Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104795 articles
Browse latest View live

MBOWE Usipobadili Aina ya Siasa CHADEMA Hakika Tutakudai na 2020 Mtaangukia PUA Tena....

$
0
0
Naomba juu ya hili nitumie nafasi hii kimshauri kamanda wangu kubadili aina ya siasa anayotaka kwenda na utawala wa awamu hii. Sina mashaka kabisa na ufundi wa siasa kwenye kichwa cha Kamanda Mbowe lakini naona kama kuna mtu anamshauri sivyo.

Nisiwe mnafki na uzi huu usiwe chanzo wa kufungua midomo ya maadui wakubwa wa CHADEMA wasiompenda Mbowe na wanachema kwa ujumla.Ni kazi nzuri sana anayofanya Mh Mbowe lakini muda unakimbia, CCM wameamua kutumia mikutano yao kujinadi kwa koti la ziara za Serikali.Hii siao sawa.


Kwa bahati mbaya sana niko nje ya nchi kwa kuda kidogo kunoa ubongo na ningekua nyumbani pasinashaka ningeufikisha ujumbe huu kwa mdogo moja kwa moja, naomba nieleweke hivyo.Ningemweleza Mh Mbowe kila kitu na namna ya kukabiliana na CCM.


CHADEMA kuna front lines nzuri sana za vijana haraka wa kazi walioiva kisiasa mfano kina Halima Mdee,Lundu Lissu,Boniface Jacob,John Mnyika Heche ,Kigaila,Waitara ,Salum Mwalimu,Sugu,Bint Peneza,Godbless Lemma,Davidi Kafulila, Petter Lijualikali na makamanda wengineo. Hawa wakipewa mwelekeo mzuri ni watu wasioogopa kusonga mbele.Hawa ni vijana jasiri sana wanao uwezo wa kubadili taswira ya Chama nchi nzima mwezi mmoja tuu.Operation ya kukieneza chama inaweza kubuniwa vizuri kwa kuangalia mazingira,wakati na aina ya utawala tulip nao.Je,hili Mbowe analifikiria?


Tafadhali sana Mbowe, umma wa watanzania hauitegemei CCM kuwasemea matatizo yao zaidi ya Upinzani. Usipooze hivyo my brother, msijipe moyo kwa kusema mko vizuri ilihali kugikia 2020 ni kesho tu.


Najua watu watauliza kua siasa hizi zitafanikiwa vipi ikiwa mikutano imezuiliwa? Tutambue kua kufanya mikutano ya siasa ni utaratibu wa katiba ya nchi na sio maelekezo ya mtu binafsi,hatujazoea kuishi bila kufuata sheria. Sheria iko wazi, kinachwafanya kulalamikia nyoyoni ni kitu gani? Kwani mkifanya mikutano kwa kufuata taratibu za kisheri mtazuiliwa kwa sababu zipi ikiwa wao CCM wanafanya?


Ustaarabu mnaotaka kuuonesha kuepusha siasa za malumbano Mh Mbowe usitegemee kama mtaupata ustaarabu kutoka CCM, hawana utani wanatazama weakness zenu. Mkipigwa mkwara nanyi mnakaa kimya ndivyo mnavyojimaliza wenyewe.

Hebu mniambie nijue kitu kimoja, kama Pole pole anazunguka na kufanya mikutano ya hadhara maeneo mbali mbali ya nchi...Je, akitoka Benson Kigaila au Tumain Makene nae akaifanya hivyo kwani iwe kosa? CCM sio chama? CHADEMA sio chama?
Woga wako Mh Mbowe usiwaambukize hawa vijana wapambana. Wagawie majukumu wewe ukiwa msimamizi mkuu kazi oende. Siasa za kukaa kimya unabaki kilalamikia chini so siasa hizo.

By Mahanju/JF

JOHN Cheyo Apigilia MSUMARI "Rais Mwinyi Yuko Sahihi, Magufuli Anastahili Kuongezewa Muda wa Kuongoza

$
0
0
Kwa upande wangu pia nauungana na Rais Mstaafu Mwinyi na John Momose Cheyo pamoja na wananchi wengi wanaopenda Rais Magufuli afikiriwe zaidi ya awamu mbili za kuongoza. Rais Magufuli anafanya kazi iliyotukuta na kwa kasi ya ajabu... Huku mitaani mamillioni ya wananchi wanakubaki utendaji wa Rais Magufuli

JE WEWE Mdau Unamkubali?

VIDEO:Hali Ngumu ya Maisha Yasababisha JOTI Kumkana Mwanae

$
0
0
Ama kweli ng’ombe wa masikini hazai na asiye na bahati habahatiki, ndicho kilichomtokea Mjomba Nishai wakati anadhani matatizo yake yamekwisha baada ya kuokota burungutu kumbe doooh mzigo wa watu.

VIDEO:Nikki Mbishi Atoa Video na Kuwadiss Waliodai Kutekwa, na Bashite

$
0
0
Mwanamuziki wa miondoko ya kufoka foka, Nikki Mbishi au muite Baba Malcom amechia video ya wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la Kama Unatafuta Kiki.

Wimbo huu umewa-diss wasanii mbalimbali nchini ambao anadai kuwa wanafanya mambo ili wapate kiki.

Ngoma hii imeongozwa na Gruzzie Prfect na audio kafanya Ghetto Ambassador

TAIFA Stars Yawapa Watanzania Zawadi......

$
0
0
Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ imeibuka mshindi wa tatu katika michuano ya Kombe la Castle Cosafa 2017 baada ya kupata ushindi wa magoli 4-2 dhidi ya Lesotho nchini Afrika Kusini.

Magoli hayo yaliyofungwa kwa mikwaju ya penalti baada ya mechi kumalizika dakika 90 kwa sare ya bila kufungana.

Katika mchezo huo uliochezwa katika Uwanja wa Moruleng, Kipa wa Taifa Stars, Said Mohamed alifanya kazi ya ziada kuokoa mashuti mengi yaliyolisakama lango la Stars, ikiwa ni pamoja na kuokoa mkwaju mmoja wa penalti.

Taifa Stars ilikuwa ya kwanza kupiga mkwaju wa penalti kupitia Shiza Kichuya ambaye alipaisha mkwaju huo.

Hata hivyo, Lesotho nao walipoteza penalti mbili, ambapo moja iligonga mwamba wa pembeni na kutoka nje huku nyingine ikiokolewa na kipa wa Stars, Said Mohamed.

Vijana wa Stars waliofunga mikwaju ya penalti ni Himid Mao, Simon Msuva, Abdi Banda huku Alpha akimalizia mkwaju wa mwisho na kuipa furaha Stars.

Taifa Star imeingia kwenye kusaka nafasi ya tatu baada ya kufungwa na Zambia goli 4-2.

EDWARD Lowassa Aguswa na Kifo cha Waziri wa Usalama wa Kenya

$
0
0
Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa ametuma salamu la rambirambi kufuatia kifo cha Waziri wa usalama wa Kenya, Meja mstaafu Joseph Nkaissery aliyefariki ghafla katika hospitali ya Karen iliyopo Nairobi muda mfupi baada ya kupelekwa kwa uchunguzi.

Meja Joseph Nkaissery alipelekwa hospitali kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa kiafya kabla ya umauti kumkuta, Mkuu wa Utumishi wa Umma wa Kenya Joseph Kinyua amethibitisha kutokea kwa kifo cha Waziri wa Ulinzi wa Kenya.

Baada ya taarifa hizo kusambaa Waziri Mstaafu Edward Lowassa amesema Nkaissery alikuwa ni rafiki mzuri na kiongozi mzuri na wakupigiwa mfano

"Natuma salamu zangu za pole kwa familia na watu wa Kenya kwa kumpoteza Waziri Joseph Nkaissery, alikuwa ni rafiki mzuri na kiongozi mzuri wa kupigiwa mfano, Mungu amumlaze mahali pema peponi" alisema Lowassa

Joseph Kasaine Ole Nkaissery alikuwa ni mwanasiasa wa Kenya, Mbunge kutoka mwaka 2002 mpaka 2014 na baadaye aliteuliwa kuwa Waziri wa usalama wa Kenya mpaka kifo chake, mbali na hilo Nkaissery alikuwa kiongozi Mkuu wa jamii ya Maasai nchini Kenya.

MBWANA Samatta Kabadilishiwa Namba ya Jezi KRC Genk

$
0
0
STRAIKA Mbwana Samatta wa KRC Genk ya Ubelgiji kuanzia msimu ujao atavaa jezi namba 10 katika kikosi hicho akiachana na namba 77 aliyokuwa akiivaa tangu alipojiunga nao.
Samatta ambaye pia ni nahodha wa Taifa Stars, amekuwa akivaa jezi namba 10 pia katika kikosi cha timu ya taifa lakini tangu alipojiunga na Genk mwaka jana amekuwa akivaa jezi namba 77.
Katika taarifa iliyotolewa na Mtandao wa Genk, kuanzia msimu ujao Samatta atavaa jezi namba 10 ambayo awali ilikuwa ikivaliwa na kiungo mshambuliaji Tino- Sven Susic raia wa Bosnia na Herzegovina.

Samatta alijiunga na Genk akitokea TP Mazembe na hadi sasa ameichezea mechi 51 na kufunga mabao 17 na amekuwa mmoja kati ya wachezaji muhimu katika kikosi cha timu hiyo.
Msimu uliopita aliiwezesha Genk kufika robo fainali ya Europa League wakitolewa na Celta de Vigo katika hatua hiyo kwa mabao 4-3 ambapo katika mchezo wa kwanza ilifungwa 3-2 halafu ikatoka sare ya bao 1-1.

Bado Samatta ni mchezaji wa Genk, japokuwa zimekuwepo tetesi za mshambuliaji huyo kutakiwa na klabu nyingine.

MWANDISHI WETU, CHAMPIONI

SHAMSA Ford Afunguka Kutopata Mtoto na Chid Benz

$
0
0
WAKATI ndoa yake na Rashid Said ‘Chid Mapenzi’ ikiwa na miezi kumi bila kujibu kwa kupata ujauzito, staa wa filamu za Kibongo, Shamsa Ford ameibuka na kufunguka sababu iliyomfanya kutobeba mimba hadi sasa.

 Shamsa Ford akiwa na mapenzi wake Rashid Said ‘Chid Mapenzi’ (kushoto).
Shamsa aliliambia Risasi Jumamosi kuwa, watu wengi walishakariri kwamba mtu akiingia kwenye ndoa tu, anapata ujauzito kwa kipindi kifupi, jambo ambalo kwa upande wake ni tofauti kwa kuwa yeye na Chid Mapenzi walikubaliana kujipanga kimaisha kwanza ndipo waanze kutafuta mtoto. “Tunajipanga kwanza kimaisha.

Hatuwezi kukurupuka tu ila ndani ya mwaka huu tunaanza kutafuta mtoto na tunamuomba Mungu atusaidie maana mtoto hutoka kwa Mungu, siyo kwa binadamu na kwa kuwa tutakuwa tumeshajipanga watakuwa wanapishana miezi sitasita tu,” alisema Shamsa mwenye mtoto mmoja aliyezaa na jamaa aitwaye Dickson Matoke.

OMMY Dimpoz Ajibu Tuhuma za Wizi wa Nyimbo

$
0
0
Msanii Ommy Dimpoz ambaye sasa anatamba na ngoma yake mpya 'Cheche' amefunguka na kuweka wazi tuhuma za yeye kuiba wimbo na kusema hausiki hata kidogo kwani wimbo huo mpya aliandikiwa na kufanyiwa kila kitu na Goodluck Gozbert (Lollipop).

Ommy Dimpoz amesema hayo jana kupitia Friday Night Live (FNL) na kusema yeye hapaswi kuhusishwa hata kidogo kwani yeye alifuata utaratibu wote na kupata wimbo huo hivyo mtayarishaji wa muziki Aby Dad pamoja na msanii wake wanapaswa kudeal na Goodluck Gozbert (Lollipop) na si yeye kwani yeye ataendelea kuipa nguvu kazi hiyo sababu tayari ameshawekeza.

"Lollipop alisikilizisha chorus hiyo ya Cheche nikaipenda ila akaniambia wimbo huu haujakamilika, baada ya hapo aliutengeneza wimbo ule mwanzo mwisho kwa kuweka sauti zake mimi nilichofanya ni kufuatisha kile ambacho yeye amefanya, sijaandika chochote, wala kutunga melody wala chochote kile" alisema Ommy Dimpoz

Ommy Dimpoz aliendelea kusimulia kuwa
"Sasa baada ya wimbo kutoka baada ya mwaka mmoja kijana ndiyo ananiambia kuwa wimbo wa kwake, mimi ikabidi nimuulize Lollipop inakuaje hii akasema yeye alikwenda studio ya Aby Dad kufanya kazi zingine anadai baadaye akatengeneza kiitikio hicho na kuingiza sauti lakini Aby Dad akasema amependa kiitikio hicho atumie msanii wake, sababu yeye Lollipop haimbi nyimbo za hivi yeye anaimba nyimbo za dini tu, ila naomba hili nisiliongelee sana kwa sababu Lollipop mweyewe yupo naomba mumtafute ili aweze kuongea mwenyewe" alisisitiza Ommy Dimpoz

Mbali na hilo Ommy Dimpoz anasema yeye hakuna anayemlaumu hata mmoja kati yao
"Mimi sijui nini kimetokea kati ya hao watu wawili AbyDad pamoja na Lollipop lakini pia mimi simlaumu yoyote kati yao ila nachoomba tu wao wasinihusishe kwenye mambo yao waniache mimi niendelee na mambo yangu, sababu siwezi kurudi nyuma nishawekeza kwenye wimbo huu" alisema Ommy Dimpoz

Ommy Dimpoz ambaye sasa yupo chini ya usimamizi wa Rock Star4000 ameahidi wiki ijayo video ya wimbo huo 'Cheche' ndiyo itatoka rasmi.

ALI KIBA Afafanua Kwanini kolabo na Yvonne Chaka Chaka na Davido hazijatoka

$
0
0
Kipindi cha nyuma kulikuwa na taarifa za Alikiba kufanya kolabo na Yvonne Chaka Chaka na Davido lakini hadi leo hazijatoka, sasa Alikiba amelizungumzia hilo.



Muimbaji huyo wa Bongo Fleva ambaye December mwaka jana alionekana akiwa studio nchini Afrika Kusini na Yvonne Chaka Chaka, ameiambia XXL ya Clouds FM kuwa kazi na Mwana Mama huyo ilishafanyika ila kuna mipango inaweka sawa kwanza.

“Kiufupi kwamba nyimbo zipo na taratibu tulishafanya kama mlivyoona tupo studio lakini kuna ratiba lazima ziwepo sio tu umefanya halafu unatoa. Kuna mipango tupo nayo tayari na kila nyimbo itatoka kwa muda wake, na wimbo wangu unatoka hivi karibuni siwezi nikasema ni lini,” amesema Alikiba.

Kuhusu kolabo na Davido alisema, “unajua wasanii kama wasanii muda mwingine tunakuwa na maneno ya kuridhisha watu lakini kiukweli hakijafanyika chochote ila plan zipo za kufanya na muda tukiupata tutafanya il sijajua ni lini kwa sabau nyimbo nilizonazo ni nyingi sana,” amesisitiza.

Mwaka 2015 Davido aliwahi kuulizwa kuhusu na kolabo na Alikiba na jibu lake lilikuwa, “I have a song coming out with Alikiba too, that’s gonna be crazy”.

MWINGINE Auwawa Kibiti Usiku wa Kuamkia leo

$
0
0
Mkazi mmoja wa kitongoji cha Nyambwanda kilichopo katika Kijiji cha Hanga wilayani Kibiti aliyetambulika kwa jina la Hamis Ndikanye (54) ameuawa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia leo Jumamosi akiwa nyumbani kwake.

Kwa mujibu wa maelezo ya ndugu wa marehemu alijitambulisha kwa jina la Hamis Saidi amesema watu kama watano wakiwa na bunduki walifika nyumbani kwa ndugu yake saa 6 usiku, kisha kufanya mauaji hayo.

Alisema kabla ya kufanya mauaji hayo walimfunga mke wa marehemu kitambaa usoni na kisha kumpiga risasi mbili mume wake.

Mganga wa Kituo cha Afya Kibiti Dk Sadock Bandiko amesema Ndikaye amepigwa risasi mbili mwilini mwake, moja kichwani na nyingine mgongoni.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kipolisi wa Rufiji, Onesmo Lyanga, amesema polisi wamekwenda eneo la tukio kwa ajili ya uchunguzi.

CHIN Bees: Siwezi Kubadilisha Jina Kwa Sababu ya Chid Benz

$
0
0
Msanii wa Bongo Fleva, Chini Bees amesema hawezi kubadilisha jina ili kumkwepa Chid Benz.

Wiki iliyopita rapper Chid Benz alimtaka msanii huyo kubadili jina kwa sababu yanafanana kitu ambacho Chin Bees amekuja kukupinga.

“Mimi siwezi kubadilisha jina kwa sababu ya Chid Benz kwa sababu halifananini, very different. Mimi nafanya muziki wangu, siwezi nikakaa nipiganie jina, hivyo bro kama anahitaji jina dah!, sidhani kama jina langu linaendana na lake  me am do my thing,”  Chin Bees ameiambia E-News ya EATV.

Sababu ya Chid Benz kumtaka Chin Bees kubadili jina aliadai kwanza yamefanana na pili yeye ana hit song song 32 huku akiadai C. Bees hana hata nyimbo saba, hivyo hawafanani.

ABIRIA Waomba Kuruhusiwa Kusafiri Usiku

$
0
0

Abiria wa mabasi yanayotoka mikoa ya bara yanayopita mkoani Morogoro kuelekea jijini Dar es Salaam wameiomba serikali iruhusu mabasi ya abiria kusafiri baada ya saa sita usiku hasa katika maeneo ambayo sio hatarishi kwa usafiri wa wakati huo.

Abiria hao walitoa ombi hilo jana Ijumaa wakati wakizungumza na Mwananchi katika kituo cha mabasi Msamvu.

Wamelalamikia kitendo cha kuzuiwa kuendelea na safari hata kabla ya saa sita usiku na kubainisha kuwa kinasababisha usumbufu mkubwa kwa abiria wengi.

Kwa muda mrefu sasa serikali imepiga marufuku mabasi ya abiria kuendelea na safari baada ya saa sita usiku hivyo baadhi ya mabasi yanayotoka mkoani Mwanza na Mbeya kuelekea Dar es Salaam yanalazimika kulala mkoani Morogoro.

Abiria Shiraji Nyanda alisema kulala njiani kunawaongezea wasafiri gharama na wale wenye watoto wanapata usumbufu zaidi.

"Nia ya serikali ni njema ya kuhakikisha usalama wa watu wake lakini kwa barabara ya Dar-Moro ni salama sana… wangeruhusu tu mabasi yaendelee na safari. Lakini kibaya zaidi tunazuiliwa hapa kabla hata ya hiyo saa sita," alisema Nyanda.

Hata hivyo, kwa mujibu wa kanuni zilizopo, mabasi ya abiria hayaruhusiwi kusafiri baada ya saa nne usiku.

Abiria mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Jane Arnold, ambaye alikua anasafiri na watoto, alisema kulala kwenye basi na watoto kumemsababishia usumbufu na kumuongezea gharama za safari.

Akizungumzia malalamiko hayo, Mkuu wa kikosi cha Usalama Barabarani wilaya ya Morogoro, Victor Ayo, alisema mabasi hayo yanazuiliwa Morogoro sit u kwa kuogopa kutenkwa, bali pia kwa usalama wa abiria na vyombo hivyo vya usafiri.

Akifafanua, alibainisha kuwa mabasi yanazuiliwa kusafiri usiku ili pia kupunguza ajali zinazoweza kutokea kutokana na uchovu wa dereva.

Alisema kwa wakati huo dereva anakuwa amechoka baada ya kuendesha gari kwa muda mrefu na barabara hiyo inakuwa na msongamano wa malori.

"Niwashauri tu abiria wawe wavumilivu katika hili kwani linafanyika kulinda usalama wao," alisema.

Ofisa huyo pia aliwataka madereva kutii sheria za usalama barabarani ili kulinda usalama wao na usalama wa watumiaji wengine wa barabara.


WABUNGE Tisa Walivyolichangamsha Bunge kwa Hoja, Misimamo

$
0
0
Mkutano wa saba uliomalizika mjini hapa wiki iliyopita, haukuacha rekodi ya kufanya mabadiliko makubwa katika Bajeti Kuu ya Serikali pekee, bali pia baadhi ya wabunge kuacha gumzo kutokana na hoja na mambo yao.

Mkutano huo ulioanza Aprili 4 na kumalizika Jumatano iliyopita, ulipitisha bajeti ya Sh31.7 trilioni iliyokuwa na nafuu kwa wamiliki wa magari, wamiliki wa malori lakini pia kuuma kwa upande mwingine, huku likipitisha sheria mpya za usimamizi wa madini zitakazofumua mikataba ya sasa inayoonekana kuwa ni ya kinyonyaji.

Ili yote hayo yatokee, ilikuwa ni lazima wabunge washiriki katika mijadala na hapo ndipo kila mmoja aliacha nyayo zake.

Miongoni mwa wabunge ambao walitikisa kwa hoja zao kuvutia, kufikirisha au kuwachoma wengine ni Joseph Msukuma (Geita Vijijini), John Mnyika (Kibamba), Peter Msigwa (Iringa Mjini), Zitto Kabwe (Kigoma Mjini) na Halima Mdee (Kawe), kwa mujibu wa mwandishi wetu, Sharon Sauwa aliyeripoti shughuli za Bunge la Bajeti kuanzia mwanzo hadi mwisho.

Wengine ni Philipo Mulugo (Songwe), Salma Kikwete (kuteuliwa), Mwita Waitara (Ukonga) na Hussein Bashe (Nzega Mjini).

Kiboko yao alikuwa Msukuma kwa jinsi alivyowachachafya baadhi ya mawaziri  kila alipokuwa akitoa michango yake kwenye bajeti mbalimbali. Alidiriki kutaka baadhi ya mawaziri wafanyiwe usaili kabla ya kupewa nafasi hizo ambazo hutokana na uteuzi wa Rais.

Pamoja na kuwashambulia mawaziri, alipongeza ripoti mbili za kamati zilizoundwa na Rais John Magufuli kuchunguza mchanga wa madini ya dhahabu na kuwataka wenzake wawe jasiri, akiwataja makada wa CCM ambao wapo bungeni.

“Tufike mahali tuambiane ukweli tuache mizaha, tumeangalia (ripoti) watu wote. Maprofesa, watu tusiosoma na wananchi wetu kule vijijini, halafu wabunge mliotajwa kutoka CCM mnaanza kuweka kwenye Twiter (mtandao) mimi sihojiwi mpaka nini?” alihoji Msukuma, ambaye pia ni mwenyekiti wa CCM mkoani Geita.

“Hivi kweli wezi wana kinga gani? Kama kweli wametajwa ni wezi hata kama wapo CCM hili sio suala la mizaha. Kuna maisha ya watu na watu tumeumia. Watu mmetajwa, wabunge wenzangu wa CCM humu halafu mzee wetu tunayemheshimu humu ndani anasema hawezi kuhojiwa mpaka mahakamani yeye ni nani?

“Naomba kama kuna uwezekano hawa watu kama ni mbunge, kama ni nani wakamatwe. Wanaotusumbua humu ndani ni hao hao wametajwa kwa Profesa (Nehemiah) Ossoro. Katajwa (Dalaly) Kafumu, (William) Ngeleja na  (Andrew) Chenge.

“Wana kinga gani kama ni wezi? Kwani magereza imewekwa kwa ajili ya kina Babu Seya peke yao? Tufike mahala tulipiganie Taifa hili, CCM si kichaka cha wezi. Kila mwaka kila tuhuma mtu anatajwa tufike mahali tuwe serious (makini) kwenye suala hili.”

Wakati Msukuma akitaka wachukuliwe hatua, Mnyika yeye alijikitika kwenye miswada ya rasilimali za nchi ambayo iliwasilishwa kwa hati ya dharura.

Alinukuu kauli ya Msigwa aliyoitoa bungeni mwaka 2012 kuwa Bunge dhaifu huzaa Serikali dhaifu.

“Kinyume chake, Serikali dhaifu husababisha Bunge kuwa dhaifu na ndio hali tuliyonayo hivi sasa. Bunge letu limefanywa dhaifu sana,” alisema Mnyika.

 “Wakati Bunge lenye nguvu lingesema leo tunajadili mkabata huu na kesho mkataba huu, kwa udhaifu huu wa Bunge unaoendelea, tunaijadili yote.”

Kauli hiyo ilimfanya Spika Job Ndugai aingilie kati na kumjibu kuwa anayeona wenzake waliochaguliwa na wananchi kuwa ni dhaifu, basi naye ana matatizo.

“Huwezi tu-- hivihivi una akili timamu-- halafu ukawaona wenzako wote kundi la wajinga fulani,” alisema.

Pia, katika mkutano huo, Mnyika alizua kizaazaa kilichosababisha atolewe nje alipotumbukiza suala la ripoti ya makinikia wakati akichangia moja ya bajeti za wizara.

Wakati akitoa mwongozo kwa mbunge wa Mtera, Livingstone Lusinde kuwa wapinzani hawatetei wezi bali dhahabu inaendelea kuibiwa licha ya Serikali kupiga marufuku usafirishwaji nje wa mchanga, sauti ilisikika ikimwita Mnyika kuwa mwizi.

Hapo ndipo alipochachamaa kutaka hatua zichukuliwe dhidi ya mtu huyo, lakini Spika alikana na badala yake akamtoa nje.

Siku chache baadaye, Serikali ilitangaza kuanzisha kodi ya asilimia moja kwa dhahabu ambayo itakuwa ikisafirishwa nje.

Msigwa

Mbunge mwingine ambaye amekuwa akisisimua vikao vya Bunge ni Msigwa, ambaye safari hii aliiponda Serikali akisema tangu mwaka 1980 hadi 2010 nchi za Afrika pamoja na rasilimali ilizonazo zimepoteza dola 1.4 trilioni za Kimarekani 1.4 kutokana na uongozi mbovu.

“Katika Serikali ya Awamu ya Tano kumekuwa na changamoto kubwa ambazo takwimu hizi zinashabihiana kuwa tutaendelea tena kupoteza mali tulizonazo kutokana na uongozi,” alisema mchungaji huyo wa Kanisa la Vineyard.

“Nchi yetu ipo katika giza kinene kwa sababu watu wengi wamepewa mamlaka kuamrisha, lakini wao wenyewe hawajawahi kujifunza namna ya utii. Tatizo kubwa tulilonalo ni poor leadership skills (stadi dhaifu za uongozi), ambayo inaweza kutupeleka kuingia katika matatizo makubwa sana.

“Wanadhani kumsifu Rais kila anachosema ni uzalendo. Tukifanya hivyo tunatengeneza Taifa la watu waoga. Tupo hapa kuwafanya viongozi wetu wawe wanawajibika na ndiyo wajibu wetu.”

Zitto

Zitto Kabwe, ambaye safari hii ameingia bungeni kwa tiketi ya ACT Wazalendo, ni miongoni mwa wabunge wanaoacha nyao kwa hoja zao. Safari hii, Zitto kiongozi aliyerejea ahadi ya Rais ya kumtua mama ndoo, kuwa haiendani na bajeti ya Wizara ya Maji ambayo fedha za maendeleo zimepungua kutoka Sh915 bilioni hadi Sh623 bilioni.

Alisema wabunge wana mamlaka na kanuni za Bunge zinawaruhusu kuitaka Serikali ikapange upya bajeti hiyo na njia moja tu ya kumsaidia waziri ni bajeti hiyo kuandikwa upya.

Mdee

Mdee pia alitikisa Bunge kwa matendo yake. Kwanza alishtakiwa kwa kumtolea Spika maneno yasiyofaa, lakini akaomba msamaha ulioonekana wa dhati na kusamehewa.

Baadaye, Halima na mbunge mwenzake wa Chadema, Ester Bulaya walifungiwa kwa mwaka mmoja kutokana na kuonyesha vitendo ambavyo Bunge liliviona ni vya ukiukwaji wa kanuni.

Wakati Mnyika akitolewa na askari wa Bunge kwa kutotii kiti cha Spika, Mdee aliwafuata askari hao na kujaribu kumvuta mmoja bila ya mafanikio.

Kwa kuwa wawili hao walishamaliza adhabu zote, Bunge liliamua kuwazuia kuhudhuria vikao kwa mwaka mzima.

Mulugo

Mulugo ambaye aliwahi kuwa Naibu Waziri wa Elimu, akichangia bajeti ya wizara hiyo alisema kitendo cha kuchapisha vitabu vyenye makosa kinaitia doa Serikali. Alisema watalaamu waliopo katika Taasisi ya Elimu Tanzania wanatakiwa kuangaliwa.

“Suala la vitabu unaweza ukalia, nimefanya uchunguzi wa vitabu ni hatari na aibu ya dunia kuna mambo mengine lazima tuseme Serikali ni ya kwangu, nchi ya kwangu, hatuwezi kufumbia macho.”

Waitara

Waitara, ambaye ni mbunge wa Ukonga (Chadema), aliamua kuwashambulia wabunge wa CCM kwa kile alichoikiona kuwa ni kuisaidia Serikali kujibu. Alikuwa akichangia muswada wa Marekebisho ya Sheria Mbalimbali wa mwaka 2017.

“Tunatarajia kama hoja tumetoa sisi (upinzani), waziri aje kujibu, sio wabunge wa CCM mnaijibia Serikali. Mwisho wake mawaziri wanashindwa kufanya kazi vizuri,” alisema Waitara.

Bashe

Hussein Bashe, mmoja wa wabunge walioingia kwa mara ya kwanza na ambao wameonekana kuwa na hoja nzito, alizungumza kwa uchungu wakati akizungumzia vitendo vya utekaji nyara watu vilivyojitokeza mapema mwaka huu.

Bashe alisema kuna wabunge 11 ambao wamo katika orodha ya kutekwa.

Alisema watu kadhaa wamekuwa wakitekwa akitoa mfano wa yeye mwenyewe,  Msukuma, Adam Malima, Ben Saanane na msanii wa Bongo fleva Roma Mkatoliki na kutaka suala hilo lijadiliwe.

“Ni jambo la dharura kwa sababu hawa ni watu wanaofahamika. Hatujui ni Watanzania wangapi wasiofahamika katika ngazi za chini (wanaotekwa),” alisema Bashe.

“Mheshimiwa Naibu Spika, ninasema jambo hili ni la dharura  kwa sababu kikundi hiki kilichoko ndani ya Idara ya Usalama wa Taifa kilichoamua kuchukua mamlaka haya ya kuteka watu, kinaharibu heshima ya Serikali yetu.

“Kinaharibu heshima ya chama changu, ambacho mimi na wabunge wenzangu wa CCM tuliomba ridhaa ya kuwaongoza na si kuhatarisha maisha yao. Naibu Spika naomba uruhusu Bunge kujadili jambo hilo.”

“Hali ya nchi si salama. Watanzania wanataharuki. Watanzania wanajadili mambo hayo katika mtandao na hakuna kauli ya Serikali.”

HATARI ya Kufanya Mapenzi Kwa Njia ya Mdomo......

$
0
0
Shirika la Afya Duniani (WHO) limethahadharisha kuwa, kushiriki mapenzi kwa njia ya mdomo kunasababisha ongezeko la ugonjwa wa kisonono ambao kwa sasa umekuwa mgumu kutibika kutokana na bakteria wanaosababisha kuwa sugu.

Aidha, WHO imeeleza kwamba, kupungua kwa mtumizi ya mipira ya kujamiiana (condoms) kunachochea kwa kiasi kikubwa kusambaa kwa ugonjwa huo wa zinaa.

Ugonjwa wa kisonono kwa sasa umekuwa mgumu kutibika na katika mazingira mengine hautibiki kabisa kutokana na kuendeleza usugu wa dawa (antibiotics) kwa kasi sana.

Ugonjwa wa kisonono husababishwa na bakteria wanaojulikana kitaalamu kwa jina la Neisseria gonorrhoea. Ugonjwa huu husambazwa kufanya ngono isiyo salama kwa njia ya uke, mdomo au njia ya haja kubwa.

Dalili za ugonjwa huu ni pamoja na kutoka maji maji ya njano au kijani katika sehemu za siri, maumivu makali wakati wa kukojoa, pamoja na kutokwa na damu.

Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na WHO katika nchi 77, bakteria wanaosababisha kisonono wameonekana kuwa sugu katika dawa zilizokuwa zikitumika kutibu.

Dr Teodora Wi, kutoka WHO amesema kulikuwa kuna kesi tatu kutoka Japan, Ufaransa na Uhispania ambapo ugonjwa huo ulishindikana kabisa kutibika. Alisema kila mara wakianzisha dawa mpya kutibu ugonjwa huo, bakteria huyo aliweza kuihimili dawa hiyo mpya.

Jambao hatarishi zaidi ni kuwa, maambukizi ya ugonjwa huu yapo kwa wingi katika nchi maskini ambapo usugu huo ni mgumu kugundulika.

Ugonjwa wa kisonono unaweza kuathiri uke au uume, njia ya haja kubwa pamoja na koo. Lakini athari za koo ndizo zinazotishia dunia kwa sasa kutokana na watu wengi kujihusisha na mapenzi kwa njia ya mdomo.

Dr Wi alieleza kuwa bakteria hao hukaa sehemu ya nyuma ya koo na mgonjwa anapoanza kupata maumivu na kutibu kwa kutumia dawa za kawaida, hupelekea bakteria hao kujenga usugu dhidi ya dawa hizo na nyingine zitakazotumika mbeleni.

BODI ya Mikopo Yatangaza Adhabu Kwa Wanafunzi Wakwepa Kurejesha Mikopo......

$
0
0

Na Haji Nassor (OUT), Pemba

Kiasi cha  shilingi bilioni 39.7 kati ya shilingi bilioni 42 zilizotolewa na Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu Zanzibar (BMEJZ) kwa ajili ya kuwakopesha wanafunzi waliosoma elimu ya juu, ziko mikononi mwa wadaiwa hao, kuanzia mwaka 2006 hadi mwezi Juni mwaka huu.

Wakati fedha hizo zikiwa mikononi mwa wadaiwa, tayari shilingi bilioni 2.3 ndizo pekee, zilizokwisharejeshwa na wakopaji, ambapo kati ya hizo shilingi bilioni 42, shilingi bilioni 7.7 Bodi hiyo ilizirithi kutoka kwa uliokuwa mfuko wa elimu ya juu Zanzibar, ambao ulikoma kufanya kazi zake mwaka 2011.

Bodi hiyo ya mikopo ya elimu ya juu, kila mwezi hukusanya wastani wa shilingi milioni 100, kutoka kwa wakopaji ambao ni wanafunzi kila mwezi hadi mwezi Juni mwaka huu wa 2017.

Aidha taarifa ya Bodi hiyo inaeleza kuwa, tokea kuanza kwake mwaka 2011, wanafunzi zaidi ya 18,994 waliomba kupatiwa mikopo, ingawa baada ya kupitia vigezo husika, ni wanafunzi 5, 293 ndio walioteuliwa kwa kipindi hicho, hadi mwaka huu.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi ofisini kwake mjini Chakechake, Mratibu wa Bodi hiyo, kisiwani Pemba Ahmada Omar Juma kwa niaba ya Mkurugenzi wake, Idd Khamis Haji, alisema urejeshaji umekuwa wa kusuasua.

Mkurugenzi Iddi alisema, fedha ambazo ziko mikononi shilingi bilioni 39.7 kwa wanafunzi ambao wameshahitimu bado ni nyingi, hivyo ni lazima kwa waajiri iwe wa serikali au taasisi binafsi, kufanya uhakiki na wakiwagundua waliosomeshwa na Bodi hiyo, wasisite kutoa taarifa kwao.

Alieleza kuwa, zipo sheria za Bodi hiyo, ambazo bado hazijatumika ipasavyo juu ya wanafunzi waliomaliza na kutotoa taarifa za makato, lakini kama wataendelea kuwa wasugu, zitatumika ikiwa ni pamoja na kuanza na wadhamini wao.

“Kuna adhabu mpaka shilingi millioni 5,000,000 au kifungo kwa madhamini, lakini hata kwa mkopaji kutakiwa kulipa deni kwa mkupuo au kuligawa, endapo kutakuwa na hali ya kukimbia ulipaji wa deni lake”,alifafanua.

Hata hivyo Mkurugenzi huyo alisema, changamoto kubwa hasa inayowakabili, ni pamoja na wale wanaoajiriwa kwenye mashirika binafsi na kisha waajiri kushindwa kutoa ushirikiano wa dhati na bodi.

Aidha amesema wengine hata kwa mashirika ya umma, wamekuwa wazito kutoa taarifa za waajiriwa wapya, na wale wanaoondoka nchini kufuata ajira nje ya nchi.

“Suala la kurejesha mikopo halimuhusu mkopaji pekee, bali hata muajiri na mdhamini ni lao, maana fedha hizo zinahitajika kuzngurushwa, ili na wengine wapate kuziomba”,alisema Mkurugenzi huyo.

Kwa upande wake Hassan Khamis Hassan wa Konde, alisema yeye alishawahi kumpelekea ripoti mwanafunzi aliemdhamini, ambae kwa sasa anaendelea kukatwa.

“Nilimuuliza kuwa, umeshaanza mikato, akanionyesha dharau, lakini baadae nilipomfahamisha alikubali kwenda kujipelekea ripoti na sasa anaendelea kukatwa”,alisema.

Hata hivyo mwanafunzi Asha Mohamed Ali, alisema lazima fedha za kujikimu ziongezwe, maana maisha hasa ya chuoni yamekuwa magumu kutokana na kupanda kwa bei ya vyakula.

Wakati huo huo Mratibu wa Bodi ya mikopo ya elimu ya juu, kisiwani Pemba Ahmada Omar Juma, amempongeza rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Mhe: Dk Ali Mohamed Shein, kwa kutimiza ahadi yake ya kuwaongoeza bajeti kwenye bodi yao.

Alisema ongezeko hilo ni kutoka shilingi bilioni 6.8 kwa mwaka uliomalizika wa fedha 2016/2017 hadi kufikia shilingi bilioni 10.2 kwa mwaka 2017/2018, jambo ambalo limewapa kufanya kazi zao kwa ufanisi.

“Lazima tumpongeza rais wetu pamoja na waziri na hata baraza la wawakilishi, kwa kukubali kutuongezea na kupitisha ongezeko la bajeti kwenye bodi yetu”,alifafanua Mratibu huyo.

Idadi ya wanafunzi wanaopatiwa mikopo na Bodi hiyo, imekuwa ikiongeza kila mwaka, ambapo mwaka 2011/2012 walikuwa wanafunzi 209, mwaka 2012/2013 887, kisha wanafunzi 1,417, wanafunzi 1,611, baadae wanafunzi 575 na mwaka 2016/2017 ni 594 huku malengo ya bodi kwa mwaka 2017/2018 ni kufikia wanafunzi 1,600.

Malinzi ajiuzulu Urais TFF Akiwa Rumande

$
0
0

RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amejiuzulu wadhifa wake wa Ujumbe wa Kamati ya Maendeleo ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA).

Kupitia kwa wakili wake, kampuni ya Rwegoshora, Malinzi amewaandikia barua FIFA kuwataarifu kujitoa kwenye Kamati hiyo kutokana na kuwa mikononi mwa dola kwa sasa.

Malinzi, pamoja na Katibu wa TFF, Selestine Mwesigwa na Mhasibu, Nsiande Isawafo Mwanga.
wapo rumande hadi Julai 17, upepelezi wa kesi yao utakapokamilika baada ya kunyimwa dhamana Julai 3 katika kesi inayowakabili.

Watatu hao walipandishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam kwa mara ya kwanza Juni 29 na kusomewa mashitaka 28 ya kughushi na kutakatisha fedha kupitia akaunti ya TFF iliyopo katika banki ya Stanbic, Dar es Salaam.

Katika mashitaka hayo, 25 yanakwenda moja kwa moja kwa Rais wa shirikisho hilo, Malinzi akidaiwa kughushi michakato mbalimbali ya kifedha, huku matatu yakiwahusu wote na Katibu wake na Mhasibu wake Nsiande Isawafo Mwanga.

Katika kesi hiyo, Serikali inawakilishwa na jopo la mawakili watano, wakiongozwa na Pius Hila huku upande wa washtakiwa ukiwakilishwa na mawakili watano, wakiongozwa na Jerome Msemwa.

Mawakili hao watano kwa pamoja wameshindwa kuafikiana ili washitakiwa wapatiwe dhamana.
Malinzi aliingia madarakani TFF Oktoba mwaka 2013 baada ya kupata kura 72 kati ya 126 zilizopigwa akimshinda aliyekuwa mpinzani wake wa karibu, Athumani Nyamlani.

Lakini baada ya kesi hii kuanza kuunguurma na kuwekwa rumande, Kamati ya Utendaji ya TFF ilikutana na kumteua Makamu wake, Wallace Karia kukaimu Urais wa shirikisho hilo.

Lakini kwa mwenendo wa kesi, Malinzi ndiyo kama amekwishaaga TFF, kwani uchaguzi unatarajiwa kufanyika Agosti 12 mjini Dodoma naye hatashiriki tena kutokana na kukosekana kwenye usaili.

KIMENUKA...Wafuasi 51 wa Chadema Wakamatwa na Polisi, Chato

$
0
0
Wafuasi na Viongozi  51 wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) waliokamatwa jana Ijumaa  wakiwa kwenye kikao cha ndani wilayani Chato wanaendelea kushikiliwa na polisi kwa mahojiano.

Miongoni mwa waliotiwa mbaroni wanaoendelea kusota mahabusu ni pamoja na Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Geita, Fabian Mahenge na Katibu wake, Sudi Kanganyala.

Mwenyekiti wa Serikali kijiji cha Mkuyuni, Anaclet Twegosora, ambaye pia ni Mwenyekiti wa chama hicho Kata ya Chato, amewataja viongozi wengine wanaoshikiliwa kuwa ni mwenyekiti wa Baraza la Wazee mkoani Geita, Vitus Makange na Neema Chozaire ambaye ni Mwenyekiti wa Bavicha mkoa.

Wengine ni Kaimu Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Chato, Uhuru Selemani, Katibu wake Mangesai Rudonya na diwani mstaafu kata ya Muganza, Marko Maduka.

Kama ilivyokuwa jana, hakuna kiongozi wa Jeshi la Polisi anayekuwa tayari kulizungumzia suala hili.

Wakati Mkuu wa Polisi Wilaya ya Chato, Alex Mkama, ambaye tukio hilo linaendelea wilayani kwake akisema hawezi kulizungumzia, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Mponjoli Mwabulambo, amesema yuko likizo na kuelekeza atafutwe kaimu wake Allan Bukumbi ambaye tangu jana hapokei simu yake ya kiganjani wala kujibu ujumbe mfupi wa maneno anaotumiwa.

Makamu Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Ziwa Victoria, Ansbert Ngurumo, amesema kutawanywa kwa mabomu ya machozi na kukamatwa kwa viongozi na wanachama hao ambao walikuwa katika mkutano wa ndani ni kinyume cha sheria kwa sababu vikao vya ndani havihitaji kutoa taarifa wala kibali cha polisi kwa mujibu wa sheria namba 5 ya vyama vya siasa ya mwaka 1995.

Ma ex Girlfriends wa Mume Wangu Wameungana Kunishambulia

$
0
0
Mimi ni mama wa watoto wawili mapacha.
Niliolewa 2010 na kijana m handsome sana.
Sikufanya effort yeyote kumpata. Sikumwendea kwa waganga wala sikulala makaburini ili anioe.
Nilikutanae kwenye ndege na tulikaa pamoja, huo ulikuwa ndio mwanzo wa mapenzi yetu.
Miaka mitatu ya uchumba ilikuwa mitamu sana na haikuwa na makuu.
Baada ya kuolewa ndipo makasheshe yalipoanza.\

Siku moja nikiwa dukani kwangu walikuja wadada wawili wakajitambulisha mmoja ni Jack na mwingine ni Irene, wakaniambia mume wangu alikuwa ni boyfriend wao kwa nyakati tofauti na hawawezi kuishi bila yeye.

Kwakweli nikaona ni kama sinema, wakaniomba niwape ruhusa wawe wanakuja nyumbani kulala na mume wangu.

Kwakweli walinikera, nikaondoka dukani na kurudi nyumbani huku nikilia kwa hasira.
Mzee alipokuja nikampa kisanga kizima.
Tangu hapo wanawake hao wamekuwa wakinisakama kwa msg za matusi.
Wanamtukana pia mume wangu kuwa eti nimemroga.
Kwa kweli wamekuwa ni kero kwa familia yetu.
Jamani sijui wadada wengine wameumbwaje?
Mume wangu kasema atawapeleka polisi iwapo watanifuata tena dukani. Dukani sasa hawaji ila tunakomaje na mitusi ya kwenye sms?

HATIMAYE Prof Jay afunga ndoa leo

$
0
0
Siku chache tangu Mbunge wa Mikumi Joseph Haule Aseme kwamba Ndoa yake yakaribia ambapo leo yametimia

Mbunge huyo ambaye ni Mkali wa Muziki wa Bongo Hip Hop Prof Jay  amefungua ndoa leo kwenye kanisa la St Joseph Jijini dar es Salaam
Viewing all 104795 articles
Browse latest View live




Latest Images