Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104789 articles
Browse latest View live

Kutana Mtaalam wa Tiba Asili Mwenye Uwezo Mkubwa wa Kutatua Matatizo Kwa Nyota na Dua

$
0
0
KUTANA NA TABIBU MWENYE KUBRI KUTOKA KWA ALAH MAALIM ISSA NAJIMU. NI SHARIFU
MWENYE UWEZO WA KUBAINI TATIZO LAKO PUNDE TU UNAPO MFANYIA MAWASILIANO KUPITIA
WASAA NA SIKU KWA MAWASILIANO:-
MAALIM ISSA NAJIMU KUTOKA MKOA WA TANGA MWAMBONI MAGOFU KATA YA NGUVU MALI
NCHINI TANZANIA, NI TABIBU MWENYE KUBRI TOKA KWA ALAH ANATIBU KWA NJIA YA VITABU VYA
QUR-AN, DAWA ZA ASILI PAMOJA NA DAWA ZA KIARABU.
ANATIBU KWA NJIA YA SIMU UKIWA NCHI YOYOTE / MKOA WOWOTE KWA MATATIZO YAFUATAYO:-

 ULIJALI (NGUVU ZA KIUME) 
 MIGUU KUWAKA MOTO 
 KUTAFSIRI NDOTO 
 MFARAKANO WA WANANDOA 
 MFARAKANO KAZINI 
 KUPANDSHWA CHEO 
 KUTOA PETE YA BAHATI 
 ANAO UWEZO WA KUPANDIKIZA NYOTA YA KUBASHIRI 
 KUFUNGUA UZAZI KWA WALIYO FUNGWA KWA NJIA YA USHIRIKINA 
 KUTOA VIFUNGO VYOTE VILIVYO FUNGWA IKIWA NI KWENYE MWILI WA BINADAMU /MAJUMBANI NA KWENYE BIASHARA. 
 ANA UWEZO MKUBWA WA KUPANDIKIZA NYOTA YA KUMPATA YEYOTE UMPENDAYE KWA 
KUMUOA AU KUWA NAYE. 
 ANAO UWEZO WA KUMRUDISHA ALIYE MBALI PIA ALIYE CHUKULIWA KWA NJIA YA MSUKULE 
 ANAO UWEZO WA KUUAq KESI SUGU NA PYA NDANI SIKU 7 TU. 

 MENGINEYO MENGI ZAIDI YALIYO KUWA SUGU PIGA-
 Mobile; 0717 70 32 41. 
 WhatsApp 06226 535419.

Kimenuka...Mahakama Yatoa ONYO la Mwisho Kwa Tundu Lissu.....

$
0
0
Mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu imempa onyo la mwisho Tundu Lissu kuhakikisha anafika katika kesi ya uchochezi inayomkabili Mahakamani hapo.

Onyo hilo limetolewa na Hakimu Mkazi Mkuu, Godfrey Mwambapa baada ya wakili wa serikali Mutalemwa Kishenyi kudai shauri hilo limeitishwa kwa ajili ya kusikilizwa lakini mshtakiwa Lissu hajafika Mahakamani.

Wadhamini wa Lissu hawakufika pia Mahakamani huku Wakili wa Lissu Jeremiah Ntobesya amedai kuwa mteja wake ana udhuru ambapo baada ya kuelezwa hayo, Hakimu Mwambapa amesema hii ni mara ya pili Lissu hajafika katika kesi hiyo hivyo anatoa onyo la mwisho ahakikishe anafika.

Hakimu huyo amesema kinyume na hapo hatua za kisheria zitachukuliwa ambapo baada ya maneno hayo  ameahirisha kesi hiyo hadi August 14/2017.

Katika kesi hiyo ya uchochezi (Dikteta uchwara) Lissu anadaiwa alitenda kosa hilo July 28/2016 katika eneo la Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Ilala Dar es Salaam.

Maelezo ya Waziri wa Viwanda Charles Mwijage Baada Rais Magufuli Kutamka Hadharani kwamba Haridhiki na Utendaji Wake

$
0
0
Jana (August 6, 2017) Rais Magufuli  alitoa kauli ya kutoridhishwa na hatua zinazochukuliwa na Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji dhidi ya watu waliouziwa viwanda na kuvitelekeza ambapo alimtaka Waziri Mwijage kuwanyang’anya na kuwapatia wawekezaji watao viendeleza.

Leo August 7, 2017 Waziri wa Viwanda Charles Mwijage amehojiwa kwenye Clouds 360 Clouds TV na kuelezea kuhusu hiyo kauli ya rais na kutoa hizi kauli.

”Kujenga viwanda sio mchezo, yapo maelekezo ya Rais viwanda vilivyo binafsishwa na havitumiki virudishwe, Rais alichokitegemea kwangu sio kile anachokiona sababu viwanda haviendi kwa kasi anayoiona na hii kuna sababu kadhaa.

“Hii sekta ya viwanda ni multi-sector maana kuna viwanda vipo chini ya Wizara ya Mifugo, vingine maliasili…. kuna viwanda vimechukuliwa lakini havipo kwenye orodha ya viwanda vilivyobinafsishwa, nahitaji Wakuu wa mikoa waingie hapa.

“Kuna watu wengine wameingia kwenye sekta ya viwanda lakini hawajui shughuli yake wengi wanang’ang’ania faida tu…. moja ya masharti ya viwanda watu walitakiwa kuviendeleza lakini kuanzia Ijumaa mimi nitaanza kutenda bila kuwa na maneno.

“Suala la kiwanda cha Mang’ula tayari mgogoro wake umefika Bungeni na mmiliki wake tayari ameitwa Bungeni kuhojiwa, kiwanda cha matairi Arusha tumekiongezea nguvu lakini tunahitaji muwekezaji ataekuwa na nguvu zaidi kwenye uzalishaji.

“Kiwanda cha General Tyre kina historia kubwa zaidi kilikuwa cha jumuiya ya Afrika Mashariki lakini sasa ni mali yetu, siwezi kumsemea Mh Rais najua ana imani na mimi sana ndio maana nilimuomba asinikumbushe tena siku nyingine.

“Anayetaka kujua viwanda vingapi vipo mkoa wa Pwani aanzie mkuranga mpaka zegereni kuna zaidi ya viwanda 20 hapo, kiwanda cha Mgololo mufindi kinafanya kazi lakini kuna baadhi ya shughuli nyingine za uzalishaji zinaendelea nje ya nchi.”  Amesema Waziri  Mwijage

JPM Awaziba Midomo Wanaotaka Aongezewe Muda wa Urais...Magazeti ya Leo Jumanne

$
0
0

JPM Awaziba Midomo Wanaotaka Aongezewe Muda wa Urais...Magazeti ya Leo Jumanne

Serikali Yaionya Kampuni Iliyosema Clouds FM Inaongoza Kusikilizwa Nchini Tanzania....

$
0
0

Siku chache tangu Kampuni ya GeoPoll ilipotoa takwimu za vituo vya redio na runinga vinavyosikilizwa na kutazamwa zaidi nchini, Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) imeingilia katika na kusema kuwa takwimu hizo ni batili.

Katika taarifa yake iliyotolewa leo Agosti 7, 2017, Ofisi ya Taifa ya Takwimu imesema kwamba takwimu hizo si rasmi kwa kuwa hukusanywa kwa mfumo ambao hautambuliki na NBS kwa mujibu wa kifungu cha 20 cha Sheria ya Takwimu ya mwaka 2015.

Siku chache zilizopita kampuni hiyo ilitoa takwimu zilizoonyesha kuwa Kituo cha Redio cha Clouds Fm ndicho ambacho husikilizwa zaidi nchini Tanzania huku kikifuatiwa na Radio Free Africa (RFA) na TBC Taifa.

Kwa upande wa vituo vya runinga, takwimu wa GeoPoll zilionyesha kuwa Clouds Tv ndiyo inaongoza kwa kutazamwa zaidi, huku ITV ikishika nafasi ya pili na kufuatiwa na East Africa Tv.

Kuona ripoti nzima ya GeoPoll kuhusu utazamwaji na usikilizwaji wa vyombo vya habari Tanzania bonyeza hapa

Katika taarifa ya Ofisi ya Takwimu hapa chini, wameitaka Kampuni hiyo kufuata taratibu zilizoanishwa katika Sheria ya Takwimu kwani takwimu zao za sasa hazijakidhi vigezo.

Kenya Waanza Kupiga Kura, Wadamka Usiku wa Manane

$
0
0
Wananchi nchini Kenya wameanza kupiga kura katika Uchaguzi Mkuu, wengi wakiwa wamewasili kwenye vituo vya kupigia kura usiku wa manane.

Kwenye kituo cha Shule ya Msingi Mutomo ambako Rais Uhuru Kenyatta atapiga kura watu wamefika hapo tangu saa kumi alfajiri.                      

Pia, kwenye kituo hicho cha Mutomo watu walikuwa wanafanya maombi huku wakiwashirikisha maofisa wa Tume ya Uchaguzi isiyokuwa na mipaka (IEBC) wa kituo hicho kuombea uchaguzi wa amani.                      

Kwenye kituo cha kupiga kura kilichopo Embakasi Social Hall kwenye jimbo la Embakasi East watu walikuwapo hapo tangu saa tisa usiku na kwa mujibu wa mwandishi wetu aliyeko Kenya Noor Shija anasema  foleni hiyo  ilikuwa ndefu umbali wa kiasi cha kilomita tatu.                      

Maeneo mengine ambayo watu wameamka  usiku  ni Mombasa, Naivasha na  Nairobi kwenye kituo cha Shule ya Msingi Kahawa ambako tangu saa kumi Watu wamejazana wakati muda wa kufungua vituo ni saa kumi na mbili.                      

Maeneo mengine imeelezwa vijana walikuwa wakizunguka mitaani wakipuliza mavuvuzela kuamsha watu wakapige kura.                      

Kwa upande wa Nasa  ratiba ya upigaji kura kwa wagombea wao ambapo Raila Odinga atapiga kura   Shule ya Msingi Olympic saa nne na nusu asubuhi                      

Kalonzo Musyoka atapiga kura Shule ya Msingi Tseikuru saa nne asubuhi                      

Musalia Mudavadi atapiga kura kituo cha Shule ya Msingi Chemakanga saa tatu asubuhi

Bunge la Afrika Kusini leo Litapiga Kura ya Kutokuwa na imani na Rais Zuma

$
0
0
Wabunge nchini Afrika Kusini leo wanatarajia kupiga kura ya siri ya kuamua kuhusu hoja ya kutokuwa na imani na Rais wa nchi hiyo, Jacob Zuma.

Baleka Mbete ambaye ni spika wa bunge hilo amefikia uamuzi huo mara baada ya vyama vya upinzani kufungua kesi mahakamani wakitaka ipigwe kura ya siri dhidi ya Rais wa nchi hiyo ya kutokuwa na imani naye.

Aidha, Wabunge hao wanaamini kwamba iwapo kura ya siri itapigwa, basi wabunge wa chama tawala cha African National Congress (ANC) ambao wanampinga Zuma watakuwa na uhuru wa kupiga kura dhidi ya rais huyo.

Chama cha ANC, ambacho kimetawala Afrika Kusini tangu kumalizika kwa utawala wa ubaguzi wa rangi wa Wazungu mwaka 1994, kina idadi kubwa ya wabunge katika bunge la nchi hiyo.

Hata hivyo, hili ni jaribio la hivi karibuni la kutaka kumuondoa madarakani Rais Zuma na linatokea mara baada ya  kumfukuza kazi waziri wa fedha aliyekuwa anpendwa sana na wabunge wengi, Pravin Gordhan pamoja na mawaziri wengine katika mabadiliko yake kwenye baraza la mawaziri mwezi Machi.

Alichopatia na Kukosea Rais Mgogoro wa Ruge na Paul Makonda...

$
0
0
Wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi kwa ajili ya ujenzi wa bomba la kusafirishia mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga, Tanzania mambo mengi yaliibuka na kufurahisha watu lakini mengine yaliwasikitisha na mengine kuibua mshangao mkubwa kwani hawakutarajia kama yangetokea.

Wakati akihutubia mamia ya wananchi waliojitokeza katika Kijiji cha Chongoleani nje kidogo ya Jiji la Tanga, Rais Magufuli alieleza ni kwa namna gani bomba hilo litaweza kuzinufaisha nchi hizi mbili (Tanzania na Uganda), lakini pia nchi nyingine za Afrika Mashariki.

Mbali na hilo, Rais Magufuli alivipongeza vikundi mbalimbali vya burudani vilivyotumbuiza katika sherehe hiyo vikiwepo vikundi vya kitamaduni na pia bongo fleva. Wakati akitoa pongezi hizo, alimuita jukwaani Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

Wawili hawa walikuwa na msuguano wa muda mrefu kufuatia tuhuma (ni tuhuma kwa sababu mahakama ndiyo yenye mamlaka ya kumtia mtu hatiani) zilizotolewa kuwa, alivamia ofisi za Clouds Media Group akiwa na Polisi wenye silaha na kushinikiza kurushwa kwa kipindi ambacho kwa mujibu wa Ruge, hakikuwa na uwiano kwani hakikushirikisha pande mbili wakati wa kukiandaa.

Kufuatia tukio hilo, vyombo mbalimbali vya kitaifa na kimataifa, taasisi na wanaharakati wa haki za binadamu na uhuru wa vyombo vya habari, wanasiasa waliungana pamoja wakitaka Rais Magufuli amuwajibishe Makonda lakini pia sheria ichukue mkondo wake ikiwa ni pamoja na Makonda kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma hizo.

Hadi naandika makala hii, hakuna hatua hata moja iliyochukuliwa kufuatia madai hayo ambayo hadi leo yameacha vidonda kwenye baadhi ya vyombo vya habari dhidi ya kiongozi huyo.

Baada ya Rais kuwaita jukwaani vijana hawa wawili, aliwataka washikane mikono na wafanye kazi pamoja. Rais aliamini kuwa kwa kufanya hivyo atakuwa amesuluhisha mgogoro wa pande hizo mbili na vijana hao wanaweza kushirikiana tena kwa ajili ya maendeleo ya jamii. Lakini ambacho wengi wamekiona, ni kama vijana hao wameamriwa kushirikiana (ombi la mkubwa ni amri), bila kutatua kwa usahihi matatizo yaliyowatenganisha.

Tukichambua kwa ufupi kitendo kilichofanywa na Rais mbele ya kadamnasi, tunaweza kufikia hitimisho kwa upande mmoja kwamba, lengo la Rais lilikuwa jema na zuri kabisa. Lengo la Rais ni kutaka kuona vijana hao na wengine nchini wanashirikiana na kufanya kazi kwa pamoja kwani huo ni msingi wa maendeleo. Hata wahenga walisema Umoja ni Nguvu na Utengano ni Udhaifu. Kwa lengo hili la kuleta umoja wa kitaifa, Rais alifanya kitu sahihi, na anastahili kupongezwa.

Kwa upande mwingine, licha ya kuwa lengo lake lilikuwa ni sahihi na lenye kujaa nia njema, njia aliyotumia kulifikia lengo lake haikuwa sahihi.

Mgogoro uliokuwepo/uliopo kati ya Ruge na Makonda si mgogoro wa watu wawili tena kiasi kwamba unaweza ukawaita na kuwaweka katika chumba ukawapatanisha wao na mambo yakawa sawa. Mgogoro huo ulipofikia ulikuwa ni mgogoro wa jamii dhidi ya kiongozi, mgogoro wa taasisi dhidi ya kiongozi, mgogoro wa tasnia ya habari dhidi ya kiongozi.

Tuchambue kwa ufupi, kwanini tunaeleza kwamba kuwashikisha mikono watu hawa wawili kunaweza kusitoe suluhisho la kudumu kwenye mgogoro wao;

Wakati tukio hilo limetokea, Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) lililaani tukio hilo na kuvitaka vyombo vingine vya habari kutoandika habari za Makonda wakiamini kuwa kwa kufanya hivyo ingekuwa ni njia bora ya yeye kujirudi na kuomba radhi kwa kitendo kile, au ilikuwa ni njia ya kuonesha Wahariri na waandishi wa habari katika umoja wao, hawaungi mkono kitendo cha kuvamiwa kwa kituo cha habari.

Lakini sasa tujiulize, Rais kuwataka Ruge na Makonda wapatane, msimamo wa Jukwaa la Wahariri Tanzania unakuwa upande gani. Chombo hiki maalum kwa ajili ya kutetea maslahi ya waandishi wa habari kimeachwa katika hali gani?

Mbali na TEF, vyombo vingine vya habari kwa kuchukizwa na kitendo hicho, vilisitisha kurusha habari za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam. Lakini baada ya kilichotokea mwishoni mwa juma, vyombo hivi vinaendelea na msimamo upi? Endapo wewe ulimchukia mtu kwa vile alimpiga rafiki yako, waliopigana wakipatana, wewe utabaki na chuki au utamsamehe aliyempiga rafiki yako?

Kama ilivyo kwa vyombo vya habari vilivyoachwa njia panda visijue cha kufanywa, ndivyo vivyo hivyo ilivyo kwa maelfu ya wananchi na wanaharakati wa haki za binadamu na walivyoachwa njia panda bila kujua msimamo wao ni upi.

Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kililaani kitendo cha kuvamiwa kwa Clouds Media Group huku waandishi wa habari wakitishiwa kutajwa katika orodha ya watumiaji wa dawa za kulevya. Taasisi hii na nyingine zilizotaka hatua sahihi zichukuliwe ili wahusika waadhibiwe kuweza kuzuia vitendo kama hivi wakati mwingine, vimeachwa katika hali gani?

Ieleweke kwamba, hakuna mtu aliyetaka mgogoro huu baina ya pande hizo mbili uendelee. Kuendelea kwake hakutoi mazingira mazuri kwa ukuaji wa sanaa kwa namna moja, lakini pia wananchi nao walikuwa wanakosa baadhi ya taarifa kutoka kwa kiongozi wao wa mkoa kwa upande mwingine.

Lakini wengi walitaka jambo hili limalizwe katika njia ambayo pande zote zingeriadhia na bila kuacha manung’uniko ya huyu kuona hakutendewa sawa.

Kwa ushahidi wa kimazingira, ni dhahiri kuwa mgogoro huo umekwisha na kama haujaisha basi kwa sasa hauna kichwa wala miguu, lakini swali moja linalobaki ni, Je! Wahusika wameriadhia kwa mioyo yao kuyamaliza au kwa sababu ametakiwa kufanya hivyo na Rais. Na ujue, huwezi kukataa ombi la Rais, kwani kiuhalisia hakuombi, anakuagiza!

Utatuzi huu unatoa nafasi ya tatizo kujirudia au kutojirudia?

Okwi Afunguka 'Mnaosema Nimeishiwa Njooni Muone Mavitu Yangu....

$
0
0
KIUNGO mshambuliaji wa Simba, Mganda, Emmanuel Okwi amefunguka kuwa amejipanga kuonyesha kiwango cha hali ya juu kwenye mchezo wa leo ili kuwathibitishia mashabiki ambao wana hofu na uwezo wake baada ya kushindwa kutamba alipokwenda nchini Denmark kabla ya kurudi kwao Uganda.

Okwi aliyetua Simba akitokea SC Villa, ataungana na mastaa wengine wa Simba waliosajiliwa hivi karibuni kuonekana kwa mara ya kwanza wakikichezea kikosi hicho kwenye mchezo waSimba Day mbele ya Wanyarwanda,Rayon Sports.

Mshambuliaji huyo ameliambia Championi Jumanne, kuwa atabadilisha mawazo ya mashabiki wengi leo ambao walimuona hana jipya baada ya kushindwa kutamba alipokwenda Denmark kwa kuonyesha kiwango cha hali ya juu dhidi ya Rayon Sports.

“Najua mashabiki wengi wana hofu na uwezo wangu kwa sababu muda mrefu umepita baada ya kuondoka hapa Tanzania, lakini niwaambie kwamba kama wanataka kuona nini ambacho nitakifanya basi waje uwanjani katika Simba Day.

“Kile ambacho nitakifanya kwa kila mmoja kitabaki historia, na nikwambie niko vizuri sana na naelewana na wenzangu vizuri baada ya kukaa nao kule Afrika Kusini tulipokuwa kambi,” alisema Okwi.

Mwimbaji Lulu Diva Alilia Penzi la Belle 9

$
0
0
Mwimbaji Lulu Diva Alilia Penzi la Belle 9
MREMBO aliyewahi kutikisa kwenye masuala ya kuuza sura kwenye video za Kibongo, kisha kuhamia kwenye muziki, Lulu Abbas ‘Lulu Diva’ , amefunguka kuwa hajawahi kujutia hata siku moja kuwa na mahaba na mwanamuziki Abednego Damian ingawa malengo yake ya kuwa naye kwenye uhusiano hayakuwahi kufanikiwa.

Akizungumza na Uwazi Showbiz, Lulu Diva alisema Belle 9 ni kijana ambaye amewahi kuutesa sana moyo wake na yeye analifahamu hilo kwa sababu alishawahi kumwambia, hata hivyo hakuweza kumkubalia kwa sababu alimwambia kuwa yupo kwenye uhusiano na hakuwa tayari kuchepuka.


“Sijawahi kujutia kumpenda Belle 9, kwa ndoto za kuwa naye kwa sasa sina tena maana ilishindikana wakati moyo wangu unamhitaji zaidi, kwa sasa nipo kwenye uhusiano, ninampenda mtu niliyenaye lakini hata Belle 9 nitaendelea kumpenda na kumheshimu kwa sababu ni miongoni mwa watu wenye nafasi moyoni mwangu,” alimaliza Lulu Diva.

 STORI: BONIPHACE NGUMIJE

Mama Anayedaiwa Kumuacha Mwanae Peke yake Asubuhi Hadi Usiku Kila siku

$
0
0
Hekaheka ya leo August 7, 2017 inamuhusu mama ambaye analalamikiwa na majirani akidaiwa kumuacha mtoto wa miaka mitatu mtaani kuanzia saa 12 Asubuhi hadi saa 3 Usiku bila kujua anakula wapi wala anacheza wapi.

Mama huyo amelalamikiwa na majirani ambao wanasema amekuwa akimuachia mtoto huyo Tsh. 1000 huku akidai kumuacha mtoto huyo kwa mama muuza mboga ambaye pia hashindi nyumbani.

Bonyeza Play hapa chini kusikiliza mkasa mzima..

Soma Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo

$
0
0

Mwimbaji Ben Pol Aamua Kuufanya Uhusiano Wake na Ebitoke Uwe wa Siri...Ataki Maswali

$
0
0
Msanii wa RnB Bongo, Ben Pol ameweka wazi kuwa kwa sasa hapendi kuulizwa maswali kuhusu Ebitoke, mtoto na mahusiano.



Muimbaji huyo amesema kutokana na kazi zake ambazo anataka kuzifanya kwa sasa inamlazimu kufanya hivyo.

“Kwa series ya kazi zangu zinazokuja ningependa sana vitu binafsi nisiviongelee zaidi au hadi pale nitakapokuwa tayari kuzungumzia Ben Pol anafanya nini sasa hivi nianze kuzungumzia,” Ben Pol ameiambia Bongo5.

Ameongeza kuwa, “kwa hiyo sipo comfortable sana kusema vitu binafsi mahusiano, sijui mtoto nataka kupunguza kuvizungumzia hivyo vitu kwa sasa hivi kusema kweli,” amesisitiza.

Ben Pol ambaye anadai kuwa katika uhusiano wa kimapenzi na mchekeshaji Ebitoke amebainisha hilo ili kufanya uhusiano wao kuwa binafsi zaidi.

Video: Madee Amemchana Tena Nay Wa Mitego

$
0
0
Msanii wa Bongo fleva kutoka kitaa cha Manzese ambaye ndiye anayetambulika kama Rais wa Manzese, Madee, amemchana mwenzake kutoka kitaa hicho, Nay wa Mitego kwamba yeye ni raia wa kawaida na hana uwezo wa kuwa Rais wa Manzese

Katika mahojiano maalumu na mtandao wa Muungwana Blog msanii Madee aliamua kujibu kwa kusema " Sijawahi kuwa na matatizo na mtu yoyote, Nay ni mdogo wangu kabisa amekuwa ninamuona, kwa hiyo ni Nay ninamuona raia wangu mwema kama wengine wanaoishi mnzese"

TAZAMA FULL VIDEO HAPO CHINI

Nchi ya Congo Imefungia Mitandao yote ya Kijamii

$
0
0

Serikali ya DR Congo imetoa amri ya kusitishwa kwa mitandao yote ya kijamii ili kuzuia usambazaji wa picha na video za ghasia zinzoendelea katika kanda hiyo .

Aidha hatua hiyo imechukuliwa kufuatia ongezeko la upinzani dhidi ya rais Joseph Kabila ambaye amekataa kujiondoa madarakani wakati awamu yake inamalizika mwezi Desemba .

Migomo ya kitaifa imepangwa kufanyika Jumanne na Jumatano .

Mapigano ya Jumatatu baina ya kundi la Bundu dia Kongo na vikosi vyaa usalama ,lilipelekea vifo vya watu 14 kutokea .

Mkuu wa idara ya mawasiliano nchini humo Oscar Manikunda Musata amefahamisha kwamba mitandao ya kijamii kama Twitter,Whatsap ,Facebook na Instagram itafungwa kwa muda .

Madai ya Mwanamuziki Nandy Kudaiwa Kuchukua Nafasi ya Ruby.."Ruby Afungukia Nandy"

$
0
0
Madai ya Mwanamuziki Nandy Kudaiwa Kuchukua Nafasi ya Ruby.."Ruby Afungukia Nandy"
Msanii wa muziki Bongo, Ruby amesema hawezi kumchukia msanii mwezake Nandy ambaye watu wamekuwa wakidai amechukua nafasi yake kwenye muziki.

Hitmaker huyo wa ‘Na Yule’ amedai maneno ya watu hayawezi kumfanya akamchukia Nandy au kuonea wivu mafanikio wake bali anafurahi pia anapoona anafanikiwa zaidi.

“Kwanza siwezi nikamchukia Nandy kwa sababu watu kama hawajui sisi tumeshafanya kazi, kuna wimbo kipindi nipo THT unaitwa Mama ya Butterfly Group, tupo mimi Nandy, Maua Sama na Alice, kwa hiyo siwezi nikamchukia kwa sababu anafanikiwa,” Ruby ameiambia FNL ya EATV na kuongeza.

“Furaha yangu ni kuona anafanikiwa maisha yake yote kwa sababu ni mtu nimeshafanya naye kazi mara kibao, tumeshakutana mara kibao studio. Kwa hiyo mimi naona hizi rumors za watu zinazoendelea out site sijui kachukua nafasi yangu ni maneno ya watu ambayo yapo kila kukicha lakini hayawezi kunigusa mimi nimchukie Nandy na siwezi nikajifaninisha naye,” amesisitiza Nandy.

Msanii wa Nay wa Mitego katika wimbo wake uitwao Moto kuna mistari anatamka kuwa pengo la Ruby ni Nandy kitu ambacho kimekuwa kikizungumzwa mtaani na mitandaoni.

Kutana na Mtabibu wa Asili Allan Shariffu Musa Mtabibu wa Nyota za Binadamu na Dawa za Asili

$
0
0
Kutana na Mtabibu Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH shariffu musa Mtabibu wa Nyota za Binadamu na Dawa za Asili ya Africa Mwenye UWEZO Kubaini tatizo lako Pindi tu Utakapo Fanya Mawasilino Kupitia Wasaa Husika..JE UNASUMBULIWA NA Mapenzi? (Umeachwa na Umpendae,Awe Mume,Mke na Bado unampenda?Na Umejaribu Sehemu nyingi Bila Mafanikio?Wasilina na shariffu musa Ujione muujiza wa Papo kwa Papo.. anauwezo WA KURUDISHA MAHUSIANO NA KUIMARISHA NDOA YAKO NDANI YA SAA 12 TU. Umekimbiwa na Mumeo,mkeo au Mpenzi na anaishi na mtu mwingine? Muone akutatulie Anauwezo wa Hali ya Juu wa Kusambalatisha Mahusiano yao Endapo utafata Atakacho kuelekeza.
Atamfanya Atimize Ahadi zote kwa Muda Mfupi.
Maalim Hussein Anatumia Jina la Muhusika au Picha Kumaliza Tatizo lako..
Anatibu kwa Kutumia Vitabu vya QUR-AN Dawa za Asili za Africa,Dawa za Kiarabu na Majini.Anatafsiri Ndoto. Kushinda BAHATI NASIBU, KUSAFISHA NYOTA. Mvuto wa Mwili na BIASHARA, Kinga ya Mwili,ZINDIKO za Nyumba.MIGUU Kufa GANZI.Kufungua KIZAZI kwa wale walio fungwa kwa njia za KISHIRIKINA. Anakupa Jini la Mali kwa yule anaehitaji Utajiri BILA MASHARTI. Nguvu za KIUME, Humaliza Kesi zilishindika ndani ya siku 14 tu..na mengi zaidi

+255 629793352 au watsap
+255 679119679

NB: TIBA KWA DINI ZOTE NA IMANI ZOTE...

Video: Baby Madaha Afunguka Kisa Cha 'Jini Kabula' na Kuugua Kwake Ukichaa

$
0
0
Video: Baby Madaha Afunguka Kisa Cha 'Jini Kabula' na Kuugua Kwake Ukichaa

Msanii wa muziki wa bongo fleva, Baby Madaha amefunguka sababu zilizopelekea msanii Jini Kabula kupatwa na matatizo na kusema kuwa Jini Kabula aliamua kuachana na muziki wa dunia na kuanza kufanya muziki wa Mungu.

Baby Madaha anasema msanii huyo alipojitoa kwenye kundi lao la Scorpion girl alipata rafiki mwingine ambaye walikuwa wakishirikiana katika mambo yao na kusema mpaka anapatwa na matatizo hayo walikuwa ni marafiki lakini cha ajabu rafiki yake huyo na Jini Kabula alikuwa anaficha juu ya ugonjwa wa Jini Kabula.

Tazama Video hapa kufahamu mengi zaidi kutoka kwa Baby Madaha na Isabela

Kimenuka..Halima Mdee Aiwashia Moto Bodi ya Mikopo..Adai Inabagua Watu Kielimu

$
0
0

Mbunge wa jimbo la Kawe kwa tiketi ya CHADEMA Mhe. Halima Mdee ameijia juu Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu nchini (HESLB) na kusema bodi hiyo inataka kukandamiza elimu sekta ya elimu kwa kufanya ubaguzi.

Halima Mdee amesema hayo leo alipokuwa akiongea na waandish wa habari katika Makao Makuu ya Chama Cha Demokrasia na Mandeleo (CHADEMA) yaliyopo Kinondoni jijini Dar es Salaam

"Kifungu cha tisa kinasema kuwa waombaji ambao wazazi wao ni Wakurugenzi au Mameneja Waandamizi katika makampuni binafsi yanatotambulika na mamlaka za mapato na usajili hatarajiwi kuomba, lakini kifungu cha pili cha kumi kinasema waombaji ambao wazazi wao ni viongozi wa Umma, au kisiasa ambao wanatajwa na sheria ya maadili na viongozi wa umma na wenyewe hawatarajiwi kuomba mikopo, sasa watu wa kawaida wakisikia viongozi ambao wanajaza fomu za maadili wanajua labda kwenye ubunge au mawaziri lakini hata katika hizo gazi za ubunge, uwaziri au mameneja unamnyimaje mtu haki yake ya Kikatiba ya mtoto wake kupewa fursa ya elimu sambamba na mikopo kwa kudhania kwa kuwa mtu huyo ana nafasi hiyo anaweza kulipa utajuaje pengine mtu huyo analipia watoto kumi au ishirini kwa mwaka" alihoji Halima Mdee 

Halima Mdee amedai kuwa wanatumia hoja nyepesi na hovyo zisizo na mantiki kuwabagua watu kielimu

"Wakati UKAWA tunaeneza Ilani yetu tulisema kuwa tutatoa elimu bure mpaka Chuo Kikuu pasipokubagua kwa sababu ni jukumu la serikali kutoa elimu kwa watoto wake, sasa wenzetu wao wanaotuambia kila mwezi mapato TRA yanakuwa wanaanza kutapatapa yaani wali copy na kupaste sera ambayo hawawezi kutekeleza sasa hivi wanaanza kutumia visingizio kuanza kubagua Watanzania, sasa hili suala tutalikemea na kuendelea kukemea" alisema Halima Mdee 

Siku ya Jumamosi ya tarehe 5 Agosti mwaka huu Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu nchini (HESLB) imetoa mwongozo na vigezo vya utoaji mikopo kwa mwaka wa masomo 2017/2018 ambapo bodi hiyo imeanza kupokea kupokea maombi ya mikopo kuanzia tarehe 6 Agosti 2017 hadi tarehe 4 Septemba, 2017.

Rais Yoweri Kaguta Museveni Atoa Kali, Abadili Tarehe yake ya Kuzaliwa ili Agombee Urais Tena

$
0
0
Rais Yoweri Kaguta Museveni Atoa Kali, Abadili Tarehe yake ya Kuzaliwa ili Agombee Urais Tena
Kwa muda mrefu sana kumekuwa na mijadala hasa katika mitandao ya kijamii nchini Uganda kuhusu umri halisi wa Rais wa nchi hiyo, Yoweri Kaguta Museveni.

Kwa mara kadhaa serikali ya Uganda imekuwa ikinukuliwa ikisema kwamba Rais Museveni alizaliwa mwaka 1944, lakini kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka jana vyama vya upinzani vilikuwa vikimkosoa Rais Museveni kwamba anadanganya kwa kusema ana miaka 71. Vyama hivyo vilidaiwa kuwa alikuwa na zaidi ya umri wa miaka 75 na asingeweza kugombea tena.

Lakini mjadala mpya umeibuka ambapo Ikulu ya Uganda imechapisha nyaraka kwenye ukurasa wake wa Facebook zinazoonyesha kwamba nyaraka za ubatizo wa Rais zimeandikwa tarehe yake ya kuzaliwa ambayo ni 3 Agosti 1947 na hivyo sasa ana miaka 70.

Kwa minajili hiyo, Rais Museveni atakuwa na umri wa maika 74 wakati Uganda itakapofanya uchaguzi mwingine mwaka 2021 na hivyo ataweza kugombea tena katika awamu ya sita.


Museveni alibadilisha katiba ya Uganda mwaka 2006 ili kuweza kugombea awamu ya tatu. Kwa mujibu wa gazeti la Daily Monitor la nchini humo, Rais amewahi kusema kwamba hafahamu tarehe yake ya kuzaliwa.
“Wazazi wangu hawakwenda shule na hivyo hawakujua tarehe,” alinukuliwa Rais Museveni mwaka 1997 alipokuwa akitoa taarifa zake katika mahojiano maalum.
Nyaraka zake za Ubatizo zilizotolewa na Ikulu ya Uganda.


Mkanganyiko huu umekuja ikiwa ni takribani wiki moja tangu Rais Museveni aliposema kuwa katika kipindi cha miaka 31 alichokuwa madarakani hajawahi kuugua.

“Umewahi kusikia Museveni ameumwa na miguu yake kuning’inizwa hospitalini kwa miaka 31 iliyopita? Hii ni kwa sababu nafuata hatua za msingi za afya ambazo zimenisaidia kuepukana na magonjwa. Magonjwa haya yanaweza kuzuilika,” alisema Museveni akitamba kwamba afya yake ni imara.
Viewing all 104789 articles
Browse latest View live




Latest Images