Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104789 articles
Browse latest View live

Kwa Sasa Nina Kazi Kubwa ya Kumlinda Vanessa Mdee - Jux

$
0
0
Kwa Sasa Nina Kazi Kubwa ya Kumlinda Vanessa Mdee - Jux
Msanii Jux amesema sasa hivi ana kazi kubwa ya kumlinda aliyekuwa mpenzi wake, Vanessa Mdee machoni mwa watu ili asiweze kuonekana mbaya kwa chochote atakachokifanya baada ya kuachana kwao.

Akizungumza kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Jux amesema Vanessa sasa hivi yupo kwenye wakati mgumu katika kufanya mambo yake ya kawaida, hivyo ni jukumu lake kuhakikisha haeleweki vibaya mbele za watu.

“Kuna vitu mimi siwezi kuvifanya ili kumlinda na yeye hawezi kufanya kunilinda mimi, japo watu watasema vingi hasa kwa mwanamke pale anapoamua kufanya baadhi ya vitu vyake binafsi. Natakiwa kumlinda Vanessa sasa hivi kwa kuwa kila jambo ambalo atalifanya watu watamfikilia vibaya hivyo napaswa kumlinda kutokana na hilo kwa sababu wanawake wenyewe wako wachache”, alisema Jux.

Jux aliendelea kwa kusema kuwa wakati bado wako kwenye mahusiano Vanessa alikuwa na uhuru wa kufanya jambo lolote, kwani karibia kila mmoja aliamini yupo na Jux ndiye mtu wake.
“Muda mwingine anaweza akashindwa hata kufanya vitu vingine, mwanzo hata akionekana na mtu wana-shoot au wanafanya nini, wanajua yupo na Jux, lakini sasa hivi hawezi”, alisema Jux
Pia Jux aliweka wazi kuwa ingawa bado ana kidonda cha maumivu ya kuachana na mpenzi wake huyo, lakini haikuwa ngumu kwao kufikia uamuzi huo, kwani kabla ya kuanza mahusiano walikuwa marafiki wa kawaida, kitu ambacho mpaka sasa bado wanacho

Ongeza Hips, Makalio na Mapaja, Kuwa Mweupe na Softi, Ongeza Maumbile ya Kiume na Hamu ya Tendo

$
0
0
MAMBO HAYOOOO!! ONGEZA HIPS, MAKALIO NA MAPAJA, KUWA MWEUPE NA SOFTI, ONGEZA MAUMBILE YA KIUME, NGUVU NA HAMU YA TENDO N.K @markson_beauty_pr Tunakuletea bidhaa bora zenye matokeo ya uhakika na haraka zisizo na kemikali wala madhara. Zimetengenezwa kwa mimea na matunda na kudhibitishwa kiafya. NB. Matokeo ni uhakika na garantii na risiti


BIDHAA ZETU:- 1.Kurefusha nywele na kuzuia kukatika ovyo @130000@130,000/=
2.Kuongeza shepu (hips, makalio na mapaja) kwa:-
(a)BOTCHO MULT-PLUS 10× @200000@200,000/=
(b)Vidonge @180000@180,000/=
(c)BOTCHO 10× ya kupaka @170000@170,000/=
3.Kuwa mweupe na softi mwili mzima kwa:- (1)Mafuta @130000@130,000/=
(11)Vidonge @150000@150,000/=
4. Kupunguza unene na manyama uzembe @150000@150,000/=
5.Kuongeza uume pamoja na nguvu za kiume kwa:-
(a)SHARK POWER gely ya kupaka (Inaongeza inch 6-7) @150000@150,000/= (b)Vidonge kwa ajili ya kuongeza nguvu na hamu ya tendo la ndoa hata kwa wenye kisukari @150000@150,000/= (C)HANDSOME UP ORIGINAL- kifaa cha kuongeza maumbile kwa size uipendayo @250000@250,000/=
6.Kuondoa mvi milele zisiludi tena @150000@150,000/=
7.Kuongeza unene wa mwili mzima na uzito pamoja na hamu ya kula @130000@130,000/=
8.Kupunguza tumbo (kitambi) na nyama za pembeni kwa:-
(a)Dawa ya kunywa au kupaka @130000@130,000/= (b)Mkanda wa kawaida @120000@120,000/= (c)Micro-computer belt wa umeme @200000@200,000/=
9.Kupunguza maziwa na kuyasimamisha hata kwa walionyonyesha @130000@130,000/=
10.Kushepu miguu (CHUPA YA BIA) na kuondoa vigimbi @130000@130,000/=
11.Kuondoa mipasuko mwilini (michirizi) @120000@120,000/=
12.Kurudisha usichana (bikra) @120000@120,000/=

Wasiliana nasi :- (+255) 0767447444 au. 0714335378

TAHADHARI: Hakikisha unapata risiti yenye muhuri halisi wa MARKSON CO pamoja na garantii ili kukuhakikishia kufanikiwa kwako. 👉🏻Ili kuona bidhaa zaidi na shuhuda za waliotumia bidhaa zetu. ............... Follow us on instagram @Markson_beauty_pr

Sijawahi Kumuhonga Mwanamke Pesa Ili Anipende - Mwana FA

$
0
0
Sijawahi Kumuhonga Mwanamke Pesa Ili Anipende - Mwana FA
RAPA asiyechuja kwenye muziki wa Hip Hop Bongo, Hamis Mwijuma ‘Mwana FA’ ametoa kali ya mwaka baada ya kusema kuwa katika maisha yake yote ya ujana, hajawahi kumhonga mwanamke pesa ili apendwe.

Akichonga na Risasi Vibes, Mwana FA alisema tabia ya kuhonga honga wanawake pesa na vitu vingine vya thamani ili kupendwa hilo kwake halijawahi kutokea tangu alipopata akili mpaka alipo sasa kwenye ndoa.

“Nihonge ili nipate nini, sijawahi kuhonga hata siku moja najua wengi wanaweza wasiamini lakini ndiyo hivyo, tabia hizo naishia kuziona kwa washkaji zangu huku mtaani lakini kwangu hazijawahi kuwepo maana kitendo hicho nakichukulia kama biashara ya kikahaba ambayo binafsi naichukia” alisema Mwana FA

Korea Kaskazini Yaonywa na Baraza la Usalama la UN

$
0
0
 Korea Kaskazini Yaonywa na Baraza la Usalama la UN
Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limelaani kitendo cha Korea Kaskazini cha kurusha kombora kupitia anga ya Japan, huku nchi hiyo ikithibitisha kutekeleza.

Taarifa iliyoandikwa na Marekani, haikutishia kuiwekea vikwazo vipya Korea kaskazini.
Lakini Baraza la Usalama limeitaka Korea Kaskazini kusitisha majaribio zaidi na kusitisha mpango wake wa nuklia.

Wanachama 15 wa Baraza hilo la Usalama wameitaka Korea Kaskazini kuchukua hatua za haraka kupunguza hali ya wasiwasi uliyopo.
Majeshi ya Korea Kusini na Marekani yamekuwa yakifanya mazoezi ya pamoja karibu na mpaka wa Korea Kaskazini, jambo ambalo Pyongyang inasema ni mazoezi yenye kulenga uvamizi wa kijeshi.

Hivi Ndivyo Lulu Anavyoteswa na Matiti Yake

$
0
0
Hivi Ndivyo Lulu Anavyoteswa na Matiti Yake
MUIGIZAJI nyota wa filamu Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ mwishoni mwa wiki iliyopita aligeuka kuwa gumzo baada ya nguo aliyovaa kuonekana kumtesa kutokana na matiti yake kutaka kuchomoza kila wakati.

Tukio hilo lilitokea katika Ukumbi wa Cinema, Mlimani City Jumamosi iliyopita wakati wa uzinduzi wa Filamu ya Heaven Sent ya muigizaji mwenzake, Wema Sepetu ambayo ilikutanisha mastaa wa fani mbalimbali nchini.

Lulu aliyekuwa amependeza kwa mavazi yake, akiwa amevalia gauni jeusi refu lenye mpasuo mkubwa, alijikuta akipata taabu ya kuirudisha nguo yake sehemu ya kifuani, kwani kila wakati matiti yalionekana kutaka kutoka nje, lakini akawa anafanya kazi kubwa ya kuirudishia.

“Jamani muoneni Lulu anavyohangaika na hiyo nguo, sasa tangu nyumbani hakujua kama inamsumbua abadilishe? Au ndiyo mbwembwe za kutaka watu waone nido zake zilivyo nzuri?” alisikika akisema shabiki mmoja aliyeonekana kumfuatilia sana muigizaji huyo.
Licha ya Lulu, mastaa wengine kibao wa filamu walihudhuria uzinduzi huo na mashabiki wa kawaida wa tasnia hiyo, huku Wema Sepetu mwenyewe akiwa amesindikizwa na aliyekuwa mpenzi wake wa zamani, mshindi wa Big Brother Hotshot, Idris Sultan.


Nafanya Sanaa Kwakua Ipo Ndani ya Damu Sigangi Njaa- Dully Sykes

$
0
0
Nafanya Sanaa Kwakua Ipo Ndani ya Damu Sigangi Njaa- Dully Sykes
.MKONGWE wa muziki wa kizazi kipya, Dully Sykes ‘Mr Misifa’ amejinasibu kuwa anafanya sanaa hiyo kwa vile iko ndani ya damu yake na si kuganga njaa kama wengine wanavyofanya. Akizungumza na Risasi Mchanganyiko, baba huyo wa watoto wanne, alisema familia yake yote imekuwa ikifanya muziki, kuanzia babu yake hadi baba yake.

“Mimi tangu babu yangu Mzee Wahed Abdul Sykes alikuwa mwanamuziki na Mwenyekiti wa chama cha muziki wa dansi Tanzania baba yangu pia alikuwa mwanamuziki, kwa hiyo Watanzania wengi wanafahamu kuwa mimi siyo mganga njaa, ni mwanamuziki mahiri mwenye uwezo wa kuimba na kupangilia mashairi. Alisema anachofahamu ni kwamba muziki umempa heshima, lakini siyo jina kwa
sababu familia yao imepata jina kubwa kupitia muziki tangu zamani.

“Siwezi kusema muziki ndiyo umenipa jina, hapa jina hili lilikuwepo tangu enzi hizo za babu yangu akitamba, lakini nasema muziki ndiyo umenifikisha hapa nilipo, hivi sasa nina studio yangu pale Tabata Kimanga nimeipa jina la 4.12,” alisema.

Aliongeza kuwa pamoja na kutoa vibao vingi katika muziki wake, lakini Wimbo wa Julieta ndiyo anaoukubali zaidi na akikisikia kibao hicho kinagongwa katika redio au chombo chochote kile lazima asimame akisikilize.

Bado Naipa Nafasi Yanga ya Kutetea Ubingwa - Msuva

$
0
0
Bado Naipa Nafasi Yanga ya Kutetea Ubingwa - Msuva
LICHA ya Yanga kuanza ligi kwa sare, lakini kiungo wa zamani wa timu hiyo, Simon Msuva, ameibuka na kusema kuwa, bado anaipa timu hiyo nafasi ya kutetea ubingwa wake msimu huu.
Yanga ambayo ni bingwa mtetezi wa ligi hiyo, Jumapili iliyopita ilitoka sare ya bao 1-1 na Lipuli FC, huku wapinzani wao wa jadi, Simba wakianza kwa ushindi mnono wa mabao 7-0 dhidi ya Ruvu Shooting.

Msuva ambaye kwa sasa amejiunga na Klabu ya Difaa Al Jadida ya Morocco, amesema kuanza taratibu kwa Yanga hakumaanishi moja kwa moja kwamba haiwezi kutetea ubingwa wake, bali nafasi ya kufanya hivyo ipo tena kubwa.

“Nimefuatilia mechi za mwanzo za ligi ya Tanzania na nimesikia Simba wameanza kwa kushinda 7-0, wakati timu yangu ya zamani ya Yanga ikitoka sare, watu wengi wanasema Simba itakuwa bingwa, lakini binafsi naona Yanga ndiyo yenye nafasi ya kufanya hivyo tena.

“Nasema hivyo kwa sababu ukiangalia kweli zote zimefanya usajili wa maana, lakini Yanga ina wachezaji wengi waliokaa pamoja na kuzoeana tofauti na Simba yenye sura nyingi mpya. “Lakini pia, Donald Ngoma amerejea vizuri, na yule kiungo mkabaji waliyempata (Papy Tshishimbi), nadhani lile tatizo la siku nyingi limepata mtu sahihi wa kulitibu,” alisema Msuva.

Hii Hapa Taarifa Iliyotolewa Kuhusu Kuonekana kwa Fuvu la Kichwa Katika Uwanja wa Taifa

$
0
0
Hii HapaTaarifa Iliyotolewa Kuhusu Kuonekana kwa Fuvu la Kichwa Katika Uwanja wa Taifa
Baada ya taarifa kusambaa katika mitandao ya kijamii na picha zikisambaa kutoka uwanja wa Taifa kwa madai kuwa, kipindi hiki ukarabati wa uwanja huo sehemu ya pitch imeonekana fuvu la kichwa cha mtu, taarifa ambazo zimesambaa sana katika mitandao ya kijamii.

Mkurugenzi msaidizi wa idara ya michezo Alex Nkenyenge ili atoe taarifa kamili kuhusiana na tetesi zilizokuwa zinasambaa ni kweli ni fuvu?

“Kwanza hiyo ni taarifa ya uongo na hakuna fuvu isipokuwa ni madude ambayo yamepatikana kwenye mchanga baada ya kuwa tumefukua sehemu ya uwanja, kwa hiyo hakuna kitu kinachoitwa fuvu la mtu wala nini ni madude tu yaani mamimea yale yaliyooza basi yanafanana kama magimbi ambapo ndani lilikuwa limeshaliwa”

“Sasa kwa sababu mtu analiona kwa mbali anasema fuvu sasa sijui fuvu litakujaje hapa, kwanza kilichotokea hilo dude limekuja na mchanga wala halikuwa ndani ya uwanja, yaani kwenye mchanga uliyoletwa ambao tulikuwa tunajaza kwenye pitch baada ya kuwa tumeondoa lea ya juu”

“Kwa hiyo hakuna kitu kama hicho bahati mbaya kwa watanzania wanapenda kuzungumza vitu vibaya kuliko vizuri, maana mtu haulizi wala kushangaa ile inayosafisha uwanja, sasa kama ni fuvu unataka kusema uwanja wa Taifa kulikuwa na makaburi?”




Ali Kiba: Kumfunga Anayetumia Dawa za Kulevya ni Kumtesa

$
0
0
Ali Kiba: Kumfunga Anayetumia Dawa za Kulevya ni Kumtesa
Msanii Alikiba amejitosa kwenye suala la dawa za kulevya kwa kumtetea aliyekuwa swahiba wake Chid Benz kwa kusema anapofungwa mtumiaji wa dawa za kulevya ni kumtesa bali anapaswa kupelekwa katika vituo vya afya ili aweze kupatiwa tiba mbadala.

Alikiba ameeleza hayo baada ya Chid Benz kukamatwa na dawa za kulevya hivi karibuni na Jeshi la Polisi na kuweka chini ya uangalizi mkali wa Mahakama jambo ambalo watu wengi walishtushwa na taarifa hizo kwa kuwa walitegemea pengine atabadilika tabia hiyo alivyotoka 'Rehab'.

"Unapomfunga mtu ambaye ni mtumiaji wa dawa za kulevya ni mateso makubwa kwa kuwa mtu huyo anapaswa apelekwe kitengo maalum ili apatiwe dawa za kuzuia kutamani vitu vya aina hivyo, pia yeye mwenyewe tunapaswa tumshauri ili aweze kushinda nafsi yake. Ujue vitu kama hivyo ni kuishinda tu nafsi katika kuamua na akae navyo mbali.

Pamoja na hayo, Alikiba aliendelea kwa kusema "kama ametoka 'Rehab' hivi karibuni halafu inasemekana amejihusisha tena na hivyo vitu ni makosa makubwa kwa sababu tayari umetoka katika kupata tiba halafu unayakaribia tena hiyo haifai kabisa", alisema Alikiba.

Inasikitisha.. Muuguzi Awaua Wagonjwa 90 Ili Awafufue Tena

$
0
0

Inasikitisha.. Muuguzi Awaua Wagonjwa 90 Ili Awafufue Tena
Muuguzi nchini Ujerumani anayetumikia kifungo cha maisha kwa kuwaua wagonjwa sita, imebainika aliwaua wengine 84.

Idadi ya watu aliowaua imemwingiza katika rekodi ya mwanamke aliyefanya mauaji mengi kuliko wote nchini humo.

Mwanamke huyo, Niels Hoegel (40), alifungwa mwaka 2015 baada ya kupatikana na hatia ya kuwaua wagonjwa sita kwa kuwachoma sindano inayosababisha moyo kusimama ghafla.

Mamlaka za nchi hiyo zimekuwa zikifanya uchunguzi wa maelfu ya vifo, ikiwamo kufukua maiti za wagonjwa waliokufa chini ya uangalizi wake katika hospitali binafsi za Delmenhorst na Oldenburg ambazo amewahi kufanya kazi.

Polisi nchini humo wameliambia Shirika la CNN kuwa, wanaamini Hoegel aliua wagonjwa 36 katika Hospitali ya Oldenburg kati ya mwaka 1999 na 2001, na wengine 48 katika Hospitali ya  Delmenhorst.

Pia, wanasema idadi ya watu aliowaua inaweza kuwa kubwa zaidi lakini ushahidi hautapatikana kwa kuwa miili mingi ilichomwa moto, hivyo si rahisi kugundua sababu ya kifo kwa kupima majivu.

Katika mwendelezo wa kesi zake, Hoegel amekiri kuwachoma sindano wagonjwa ili moyo ushindwe kufanya kazi naye ajaribu kuwafufua kwa kuuamsha.

Amesema alitamani kuona anamfufua mtu baada ya kumchoma sindano hiyo na kwamba, alifadhaika aliposhindwa kuwarudishia uhai.

Johann Kuehme, ofisa wa polisi katika Mji wa Oldenburg aliwaambia wanahabari jana Agosti 29 kuwa idadi hiyo ya vifo imewaduwaza.

"Mauaji huenda yasingekuwa makubwa kiasi hiki kama hospitali hizi zingechukua hatua kuchunguza vifo au kutoa taarifa kwa mamlaka kuhusu vifo hivyo ili vichunguzwe,” amesema.


Ajari Yaua Sita na Kujeruhi 42 Mkoani Singida

$
0
0
Ajari Yaua Sita na Kujeruhi 42 Mkoani Singida
Watu sita wamefariki dunia na wengine 42 wamejeruhiwa baada ya lori lenye namba za usajili T.806 AEL aina ya scania mali ya Abdalla Mussa mfanyabiashara wa Mjini Singida, kuacha njia na kupinduka katika Kijiji cha Kijota, Mkoani Singida.

Akitoa taarifa hiyo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, ACP Debora Magiligimba, amesema ajali hiyo imetokea Agosti 27  katika kijiji cha Kijota wakati lori hilo likitokea mnadani katika kijiji cha Mtinko Singida vijijini, likielekea Singida mjini ambapo amebainisha kuwa chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva.

Kamanda Magiligimba amesema dereva wa lori hilo Jumanne Kidanka hakuwa makini na barabara wakati anaendesha lori hilo lililosheheni abira na mizingo mingi.
Aidha waliofariki wametajwa katika ajali hiyo ni pamoja na Haji Jumanne, Mikidadi Mohammed wote wawili wakazi wa kijiji cha Mrama, Musa Salimu mkazi wa kijiji cha Mwakiti, wengine ni Allen Mwangu mkazi wa wilaya ya Ikungi, Lucas Stephano mkazi wa kijiji cha Mrama na Sharifa Omari mkazi wa kijiji cha Ilongero.

Akizungumzia majeruhi wa ajali hiyo Kamanda Magiligimba amesema kuwa majeruhi 20 wamelazwa katika hospitali ya Mkoa wa Singida, 10wamelazwa hospitali ya misheni ya Mtinko na wanne ambao hali zao ni mbaya, wamelazwa katika hospitali ya misheni ya Hydom mkoani Manyara.

Wabunge Wakerwa na Uwanja wa Ndege Dar Wasema Unatia Aibu

$
0
0

Wabunge Wakerwa na Uwanja wa Ndege Dar Wasema Watia Aibu
Hali ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam imewaibua baadhi ya wabunge ambao wamesema ni mbaya, jambo linalotia aibu.

Mbunge wa Mwanakwerekwe (CUF), Ali Salim Khamis amesema katika jengo la abiria paa linavuja na kuna joto kali.

“Naweza nikapata shaka iwapo Terminal III nayo kwa miaka saba inaweza ikaanza kuvuja, Uwanja wa Julius Nyerere kwa kweli unatuaibisha,” amesema.

Mbunge huyo alitoa kauli hiyo jana Agosti 29, wakati Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (Pac) ilipokutana na Mamlaka vya Viwanja vya Ndege Tanzania (Taa).

Amesema Taa ina viwanja vingi vya ndege lakini vinavyochangia mapato ni vichache, huku vingine vikiwa havifanyi kazi.

Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Munde Tambwe amewataka wabunge waisaidie mamlaka hiyo ipate fedha za kutosha ili kuboresha viwanja vya ndege nchini.

“Kwa kweli ni aibu uwanja wa ndege Dar es Salaam. Tuwasaidie ili waweze kuongezewa fedha,” amesema.

Katika hatua nyingine, Mwenyekiti wa Pac, Naghenjwa Kaboyoka amesema hali katika uwanja huo ni aibu lakini Serikali badala ya kuukarabati inajenga viwanja vingine, kikiwemo cha Chato.

Amesema kuendelea kuwabana viongozi wa mamlaka hiyo ni kuwaonea kutokana na fedha wanazokusanya.

“Hawa watu tunaweza tukawa tunawaonea. Ni aibu tuone namna ya kuwasaidia,” amesema.

Kamati hiyo pia, imemwagiza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kufanya ukaguzi maalumu kwa hesabu za mamlaka hiyo kutokana na upungufu uliojitokeza katika taarifa za fedha kwa mwaka wa fedha 2015/16.

Awali, wabunge walisema wanapinga taarifa za fedha za mamlaka hiyo kwamba hazijafuata vigezo vya kisheria na mwongozo wa kimataifa.

Mbunge wa Vwawa (CCM), Japhet Asunga amesema hesabu za mamlaka hiyo zina upungufu hali inayotia shaka ilipataje hati safi ya ukaguzi wa hesabu.

Baadhi ya wabunge wamehoji kuhusu utata wa umiliki wa Kampuni ya Maendeleo ya Uwanja wa Ndege wa Kilimanjaro (Kadco).

Mbunge wa Sikonge (CCM), Joseph Kakunda amewataka wabunge na viongozi wa taasisi hiyo kuwa wazi kwa kuwa kuna vigogo wana masilahi ndani ya Kadco.

Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Felister Bura amesema kuna jambo katika kampuni hiyo ndiyo maana viongozi wamekuwa wakizunguka kuusema ukweli.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Taa, Profesa Ninatubu Lema amesema Kadco imekuwa ikiripoti moja kwa moja serikalini tofauti na viwanja vingine vya ndege nchini.


Alichokisema Ali Kiba Baada ya Kutajwa Kwenye Orodha ya Vijana 100 Wenye Ushawishi Afrika

$
0
0
Alichokisema Ali Kiba Baada ya Kutajwa Kwenye Orodha ya Vijana 100 Wenye Ushawishi Afrika
Baada ya msanii wa Bongo Fleva, Alikiba kutajwa kuingia katika orodha ya vijana 100 wenye ushawishi Afrika 2017, ameelezea furaha yake.

“Najisikia vizuri kwamba Africa nzima imekutambua, kuna watu ambao wanatamani kuwa kama Alikiba na vitu kama hivyo. Kwa hivyo nawahamasisha vijana wengine kufanya kazi nzuri kama mimi nivyofanya, nashukuru sana, najisikia vizuri,” ameiambia The Playlist ya Times Fm.

Vijana wengine wa kitanzania waliotajwa katika orodha hiyo iliyotolewa na African Youth Awards  ni pamoja na Nancy Sumari, Diamond Platnumz, Elizabeth ‘Lulu’ Michael, Flaviana Matata, Millard Ayo na Jokate.

Utendaji wa Sekta ya Afya Kuwekwa Hadhalani Leo

$
0
0
Utendaji wa Sekta ya Afya Kuwekwa Hadhalani Leo
Baada ya kutoa ripoti ya utafiti wa hali ya usalama nchini mwezi uliopita, asasi ya kiraia ya Twaweza leo asubuhi inazindua matokeo ya utafiti mwingine unaoangazia changamoto za sekta ya afya.

Matokeo ya utafiti huo uliopewa jina la Sauti ya Wananchi, ulifanywa kati ya Mei 11 na 25 mwaka huu kwa kuhusisha sampuli ya watu 1,801 wa Tanzania Bara.

Miongoni mwa mambo yanayotazamiwa katika utafiti huo wa mfululizo wa 19 wa Sauti za Wananchi ni iwapo changamoto katika sekta ya afya zimepungua katika uongozi wa Serikali ya Rais John Magufuli, ikilinganishwa na miaka ya nyuma.

Twaweza inasema ripoti ya mwezi huu ambayo utafiti wake ulifanywa kwa njia ya simu inaweka bayana takwimu za mtazamo wa wananchi juu ya upatikanaji wa huduma za afya na ustawi wa jamii.

“Ni mambo gani wananchi hukutana nayo wakati wanaenda kupata huduma ya afya? Wanasubiri kwa muda gani kuzipata huduma hizo na je, hukumbana na uhaba wa dawa, watumishi au vifaa wanapoenda kutibiwa” inaeleza taarifa ya Twaweza kwa vyombo vya habari.

“Je, wanaotakiwa kupata huduma za bima wanazipata ipasavyo. Wananchi wangapi wana bima za afya? Ni wananchi wangapi wanafahamu huduma zinazotolewa na maofisa ustawi wa jamii wa wilaya?” inaongeza.

Mapema Agosti mwaka jana, Twaweza walizindua utafiti unaofa nana na huu ulioitwa “Nyota njema huuonekana asubuhi?” ambao pamoja na mambo mengine ulibainisha kuwa wananchi sita kati ya 10 hupata huduma za afya kutoka kwenye vituo vya afya vya umma.

Lisu Aikana Tweet Iliyosambaa Kwenye Mitandao ya Kijamii Kuhusu Ali Kiba na Diamond

$
0
0
Lisu Aikana Tweet Iliyosambaa Kwenye Mitandao ya Kijamii Kuhusu Ali Kiba na Diamond
Mwanasheria wa Chadema na Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu ameikana akaunti ya Twitter iliyoandika maoni kumpongeza mwanamuziki Alikiba, huku ikiwa na picha ya wanamuziki wanaofanya kazi chini ya lebo wa Wasafi.

Lissu amesema hafahamu chochote kuhusu akaunti hiyo na maoni yaliyotolewa akitaka mwandishi amfafanulie.

“Wananisingizia kaka ni wimbo gani wa Alikiba?” akimaanisha haelewi chochote kinachoendelea kuhusu uwepo wa wimbo wa “Seduce Me.”

Amesema akaunti hiyo si yake: “Hiyo akaunti ya Twitter si yangu na nilishasema tangu mwaka jana kaka.”

Jana Agosti 29, akaunti hiyo ilikuwa gumzo kwenye mitandao ikiwa imebeba ujumbe unaosema: “Hakuna kitu kibaya kama wanaume sita kuvaa mawigi kupambana na mtu mmoja. #seduceme#.

Tweet hiyo iliambatanishwa na picha ya Kundi la Wasafi wakiwa wamevaa mawigi ambayo waliitoa sambamba na wimbo wao wa “Zilipendwa”.

Mashabiki wanaomuunga mkono Alikiba walifurahi wakiamini kiongozi huyo amejiunga na wengine wengi ambao walijitokeza hadharani kumpongeza Alikiba.

Baadhi ya viongozi waliompongeza Alikiba ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Hamis Kigwangalla; Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete; Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja na Mbunge wa Viti Maalumu, Halima Bulembo.



Video: Makonda Awatoa Hofu Wakazi wa Dar Sakata la Bomoa Bomoa

$
0
0
Makonda Awatoa Hofu Wakazi wa Dar Sakata la Bomoa Bomoa
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda leo August 30, 2017 ametembelea eneo la bomoabomoa Toangoma katika Wilaya ya Temeke na kuzungumza na wananchi wa eneo hilo kuhusu masuala mbalimbali ikiwemo ishu ya bomoabomoa katika eneo hilo.

Akiwa katika eneo hilo RC Makonda amewatoa wasiwasi wananchi ambao wamekuwa na hofu baada ya kuambiwa watabomolewa nyumba zao lakini akawaambia kuwa hakuna atakayewabomolea nyumba zao.

”Nawaomba tujiepushe na sehemu hatarishi, kila kinachofanywa na Serikali ni kwa ajili ya kuwaokoa wananchi. Hakuna mtu atakayewabomolea nyumba zenu, hata Rais aliniambia hamkumchagua ili awabomolee nyumba zenu.

“Tulikubaliana na Rais kuwa nyinyi mjiepushe kujenga kiholela na kwenye maeneo hatarishi na mfuate utaratibu.” – RC Makonda.

Maporomoko Congo DRC Yaua Watu 60

$
0
0
Maporomoko Congo DRC Yaua Watu 60
Takriban watu 28 wamefariki kufuatia maporomoko kusini mwa mji wa uchimbaji madini wa Kolwezi katika Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo kulingana na chombo cha habari cha Actualite.
Eneo hilo ni muhimu kwa madini ya Shaba .

Maporomoko ya hivi karibuni katika eneo la kaskazini-mashriki yaliwaua watu 200, kufuatia mvua kubwa iliosababisha mlima kuangukia kijiji kimoja cha uvuvi katika fukwe za Ziwa Albert.
Mshirikishe mwenzako Unavyoweza kumshirikisha mwenzako


BREAKING NEWS: RC Makonda Asitisha Bomoa Bomoa Dar

$
0
0
RC Makonda Asitisha Bomoa Bomoa Dar
Hatua hiyo imefuata baada ya kuwepo taarifa kutoka baraza la mazingira la taifa kuwa Nyumba Elfu kumi na saba mkoani humo katika eneo la bonde msimbazi zitabomolewa muda wowote kuanzia sasa.

Kwamujibu wa RC Makonda amedai Ofisi yake kutokuwa na taarifa hizo na kwamba agizo haliwezi kuwa na uhalali, ambapo ameongeza kuwa hata kama zoezi hilo lipo ni lazima yeye na wataalamu wake wajiridhishe hivyo basi zoezi hilo kwasasa amelisitisha.

Ametoa kauli hiyo leo mbele ta wakazi wa  kata ya Kigogo, Wilaya ya Kinondoni Jijini humo.

Tume ya Kupambana na Picha na Video za Ngono Yaundwa

$
0
0
Tume ya Kupambana na Picha na Video za Ngono Yaundwa
Serikali ya Uganda imeunda tume maalum pamoja na kuitengea bajeti ya pesa itakayotoka kila mwaka kwa ajili ya kudhibiti usambazaji wa picha, video na vitu vingine vinavyochochea ngono.

Imeelezwa kuwa maamuzi hayo yamefikiwa ili kuokoa nguvu kazi ya taifa ambayo imeathiriwa kwa kiasi kikubwa kutokana na watu wengi nchini humo kuendekeza masuala ya ngono.

Kwa mujibu wa Waziri wa Maadili wa Uganda, Simon Lokodo, tume hiyo itakayokuwa na wajumbe tisa na watalaam wengine kati ya 30 hadi 40 itatengewa bajeti ya Shilingi Bilioni 2 kila mwaka.

Bw. Lokodo amefafanua kwamba, tume hiyo itakuwa na vifaa vya kisasa kuingilia watu wanaohusika na kusambaza, kupakua, na kuangalia picha na video za ngono kisha kuwafikisha mbele ya vyombo vya sheria.

Amedai kuwa vitendo hivyo vinaliangamiza taifa hilo kwa kuchochea ongezeko la mimba za utotoni, matumizi ya dawa za kulevya, ushoga na ubakaji.

Upelelezi wa Kesi ya Aveva na Kaburu Umepelekwa kwa Mtaaramu wa Maandishi

$
0
0
Upelelezi wa Kesi ya Aveva na Kaburu Umepelekwa kwa Mtaaramu wa Maandishi
Upande wa Mashtaka katika kesi inayomkabili Rais wa Simba SC, Evans Aveva na Makamu wake, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ umeieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa wamekusanya nyaraka za upelelezi na zimepelekwa kwa mtaalamu wa maandishi.

Hayo yamesemwa na Wakili wa Serikali, Estazia Willson mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Victoria Nongwa wakati kesi hiyo ilipoitishwa kwa ajili ya kutajwa.

Wakili Wilson amedai kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika, pia wamekusanya nyaraka na zimepelekwa kwa mtaalam wa maandishi, hivyo wanasubiri ripoti.

Hakimu Nongwa ameahirisha kesi hiyo hadi September 8, 2017.


Viewing all 104789 articles
Browse latest View live


Latest Images