Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104789 articles
Browse latest View live

Tamasha Lafutiliwa Mbali Uholanzi Kutokana na Tishio la Ugaidi

$
0
0
Tamasha Lafutiliwa Mbali Uholanzi Kutokana na Tishio la Ugaidi
Gari lililokuwa na mikebe ya gesi ya kutoa machozi limepatikana katika ukumbi ambapo kulipangiwa kufanyika tamasha ya muziki mjini Rotterdam nchini Uholanzi, saa chache baada ya tahadhari kutoka kwa polisi wa Uhispania kusababisha kufutiliwa mbali kwa tamasha hilo la muziki.
Dereva wa gari hilo lililosajiliwa nchini Uhispani amekamatwa na kuziliwa na polisi, meya wa mji wa Rotterdam Ahmed Aboutaleb amewaambia wanahabari.

Bendi kutoka Marekani ya Allah-Las, ambayo mara nyingi hupokeza vitisho kutokana na jina lake, ilikuwa imepangiwa kutumbuiza katika ukumbi wa The Maassilo.
Lakini tahadhari kutoka kwa polisi lilisababisha kufutiliwa mbali kwa tamasha hiyo dakika za mwisho.

Hata hivyo Bw Aboutaleb amesema haijabainika iwapo gari hilo lina uhusiano na tishio la shambulio la kigaidi.
Lakini tahadhari hiyo ya polisi wa Uhispania ilitolewa kukiwa na hali ya juu ya tahadhari baada ya mashambulio kadha kutekelezwa Uhispania wiki iliyopita.

Lakini maafisa wa mahakama wameambia shirika la habari la Reuters kwamba hakuna uhusiano wowote kati ya mashambulio hayo ya Uhispania na onyo kutoka kwa polisi wa Uhispania, ambalo inadaiwa limetokana na uchunguzi wa muda mrefu.

Polisi wa Uholanzi pia wamemkamata dereva wa gari hilo kutoka Uhispania na anahojiwa.
Kikosi cha kuchunguza na kutegua mabomu kimetumwa eneo hilo, taarifa zinasema.
Polisi waliovalia fulana zisizopenya risasi wamefika eneo hilo, baada ya watu wote kuamrishwa kuondoka.

"Polisi walikuwa wamezingira eneo la ukumbi huo na hilo lilisaidia kupatikana kwa mikebe hiyo ya gesi," Bw Aboutaleb amesema.
Katika mashambulio ya wiki iliyopita katika jimbo la Catalonia nchini Uhispania, watu 15 waliuawa katika mashambulio Barcelona na katika mji wa Cambrils.

Mashambulio hayo yalitekelezwa baada ya mlipuko katika nyumba iliyokuwa imejaa mikebe ya gesi ambapo washambuliaji inadaiwa walikuwa wanaandaa vilipuzi zaidi.

Katika mahojiano mwaka jana, kundi hilo la muziki aina ya Rock la Allah-Las liliambia gazeti la Guardian la Uingereza kwamba huwa linapokea vitisho mara kwa mara kutoka kwa Waislamu ambao hukerwa na kutumiwa na neno Allah - Mungu kwa Kiarabu - kama jina lake.

Kundi hilo lilisema lilitaka kuwa na jina lenye sifa za kidini baada ya kuhamasishwa na kundi jingine liitwalo Jesus and Mary Chain.

Haruna Niyonzima, Okwi na Haji Manara Baada ya Ushindi vs Yanga

$
0
0
Uwanja wa Taifa Dar es Salaam game ya ngao ya hisani ya Simba vs Yanga imechezwa na Simba kufanikiwa kupata ushindi kwa penati 5-4, Yanga wao walikosa penati mbili zilizopigwa na Juma Mahadhi na Kelvini Yondani wakati penati ya Simba ilikoswa na Mohammed Hussein Tshabalala.

Baada ya ushindi Haruna Niyonzima aliyejiunga na Simba akitokea Yanga na kutajwa kuwa ndio mchezaji ghali kwa sasa katika kikosi cha Simba leo amecheza game yake ya kwanza dhidi ya Yanga baada ya kuhama timu hiyo, presha kwake ilikuwaje”

Kucheza kwa mara ya kwanza dhidi ya Yanga presha ilikuwa kubwa unajua mimi ni mchezaji na hii ni kazi yangu hivyo nilimuomba Mungu aweze kunitoa hofu kwa sababu kitu kikubwa nilichokuwa nacho ni hofu, Yanga ni kama ndugu zangu nimecheza nao kwa muda mrefu” Niyonzima VIDEO:

Shilole Aruhusiwa na Mchumba Wake Kuvaa Nusu Utupu

$
0
0
Shilole Aruhusiwa na Mchumba Wake Kuvaa Nusu Utupu
JAMAA ambaye ndiye usingizi wa staa wa Bongo Fleva, Zuwena Mohamed, Ashrafu Uchebe, ameibuka na kumpa ruksa mpenzi wake ya kuvaa nguo za nusu utupu na kuwaambia mashabiki wamuache avae kwa sababu kazi yake inamruhusu.

Akizungumza na Amani, Uchebe alisema kuwa, anawashangaa wanaomwambia ‘baby’ wake huyo hana mavazi ya staha wakati yeye anamuona yupo sahihi.

“Jamani baby wangu wanataka avae dela apande nalo jukwaani wakati mavazi ya kupanda jukwaani yapo? Naomba waniachie malkia wangu kama wanataka na wao wavae,” alisema Uchebe ambaye uhusiano wake na mwanamuziki huyo umekuwa gumzo kwenye mitandao ya kijamii

MZEE MAJUTO:Hali Yangu Haijatengemaa Bado Naumwa

$
0
0

MZEE MAJUTO:Hali Yangu Haijatengemaa Bado Naumwa
Mungu tenda! Ikiwa ni siku chache tangu muigizaji mkongwe, Amri Athman Amri ‘King Majuto’ kupata unafuu kufuatia upasuaji aliofanyiwa kutokana na tatizo la ugonjwa wa ngiri (hernia), hali yake bado haijatengemaa na anatumia muda mwingi kulala, Amani limezungumza naye kwa tabutabu.

Jumatatu ya wiki hii, mwandishi wetu alimpigia simu mzee huyo kwa lengo la kumjulia hali na kufanya naye mazungumzo mengine, lakini King Majuto alisikika kwa shida na kudai amelala na anahitaji muda mwingi wa kupumzika na kwamba bado anaumwa na anasikia maumivu makali.

Hata hivyo, mwandishi aliendelea kumdadisi kwa kina ili kujua ni nini hasa kinachoendelea kumsumbua kwani kama ni tatizo la awali alishafanyiwa upasuaji, ambapo aligoma kabisa kuendelea na mazungumzo na kugeuka ‘mbogo’ kwa muda kwa madai ya kutopenda mazungumzo na wanahabari.

“Bado nimelala jamani na sijui unataka nini tena? Naumwa na ninasikia maumivu sana na sitaki kuzungumza zaidi maana nimechoka, elewa tu kwamba bado naumwa na ningependa sana uniache ili nipate muda mwingi wa kupumzika, ni kweli hivi karibuni nilipata nafuu kabisa na kuanza kutembea lakini ndiyo hivyo bwana, bado hali haijakaa sawa,” alisema King Majuto.

Amber Lulu` Atoa Sababu ya Kuamua Kustaafu Kazi ya U-video Gueen

$
0
0
Amber Lulu` Atoa Sababu ya  Kuamua Kustaafu Kazi ya U-video Gueen
MWANADADA machachari Bongo, Lulu Eugen ‘Amber Lulu`ameamua kustaafu kazi ya u-video queen kutokana na watu wanavyoidharau kazi hiyo na kuamua kujikita kwenye muziki wa Bongo Fleva.
Akibonga na paparazi wetu juzikati, Amber anayetamba na wimbo wa Only You, alisema kwenye maisha mtu anapaswa kusonga mbele na siyo kurudi nyuma hivyo ameshavuka kwenye sekta ya kuuza nyago kwenye nyimbo za watu na kuamua kukomaa kwenye fani ya muziki.

“Sitarajii tena kuwa video queen kwenye nyimbo za watu, kwanza muziki unanilipa zaidi kuliko fani ya kuuza sura inayodharaulika, hata mtu anipe dau gani siwezi kuuza sura kwenye wimbo wake,” alisema Amber.

Bill Nas Amkana Nandi Kuhusu Kutoka Kimapenzi

$
0
0
Bill Nas Amkana Nandi Kuhusu Kutoka Kimapenzi
Rapa Bill Nas ambaye sasa anafanya vyema na wimbo wake mpya wa 'Sina Jambo' amefunguka kwa kumtolea nje Nandy kwa kudai hajawahi kutoka naye kimapenzi kama watu wanavyofikilia katika vichwa vyao kila kukicha.

Bill Nas ameeleza hayo kupitia eNewz kutoka EATV baada ya yeye kuhusishwa katika suala la kimapenzi na msanii wa bongo fleva Nandy na kusema hilo jambo halina ukweli wowote hata watu wake wa karibu wanashangaa kusikia hilo jambo.

"Siyo kweli, sijawahi kuhusiana na msanii yoyote wa kike iwe wa bongo fleva au bongo 'movie'. Mtu wangu wa mwisho niliyekuwa naye alikuwa ameajiriwa katika kampuni binafsi. Mimi nipo 'single' hata watu wangu wa karibu wanaelewa hilo halafu hizo stoti mimi nazisikia kutoka kwa watu wa mbali ", alisema Bill Nas.

Pamoja na hayo, Bill Nas amesema kwa upande wake suala la mapenzi hawezi kulipa kipaumbele kama watu wengine wanavyofanya kwa madai linampoteza 'focus' katika vile alivyovipanga kuvitekeleza katika maisha yake

Toleo jipya la Samsung Galaxy Note 8 Yazinduliwa

$
0
0
 Toleo jipya la Samsung Galaxy Note 8 Yazinduliwa
Kampuni ya simu za mkononi ya Sumsung, imezindua simu yake mpya ya Galaxy Note 8, ambayo ni ya kisasa zaidi na yenye ushindaji zaidi katika soko.

Hatua hii inakuja baada ya kampuni hii kupata msukosuko wa kibiashara ikiwa ni takribani mwaka mmoja tangu ilipotoa simu aina ya Galaxy note 7 ambayo betri zake zilikuwa zinalipuka hivyo kulazimika kutolewa sokoni.

Kampuni hii ya Sumsung kutoka Korea kusini, katika toleo hili jipya la simu ya Galaxy note 8 imekuja na vitu vipya katika teknolojia ya usalama, ambapo ina uwezo kutambua muonekano wa mmiliki wa simu, alama za vidole, mboni ya jicho na mfumo mpya wa kiusalama ujulikanao kama Samsung Bixby ambayo inatoa sauti maalumu za maelekezo ya kuweka ulinzi wa siri wa simu hiyo ubora mpya wa picha.

Simu hii ya Note 8,imekuja na kioo chenye upana wa nchi 6.3 kutoka kona moja na nyingine,ongezeko la ukubwa wa nchi 0.1 ikilinganishwa toleo la S 8.

Hii Hapa Siri ya Senga ya Namna Anavyopiga Mkwanja

$
0
0
Hii Hapa Siri ya Senga Namna Anavyopiga Mkwanja
MCHEKESHAJI mkongwe, Ulimboka Mwakisikye ‘Senga’ amesema kwa sasa sanaa imekuwa ngumu hivyo kitu pekee kinachomuingizia pesa ni kufanya vichekesho vya majukwaani huko mikoani pamoja na kualikwa kwenye shughuli mbalimbali za kijamii hivyo kulipwa chochote kidogo ili kuyasongesha maisha.

Akipiga stori na mwandishi wetu hivi karibuni kupitia simu ya mkononi, Senga ambaye alidai yupo wilayani Kahama, Shinyanga kufanya shoo, alisema kuwa, imebidi kubadili maisha badala ya kusubiri tenda za filamu hivyo amekuwa akisafiri mikoa mbalimbali ambako kuna soko kubwa la sanaa ya uchekeshaji.

“Maisha yamebadilika sana, kama msanii ukitegema dili za filamu, utaua watoto kwa njaa, lazima utoke kuhangaika, mimi na mwenzangu, Pembe tunatumia fursa ya kwenda mikoani kufanya shoo za majukwaani na kupata mialiko ya sherehe mbalimbali za watu na kupewa pesa,” alisema Senga

Soma Nafasi za Kazi Zilizotangazwa Siku ya Leo

$
0
0

Kutana na Mtabibu Wanyota za Binadamu Duniani Kote Maalim Fadhili Rashidi Kutoka Comoro

$
0
0
KUTANA NA MTABIBU WANYOTA ZA BINADAMU DUNIANI KOTE MAALIM FADHILI RASHIDI KUTOKA COMORO




KWA SASA YUPO TANZANIA MAALIM FADHILI RASHIDI ANA UWEZO WAKUJUWA JAMBOLAKO KWAHARAKA NAKULITATUWA KWAMUDA MFUPI




MAALIM FADHILI RASHIDI ANAJUWA UMEHANGAIKASANA LAKINI HUJAFANIKIWA MUONE HARAKA AKUSAIDIE





MAALIM FADHILI RASHIDI NIBINGWA WAKUTIBU MARADHI SUGU KAMA VILE MIGUU KUUMA MIGU KUWAKA MOTO




KISUKARI VIDONDA VYATUMBO PUMU TEZI NA UVIMBE TUMBONI ANA UWEZO WAKURUDISHA MTU ALIE POTEA KIMAZINGIRA (MSUKURE)




KUMFANYA MKE MUME MPENZI ASIKUSALITI DAWA YA (LIMBWATA) KUMTAWALA MPENZI WAKO UNAVYOTAKA




KUMUONA MBAYA WAKO LIVE KWASABABU MAALUMU ANATOWA PETE YABAHATI INAYO ENDANA NA NYOTA YAKO




ITAKAYO KULETEA PESA BILA YA MASHARITI YEYOTE NAKUMILIKI MALI ZA MAJINI KWAYULE ANAE HITAJI




DAWA YAKUONGEZA UUME ZAIZI UIPENDAYO DAWA YANGUVU ZAKIUME PIA ANAYO DAWA YA KUONGEZA HIPSI SHEPU KUWA NA




UMBO BOMBA KAMA UMEIBIWA AMA KUDHURUMIWA UTARUDISHIWA MALIYAKO NDANI YASIKU (3) ANAFUNGA KESI NAKUPATA MALIYAKO KWA HARAKA




DAWA YA MVUTO WABISHARA KUUZA MALIYAKO KWA HARAKA KUZUIYA CHUMA ULETE KWENYE BIASHARA KUSAFISHA NYOTA




NAKUTOWA MIKOSI NAKUPANDISHWA CHEO KAZINI NJOO UONE MIUJIZA YA MAALIM FADHILI RASHIDI NJOO UFUNGULIWE VIFUNGO




ULIVYOFUNGWA ACHAKUTESEKA CALLING +255719362806/ +255763276239

KWA WHATSAPP IMO +255785786436/

TFF Yawaangukia Simba Ngao ya Jamii

$
0
0
TFF Yawaangukia Simba  Ngao ya Jamii
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), linaomba radhi wanafamilia wote wa mpira wa miguu kutokana na makosa ya maandishi yaliyoonekana kwenye utambulisho wa Ngao ya Jamii iliyotolewa Jumatano Agosti 23, 2017.

Ngao hiyo ilitolewa mara baada ya mchezo uliokutanisha timu za Simba SC na Yanga SC za Dar es Salaam kwenye Uwanja Mkuu wa Taifa jijini. Katika mchezo huo, Simba ilishinda kwa mikwaju ya penalti 5-4 dhidi ya Yanga na kutwaa Ngao hiyo.

Watanzania hususani wanafamilia ya mpira wa miguu popote pale, TFF hatujapokea vizuri mwonekana wenye makosa kwenye Ngao hiyo ya Jamii kama ambavyo wadau hawajapokea vema suala hili.

Kutokana na makosa hayo, Kaimu Katibu Mkuu wa TFF, tayari amechukua hatua za kinidhamu kwa watumishi waliohusika kadhalika kuwasiliana na uongozi wa Simba SC kuirejesha Ngao hiyo ili kufanyiwa marekebisho yatakayobaki kwenye kumbukumbu sahihi

Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema Akamatwa na Polisi

$
0
0
Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema Akamatwa na Polisi
JESHI la Polisi mkoani Arusha limemkamata Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema  kwa madai ya kuzidisha muda wakati akihutubia kwenye mkutano wake na wananchi jana Jumatano, Agosti 23, 2017 jijini humo.

Polisi wamedai kuwa Lema alimaliza mkutano wake saa 12:7 jioni badala ya saa 12:00 kama ilivyo utaratibu.
Hivyo askari polisi walimzuia katika mzunguko wa barabara wa Mnara wa Saa (round about) kwa kusimamisha gari mbili (moja mbele na nyingine nyuma), kisha kuingia katika gari yake na kumuelekeza Kituo Kikuu cha Polisi (Central Police) mjini Arusha.

Tanroads Yabanwa na Mahakama Bomoa Bomoa Nyumba Zilizoziwekewa Kinga

$
0
0
Tanroads Yabanwa na Mahakama Bomoa Bomoa Nyumba Zilizoziwekewa Kinga
Baada ya Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) kubomoa baadhi ya nyumba zilizowekewa kinga ya muda, Mahakama Kuu Divisheni ya Ardhi imesema hilo ni kosa la kuupuza amri ya mahakamana na kueleza hatua ambazo waathirika wanapaswa kuzichukua.

Akizungumza na Mwananchi jana, msajili wa mahakama hiyo, Frank Mahimbali alisema kuwa wanachoweza kufanya waathirika ni kwenda mahakamani kuomba iwaite waliohusika na ubomoaji huo ili wajieleze ni kwa nini wasifungwe kwa kupuuza amri ya mahakama.

Mahimbali alisema mtuhumiwa akitiwa hatiani anaweza kufungwa jela.

Ijumaa iliyopita, mahakama hiyo ilitoa amri ya zuio la muda la ubomoaji kwa nyumba 286 zilizoko katika operesheni ya bomoabomoa maeneo mbalimbali kati ya Ubungo Maji na Kiluvya, zilizojengwa ndani ya umbali wa mita 121.5 kutoka katikati ya Barabara ya Morogoro.

Amri hiyo ilitolewa na Jaji Leila Mgonya baada ya maombi ya dharura yaliyowasilishwa na wakazi 286 wa maeneo hayo, wakiomba mahakama itoe zuio nyumba zao zisibomolewa kusubiri kesi yao ya msingi itakapoamuriwa.

Hata hivyo, juzi Tanroads ilibomoa nyumba tatu katika eneo la Kimara Stop Over, ambazo ni kati ya hizo 286. Nyumba hizo zilizobomolewa ni pamoja na Nicomed Leo na ya Aisha Juma.

Wakati mahakama ikitoa msimamo na maelekezo hayo kwa waathirika wa bomoabomoa hiyo ambao nyumba zao zimewekewa kinga hiyo, wakili wao Benedicto Mandele alisema jana kuwa tayari wameshamwandikia barua Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), kueleza malalamiko yao na hatua wanazopanga kuzichukua.

Wakili Mandele alisema katika barua hiyo ambayo pia nakala yake imetumwa kwa Jaji Mgonya, Meneja wa Tanroads Mkoa wa Dar es Saalam, Ofisa Mtendaji wa Tanroads, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam na Kamanda wa Polisi Kinondoni, wateja wake wameeleza kusikitishwa kwao na kitendo hicho wakati kuna amri ambayo ilibandikwa kwenye nyumba hizo.

“Tayari barua hiyo imepokewa leo (jana) saa nne na sasa hapa ninaandaa maombi kwa ajili ya kumuita meneja wa mkoa wa Tanroads afike mahakamani kujieleza ni kwa nini asifungwe jela kama mfungwa wa kesi ya madai kwa kupuuza amri ya mahakama,” alisema Wakili Mandele na kuongeza kuwa maombi hayo dhidi ya meneja huyo wa Tanroads atapeleka mahakamani leo baada ya wateja wake kuweka saini.

Haya Ndiyo Mabadiriko Aliyoyafanya IGP Sirro kwa Makamanda wa Polisi Mikoani

$
0
0
Haya Ndiyo Mabadiriko Aliyoyafanya IGP Sirro kwa Makamanda wa Polisi Mikoani
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Nyakoro Sirro amefanya mabadiliko ya makamanda wa polisi mikoani.

Taarifa ambayo imetolewa na msemaji wa Jeshi la Polisi   Barnabas Mwakalukwa  imesema kwamba  Sirro amemteua Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Juma Yusuf Ally kuwa Kaimu Kamishna wa Polisi Zanzibar.

Uteuzi huo unafuatia kustaafu kwa aliyekuwa Kamishna wa Polisi Zanzibar Kamishna Hamdani Omari Makame kwa mujibu wa sheria baada ya kutimiza umri wa miaka sitini (60).

Kabla ya uteuzi huo DCP Juma alikuwa ni Mkuu wa Utawala na Fedha Makao Makuu ya Polisi Zanzibar.

IGP Sirro pia amemteua Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi  (SACP) Lazaro Mambosasa kuwa Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam.

Kabla ya uteuzi huo, SACP Mambosasa alikuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma.

Kufuatia uteuzi huo, aliyekuwa Kaimu Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam anakwenda kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, na aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi  (SACP) Neema Mwalimu Mwanga anakwenda Makao Makuu ya Polisi Dar es Salaam.

IGP Sirro pia amemteua aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Temeke Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Gilles Bilabaye Mroto kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma na  Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Emmanuel Lukula kwenda kuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Kipolisi Temeke.

Kabla ya uteuzi huo, ACP Lukula alikuwa Ofisa Mnadhimu wa Polisi mkoa wa Mbeya.

Jeshi la Polisi linatoa wito kwa wananchi wote kuendela kushirikiana na Jeshi hilo kwa kufichua taarifa za uhalifu na wahalifu ili kwa pamoja tuendelee kuiweka Tanzania salama.








Ushauri Alioutoa Ney wa Mitego Kwa Ali Kiba, Dimpoz Pamoja na Diamond

$
0
0
Ushauri Alioutoa  Ney wa Mitego Kwa Ali Kiba, Dimpoz Pamoja na Diamond
Wakati vita baridi ikiendelea kuunguruma huko mitandaoni kati ya wanamuziki Diamond, Ally Kiba na Ommy Dimpoz, rapa Nay wa Mitego ameibuka na kutoa neno lake la kukemea kuwahusisha wazazi katika mabifu yao.


Licha ya Nay kuwahi kuimba kwenye ngoma yake mstari unaosema, “nampenda demu wangu kuliko mama yangu”, lakini ameonekana kuguswa na kuchukizwa na kitendo cha Dimpoz, kumhusisha mama wa Diamond katika ugomvi wao.

“Gombaneni, roganeni mpaka muuane, napenda kusikia changamoto kwenye gemu, ila tusiwaingize wazazi wetu tafadhali, tukananeni matusi yote wenyewe kwa wenyewe ikibidi piganeni kabisa atakaye kufa tutazika na itakuwa historia kama Big na Pac.
nay wa mitego

“Ila kuwaingiza wazazi ni ujinga, sipo upande wowote si kwa Kiba, Dimpoz wala Diamond, endeleeni na vita yenu kama wanawake mmechukuliana mabwana, ila suala la wazazi mnavuka mipaka,” aliandika Nay wa Mitego katika akaunti yake kwenye mtandao wa Instagram.


Dayna Nyange:Sijawahi Kutoka Kimapenzi na Star Yoyote wa Bongo

$
0
0
Dayna Nyange:Sijawahi Kutoka Kimapenzi na Star Yoyote wa Bongo
Msanii wa Bongo Flava, Dayna Nyange amesema hajawahi kutoka kimapenzi na star yeyote Bongo na hataki kufanya hivyo.

Muimbaji huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake mpya ‘Chovya’, amesema sababu ya maamuzi yake ni kufanya mahusiano yake kuwa binafsi zaidi.

“No siyo star, sijawahi date na star na sitamani ku-date na star na sitaki ku-date na star na sito-date na star,” Dayna.

Pia msani huyo ameeleza kuwa yupo kwenye mahusiano lakini anapenda kuyafanya siri sana kiasi kwamba hata mama yake mzazi hajui.

“Naogopa atakasirika ataniacha kwa sababu nampenda, ni mtu ambaye ana wivu, nilishawahi kusema sina mahusiano akachukia nikaoni ok, isiwe shida nipo kwenye mahusiano lakini hayatambuliki kokote hata mama hamjui,” amesema Dayna

MWIGULU NCHEMBA: Atakaokiuka Sheria za Nchi na Kujiingiza Kwenye Ujambazi na Ujangiri Atafutiwa Uraia

$
0
0
MWIGULU NCHEMBA: Atakaokiuka Sheria za Nchi na Kujiingiza Kwenye Ujambazi na Ujangiri Atafutiwa Uraia
Serikali kupitia wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi imesema kuwa inaweza kuwafutia uraia watanzania wapya waliopewa uraia wale ambao walikuwa wakimbizi wanaoishi makazi ya katumba Mishamo na Ulyankulu iwapo wataonekana kushindwa kufuata sheria za nchi na kujihusisha na vitendo vya uharifu na uvunjifu wa sheria za nchi,vitendo vya ubaguzi wenyewe kwa wenyewe ubaguzi wa kitabaka kubaguana kisiasa, kidini na kwa namna yeyote hawawezi kuvumiliwa hata kidogo.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Mwigulu Nchemba wakati akiwahutubia raia hao wapya kwenye Makazi ya Katumba Halmashauri ya Nsimbo Wilayani Mpanda Mkoani Katavi wakati akiwataka kujiepusha na vitendo vya kubaguzi.

“Mimi najua uraia usiofutwa ni ule wa kuzaliwa mtu kama akishazaliwa kama ni Muafrika ata akiandikishwa kwingine anaendelea kuwa Muafrika. Lakini kama watu wanafanya vitu vya kinyama ambavyo hatujazoea na ubaguzi huo ndio uliosababisha matatizo kule hatuwezi tukaamisha matatizo kutoka kule tukayaishi tukiwa huku kama ugomvi kule ulizuka na watu wakakimbia yaliyogombana hayakuwa mabonde nama milima yalikuwa ni hao hao watu,” alisema Mwigulu.

“Kwahiyo ukianzisha ubonde na ummlima ukauhamishia hapa unaleta ugomvi ambao sisi hatuuzoea kwa maana hiyo leo naongea kindugu kwa maana hiyo muonyane wenyewe kwa wenyewe ambiazaneni na mkimuona mtu yupo wa aina hiyo kwani nyinyi hamna wazee wambie hilo lina gaharama hapa sio mahali pakee na kwa bahati nzuri kamati ya ulinzi na usalama ipo hapa mtakapo muona mtu anafanya kaubaguzi wataweka mapendekezo na hamtajua ni saa ngapi wameweka kwahiyo kama mnapendana shaurianeni mapema sana hatutaki kusikia lugha za huyu anakaa juu anakaa bondeni hayatusaidii sisi hapa kwa yoyote atakae thibitika ni jangili,jambazi nitafuta uraia wake hatutampa muda wa kuchomoa chaji kwenye soketi tuamuondoa.”

Wakili wa Tundu Lisu Aiomba Mahakama Kumfikishwa Lisu Mahakamani

$
0
0
Wakili wa Tundu Lisu Aiomba Mahakama Kumfikishwa Lisu Mahakamani na Polisi
Wakili wa Tundu Lissu, Peter Kibatala ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa wanauomba upande wa Serikali, ufikishe ujumbe kwa Jeshi la Polisi ili wamfikishe Lissu Mahakamani hapo.

Kibatala ameyasema mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Godfrey Mwambapa baada ya Wakili wa Serikali, Mutalemwa Kishenyi kusema mshtakiwa hayupo anashikiliwa na Jeshi la Polisi, hivyo anaomba kesi hiyo iahirishwe hadi Jumatatu August 28, 2017.

Baada ya kueleza hayo, wakili Kibatala akamuomba Kishenyi afikishe ujumbe kwa Polisi kwamba Lissu afikishwe Mahakamani ambapo kesi iliahirishwa hadi August 28, 2017

Hii Hapa Taarifa ya Mganga Mkuu Morogoro Kufuatia Ajari ya Tren na Coaster

$
0
0
Hii Hapa Taarifa ya Mganga Mkuu Morogoro Kufuatia Ajari ya Tren na Coaster
IKIWA imepita takribani miezi mitatu tangu wanafunzi wa Shule ya Lucky Vincent ya Mkoani Arusha wapate ajali na watu 35 kupoteza maisha, leo majira ya saa moja asubuhi, treni ya abiria iliyokuwa ikitokea Bara imegongwa na basi la abiria aina ya Coaster lenye namba za usajili T 438 ABR katika eneo la TANESCO, mjini Morogoro.

Coaster hiyo inayofanya safari zake kati ya Morogoro mjini na Kihonda ilikuwa imebeba wanafunzi wa shule tofauti wakielekea shuleni, mmoja wao anadaiwa kupoteza maisha huku wengi wao wakijeruhiwa kutokana na ajali hiyo tofauti na taarifa zilizosambaa mwanzo kuwa watu watatu walikuwa wamefariki.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini humo, Mganga Mkuu wa Hospital ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro, Dkt. Frank Jacob amesema leo asubuhi amepokea maiti ya mwanafunzi mmoja na majeruhi kadhaa ambapo wawili kati yao hali zao ni mbaya.

Baada ya kutokea kwa ajali hiyo mwandishi wetu alifika haraka eneo la tukio na kukuta umati mkubwa wakimshushia kichapo dereva wa daladala hiyo ambaye jina lake halikupatikana mara moja wakati akitaka kukimbia baada ya tukio hilo.

Umati wa wananchi wa Morogoro umejazana nje ya hospital hiyo kwa lengo la kuwashuhudia majeruhi hao, pia uongozi wa Mkoa wa Morogoro upo hospitalini hapo.

Madee Ampa Makavu ROMA Kuhusu Kuchunguza na Kutumia Simu ya Mkewe

$
0
0
Madee Ampa Makavu ROMA Kuhusu Kuchunguza na Kutumia Simu ya Mkewe
Rais wa Manzese, Madee amefunguka kwa kumchana rapa Roma Mkatoliki aache tabia yake ya kupenda kuichunguza simu ya mke wake na kuitumia kila mara kwani ipo siku yatakuja kumkuta makubwa asipoangalia.

Madee amebainisha hayo baada ya msanii Roma kudai hamiliki simu ya kiganjani tokea alipopatwa na matatizo ya kutekwa na watu hivyo sasa anatumia simu ya mke wake Nancy kwa kufanya mawasiliano mbalimbali.

"Watu wa kitanga si unajua jinsi walivyo tabia zao za kupenda kukaa na simu za wake zao muda wote, kuangalia angalia mwisho wa siku unaweza ukakuta kitu mule ukanza kuzua ugomvi kwa hiyo Roma acha kutumia simu ya mke wako mshkaji wangu", alisema Madee.
Pamoja na hayo, Madee aliendelea kufunguka kwa kubainisha baadhi ya mambo baina yake na familia ya Roma Mkatoliki na kusema amekuwa mtu wao wa karibu sana japo watu wa nje hawafahamu hilo.

"Watu wanatakiwa watambue sisi ni wanamuziki pia watu wa kawaida, Roma pamoja na familia yake yote ni watu ambao tunataniana muda wowote na sehemu yoyote ile. Sasa watu wa nje ndiyo wanakuwa hawajui halafu wanaanza ku-panic", alisisitiza Madee.

Kwa upande mwingine, Madee amesema anajivunia kuwa msanii wa kwanza Tanzania kutengeneza video ya wimbo kwa 'style ya animation' huku akijitapa kuwa hata watu wakiiponda lakini yeye ndiyo ameshaweza kuweka historia aliyokuwa anaitaka kwa kipindi kirefu.
Viewing all 104789 articles
Browse latest View live




Latest Images