Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104799 articles
Browse latest View live

Sababu za Wanawake Wengi Kutokuwa na Hamu ya Kufanya Mapenzi.....Wengi Huficha Hili

$
0
0
KUKOSA hamu ya ngono ni tatizo ambalo wengi huona aibu kulizungumzia ingawa ni kitu kinachowanyima raha wanawake wengi. Inakadiliwa kuwa asilimia 40 ya wanawake hupatwa na tatizo hili katika maisha yao, hata hivyo tatizo hili huwapata zaidi wanawake wenye umri kati ya miaka 45 na 65.

Wataalamu wengi wa afya huwaambia wanawake wenye tatizo hili kuwa wana matatizo ya homoni. Kuwa na homoni za kutosha katika mwili ni muhimu kwa tendo la ndoa. Homoni iitwayo istrojeni huhamasisha damu kwenda kwenye uke na kusaidia kulainisha uke wakati homoni iitwayo testosteroni huchochea hamu ya ngono. Hata hivyo, hamu ya ngono kwa wanawake ni kitu chenye utata mwingi kwa maana msongo wa mawazo, mkazo, afya yake na uhusiano aliopo huchangia kuwa na hamu au kutokuwa na hamu ya tendo la ndoa.

Wanawake wengi mwanzo wanakuwa wanafanya ngono mara tano kwa wiki na baadae hamu hupotea na kuanza kufanya ngono mara moja kwa mwezi tena kwa kujilazimisha. Tatizo hili linaweza kuanza kwa mwanamke kukosa msisimko (raha ya tendo), kutofikia kileleni au kufika kileleni na kushindwa kuendelea na tendo la ndoa baada ya mzunguko mmoja.

Wanawake walio katika hatari ya kupata tatizo hili

Wanawake ambao waliwahi kupatwa na tatizo la kupungua hamu ya kujamiiana hapo mwanzo wanaweza kupatwa na tatizo hili kwa mara ya pili. Wale ambao wamefanyiwa upasuaji wa kuondoa mayai yao ya uzazi kutokana na sababu mbalimbali kama magonjwa au uzazi wa mpango. Wanawake ambao waliofika umri wa kukoma hedhi mara nyingi huanzia kati ya miaka 45 na 55 ingawa kuna wachache huanza kabla ya umri huo.

Matatizo ya homoni si chanzo pekee cha kukosa hamu ya ngono. Sababu zingine ni pamoja na:

Mzunguko mbovu au kukosa kabisa hedhi

Ikiwa mwanamke ana mzunguko wa kati ya siku 24 hadi 34 ni dalili kuwa ovari na homoni zake zinafanya kazi vizuri. Mzunguko mbovu wa hedhi au kutopata kabisa hedhi huwa ni ishara kuwa homoni za mwanake haziko vizuri. Kukosa hedhi kwa zaidi ya miezi sita ni ishara kwamba hakuna uwiano mzuri wa homoni ya istrojeni. Tatizo hili linaweza kuathiri tendo la ndoa hivyo ni vyema kumuona daktari kwa msaada zaidi.

Kukoma hedhi (Menopause)

Baada ya hedhi kukoma, ovari za mwanamke huacha kutengeneza homoni, hivyo kiasi cha homoni ya istrojeni na istrojeni hupungua na wakati mwingine huisha kabisa. Wanawake wengi katika kipindi hiki hupatwa na shida ya uke kukauka (kukosa ute wa kutosha) na kupungua hamu ya tendo la ndoa. Kupungua kwa homoni ya istrojeni husababisha nyama ya uke kuwa nyembamba na kukauka hivyo kusababisha maumivu wakati wa tendo la ndoa.

Ikiwa tendo la ndoa litasababisha maumivu kwa mwanamke hatataka kufanya tendo hilo mara kwa mara na jinsi anavyofanya mara chache ndivyo tatizo linavyozidi kukua. Wakati mwingine tatizo la uke kukauka linaweza kutatuliwa kwa kupaka mafuta ya kulainisha uke au mafuta ya nazi. Matumizi ya virutubishi vya homoni ya testosterone yanaweza kusaidia na kuongeza hamu ya tendo la ndoa kwa wanawake waliokaribia kukoma hedhi na wale waliokoma, ingawa virutubisho hivi huweza kusababisha chunusi, kuota nywele mwilini na huongeza kiwango cha lehemu (cholesterol) kitu ambacho kinaweza kusababisha matatizo ya moyo.

Matatizo ya kihisia

Kuwa na wasiwasi, msongo wa mawazo na mikazo katika maisha ambayo huchangiwa na matatizo ya uchumi, matatizo katika uhusiano kama ugomvi, kutoelewana, kutoaminiana huathiri mwili na kufanya homoni muhimu kwa ajili ya tendo la ndoa kutotengenezwa kwa kiwango cha kutosha. Pia mzunguko wa damu katika tupu ya mwanamke hupungua na hivyo kusababisha maumivu wakati wa kujamiiana. Historia ya kubakwa au kupata maumivu wakati wa kujamiiana hapo awali kutokana na mwanamke kutokuwa tayari au kutotayarishwa vyema husababisha uke kuwa mdogo kuruhusu uume kupita, tatizo ambalo kitaalamu huitwa vaginismus.

Matumizi ya vilevi

Matumizi ya dawa za kulevya na unywaji pombe kupita kiasi hupunguza hamu ya tendo la ndoa, ingawa kuna baadhi ya watu huamini kuwa unywaji pombe kali huongeza hamu ya kujamiiana au kupunguza uzito. Pombe kali au kilevi cha aina yoyote vikitumiwa kupita kiasi hupunguza hamu ya kujamiiana na pombe huongeza uzito na kusababisha utapiamlo hasa kitambi.

Maradhi

Magonjwa kama kisukari, magonjwa ya mifupa (arthritis), magonjwa ya moyo, saratani ya aina yoyote ile, matatizo ya kupungua kwa homoni ya tezi la koo (hypothyroidism) ambayo hutokea zaidi kwa wanawake kuliko wanaume husababisha kupungua hamu ya tendo la ndoa.

Vilevile madhara ya dawa mbalimbali kama za kushusha shinikizo la damu na za saratani.

Ujauzito, kujifungua na kunyonyesha

Mwanamke anaweza kukosa hamu ya tendo la ndoa kutokana na mabadiliko katika mfumo wa homoni au vichocheo wakati wa ujauzito. Pia kutokana na mabadiliko ya maumbile ya wanawake wakati huo na kufanya mwanamke kutojiamini kufanya tendo la ndoa.

Mwanamke akijifungua na kuanza kunyonyesha homoni ya prolactin huwa katika kiwango cha juu. Homoni hii hufanya kazi ya kumfanya mtu kuridhika baada ya ngono/tendo la ndoa, hushirikiana na homoni/kichocheo nyingine iitwayo dopamine inayofanya mtu kufikia kilele wakati wa tendo la ndoa. Hata hivyo, homoni ya prolactin inaweza kuongezeka wakati mtu akiwa kwenye usingizi mzito hasa wakati wa alfajiri, baada ya kufanya mazoezi, kula, baada ya tendo la kujamiana, baada ya upasuaji mdogo na hata baada ya kupata degedege. Sababu zingine za kuongezeka kiwango cha homoni hii ni kuwa na saratani ya ubongo.

Vidonge vya uzazi wa mpango

Vidonge vingi vya uzazi wa mpango hugandisha homoni ya testosteroni kwenye mwili na huweza kusababisha kupungua kwa hamu ya ngono kwa baadhi ya wanawake. Ikiwa una hofu juu ya njia ya uzazi ya mpango yenye homoni ni vyema kuzungumza na daktari juu ya njia nyingine isiyokuwa na homoni. Usiache tu kutumia vidonge vya uzazi wa mpango kwa kuhisi ndio sababu ya wewe kutopata hamu ya tendo la ndoa bila kuzungumza na mtaalamu wa afya.

Mambo Mengine

Uharibifu wa neva inayohusika na kuongeza msisimko wakati wa kujamiana (pudendal nerve) wakati wa upasuaji wa kuondoa mfuko wa uzazi kwa mwanamke mwenye matatizo ya uzazi au katika mfuko wa kizazi. Uchovu mwingi baada ya majukumu ya kulea mtoto/watoto, kazi na kumhudumia mume wake. Matumizi ya vifaa vya kieletroniki kupita kiasi hasa uraibu wa mitandao ya kijamii kama Facebook & Instagram.

Kupenda kuchat au kutumia intaneti kupita kiasi na hivyo kusababisha msisimko kupotea kati ya wenza wawili mwishowe kupungua uwezo au hamu ya kujamiiana.

Ikiwa unapata hedhi katika mpangilio mzuri, husikii maumivu ukifanya tendo la ndoa na hautumii njia yoyote ya uzazi wa mpango yenye homoni basi tatizo lako la kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa linaweza lisiwe tatizo la homoni moja kwa moja. Ni vyema kumuona daktari kwa msaada zaidi.

Dayna Nyange: Bado Sijakabiziwa Tuzo Zangu MbIli za BEA Awards 2017

$
0
0
Dayna Nyange: Bado Sijakabiziwa Tuzo Zangu MbIli za BEA Awards 2017
Msanii wa Bongo Flava, Dayna Nyange amefunguka kutokabidhiwa tuzo zake mbili alizoshinda katika BEA Awards, 2017 ambazo hutolewa nchini Nigeria.

Muimbaji huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma ‘Chovya’, amesema alishafanya mchakato wa kupata tuzo hizo kipindi cha nyuma lakini hakufanikiwa na kuna kazi zimekuja kumtinga, hivyo kusitisha kufanya hivyo lakini ni kitu ambacho anatamani kukipata.

“Sijapatiwa hadi leo process zao za kutuma sijajua zimekuwaje, imekuwa na uzito wa ugumu nimejaribu kuongea nao mara kwa mara wakaniambia kuna mtu alikuwa atume halafu ikatokea dharura akawa amesafiri akawa amechelewa kurudi na mimi nikawa bize, kwa nikajikuta kila ikitakiwa hivi kuna kuwa na kona kona nyingi au niseme ni mitihani imekuwa mingi japo bado nawasiliana nao, kwa hiyo hazijanifiki,” ameiambia Bongo5.

“Ni kitu ambacho nakitamani kwa sababu ni tuzo zangu za kwanza kupata nje ya Tanzania. Ninaamini tuzo za BEA zimeniongezea kitu kkunikuza na hata kuwepo tena kwenye Afrimma inanifanya nisishtuke,” amesema Dayna.

April 5 mwaka huu Dayna alitangazwa na BEA kushinda katika kipengele cha Best African Artist pamoja na Best Vocal Performance Female.

SOMA Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo Jumanne Kutoka Kwenye Makampuni Mbali Mbali

$
0
0

Mnaomshambulia Tundu Lissu Mkapimwe Akili...Vitendo vya Kishenzi Anavyovipinga Vinatia Taifa Letu Doa

$
0
0
Mnaomshambulia Tundu Lissu Mkapimwe Akili...Vitendo vya Kishenzi Anavyovipinga Vinatia Taifa Letu Doa

Ndugu zangu amani iwe nanyi, nasema kwa uwazi mnaomshambulia na kumkejeli Tundu Lissu hamjitambui inawapasa mujitathimini.

Nasema haya kwa sababu tamko la kutaka mawakili wagome halijatolewa na lisu limetolewa na baraza la uongozi TLS.

Pia nawaasa msilijukulie swala hili kisiasa kwani sio la kisiasa,.nilitegemea watanzania kwa umoja wetu tulaani tukio hilo la kigaidi la kuteka walinzi na kulipua ofisi za mawakili.

Naomba niwakumbushe historia japo kidogo, kwa miaka yote tangu uhuru TLS imekuwa ikiongozwa na makada wa CCM na kiukweli ilipoteza mwelekeo na kuwa tawi la CCM.

Katika kipindi chote hicho ili uwe rais wa TLS ilikuwa lazima uwe kada wa CCM. Hata katika uchaguzi uliomweka Lissu kuwa mwenyekiti wa TLS uligubikwa na nizengwe mingi ikiwemo kuingiliwa na serikali.

 Niwakumbushe pia katika uchaguzi wa TLS tulishuhudia kila mizengwe ya kumkwamisha Lisu asogombee Urais ikiwemo kukamatwa airport na kuwekwa ndani mpaka mahakama ilipoamuru apewe dhamani cku ili ili ya uchaguzi.

Nawashauri ndugu zangu tuache siasa za kijinga kwenye masuala yanayogusa maisha ya binadamu, maana wale walinzi wanafamilia zao wangeweza hata kuuwawa nani anajali?

Tumeshuhudia watu wakipotezwa, maiti zikiokotwa kwenye viroba zikielea mtoni, leo ofisi za mawakili zinalipuliwa nani anajua kesho kutatokea nn au zamu ya nani?

Tuache ushabiki wa kisiasa kwa pamoja tulaani vitendo hivi vya kishenzi vinavyolitia doa taifa letu Tanzania mbele ya uso wa dunia.

Mungu ibariki Afrika.
Imeandikwa na Kimpawwe/JF

Hospitali ya Kairuki Yakanusha Tuhuma za Mgonjwa Kuachwa na Vifaa Tumboni Wakati wa Upasuaji

$
0
0
Hospitali ya Kairuki Yakanusha Tuhuma za Mgonjwa Kuachwa na Vifaa Tumboni Wakati wa Upasuaji

TAARIFA KWA UMMA KUKANUSHA TUHUMA ZA MGONJWA KUACHWA NA VIFAA VYA KUZALISHIA UKENI​

Uongozi wa Kairuki Hospital umepokea na kusoma kwa masikitiko taarifa zilizoandikwa na magazeti ya tarehe 28/8/2017 pamoja na kusambazwa kwenye rnitandao mbalimbali ya kijamii kuwa hospitali yetu imemsababishia mgonjwa madhara ya kizazi kwa kurnuacha na vifaa vya kuzalishia ukeni.

Magazeti yaliyotufikia yakiwa na tuhuma hizo ni pamoja na gazeti la Uhuru toleo na. 22847, Mtanzania toleo Na. 8651 pamoja na Daily News lenye toleo Na. 12021 yote yakiwa ya tarehe tajwa hapo juu.

UKWELI KUHUSU MGONJWA ANAYETAJWA
Hospitali inakiri kuwa iliwahi kumhudumia mama mjamzito aitwaye Khairat Shaib Omary mkazi wa Mbezi Beach Dar es Salaam mnamo mwaka 2016. Mama huyo alihudumiwa kwa muda wa ujauzito wake kwa nyakati tofauti alizofika hospitalini kwetu. Pia alihudumiwa kwa kupewa huduma za kujifungua ambapo tarehe 15/12/2016 alijifungua kwa njia ya upasuaji baada ya njia za kawaida kushindikana kwa sababu zisizozuilika kitabibu. Mnamo tarehe 17/12/2016 mama huyo na mtoto wake waliruhusiwa kwenda nyumbani baada ya madaktari wetu kuridhika kuwa afya ya mama na mtoto zilikuwa salama na wakiendelea vizuri.

Mama huyo alirejea tena hospitalini kwetu tarehe 21/12/2016 kwa ukaguzi wa kawaida baada ya kujifungua ambapo daktari aliyemhudumia aliridhika kuwa afya ya mama huyo ilikuwa salama na hakuwa na tatizo lolote kwani hata kidonda cha mshono wake kilikuwa kikiendelea kupona vizuri. Mama huyo hakurejea tena hospitalini hapo kwa matibabu wala huduma zaidi ya hapo mpaka leo.

TUHUMA KUHUSU KUACHWA NA VIFAA VYA KUZALISHIA UKENI
Kwa mara ya kwanza, tuhuma kuhusu mgonjwa aitwaye Khairat Shaib Omary, ziliwasilishwa kwetu mnamo tarehe 10/7/2017 kufuatia barua ya wakili wake aitwaye Jonas Estomih Nkya wa kampuni ya Jonas & Associates Law Chambers ambaye alitutaka tumlipe mteja wake Milioni mia Sita (Tshs.600,000,000/=) pamoja na riba ya asilimia ishirini na moja (21%). Hospitali yetu ilikanusha

kuhusika na tuhuma na madai ya Bi. Khairat Shaib Omary ambaye aliamua kufikisha madai yake katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Dar es Salaam, Kisutu katika kesi Namba 184 ya mwaka 2017 akidai fidia mbalimbali.

Wakati kesi hiyo ikiwa tayari imepangiwa Hakimu wa kuisikiliza pamoja na tarehe ya kuitaja mahakamani, mgonjwa huyo ameendelea kutumia vyombo vya habari kutuchafua kwa nia ambayo sisi tunaamini ni kutaka kushinikiza hukumu yenye upendeleo kutoka mahakamani, kitendo ambacho hakikubaliki kamwe.

Hospitali yetu inapenda Umma ufahamu kuwa baada ya tarehe 21/12/2016, Bi Khairat Shaib Omary, anakiri katika hati zake za madai, kuwa alihudumiwa katika hospital nyingine tofauti kama vile Tanzania Occupational Health Services, Regency Hospital na Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa nyakati tofauti. Hata hivyo, hakuwahi kutaarifu hospitali yetu kuhusu huduma alizopewa kwenye hospitali hizo.

Hospitali inakanusha tuhuma zilizoandikwa na magazeti tajwa hapo juu kwa kuwa hazina ukweli wowote. Endapo mgonjwa anayetajwa na magazeti anayo madai ya msingi dhidi ya Kairuki Hospital, alitakiwa kusubiri taratibu za Mahakama alizokwishazianzisha iii alete ushahidi na kuthibitisha tuhuma zake.

Kairuki Hospital tunasikitika kuona vyombo vya habari tajwa hapo juu vikiandika habari za kututuhumu bila kutuhoji wala kutupatia fursa ya kueleza nafasi yetu na nini kilifanyika kuhusu mgonjwa huyo. Kitendo hicho ni ukiukwaji wa haki zetu za msingi pamoja na maadili ya wanahabari.

Kairuki Hospital tunataka Umma, wateja wetu, wadau na wafanyakazi wote kuwa wazipuuze tuhuma zinazoendelea kuandikwa kwenye magazeti na mitandao ya kijamii kuhusu kuacha vifaa vya kuzalishia kwenye uke wa mgonjwa kwani hazina ukweli. Aidha, tunasikitika kwa usumbufu ambao umeshajitokeza kufuatia taarifa hizo.

Kwa sasa, Kairuki Hospital ipo katika mchakato wa kuchukua hatua za kisheria kuhakikisha haki inatendeka kwa upande wetu na kukomesha vitendo vya wanahabari kutuhumu bila kupata maoni na taarifa sahihi za upande wa pili.

Imetolewa leo tarehe 28/8/2017.

Arafa Juba

Afisa Habari

KAIRUKI HOSPITAL

Download App ya UDAKU SPECIAL Kwenye Simu Yako Kupata Habari zetu Kwa Urahisi..Bonyeza Hapa

$
0
0
Download  Application ya Udaku Special Blog Kwenye Simu yako Kutoka Play Store Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi

Bonyeza Hapa CLICK HERE 


Au Kama Unayotayari Bonyeza HAPA Ku Update Uweze Kupata Ikiwa na Muonekano Mpya

BREAKING NEWS: Tundu Lisu na LHRC Waungana Kupinga Kuvamiwa na Kulipuliwa Ofisi ya Mawakili

$
0
0
BREAKING NEWS: Tundu Lisu na LHRC Waungana Kupinga Kuvamiwa na Kulipuliwa Ofisi ya Mawakili
Mbunge wa Singida Mashariki ambaye pia ni Mwanasheria wa CHADEMA na Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika, TLS, Tundu Lissu na Kituo cha Haki za Binadamu wameungana kwa pamoja katika kupinga kitendo cha kuvamiwa na kulipuliwa Ofisi za IMMMA Advocates.

Katika mkutano wa pamoja wamesema lengo ni kuonesha namna gani Sheria inatakiwa kuthaminiwa na kitendo kilichofanywa kinatakiwa kukemewa kwa nguvu zote

Simba Waitupia Lawama TFF kwa Kubadirisha Ratiba ya Ligi Kuu

$
0
0
Simba Waitupia Lawama TFF  kwa Kubadirisha Ratiba ya Ligi Kuu
Afisa habari wa klabu ya Simba, Haji Manara amefunguka kwa kuwatupia lawama Bodi ya Ligi (TPLB) ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kuwa wanachokifanya siyo sawa wanabidi wabadilike.

Manara ameeleza hayo baada ya Bodi hiyo kufanya mabadiliko ya ratiba za mechi zinazoshiriki katika Ligi Kuu ili kupisha mechi ya kirafiki baina ya Tanzania na Botswana iweze kuchezwa mnamo Septemba 2 mwishoni mwa juma hili.
"Nimesikitika sana kuona kwamba ratiba ya Ligi Kuu imebadilishwa, mechi hizi zipo kwenye kalenda ya FIFA. Mnapanga ratiba mechi ya pili tu mnaanza kubadilisha ratiba kwa hiyo sisi mechi yetu na Azam FC haitakuwepo ?", alisema Manara

Pamoja na hayo, Manara ameendelea kwa kusema "mnatupunguza ile nguvu tuliyoanza nayo, hili jambo nilishalisema sana kwa nini mnavyopanga ratiba zenu bodi ya Ligi msiwe mnaangalia kalenda ya FIFA. Hivi mshawahi kusikia wapi duniani mtu anabadilisha ratiba la ligi katika mechi ya pili ? hii ni 'only' Tanzania, ingekuwa ya tisa au ya 10 hapo sawa lakini ya pili.
Kwa mengine mengi msikilize hapa chini Haji Manara akifunguka kuhusiana na kubadilishwa ratiba ya michuano na Bodi ya Ligi.


Diamond Atupa Dongo kwa Watu Waliochoshwa na Nyota Yake

$
0
0
Diamond Atupa Dongo kwa Watu Waliochoshwa na Nguvu ya Nyota Yake
Staa wa Bongo Fleva Diamond Platnumz amezungumzia nguvu ya NYOTA yake na jinsi watu flani wakubwa wanavyochoshwa nayo.

Kupitia IG yake Diamond ametoa gongo Hili “Ka diamondi kenyewe basi, kadogodogooo tokea Tandale… sema kanavyo washuhurisha watu na Midevu yao😃😃… Hii nyota yangu sjui itakuwa jina lake linaitwaje…..😃 #ZILIPENDWA“

Kwa sasa Diamond na kundi lake la Wasafi wana HIT na rekodi yao mpya Zilipendwa amabyo InTrend Nchini Kenya ikiwa imetazamwa na watu zaidi ya Milioni 1 na laki mbili.






Duka La Jux Lakumbwa na Bomoa Bomoa Mwenyewe Afunguka Haya

$
0
0
Duka La Jux Lakumbwa na Bomoa Bomoa Mwenyewe Afunguka Haya
Msanii Jux ambaye ni mmiliki wa duka linalo uza nguo za 'brand' yake ya 'African Boy', ametoa sababu iliyofanywa duka hilo lipitiwe na bomoa bomoa, katika eneo la Sinza jijini Dar es salaam.

Akizungumza na mwandishi wa East Africa Television, Jux amesema duka hilo limevunjwa kwa sababu mwenye nyumba alikuwa na mgogoro na Mahakama kuhusu kiwanja hicho ndipo Mahakama ilipoamuru nyumba hiyo ivunjwe japo hawakupewa taarifa ya aina yoyote na mwenye nyumba huyo.

Nimepata hasara kubwa kwa kuvunjwa kwa jengo hilo kwa kuwa kuna baadhi ya vitu vimepotea pamoja na pesa taslimu shilingi Milioni moja imeibiwa na mpaka sasa, baba mwenye nyumba wangu hapatikani na sijui yupo wapi ?", alisema

Mwigulu Nchemba Atoa Agizo kwa Idara ya Magereza Kutaka Wafungwa Kupatiwa Kazi Magerezani

$
0
0
Mwigulu Nchemba Atoa Agizo kwa Idara ya Magereza Kutaka Wafungwa Kupatiwa Kazi Magerezani
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba ameliagiza jeshi la Magereza na idara zingine zenye mashirika ya uzalishaji ambazo zipo chini ya wizara yake zifanye uzalishaji mali pamoja na kuwatumia wafungwa katika kufanya kazi ndani ya jeshi.

 Waziri Nchemba ameongea hayo akiwa katika ufunguzi wa nyumba tano za maaskari wa jeshi la magereza mkoa wa Arusha nyumba zilizojengwa kwa kutumia fedha za shirika la magereza la uzalishaji mkoani humo.

Mh. Nchemba ametoa rai kwa jeshi hilo kuona kama inawezekana jeshi hilo kutumia wafungwa ambao wamemaliza mafunzo yao na wakaona wamerekebika kitabia na kuwachukua waendelee kufanya kazi kwa mkataba katika mashirika hayo kwani itarahisisha kupunguza wahalifu zaidi kuliko kwenda uraiani wakiwa hawana uwezo wakufungua biashara na kurudia makosa.

Naye mkuu wa Magereza Tanzania Dr Juma Malewa amewataka wananchi na mashirika ya umma na serikali kutumia jeshi la Magereza nchini katika shughuli za ujenzi kwani gharama zake ni nafuu sana lakini zenye ubora zaidi.

Kwa upande wa Mkuu wa Jeshi la Magereza mkoa wa Arusha, Hamis Nkabasi amesema nyumba hizo zimetumia gharama ndogo za ujenzi kwasababu rasilimali watu wametumia askari wenye ujuzi wa ujenzi na wafungwa ambapo imegharimu milioni 50 kila nyumba na itaweza kuchukua askari 12 ambapo zote zitachukua askari 60 na kama wangechukua kampuni kujenga basi ingegharimu fedha nyingi zaidi.

Israel: Iran Inajenga Kiwanda cha Makombora Syria

$
0
0
Israel: Iran Inajenga Kiwanda cha Makombora Syria
Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema kuwa Iran inajenga viwanda nchini Syria na Lebanon ili kutengeza makombora.

Benjamin Netanyahu ameishutumu Iran kwa kuifanya Syria kuwa kambi yake kutengeza vifaa vya kijeshi kama mpango wake wa kutaka kuiangamiza Israel.
Majeshi ya Iran yanamsaidia rais Bashar al Assad katika vita vya Syria huku ikiliunga mkono kundi la wapiganaji wa Lebanon Hezbollah.

Matamshi ya Netanyahu yanajiri baada ya kufanya mazungumzo na katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Gutierrez mjini Jerusalem
Bwana Guterres amefanya ziara yake ya kwanza katika enewo hilo tangu kuchukua mamlaka mnamo mwezi januari.

Bwana Netanyahu hakutoa maelezo kuhusu viwanda hivyo vya Iran lakini akaonya kwamba hicho ''ni kitendo ambacho Israel haitakubali''.
Wiki mbili zilizopita, kampuni ya Israel Imgesat ilichapisha picha ilizosema zinathibitisha ripoti ya gazeti moja la upinzani nchini Syria kwamba kiwanda cha makombora kilikuwa kikijengwa kaskazini magharibi mwa Syria chini ya uangalizi wa Iran.

Halima Mdee Alia na Polisi Kushindwa Kuwakamata Matapeli Wanaotumia Jina Lake

$
0
0
Halima Mdee Alia na Polisi Kushindwa Kuwakamata Matapeli Wanaotumia Jina Lake
Mbunge wa Kawe kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Halima Mdee amefunguka na kusikitishwa na jeshi la polisi kushindwa kuwakamata matapeli ambao wamekuwa wakitapeli wananchi kwenye mitandao kupitia jina lake.

Halima Mdee amesema kuwa ni muda mrefu alishatoa taarifa kwenye jeshi la polisi kuhusu watu hao wanaotumia jina lake kwenye mitandao ya kijamii na kujifanya kutoa mikopo yenye riba ndogo na kuwatapeli wananchi pesa zao.
"Wanaojitambulisha kutoa mkopo kwa jina langu ni matapeli, sihusiki nao !Nimetoa taarifa polisi inaonekana hawakamatiki" alisema Halima Mdee

Aidha watu hawa wanaojitambulisha kama Halima Mdee wanatumia mpaka jina la Waziri Mkuu Kassim Majaliwa katika kufanya utapeli huu na kuwaumiza wananchi wa chini ambao wanashida na kutaka kujikwamua kimaisha kupitia mikopo hiyo na badala yake wanakwenda kuongeza matatizo kwani hata kidogo walichokuwa nacho pia hutapeliwa.

Mbali na Halima Mdee jina lake kutumika katika utapeli huu lakini pia viongozi wengine mbalimbali na watu maarufu wamekuwa wakitumiwa na watu hawa katika kuendelea kufanya utapeli huu, mfano jina la Waziri Mkuu Kassim Majaliwa. Lakini pia Mbunge wa Kigoma Mjini Mhe. Zitto Kabwe ameshawahi kulalamika juu ya utapeli huu unaofanya na watu hawa mitandaoni.

Video: Lisu Waungana na Mawakili Kugoma Kufanya Kazi Baada ya Ofisi ya Mawakili Kulipuliwa

$
0
0
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu nchini (LHRC) chaungana na wanachama wa TLS kulaani tukio la ofisi za IMMMA Advocates kupigwa bomu.

Kwamujibu wa Mkurugenzi wa Kituo hicho Hellen Kijjo Bisimba amesema hatua hiyo inaashira kuonesha kutoridhishwa na kitendo hicho na kwamba vyombo vya dola vinatakiwa kufanya uchunguzi wake kwa haraka na kutoa majibu yaliyosahihi.

Hata hivyo Rais wa TLS kwaniaba ya mawakili wenzie Tundu Lissu ameeleza kuwa hawataki kuona Tanzania ya Mabomu kwakuwa vitendo vya namna hiya na vile alivyoviita vya kikatili wamekuwa wakifanyiwa mawakili bila kujali kuwa wana ulinzi kisheria.


 

Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoani Songwe Yaagiza Kukamatwa Mbunge wa Tunduma

$
0
0
Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoani Songwe Yaagiza Kukamatwa Mbunge wa Tunduma
Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Momba mkoani Songwe imeagiza kukamatwa mara moja kwa Mbunge wa Jimbo la Tunduma kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mh.Frank Mwakajoka kwa tuhuma za kuwadhihaki wateule wa Rais.

Kamati ya Ulinzi na usalama wilayani ya Momba imeagiza kiongozi huyo kukamatwa baada ya kumdhihaki Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Mkuu wa Mkoa wa Songwe Mhe. Chiku Galawa pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Momba Mhe. Juma Said Irando.



Je Dada Unahitaji Kuwa Mrembo na Ule Muonekano Bomba wa Kisuperstaa na Kaka Kuwa Mtanashati? Waone Hawa

$
0
0
Je Dada unahitaji kuwa Mrembo na ule muonekano bomba wa kisupersta, kaka unahitaji kuwa mtanashati na mvuto zaidi wa KIUME?fika black beauty company utatimiza ndoto zako,hawakosei hata siku moja kwa products original na zenye matokeo yaharaka sana,bila madhara, BLACK BEAUTY COMPANY  ni kampuni yenye uzoefu wa hali ya juu sana

1)kuongeza hips,makalio,mapaja@150000
(b)kuongeza hips,makalio,mapaja na miguu@200000/=
2)kuongeza miguu ,kuondoa vigimbi@120000/=
3)kuwa mweupe mwili mzima (Rangi moja)@150000/=
4)Kupungua mwili mzima@150000/=
5)kupunguza tumbo@100000/=
6)kupunguza au kuongeza matiti@100000/=
7)kukuza nywele@100000/=
8)kuondoa michirizi @100000
9)kuondoa madoa,mabaka na chunusi sugu@100000/=
10)kuongeza uume na nguvu za kiume@150000/=
Dawa zetu niuhakika sana100%na utaletewa popote ulipo,mikoani tunatuma,nje ya nchi tunatuma DHL,ofic zetu zipo kariakoo msimbazi police,

Karibuni kwa mawasiliano zaidi WhatsApp +255657778924,au call0743534406 au unaweza kutufollow
👇👇👇👇👇👇
@black_beauty_company

Diamond Platnumz Kwa Hili Ulilolifanya Una Deni Kubwa Kwa Ali Kiba.......

$
0
0
Habari zenu wadau,nianze na kilichonileta hapa,,,Diamond platnumz unatakiwa ujue kuwa kwasasa una deni kubwa sana kwa kinachoendelea sasahivi na huu upepo wa TSUNAMI wa SEDUCE ME ya KING ALIKIBA,,kama tunavyoona wewe umeonekana ndo looser kwenye huu mpambano japo ulianza vizuri na kilicho kuharibia zaidi target yako ni ngoma ya ZILIPENDWA..

-Rekodi yako ya youtube imevunjwa..
-Watu wanakuponda.
-Umeongeza kejeri kwa uchokozi wako..

Kitu kitakachokuweka salama ni kuvunja rekodi ya video mpya ya Alikiba tena ambayo imetazamwa mara 1000000 ndani ya saa 38 tu..

Kwahiyo jipange maana siyo kitu cha mchezo mchezo..Maoni yenu wanajukwaa..

Duka la Msanii Jux na Dada yake Fatma Limebomolewa Bila Taarifa yoyote

$
0
0
Dada yake Jux aitwaye Fatma ajirekodi video akionyesha duka lake lililobomolewa bila taarifa yoyote ile. inasemekana wamiliki wa duka hilo ni Jux na dada yake huyu aitwaye Fatma.

VIDEO:

Diamond Platnumz Jihadhari na Washauri Wako.....Wanakuingiza Choo cha Kike Ukiwa Unaona

$
0
0
Diamond Platnumz Jihadhari na Washauri Wako.....Wanakuingiza Choo cha Kike Ukiwa Unaona

Kwa wiki nzima hii ukifuatilia kinachoongelewa katika mitandao ya kijamii na kwenye vipindi vya burudani ni ugomvi unaowahusisha Diamond na Alikiba, yote ikianza baada ya wimbo wa Fid Q aliowashirikisha Diamond na Rayvanny kutoka na kusikika mashairi yaliyoonekana kama yanamlenga Alikiba. Mara baada ya wimbo ule kutoka Alikiba alimjibu kwa kebehi Diamond na kumfananisha na Malkia wa Nguvu huku Ommy Dimpoz ambaye yuko menejimenti moja na Kiba alijaribu kumtetea swahiba wake akaishia kuchanwa katika wimbo mwingine ambao Diamond aliutoa kama kujibu mapigo ambapo Ommy alienda mbali zaidi kwa kumjibu kupitia Instagram katika picha aliyopozi na mama yake Diamond, Bi Sandra kitu ambacho kilionyesha kuchochea zaidi ugomvi huku mashabiki wakigawika pande mbili.

Siku 3 baadae Alikiba alitoa wimbo wake mpya alioupa jina la Seduce Me ambapo saa moja baadae Diamond kupitia instagram yake alipost picha ya mtu anaecheka kwa kebehi ikatafsiriwa kama vile ameudharau wimbo wenye, jioni yake Diamond nae akawatangazia mashabiki wake kuhusu kuachia wimbo mpya aliowashirikisha wasanii wote walio chini ya label ya Wasafi uliopewa jina la Zilipendwa na kilichofuatia hapo ni ushindani mkubwa wa mashabiki ambao wamekuwa wakitupiana maneno.

Hata hivyo suala la Diamond kutoa wimbo ni kama vile halijapokelewa vizuri na wasanii wengine ambao wanaona lengo lake ni kujaribu kuuzima wimbo wa Alikiba na wengi ukifuatilia utagundua wamechagua upande wa Seduce Me badala ya Zilipendwa. Yameibuka maneno zaidi kuhusu namna ambavyo label ya Wasafi imekuwa na tabia ya kutoa nyimbo siku msanii yeyote mkubwa akiachia wake, kana kwamba wanataka wao tu ndio wasikike msanii mwingine asiwe juu yao.

Ninavyomfahamu mimi Diamond ni mtu ambaye yuko humble sana ukiongea nae, na nyuma ya pazia huwasaidia wasanii wengi tu wanapokuwa na matatizo. Hili suala la ugomvi wa kujaribu kuwabania wasanii wengine wasisisike inajulikana wazi ni management yake imekuwa ikilisukuma. Ushauri wangu kwake ni kuwa ajihadhari na hii tabia na kubali kwamba ushindani ni mzuri kwenye muziki lakini isifikie hatua ya kutaka kumharibia msanii mwenzake. Asiruhusu mameneja wake Babu Tale na Sallam kumuingiza kwenye ugomvi na wasanii wengine ambao asilimia kubwa Diamond anawaheshimu kama kaka zake, atambue nguvu ya umma iliyotumika kumtetea Alikiba inaweza kuhamia kwenye kazi zake nyingine na kumshusha kabisa.

Ni hayo tu.

TFF Kutengeneza Ngao Mpya ya Simba

$
0
0
 TFF Kutengeneza Ngao Mpya ya Simba
Baada ya shirikisho la soka Tanzania TFF kuomba radhi kwa kutoa Ngao ya Hisani kwa Simba iliyokuwa na makosa ya kiuandishi, leo shirikisho hilo limeonesha na kutangaza kuitengenezea Ngao mpya Simba ambayo watawakabidhi siku ya mchezo wa Ligi Kuu kati ya Simba dhidi ya Azam FC.

Kama utakuwa unakumbuka TFF ambao ndio waandaaji wa mchezo wa Ngao ya Hisani kati ya Simba dhidi ya Yanga uliyochezwa uwanja wa Taifa August 23 na Simba kupata ushindi wa penati 5-4, ilitolewa Ngao ya Hisani ambayo iandikwa kimakosa ‘SHEILD’ badala ya ‘SHIELD’ lakini imesema imewaadhibu wahusika waliyofanya kosa hilo.

Hivyo TFF wamewatengenezea Ngao mpya Simba ambayo haina makosa, pamoja na hayo TFF imethibitisha nahodha wa Taifa Stars Mbwana Samatta na Elias Maguli wamewasili kambini wakati Abdi Banda ataingia mchana wa leo na Simon Msuva usiku wa leo.

Viewing all 104799 articles
Browse latest View live




Latest Images