Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104803 articles
Browse latest View live

Chadema Wampongeza Kenyata

$
0
0
Chadema Wampongeza Kenyata
Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia kwa Mwenyekiti wake Freeman Mbowe na Mjumbe wa Kamati Kuu Edward Lowassa wametoa pongezi kwa Rais Mteule wa Kenya Uhuru Kenyatta kwa kuchaguliwa tena kuongoza nchi ya Kenya kwa awamu ya pili.

Mbowe amewapongeza wananchi wa Kenya kwa kuweza kufanya uchaguzi wa uwazi na haki
"Kwa niaba ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), na wapenda Demokrasia wa Tanzania, natoa pongezi kwa chama cha Jubilee na Uhuru Kenyatta kwa kuchaguliwa tena kuiongoza nchi ya Kenya.Lakini pia nawapongeza zaidi wananchi wa Kenya kwa uchaguzi wa uwazi na haki, Mungu ibariki Jumuiya ya Afrika Mashariki' alisema Mbowe
Aidha Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA Mhe, Edward Lowassa pia amempa neno Rais Mteule wa Kenya na kusema kuwa ushindi huo wa pili wa Uhuru Kenyatta ni kwamba wananchi wa Kenya wamezungumza kupitia kura kuwa wana imani na uongozi wake na maono yake katika nchi hiyo.

Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kilikuwa kinamuunga mkono Rais Uhuru Kenyatta katika kampeni mbalimbali na kiliweka wazi uhusiano huo kwa kile kilichodai kuwa Uhuru Kenyatta ni mtu ambaye anasimamia Demokrasia.



Yanga Kumchezesha Kipa wa Serengeti Boys Leo kwa Majaribio

$
0
0

Yanga Kumchezesha Kipa wa Serengeti Boys Leo kwa Majaribio
Kuna uwezekano mkubwa kwa kipa chipukizi wa Yanga, Ramadhan Kabwili, leo Jumamosi kwa mara ya kwanza akakaa langoni kuichezea timu yake hiyo dhidi ya Ruvu Shooting katika mchezo wa kirafiki kwenye Uwanja wa Azam Complex, uliopo Chamazi jijini Dar es Salaam.

Uwezekano wa Kabwili aliyejiunga na Yanga hivi karibuni akiwa kipa namba moja wa timu ya taifa ya vijana ya Tanzania chini ya miaka 17, Serengeti Boys, kucheza mechi hiyo umekuja kutokana na wenzake kuwa majeruhi.

Makipa Rostand Youthe na Beno Kakolanya wanaopokezana langoni, wote hawakufanya mazoezi ya Yanga juzi na jana Ijumaa kutokana na kuwa majeruhi, hivyo Kabwili ana nafasi kubwa ya kucheza leo. Daktari wa Yanga, Edward Bavu, ameliambia Championi Jumamosi kuwa:

“Makipa wetu wawili Rostand na Kakolanya bado ni wagonjwa lakini wanaendelea vizuri, hivyo katika mechi ya kesho (leo) tunaweza kumtumia Kabwili. “Matarajio yetu ni kwamba Rostand atakuwa fiti hivi karibuni na ataungana na wenzake haraka iwezekanavyo baada ya kuumia mgongo, wakati Kakolanya yeye akiendelea na matibabu ya goti.”

Gari La Kubeba Maiti Zisizo na Ndugu Lanunuliwa Dar

$
0
0
Gari La Kubeba Maiti Zisizo na Ndugu Lanunuliwa Dar
Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam, imenunua gari la kisasa la kubebea miili ya marehemu waliokosa ndugu na kupeleka katika makaburi kwa ajili ya maziko.

Akizundua gari hilo jana meya wa jiji hilo, Isaya Mwita aliwaambia wanahabari kuwa gari hilo aina ya Isuzu lina thamani ya  Sh 100 milioni.

Mwita ambaye pia ni diwani wa Vijibweni amesema  gari hilo lina uwezo wa kubeba miili minane hadi 16 kwa wakati mmoja.

“Ndani ya gari hili kuna hili mafriji manne na fedha za kununua gari hili zimetokana na mapato ya ndani ya jiji,” alisema Mwita.

“Tumejaribu kuangalia mbadala wa kuhifadhi ndugu zetu wale ambao hawana ndugu, kuna watu wanakutwa katika hospitali zetu hawana ndugu hivyo tumeamua kuleta gari ambalo litasitiri miili yao.

Alisema gari litatumika kwa wakazi wote wa Dar es Salaam na kwamba  gari litakuwa na faida kubwa kwa wananchi wa jiji hilo ambapo awali miili yao ilikuwa ikibebwa na malori.


Rais Magufuli Amteua Bernard Konga kuwa Mkurugenzi Mkuu (NHIF)

$
0
0




Rais Magufuli Amteua Bernard Konga kuwa Mkurugenzi Mkuu (NHIF)

 Rais John Magufuli amemteua, Bernard Konga kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF).

Taarifa iliyotolewa leo Jumamosi na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi wa Konga umeanza Agosti 9, 2017.

Kabla ya uteuzi huo Konga alikuwa akikaimu nafasi hiyo.




Bill Gates Ajiunga Istagram Akiwa Tanzania na Kuweka Picha akiwa Anakula Chakula na Wanafunzi wa Shule ya Msingi Tanga

$
0
0
Bill Gates Ajiunga Istagram Akiwa Tanzania  na Kuweka Picha akiwa Anakula Chakula na Wanafunzi wa  Shule ya Msingi Tanga
Jarida la Fobers limeripoti kuwa tajiri namba moja duniani Bill Gates amejiunga Instagram akiwa nchini Tanzania na kurusha picha tatu ikiwemo aliyopiga na watoto akiwa Muheza mkoani Tanga.

Gates ameijunga na mtandao huo wa kijamiii kwa jina la thisisbillgates na kurusha picha zake za kwanza tatu zote akiwa Tanzania.

Gates katika mtandao huo aliandika hiki, “Hello kutoka Tanzania, Instagram! Nimepata chakula cha mchana kizuri nikiwa na watoto wanaovutia katika Shule ya Msingi Kicheba Muheza na nikakutana na Upendo Mwingira ambaye amejikita katika kupambana na magonjwa yasiyopewa kipaumbele. Melinda na mimi tumekuwa tukija Tanzania kwa miaka mingi sasa. Huwa napenda kuona maendeleo nchi iliyoyafanya katika kuboresha afya na kutoa nafasi.”

Kwa Kiingereza aliandika hivi “Hello from Tanzania, Instagram! I just had a great lunch with some amazing kids at Kicheba Primary School in Muheza and met Upendo Mwingira, a remarkable physician who has dedicated her career to fighting neglected tropical diseases. Melinda and I have been coming to Tanzania for many years now. I always love seeing how much progress the country has made to improve health and provide opportunity. Plus, the scenery is stunning. Whenever I travel to places like this, I wish others could come along and meet the people I get to meet. I have no doubt it would leave them as optimistic as I am about progress happening around the world. I’ll be sharing photos from my adventures here on Instagram, and I hope you’ll follow along.”

China Yampa Onyo Trump Juu ya Matamshi Yake

$
0
0

China Yampa Onyo Trump Juu ya Matamshi Yake
Sambaza habari hii Facebook  Sambaza habari hii Twitter  Sambaza habari hii Messenger  Sambaza habari hii Email  Mshirikishe mwenzako.


Rais wa China Xijinping amemtaka rais Donald Trump kuchunga mtamshi na vitendo vinavyozidisha hali ya kuzua wasiwasi ,chombo cha habari cha kiserikali kimeripoti.
Rais Trump na Korea Kaskazini wamekuwa wakirushiana cheche za maneno huku rais rais huyo wa Marekani akionya kuikabili kivita vikali Korea Kaskazini.
Lakini China ambaye ni mshirika mkuu wa Korea Kaskazini ametaka pande zote mbili kuwa na uvumilivu.

Rais Kim Jong-un na mwenzake wa Marekani Donald Trump wamekuwa wakirushiana cheche za vitisho


Rais Kim Jong-un na mwenzake wa Marekani Donald Trump wamekuwa wakirushiana cheche za vitisho
Taarifa ya ikulu ya Whitehouse imesema kuwa Marekani na China zilikubaliana kwamba Korea Kaskazini inafaa kusitisha uchokozi na tabia mbaya.

Hofu kubwa inayoendelea kutanda kuhusu mpango wa kinyuklia wa Korea Kaskazini ilizidi baada ya taifa hilo kufanyia majaribio makombora yake ya masafa marefu mnamo mwezi Julai.
Mshirikishe mwenzako Unavyoweza kumshirikisha mwenzako

"Anayetegemea Kupata Nafasi ya Uongozi TFF Ili jipatia Fedha Amepotea Njia"- Mwakyembe.

$
0
0

"Anayetegemea Kupata Nafasi ya Uongozi TFF Ili Ajipatia Fedha Amepotea Njia"- Mwakyembe.

Mwakyembe amesema ili kuweza kupiga hatua mbele katika soka la Tanzania wajumbe wanapaswa kutumia vizuri nafasi zao kuchagua viongozi wenye maono, wazalendo na wasioteteleka kwa ushawishi wa muda mfupi.

"Ndugu wajumbe viongozi bora huibuliwa na wajumbe makini wanaoongozwa na dhamira njema na uzalendo usioteteleka kwa vishawishi vya mpito, serikali inaamini tuna wajumbe makini huku ndani wasioyumbishwa na vishawishi vya muda na vishawishi vya mpito, tunataka viongozi wanaongozwa na uzalendo wa hali ya juu, hivyo tunataka viongozi bora wa TFF wenye hali, moyo, uelewa, weledi na uadilifu unaotakiwa kupeleka soka letu mbele" alisema Mwakyembe

Aidha Waziri Mwakyembe alisisitiza kuwa yoyote ambaye anaona amegombea nafasi yoyote ndani ya TFF kwa lengo la kujipatia fedha au kutajirika basi anapaswa kutambua kuwa amepotea njia.
Msikilize hapa Mwakyembe akifunguka zaidi.

Mwakyembe amesema rais na wajumbe watakaopatikana leo wataapishwa mbele ya wapiga kura wote wa uchaguzi tofauti na miaka ya nyuma ambapo walikuwa wakishahau haki ya waliowachagua kwa kuwaapisha nje ya utaratibu.

Manara - Mkutano Mkuu wa Simba Upo Pale Pale

$
0
0




Manara -  Mkutano  Mkuu wa Simba  Upo Pale Pale
Simba SC imewatangazia wanachama wake na wadau wa soka nchini kuwa Mkutano wao Mkuu bado upo pale pale na hivyo kuwaomba kuhudhuria siku ya Jumapili ya Agosti 13 katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere uliopo Posta Jijini Dar es salaam

Hayo yameelezwa na Mkuu wa kitengo cha Habari na Mawasiliano cha klabu hiyo, Haji Manara.

Klabu ya Simba inawatangazia Wanachama wake na wadau wa mchezo wa kandanda kote nchini kuwa Mkutano wake mkuu wa kawaida wa kila mwaka upo pale pale.

Hatua hiyo inafuatia na Hukumu iliyosomwa jana katika Mahakama ya kisutu, kufuatia zuio la kuzuia Mkutano huo, liliowekwa na mmoja wa wadhamini wa klabu Mzee Hamis kilomoni.

Kwenye hukumu hiyo,mahakama hiyo ilitupilia mbali shauri hilo. Mkutano huo utafanyika siku ya Jumapili tarehe 13-8-2017, kuanzia saa Nne kamili asubuhi, ukitanguliwa kwa Wanachama wa klabu kujiandikisha kuanzia saa mbili kamili asubuhi.

Klabu imeamua kufanyia mkutano huo kwenye Ukumbi wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere (Mwalimu Nyarere international Conference Centre). Ukumbi huo wa kisasa kabisa nchini upo maeneo ya Ocean Road, jirani na Chuo cha Usimamizi wa fedha(IFM), Na itakuwa mara ya kwanza kwa vilabu vya michezo nchini kufanyia mkutano wake kwenye kituo hicho kilichobeba jina la Baba wa Taifa hili.

Uongozi wa Simba unawaomba wanachama wake kuhudhuria kwa wingi kwenye mkutano huo muhimu,huku mahitaji yote muhimu yakipatikana siku hiyo ikiwemo Vinywaji baridi na Chakula cha mchana.

*Mwisho* klabu inawaomba tena Wanachama wake wenye hoja tofauti waje kuzitoa ndani ya Mkutano huo kama inavyoagiza katiba ya klabu. Hakika huu ni ushindi mkubwa sio tu kwa klabu, bali kwa Mustakbali mzima wa maendeleo ya mchezo huu murua zaid nchini na kote Ulimwenguni.

Nuh Mziwanda Afunguka Aliyekuwa Mkewe Nawal Kuolewa Bila Kumpa Talaka

$
0
0




Nuh Mziwanda Afunguka Aliyekuwa Mkewe Nawal Kuolewa Bila Kumpa Talaka
Msanii wa muziki, Nuh Mziwanda amedai Baby Mama wake, Nawal alishinikizwa kuolewa na wazazi wake kabla hata ajampatia talaka.

Muimbaji huyo amedai ingawa tayari aliyekuwa mke wake huyo ameshaolewa mtu mwingine lakini bado hajampatia talaka ya kusema kwamba wameachana.

“Mimi sijaachana na Nawal, mpaka sasa mimi sijatoa talaka kusema mimi wewe sikutaki endelea na maisha yako.,” Nuh aliimbia Times Fm. “Lakini kulikuwa na msuguano wa hapa na pale ambao naamini haukuwa unatokana na mimi na yeye, ulitokana na familia yake. Kwahiyo haikuwa kwamba mimi simtaki Nawal yeye hanitaki mimi ila familia yake ndio iliyosimamia huu mchongo,”

Nuh alisema ingawa hajamuacha Nawal lakini sio mke wake tena kwa sababu tayari ameshaolewa na mwanaume mwingine.

Wawili hao walifanikiwa kupata mtoto mmoja wa kike aitwaye, ‘Anyaghile’.


Morocco Yaomba Kuandaa Kombe la Dunia 2026

$
0
0


Morocco Yaomba Kuandaa Kombe la Dunia 2026
Shirikisho la soka nchini Morocco limetangaza kuwa litawasilisha ombi la kuandaa kombe la dunia 2026.

Shirikisho la soka nchini Morocco limetangaza kuwa linasema uwa litawasilisha ombi la kuandaa kombe la dunia 2026.

Shirikisho la soka nchini Morocco limetangaza kuwa linasema uwa litawasilisha ombi la kuandaa kombe la dunia 2026.
Fifa tayari imethibitiha kuwa ilipata ombi hilo la kuandaa mchuano huo kutoka taifa hilo la Afrika kufikia siku ya ijumaa.

Marekani, Canada na Mexico tayari zilikuwa zimetangaza mnamo mwezi Aprili kwamba zinataka kuandaa dimba hilo ka ushirikiano.
Kombe la dunia liliwakuandaliwa na Afrika Kusini 2010 na hii itakuwa mara ya tano kwa Morocco kuwasilisha ombi.

Shirikisho la soka barani Africa Caf iliunga mkono ombi hilo la Morocco mnamo mwezi Julai.
Jumla ya timu 48 badala ya 32 zitashiriki katika kinyanganyoro kilichopanuliwa na kuongezwa idadi ya timu 2026 baada ya mabadiliko kutangazwa mwaka huu.

Uamuzi kuhusu ni nani anayefaa kuandaa dimba hilo utafanywa 2020.
Sera ya Fifa ya kuandaa dimba hilo kwa zamu inamaamisha kwamba Afrika ni mojawapo ya mashirikisho ambayo yanaweza kuandaa fainali za 2026 kwa kuwa Ulaya itaanda mwaka 2018 kupitia Urusi na Asia ikiandaa 2022 kupitia Qatar.

Imefichuka...Mama yake Diamond Platnumz na Esma Wanaswa Walipomtembelea Hamissa Mobetto Hospitalini Kumuona Mtoto

$
0
0
Baada ya mda mrefu kuibuka maneno ya chini chini kuwa Mtoto aliyejifungua Hamissa mobeto ni wa Diamond Platnumz huku Mama Diamond na Diamond mwenyewe wakishindwa kukana tuhuma hizo

Siku ya jana Ijumaa kamera za shilawadu ziliwanasa live hospitalini Mama Diamond,Mama Rommy na Esmaplatnumz hospitalini wakitoka kumjulia hali Hamissa Mobeto

 TAZAMA VIDEO YA KUNYAPIA NYAPIA

Mrembo Lulu Diva Adai Wizkid Hakufanikiwa Kupata Penzi Lake....Aliambulia Patupu

$
0
0
Msanii wa Bongo Flava, Lulu Diva amekanusha tetesi za kuwahi kutoka kimapenzi na msanii Wizkid kutoka nchini Nigeria.

Hitmaker huyo wa Usimwache na Utamu ambaye kwa sasa ameachia ngoma mpya ‘Give It To Me’, ameiambia Clouds Fm kuwa yeye kukutana na Wizkid ilikuwa ni mipango ya kazi na si vinginevyo.

“Alikuwa na special appearance na mimi nilikuwepo siku hiyo na tulipanga mimi na meneja wangu kwa sababu kuna mtu alikuwa anajuana naye alimuita Wizkid pale, kwa hiyo waliongea kuwa tunaenda kukutana kama wasanii na tuliongea kuhusu muziki, so we have fan pale na ikaishia hapo hakukua na kitu kingine,” amesema na kuongeza.

“After party hakuna niliwahi kuondoka tuliongea kuhusu muziki tu…, yeah tutarajie kitu kwa sababu yeye ni msanii na mimi ni msanii hivyo tunaweza tukafanya kitu kizuri zaidi,” amesisitiza.

Mkuu wa Mkoa wa Kilombero piga Marufuku Wananchi Wa Mkoa Huo Kufanya Sherehe

$
0
0

Mkuu wa Mkoa wa Kilombero piga Marufuku Wananchi Wa Mkoa Huo Kufanya Sherehe
Mkuu wa wilaya ya Kilombero James Ihunyo amepiga marufuku mtu yeyote kufanya sherehe bila kibali kutoka kwa mtendaji wa eneo husika ikiwa ni pamoja na kuuza chakula kiholela kama njia ya kuthibiti utumiaji hovyo wa chakula.

Ihunyo amesema ameamua kupiga marufuku hiyo ili kuthibiti utumiaji hovyo wa chakula kilichopatikana msimu huu wa mavuno na kujikinga na baa la njaa katika wilaya yake.

Mkuu wa wilaya hiyo ya Kilombero akiongea leo kwenye kikao cha baraza la madiwani la mji wa Ifakara Ihunyo amesema serikali yake ya wilaya imejipanga kuhakikisha sherehe zisizo za lazima hazifanyiki na kuwataka Watendaji na Madiwani kushirikiana kukemea vitendo hivyo.

Mbali na hilo Diwani wa Kata ya Viwanja Stini amelalamika ucheleweshaji wa fedha kutoka serikali kuu na kudai jambo hilo linakuwa linakwamisha mipango ya maendeleo katika halmshauri hiyo na kata zake.

Awali kabla ya kikao hicho kuanza Mbunge viti maalum mkoa wa Morogoro kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) mchungaji Getruda Lwakatare aliapishwa kuwa mjumbe kamili wa baraza hilo la madiwani.


Serikali Yasitisha Utoaji wa Maeneo Mapya ya Utawala

$
0
0

Serikali Yasitisha Utoaji wa  Maeneo Mapya ya  Utawala
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali imesitisha zoezi la kutoa maeneo mapya ya utawala hadi itakapotangazwa vinginevyo.

“Kwa sasa tumesitisha kutoa maeneo mapya ya utawala ili tuimarishe kwanza yale ya awali. Tunaimarisha kwanza miundombinu ya majengo ya ofisi,  nyumba za watumishi kwenye wilaya na Halmashauri mpya, zikitengamaa tutafanya maamuzi mapya, ” alisema.

Waziri Mkuu alitoa kauli hiyo jana (Ijumaa,  Agosti 11, 2017) katika mikutano ya hadhara iliyofanyika Ulyankulu na Kaliua, wilayani Kaliua mkoani Tabora.

Alikuwa akijibu maombi ya wabunge wa majimbo ya Ulyankulu na Kaliua ambao walisema kuna haja ya kuigawa wilaya ya Kaliua ili kusogeza huduma kwa wananchi waishio kwenye kata zilizo mbali na tarafa.

Akizungumzia kuhusu migogoro baina ya wanavijiji na maeneo ya hifadhi, Waziri Mkuu alisema Serikali bado inafanya uhakiki wa mipaka katika maeneo ya hifadhi na ikikamilisha zoezi hilo itatoa taarifa.

Ili kuharakisha zoezi hilo,  Waziri Mkuu amewataka wananchi wanaoishi pembezoni mwa vijiji vinavyopakana na maeneo ya hifadhi, wasifanye upanuzi wowote hadi zoezi la kuhakiki mipaka ya hifadhi litakapokamilika.

“Tumeamua kuweka beacons katika maeneo yote ya hifadhi ili kubaini mipaka imepita wapi.  Wananchi mkiwaona watu wa hifadhi wanapita huko msigombane nao. Ni hatua ya awali ya kubaini maeneo ya mipaka. “

“Niwasihi wanavijiji wote, vijiji vilivyomo kwenye hifadhi visiendelee kupanua maeneo yake. Mbaki hivyo hivyo hadi Serikali itakapoamua vinginevyo, ” alisema.

Alisema zoezi la uhakiki wa mipaka ya hifadhi likikamilika na taarifa kutolewa, Serikali itatoa uamuzi juu ya vijiji vilivyobainika kuwa ndani ya maeneo ya Hifadhi.

Akiwa Kaliua, Waziri Mkuu alielezwa na Mbunge wa jimbo hilo,  Mheshimiwa Magdalena Sakaya kuwa wananchi wanashindwa kujenga makazi ya kudumu katika maeneo waliyopo kwa sababu wanatishiwa kwamba wapo hifadhini.

Waziri Mkuu alisema Serikali inafanya mapitio na ikilazimu itabidi ifanye marekebisho ya Sheria inayohusu Misitu ya Hifadhi pamoja na Sheria inayohusu masula ya Wakimbizi. 

Gigy Money asema Wanawake Wanapenda Pesa

$
0
0

Gigy Money asema Wanawake Wanapenda Pesa
Msanii wa muziki wa bongo fleva Giggy Money amefunguka na kusema kuwa hakuna mwanamke anapenda mwanaume bali wanawake wanapenda pesa tu hivyo amedai yeye sasa hajali kumfurahisha mwanaume kwa umbo lake ila anachoangalia yeye anapiga pesa.

Mbali na hilo Giggy Money anadai kuwa ndoto zake za kuja kutoka kimapenzi na msanii Wizkid kutoka Nigeria bado ziko pale pale na kusema siku zikitimia atawathibitishia watu kuwa jambo hilo limetimia.

Ice Boy Akana Kutoka na Mpenzi wa Darasa

$
0
0





Ice Boy Akana Kutoka na Mpenzi wa Darasa
Msanii Ice Boy ameeleza kushangazwa na taarifa za yeye kutoka kimapenzi na mrembo ambaye anatajwa kuwa ni mpenzi wa rapper Darassa.

Ice Boy amesema huyo mrembo ni rafiki yake na wanafanya wote biashara na kila mmoja ana shughuli zake na vitu vingine kuhusu wao ni vya ndani zaidi ila kilichoibua hilo ni baada ya kuweka picha kwenye mtandao wakiwa pamoja.

“Kwa sababu tu nilimposti watu kibao wakachanganya mambo, sasa dili nini?, kwa sababu ni demu wa Darassa. Sio mvutano, sidhani kama ni mvutano kwa sababu mimi sijawahi kuonana naye au kupata comment kutoa kwake hata sijawahi kujua kwamba ni demu wake,” ameiambia E-Newz ya EATV na kuongeza.

“Halafu you never know unaweza kukuta Darassa ameshawahi kudate na mademu kibao ambao wanadate na wana tu halafu yeye mwenye hana hata mchongo nao kwa sababu mademu siwapo tu mshikaji wangu,” amesema Ice Boy.

Graca Machel Ataka Wanawake Wawe Chachu ya Mabadiliko Afrika

$
0
0
Graca Machel Ataka Wanawake Wawe Chachu ya Mabadiliko Afrika
Mwenyekiti wa mfuko wa Graca Machel, Graca Machel amewataka wanawake kuwa chachu ya mabadiliko katika nchi za Afrika.

Akizungumza leo Jumamosi wakati wa kufunga mkutano wa siku nne wa kuwaendeleza wanawake kiuchumi na kijamii, Machel alisema wanawake wengi wamekuwa wakifanya shughuli zao nyuma ya pazia na kutegemea msaada wa wengine.

Alisema walio wengi wanaweza kujisimamia wenyewe kutokana na kufanya vitu vingi, lakini wanaogopa kufanya hivyo kwa kusikiliza nafsi inayowakatisha tamaa.

" Mnaweza, kuweni sehemu na chachu ya mafanikio, fikirieni vitu vikubwa, kuweni mabalozi wa wasiolisikia hili" alisema Machel.

Kwa upande wake Evelyne Warioba ambaye ni mke wa waziri mkuu mstaafu Joseph Warioba alisema mbali na kujenga uhusiano, kukutana na wanawake wengi wa Afrika, alichojifunza na anachokwenda kufanya ni kuhakikisha wanawake wanafikiwa popote pale walipo.

Alisema hatua ya kwanza kabla ya kupiga mwendo ni kuhakikisha wanawake wanashikana mkono na kwenda pamoja.

" Tuwafikie, tuwaeleze, wajue kuwa wao ni sehemu ya maendeleo ya nchi na Afrika kwa ujumla," alisema Warioba.

Zijue Njia Rahisi za Kujua Kama we Mwanaume Una Nguvu za Kiume au Unachafua tu Wenzako Sita Kwa Sita

$
0
0

  1. Kama ukiwa umekaa mahala popote halafu akapita Mwanamke mwenye Inye Ndembendembe ( Matako / Makalio ) makubwa halafu ukimwangalia tu huyo Mwanamke Uume / Mkuyenge wako haushtuki na haudindi / hausimami jua imeshakula Kwako na sasa Wewe ni Joka la Kibisa tu.
  2. Kama ukiona umeingia tu ama Gesti / Loji au Chumbani kumbandua / kufanya Mapenzi na mwenza wako halafu hadi unavua nguo na unalala Kitandani kuanza Shughuli bado tu hujadindisha / hujasimamisha basi jua ya kwamba tayari imeshakula Kwako andika tu maumivu.
  3. Ukiona umemaliza tu mshindo wa Bao / Kupizi / Kupiga Bao halafu huyo Mwanamke unayembandua hajakukumbatia tena kwa Kukukaba kama wale Vibaka wa Mchikichini Ilala nyuma ya Kiwanda cha Bia TBL basi jua tu kwamba imeshakula Kwako na anza tu Kuungama kwa Mungu wako.
  4. Ukiona tokea umeamka asubuhi hadi usiku unaenda Kulala mnara haujasimama hata mara moja tu kivyake basi jua ya kwamba tayari imeshakula Kwako na jiandae tu Kuchapiwa na wenye nguvu zao.
  5. Kama ukiona Mwanamke / Mpenzi wako uliyenae Kwako ndiyo mwenye Sauti, Amri na ndiyo mpangaji wa kila kitu hapo huku Wewe ukiwa ni Msikilizaji tu na Kukubali jua una tatizo kubwa sana na lililotukuka mno la upungufu wa nguvu za Kiume ( mgongesha Besela ) kwani kwa Saikolojia ya Wanawake pindi akishajua Mwanaume aliyenae ni Kamilifu Kinguvu za Kiume huwa wanawaheshimu na kuwaogopa sana.

Ni hayo wadau hivyo naomba kila Mwanaume mwenzangu hapo ulipo hebu anza Kujitathmini mwenyewe na kisirisiri kutokana na hizo dalili saba ( 5 ) za hapo juu kisha mniletee mrejesho ila nimeamua tu kuwapeni hizo dalili za awali ili niwasaidieni tu msipoteze Pesa zenu kuzunguka Mahospitalini au kwa Waganga wa Kienyeji kutafuta Kiini cha tatizo hilo ambalo kwa sasa limekuwa ndiyo Kero namba moko / moja kwa Wanaume wengi nchini Tanzania.

Kila la kheri.

Nawasilisha

BY GENTAMYCINE

Maskini Sumaye Afunguka Haya 'Sirudi CCM Pamoja Kuwa Natateseka Kwa Visasi na Kunyang'anywa Mashamba yangu yote'

$
0
0
"Mmeamkaje? Kwangu mambo siyo mazuri. Mtakumbuka baada tu ya kuingia upinzani serikali ilitishia muda mrefu kuchukua mashamba yangu bila sababu za msingi, hata wakati wa kampeni baadhi ya viongoz wa ccm walitamka hadharani kuwa huyu dawa yake ni kumnyang'anya mashamba yake. Shamba la mabwepande ekari 33 wameagiza wiki hii halmashauri iligawe kwa wavamizi na wengineo.

Jana nimepokea barua kuwa shamba la mvomero ekari 326 limetwaliwa na rais na sitakiwa kukanyaga hapo. Shamba hilo lina majengo, mazao, mashine mbali mbali, visima virefu vya maji, umeme na mifugo mchanganyiko zaidi ya 200. Kisingizio shamba halijaendelezwa! Shamba lenye vitu vyote hivyo halijaendelezwa??

Mbaya zaidi katika kupinga dhamira hizo nilifungua kesi mahakama kuu kwa mashamba yote na mahakama zimeweka zuio la kutokuingiliwa mashamba hayo mpk mashauri ya msingi yatakapoamuliwa.

Lakini wameshaamua kwa hiyo mahakama hazina kazi. Utawala huu haufuati sheria ni udikteta mtupu! Kuna mwana ccm moja alisema "tutamfilisi mpk atakapotembelea ndala ndo atakumbuka kurudi ccm."

Hilo litawezekana kama Mungu huyu ni wa ccm. Ccm sirudi pamoja kuwa najua nitateseka na familia yangu! Kisasi hiki mimi sitakiweza namwachia Mungu ndiye atakayetufuta machozi mimi na familia yangu."

FREDRICK TLUWAY SUMAYE.
WAZIRI MKUU MSTAAFU.


Source: JF

Kimenuka..Mtoto wa Mgombea TFF Adakwa Live Chooni na Burungutu la Hela Dodoma leo

$
0
0
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Lazaro Mambosasa amethibitisha kuwa jeshi la Polisi kwa kushirikiana na TAASISI ya kuzuia na kupamabana na rushwa TAKUKURU inamshikilia kijana mmoja kwa tuhumza ya kujihusisha na vitendo vya rushwa.


Kijana huyo aliyejulikana kwa jina la Endru Kevela Yono ambaye baba yake ni miongoni mwa wagombea amekutwa chooni katika ukumbi wa mikutano wa St. Gaspar mjini Dodoma ambao ndiyo uchaguzi wa TFF unapofanyika akiwa na burungutu la laki tano huku akiwa amegawa katika mafungu ya shilingi elfu hamsini yakiwa tayari kwa kupatiwa baadhi ya wa jumbe ambao orodha ya majina yao yameandikwa

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Lazaro Mambosasa  akizungumza na Shirika la utangazi Tanzanai (TBC) amesema “Tumemkuta chooni ambako aliandaa mazingira kwamba wajumbe wanapo kwenda kule basi wapewe hizo bahasha kwahiyo hakuna ubishi ni swala la rushwa”, amesema.

Kamanda Mambosasa ameongeza kuwa “Niendelea kutoa wito na rai kwa wajumbe na wapambe wao waliyokuja kufuatilia shughuli hii, tulichoonya ndicho tunachokifanya yeyote ambaye atajaribu kuendelea kupuuza kujihusisha na vitendo hivi vya rushwa ajue hatakuwa salama kama alivyokuwa huyu kijana”.

“Huyu kijana sasa yupo mbaroni anaendelea kuhojiwa na jeshi la polisi kwa kushirikiana na TAKUKURU kwahiyo niseme tu kwamba yeyote anayetaka kuendelea nkujihusisha na vitendo hivi hayupo salama nilisema hapo jana kuingia ni rahisi lakini utokaji ni shighuli”amesema kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Lazaro Mambosasa.

By Hamza Fumo
Viewing all 104803 articles
Browse latest View live


Latest Images