Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104809 articles
Browse latest View live

Tanzania Hatuna Bahati...Tumeshuka Tena Viwango vya Mpira FIFA.......

$
0
0
SHIRIKISHO la Soka la Kimataifa (Fifa), jana Alhamisi lilitoa viwango vya soka vya mwezi Julai kwa mataifa mbalimbali ambapo Tanzania imeshuka kwa nafasi sita kutoka 114 ya hadi 120.

Wakati kimataifa Tanzania ikishika nafasi ya 120, kwa upande wa Afrika ipo nafasi ya 35, huku ikiwa ya nne katika Ukanda wa Afrika Mashariki ambapo Uganda inaongoza ikifuatiwa na Kenya, kisha Rwanda na Burundi inaburuza mkia. Katika nafasi kumi za juu kwenye orodha hiyo, Brazil inaongoza ikifuatiwa na Ujerumani, Argentina, Uswizi, Poland, Ureno, Chile, Colombia, Ubelgiji na Ufaransa inahitimisha.

Wema Sepetu Afunguka Haya Kuhusu Wahasimu Wake Kajala Masanja na Munalove

$
0
0
Wema Sepetu Afunguka Haya Kuhusu Wahasimu Wake Kajala Masanja na Munalove
STAA wa filamu mwenye nyota ya kipekee Bongo, Wema Sepetu amefunguka kwa mara ya kwanza kuwa hajawahi kuwakumbuka (kuwamis) waliokuwa mashoga zake wa damu, Muna Alphonse ‘Muna’ na Kajala Masanja na kudai alishawatoa kwenye akili yake.

Akizungumza na Star Mix, Wema alisema kuna baadhi ya watu ambao hajaonana nao muda mrefu na anawakumbuka kila mara lakini kwa upande wake hajawahi kuwakumbuka rafiki zake hao ambao huko nyuma walikuwa kama kumbikumbi.

“Sitaki kusema dhambi jamani sijawahi kuwamisi hawa watu (Muna na Kajala) kabisa naona kama niliwafuta kwenye kichwa changu maana najikuta kuna watu nawakumbuka lakini hao hapana,” alisema Wema.

Roma Mkatoliki si Mtu Mzuri...Wimbo wake Wazidi Kuleta Taharuki Kwa Mashabiki

$
0
0
Katika wimbo huo Roma Mkatoliki amejaribu kuhusisha matukio mbalimbali ya kisiasa pamoja na lile la kwake kubwa la kutekwa ambapo hii ndiyo kazi yake ya kwanza tokea ule mkasa wake wa kutekwa kuisha na kusababisha maumivu mengine makali kutoka kwa mashabiki zake baada ya kuona 'video' yake mpya iliyojaa hisia kali za maumivu.

Hata hivyo, kupitia ukurasa wake wa 'youtube' alioweka video hiyo mpya watu zaidi ya 668 wametoa maoni yao jinsi walivyoupokea ujio mpya wa Roma na hizi ni baadhi tu ya zile zilizoandikwa na mashabiki wa Roma.

Pharergy Ramson: "Roma ukienda Zimbabwe harakat atazifanya nani 'but' ngoma iko poa hujawahi kuniangusha ila umebadirika kidogo mzee. Nadhan kwenye hii ngoma umejibu maswali ya watu wengi sana kipindi unafanya 'show' pale 'Dar live' nilitamani urudie hii nyimbo 'but' sikuwa na uwezo ila umefanya vizur."

Blandina Bilau: "Simjui sana Roma wala kufuatilia nyimbo zake lakini huu wimbo umeniliza, 'message' imefika jipe moyo. Mtetezi wako Mungu aendelee kukutetea"
Arthur Oyaro: "Duuh 'so sad' na utu uzima huu machozi nimeshindwa kuyazuia,'thank' pia kwa kunifikirisha. Viva Roma viva''

Mdachi Classic: "Nimefatilia 'comment' nyingi sana ila sijaona hato komenti inayozungumzia vibaya hii ngoma zaidi ni za upendo na za kuumizwa tu. 'In short' hii imetugusa sana pole sana kaka yupo mungu hakimu wa yote".

Ibrahim Utenga: ''This song reflects the real prevailing situation, it's very sensitive song, congratulations to you brother, God save you "

Ndongo Nyambalya: "Nina wasiwasi wewe Mkatoliki hicho siyo kichwa ni semi-computer,  kwenye Mungu wa John na Daud hapo nimefikiria hadi najikuta nurudiarudia kusikiza, U deserve bro! Gat u! 100".

Kwa upande mwingine, Roma Mkatoliki amemwagiwa sifa kedekede na mashabiki zake ambao walikuwa wamemisi kusikia na kuona kazi zake kwa kipindi kirefu tokea alipopatwa na mkasa wa kutekwa miezi michache iliyopita na kuweza kurudi katika uhalisia wake bila ya kuhofia jambo lolote litakaloweza mtokea tena mbele yake kwa ukali wa tungo zilizojaa za kufikirika.

Serikali ya JPM si Mchezo Yataifisha Magari ya Kifahari Yaliyokamatwa Rais Bandarini

$
0
0

  Serikali ya JPM si Mchezo Yataifisha Magari ya Kifahari Yaliyokamatwa Rais Bandarini
Serikali imetaifaisha magari matatu ya kifahari kati ya saba yaliyokutwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwenye makontena, alipofanya ziara ya kushtukiza bandarini na kubainika hayakuwa na Nyaraka stahiki.


Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Biswalo Mganga amesema kuwa Mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu imeamuru washtakiwa wa magari hayo Sulatani Ibrahimu raia wa Uganda na Ramadhani Ukwaju wa Tanzania kulipa faini.

Kati ya Makosa wanayoshtatikiwa nayo watuhumiwa hao ni pamoja na udanganyifu kwa maafisa forodha kuhusu vitu walivyokuwa wameviingiza nchini ambapo nyaraka zao walionyesha walikuwa wameingiza viatu na nguo za mitmba lakini kwenye makontena kulikua na magari hayo ya kifahari.

Aidha kosa lingine wanaoshatikiwa watuhumiwa hao ni pamoja na kusabiashia serikali hasaara zaidi ya milioni tisini kutokana ukwepaji wa kodi kutoka na uingizaji huo wa magari ya thamani kwa kulipa ushuru kidogo wa nguo na viatu.

Mke wa Roma Afunguka Asema Kuchepuka ni kwa Kila Mwanaume Si Roma Tu

$
0
0
Mke wa Roma Afunguka Asema Kuchepuka ni kwa Kila Mwanaume Si Roma Tu
Mke wa msanii Roma ameelezea jinsi mahusiano yake ya ndoa na rapper huyo yalivyo na kudai kuwa tabia ya wanaume kuchepuka kwenye ndoa ni wote wanayo.

Baby Mama (Nancy) huyo ambaye alifunga ndoa na Roma mwaka 2015 ameiambia XXL ya Clouds Fm kuwa ni vigumu kujua kinachoendelea nyuma ya pazia kwa mwanaume ila kutokana na urafiki na upendo kuna baadhi ya mambo kwa mumewe husamehe tu.

“Kucheat ni kwa kila mwanaume, siyo Roma tu ni vitu ambavyo vipo, unaweza ukachitiwa pasipo kujua au kwa kujua, huwezi kujua nyuma ya mwanaume kuna nini, unaweza kusema mimi namjua lakini hapana huwezi ukamjua kwa asilimia zote, sijawahi kuona kwa macho ila tabia ipo kwa wanaume ndani yao,” amesema

Kuhusu kuweza kudumu katika ndoa na mtu maarufu hasa msanii, alisema, “kikubwa ni upendo halafu kingine nilielewa kazi yake mapema, nikawaza kuhandle situation yote maana kuwa na mtu maarufu kuna vitu vingi katikati, yeye ni mwanaume, kwa kawaida wanaume wanakuwa na tabia tofauti halafu kuongeza na ule maarufu inazidi kuzaa vitu vingine tofauti,” amesema na kuongeza.

“Halafu kingine kilichosaidi kudumu mimi na Ibra ni rafiki yangu kabla hatujawa wapenzi, kwa hiyo ukiweka upendo, urafiki, hata akifanya nini unaona ngoja nimsamehe tu,” amesisitiza.

Mke wa Roma ndiye aliyepita katika media mbali mbali kutambulisha wimbo mpya wa Roma ‘Zimbabwe’ kwa madai kuwa mumewe amepata safari ya ghafla kwenda nchini Zimbabwe.

WanaompondaHamisa Mobetto Kwasababu ya Zari Watolewa Povu na Msanii Lucy Komba

$
0
0
Msanii wa filamu, Lucy Komba amewatolea uvivu Watanzania katika mitandao ya kijamii ambao wanamponda mtanzania mwenzao, Hamisa Mobetto kisa mama watoto wa Diamond, Zari The Bosslady.

WanaompondaHamisa Mobetto Kwasababu ya Zari Watolewa Povu na Msanii Lucy Komba


Mobetto ambaye ni mwanamitindo maarufu nchini, wiki iliyopita alijifungua mtoto wa kiume ambaye baba yake hakutambulika mara moja. Lakini tetesi ambazo zinazunguzwa kwenye mitandao ya kijamii ni kwamba mtoto huyo ni wa Diamond hali ambayo imezua hataruki kati ya timu Zari na timu, Mobetto.

Ukweli wa yote anaujua mwanamitindo huyo lakini katika mitandao ya kijamii kimezuka kikundi ambacho kinajiita ni timu Zari na kuamua kumtukana Mobetto hali ambayo imemfanya muigizaji, Lucy Komba ambaye anaishi nchini Sweeden ashindwe  kuvumilia na kuamua kuingilia kati sakata hilo.

“Samahani lakini kimenichoma. MABOGAS YA TZ YANAMPONDA MTZ MWENZIO YANAMSIFIA BOGAS MWENZIO sijui yanafikiri yatapewa ule urithi. Mbona waganda hawambabaikii acheni umasikini wa kujirahisisha. Au mnafikiri mtapitishiwa kila mmoja karanga moja moja ya bure,” aliandika Lucy Komba Instagram.

Aliongeza, “Hongera mwanamke mwenzangu, wanajifanya roho ngumu tu kukuponda wakati roho zinawauma unatoa vitu hasa mwanamke unazaa huku unatabasamu ☺. Wale wanaoniponda eti ningekuwa mzalendo nisingeolewa na mzungu, Yes nimeolewa na mzungu sababu sina ubaguzi wa rangi wala ukabila na tangu nimeolewa sijawahi kutukana kaka zangu wakisfrika kwa hiyo lazima mjue kutofautisha A na B. Pili anayewapa taarifa nimeachwa nahisi kama kachelewa kuwataharifu halafu mwambieni awape taarifa kamili maana huwa anaingia insta na kuzizungusha bado hajawapata taarifa za kunichamba huku mmesimaisha visimi 😂😂😂. Ukweli unauma mmepewa ukweli wa huyo stranger wenu aliyenenepesha miguu kiuno kimeshindikana kukipunguza mnalia chambeni tu mniongezee followers maana nilikuwa sijaamka bado kujua kumbe umaarufu wa bongo unatokana na vichambo 😂😂😂😂😂😂😂 GOODMORNING.,”

Mpaka sasa bado mwanamitindo huyo hajaweka wazi kwamba mtoto huyo ni wa nani. Pia huyo ni mtoto wa pili ambapo  wa kwanza alizaa na Mkurugenzi wa EFM, Majay

MBOWE: Kilimanjaro Hatutegemei CCM

$
0
0
Mbunge wa Hai na Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe amefunguka na kusema kuwa mkoa wa Kilimanjaro hawategemei CCM kwa ajili ya maendeleo ya mkoa huo na kusema kitu pekee ambacho kinafanya mkoa huo kuwa wa mfano kwa mageuzi ni kutokana na elimu.


Freeman Mbowe amesema hayo alipokuwa akizungumza na wakazi wa Machame Uroki katika ziara yake ya jimbo na kusema kuwa Kilimanjaro inakuwa kimaendeleo kutokana na baadhi ya wazee miaka hiyo kupata elimu ya kutosha ambayo ndiyo imekuwa chachu ya maendeleo hayo.

"Sifa kubwa ya kwanza katika taifa hili kuhusu mkoa wa Kilimanjaro ni elimu, wazee wetu walisoma siyo wote ila wachache waliosoma walisoma sana kulinganisha na mikoa mingine kwa hiyo maendeleo ya Kilimanjaro hayategemei CCM, bala maendeleo ya Kilimanjaro yalikuwepo hata kabla ya uhuru watu walisoma siku nyingi na watu walipata imani siku nyingi, sifa hii ni lazima tuirejeshe, tuna shule nyingi lakini shule nyingi ni zile ambazo hazina sifa ya kuitwa shule" alisema Mbowe 

Aidha Mbowe aliwataka watu kuwekeza nguvu kubwa kwenye elimu kwa watoto wao kutokana na ukweli kwamba ardhi ya kuweza kuwarishisha watoto kwa sasa haipo Kilimanjaro hivyo wanapaswa kuwekeza zaidi na zaidi kwenye elimu na kusema anatambua kuwa wanafanya hivyo ila bado haitoshi wanapaswa kuongeza nguvu zaidi na zaidi.

Tembelea Blogu ya Asili zetu Upate Kufahamu Mambo Mbalimbali Kuhusiana na Tiba za Kisunnah na Asili

$
0
0
Tembelea Blogu ya Asili zetu upate kufahamu mambo mbalimbali kuhusiana na tiba za kisunnah na asili, utabiri wa nyota yako, aina za majini wanaowatesa wanadamu, viumbe wanaoharibu biashara za  watu, ilimu ya nyota na masuala ya mahusiano.

Pia kwa wale wanaosumbuliwa na ndoto mbaya, wanaohitaji kusafisha nyota, mvuto wa biashara, kupandishwa cheo, kufata kesi mahakamani, kumvuta umpendae, dawa za nguvu za kiume na waliodhulumiwa mali zao.

Tembelea Asilizetu.wordpress.com

Tulisema Kwamba "Roma Mkatoliki Usiposema Ukweli Utatukosea Sana... " Leo Umesema kwa njia ya Sanaa

$
0
0
Nimeisikiliza wimbo mpya wa Roma mkatoliki Leo
Nimependa pale anaposema ""Mungu wa daudi mungu wa Paulo na mungu wa yohana""""
Hio sentensi hapo naona inamajibu karibu yote ya kutekwa.

Rapa Roma Mkatoliki ameachia video ya wimbo wake ‘Zimbabwe’ ukiwa ni wimbo wake wa kwanza tangu alipotekwa na kuteswa kwa siku tatu.
Kupitia ‘Zimbabwe’ Roma amesimulia tukio la utekaji wake, watu anaoamini walimteka na sababu za kuamua kutoendelea kufuatilia jarada la upelelezi wa tukio hilo.

Mkali huyo pia amezungumzia kitendo cha baadhi ya wasanii wenzake kutomtembelea alipokuwa anauguza majeraha ya mijeredi ya watesi wake.
Pia, rapa huyo amezungumzia kauli ya Mbunge aliyedai bungeni kuwa amemtukana mkuu wa nchi.

Mkali huyo wa mashairi yenye mvuto wa maajabu (Rhymes of Magic Attraction) amekanusha tetesi kuwa watekaji wake walikuja na Noah huku akiwachana kuwa waachane na tabia za kutekana na kutumia silaha bali washindane kwa hoja. VIDEO:


Mashairi ya Wimbo

Wengi mlijiuliza walionteka ni maaskari?
Mkanitafuta vituo vyote central hadi stakishari
Wakasema… hawajui nilipo mama alienda hadi mochwari
Dah.....
Ya Kaisari mwachie Kaisari
Machozi yenu yatalipwa mimi nafunga na kusali

IMBA ROMA IMBA X3

Mungu wa Paulo… ndio Mungu wa daudi
Na ndio Mungu wa John mnayemuita Yohana wa Yahudi
Mwanangu alimuuliza, mama baba lini atarudi?
Na mke wangu aliwaliza kuwashukuru sinabudi

Fahamu yakuwa..

Me sio tu rappa pia ni baba wa familia
Na watoto mahitaji nawapa kama isemavyo biblia

Kipi bora?..

Nife museme nilikufa kiharakati?
Siogopi kufa… ila nnawaachaje waliobaki?

Je?..

Nani katiyenu mwanangu atampa malezi?
Wapi atapata mahitaji?
Wapi atapata mapenzi?
Mama naye?..
Wapi atapata mahitaj na malezi?
Na report ya upelelezi
Vipi akiteka mtekaji?

Je?…

Kaburi langu mtalipalilia majani?
Nimeumwa hamjakuja kuniona
Mnangoja mje msibani?
Nlipokuwepo skuwa nnajua hii saa nne hii saa nane
Nlichohitaji… nitoke mzima na ndugu zangu tuonane

Nimechapwa mijeledi
Nimevunjwa bila huruma
Ahsante mliopaza sauti
Nimeiona nguvu ya umma
Siku tatu nimefumbwa macho
Mikono nimefungwa nyuma....

NAKWENDAA ZIMBABWE ZIMAMA YELELE MAMA WEE X4

IMBA ROMA IMBAA...SEMA BABA WEEEE

Nasimama na nnaunga hoja kwenye uchumi wa viwanda
Nanasi linaoza msoga kibiti linaoza shamba
Walioniteka hawakuja na noah… ni uvumi na visanga
Ila KUTEKANATEKANA Ni uhuni wa kishamba…
Weka bunduki chini si tubishane kwa hoja
Maana sote lengo letu ni kuijenga Tanzania moja
Me skuona nyota kwa shoulder ila najua we ni soja

Inshaalah..

Ulikuja mwenyewe ama ulipewa order?

Ewalah..

Aminini siku hazigandi
We ni yanga me ni samba kuwa mpinzani sio dhambi
Ipo siku mtawala atakuwa mpinzani
Samba akichukua kombe sijui atapona nani?

Na kuna Mbunge alisema eti nimemtukana mkuu
Utahukumiwa na mkono wa Mungu… namshtakia aliye juu

Kwanza lini?
Na kwanini?
Me nimtukane mjomba?
Umepewa gari ya wagonjwa mimi Tanga nalililia bomba

Me mbarikiwa na nikifa kuume kwa baba ntaketi
Na mtu wa watu.. that’s why lilisimama bunge la
bajeti Kunijadili mtanzania kuwa MAKINI PIA MAKINIKIA
NAYATUNGIA MAPINI PIA

Me nlitabiri utakuwa rais kipindi unaitwa waziri
Japo maisha sio rahisi ila pongezi unastahili
Waliosadiki Roma ataonekana kabla ya Jumapili
God bless imetimia injili niliyoitabiri

NAKWENDAA ZIMBABWE ZIMAMA YELELE MAMA WEE X4

IMBA ROMA IMBAA
SEMA BABA WEEEE

Juma Nature Naye Amgeukia Gigy Money, Amtaka Afunge Mdomo na Asiongee Ongeee

$
0
0
Msanii Juma Nature amewakingia kifua wasanii wa kike wa zamani ambao Gigy Money amesema walikuwa hakuna cha maana wanachokiimba, na kumtaka atulie kwani bado ni mdogo kwenye tasnia.

Akizungumza na mwandishi wetu Juma Nature amesema kitu ambacho Gigy Money anatakiwa kufanya sasa hivi ni mazoezi ili aweze kuandika nyimbo, na sio kuongea hovyo kuponda watu wazima, kwani hajapitia mikiki kwenye maisha ya muziki.

"Hawezi kuwa na dharau wakati mtu mwenyewe hata albam saba hajafikisha, bado mdogo sana afanye mazoezi atunge nyimbo zenye hekima, anaweza akapata matuzo kibao, lakini asiongee ongee hovyo bado mdogo sana huyo mtoto, hajawahi kupata mikiki, aingie kwenye mikiki mikiki awaulize wenzake kina Zay B  watamfundisha wanawake wenzake, sisi wanaume kwetu ndiyo asiingie kabisa kwa sababu huku vitani", alisema Juma Nature.

“Bill Gate Ameamua Mwenyewe Kutuletea Hizi Fedha Sikumuomba…” – Rais Magufuli

$
0
0
Magufuli leo amekutana na kufanya mazungumzo na tajiri Namba 1 Duniani Bill Gates ambaye kupitia Taasisi yake ya Bill and Melinda Gates ametengea zaidi ya Dola Milioni 350 kuisaidia Tanzania.

”Tunamshukuru sana, ameamua mwenyewe kutuletea hizi fedha na anasema tunaenda vizuri. Kwa hiyo ameona hana mahala pa kuzipeleka hizi hela anazileta Tanzania kwa sababu tunajua kuzitumia.

“Hataki hela yake anaihangaikia kule halafu inakuja hapa inatumika ovyo. Tumemueleza hatua zetu na amekuwa akizisikia, anaziona hatua tunazochukua za kupambana na Ufisadi.” – Rais Magufuli. 

VIDEO:

Malinzi na Mwesigwa Hali si Shwari, Waendelea Kusota Jela.....

$
0
0
Kesi inayowakabili viongozi wa nafasi za juu katika Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi na Selestine Mwesigwa imehairishwa mpaka Agosti 24 mwaka huu ambapo watarudishwa tena Mahakamani kusomewa mashtaka yao.

Uamuzi huo umetolewa na Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisutu Jijini Dar es Salaam, Wilbard Mashauri, ambapo ndipo mashtaka hayo yalifunguliwa mara ya kwanza na kuendelea kusomewa mpaka sasa.

Hata hivyo, Wakili wa utetezi, Nehemiah Nkoko amedai kwamba inaonyesha vielelezo tayari vimeshafikishwa Mahakamani lakini upande wa mashtka unachelewesha kutolewa uamuzi.

Kwa upande mwingine, viongozi hao wanatuhumiwa na makosa mbalimbali  yakiwemo ya matumizi mabaya ya madaraka waliyokuwa nayo katika uongozi wao pamoja na kughushi na kutakatisha fedha kupitia akaunti ya TFF.

Wakuu wa Mikoa Minne Waanza Kutekeleza Agizo la Magufuli

$
0
0

Wakuu wa Mikoa Minne Waanza Kutekeleza Agizo la Magufuli

Tanga. Wakuu wa mikoa iliyopo Kanda ya Kaskazini wamejiwekea mkakati endelevu wa kukagua mafuta kwenye vituo vilivyopo maeneo yao ikiwa ni kufanyia kazi agizo la Rais John Magufuli aliyetaka mafuta yanayoingia nchini kupitia Bandari ya Tanga yauzwe kwa bei ya chini.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Ijumaa, Agosti 11 jijini hapa, Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martine Shigela alisema yeye na wenzake, Joel Bendera wa Manyara, Anna Mghwira wa Kilimanjaro na Mrisho Gambo wa Arusha wameweka mkakati wa pamoja wa kuendesha ukaguzi wa kila kituo chapetroli, dizeli na mafuta ya taa kujua kama yanauzwa kwa bei inayolingana na yalikotolewa.

“Hili la mafuta tayari mimi na mwezangu, Bendera, Mghwira na Gambo tumeshaanza kufanyia kazi tangu jana (Alhamisi) ukaguzi unaendeshwa na tutahakikisha tunapita vituoni kujiridhisha kama wauzaji wa mafuta

wanayauza kwa bei ya Tanga au ya kutoka Dar es Salaam,” alisema Shigela.

Akizungumza wakati akiweka jiwe la msingi la upanuzi wa maghala ya Kampuni ya GBP Jijini Tanga, Rais Magufuli aliwaagiza wakuu wa

mikoa ya Tanga, Kilimanjaro, Manyara na Arusha kufanya ukaguzi kwenye vituo vya mafuta kuhakikisha yanayotolewa Tanga yanauzwa kwa bei ya chini kuliko ya Dar es salaam.

Alisema ameamua kutoa agizo hilo ili uwekezaji uliofanywa na kampuni

ya GBP jijini Tanga wa maghala ya kupokea mafuta kutoka nchi za Uarabuni yaweze kuuzwa kwenye mikoa ya Kanda ya Kaskazini na hivyo kuondoa msongamano katika Bandari ya Dar es salaam.

Mbunge wa CCM Ashikiliwa na Polisi

$
0
0

Mbunge wa CCM Ashikiliwa  na Polisi
Singida. Jeshi la polisi mkoani Singida linamshikilia Mbunge Manyoni(CCM), Daniel Mtuka (51) kwa tuhuma ya kumgonga kwa gari mwanafunzi wa darasa la kwanza Shule ya Msingi Sukamahela, Salome Paschal (10) na kusababisha kifo chake papo hapo.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoani hapa, debora Magilingimba alisema tukio hilo limetokea jana katika Kijiji cha Sukamahela tarafa ya Kilimatinde Wilaya ya Manyoni.

Alisema siku ya tukio mbunge huyo akitokea Dodoma mjini akiwa njiani kurundi jimboni kwake akiendekesha gari lake aina ya Toyota Prado alimgonga mwanafunzi huyo aliyekuwa  akijaribu kuvuka kutoka upande wa kulia kwenda kushoto mwa barabara.

Kamanda huyo alisema kuwa uchunguzi wa awali umebaini kuwa chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva Mtuka, kushindwa kuchukua tahadhari kwa watumiaji wengine wa barabara.

“Mtuhumiwa mbunge Mtuka  anashikiliwa na jeshi la polisi kwa mahojiano na baada ya mahojiano, atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma inayomkabili. Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Manyoni kwa uchunguzi wa daktari na baada ya hapo, utakabidhiwa kwa ndugu kwa hatua za mazishi,”alisema.

Katika hatua nyingine, Kamanda Debora alisema watu wawili akiwemo Ofisa Elimu Sekondari Wilaya ya Ngara mkoani Kigoma, Alfred Kafuku  wamefariki dunia  papo hapo, baada gari walilokuwa wakisafiria kugonga lori aina ya DAF kwa nyuma.

Amewataja waliofariki kuwa ni  dereva wa gari raia wa Congo ambaye jina lake halikuweza kupatikana na wala kitambulisho chake.


Msichana Wangu Kanipa Kisonono, Nimuache au Niendelee Naye?

$
0
0
Nina msichana wangu nimedumu naye miezi miwili sasa.

Ni mzuri balaa na kwa muonekano wa nje anaonekana ni binti anayejisheshimu haswa, nilipata shida sana mpaka kumpata.

Lakini cha ajabu ndo amenipa kisonono. Nimepata hasira sana, natamani kumuacha lakini roho inasita, naona kama sitopata mzuri kama yeye.

Nifanyaje sasa wakuu?

Mnanisaidiaje kwa hili?

Rais Magufuli Awakosha Wafanyakazi wa Tanesco

$
0
0
Rais Magufuli Awakosha Wafanyakazi wa Tanesco
Chama cha Wafanyakazi wa Shirika la Umeme Tanesco (Tuico) wamepongeza Rais John Magufuli kwa uamuzi wake wa kutekeleza mradi wa umeme wa maji Rufiji.

Akizungumza leo Alhamisi,Mwenyekiti wa Tuico Tanesco, Athuman Hassan amesema mradi huo wa megawati 2000 utakuwa na manufaa kwa uchumi wa viwanda.

"Wafanyakazi tunamuunga mkono, tutamsaidia kwa kufanya kazi kwa weledi ili kuhakikisha tatizo la umeme Tanzania linakuwa historia,"amesema.

Amesema kukamilika kwa mradi huo wa Stieglers Gorge utamaliza tatizo la umeme na mwingine kuuzwa nje ya nchi.

Kuhusu vishoka, amesema watakuwa wakali kwa watu wanaojitambulisha kuwa ni wafanyakazi wa Tanesco wakati siyo.

"Tunaomba wananchi kutupa ushirikiano ili kuwatia nguvuni vishoka wanaowatapeli wateja wetu,"amesema.


Mke Wangu Anavaa Vikuku Miguu Yote Miwili je Nini Maana Yake?

$
0
0
Mke Wangu Anavaa Vikuku Miguu Yote Miwili je Nini Maana Yake?
Mimi ni kijana wa miaka 28 ninampenda mke wangu lakini kuna baadhi ya tabia zimekuwa changamoto kubwa kwangu ambazo zinapelekea baadhi ya ndugu zangu na marafiki zangu kutompenda mke wangu.

Mke wangu anapenda kuvaa vikuku wakati anatokana, huwa anapenda kuvaa miguu miwili, hili limekuwa tatizo kubwa kwangu kutokana na watu huwa wananipa maana mbaya ya mwanamke anayevaa vikuku viwili katika miguu yake.

Kila ninapomuuliza mke wangu uniambia anavaa kama urembo kama anavyovaa urembo mwingine, ndugu zangu nahitaji kujua maana yake na kama ina maana mbaya nifanye nini ili mke wangu aache kuvaa naomba ushauri wenu.
Mke Wangu Anavaa Vikuku Miguu Yote Miwili je Nini Maana Yake?

Faida na Hasara za Mwanamke Aliyezoea 'Kujichezea' au Kujichua

$
0
0
Kujichua  au kujichezea(kupiga puri au punyeto) sio kwa wanaume tu bali hata wanawake wanafanya hivyo ila wengi wao huwa hawako huru kulizungumzia au kukili kuwa wakizidiwa huwa wanajisaidia…….

Wakati mwingine mtu anashindwa kabisa kupata usingizi mpaka upige moja-mbili ndio usingizi unakuja au asubuhi unajisikia mzito kuamka kitandani mpaka upige moja ndio nguvu zinakuja…hasa kama umezoea dozi za maana lakini sasa mpenzi hayupo karibu.
Leo  nitaongelea  Hasara na faida za kujichua au kujichezea kwa  mwanamke.

HASARA ZA  MWANAMKE  ALIYEZOEA  KUJICHUA

Kujichua kwa mwanamke kiasili hakuna madhara yeyote, lakini kama unatumia au unajingizia vitu au vifaa Ukeni (Sanamu) zinaweza kukusababishia maaambukizo, "kutifua" misuli ya uke na kusababisha uke wako kulegea, nyama kujitokeza kwa nje.

Ukizoea kutumia Sanamu kujichua utashindwa kusikia utamu kila utakapofanya ngono na mwanaume kwa vile sanamu ni ngumu japokuwa watu watakudanganya kuwa ziko na texture kama uume asilia lakini sio kweli, Mungu aliumba uume kwa ajili ya kuingia ukeni na sio sanamu.

Mazoea hayo yatakufanya kihisia udhani kuwa mwanaume hana uwezo wa kukuridhisha kingono na hivyo kumuomba akufanye kwa kutumia sanamu badala ya uume wake kitu ambacho nitakiita "madhara ya kujichua kwa kutumia sanamu".

FAIDA  ZA  KUJICHUA:

1)Kuongezeka kwa hamu ya kufanya mapenzi kwa vile utakuwa unajua utamu wake.

2)Kujua "vipele vyako viliko".

3)Kutokuusaulisha mwili wako ikiwa uko nje ya uhusiano au umeamua kuwa single kwa muda.

4)Kuepuka mimba na maambukizo ya virusi vya UKIMWI na magonjwa mengine.

Maamuzi ni yako.Kumbuka kila kilicho na faida hakikosi hasara.

Jinsi Ya Kumsisimua Mwanamke Kabla Ya Kulala Naye

$
0
0
Wakati umemualika mwanamke sehemu unayoishi ama wakati umetoka deti katika bar, unapaswa kujua ya kuwa kumsisimua mwanamke huanza kabla ya nyinyi wawili kulala pamoja.

Unapaswa kumsisimua kuanzia nafasi ya kwanza ambayo utaipata kutoka kwake. Kufanya hivyo kutamfanya akutake hata zaidi na kumfanya ajiandae na mapema kabla hata kulala naye. Lakini ni mbinu gani inayoweza kutumika kumsisimua mwanamke kabla hamjalala pamoja?

Zama nami...

Kutumia maneno
Maneno yanaweza kumsisimua mwanamke asilimia mia. Mwanzo wanawake husisimuliwa na vitu wanavyosikia zaidi kuliko wanavyoona. Hii ndio tofauti kuu kati ya jinsi ya kumsisimua mwanaume na mwanamke. Hauhitaji kuonekana mchafu wakati ambapo unamsisimua mwanamke kwa kutumia maneno. Mwanzo anaweza kusisimulika na jinsi ambavyo anakusisimua wewe. Unaweza kumwambia maneno kama "Siwezi kungojea ile siku ambayo nitakuwa pekeangu na wewe", "Nimeanza kuingiwa na mawazo nikifikiria hio nguo uliyovaa inaficha nini" ama maneno mfanano na haya.

Lakini kando na kuwa maneno yanamsisimua mwanamke, kutategemea pia na vile ambavyo unamshika na miguso yako.

Kutumia miguso
Hapa ndipo utaleta utofauti wa yote. Miguso ni mbinu nzito na ya nguvu kama unaazimia kumfanya akutamani, kabla hata nguo za yeyote kuvuliwa, kabla ya nyinyi wawili kuanza kubusiana ama kufanya chochote. Baadhi ya mifano ya kufuata ya kumsisimua mwanamke kwa miguso ili aweze kukutamani kabla ya nyinyi wawili kulala pamoja ni kama ifuatayo: [Soma: Hatua za kumfanya mwanamke awe huru unapomgusa]

Kuzivuta nywele zake kiulaini: Usizivute nywele zake hadi ukazing'oa kichwani mwake. Lakini usiogope kuzishika baadhi ya nywele zake na kuzichezea kimvuto.

Miguso ya kukawia: Wakati ambapo unamgusa kikawaida - kwa mfano, wakati mikono yako iko katika mabega yake, mgongo au mkono - usiogope kuuzuia mkono wako ukawie sehemu hizo kwa dakika moja.

Karibu kumla dende: Hii ni siri kubwa ambayo inahakikisha gemu yako kuwa ya juu. Usikimbilie kumbusu. Jiweke katika hali ambayo nyinyi wawili mko "karibu" kubusiana. Hii itamfanya aingiwe na wazimu wa kutaka kuibusu midomo yako haraka kuliko ulivyokuwa ukitarajia.

Kumkwaruza kiulaini: Unapomgusa, usiogope kuzipitisha kucha zako kwa mgongo wake, nyuma ya shingo yake na sehemu mfanano na hizi. Hii unaweza kuitumia wakati ambapo mshajenga uhusiano wa ndani kati yenu.

Mtizamo wa macho: Kumuangalia mwanamke kwa macho pekee kunaweza kumfanya apandwe na mzuka. Mwangalie machoni, zaidi kuliko yeye. Kufanya hivyo kunaashiria ujiaminifu. Ijapokuwa mbinu hii haitumii miguso, inaweza kufanya kazi sawa na kama vile matumizi ya miguso kabla nyinyi wawili kulala pamoja.

Ok hizi ni baadhi ya mbinu za kumfanya mwanamke asisimke kabla kulala na yeye. Unaweza hata pia kuamua kumpandisha nye...ge bila kutumia miguso yeyote.

Kulala Chali ni Hatari Kwa Mama Mjamzito....Chukua Tahadhari

$
0
0
Wanawake wajawazito wanaopenda kulala chali  wapo kwenye hatari  ya kuzaa mtoto mfu(stillbirth),kulingana na wanasayansi.

Katika utafiti  uliofanyika nchini Ghana, wanawake wajawazito ambao walipenda kulala chali wakati wa ujauzito  walikuwa  kwenye hatari mara tano zaidi ya kuzaa watoto wenye uzito mdogo na  kwa wanawake wengine walizaa watoto wafu.
Utafiti huu ulifanyika nchini Ghana kutokana na kuwa kati ya watoto 1000 wanaozaliwa 20 hadi 50 kati yao huwa ni watoto wafu.

Hata hivyo, utafiti mpya uliofanyika nchini New Zealand pia umehusisha kulala chali kwa mwanamke mjamzito na idadi kubwa ya  watoto wafu wanaozaliwa  katika nchi zenye raia wenye kipato kikubwa.

Mkuu wa utafiti huu,Louise O’Brien  kutoka chuo kikuu cha Michigan, nchini Marekani amesema kama kutokulala chali wakati wa ujauzito hupunguza uwezekano wa kuzaa mtoto mfu basi ni vizuri kuhamasisha kina mama wajawazito kutolala chali kwani hii ni njia rahisi na isiyokuwa na gharama yoyote ile.

Tabia hii ya kulala chali wakati wa ujauzito inaweza kuepukika kwa kuwashauri  kina mama wajawazito madhara yanayopatikana kwa kulala chali.

Matokeo ya utafiti huu yanaonyesha ya kwamba zaidi ya robo ya idadi ya watoto wanaozaliwa wafu inaweza kuepukika kwa kubadilisha staili ya kulala tu kwa wanawake wajawazito.
Mtoto Aliyelala

Siku zote madaktari wanashauri kina mama wajawazito kulala ubavu mmoja hasa upande wa kushoto ili kuepuka kuzaa mtoto mfu au mtoto mwenye uzito mdogo kwa sababu mwanamke mjazito anapolalia ubavu wake wa kushoto huongeza mzunguko wa damu kwa kiumbe kilichomo ndani yake.
Utafiti huu uliofanyika nchini Ghana unaunga mkono utafiti uliofanyika hivi karibuni nchini Australia unaojulikana kama Sydney Stillbirth Study ambao ulisema ya kwamba wanawake wanaolala chali wakati wa ujauzito wako kwenye hatari ya mara sita zaidi ya kuzaa watoto wafu.
Utafiti huu wa Australia ulifanyika kwa miaka mitano na ulihusisha wanawake wajawazito 295 kutoka katika hospitali nane nchini Australia. Naye mtafiti mkuu katika utafiti huu Dr. Adrienne Gordon, kutoka Sydney’s Royal Prince Alfred Hospital amesema “Tafiti za awali zilionyesha ya kwamba wanawake wanaolala chali wakati wa ujauzito, hupunguza mzunguko wa damu unaotakiwa kwenda kwa mtoto.Lakini  pia ni vizuri kwa wanawake ambao ni wajawazito  kutotaharuki kama wakati mwingine watalala chali.’’

Kutokana na idadi ndogo ya wanawake wajawazito waliohusishwa kwenye utafiti huu sisi wana Tanzmed tunachelea kusema ya kwamba ni vigumu kusema utafiti huu umetoa mapendekezo sahihi ya  namna ya kulala kwa wanawake wajawazito.Pia kutokana na kutoangalia muda ambao wanawake hao walilala wakiwa chali (mfano kama walilala masaa 4,6 au 8 kwa siku na kwa siku ngapi) na tofauti ya hatari kati ya wanawake wajawazito waliolala muda mfupi na mrefu, hivyo tunawaambia wanawake wajawazito kutohofu kama watalala chali lakini ni bora kuchukua tahadhari mapema.Tafiti hii inatoa changamoto kwa watafiti wetu wa afya kuangalia jinsi ya kufanya tafiti kama hizi katika mazingira ya kwetu.
Viewing all 104809 articles
Browse latest View live


Latest Images