Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104795 articles
Browse latest View live

Makaburi 38 ya Pamoja Yagundulika Kasai, DR Congo

$
0
0
Taarifa ya Vikosi maalum vya kulinda amani vya umoja wa Mataifa(MONUSCO) ilieleza kuwa makaburi mengine 38 ya pamoja yaligundulika katika mkoa wa Kasai.

Idadi hii inapelekea kufikia jumla ya makaburi ya pamoja 80 ambayo yamegunduliwa tangu mwaka uanze.

Makaburi haya 38 yaligunduliwa katika maeneo ya Diboko na Sumbula katika ukanda wa Kamonia.

Eneo la Kasai ni makao makuu ya kundi la kijeshi la Kamuina Nsapu. Mgogoro na serikali uliongezeka mnamo mwaka 2016 baada ya vikosi vya serikali kumuua kiongozi wa kundi hilo.

Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa mwezi Aprili, zaidi ya watu 400 wamefariki tangu mapigano kati ya majeshi ya serikali na wanamgambo hao yapambe moto.

Huyu Ndiyo Mwanamke Tajiri zaidi Afrika, Azidi Kutajirika zaidi

$
0
0
Bi Santos amechukua udhibiti wa benki hiyo ya BFA baada ya kampuni yake kununua hisa zaidi katika benki hiyo na kudhibiti zaidi ya asilimia 50 ya hisa katika benki hiyo.

Hatua hiyo imewaacha waangalizi kutojua ikiwa watamshangilia mama huyu mjasiria mali au kulalamikia mamlaka na ushawishi wa kiuchumi walio nao matajiri wachache sana barani afrika.


Isabel dos Santos mwenye umri wa miaka 43, amefanikiwa na angali na ari ya kufanikiwa zaidi katika kanda ambayo wanaume wanatawala katika ofisi nyingi za umma na za kibinafsi.

Bi Dos Santos, ni bintiye rais wa angola Jose Eduardo dos Santos, ambaye ameongoza taifa hilo tangu mwaka wa elfu moja mia kenda na sabini na tisa.

Angola ni moja ya mataifa masikini zaidi duniani.

Katika miaka ya hivi karibuni ilinufaika pakubwa kutokana na mapato yanayotokana na mauzo ya mafuta na uwekezaji kutoka uchina.

Hata hivyo ufisadi na umaskini vimesalia kuwa changamoto kubwa zaidi nchini humo.


Bi Dos Santos mara kwa mara amepuuzilia mbali madai kuwa familia ya rais inapewa nafasi zaidi kuliko raia wengine kuthibiti uchumi na masuala ya kisiasa ili kuhakikisha kuwa familia hiyo itaendelea kutawala Angola baada ya rais Dos Santos kustaafu, kama alivyohaidi hivi majuzi.

Kwa sasa Bi Dos Santos anasimamia shirika la mafuta la taifa na kampuni kubwa zaidi ya kutoa huduma za simu na sasa anadhibiti benki kubwa zaidi nchini Angola BFA.

Hii ikiashiria kuwa ushawishi wa familia ya rais dos santos itaendelea kuchukua nafasi kubwa zaidi katika masuala ya kiuchumi na kisiasa nchini Angola miaka zijazo.

JE Dada Unahitaji Kuwa Mrembo na Muonekano Bomba na Kaka Kuwa na Mvuto wa Kiume...Waone Hawa....

$
0
0
BLACK BEAUTY COMPANY
JE Dada unahitaji kuwa Mrembo na ule muonekano bomba wa kisuperstar👌🔥,kaka unahitaji kuwa mtanashati na mvuto zaidi wa KIUME?fika black beauty company utatimiza ndoto zako,hawakosei hata siku moja kwa products original na zenye matokeo yaharaka sana,bila madhara,ni kampuni yenye uzoefu wa hali ya juu sana🔥
1)kuongeza hips,makalio,mapaja@150000
(b)kuongeza hips,makalio,mapaja na miguu@200000/=
2)kuongeza miguu ,kuondoa vigimbi@120000/=
3)kuwa mweupe mwili mzima (Rangi moja)@150000/=
4)Kupungua mwili mzima@150000/=
5)kupunguza tumbo@100000/=
6)kupunguza au kuongeza matiti@100000/=
7)kukuza nywele@100000/=
8)kuondoa michirizi @100000
9)kuondoa madoa,mabaka na chunusi sugu@100000/=
10)kuongeza uume na nguvu za kiume@150000/=
Dawa zetu niuhakika sana100%na utaletewa popote ulipo,mikoani tunatuma,nje ya nchi tunatuma DHL,ofic zetu zipo kariakoo msimbazi police,🔥karibuni kwa mawasiliano zaidi

WASILIANA NASI

WhatsApp+255657778924,au call0743534406 



Au unaweza kutufollow INSTAGRAM
👇👇👇👇👇👇
@black_beauty_company

Sifa 5 Unazotakiwa Kujua Kabla ya Kuoa / Kuolewa

$
0
0
Kuna watu wenye tabia mbaya kiasi kwamba wapenzi wao wanajuta kuoana nao, wanaona ni heri zaidi kama wangeishi peke yao. Sasa, utamjuaje mwanaume aumwanamke mwenye tabia mbaya, ili ujiokoe na ndoa yenye utata?

1. Tabia zake haziendani na wewe.
Kama tabia zako haziendani na mwanaume au mwanamke unayetaka kuoana naye, ujue mapema ya kuwa ndoa yenu itajaa mfurulizo wa matatizo bila kukoma na hivyo mtadumu katika migogoro na ugomvi usioisha.

2. Huishusha hadhi yako mbele ya familia na rafiki zake.
Atakuwa mume au mke mbaya kama umegundua tabia yake ya kupenda kuishusha hadhi yako mbele ya familia au rafiki zake. Hasa kama ni mwepesi wa mapungufu yako mbele ya rafiki zake, hata kabla hajakwambia lolote juu ya udhaifu wako, unamkuta mtu mzima anadiriki hata kuwaeleza rafiki zake juu ya udhaifu wako faragha, ukimjua huyo usithubutu ndoa.Ana sifa hizi 5? Usikubali ndoa

3. Hawakubali wana familia na rafiki zako.
Kama anakuwa mtu wa kusimamisha bendera nyekundu (red flag), kila mara unapojumuika na familia au rafiki zako, unatakiwa kuwamakini, anaweza kuwa mpenzi mbaya huyo!.

4. Hapendwi na familia na hata rafiki zako pia.
Kama sehemu kubwa ya rafiki na familia yako wanakushuhudia mambo mengi mabaya juu yake, ni vyema ukawa makini  na kuchukua tahadhari kwani yawezekana umepofushwa tu na hisia zako za mahaba juu yake, hivyo unashindwa kuyaona mambo mabaya yanayotazamwa na wengine. Familia na rafiki zako wanakupenda na wanataka uwe na maisha bora, kuwa makini.

5. Kama hakuna muunganiko wa ndani ya moyo unaojisikia kati yenu.
Mapenzi hutawaliwa na hisia kwa asilimia kubwa, usikubali kuwa na mtu eti kwasababu ni kijana mtanashati au ana urithi wa mali nyingi, Amini nakwambia penzi lenu halitodumu kabisa, yawezekana akaanza yeye au wewe kumsariti mwingine kwa kuuelekezea moyo wako kule unakojisikia upendo zaidi.

Ni heri ukosee njia au ukapoteza mali zako zote kwa kuwa unao uwezo wa kujipanga upya na ukajiimarisha tena, kuliko kukosea kuchagua mtu wa kuoana naye, kumbuka hilo ni janga lako la maisha.

Abdi Banda Akwea Pipa Kucheza Soka la Kulipwa....Acha Neno Kwa Simba

$
0
0
Hatimaye beki wa Taifa Stars, Abdi Banda ameondoka leo kuelekea nchini Afrika Kusini kwenda kusakata soka la kulipwa katika timu yake mpya ya Baroka FC ambayo amesaini kandarasi ya miaka mitatu

Beki huyo amekwea 'Pipa' licha kutopata barua ya kuondoka katika klabu yake ya Simba alipokuwa anachezea msimu uliyopita, mbali na hilo Banda ameshauri wachezaji wenzake ambao wanatamani kupata nafasi ya kucheza nje ya nchi wasiangalie nyuma pindi wanapokuwa wamepata nafasi hizo.

"Wachezaji wajitume na wanatakiwa kuwa makini na nafasi zinapotokea nafasi za kutoka kwenda kucheza nje ya nchi, wasiangalie nyuma wazitumie nafasi hizo. Tunahitaji timu ya taifa nzuri, bila wachezaji wengi kucheza nje ya Tanzania hatuwezi kupata timu nzuri ya taifa na kikubwa ni kuongeza juhudi na kufanya mipango ili wachezaji wengi tucheze nje ya nchi", amesema Banda.

Banda tayari alishasaini mkataba wa kujiunga na klabu hiyo wakati akiwa kwenye michuano ya COSAFA Cup 2017 mashindano ambayo yamemalizika Afrika Kusini huku Tanzania ikishika nafasi ya

Diamond Apoteza Ladha Kwenye Mziki Wake....Namshauri Akae Kimya Mwaka Kulisoma Game Upya....

$
0
0
Mimi ni shabiki mkubwa sana wa huyu jamaa tokea kamwambie till this time.....lakini recently naona kama jamaa anaanza kupwaya hivi maana yule Diamond wa kutoa ngoma za Taifa zinazosumbua Media kuanzia Bongo hadi nchi za nje simuoni tena....Inasikitisha na kutia wasi wasi sana kama kuna nuru uko mbele inabidi yeye na manejiment yake wakae watulize vichwa ili kupata jawabu zuri ni wapi jamaa anakosea.......

Nyimbo zake kwa sasa zinapata air time tu kwa vile tayari ni maarufu ni ngumu kwa Media kuzikwepa ila sio nzuri kivile kama zile za zamani.

Kwa ushauri mzuri ikiwezekana akae pembeni kwanza ili alisome game vizuri......Mfano Davido aliamuwa kuwa kimya kwa takribani mwaka mzima na akilisoma game na come back yake imekuwa nzuri kupita Kiasi.....

By isho_boy

Beyonce Awaweka Hadharani Mapacha wake

$
0
0
Beyonce ameamua kuwaonyesha hadharani watoto wake mapacha.


Muimbaji huyo kupitia mtandao wa Instagram, ameonyesha kuwa watoto hao wana mwezi mmoja tangu wamezaliwa.

“Sir Carter and Rumi 1 month today.  ,” ameandika Queen Bey kwenye mtandao huo.

Mapacha hao waliozaliwa ni mmoja wa kike na mwingine wakiume na tayari walishapewa majina ya Sir na Rumi.

Picha: AY Amvisha Pete Mpenzi Wake wa Muda Mrefu

$
0
0
Rapper Ambwene Yessayah maarufu kama AY ameonyesha kuwa amechoshwa na ukapela.


Msanii huyo Alhamisi hii ameamua kumvisha pete mchumba wake wa muda mrefu Remy, raia wa Rwanda ambaye ajabu amekuwa naye tangia mwaka 2008.


Kwa mara yakwanza AY amemtambulisha mpenzi wake huyo Disemba mwaka jana wakati wa birthday ya mrembo huyo.


Sherehe hiyo ilihudhuriwa na watu wa karibu na wawili hao. Kwa kitendo hicho tunatarajia kuiona ndoa ya Ay na mpenzi wake huyo sio nyingi.

Picha na Mx Carter

Kutana na Shabiki Aliyemvamia Rooney Katikati ya Mchezo (Video)

$
0
0
Katika mchezo wa Everton Vs Gor Mahia uliomalizika kwa The Blues kuibuka na ushindi wa 2-1, imeibua matukio mengi huku kubwa kuliko yote ni lile la shabiki mmoja kuingia uwanjani na kumkumbatia mshambuliji mpya machachari wa Everton, Wayne Rooney.



Rooney hakuonyesha dalili yoyote ya kumkwepa kijana huyo aliyevalia jezi ya Manchester United klabu ya zamani ya mshambuliaji huyo.

Jeshi la posili lilimshikilia kijana huyo kabla ya kuachiwa muda mfupi baadaye baada ya viongozi wa Tanzania kutaka aachiwe.

Hizi Ndizo Sababu za Lulu Kupungua

$
0
0
MSANII kutoka Bongo Muvi, Elizabeth Michael ‘Lulu’ kwa mara ya kwanza amefungukia sababu zinazomfanya kupungua sana mwili kuwa ni kushinda kwa kula matunda pamoja na mazoezi makali ya viungo.

Akizungumza na Star Mix, Lulu alisema kuwa, ameamua kupunguza mwili kwa makusudi na kwamba kila siku anashinda akila matunda na kufanya mazoezi magumu ya viungo.

“Watashangaa sana kuniona napungua lakini nafanya hivi wala sijashauriwa na mtu ni kuweka tu mwili wangu sawa. Nafanya sana mazoezi, naenda gym kila siku na kuhakikisha muda mwingi nashinda kwa kula matunda kuliko chakula,” alisema Lulu.
Wiki mbili zilizopita, Lulu alizua gumzo katika Ukumbi wa King Solomon, Namanga jijini Dar baada ya kuonekana akiwa amepungua tofauti na zamani.

Umesikia Puvu la Manara kwa Kuhusu Rooney

$
0
0
Msemaji Machachari aliyefungiwa  wa klabu ya Simba Haji Manara, ametoa ya Moyoni kuwa  hajapendezeshwa timu ya Everton inayotokea Uingereza kuondoka nchini bila ya kucheza na klabu ya Simba na Yanga.

Manara ameeleza hayo kupitia ukurasa wake wa Instagram muda mchache ulipomalizika mchezo wa kirafiki baina ya Everton dhidi ya Gor Mahia ya Kenya mtifuano ulichezwa katika uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaama jana Jioni.


"Sijapenda kwa Klabu zetu mapacha kukosa nafasi ya kucheza na kina Rooney, ila Mungu ni fundi maana wangepata nafasi wale jamaa wangejiita wa mbinguni, jina la wakimataifa wangeliacha", ameandika Manara.

Katika hatua nyingine, timu ya Everton ilifanikiwa kuwachapa Gor Mahia kwa mabao 2-1 ambapo ndani ya dakika 34 za kipindi cha kwanza Rooney aliweza kupachika bao la kwanza lakini ilipofika dakika ya 36 bao hilo lilisawazishwa na Tusiyenge mchezaji kutoka Gor Mahia.
Kama hiyo haitoshi ilipofika dakika 80 kipindi cha pili Everton waliongeza bao la pili kupitia mchezaji wake Dowell na kupelekea mpaka kinapulizwa kipenga cha mwisho Everton kuwa mbele kwa mabao 2-1 na kuifanya timu hiyo kuwa mshindi.

Hakuna Msalie Mtume....Vituo vya Mafuta Kuendelea Kufungwa

$
0
0
Vituo kadhaa vya kuuza  dizeli, petroli na mafuta ya taa vimefungwa jijini hapa kutokana na kutokuwa na mashine za kielektroniki za kutoa risiti (EFDs).

Hatua hiyo inayotekelezwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), imeelezwa kuwaathiri si tu wenye vituo bali hata watumiaji.

Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi wa TRA, Richard Kayombo amesema leo  Julai 14 na kuongeza kwamba  wanaendelea na kazi hiyo nchi nzima ili kuhakikisha sheria inatekelezwa.

Kimenuka...Machangudoa Waundiwa Vikundi vya Ulinzi Moshi

$
0
0
 Wananchi wa Kata ya Mawenzi, Manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro, wamelazimika kuunda vikundi vya ulinzi katika mitaa yao nyakati za usiku kwa lengo la kutokomeza biashara ya uchanguduo na uhalifu uliokithiri katika kata hiyo.

Hayo yamebainishwa na wananchi hao katika mkutano uliotishwa na diwani wa kata hiyo, Hawa Mushi, kwa lengo la kujadili changamoto zinazowakabili katika maeneo yao na kutoa maazimio.

Janeth Mbwambo, mkazi wa eneo hilo, amesema tatizo la machangudoa kuzagaa katika maeneo ya kata hiyo limekuwa kero nyakati za usiku pamoja na vijana wanaofanya uhalifu pia wamesababisha watu kuwa na hofu ya usalama wao.

Mkazi wa kata hiyo, Mary William, amesema pamoja na juhudi zinazofanywa za kuimarisha ulinzi bado hali imekuwa mbaya kwa kata yao huku akidai kuwa kama hawataimarisha ulinzi wao wenyewe tatizo hilo litaendelea kuwepo.

Diwani wa kata hiyo amesema wamejitahidi kupambana na uhalifu na machangudoa lakini bado tatizo limekuwa likiendelea na kwamba wataingia katika ulinzi wenyewe ili kukomesha kabisa jambo hilo.

“Tunaingia katika mapambano wenyewe ili kuwakabili machangudoa pamoja na  uhalifu unaofanywa na watu kutoka nje ya kata yetu na si wakazi wa eneo husika, hali hiyo imeichafua sana kata yetu,” amesema Diwani Mushi.

Akijibu kero za wananchi hao kuhusu kelele za mziki nyakati za usiku, Meya wa Manispaa ya Moshi, Raymond Mboya amesema suala hilo limeshatolewa maelekezo kwa mkurugenzi wa manispaa hiyo.

Amesema kama mtu hataweza kufuata masharti ya kupiga muziki usiku, vyombo vyake vya muziki vitachukuliwa na kupelekwa katika halmashauri hiyo na akiendelea kukaidi atafungiwa na faini yake ni kiasi cha Sh.1 Millioni.

Akizungumzia suala la wafanyabiashara maarufu kama wamachinga Mbunge wa Jimbo la Moshi Mjini, Jaffar Michael, amesema suala lao limeshapitishwa bungeni kwamba ili waweze kutambulika wanatakiwa kila mmoja ajisajili.

Amesema jambo hilo litasaidia kuepusha migongano na itawaepushia kufukuzwa na kupigwa na baadhi ya mgambo, na sheria hiyo inatakiwa ianze Julai Mosi mwaka huu kwani watakuwa wanatambulika kisheria.

Mahakama Yakataa Ombi la Harbinder Singh Kutibiwa nje, Yasema Atibiwe Muhimbili

$
0
0

Mawakili wanaomtetea mfanyabiashara Harbinder Singh Seth wameiomba Mahakama imruhusu mteja wao akatibiwe nje ya nchi, kutokana na kuwa na uvimbe na Baloon tumboni hali inayomsababishia maumivu makali na kumnyima usingizi kwa wiki ya nne, ombi ambalo limekataliwa na Mahakama na kuagiza atibiwe Muhimbili

Mume Hafiki Kileleni ni Kawaida au Matatizo?

$
0
0
Habari zenu wapendwa, Weekend nilipata mgeni ambae ni ndugu yangu, ameolewa ana miezi 3 tu, lililomleta hasa ni kutafuta ufumbuzi anasema tangia ameolewa Mume wake alifika kileleni siku ya Honey Moon tu wana miezi 3 sasahivi hajawai fika tena lakini akiingia uwanjani anaweza ata kukesha tatizo ni hilo hafiki mwisho, amemuuliza kwanini anasema nayeye hajui kwanini, nimeona niwaletee nyinyi wana JF mabingwa wa TIBA ya kila tatizo, maana mdogo wangu amekosa amani ameshaanza kuona kupata watoto itakuwa ndoto

Nick Minaj Ajazwa Ujauzito na Nas.......?

$
0
0
RAPA Onika Tanya Maraj ‘Nicki Minaj’ huenda amenasa ujauzito kutoka kwa bwana wake mpya ambaye pia ni rapa, Nasir Jones ‘Nas’ baada ya kuposti picha ya ‘emoji’ ya mtoto mchanga.

Kupitia ukurasa wake katika Mtandao wa Twitter, Nicki aliposti picha ya emoji hiyo iliyoamsha hisia za mashabiki wengi huku wengine wakimpa ‘za chembe’ kuwa, badala ya kuachia wimbo mpya ndiyo kwanza anashika mimba. Hii si

mara ya kwanza kwa Nicki kuposti viashiria vya kunasa ujauzito, wiki mbili zilizopita aliandika maneno ya kuashiria kuwa mtoto wake yupo njiani kuja duniani. Mei mwaka huu, katika shoo ya The Ellen DeGeneres, Nicki alithibitisha kutoka na Nas na angependa kumzalia.

Fedha za Escrow Noma..... Zamuibua John Shibuda Mafichoni.........

$
0
0
MWANASIASA Mkongwe nchini na Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa, John Shibuda amewataka waliopokea fedha za mgao wa Escrow kuzirejesha

Shibuda ambaye amewahi kuwa Mbunge wa Maswa Magharibi na  kwa sasa ni Katibu Mkuu wa Chama cha Ada Tadea, alisema dini zote zinasema asamehewe yule ambaye anatubu na kukubali.

Alisema   anaona  Ngeleja anatakiwa asamehewe kwa vile  amefanya kitendo cha kishujaa, kukiri  na kuamua kuzirejesha fedha hizo

Shibuda ametoa kauli hiyo siku chache baada ya Mbunge wa   Sengerema, William Ngeleja (CCM) kurejesha Sh milioni 40.4 alizopewa na mfanyabiashara, James Rugemalira.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Shibuda alisema kitendo kilifanywa na Ngeleja ni cha kishujaa na anapaswa kusamehewa kwa kuwa ametambua kosa lake mbele ya umma.

‘’Kwa kitendo chake Ngeleja kutubu, tukubali tusiwe na inda na choyo ila wale wengine nao wakubali kuzirejesha fedha na Mheshimiwa Rais awasamehe kama dini zetu zinavyosema, mtu akitubu asamehewe,’’alisema.

Wakati huohuo,  Shibuda amewashambulia wapinzani kwa akidai   wanatakiwa kuwa  na ajenda mpya kwa vile  zilizopo, Rais wa sasa Dk. John Magufuli amekwisha kuzitatua kwa kiwango kikubwa.

Alisema Serikali ya awamu ya tano imo katika dunia ya mabadiliko ya mila, jadi na utamaduni na kokomesha uzembe.

Alisema ajenda ya vyama vya upinzani kama rushwa, ufisadi  imenyauka na kuvitaka kutafuta sehemu ya kutokea.

“Vyama vya upinzani kwa sasa ajenda yao ni nini? Ni zile zile za wakati ule Mwalimu   Nyerere aliporuhusu vyama vingi.

“Wanasayansi walianza na dawa ya Panadol  lakini leo kuna dawa zaidi ya tatu basi na wapinzani wawe na vikosi kazi vya kubuni tiba mbadala ya kutengua utumishi uliotukuka wa Rais Magufuli,’’ alisema.

Shibuda alisema serikali ya awamu ya tano inafanya vizuri huku akidai Taifa limepata Rais mwenye utumishi wachangamfu na kugusa hisia za jamii.

ACACIA Kulipa Mirabaha iliowekwa Katika Sheria Mpya za Madini

$
0
0
Kampuni inayomiliki Makampuni ya Uchimbaji wa Madini ya ACACIA imesema italipa mirabaha iliowekwa katika sheria mpya za madini.

Sheria mpya ya madini inawataka wawekezaji katka sekta hiyo kulipa asilimia 6 ya mirabaha ikiwa ni ongezeko la asilimia 2 zilizokuwepo awali, ambapo asilimia 1 ni kwaajili ya usafirishaji kwenda nje.

Teknolojia ya Panya Kutoka Tanzania Ambayo inashinda za Wazungu

$
0
0
Kutoka Tanzania wanapatikana Panya ambao wana uwezo wa kutambua ugonjwa wa Kifua Kikuu ‘TB’ kwa haraka zaidi kuliko teknolojia nyingine Duniani.

Mtafiti wa viumbe hai kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine, Morogoro (SUA) Dkt. George Mkode ameelezea tecknolojia ya kuwafundisha Panya kutambua ugonjwa wa Kifua Kikuu ‘TB’ kwa haraka zaidi na uhakika kupitia makohozi ya binadamu anayeugua ugonjwa huo.

Panya huyo ana uwezo wa kupima wagonjwa zaidi ya 100 hadi 150 kwa dakika 20 tu ambapo njia zitumikazo Hospitali huchukua muda mwingi na gharama kubwa. Hositali 28 zimeshafikiwa hadi sasa nchni kote ingawa lengo ni kuzifikia Hospitali nyingi zaidi ndani na nje ya nchi.

VIDEO:Sumeye akishushia tuhuma CCM, Kubenea Alaa Sahani Moja na Sakaya

$
0
0
Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Kanda ya Pwani Frederick Sumeye amekituhumu Chama Cha Mapindu CCM kuwa kinaratibu Mpango wa Kivuia vyama vya upinzani Nchini.

Wakati huo huo Kaimu Mwenyekiti wa Kanda Saed Kubenea ameeleza kuwa Kaimu Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF  Bi Magdalena Sakaya sio Mwanachama halali wa CUF
Viewing all 104795 articles
Browse latest View live




Latest Images

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596344.js" async> </script>