Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104809 articles
Browse latest View live

KIMENUKA...Tuhuma za Watuhumiwa wa Dawa za Kulevya Kuishi Kifahari Gerezani Latinga Bungeni!!!

$
0
0
Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, imesema hakuna ukweli wowote kuwa baadhi ya watuhumiwa ambao walihusika na dawa za kulevya wanapokuwa gerezani wanaishi maisha ya kifahari.



Hayo yameelezwa leo bungeni na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Hamad Masauni wakati akijibu swali la mbunge wa Viti Maalum Faharia Hamisi aliyehoji;

Kwakuwa baadhi ya vyombo vya habari vilizungumzia kwamba baadhi ya watuhumiwa ambao walihusika na dawa za kulevya wanapokuwa gerezani wanaishi maisha ya kifahari Je, tuhuma hizi zina ukweli?

“Kuhusiana na ukweli wa tuhuma zinazosambazwa kimsingi si za kweli, nimhakikishie Muheshimiwa mbunge na wananchi kwa ujumla kuwa Jeshi la Magereza linafanya kazi zake kwa kuwasimamia na kuwahifadhi wafungwa ikiwa ni kiuwarekebisha tabia kwa umahili na uamakini wa hali ya juu,” amesema Masauni.

“Sio rahisi na sisi katika kufuatilia kwetu ambapo tumekuwa tukifanya ziara hizi mara kwa mara tumeshuhudia jinsi ambazo askari wa jeshi la Magereza zinafanya kazi yake vizuri na kwa weledi wa hali ya juu kwahiyo tuhuma hizo kimsingi sio za kweli naomba Watanzania wazipuuze.”

JESHI la Polisi Ladaiwa Kumkamata Manji Tena....

$
0
0
JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam linadaiwa kumshikilia aliyekuwa Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga, Yussuf Manji.

Taarifa kutoka ndani ya Jeshi la Polisi ziliambia MTANZANIA kuwa Manji pamoja na ofisa wake mmoja wanashikiliwa tangu Ijumaa ya Juni 30, mwaka huu ambapo inadaiwa katika moja ya ghala la kampuni yake lilihifadhi sare za Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ).


Mfanyabishara huyo Casto Ngogo (35), ambaye anatajwa kukamatwa na Manji, alipandishwa kizimbani Juni 21, mwaka huu  katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam akikabiliwa na mashitaka ya kukutwa na sare za jeshi hilo zikiwmao suruali 5,000.

Inadaiwa kuwa Juni 15, maeneo ya Bandari Kavu ya Galco, Chang’ombe, Temeke, Dar es Salaam, Ngogo alikutwa na suruali hizo 5,000 za JWTZ kwenye kontena namba PCIU 82851 (5) zikiwa na thamani ya Sh milioni 59 mali ya Serikali bila kibali.

Hatua ya kukamatwa kwa Manji inatajwa kuwa ni sehemu ya kusaidia maelezo katika kesi hiyo ambapo anahusishwa kwa maghala yake kuhifadhi sare hizo za jeshi.

Gazeti hili lilipomtafuta Msemaji wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Mussa Misalaba, alisema yupo nje ya ofisi ambapo alimtaka mwandisi kuwasiliana na Mkurugenzi wa Uchunguzi wa Takukuru, Alex Mfungo.

Alipotafutwa Mfungo kuhusu suala hilo naye alimtaka mwandishi kumtafuta tena msemaji wa Takukuru kwani ndiye anayehusika na kuzungumzia suala hilo.

“Mtafute msemaji ndiye anahusika na mambo yote mimi siwezi kuongea kwani tutakuwa tunaingiliana majukumu,” alisema mkurugenzi huyo.

Kutokana na hali hiyo gazeti hili lilirudi tena kwa Misalaba, ambapo alisema ni kweli Mkurugenzi huyo hawezi kuzungumzia suala hilo huku akimtaka mwandishi kuwa na subira kuhusu suala hilo la Manji.

“Kesho (leo) nitawatafuta wahusika na kisha nitakuambia,” alisema Misalaba.

Pamoja na hali hiyo alipitafutwa Mkurugenzi wa Takukuru, Valentino Mlowola, alisema kuwa hana taarifa za kukamtwa kwa Manji kwani yupo nje ya ofisi huku akimtaka tena mwandishi kumtafuta Msemaji wa Takukuru.

Kutokana na mzunguko huo wa Takukuru MTANZANIA ilimtafuta Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lucas Mkondya, ambapo simu yake haikupokewa wala hakujibu  ujumbe mfupi wa simu.

Inadaiwa kuwa Manji ambaye kwa sasa yupo mahabusu katika Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam kwa mahojiano zaidi, anatarajiwa kufikishwa mahakamani leo.

Februari 9, mwaka huu Manji alikamatwa  na Polisi baada ya kujisalimisha katika Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam,  baada ya kutajwa katika orodha ya watu 65 wanaodaiwa kujihusisha na dawa za kulevya.

UVCCM Wamjia Juu Sumaye na Kumchambua Kama Karanga

$
0
0

UMOJA wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi  (UVCCM), umesema Waziri Mkuu Mstaafu Fredrick Sumaye, hafahamu wala hajui dhana ya demokrasia ya vyama vingi,  jambo linalomfanya kiongozi huyo kila siku kuilaumu Serikali.

Kauli hiyo ya UVCCM, imekuja siku chache baada ya Sumaye kudai kwamba watawala wa Serikali wa sasa wanaiogopa Katiba Mpya na kugeuka kuwaandama wapinzani kwenye mfumo wa vyama vingi.

Hayo yalisemwa jana mjini hapa na Kaimu  Katibu Mkuu wa UVCCM, Shaka Hamdu Shaka, alipokuwa akizungumza na vijana wa CCM Mvomero wakati akielekea mkoani Dodoma ambapo alisema hatua hiyo ya Sumaye ya kudai kuna mfumo mgumu wa demokrasia haileti mantiki kwa sasa.

Alisema msingi wa kuruhusiwa vyama vingi nchini si kukwamisha maendeleo ya kiuchumi na kijamii au kuwafanya wananchi kila siku wakusanyike viwanjani kusikiliza mikutano ya hadhara bila kutilia maanani uzalishaji mali viwandani, mashambani na maofisini.

“Vijana wenzangu hata ligi ya soka au mashindano ya kutafuta warembo yana msimu na vipindi vyake, timu haziwezi kushiriki michuamo mwaka mzima bila wachezaji na waamuzi kupumzika, domokrasia ya wapi ambayo haina vipindi vya kampeni.

“…uchaguzi au watu kutakiwa kufanya kazi za maendeleo acheni kusikiliza poroja za wanasiasa waliochoka vijana chapeni kazi sasa ili kujiletea maendeleo endelevu,” alisema Shaka .

Alisema UVCCM imeshangazwa na matamshi ya Sumaye anayedai kuwa serikali ya awamu ya tano inakandamiza  misingi ya demokrasia kwasababu tu imevitaka vyama kuendesha shughuli za kisiasa kwenye mikutano ya ndani ili kuwapa nafasi wananchi kujituma na kuzalisha.

Kaimu huyo Katibu Mkuu alisema hata kanuni na fomula za masomo ya hesabu, kemia na baiolojia hazilingani katika kupata majawabu halisia hivyo akataka ifahamike  demokrasia nayo ina vipindi vya kampeni , mikutano ya hadhara, uandikishaji, upiga kura, kuhesabu na kutangazwa matokeo .

“UVCCM tunamfahamu Sumaye toka akiwa Naibu Waziri wa Kilimo hadi Waziri Mkuu, hana rekodi nzuri ya kiutendaji ilioleta tija, mafanikio au ufanisi katika maeneo  aliyoyaongoza, yaonyesha ni mshabiki wa hadithi kuliko kufanya kazi,” alisema.

Kutokana na hali hiyo alimtaka mwanasiasa huyo kufuta ndoto na fikra siku moja itatokea CCM kudondoka madarakani kisha yeye au mshirika wake Edward Lowassa mmoja kati yao awe urais wa Tanzania.

“Tanzania imechoka kuwa ombaomba wa kila msaada toka kwa wahisani na washirika wa maendeleo, Serikali ya CCM  imezinduma usingizini na kujitambua, haitaruhusu upuuzi usio na manufaa ili ionekane demokrasaa maana yake ni mikutano ya hadhara bila uzalishaji mali,” alisema

Manji na Mahakama Ngoma Ngumu...Hizi Ndio Sababu Zilizosababisha Akamatwe Tena...

$
0
0

Mfanyabiashara maarufu na aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga Yusuf Manji na wenzake wawili wamefungua kwa hati ya dharura maombi katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya DSM wakiomba waachiwe kwa sababu wamekamatwa isivyo halali.

Mbali na Yusuf Manji katika maombi hayo yaliyowasilishwa leo July 4, 2017 na kupangiwa mbele ya Jaji Lugano Mwandambo, walalamikaji wengine ni Deogratius Kisinda na Thobias Fwere ambapo wamefungua maombi hayo dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), George Masaju, Simon Sirro na Mkuu wa Upelelezi Kanda ya DSM.

Kwa mujibu hati ya kiapo ambayo imewasilishwa na Wakili Gudson Ndusyepo, Manji na wenzake wanaiomba Mahakama Kuu iwaachie kutokana na kukamatwa isivyo halali huku wakiiomba Mahakama hiyo kutoa amri ya kuwataka walalamikiwa wawafikishe Mahakamani ili washughulikiwe kwa mujibu wa sheria.

Katika hati hiyo, Wakili Ndusyepo amebainisha kuwa Manji na wenzake walikamatwa nyakati tofauti tofauti ambapo mlalamikaji Kisinda alikamatwa June 30, 2017 saa 10 jioni wakati Manji na Fwere walimatwa July 1, 2017 saa 5 asubuhi katika Jengo la Quality Center Barabara ya Pugu, DSM.

Manji na wenzake walikamatwa kwa tuhuma za kukutwa na sare za Jeshi katika ghala la Quality Motors Group ambapo kupitia hati hiyo ya kiapo, Wakili Ndusyepo amebainisha kuwa kukamatwa kwa walalamikaji sio halali kwa sababu kosa linalodaiwa dhidi yao linahusiana na masuala ya Kampuni ya Quality Motors ambayo inaongozwa na Wakurugenzi wake na Manji.

Mara baada ya kukamatwa kwa walalamikaji hao waliombewa dhamana lakini ilikataliwa kwa sababu zisizojulikana:”Kama Wakili wa waombaji nimefuatilia suala la dhamana hadi sasa saa 48 zimeshapita tangu walipokamatwa, lakini hawajafikishwa Mahakamani. Jambo hilo ni kinyume na sheria.” – Wakili Ndusyebo.

RAIS Magufuli Awashukia NGO's Zinazotetea Wanafunzi Wanaopata Mimba Shuleni....

$
0
0

Rais John Magufuli amezitaka Asasi za Kiraia (NGO’s) kufungua shule kwa wanafunzi wanaopata mimba shuleni kama kweli zinawapenda wanafunzi hao.


Rais ameyasema hayo leo (Jumanne, Julai 4) alipokuwa akihutubia wakati wa uzinduzi wa mradi wa maji Sengerema.


“Si kwamba nawachukia wenye mimba, hata kwa bahati mbaya akapata mimba, kama hizo NGO zinawatetea sana, zifungue shule za wenye mimba, kwa sababu zinawapenda wenye mimba, wafungue shule zao,”amesema Rais leo.


Amesema hata hao wanaofanya makongamano ya kuhamasisha watu wapate mimba wafungue shule zao kwa ajili ya wanafunzi hao.


“ Haiwezekani fedha za walipa kodi, Sh 17 bilioni kila mwaka za kusomesha watoto wetu, kwenda kusomesha wakinamama, wazunguke, waimbe, waseme nini mimi ndiyo Rais, huo ndio ukweli,”amesema.


Amesema tatizo si wanaopata mimba, kwani wapo waliopata matatizo, kama kuugua kwa muda mrefu wakashindwa kwenda shule lakini ulianzishwa mpango maalum wa kuwasomesha katika mfumo usio rasmi.

MTAZAMO... Ukitaka Kuaminiwa, Jenga Mazingira ya Kuaminika..!!!!

$
0
0

“Nina mke asiyeniamini kabisa,” aliniambia bwana mmoja hivi majuzi. “Hana imani kabisa na mimi. Juzi kati hapa nimemkuta anachunguza simu yangu. Tuligombana sana.” Nilimwuliza kwa nini anafikiri mke wake hamwamini. “Basi tu ndivyo alivyo. Hata ufanyaje hana imani.”

Sote, kama alivyo bwana huyu, tuna hitaji la kuaminiwa. Tunatamani watu wasiwe na mashaka na sisi. Tunatamani watu waamini yale tunayowaambia.

Pengine nawe, kama huyu bwana umewahi ‘kuwadai’ watu wakuamini. Umekwenda kwa rafiki, mathalani, kumkopa fedha. Rafiki yako anasita. Hakuamini. Kutokuaminiwa kunaumiza hisia kwa sababu, kama tulivyosema, kuaminiwa ni hitaji la kila mtu. Hata mwongo naye anapenda watu wamwamini.

Ufanye nini sasa??? Twende pamoja....

A. Kuaminiwa ni matokeo

Mambo mengi hayaendi bila kuaminiwa. Kazini, wakubwa wa kazi wanapenda mtu anayeaminika. Bila kuaminika, huwezi kupata mafanikio. Mfanyabiashara naye, anapoaminiwa na watu anakuwa kwenye nafasi kubwa ya kupata mafanikio.

Urafiki kati ya watu wawili, hali kadhalika, unategemea kwa kiasi kikubwa namna watu hao wanavyoaminiana. Huwezi kuwa na urafiki mzuri na mtu kama hamuaminiani. Kuaminiwa ni msingi wa mahusiano yoyote ya karibu na hata shughuli zinazohusisha watu zaidi ya mmoja.

Kuaminiwa, hata hivyo, si tukio la siku moja wala haki inayoweza kuidaiwa kwa watu. Mke hawezi kudai ‘aaminiwe’ na mume wake. Mume hali kadhalika. Kuaminika ni zao la tabia zetu. Kuaminiwa ni sawa miamala ya Benki. Unaweza kuchukua kile ulichokiweka. Huwezi kudai zaidi. Fanya mambo matatu uaminiwe.

B. Sema ukweli daima

Fikiria uko mahali na rafiki yako ukamsikia akimdanganya mwenzake kwenye simu. Hata kama aliyedanganywa ni mwingine, kwa vyovyote vile imani yako kwa aliyedanganya inapungua. Uongo unapunguza kuaminika.

Ukitaka kuaminika, jenga tabia ya kusema ukweli. Epuka kusema kitu usichomaanisha kwa lengo tu la kuwafurahisha watu. Usimdanganye mtu hata kama unajua hatagundua. Ukitambulika kama mtu mwenye tabia ya kusema ukweli unawafanya watu wasiwe na wasiwasi na maneno yako. Utaaminika.

C. Timiza ahadi zako

Ni rahisi sana kutoa ahadi hasa kama hujiamini na unatamani kuwaridhisha watu. Hata hivyo, ni vizuri kuelewa kuwa ahadi ni kipimo cha ukomavu wako. Usipotekeleza ahadi zako watu wanakuchukulia kama mtu asiye na ukomavu. Huwezi kuaminika katika mazingira unayoonekana huna ukomavu.

Kuliko kutoa ahadi kwa lengo la kumridhisha mtu, ni bora usiahidi kabisa. Punguza matarajio ya watu kwako, kisha fanya jitihada za kuzidi matarajio hayo. Unapoahidi kufanya kitu, tekeleza. Ukishindwa kutekeleza, kuwa mwuungwana. Omba msamaha. Kwa namna hii watu watakuamini.

D. Heshimu uheshimike

Mtu asiyeheshimika ni vigumu kuaminiwa. Wapo watu wanaaminiwa kirahisi kwa sababu tu wamejijengea taswira ya heshima kwa jamii. Heshima ni zaidi ya vitu ulivyonavyo na namna unavyoonekana. Heshima kubwa unayoweza kupewa na watu inategemea vile unavyowaheshimu. Ukitaka kuheshimiwa, heshimu watu.

Unapokuwa na tabia ya kuwadharau watu; kujiona bora kuliko wengine; watu wanakudharau. Hata wale unaowazidi wanastahili heshima. Hata wanaokukosea na kukutendea mabaya wanastahili heshima. Ukijenga tabia ya kulipa ubaya kwa wema utashangazwa na matokeo.

Jambo la kukumbuka ni kwamba watu wanaweza kupoteza imani na wewe kimya kimya. Si kila mtu anaweza kukutangazia kuwa hana imani na wewe. Linda sana tunda la uaminifu. Imani ikipotea, ni vigumu kuirejesha. 

E. Jifunze kwenda na muda 

Watu wengine wanashindwa kuaminiwa kwa sababu ya kutotunza au kwenda muda ipasavyo. Unaaambiwa uje muda fulani kwa mfano saa 7 kamili mchana wewe unakuja saa 8 kasoro huku ukiwa na sababu lukuki (nyingine zisizo na maana). Hii ni tofauti kabisa na wenzetu wazungu ambao wao huenda na muda kisawasawa (Sijamaanisha waafrika/watanzania wote hatuendi na muda). Kwa taarifa yako ni kuwa watu hupimwa uaminifu kwa uwezo wao wa kutumia muda vizuri.

Habari njema, hata hivyo, ni kwamba kadri unavyojiwekea mazingira ya kuaminika, ndivyo utakavyoendelea kuaminika.

"When you're honest from the beginning you don't have to lie to cover up the lie you already told. Honesty is always the best policy"

BREAKING News: Polisi wamkamata Halima Mdee nyumbani kwake

$
0
0

Mbunge wa Kawe, Halima Mdee amekamatwa na polisi wanne na kupelekwa Kituo cha Polisi cha Oysterbay saa  moja iliyopita.

Katibu wa Chadema Mkoa wa Dar es Salaam, Henry Kilewo, amezungumza majira ya  saa 12 jioni na kueleza kuwa Mdee amekamatwa akiwa nyumbani kwake Makongo Juu.

 Awali akizungumza na waandishi wa habari leo asubuhi,  Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ali Hapi aliagiza Jeshi la Polisi kumkamata mbunge huyo  kwa madai kuwa amemkashifu Rais John Magufuli.

Kamanda wa Polisi, mkoa wa Kinondoni, Suzan Kaganda amesema amefanya  hivyo kwa amri ya mkuu huyo wa wilaya.

“Wapi kakamatwa? Sisi tunachojua ni kuwa tunatekeleza agizo la DC (mkuu wa wilaya) mengine muulize kamishna wa kanda maalum, nimetimiza,” amesema.

MADHARA Ya Kuangalia Video za Ngono Na Namna Ya Kuacha

$
0
0

Kuangalia video za ngono sio jambo jipya kwa jamii yetu, kimsingi ni watu wachache sana wanaweza kujizuia kujichua au kupiga punyeto baada ya kuangalia video za ngono.

Bahati mbaya tabia ya kuangalia video hizi watu wengi huipata wakiwa wadogo sana na usipokua makini tabia hii itakufanya vibaya sana kisaikolojia.

Tabia ya kujichua sasa iko wazi kwa jinsia zote yaani wanawake na wanaume japokua imekua ikiathiri zaidi wanaume sababu ya maumbile yao.

Japo wengi hufanya kwa siri na kuficha ili wasijulikane na wengine. Vijana wengi wamekuwa wakiangalia video hizo wakiwa wamejificha wenyewe chumbani, na hasa nyakati za usiku.

Kuangalia video za ngono kuna madhara mbalimbali ya kiafya na kisaikolojia. Haya hapa ni baadhi ya madhara unayoweza kuyapata kama utaangalia sana video za ngono.
Kuishiwa hamu ya tendo la ndoa na nguvu za kiume

Kuangalia sana video za ngono hukufanya ushindwe kusisimuliwa na mwanamke au mwanaume wa kawaida, video za ngono zina wanawake na wanaume wazuri sana ambao wako vile sababu ya kufanyiwa upasuaji mbalimbali wa kuongeza makalio na matiti, hata wanaume hufanyiwa upasuaji wa kuongeza uume hivyo mwanamke anayeangalia atatamani uume mkubwa kama ule au mwanaume anayeangalia atatamani mwanamke kama yule ambaye katika mazingira ya kawaida hayupo.

Sasa wanaume wanao angalia video za ngono hawawezi kusisimka au kuamsha uume hata mwanamke wa kawaida akipita uchi na hii huweza kuathiri sana mahusiano yao na kuonekana hawana nguvu za kiume kwani wao hutegemea video hizo kuamsha uume.

Kujichua au kupiga punyeto sana
Video za ngono zina wanawake na wanaume tofauti, kila video nzuri unayoangalia utaenda kujichua huku ukimuwaza wanaume au mwanamke husika. Hii itakufanya ujichue hata mara kumi kwa siku kama unaziangalia mara kwa mara. Kuishiwa nguvu za kiume, kusahau sana, kushindwa kumpa mwanamke mimba, kuchoka sana na kufika kileleni haraka wakati wa tendo la ndoa ni moja ya madhara makuu ya punyeto.

Kushindwa kudumu kwenye mahusiano
Kuangalia video za ngono hukufanya uwaze kujiridhisha mwenyewe tu na hata mwenza wako akitaka kulala na wewe unakua hutaki tena. Lakini hata kwa vijana ambao hawako kwenye mahusiano hujikuta wanakua waoga sana kuwafuata wanawake au wasione sababu ya kua kwenye mahusiano. Vile vile wanaume hushindwa kuwaridhisha wenza wao na wanawake kusingizia kuchoka kila siku.

Kuanza kufanya ngono ambazo sio za kawaida
Hivi karibuni idadi kubwa ya wanawake wamekua wakijihusisha sana na mapenzi ya kinyume na maumbile. Hii imesababishwa sana na kuangalia video za ngono na kuona ni kitu cha kawaida wakati kina madhara mengi. Wanawake waliozoea kuingiliwa nyuma hata wakiolewa huendelea kufanywa na wanaume wa nje hasa kama waume waliowaoa hawajawahi kujihusisha na tabia hiyo. Aina zingine za ngono ambazo zinababishwa na tabia ya kuangalia video hizi ni ushoga, usagaji, au mwanamke kulala na wanaume zaidi ya mmoja au mwanaume kulala na wanawake zaidi ya mmoja kwa wakati mmoja.

Inawezekana wewe unayesoma hapa tayari hii tabia inakuumiza sana kwa sasa na umeshindwa kuiacha, kuna mambo ya msingi unaweza kufanya ili uweze kuacha kuangalia video hizi..

Ondoa zana zote za kuangalia video hizi
Kama una tarakilishi (computer) au simu futa video zote, futa tovuti (website) zote za video ambazo unazitumia kuangalia. Kuna watu wamo kwenye makundi ya WhatsApp ya kutumiana video za ngono, ondoka kabisa huko kwani unajiharibu.

Anza kufanya mazoezi
Ni mazoezi pekee yanayoweza kumfanya mtu aweze kuachana na tabia zote ambazo sio za kawaida ambazo alikua anazifanya kipindi cha nyuma. Unapofanya mazoezi utatumia nguvu nyingi na mwili wako utachoka na kupata usingizi. Vilevile ufanyaji wa mazoezi hukuepusha na kukaa bila shughuli yoyote.

Jijengee tabia ya kukaa na marafiki zako muda mrefu au kufanya shughuli nyingine zitakazokuweka ‘busy’

Kama una tabia ya kuangalia video hizi basi, fanya mpango uwe unafanya mambo mengine muda ambao umekua ukiangalia hizi video, ikiwemo kusoma vitabu au kuongea na watu. Hii itakusaidia kusahau video hizo na kuacha kabisa.

Pata ushauri wa kitaalamu na matibabu
Unaweza kumuona mtaalamu wa ushauri wa kisaikolojia ili kukusaidia ushauri wa namna ya kufanya ili kuepukana na tabia hiyo. Kama umeshapata madhara kiafya, basi waone wataalamu wa afya hasa masuala ya uzazi ili wakushauri namna ya kulitibu tatizo lako.

Jenga mahusiano ya karibu na mpenzi wako
Hii itakusaidia kumuwaza yeye zaidi ya video za ngono na pia pale unapopata hamu ya kufanya mapenzi basi hutoogopa kumwambia ili mfanye. Kuwa karibu na mpenzi wako kutakujengea ujasiri na kuyakuza mahusiano yenu.

KIMENUKA..Wafanyakazi Flyover Tazara Wagoma

$
0
0

WAFANYAKAZI wa kampuni ya LABA Construction Ltd ambao ni vibarua wa kampuni ya Sumitomo Mitsui Construction company Ltd inayojenga barabara ya juu (Flyover) ya Tazara wamegoma wakishinikiza kuongezwa maslahi yao pamoja na kuitaka kampuni ya Laba kuondoka.

Wafanyakazi hao walianza mgomo kuanzia siku ya jana ambapo wanaitaka kampu ni ya Laba ambayo wanadia inafanya kazi ya udalali kuondoka kwa kuwa ndio inawanyonya kwani kampuni ya Sumitomo imekuwa ikilipa Sh 37,000 kwa fundi na kibarua Sh 25,000 lakini kampuni hiyo imekuwa ikilipa Sh 14,000 kwa fundi na Sh 10,000 kwa kibarua.

Akizungumza kwa niaba ya wenzake mmoja wa wafanyakazi hao Jackson Mselemu amesema, wanachodai ni kutaka kuongezewa maslahi n akwamba wanataka yalipwe moja kwa moja bila kuwepo mtu wa kati ambayo ni kampuni ya LABA.

"Hii kampuni ya LABA ndio inatudhulumu , tunakatwa hela za PPF lakini tumeenda kuuliza tunaambiwa hakuna hela iliyowahi kupelekwa kuele, kwa hiyo sisi tunaomba mtusaidie, lakini pia hatutaki fedha zetu zilipwe kupitia Tigo Pesa, tulipwe kwa njia ya benki," amesema Mselemu.

Naye Hussein Bakari amesema, kwenye mfuko wa PPF wameambiwa kampuni ya LABA haitambuliki hivyo ni vyema wakarudi kwa mwajiri wao ili wapate ufafanuzi mzuri, lakini hakuna pesa  yoyote iliyopelekwa kwa ajili yao.

Mashaka Nyerere amesema, hawajagomea kazi bali wanachokigomea ni maslahi kwa kuwa malipo wanayoyapata hayaendani n akazi wanazofanya. Alisema kazi wanazofanya ni ngumu na zinafanywa katika maeneo ya hatari, lakini maslahi wanayopokea ni mabovu.

"Sisi tuko tayari kufanya kazi lakni tunataka hii kampuni ya udalali ya LABA iondoke tuko tayari kufanya kazi tukalipwa hata Shilingi elfu kumi na Mjapani, kwasababu tunajua tutambana wapi kuliko huyu mswahili," amesema Nyerere.

Kwa mujibu wa mkataba baina ya kampuni ya LABA na mfanyakazi unaonesha malipo ya kazi kwa saa ni Sh 1,250, kwa siku Sh 10,000, malipo baada ya muda wa kazi kuisha Sh 1,875 kwa saa na siku ya jumapili na sikukuu Sh 2,500 kwa saa huku ikiwa na sehemu ya kujaza namba ya simu iliyosajiliwa na Tigo Pesa.

IMEBAINIKA Sababu ya Rais Magufuli Kutotaka Kusafiri nje ya Nchi

$
0
0
Rais John Magufuli amesema amepata mialiko zaidi ya 60 kwenda nje ya nchi baada ya kuwa Rais lakini ameikataa kwa sababu anataka kuishughulikia Tanzania kwanza.

Ameyasema hayo jana (Jumanne Julai 4) wakati akihutubia wakazi wa Sengerema katika uzinduzi wa mradi wa maji Sengerema.

Rais Magufuli amesema hana haja ya kwenda nje ya nchi kwa sababu bado ana mzigo mkubwa wa kumaliza ufisadi.

“Niende nje kufanya nini wakati ntaenda tu nikishastaafu, nataka nimalize kwanza haya ya hapa ndani,” alisem

UAMUZI wa Kikao Cha Kamati Ya Utendaji ya Shirikisho la soka nchini TFF

$
0
0
Kamati ya Utendaji (EXCOMM) ya Shirikisho la soka nchini TFF, ilikutana jana Jumanne Julai 4, 2017 katika kikao cha dharura ambako ilijadili mgawanyiko katika Kamati ya Uchaguzi ya TFF.

Kamati hiyo ya utendaji ilikutana kwa dharura kwa mujibu wa Ibara ya 35 (1) ya Katiba ya TFF inayosomwa pamoja na Ibara ya 35 (6). Kikao cha Kamati hiyo kilianza saa 8.58 alasiri hadi saa 10.51 jioni.

Katika kikao chake kilichofanyika katika Ukumbi wa Ofisi za shirikisho, Karume jijini Dar es Salaam Kamati iliamua kufanya mabadiliko madogo katika Kamati zake za Kisheria na Kamati za uchaguzi kwa mujibu wa Katiba Ibara ya 44 (7) na Ibara ya 52 inayotoa mamlaka ya kufanya mabaduiliko hayo.

Katika Kamati ya Uchaguzi, EXCOMM imeteua Mawakili kuongoza kamati hiyo wakiongozwa na Msomi Wakili Revocatus Kuuli; Mheshimiwa Wakili Mohammed Mchengelwa; Msomi Wakili Malangwe Mchungahela; Msomi Wakili Kiomoni Kibamba na Msomi Wakili Thadeus Karua.

Katika Kamati ya Rufaa Uchaguzi, EXCOMM imeteua Msomi Wakili, Abdi Kagomba kuwa Mwenyekiti wakati Makamu Mwenyekiti ni Msomi Wakili Kenneth Mwenda na wajumbe ni Msomi Wakili  Rashid Sadalla, Mhe. Jabir Shekimweri na Mohammed Gombati.

Kadhalika katika kamati za kisheria za TFF, ikianzia Kamati ya Maadili, EXCOMM imeteua Msomi Wakili Hamidu Mbwezeleni kuwa Mwenyekiti wakati Makamu Mwenyekiti ni Msomi Wakili Steven Zangira na wajumbe ni Mhe. Glorius Luoga, Walter Lungu na Amin Bakhressa.

Kamati ya Rufaa na Maadili, EXCOMM imeteua Msomi Wakili Ebenezer Mshana kuwa Mwenyekiti wakati Makamu Mwenyekiti ni Naibu Kamisha katika Jeshi la Polisi (DCP), Mohammed Mpinga na Wajumbe ni Msomi Wakili Benjamin Karume; Dk. Lisobine Kisongo na Mrakibu Msaidizi wa Polisi – ASP Benedict Nyagabona.

Kamati ya Nidhamu ya TFF, EXCOMM imeteua Tarimba Abbas kuwa Mwenyekiti wakati Makamu Mwenyekiti ni Peter Hella huku Wajumbe wakiwa ni Boniface Lyamwike, Dk. Billy Haonga na Kassim Dau.

Kamati ya Rufaa ya Nidhamu, EXCOMM imeteua Wakili Msomi, Rahim Shaban kuwa Mwenyekiti wakati Makamu Mwenyekiti ni Siza Chenja huku Wajumbe wakiwa ni Abbas Mtemvu; Amani Mulika, Amin Bakhressa na Stella Mwakingwe.

NILIIBIWA sana Facebook – Mch Anthony Lusekelo Afunguka

$
0
0
Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC), Anthony Lusekelo maarufu kama ‘Mzee wa Upako’ amefunguka kuwa yeye ni moja ya Wachungaji ambao wapo nyuma sana kwenye mitandao ya kijamii na kukiri kuwahi kuibiwa kwenye mtandao wa Facebook na watu wanaotumia jina lake.

 

Mzee wa Upako amesema kutokana na kuwa na elimu ndogo ya mitandao ya kijamii amewahi kuibiwa na watu mitandaoni waliokuwa wanawatapeli waumini wake kwa kutumia jina lake na kuwaomba watu hela.

“Nina akaunti ya Instagram na nimewafuata watu wanne tuu Magufuli, Jakaya, BBC na vyombo vingine vya habari….(kuhusu Facebook) kule niliibiwa sana kuna watu walikuwa wanatumia jina langu wanajiita Mzee wa Upako na kuwachangisha watu pesa,” amesema Mch. Antony Lusekelo kwenye mahojiano yake na kipindi cha Chomoza cha Clouds TV.

Hata hivyo Mzee wa Upako amesema kwa sasa kwenye simu yake hakuna hata Group moja la WhatsApp huku akidai kuwa wingi wa simu za kawaida zinazoingia ndiyo unamfanya asijiunge na makundi hayo kwani yanamaliza chaji.

RAIS Magufuli Asitisha Utoaji wa Leseni za Uchimbaji Madini

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli ameiagiza Wizara ya Nishati na Madini kusitisha utoaji wa leseni mpya za uchimbaji halikadhalika leseni ambazo zimeisha muda wake.



Soma taarifa kamili:

Rais Magufuli ametoa maagizo hayo alipokuwa akizungumza na wananchi wa Geita ambao walizuia msafara wake katika maeneo mbalimbali wakati akiwa njiani kuelekea Chato.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 4 Julai, 2017 amehitimisha ziara yake ya kikazi ya Siku Mbili Mkoani Mwanza kwa kuzindua mradi wa Uboreshaji wa huduma ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira katika kijiji cha Nyamazugo Wilayani Sengerema.

Mradi huo wa maji umetekelezwa chini ya mpango wa maji wa Kamisheni ya Bonde la Ziwa Victoria ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa ufadhili wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) kwa gharama ya shilingi bilioni 22.4. Mradi wa Maji Safi mjini Sengerema ulioanza tangu mwaka 2011 unatarajiwa kuwahudumia wakazi 138,000 ifikapo mwaka 2030.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Mradi huo, Mhe. Rais Dkt. Magufuli amesema kukamilika kwa mradi huo kutamaliza tatizo la maji la muda mrefu kwa wakazi wa Sengerema na maeneo ya jirani.

Mhe. Rais Dkt. Magufuli amewataka wananchi wanaozunguka mradi huo kuutunza na kuhakikisha hawaharibu vyanzo vya maji katika eneo hilo la ziwa Victoria ikiwa ni pamoja na kuacha uvuvi haramu ambao umekuwa na madhara makubwa kwa wananchi.

Aidha, ameuagiza uongozi wa Mkoa wa Mwanza na Vyombo vya Dola kuchukua hatua kali dhidi ya watu wanaochafua vyanzo vya maji katika eneo la Ziwa Victoria.

Katika hafla hiyo ya Uzinduzi wa mradi wa maji Kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo – CHADEMA HamisiHussein Maarufu TABASAM, ameamua kuachana na chama chake na kujiunga na CCCM.

Mhe. Rais Dkt. Magufuli ameendelea kusisitiza msimamo wa Serikali kuwa hakuna mwanafunzi atakayepata ujauzito ataruhusiwa kuendelea na masomo na ameyataka Mashrika yasiyo ya Kiserikali ambayo yamekuwa yakipinga uamuzi huo kufungua Shule zao wenyewe ambazo zitawasomesha wanafunzi wanaopata ujauzito.

“Haiwezekani Serikali itoe pesa kuwasomesha wanafunzi halafu wapate mimba waendelee na masomo hilo haiwezekani, hizo NGOs zinazotetea hali hiyo zikitaka zijenge shule kwa ajili ya kuwasomesha wanafunzi watakaopata ujauzito”amesema Rais Magufuli.

Mhe. Rais Magufuli amezungumzia uamuzi wa Serikali kupeleka Miswada Mitatu ya dharura Bungeni kuwa unatokana na umuhimu wa hilo katika kutetea maslahi mapana ya nchi na kuhakikisha rasilimali za nchi zinawanufaisha wananchi.

Mhe. Rais Magufuli amewaonya wanachama wa Chama cha Mapinduzi CCM wenye nia ya kugombea nafasi mbalimbali katika Uchaguzi wa Chama hicho kutojihusisha na rushwa kwa vile rushwa ni adui wa haki, hivyo, atakayebainika kutumia rushwa atapoteza sifa ya kuwa Mgombea.

Akizungunzia ujenzi wa barabara ya kutoka Kamanga hadi Sengerama kwa kiwango cha lami, Mhe. Rais Dkt. Magufuli amesema kwa sasa Serikali imeshampata mkandarasi kwa ajili ya kufanya upembuzi yakinifu na usanifu ili barabara hiyo ianze kujengwa katika kutimiza ahadi aliyoitoa wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.

Rais Magufuli pia amewataka Wakuu wa Mikoa na Wilaya nchni kufafanua kwa wananchi na kusimamia uamuzi wa Serikali wa kufuta tozo zaidi ya 80 katika mazazo ya Kilimo, tozo 7 za Mifugo na tozo 5 za Uvuvi ambao lengo lake ni kuwaondolea kero wananchi.
Aidha, amesema Serikali inafanya uchambuzi ili kubaini wale wote waliotoa pembejeo hewa na atakayebainika atachukuliwa hatua kali za kisheria.

Wakati huo huo, Mheshimiwa Rais Magufuli ameiagiza Wizara ya Nishati na Madini kusitisha utoaji wa leseni mpya za uchimbaji na halikadhalika leseni ambazo zimeisha muda wake. Ametoa maagizo hayo alipokuwa akizungumza na wananchi wa Geita ambao walizuia msafara wake katika maeneo mbalimbali wakati akiwa njiani kuelekea Chato.

Jaffar Haniu
Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Sengerema,Mwanza
04 Julai 2017.

Kutana na Mtabibu Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH CHIEF SULTAN MAKATA Mtabibu wa Nyota za Binadamu na Dawa za Asili ya Africa

$
0
0
Kutana  na Mtabibu Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH CHIEF SULTAN MAKATA Mtabibu wa Nyota za Binadamu na Dawa za Asili ya Africa Mwenye UWEZO Kubaini tatizo lako Pindi tu Utakapo Fanya Mawasilino Kupitia Wasaa Husika

Anatibu kwa Njia ya Simu Ukiwa Nchi Yoyote / Mkoa wowote
..JE UNASUMBULIWA NA Mapenzi? (Umeachwa na Umpendae,Awe Mume,Mke na Bado unampenda?Na  Umejaribu Sehemu nyingi Bila Mafanikio?Wasilina na Chief Sultan Ujione muujiza wa Papo kwa Papo..

anauwezo WA KURUDISHA MAHUSIANO NA KUIMARISHA NDOA YAKO NDANI YA SAA 12 TU(LIMBWATA). Umekimbiwa na Mumeo,mkeo au Mpenzi na anaishi na mtu mwingine?Una Mpenzi wako ana Pesa na Unataka kumkamata? Muone akutatulie Anauwezo wa Hali ya Juu wa Kusambalatisha Mahusiano yao Endapo utafata Atakacho kuelekeza.
Atamfanya Atimize Ahadi zote kwa Muda Mfupi.

Chief Sultan Anatumia Jina la Muhusika au Picha Kumaliza Tatizo lako..
Anatibu kwa Kutumia  Vitabu vya QUR-AN Dawa za Asili za Africa,Dawa za Kiarabu na Majini.Anatafsiri Ndoto. Kushinda BAHATI NASIBU, KUSAFISHA NYOTA,Hutoa  PETE ZA BAHATI inayoendana na NYOTA YAKO. Mvuto wa Mwili na BIASHARA, Kinga ya Mwili,ZINDIKO za Nyumba.HUZUIA CHUMA ULETE NA KUKUPA DAWA YA KUONGEZA FAIDA KWENYE BIASHARA. HURUDISHA MALI ZILIZOPOTEA AU KUDHULUMIWA.MIGUU Kufa GANZI.Kufungua KIZAZI kwa wale walio fungwa kwa njia za KISHIRIKINA. Anakupa Jini la Mali kwa yule anaehitaji Utajiri BILA MASHARTI.Humaliza Kabisa Tatizo la Nguvu za KIUME na Kurefusha Uume kwa Saizi Unayotaka,HUMALIZA KESI YA AINA YOYOTE NDANI YA SIKU 14. na mengi zaidi

Whatsapp/Calls +255 710 279 458
 Call+255 710 279 458

Tiba ni kwa Watu wenye Imani na Dini zote

ZITTO :Amri ya Mkuu wa Wilaya Kumkamata Halima Mdee ni Mwendelezo wa Matumizi Mabaya Madaraka

$
0
0

Anaaandika Mbunge Zitto Kabwe. 
Amri ya Mkuu wa Wilaya Kinondoni kumkamata Mbunge Halima James Mdee ni mwendelezo wa matumizi mabaya ya madaraka. Inasikitisha Sana kuona viongozi vijana wanafanya mambo ya hovyo Kabisa. Sheria ya DC kumweka mtu kizuizini Ina masharti yake na haihusiani kabisa na yanayoitwa makosa ya ndugu Halima Mdee. Tunapaswa kulaani Kwa nguvu Sana mambo haya kwani yataota mizizi na kuathiri watu wengi zaidi

WANAMUZIKI wa Kike Maarufu Marekani Waangukia Mapenzi Kwa Mabilionea wa Kiaarabu...Kunani?

$
0
0
Siku za karibuni wanamuziki maarufu wa kimarekani wameangukia kimapenzi kwa Mabilionea wa kiaarabu, Rihanna mwimbaji maarufu huko Marekani ameangukia na penzi kwa bilionea wa kutoka huko Saudh Arabia Hassan Jammel ambaye pia ni mwenyekiti wa kampuni kubwa inayohusika na biashara ya magari ya Toyota huko mashariki ya kati. Mwanamziki mwingine Janet Jackson alifunga ndoa Bilionea Al Mana wa Qatar lakini baada ya kupata mtoto mmoja ndoa hiyo ilivunjika inadaiwa baada ya ndoa hiyo kuvunjika Janet Jackson anategemea kupokea dola milioni 500 kama fidia ya talaka.

Kuna uwezekano hawa wanamuziki wamegundua jinsi ya kuchuma utajiri wa haraka kutoka kwa hawa Mabilionea waarabu kwani Rihanna atakapokwenda kuishi na mume wake huko Saudi Arabia atatakiwa kuvaa mavazi ya kiislam na ni jambo hataliweza.

JOB Ndugai, Kama Bunge Limekushinda si Ujiuzulu tu?

$
0
0
Bunge hili la sasa limejaa vituko, chuki na kufitiniana kwa kiwango ambacho hakijapata kutokea huko nyuma. Sasa imefikia wabunge wanaombeana mabaya na kufikia kutaka kuzichapa kavukavu.

Hii ni dalili mbaya kuwa uongozi umeshindwa kuliweka pamoja Bunge kwa manufaa ya wananchi. Na kitendo cha wabunge kumsusia futari spika ni salamu kuwa amekuwa adui yao.


Kama hali sio nzuri sii ujipumzishe ili kulinda heshima maana yanayofanyika bungeni hayajawahi kutokea kwa watangulizi wako.

By Chakaza/Jamii Forums

Hizi Ndio Dalili za Mwanaume Kuwa ni Shoga

$
0
0
Siku hizi wanaume wengi wamekuwa na tabia mbaya za ushoga ..wengine wanaonyesha live wengine wanajificha ficha ila kuna dalili unaweza kujua kuwa ana tabia hizi ,,,Hizi ni Baadhi tu ukiona mvulana ana tabia hizi basi anza kumchunguza vizuri inawezekana kabisa kuwa si ridhiki...
-------------------------
1. Kutia kalikiti kichwani
2. Kujichubua
3. Kutinda nyusi/kujiangalia sana kwenye kioo
4. Kutoboa pua/sikio
5. Kupaka lip shine
6. Kuvaa nguo za kuacha mattako nje
7.Umbea
8.Kupigana vijembe
9.Kupenda taarabu
10. Kurembua macho/Kulegeza sauti
11.Endeleza.......


Ni ipi kati hizo umewahi kuziona kwa Kidume?

Nafasi za Ajira zilizotangazwa leo

$
0
0

KOREA Kaskazini ni Noma ...Yasema Kombora lao Linauwezo wa Kufika Marekani

$
0
0
Korea Kaskazini ilitoa picha za kombira hilo la masafa marefu ICBM likirushwa

Marekani imethibitisha kwamba Korea kaskazini ilifanyia jaribio kombora la masafa marefu ambalo kulingana na wataalama wanaamini linaweza kufika Alaska Marekani.

Waziri wa maswala ya kigeni amelitaja jaribio hilo kuwa vitisho vipya kwa Marekani na dunia na kuonya kwamba Washington haitakubali hatua ya Korea Kaskazini kujihami na nyuklia.

Pyongyang imedai siku ya Jumanne kwamba ilifanikiwa kulifanyia majaribi kombora lake la masafa marefu ICBM.

Wakijibu, Marekani na Korea Kusini zilirusha makombora kusini mwa maji Korea.
Zoezi hilo la kijeshi la pamoja lililenga kuonyesha uwezo wa mashambulizi ya mataifa hayo mawili, Pentago imesema.

Ijapokuwa jaribio la Jumanne lilionekana kuwa hatua kubwa ,wataalam wanaamini kwamba Korea kaskazini haina kombora la masafa marefu la kinyuklia.

Bwana Tillerson pia alionya kwamba taifa lolote ambalo linasaidia kiuchumi na kijeshi Korea kaskazini ama limefeli kuidhinisha kwa ukamilifu maamuzi ya baraza la usalama ya Umoja wa Mataifa linasaidia utawala hatari.

Marekani imetaka kufanyika kwa mkutano wa dharura wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kujadili swala hilo.

Mkutano wa faragha wa wanachama wa baraza hilo unatarajiwa baadaye siku ya Jumatano.

Je Korea kaskazini ilisema nini siku ya Jumanne?

Tangazo hilo katika runinga ya taifa ya Korea kaskazini lilisema kuwa kombora hilo aina ya Hwasong -14 linaloweza kurushwa kutoka bara moja hadi jingine lilisimamiwa na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un.

Ilisema kuwa kombora hilo liliruka umbali wa kilomita 2,802 na kusafiri kwa umbali wa kilomita 933 kwa dakika 39 kabla ya kuanguka baharini.

Korea Kaskazini imesema kuwa ni taifa lililojihami kinyuklia ambalo linamiliki kombora la masafa marefu linaloweza kushambulia eneno lolote duniani.

Marekani na Korea Kaskazini nini kimebadilika?

Chombo cha habari cha Korea kaskazini KCNA baadaye kilimnukuu Kim jong un akisema kuwa jaribio hilo ni zawadi kwa Wamerakani siku yao ya uhuru.

Jaribio hilo ambalo ni miongoni mwa majaribio ya makombora yake linakiuka marufuku ya baraza la usalama la Umoja wa Mataifa.

Lakini wataalam wengi wanaamini kwamba Pyongyang bado haijakuwa na uwezo wa kutengeza kichwa cha kinyuklia kinachoweza kutosha katika kombora la masafa marefu na kwamba kombora kama hilo haliwezi kushambulia eneo linalolenga.

Je kombora hilo lina uwezo wa kusafiri umbali gani?

Swala kuu ni linaweza kusafiri kwa umbali gani, alisema mwandishi wa BBC Evans Seoul.
Je linaweza kushambulia Marekani?.

David Wright , kutoka muungano wa kisayansi anasema kuwa iwapo ripoti hiyo ni ya sawa ,kombora hilo linaweza kusafiri kwa umbali wa kilomita 6.700.

''Umbali huo unaweza kulifanya kufika Alaska, lakini sio visiwa vya Hawaii ama hata majimbo mengine 48 ya Marekani'',alisema.

''Sio kombora pekee ambalo Korea Kaskazini itahitaji'', mwandishi huyo anasema.

Pia ni lazime iwe na uwezo wa kulinda kichwa cha nyuklia kinapopaa angani na sio wazi iwapo Korea kaskazini ina uwezo huo.
Viewing all 104809 articles
Browse latest View live




Latest Images