribu kuangalia iwapo bado ninapumua, lakini hawakuona kama nilikuwa bado napumua.

Wakifikiri nimefariki walinitia katika blanketi na kuanza kunipeleka katika chumba cha kuhifadhi maiti .

Lakini njiani nilikohowa. Polisi mmoja alisema, bado hajafariki, hivyobasi wakabadilisha njia ya kuelekea katika chumba cha kuhifadhi maiti na kunipelekea katika hospitali kuu ya serikali nchini Kenya.

Niliwasili nikiwa na mshangao mkubwa, nikizungumza mambo nisioelewa. Nilikuwa nusu uchi nikivuja damu huku sura yangu ikiwa na majeraha kutokana na kipigo nilichopata.

Kanisa la All saints Cathedral NairobiKanisa la All saints Cathedral Nairobi
Lakini kuna kitu kimoja kilichomshtua mwanamke aliyekuwa akisimamia matibabu, kwa sababu aligundua mimi ni bibi harusi.

”Twendeni kanisani tuone iwapo wanamkosa bibi harusi”, aliambia wauguzi.

Kwa bahati kanisa la kwanza waliloulizia ni All Saints Cathedral jijini nairobi ambapo waliambiwa kwamba kulikuwa na harusi mwendo wa saa nne Asubuhi lakini bibi harusi hakuonekana.

Chanzo: bbcswahili

Mtoto Aliyejirusha Ghorofani Shule ya DYCCC Chang'ombe sio Mwanafunzi, Hakufa

$
0
0
Mtoto anayedhaniwa kuwa ni mwanafunzi wa  shule ya DYCCC iliyopo Chang'ombe jijini Dar es Salaam amejirusha kutoka ghorofa ya nne mpaka chini huku chanzo cha tukio hilo kikiwa bado hakijafahamika haraka.

Kamanda wa polisi mkoa wa kipolisi Temeke,  Andrew Satta amekiri kutokea kwa tukio hilo ingawa taarifa hizo zipo kwenye mitandao na hazijafikishwa kituoni hapo, lakini tayari wameanza kufuatilia ili kubaini nini chanzo cha cha tukio hilo.

"Ni kweli tumeona hilo tukio hata sisi kwenye mitandao ya kijamii lakini bado hatujapata taarifa za awali na tukio bado halijaripotiwa polisi. Sisi tumechukua hatua za kuanza kufuatilia na tukishafahamu tutaweka wazi" alisema Kamanda Satta.

MUENDELEZO
Meneja wa shule ya DYCCC (jina halijafahamika) amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kukanusha kwamba mtoto huyo siyo mwanafunzi wa shule hiyo na kwamba alikwenda kusherehekea sikukuu ya Idd kwani ni utaratibu wa wa shule hiyo kuombwa uwanja kwa ajili ya sherehe kila mwaka.

"Nipo nje ya Dar es salaam, lakini anayeonekana kwenye hizo video si mwanafunzi wa shuleni kwetu. Ni mtoto ambaye ametoka Morogoro na kuja Dar es salaam kwa ndugu zake. Alipofika alijumuika na wenzake kusherehekea sikukuu. Sasa kwa tukio hili waandaji watakuwa na majibu mazuri kuliko sisi, kwa sababu wao huwa wanatuomba uwanja na sisi tunawapatia. Lakini mtoto aliokolewa yupo salama na wazazi wake" alisema Meneja wa shule ya DYCCC.
Hata hivyo jina na umri wa mtoto huyo bado havijafahamika.

Freema Mbowe Afunguka: Polisi Msituzibe Midomo

$
0
0
Mwanyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe amelitaka jeshi la polisi nchini kutowafunga midomo na kusema kitendo cha jeshi hilo kuwafukuza waandishi wa habari wakati wakifanya kazi yao si sawa.

Freeman Mbowe amesema hayo leo Alhamisi  baada ya jeshi la polisi kuwafukuza waandishi wa habari ambao walikuwa wakifuatilia tukio la kuwasili kwa Mhe. Edward Lowassa Makao Makuu ya Polisi ambapo leo alikwenda kuitika wito wa jeshi hilo baada ya juzi kutoa maelezo na kutakiwa kufika leo tena.

Mhe Edward Lowassa alipata wito kutoka kwa Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI) kumtaka kufika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi siku ya Jumanne tarehe 27 kufuatia kauli zake alizozitoa ambazo zinasemakana kuwa ni uchohezi

Lowassa juzi alifika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi na kutoa maelezo yake kwa muda wa masaa manne, kisha baada ya hapo alijidhamini mwenyewe na kutakiwa kufika siku ya Alhamisi ya tarehe 29 Julai 2017 ambapo amefika na kuambiwa uchunguzi wa jambo lake haujakamilika hivyo arudi tena tarehe 13 Julai 2017.

Install APP ya Blog Hii ya UDAKU SPECIAL Kwenye Simu yako Kutoka Google Play Kusoma Habari Kirahisi

$
0
0
Download  Application ya Udaku Special Blog Kwenye Simu yako Kutoka Play Store Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi

Bonyeza Hapa CLICK HERE 


Au Kama Unayotayari Bonyeza HAPA Ku Update Uweze Kupata Ikiwa na Muonekano Mpya

Serikali Yaingizwa Hasara Zaidi ya Bil 20

$
0
0
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeingizwa hasara zaidi ya Bilioni 20 kwa kipindi cha mwaka mmoja uliyopita kutokana na bidhaa bandia na zisizokuwa na viwango (feki) zinazoingizwa nchini.
 
Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri wa Kilimo na Umwagiliaji, Mhandisi Isack Kamwelwe wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti maalumu Shai Joseph Raymond alipotaka kujua ni hasara gani imepatikana kwa mwaka mmoja uliyopita kutokana na bidhaa bandia na zisizokuwa na viwango zinazoingizwa nchini zikiwemo Pembejeo za kilimo, dawa za mifugo, dawa za binaadamu, vyakula, vinywaji, vifaa vya majumbani n.k.

"Katika kipindi cha Januari hadi Decemba mwaka 2016, Tume ya Ushindani ilikamata bidhaa bandia zenye thamani ya shilingi Bilioni 18.67, bidhaa hizo zilikamatwa kwenye kaguzi za bandarini, vitengo vya makontena na katika masoko. Kipindi cha Julai 2016 hadi Marchi 2017 Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kwa kushirikiana na taasisi nyingine waliteketeza bidhaa mbalimbali zenye thamani ya shilingi Bilioni 2.4 bidhaa hizo ni pamoja na nguo, nyama na soseji, vilainishi vya injini, betri za magari na sola 1430" alisema Mhandisi Kamwelwe

Vile vile, Mhandisi Kamwelwe amesema Shirika pia liliweza kufanya ukaguzi wa mabati na kuteketeza 84000 ambayo hayakuweza kukidhi viwango.

Pamoja na hayo, Mhandisi Kamwelwe amesema serikali kupitia tume ya ushindani (FCC) pamoja na kushirikiana wamiliki wa nembo za biashara inaendelea kudhibiti biashara bandia zisiingie nchini ili kufanikisha ushindani wa haki katika biashara.

Rammy Aopoa Kifaa Cha Gambia Baada ya AGNESS Masogange Kumtema

$
0
0
STAA wa filamu Bongo, Rammy Gallis amenasa kifaa kipya kutoka nchini Gambia ambaye naye ni msanii wa filamu, Princess Shyngle na kusema kuwa mwanadada huyo ndiye anayemkonga nyoyo kwa sasa japo hapendi kumuuzisha sura.
Akipiga stori na Star Mix baada ya meseji za mapenzi akichati na mwanadada huyo kunaswa na paparazi wetu, msanii huyo alifunguka kuwa, yupo kwenye uhusiano na mlimbwende huyo kwa muda sasa na kwamba miongoni mwa vitu vilivyomvutia kwake ni pamoja na figa matata aliyonayo.


“Nilikutana na Princess nilipoenda kufanya filamu Nigeria, kwa kuwa yeye ni Mgambia lakini makazi yake makubwa ni Nigeria, nampenda sana naamini yeye ndiye tulizo la moyo wangu, mapenzi ya Kibongo yanitue kwa sasa,” alisema.

Mwanaume Amwoa Mwanaume Mwenzake Bila Kujua

$
0
0
Mwanaume mmoja mkoani Mtwara amekaa na mwanaume mwenzake miezi minne bila kujua.
Kwa mujibu wa maelezo mahusiano yalianza baada ya kukosea namba wakafahamiana mpaka wakafikia maamuzi ya kuoana huku akijua ni wa kike.

Baada ya kufata taratibu wawili hao wakaoana lakini tatizo likaja wakati wa kujamiiana mwenzake wakawa kilasiku anasema anaumwa ikawa hivyo ndani ya miezi mitatu ndipo akaja gundua kuwa ni mwanaume mwenzake.

Kuhusu mavazi anasema mwenzake huyo huvaa kama mwanamke na kupika pia anajua hata kujiremba anajiremba hali iliyo mpelekea kutogundua.

VIDEO: Onyo la Waziri Nchemba kwa Wabunge Wanaoshabikia Mauaji ya KIBITI

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani Mwigulu Nchemba alisimama Bungeni leo June 29, 2017 kujibu hoja za baadhi ya Wabunge wakiwemo wanaodai Serikali imeshindwa kumaliza tatizo la mauaji yanayoendelea katika Wilaya ya Kibiti, Pwani huku akiwaonya Wabunge kuacha kutoa kauli ambazo zitawasababisha kuhusishwa kwenye uchunguzi wa awali. VIDEO:

EATV na Radio Washutumiwa Kujiendesha Kwa Matakwa ya Watu Wenye Chuki Binafsi

$
0
0

KUONA OFFICE INAENDESHWA KWA MATAKWA YA WATU WENYE CHUKI BINAFSI NA MTU FLANI NI TATIZO KUBWA.

#CLOUDSMEDIA ni office ambayo ina matatizo yake na baadhi ya wasanii lakini wao wameonesha kuwa wanaendesha maswala yao ki office na sio ki mtu binafsi ndio mana unaona msanii ambaye ana tatizo nao hawamuhusishi na chochote katika program zao.

Lakini hili limeonekana kuwa somo gumu kwa EAST AFRICA REDIO na hata TV ila zaidi likionekana kwa mtangazaji mmoja @dullaplanet.
@diamondplatnumz inajulikana toka mwanzo kuna vitu vilikuwa havimfurahishi ndani ya vituo hivi na hata mtu mwenye jicho la tatu angejua na haya yalikuwa yamejidhihirisha ndio mana sikuona ajabu hata kwa @diamondplatnumz kususia tuzo zao.

Naamini kususia kwake na @wcb_wasafi kwa ujumla ni kitu ambacho hawakukipenda EATV NA REDIO lakini walishindwa kujua kuwa ni mbegu ya zile firigisu walizokuwa wanazionesha mwanzoni na hata angekuwa nani asingeshiriki.

Kitu ambacho nimekishangaa kwanza wamefungia nyimbo za msanii yoyote wa @wcb_wasafi nyimbo zake kuchezwa kwa kawaida nilijua watafata misingi ya @cloudsfmtz na @cloudstv kutojihusisha na chochote juu ya wasanii ambao wana tatizo nao ila wao wamekuwa wakiandaa mijadala ya kuwachafua wasanii wa @wcb_wasafi .

Mjadala wa kwanza ni wa @dullaplanet dhidi ya tuhuma kuwa diamond kasema hategemei media kwenye kazi zake.Ulianzishwa mjadala wa kupotosha watu kuwa diamond haheshimu vyombo vya habari kitu ambacho sio kweli lakini @dulla na #djsummer walianzisha mjadala na kushutumu vikali jambo ambalo halina ukweli.
Ila tukaona juzi ikaandaliwa interview yenye lengo la kumchafua diamond akihusishwa #menejamaneno ambaye alitumia kipindi hicho kumtuhumu diamond kuwa ni msanii mchawi zaidi ambaye ashawahi kuwa chini yake.Interview ilijaa mada ya uchawi wa diamond zaidi kuliko wasanii wengine.Ila kilichonisukuma kuandaa makala hii ni kukosa uzalendo kwa wenzetu hawa @dullaplanet na @jr na kutaka kubadilisha nyeupe kuwa nyeusi kwa kuandaa mjadala na uchambuzi kuwa @rayvanny hakuwa nominated tuzo za #BET.Nikawa najiuliza hawa wanajua weledi wa kazi zao wanaenda hewani kuongea vitu ambavyo hawana uthibitisho navyo.

KWANINI WASIOMBE RADHI.
By @abby1_thebest

Jeshi la Laua Majambazi wanne Kibiti usiku wa kuamkia leo

$
0
0

Jeshil la Polisi limeua Watu wanne wanaozaniwa kuwa ni majambazi kwenye kijiji cha Pagae , Kibiti Mkoani Pwani

Taarifa iliyotolewa kwa Vyombo vya Habari na DCP Lebaratus Sabas Mkuu wa Opereshini Maalumu ya Jeshi hilo Tanzania ambapo amesema kuwa majambazi hao wameuwa jana Majira ya Usiku
kwenye barabara inayotoka Pagae kuelekea Nyambunda.

taarifa hiyo ya DCP Sabas inasema  kuwa Askari Polisi wakiwa doria walikutana na kikundi cha watu kinachokadiriwa kuwa na watu sita wakitokea barabara kuu ya lami wakifuata barabara hiyo inayoelekea Nyambunda kilomita 100 kutoka barabara kuu.

"Watu hao walipogundua kuwa watu waliokuwa mbele yao ni Askari Polisi  walikimbia vichakani na ghafla wakaanza kuwashambulia askari kwa risasi.

Askari Polisi walijibu mapigo na kuanza kupambana na watu hao. "

Katika mapambano hayo askari Polisi walifanikiwa kuwajeruhi kwa risasi watu wanne katika kundi hilo la wahalifu  hao.

Aidha katika mapambano hayo zilipatikana silaha mbili aina ya Smg na magazine mbili pamoja na risasi 17 zilizokuwa zinatumiwa na wahalifu hao.

Watu hao wanne ambao wanasadikiwa kuwa miongoni mwa wahalifu wanaendesha vitendo vya mauaji katika wilaya za Mkoa wa Pwani.

Majeruhi hao walifariki dunia wakiwa njiani kupelekwa hospitali kutokana na kuvuja damu nyingi zilizotokana na majeraha ya risasi waliyopata, milli ya marehemu imehifadhiwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili.

Jeshi la Polisi linaendelea kutoa wito kwa wananchi kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi zitakazosaidia kuwakamata watu wanaojihusisha na vitendo hivi vya kihalifu kwenye wilaya za Mkoa wa Pwani.

Ripoti ya Mama aliyedai Kuibiwa mtoto Hospitalini Temeke yamfikia Waziri, atoa Neno

$
0
0

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema ripoti ya uchunguzi wa utata wa watoto pacha ambao mmoja anadaiwa kuibwa katika Hospitali ya Temeke imebaini kuwa, mama huyo Asma Juma alikuwa na mimba ya mtoto mmoja.

Akitoa ufafanuzi wa ripoti ya uchunguzi huo, leo (Ijumaa) Mwenyekiti wa Kamati ya Uchunguzi huo, Profesa Charles Majinge amesema kuwa inawezekana kuna makosa yalitokea katika vipimo vya utrasound na kwamba hata wataalam wa hospitali ya Temeke, walifanya makosa kwa kumfanyia huduma ya upasuaji bila kumfanyia vipimo zaidi vya ultrasound.

Pia Profesa Majinge alisema kuwa hapakuwa na sababu ya mama huyo, Asma Juma kuandikiwa kufanyiwa upasuaji wa dharura ingawa hakufanyiwa huduma hiyo ya dharura.

Kabla ya kutoa taarifa hiyo kwa vyombo vya habari, Waziri Mwalimu na Profesa Majinge walikutana na familia ya Asma na kuwapatia matokeo ya ripoti, matokeo ambayo hata hivyo yamemfanya mama huyo kuangua kilio.

Bifu la Diamond na EATV...Je Dulla Ndio Chanzo au Upotoshaji?

$
0
0

Bifu la Diamond na EATV...Je Dulla Ndio Chanzo au Upotoshaji? "Enyi wajinga, fahamuni werevu, Nanyi wapumbavu, mpate moyo wa kufahamu"

Ama kweli! "Hakuna shule ya akili" bali ufahamu wa kila mmoja kwa upana wake.

Upotoshaji ni mkubwa mno juu ya Dulla Plannet Mtangazaji wa Eatv/Ea Radio na Diamond Platnumz na team nzima ya Wasafi.

Ila ni kazi ngumu kuwaaminisha watu ukweli ambao tayari wao wana uongo wao kichwani. La hasha hatuwezi kuchoka kuhubiri ukweli uliopo.

Ingawa yapasa "Usiseme masikioni mwa mpumbavu, maana atadharau hekima ya maneno yako" ila hapana kwa hili wacha tuseme ile kweli yenye kweli ili ituweke huru.

Kuzimwa kwa kusikika kwa Diamond na Team yake katika vituo hivyo ya Eatv/Ea Radio wala hapaswi kulaumiwa Dulla. Kwa maana ya uhalisia Dulla ni mwenye jina kubwa ila kiutendaji kwenye ofisi ni mtu mdogo mno, ambaye hupewa amri kama apewae mtu mwingine yoyote katika ofisi yoyote ile.

Ila swala hili limekuwa likichochewa zaidi na wachambuzi wasio na hoja waliojaa uteam na upendeleo wa upande mmoja ambao huandika bila kujua kile ambacho anaandika.

Ni wazi jaman tusishangae haya kwa maana "Mchunga peku hapendi ila hana viatu" (Ufahamu)

Uhalisia ni kwamba ni kawaida mno kwa media kuzima kupiga nyimbo za msanii yoyote. Na hii huja pale msanii anapoenda kinyume na matakwa yao media husika.

Na hata kama mtangazaji mmoja ana tatizo na msanii fulani ni ngumu kwa nyimbo kuacha kuchezwa, isipokua katika kipindi chake tu. Ila vipindi vingine vitaendelea kucheza nyimbo za msanii huyo.

Ila kama tatizo limehusisha uongozi ni lazima vipindi vyote vizime kupiga nyimbo za msanii husika. Sasa tutafakari kwa upana je!kweli dulla kwa nafasi yake ya utangazaji anaweza kuzima kupigwa kwa nyimbo za Diamond au msanii mwingine katika Eatv/Earadio?

Nguvu ya kuaminisha mashabiki wa Diamond kuwa Dulla ni chanzo cha kuzima kupigwa kwa nyimbo za Diamond na Wasafi kwa ujumla ni kubwa. Na imani ya kuamini inaendelea kupanda.

Lakini "Mjinga husadiki kila neno"

Kimsingi haipasi hata kidogo kuendelea kumnenea Dulla lugha mbaya. Bali kutafari hoja zaidi na undani wa jambo.

Lakini kama mbwa aludiavyo matapiko yake, ndivyo mtu mjinga anavyorudia upambavu wake"
By tizneez

Je Una Tatizo la Nguvu za Kiume, Kukosa Hamu ya Tendo na Maumbile Madogo?

$
0
0
JE, UNA TATIZO LA NGUVU ZA KIUME, KUKOSA HAMU YA TENDO NA MAUMBILE MADOGO? SOMA HAPA 👇👇👇👇 Tatizo la kukosa au upungufu wa nguvu za kiume limekuwa kubwa sana, sio Tanzania tu bali duniani kote. Kupungukiwa nguvu za kiume na maumbile madogo sio ugonjwa ila ni dalili ya ugonjwa. Hii ina maana kuna dosari au udhaifu wa kiutendaji ndani ya mwili. UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME HUSABABISHA MAMBO KAMA:-
☆Kukosa hamu ya tendo la ndoa ☆Uume kusimama kwa ulegevu
☆Kuwahi kufika kileleni ☆Kushindwa kurudia tendo kwa wakati
☆Kuchoka sana baada ya round ya kwanza na hata kukinai kabisa. @Markson_beauty_pr Tunakuletea suluhisho la matatizo hayo hata kwa wenye kisukari kwa:-
1.HANDSOME UP ORIGINAL ni kifaa chenye uwezo wa 99% kuongeza uume kwa size uipendayo na kuimarisha misuli ya uume iliyolegea @220000@220,000/=
2.SHARK POWER ni gely ya kupaka inayoongeza uume kwa wastani wa inch 6.5 @130000@130,000/=
3.Vidonge maalum kwa ajili ya kuongeza nguvu na hamu ya tendo la ndoa hata kwa wenye kisukari @130000@130,000/=
4.Spray ya kuchelewesha kufika kileleni na kurudia tendo hata mara 3 bila kuchoka @130000@130,000/= KWA BIDHAA HIZI NA NYINGINE NYINGI TEMBELEA UKURASA WETU WA INSTAGRAM :- @Markson_beauty_pr @Markson_beauty_pr @Markson_beauty_pr.

Wasiliana nasi Popote ulipo duniani kwa no (+255)
0767447444 na 0714335378 

NB:Matokeo ni uhakika na garantii na hakikisha unapata risiti yenye muhuri halisi wa MARKSON CO pamoja na garantii ili kukuhakikishia kufanikiwa kwako. Bidhaa zetu zimetengenezwa kwa mimea na matunda na hazina kemikali wala madhara kwa mtumiaji. Zimethibitishwa kiafya. < WELCOME ALL>

Mjue Mgunduzi wa BUNDUKI MAARUFU IITWAYO AK 47

$
0
0
Luteni Jenerali Mikhail Timofeyevich Kalashnikov wa Urusi ndiye mgunduzi wa silaha maarufu sana katika uwanja wa mapambano duniani kote iitwayo AK 47. Ni bunduki iliyobuniwa na kutengenezwa na kamanda huyu wa Jeshi Jekundu (Red Army) la Muungano wa Kisovieti wa Urusi (USSR) wakati huo.

Luteni Jenerali MIKHAIL TIMOFEYEVICH KALASHNIKOV alizaliwa tarehe 10 Novemba 1919 eneo la Kurya, Altai, Urusi, ambalo kwa sasa linajulikana kama Altai Krai, Russia. Alijiunga na jeshi la Urusi mwaka 1938 na kupangiwa kama fundi wa vifaru na baadaye alipanda cheo na kuwa kamanda wa vifaru.

Mwezi Oktoba mwaka 1941 wakati wa Vita vya Pili vya Dunia, alijeruhiwa vibaya katika mapigano ya Bryansk na kulazwa hospitalini mpaka mwezi Aprili mwaka 1942. Akiwa hospitalini akitibiwa, aliwasikia askari wenzake wa Kirusi wakilalamikia udhaifu wa bunduki zao za Urusi katika uwanja wa mapambano.

Baada ya kubaini udhaifu huo wa bunduki za Urusi, aliamua kutumia ubunifu wake kutengeneza bunduki bora zaidi za jeshi la nchi yake. Baada ya majaribio yake ya muda mrefu, hatimaye juhudi zake zilizaa matunda mwaka 1947 alipofanikiwa kutengeneza bunduki ya AK 47. Jina hili AK 47 ni kifupi cha maneno "Avtomat Kalashnikova model 1947"; namba 47 inasimama badala ya mwaka wa ugunduzi.

Luteni Jenerali MIKHAIL TIMOFEYEVICH KALASHNIKOV alifariki hospitalini tarehe 23 Desemba, 2013 akiwa na umri wa miaka 94 huko Izhevsk, mji mkuu wa jimbo la Udmurtia Urusi.

Huyo ndiye MIKHAIL TIMOFEYEVICH KALASHNIKOV, mgunduzi wa bunduki maarufu kwa jina la AK 47 ["Avtomat Kalashnikova model 1947"].

Rais Magufuli Apeleka Kilio Kwa Mbunge Joshua Nassari

$
0
0
Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Joshua Nassari huenda bado hajaelewa nini kielikumba jimbo hilo baada ya Diwani wa Kata ya Muriet, Credo Kifukwe kujiuzulu wadhifa huo kwa kile alichosema kuwa anamuunga mkono Rais Dkt Magufuli.

Diwani huyo wa CHADEMA ambaye ni watano kujiuzulu katika jimbo hilo, alisema jana wakati akitangaza uamuzi huo kuwa, ameridhishwa na utendaji kazi wa kiongozi huyo wa nchi na kwamba kazi anayoifanya ni nzuri na inatakiwa kuungwa mkono na watu wote.

Aidha, Kifukwe alisema kuwa, hana mpango wa kujiunga na chama chochote cha siasa, na kwamba anataka kufanyakazi zake binafsi kwani siku zote amekuwa msema kweli akipigania maendeleo ya wananchi wake.

Muda mfupi baada wa diwani huyo kujiuzulu, Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema alisema kuwa kiongozi huyo na wengine wote wamekuwa wakinunuliwa na CCM katika mkakati wake wa kuidhoofisha CHADEMA, na kwamba wao hawawezi kumzuia kiongozi aliyeamua kununuliwa kwa fedha.

“Nimejiuzulu mwenyewe na sitarajii kujiunga na chama kingine cha siasa bali nataka kufanya kazi zangu mwenyewe. Nimeona kazi anazofanya Rais ni nzuri ambazo hata wapinzani tulitaka kuzifanya,” alisema Kifukwe akikanusha madai ya Lema kuwa amenunuliwa na CCM.

Madiwani wengine wanne waliokuwa wamejiuzulu kabla yake ni, Diwani wa Leguruki, Anderson Sikawa, Diwani wa Mikamba, Emmanuel Mollel, Diwani wa Maroroni, Greyson Isangya na Diwani wa Viti Maalum, Josephine Mshiu wote kutoka jimbo la Arumeru Mashariki.

Akizungumza na waandishi wa habari, Katibu wa CCM Wilaya ya Meru, Aloyce Hhayuma alisema kuwa, madai kwamba madiwani hao wamenunuliwa na CCM si ya kweli bali wamehama na wangine kuachia nyadhifa zao kutokana na kuvutiwa na kazi nzuri inayofanywa na serikali ya awamu ya tano.

Hili ni pigo kubwa kwa CHADEMA mkoa wa Arusha kufuatia madiwani hao kujiuzulu kwani watakuwa na kazi kubwa ya kuhakikisha wanashinda viti hivyo wakati wa chaguzi ndogo.

Makabila yanayokula Nyama za Binadamu

$
0
0
UKIHADITHIWA tu na mtu yeyote unaweza kusema ni hadithi ya kutungwa, lakini ukweli ni kwamba kuna watu huko kwenye visiwa vya Papua New Guinea ambavyo vimezungukwa na bahari inayoitwa Bismarck Sea wanakula binadamu wenzao.

Nchi hiyo yenye watu wapatao milioni 7.3 ina makabila mengi yanayotofautiana mila. Tena basi mengine yana mila mbaya na za kutisha na wanakiuka haki za binadamu kwa kiasi kikubwa. Katika mapori wanaoishi watu hao ni jambo la kawaida mtu ‘akionwa’ na wazee wa kimila kwamba ni mchawi, huteswa kwa kuchomwa na silaha zenye ncha kali lakini baya zaidi humalizwa kwa kukatwakatwa kisha kufukiwa kwenye shimo.

Yapo makabila mengi katika visiwa hivyo ambavyo vipo mashariki ya mbali, karibu na Indonesia na Australia. Baadhi ya makabila yanaishi maisha duni na ya enzi ya ujima. Kuna kabila ambalo mwanamke akifiwa na mume, hukatwa kidole kimoja, akifiwa na mtoto, hukatwa kidole kingine, huwa hivyo hata ukifiwa watoto watano, basi vidole vitano vitakatwa.


Wenyewe wanasema hiyo ni njia ya kuomboleza eti kwamba uwe na uchungu halisia baada ya kufiwa na ndugu yako wa damu, mtoto au mume. Haijaelezwa kwa nini wanaokatwa vidole huwa ni wanawake tu maana hata picha kwenye mitandao, wengi wa waliopoteza vidole wanaoonekana ni wanawake, tena wale wazee au wakongwe!

Makabila yanayofanya vitendo hivyo yameelezwa kuwa ni ya Dani na Kuru ambayo mengine yanapatikana katika nchi ya Indonesia pia. Inaelezwa inapotokea mtu amefariki dunia, mama mhusika huitwa na kuingizwa katika chumba maalum na kuulizwa anataka akatwe kidole gani.


Akionesha, kidole hukatwa bila sindano ya ganzi kwa pigo moja ya panga yenye makali na kupakwa dawa za mitishamba kisha mama aliyekatwa hutoka ndani huku akilia na ndipo waombolezaji wengine hudakia kulia kwa nguvu.Baada ya kidole kukatwa ncha iliyokatwa pamoja na kucha, huchomwa moto na wazee wa kimila huku wakiimba nyimbo za makabila yao.

Mara baada ya zoezi hilo kinachofuata na kidole kuchomwa moto na kuwa jivu kisha majivu yake huwekwa kwenye chombo maalum na baadaye hufuata zoezi la majivu hayo kupakwa nyuso za waombolezaji wote ambao wapo kwenye msiba huo.

Kwa kawaida watu hao hawavai nguo na badala yake hutumia magome ya miti na wanaume hufunika dhakari yao kwa aina fulani ya vibuyu. Kuna vibuyu vina ‘mkono’, basi hutumia mikono hiyo kuingiza kwenye dhakari na kuifunga kwa njia ya kitamaduni, lakini sehemu nyingine za eneo hilo nyetu huachwa wazi na hupita hata mbele ya watoto wao bila kuona haya!

Kwa upande wa wanawake, wao hufunika nyeti zao kwa magombe ya miti na matiti yao huachwa wazi vila kufunika chochote!

Kabila la Kuru wao kama aliyefariki dunia alikuwa ni kiongozi, basi ubongo wake hutolewa na kuliwa na wanaume.
Viewing all 104793 articles
Browse latest View live




Latest Images