Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104789 articles
Browse latest View live

VIDEO:MCT Wanatoa Ripoti ya Uchunguzi wa Uvamizi wa Clouds Media

$
0
0
VIDEO:MCT wanatoa ripoti ya uchunguzi wa uvamizi wa Clouds Media

Baraza la Vyombo vya Habari Tanzania(Media Council of Tanzania-MCT) Likiongea na Wanahabari mapema leo limesema kuwa tukio la Uvamizi wa Clouds Media limeongelewa kwa kirefu, hivyo waliamua kulifanyia utafiti huru ili kuelewa kilichotokea haswa.





=> Ripoti imeandaliwa kutoka maeneo mawili ya Tanzania Bara na Visiwani.

=> Methodology: Kusoma machapisho na maandiko pia kuhoji watu mbalimbali.

=> Kuna mahusiano makubwa kati ya mfumo wa kisheria na masuala ya kisiasa. Mfano kupitishwa kwa sheria mbili zinazohusu sekta ya habari.

=> Kinyume na matarajio ya wengi sheria hizi mbili zimeonekana kuwa haziwezi kukidhi nahitaji katika sekta ya habari. Ingawa zilipokelewa kwa Shangwe na wengi lakini matokeo yake ni kuwepo kwa vifingu vinavyominya Uhuru wa habari.

=> Pia zuio la kurushwa kwa matangazo ya Bunge hili pia tumeliangazia katika utafiti wetu. Wananchi wengi wamekiri kuwa usitishwaji huo umewanyima haki ya kujua nini Wawakilishi wao wanafanya ndani ya Bunge.

=> Mwaka 2016 taasisi nyingi za Print Media zilikuwa katika hali mbaya kutokana na matukio mbalimbali ya kufungiwa kwa magazeti.

=> Kupungua kwa matangazo kwenye magazeti hii imepelekea kuathiri sana shughuli za Taasisi hizo.

=> Kushuka kwa usambazaji wa magazeti kutokana na kuingia kwa mitandao ya kijamii pamoja na miundo mbinu.

=> Pia miundombinu ya usambazaji imekuwa mibovu.

=> Kutoka na sheria zisizo rafiki imekuwa pia chanzo cha mauzo ya magazeti kushuka. Pia ukosefu wa teknolojia ya hali ya juu umekuwa ni changamoto.

MAFANIKIO
=> Print media zimeendelea sana katika habari za kiutafiti.

=> Redio imeendelea kuwa chombo kinachotegemewa na watu wengi na idadi ya redio pia imeongezeka.

ZANZIBAR
=> Kwa Zanzibar kulikuwa na matukio mengi ikiwemo waandishi kunyimwa ushirikiano.

=> Baadhi yao walipewa vitisho na kulazimika kujilinda bila kujali kwamba wanafanya kazi hiyo kwa ajili ya jamii.

=> Hakukuwa na muongozo wowote wa kuwaeleza waandishi kuwa habari hii weka au hii iache.

=> Tumebaini Zanzibar mpaka leo hakuna sheria ya Right to information.

=> Waandishi wengi hawajiendelezi kielimu na baadhi ya waandishi wanafanya kazi bila kuwa na elimu ya kutosha kuhusu taaluma

=> Zanzibar kuna Vituo vya redio 25 na runinga 22.

MAPENDEKEZO
=> Kuna haja ya kutungwa kwa sheria ya Right to information

=> Kuna haja ya specialization kwenye news room

=> Pia traning kwa waandishi hasa kuhusu maslahi yao maana wengi wanajua kutetea maslahi ya jamii lakini ya kwao hawayajui.

RIPOTI YA CLOUDS
=> Baraza la habari lilitupa jukumu la kuchunguza kilichotokea kituo cha CloudsMedia Group 17 March, 2017 ambapo mkuu wa mkoa alienda studio usiku akiwa na askari.

=> Timu yetu ilikuwa na wanachama wanne.

=> Kwa mujibu wa katiba ya habari kifungu cha tatu [E] ndicho tulichokisimamia katika uchunguzi wetu.

Hadidu za rejea zilizotumika.
1. Kwanza kuchunguza kilichotokea
2. Kubaini askari walioambatana na mkuu wa mkoa
3. Kutoa mapendekezo kutokana na uchunguzi
4. Kuandika ripoti
5. Kuwasilisha kwa wananchi

=> Timu ilitembelea ofisi za Clouds na kuongea na baadhi ya wafanyakazi, ilifanya mahojiano na wafanyakazi wa TRA, Ilifanya mahojiano maafisa wa haki za bianadamu.

=> Juhudi za timu kuonana na mkuu wa mkoa hazikuzaa matunda yoyote.

=> Tulipitia sheria kuona kama kuna sheria yoyote inayomruhusu mkuu wa mkoa kufanya hicho alichokifanya.

TULICHOBAINI
=> Tarehe 17/3 mkuu wa mkoa wa Dsm akiwa na askari alienda kwenye kituo cha Clouds usiku lakini afisa wa ulinzi alisema mkuu wa mkoa huwa anaenda mara kwa mara na alishazoeleka.

=> Sio vibaya kwa vyombo vya habari kushirikiana na wanasiasa lakini Urafiki uliojengwa kati ya mkuu wa mkoa na Clouds ndio uliopelekea akawa na ujasiri wa kuingia ofisi kwa namna ile.

=> TCRA ilisema haina wajibu wa kumuadhibu mtu aliyekikosea kituo cha habari kwahiyo yunaona iwepo sheria itakayoruhusu TCRA kuweza kufanya hivyo

Chanzo:Jamii Forums

Rais wa Misri Atua Tanzania kwa Ziara ya Siku Mbili

$
0
0

Rais wa Misri Atua Tanzania kwa Ziara ya Siku Mbili
Rais wa Jamhuri ya nchi za kiarabu ya Misri, Abdel Fattah El-Sisi amewasili nchini Tanzania na kupokelewa na mwenyeji wake, Rais John Pombe Magufuli kwa ziara ya kikazi ya siku mbili.

Amewasili kwa ndege maalum ya serikali ya Misri na kupokelewa kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam..

Hii itakuwa ni ziara ya kwanza ya  nchini Tanzania tangu Dk Magufuli aingie madarakani Oktoba mwaka 2015. Kwa mujibu wa taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,

Lengo la ziara  ni kuimarisha na kukuza zaidi mahusiano mazuri yaliyopo ya kidiplomasia, kiuchumi na kijamii kati ya nchi hizi mbili, na itatoa fursa kwa viongozi hao kujadili masuala mbalimbali yanayohusu nchi hizi mbili, ya kikanda na kimataifa.



Sitegemei Mitandao ili Kuachia Nyimbo Zangu - Shilole

$
0
0




Sitegemei Mitandao ili Kuachia Nyimbo Zangu - Shilole
Msanii Zuwena Mohamed Shilole' amekanusha kauli yake ya kushindwa kuachia ngoma kwa kipindi cha miezi mitano kutokana na kudukuliwa kwa mtandao wake wa (Instagram) na badala yake alikuwa akiusoma mchezo huku akisubiria majibu ya ngoma 'Hatutoi Kiki.

Shilole amedai kuwa watu wanaozungumza kwamba yeye amekaa kimya muda mrefu ni kutokana na wengi wao kumiss kuona vituko na tashtiti zake katika mitandao ya kijamii hivyo hata wakati akiwa amejiandaa kutoa wimbo mpya bado alionekana kama kapooza.

"Siyo kweli kama nategemea Instagram kutoa kazi, kwani bila hiyo Insta zamani watu walikuwa wanafanyaje? Sijatoa wimbo kwa sababu nilitaka wimbo wa 'hatutoi kiki uendelee kusogea na siyo kwamba kwa sababu nilikuwa sina mtandao wa Instagram ndiyo nikaamua nitulie. Lakini kwa sababu najua kuna wasiosikiliza radio na na wasiotazama Tv ndiyo maana pia nilitulia kuusoma mchezo kwa kuwa nilitaka niwapate wote na mashabiki mashabiki wa mtandaoni ndiyo maana nilichelewa kidogo" Shishi alifunguka.

Hata hivyo Shilole ameongeza kuwa "mashabiki waliopokea wimbo wangu huu ndiyo mashabiki wa kweli siyo wale wanaosubiri tashititi za kukaa uchi au kelele zangu ila" Shilole.
Akizungumzia kuhusu mahusiano yake msanii Shilole amekanusha taarifa zinazoenea mitandaoni kuwa mume wake mtarajiwa ndiye mwanaume anayeonekana katika video yake mpya ya 'Kigori'.


Hali ya Kawaida Yaanza Kurejea nchini Kenya Wananchi Waanza Kurejea Kazini

$
0
0


Hali ya Kawaida Yaanza Kurejea nchini Kenya Wananchi Waanza Kurejea Kazini
Mji wa Kisumu ulikumbwa na vurugu wiki iliyopita lakini leo watu wengi wameanza kurejea kazini

Mji wa Kisumu ulikumbwa na vurugu wiki iliyopita lakini leo watu wengi wameanza kurejea kazini
Hali ya kawaida imeanza kurejea katika miji mingi nchini Kenya baada ya matokeo ya uchaguzi kutangazwa Ijumaa.

Watu wanaonekana kupuuza wito kwa kiongozi wa upinzani Raila Odinga wa kususia kazi leo kuomboleza watu waliouawa katika makabiliano kati ya polisi na waandamanaji waliokuwa wanapinga matokeo ya uchaguzi wa urais.

Wiki iliyopita, biashara nyingi zilifungwa watu wakihofia kuzuka kwa fujo kutokana na uchaguzi uliofanyika Jumanne.

Baadhi ya maeneo yakiwemo mitaa ya Mathare na Kibera jijini Nairobi na maeneo ya magharibi mwa Kenya yakiwemo Kisumu, Homa Bay na Migori.

Tofauti na hali ilivyokwa Ijumaa, biashara zimeanza kufunguliwa na magari ya uchukuzi wa abiria yameanza kufanya kazi katika barabara nyingi.

Baadhi ya wakazi mtaani Kibera wamesema wanahitaji kufanya kazi kujipatia chakula na mahitaji mengine ya kimsingi.

Lakini wengine wameamua kutekeleza ushauri wa Bw Odinga na kususia kazi.
Bw Odinga, aliyewania urais kupitia muungano wa upinzani National Super Alliance (Nasa) amekataa kukubali matokeo ya uchaguzi yaliyotangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (IEBC).

Rais Kenyatta alipata kura 8, 203, 290 ambayo ni asilimia 54.27 naye Bw Odinga akapata kura milioni 6,762,224 ambayo ni asilimia 44.74.
Muungano wa Nasa umedai mitambo ya tume ya uchaguzi ilidukuliwa na matokeo kuchakachuliwa kuhakikisha Bw Kenyatta anashinda.

Msimamo wa muungano huo unaenda kinyume na waangalizi wa kimataifa kutoka Umoja wa Afrika, Umoja wa Ulaya na Jumuiya ya Madola, miongoni mwa wengine, ambao walisema uchaguzi huo ulikuwa huru na wa haki.

Mwaka 2016 Mbaya kwa Habari Zinazochapishwa Kutokana na kuwepo Kwa Sheria Kandamizi

$
0
0


  Mwaka 2016  Mbaya kwa Habari Zinazochapishwa  Kutokana na kuwepo Kwa Sheria Kandamizi
Uwepo wa sheria kandamizi zinazoratibu magazeti umechangia kwa kiasi kikubwa mwaka 2016 kuwa mbaya kwa habari zinazochapishwa.

Hilo limeanishwa kwenye ripoti ya hali ya vyombo vya habari mwaka 2016 katika utafiti uliofanywa na Baraza la Habari Tanzania (MCT).

Akiwasilisha ripoti hiyo leo Jumatatu, Dk Joyce Bazira amesema licha ya magazeti kujikongoja hali ilikuwa mbaya.

Amesema yapo magazeti na majarida ambayo yaliamua kujiondoa yenyewe sokoni kutokana na uwepo wa sheria hizo.

Amesema kwa mwaka jana pekee jumla magazeti  437  yalifutwa  kwa pamoja.

"Haijawahi kutokea magazeti mengi hivi yakafungwa kwa pamoja ndiyo sababu tumeona ilikuwa mwaka mbaya kwa magazeti."

Amesema kulikuwepo pia suala la kushuka kwa matangazo na usambazaji wa magazeti unapungua.

"Tunaona mwaka 2016 usambazaji na mauzo ya magazeti yalipungua mno na hii ni kutokana na uwepo wa mitandao ya kijamii,"

Amesema takwimu zinaonyesha mwaka 2016 magazeti machache yamesajiliwa ikilinganishwa na mwaka 2015.


Tundu Lissu Aeleza Ushauri wa CHADEMA kwa Wakenya

$
0
0

Tundu Lissu Aeleza Ushauri wa CHADEMA kwa Wakenya
Rais wa TLS na Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA, Tundu Lissu amefunguka na kusema wao kama CHADEMA waliwaambia watu wa Kenya kuwa kama watarogwa na kumchagua Raila Odinga kuwa Rais wa nchi hiyo wangekoma kwani aliweka wazi ataongoza kama Rais wa Tanzania.

Tundu Lissu anasema kuwa katika uchaguzi uliofanyika nchini Kenya tarehe 8 Agosti 2017 unatoa mafunzo mengi kwa Tanzania kwani Kenya wameweza kupiga hatua kubwa na kutoa haki ya msingi ya kupiga kura kwa wafungwa na Raia wake waliopo nje ya Kenya jambo ambalo Tanzania ni kitu kisichowezekana.
"Kenya inatufundisha umuhimu wa kuwa na Katiba mpya, Katiba ya Kidemokrasia, Katiba inayoweka uhuru kwa wale wanaoshiriki uchaguzi kwa kuweka utaratibu wa kuhakiki taratibu za uchaguzi katika kila hatua na hilo ni jambo muhimu sana, lakini Kenya inatufundisha umuhimu wa kuwa na Demokrasia tumeona wafungwa wakipiga kura, tumeona waandishi wa habari wakiruhusiwa kuiingia gerezani kueleza umma jinsi zoezi la upigaji kura linavyoendelea hata kwa watu ambao wamepata adhabu kwa mujibu wa sheria za Kenya lakini kwetu sisi hicho kitu hakipo kabisa, tumeona raia wanaokaa nje ya Kenya wameshiriki uchaguzi sisi hilo haliwezekani" alisema Tundu Lissu
Aidha Tundu Lissu amesema kwa mambo yote ambayo yameendelea Kenya katika uchaguzi yanatoa funzo kuwa na mfumo wa Demokrasia lakini pia amegusia chama cha CHADEMA kuwa rafiki na Chama Cha Jubilee na kusema siyo dhambi.

"Sisi kuwa na chama rafiki Kenya wala siyo kitu cha ajabu sana, tuna chama rafiki Ghana tunavyama rafiki kila mahali na wakati wa uchaguzi marafiki wanaungana mkono, wakati wa uchaguzi ANC wanaunga mkono CCM, Museven na NRM yake wanaunga mkono CCM na sisi kwenye uchaguzi huo wa Kenya tumeunga mkono Jubilee, na kwenye uchaguzi huu wa juzi Raila Odinga aliwaambia wa Kenya kuwa wakimchagua ataongoza nchi kama Rais wa Tanzania ilibidi tuwaambie Wakenya kuwa mtakoma" alisisitiza Tundu Lissu

Katika Uchaguzi uliofanyika tarehe 8 Agosti 2017 nchini Kenya tumeya uchaguzi nchini humo ilimtangaza Uhuru Kenyatta kuwa mshindi wa nafasi ya Urais kwa kupata kura zaidi ya milioni nane huku mpinzani wake Raila Odinga na Muungano wa NASA wakishika nafasi ya pili kwa kupata kura milioni sita.

Wapiga Debe Waiomba Serikali Kusitisha Mpango wa Kuwaondoa

$
0
0


Wapiga Debe Waiomba Serikali Kusitisha Mpango wa Kuwaondoa
Zaidi ya vijana 200 ambayo wanaopiga debe eneo la Kamanga Ferry jijini Mwanza, wameiangukia serikali na kuiomba iwaache waendelee na shughuli zao na kusitisha mpango wake wa kutaka kuwaondoa hapo, anaandika Moses Mseti.

Vijana hao wametoa kilio chao kwa Katibu wa Umoja na Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), mkoa wa Mwanza, Mariam Amiri.

Mwenyekiti wa wapiga debe hao, Husein Manyika, amesema baada ya kusikia tangazo la serikali kupitia vyombo vya habari ambalo linawataka kuondoka na kuacha kazi hiyo, limewashtua na kwamba hawajui pa kwenda.

Amesema kuwa katika eneo hilo pia wapo wapiga debe, wachuuzi wa samaki pamoja na wafanyabiashara wadogo maarufu kama Wamachinga.

“Tunaambiwa tuondoke hapa (Kamanga), wakati serikali haijatuandalia maeneo ya kutupeleka hivyo kabla hawajatuondoa, wanapaswa kukaa na watafakari ni wapi watakapotupeleka ndipo wachukue uamuzi huo,” amesema Manyika.

Grace Matata Awapa Somo Wasanii Kuhusu Mziki wa Live

$
0
0




Grace Matata Awapa Somo Wasanii  Kuhusu Mziki wa Live
Msanii wa Bongo Flava, Grace Matata ametoa somo kuhusu muziki wa live kwa kuwataka wasanii kujielekeza zaidi katika eneo hilo kama wanataka muziki wao kudumu muda mrefu na kuwa na heshima.



Muimbaji huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wake mpya ‘Dakika Moja’ aliyomshirikisha rapper Wakazi, ameiambia The Playlist ya Times Fm kuwa anapokuwa studio hujaribu kufanya muziki ambao akiwa katika jukwaa anaweza kuufanya live.

“Ukiangalia kwenye trend ya globally watu wanatengeneza pesa kwenye vitu tofauti kama downloads, endorsement lakini live performance bado ipo juu sana lakini kama umezoea kufanya kazi ya kawaida ukifika mahali umekuwa na jina kubwa unawekwa kwenye stage kubwa hapo ndipo utaelewa kwanini kuna umuhimu wa kuwa vizuri both one stage and off stage inakupa kind of respect,” amesema.

Amesema mwaka jana alipata bahati ya kuona performance ya Oliver Mtukudzi ambaye kwa sasa ana miaka 65 ila anavyofanya ni vigumu kuamini katika umri wake lakini siri kwamba amejijenga katika hilo miaka nendarudi.

“Mimi when I start hakuna kitu nilichokuwa naogopa kama kupanda on stage nikijua na event naumwa, nikafanya majaribio mpaka nikafanikiwa. For me I inspire kuwa very good performer na nina shauri kama wewe ni masanii na una mpango wa kwenda international kufanya big thing you have to do something about live performance vinginevyo itafika mahali unapewa platform unashindwa, ni muhimu sana,” amesisitiza.




Masanja Hatimaye Baba Kijacho Mungu Ajibu Maombi

$
0
0

Masanja Hatimaye Baba Kijacho Mungu Ajibu Maombi
Wakati ndoa yake ikitimiza mwaka mmoja mwezi huu tangu ilipofungwa Agosti, mwaka jana ndani ya Kanisa la Mito ya Baraka lililopo Jangwani jijini Dar, aliyekuwa memba wa Kundi la Vichekesho la Orijino Komedi, Emmanuel Mgaya ‘Masanja Mkandamizaji’ huku masimango yakiwa mengi kutokana na kukaa muda mrefu bila mkewe, Monica kushika ujauzito, hatimaye Mungu amejibu maombi,

Chanzo makini kilicho karibu na staa huyo kililitonya  katika ndoa ya Masanja kulikuwa na changamoto kubwa kwani chokochoko na masimango vilikuwa vimeanza huku watu wakijiuliza kwa nini miezi yote hiyo mkewe hajapata ujauzito kwa sababu watu walishazoea mtu akiingia tu kwenye ndoa muda mfupi baadaye lazima ijibu.

“Kiukweli Masanja na Monica wamepitia kwenye masimango makubwa sana kwani watu walikuwa wakiwasimanga kwamba ndoa yao imechelewa sana kujibu huku wengine wakidai huenda kuna mkono wa mtu ndiyo maana wamekawia kiasi hicho

Walemavu Waitikia Wito wa RC Makonda Wafurika Kuchukua Miguu Bandia

$
0
0



Walemavu Waitikia Wito wa RC Makonda Wafurika Kuchukua Miguu Bandia
Mamia ya watu wenye Ulemavu wa Miguu wamejitokeza kwa wingi leo kwenye Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam kuchukuwa vipimo kwaajili ya kupatiwa Miguu bandia ambapo idadi imekuwa kubwa tofauti na ilivyo tarajiwa huku wengine wakitokea Mikoani.



Mwitikio huo ni kufuatia Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda kuwatangazia wenye uhitaji ya Miguu Bandia kufika ofisini kwake kwaajili kuchukuliwa vipimo ili wapatiwe miguu  hiyo bila malipo ambapo hadi saa nne asubuhi walemavu waliokuwa wamefika ni zaidi ya 500.


Makonda amesema licha ya idadi hiyo kuzidi ile ya watu 200 iliyokusudiwa atahakikisha wote wanapimwa na wataalamu na kupatiwa huduma bila ubaguzi wa Mikoa wanayotoka sababu wananchi wote wapo chini ya Rais Dr.Magufuli.


Amesema wote watakaopimwa watatengenezewa Miguu yao kulingana na vipimo vilivyochukuliwa.
Hata hivyo Makonda amesema kutokana na wingi wa watu wenye uhitaji ataongeza siku za upimaji na kuongeza idadi ya wataalamu ili wote watakaofika wahudumiwe.


Aidha amesema awamu hii ya kwanza walemavu 200 watapatiwa miguu ya bandia wakati akiendelea kufanya jitiada za kuwasiliana na wadau ili waweze kuchangia na kuhakikisha wananchi wote wanahudumiwa.


Mbali na miguu bandia pia Makonda amefanikiwa kupata Magongo ya kisasa 17 kutoka Nchini Marekani ambayo pia atayatoa bila malipo kwa wale wenye uhitaji.





Je Wafahamu Umuhimu Supu ya Pweza kwa Wanandoa?

$
0
0

Je Wafahamu Umuhimu Supu ya Pweza kwa Wanandoa?
Hamu ya tendo la ndoa kwa mwanadamu ni moja ya hisia za msingi kwa mtu wa kawaida kama ilivyo njaa au usingizi.

Pweza ni aina ya samaki ambaye anapendwa na baadhi ya watu hasa supu yake ambayo imekuwa na mkombozi kwa watu wengi haswa wanandoa.

Je Wafahamu Umuhimu Supu ya Pweza kwa Wanandoa?
Supu ya Pweza inafaida takribani Tisa mwilini mwa mwanadamu hususani kwa wanandoa na wakinamama wanaonyonyesha ikiwemo virutubisho kuukinga mwili wa mlaji dhidi ya magonjwa kama kansa.

Pweza amejawa virutubishovinavyosaidia kuongeza hamuna kuboresha tendo la ndoa hali inayosaidia mwanamke kuwa katika hali nzuri ya uwanamke wake huku mwanaume kuwa mwanaume wa shoka wakati wa tendo la ndoa


Kwa ajili ya matatizo mbalimbali yaliyo katika jumuiya, pamoja na kwamba tendo la ndoa ni jambo la msingi kwa wale waliooana, kuna wanaume aidha hawana uwezo wa kulifanya tendo hili au wana hisia ndogo na nguvu kidogo za kutekeleza tendo hili.


Ni imani ya wanaume wengi wa pwani na hata kutoka bara ambao huishi ukanda wa pwani siku hizi hupenda supu ya pweza kutokana na wingi wake wa virutubisho ambavyo huamini kuwa vinaongeza nguvu za kiume kwa waliopungukiwa.

Pweza usaidia kusisimua mwili huku wengine wakidai wanatumia kama kiburudisho tu sio kama dawa ya kuongeza nguvu.

Supu hiyo inasaidia sana kwa wanaume kuongeza mbegu na kusukuma hamu ya tendo la ndoa hivyo ufanya wanandoa kuweza kukamilisha jukumu lao la unyumba kwa namna bora zaidi.
 na kuongeza heshima kwa wanandoa hao.

'Serikali Haina nia ya Kurudisha Pombe za Viroba'- Makamba

$
0
0

'Serikali Haina nia ya Kurudisha Pombe za Viroba'- Makamba
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), January Makamba amesema Serikali haina nia ya kurudisha sokoni pombe zilizotengenezwa katika mifuko ya plastiki 'viroba'na kuwataka Watanzania kupuuza uzushi unaoenezwa kwamba pombe hizo zitarudi.

Makamba alitoa kauli hiyo leo, Jumatatu Agosti 14 alipotembelea eneo la Kimara Temboni lilipo ghala la kuhifadhi pombe mbalimbali ikiwamo viroba linalomilikiwa na Kampuni Thema.

Makamba alisisitiza kwamba Serikali uamuzi wake wa kuzuia pombe hizo upo palepale na haujabadilika hivyo watu waache kupotosha wenzao.

"Baada ya kupiga marufuku kuna kampuni zilikuja ofisi kuomba kuongezewa muda, lakini tuliwakatalia na kuwaambia waheshimu uamuzi uliotolewa sasa hizi tetesi ya kwamba vinarudi sokoni sijui zinatoka wapi," alisema Makamba.

Makamba ambaye pia ni Mbunge wa Bumbuli amesema  njia ya pekee kwa wafanyabiashara hao wa viroba wanaotakiwa kuifanya ili kupunguza hasara ni kubadilisha pombe hizo na kuziweka katika chupa zenye ujazo unaotakiwa.

Amesema kamwe Serikali haiwezi kurudi nyuma na kwamba mafanikio yameanza kuonekana kutokana na hatua hiyo.

       

Simba Nayo Yaende Kujichimbia Zanzibar Wawafuata Watani Wao

$
0
0

Simba Nayo Yaende Kujichimbia Zanzibar Wawafuata Watani Wao
Kikosi cha Simba  leo jioni kinatarajiwa kusafiri kwenda visiwani Zanzibar kupiga kambi ya wiki nzima kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa ngao ya jamii unaotarajiwa kuchezwa tarehe 23 Agosti jijini Dar es Salaam.

Watani wa jadi Simba na Yanga ndiyo watakutana katika mechi ya ufunguzi rasmi wa pazia la Ligi Kuu Tanzania Bara 2017/2018 mchezo ambao unatarajiwa kuwa na mvuto wa aina yake kutokana na klabu hizo msimu huu kuwa na mabadiliko ya aina yake katika vikosi vyao.

Klabu ya Yanga ilitangaza kupiga kambi kisiwani Pemba kwa wiki moja kwa ajili ya maandalizi ya mchezo huo na Simba nao wameamua kuwafuata watani wao wajadi huko huko Zanzibar nao wakijandaa dhidi ya Yanga na michezo mingine katika Ligi Kuu Tanzania Bara ambayo inatarajiwa kuanza Agosti 26 mwaka huu.

Madee Awatolea Povu Wanaofanya Muziki Nje ya Uwezo Wao Kwenda Kimataifa

$
0
0

Madee Awatolea Povu Wanaofanya Muziki Nje ya Uwezo Wao Kwenda Kimataifa
Msanii Madee amewafunguka juu ya wasanii wanaolazimisha kufanya vitu vikubwa vilivyo nje ya uwezo wao, ili muziki wao kwenda kimataifa kama ambavyo wengi wanakusudia, na kusema kuwa haitakiwi kuwa hivyo.Akizungumza kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio alipokuwa akitambulisha kazi yake mpya 'Sikila' ambayo amemshirikisha msanii wa Nigeria Tekno, Madee amesema kazi kwenda kimataifa zinakuja zenyewe baada ya kufanya kazi nzuri, akitolea mfano ufanyaji wa kazi zake.

"Mimi siyo yule mtu ambaye nafanya kitu kwa sababu nataka kwenda kimataifa, unapoamua kufanya kitu unafanya, kwa sababu kimataifa haiji kwa sababu wewe unataka, kimataifa inakuja yenyewe kila unachokifanya kinasogea tu, ukijifanya kulazimisha mwisho wa siku ndiyo unakuwa unaangukia pua, unaenda kufanya mavideo ya gharama huko unatoa hela unampa nani, mwisho wa siku hamna kitu unapata mawazo, mimi nafanya muziki ambao nauona ni tofauti", alisema Madee.

Madee aliendelea kusema kuwa ukifanya kitu chenye ubora na chenye kuleta utofauti, huwa kinajiuza chenyewe na kufika huko kunakoitwa kimataifa.

'Zimbabwe' ya Roma Imevunja Rekodi Mitandaoni Kwa Kuwa na Watazamaji Wengi

$
0
0



'Zimbabwe' ya Roma  Imevunja Rekodi Mitandaoni Kwa Kuwa na Watazamaji Wengi
Msanii Roma Mkatoliki ambaye sasa yupo nchini Zimbabwe na anayefanya vizuri na wimbo wake mpya Zimbabwe amevunja rekodi yake mwenyewe baada ya wimbo wake mpya kufanya vizuri zaidi katika mtandao wa You Tube.

Siku ya Alhamisi tarehe 10 Agosti 2017 Roma Mkatoliki alipandisha kwenye mtandao wa You Tube video ya wimbo wake mpya ambao umeonekana kuwagusa watu wengi kutokana na ujumbe wake na mashairi ambayo yapo kwenye wimbo huo, hali ambayo imefanya video hiyo kutazamwa na watu wengi zaidi ndani ya muda mfupi mpaka kufikia hatua ya kuwa video namba moja inayofanya vizuri kwenye mtandao huo kwa takribani siku zote tatu toka imetoka.

Ndani ya masaa 75 Video mpya wa Roma Mkatoliki imetezamwa na zaidi ya watu laki sita na kuvunja rekodi kwa video kadhaa ambazo Roma Mkatoliki amewahi kuziweka kwenye mtandao huo kwa mfano, mwaka mmoja uliopita Roma Mkatoliki alitoa wimbo unaoitwa 'Kaa Tayari' aliomshirikisha Jos Mtambo na Darassa video yake mpaka sasa imetazamwa na watu laki tatu na kitu.

Mwanzoni mwa mwaka huu tarehe 15 Januari, Roma Mkatoliki aliachia video ya wimbo wa kushirikiana unaoitwa 'Usimsahau Mchizi' akiwa na Moni Centrozone video hiyo mpaka sasa imetazamwa na zaidi ya watu laki tatu na kitu hii ndiyo ilikuwa kazi ya mwisho kwa Roma Mkatoliki kwani baada ya hapo alipatwa na matatizo ya kutekwa na aliporejea aliendelea kuuguza majeraha yake na kujiweza sawa mpaka alipokuja kudondosha wimbo huu mpya ambao unaonekana kukata kiu ya mashabiki wengi wa muziki na mashabiki wa Roma Mkatoliki.

Mpaka sasa 'Zimbambwe' yake Roma Mkatoliki imevunja rekodi kwa kuwa na watazamaji wengi zaidi ndani ya muda mfupi kwa ngoma za Roma, ikumbukwe kuwa kwa wasanii wa Hip hop video ambayo iliwahi kupokelewa kwa speed hii ni 'Muziki' ya Darassa ambayo ndani ya wiki mbili iliweza kufikisha watazamaji milioni moja na kuwa namba tano katika video zinazo 'Trend' kwa kipindi hicho, Video nyingine ambayo imewahi kuwa na kasi hiyo kwa upande wa wasanii wa Hip hop ni 'Dume Suruali' ya Mwana FA akimshirikisha Vanessa Mdee.




TFF Yatuma Salamu za Rambirambi kwa Aliyekuwa Katibu Mtendaji (FAT)

$
0
0


TFF Yatuma Salamu za Rambirambi kwa Aliyekuwa Katibu Mtendaji (FAT)
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia ametuma salamu za rambirambi kufuatia kifo cha aliyewahi kuwa Katibu Mtendaji wa kilichokuwa Chama cha Mpira wa Miguu Tanzania (FAT), Chabanga Hassan Dyamwale (76).

Mbali wa wadhifa huo katika eneo la mpira wa miguu,  pia Dyamwale atakumbukwa zaidi akiwa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii na kwa miaka ya hivi karibu alikuwa Mjumbe wa Kamati huru ya uchaguzi TFF tangu 2004 mpaka 2012.

Hayati Dyamwale aliyezaliwa Juni 01, 1941, aliondoka FAT mwaka 1978, lakini pia aliwahi kuwa Mkurugenzi wa Michezo nchini miaka ya mwanzo ya 1980 kabla ya kuhamishiwa Handeni mkoani Tanga kuwa Ofisa Utamaduni, lakini Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati huo, Mwalimu Julius Nyerere akamrudisha Dar es Salaam.

“Nimeguswa na kifo cha Mzee Chabanga Hassan Dyamwale. Inna Lillah wainaillah Rajauun. Natuma salamu zangu za rambirambi kwa familia, ndugu, jamaa, majirani na marafiki wa hayati Mzee Dyamwale ambaye nimetaarifiwa kuwa amefariki dunia Agosti 13, mwaka huu kwenye Hospitali ya Muhimbili,” amesema Karia.

“Ni msiba mkubwa kwa wanafamilia ya michezo hususani soka,” amesisitiza Rais Karia na kuomba  familia, ndugu, jamaa, marafiki kuwa watulivu katika kipindi hiki kigumu baada ya kumpoteza mpendwa Dyamwale.

Rais Karia amesema: “Namfahamu Mzee wetu huyu tangu miaka mingi akiwa mteuliwa kutoka serikalini kushika wadhifa wa utendaji ndani ya FAT wakati ule (Kwa sasa ni TFF), alifanya kazi kwa uhodari mkubwa na uadilifu,” amesema Rais Karia.

Rais Karia amesema kwamba mbali ya kuwa mtendaji ambaye alifanya mabadiliko makubwa katika soka la Tanzania kutoka ligi ya kituo kimoja hadi ligi ya mikondo miwili (nyumbani na ugenini). Taarifa zinasema kwamba alifanya kazi hiyo akiwa kwenye hema.

Pia Rais Karia alimfahamu Mzee Dyamwale alipokuwa Meneja wa Uwanja wa Taifa (sasa Uwanja wa Uhuru) aliyekuwa mtaalamu wa masuala ya ujenzi wa viwanja.

Rais Karia amesema kwamba atambukuka zaidi hayati Dyamwale kwa uhodari wake wa kazi na msimamo kwenye jambo aliloliamini lilileta mafanikio makubwa katika soka la Tanzania.


Vigogo Tuhuma ya ESCROW Kuchunguzwa na TAKUKURU Kama Wameficha Pesa Nje ya Nchi

$
0
0


Vigogo Tuhuma ya ESCROW Kuchunguzwa na TAKUKURU Kama Wameficha Pesa Nje ya Nchi
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) imesema kuwa imeamua kushirikisha taasisi zingine za kimataifa ili kuwachunguza baadhi ya watuhumiwa wa Escrow kama wamehifadhi fedha nje ya nchi.

Hayo yamesemwa na Afisa Habari na Uhusiano wa taasisi hiyo, Mussa Misalaba alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, ambapo amesema kuwa watuhumiwa wote wa Escrow bado wanaendelea kuchunguzwa.

Amesema kuwa Takukuru inaendelea kuwachunguza watuhmiwa wote huku ikishirikiana na baadhi ya taasisi za nje na kwamba uchunguzi huo unafanyika kwa umakini zaidi ili haki itendeke.

“Hili jambo linafanyika kwa umakini mkubwa, usione kimya kuna jambo linafanyika, kwa sasa ni mapema sana kusema chochote kuhusu jambo hili kwakuwa linahitautlivu mkubwa kulishughulikia,”amesema Misalaba

Aidha, hivi karibuni TAKUKURU iliwafikisha mahakamani baadhi ya watuhumiwa wa ufisadi na uhujumu uchumi ili kujibu mashtaka yanayowakabili.

Waliofikishwa mahakamani kujibu tuhuma ni pamoja na Theofilo Bwakea, Mkurugenzi wa Kampuni ya VIP Engineering and Markerting, na aliyekuwa Mkurugenzi wa Kampuni ya IPTL, James Rugemalila wote wakikabiliwa kesi ya uhujumu uchumi

Waziri Mpango Awatumbua Watumishi 4 TRA.....

$
0
0


Waziri Mpango Awatumbua Watumishi wa Nne TRA Watumbuliwa

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, amewasimamisha kazi watumishi wanne wa Idara ya Forodha, katika Mpaka wa Tanzania na Zambia, Mjini Tunduma, ili kupisha uchunguzi wa kudaiwa kuhusika na upotevu wa lakiri 10 zinazotumika kufunga kwenye shehena ya mizigo inayopita mpakati hapo kutoka nje ya nchi.

Mpango amewataja watumishi hao kuwa ni pamoja na Harrison Mwampashi, John Makorere, Stephene Josia na Frank Kessy na kuviagiza vyombo vyote vya Ulinzi na Usalama mpakani hapo viwahoji huku wakiwa wamesimamishwa kazi.

Watumishi hao wanadaiwa kuiba lakiri hizo kumi kutoka ofisi za TRA-Tunduma wanakofanyiakazi, ambapo 4 kati ya hizo lakiri zilikutwa zimefungwa kwenye mizigo ya malori yanayoshikiliwa katika mpaka huo baada ya uchunguzi kufanyika huku malori mengine 5 yakizuiwa baada ya kuonekana lakiri zao zimechezewa.

Taarifa zinasema kuwa baada ya uchunguzi, mawakala ama wamiliki wa malori hayo wamedai walipewa lakiri hizo na watuhumiwa na kwamba uchunguzi zaidi umebaini kuwa kiwango cha mizigo kilichomo kwenye makontena yaliyobeba mizigo ya magogo na kufungwa lakiri hizo za wizi hakilingani na idadi ya
mizigo iliyoko kwenye nyaraka jambo linaloashiria kuwa wanazitumia lakiri hizo kudanganya idadi na uzito wa mizigo yao ili kukwepa ushuru na kodi mbalimbali za Serikali.

“Hakuna kitu muhimu kama uadilifu kwa mtumishi wa Mamlaka ya Mapato na hatutasita wala hatutamwonei aibu mtu yeyote, tutachukua hatua kwa mujibu wa sheria ili kulinda fedha za umma,” alionya Dkt. Mpango.

Alisema kuwa Serikali imebaini baadhi ya watumishi wa Mamlaka ya Mapato na Idara za Forodha mipakani wanashirikiana na wafanyabishara wasio waaminifu kuingilia mifumo ya kukusanyia mapato, kitendo ambacho kinaweza kurudisha nyuma juhudi za serikali kuwahudumia wananchi wake.

Dkt. Mpango amewaonya wafanyakazi wote wa forodha na Mamlaka ya Mapato nchini, kuwa wazalendo na waaminifu katika kukusanya mapato ya Serikali na kuacha kujihusisha na vitendo vinavyokwaza ufanisi wa Mamlaka hayo.

Diamond Platnumz Afunguka Kumkubali Ali Kiba Mpaka Kuweka Picha yake Ofisini Kwake

$
0
0
Msanii wa Muziki Bongo, Diamond Platnumz ametoa sababu ya kuweka picha ya Alikiba katika ofisi yake ya WCB.

Muimbaji huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma ya Eneka, ameimbia Clouds Fm Top 20 kuwa ameweka picha ya kila msanii ambaye ana mchango mkubwa katika kukuza muziki wa Bongo Flava.

“Ile siyo ofisi ya Diamond, Rich Mavoko, Harmonize, siyo ofisi ya Tale, ni ofisi ya muziki wa Bongo Flava ambayo imeweka kuona ni kwa namna gani inaweza kuinua muziki wa Bongo Flava,” amesema na kuongeza.
“Bongo Flava haikuletwa hapa tu pekee yangu na wana WCB lakini kuna wasanii tofauti tofauti wana mchango wao katika muziki wa Bongo Flava, so tumeweka baadhi ambao wanamchango, tulitamani tuweke wengine wengi lakini nafasi isingetosha, tumechagua wachache ambao wana mchango,” amesema.

Ameongeza kuwa watu wanaohoji au kushangaa kitu hicho ni hisia tu na kila mtu anapaswa kuwa na hisia zake lakini haikuwa hivyo kama wanavyofikiria.

Mke ,Mume Kuweka Password Kwenye Simu ni Dalili Tosha Kwamba Mnachepuka

$
0
0
Kitu cha ajabu sana hiki. Utakuta mume ameweka password very complicated na mke nae vivyo hivyo. Hii n tabia za wachepukaji. Huwezi kuweka password mkeo au mumeo asijue.

Unaficha mapicha yako. Unaficha 'appointments'. Unaficha mwenzio asimtambue ambaye unachepuka nae.

Just be free utaenjoy life.
Viewing all 104789 articles
Browse latest View live




Latest Images