Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104799 articles
Browse latest View live

Barua kwa Rais: Mheshimiwa Jakaya Kikwete Umetisha Sana kwa Hili

$
0
0
Mheshimiwa Rais Jakaya Kikwete – natamani ningeonana na wewe ana kwa ana ili nikupe shikamoo yako nzito kwakuwa shikamoo ya kuandika siku zote huwa naiona ni yenye mapungufu. Heshima yako mkuu. Mimi kijana wako naliendeleza gurudumu la ujenzi wa taifa katika upande huu wa burudani kama kawaida. Upande ambao mheshimiwa umekuwa ukiuangalia kwa jicho la kipekee na lenye nia njema ya kuuletea neema. Upande ambao kwa viongozi wengi waliopita, ulikuwa ukichukuliwa kama wa anasa na wa kupoteza muda tu hivyo kushindwa kuupa heshima na ‘attention’ inayostahili.

Tangu uchukue madaraka, Mheshimiwa ulionesha nia njema na ya dhati ya kuwasaidia vijana walioamua kujiajiri kwa kutumia vipaji vyap walivyopewa na mwenyezi Mungu asiye mchoyo wa fadhila. Wengi walikuwa wamekwama kuendelea na masomo kutokana na sababu mbalimbali lakini kutokana na kuwa na kipawa cha kuimba ama kuigiza waliamua kutumia sauti zao kuwaburudisha watu kwa kutunga nyimbo.

Burudani ambayo kwa wengine wenye umri kama wako na waliopata nafasi kubwa serikalini wamekuwa wakiichukulia poa na kuiona kama aina moja miongoni mwa aina ya nyingi za uhuni zinazowatawala vijana wengi, imegeuka kuwa ajira muhimu kwa vijana wengi ambao maisha yao yamekuwa mfano kwa vijana wengine pia.

Mheshima Rais, tangu mwanzo, umekuwa karibu mno na vijana wanaofanya muziki wa Bongo Flava na kwao wewe ni kipenzi chao. Katika nchi hii ambayo kutokana na shida zetu, tumejikuta tukiona mabaya zaidi na kuwa watu wa kulalamika na yale mazuri tukijifanya hatuyaoni, hiki unachokifanya kwa vijana wetu kinaweza kionekane kwao cha kawaida tu. Mimi nakichukulia kwa mkazo mkubwa.

Nina imani kubwa, tasnia za burudani za majirani zetu zinatamani pia zingekuwa na Rais kama wewe, ambaye anaufahamu umuhimu wa msanii na kwa moyo mmoja amekuwa akiwajali. Naamini mheshimiwa Rais una imani kama niliyonayo mimi kuwa, wasanii wamekuwa wakitimiza wajibu muhimu katika jamii kwa kutuburudisha tuwapo na mawazo, furaha, huzuni na hali mbalimbali, kutuliwaza pale ya mambo ya dunia yanapotuelemea na kutusemea pale tunaposhindwa kuwasilisha nia zetu. Haipendezi kumuona mtu anayeitumikia jamii kwa hali hii, kuishi maisha ya tabu na ya kudharauliwa.

Na ndio maana umekuwa bega kwa bega kujaribu kuwapa ‘mashavu’ vijana wako ili maisha yao yawe mazuri. Ni ngumu kutimiza matakwa yao yote lakini ile hali tu ya kuwaweka karibu, kuwapa connection, imekufanya uonekane kuwa wewe ni rais wa pekee na ambaye umekuwa na mchango mkubwa kwenye kiwanda cha burudani.

Mheshimiwa Rais, nimeandika barua hii kwa lengo kuu la kukupongeza kwa hotuba yako inayotia moyo uliyoitoa Jumamosi iliyopita mjini Dodoma katika tamasha la uzalendo. Ile ni miongoni mwa hotuba zilizonifurahisha mno mheshimiwa. Ilinionesha jinsi ambavyo unafuatilia kwa ukaribu industry ya muziki duniani. Nilifurahi kukusikia mwenyewe jinsi ambavyo kutumia connection zako mwenyewe, umemtambulisha Diamond Platnumz kwa mdau mkubwa na muhimu katika muziki wa Marekani, Kevin Liles.

Kiukweli mimi Kevin nilimfahamu kupitia makala ya Trey Songz iliyorushwa miaka kadhaa kupitia MTV ambapo yeye alikuwa akiongea kama meneja wake. Nilivutiwa na jinsi alivyo na mchango mkubwa kwa Trey na hivyo nikaamua kumsoma zaidi kwenye mitandao. Niligundua kuwa alikuwa kuwa Rais wa Def Jam Recordings (pamoja na vyeo vingine) ambayo ni miongoni mwa label kubwa na zenye mafanikio nchini Marekani. Naamini kuwa maongezi yako na Kevin kuhusu Diamond yatazalisha kitu kikubwa hapo baadaye. Nilipenda pia uliposema kuwa unajivunia kwa hatua aliyofikia.

Ulitisha zaidi mheshimiwa pale ulipodai kuwa ulizungumza pia na meneja wa Ludacris, Chaka Zulu. Na zaidi pale ulipodai kuwa Usher na mtangazaji wa zamani wa kipindi cha 106 & Park cha BET, Terrence J ambaye kwa sasa ni mtangazaji wa E!News, watakuja Tanzania na kwamba ikiwezekana Trey Songz naye ataibuka.

Hawa watu ni muhimu mno katika burudani duniani hivyo wakija Tanzania kuongea na wasanii kuhusu masuala mbalimbali, watapandikiza masuala mengi ya muhimu kwao. Wasanii wa nyumbani watajifunza mengi kutoka kwao.

Mheshimiwa nimependa ulivyojiongeza hapa kwamba ni vyema ukamfundisha mtu kuvua samaki kuliko kumpa samaki ambao akiwala atapata njaa tena na ataendelea kuhitaji. Ungeweza kusema uwape fedha baadhi ya wasanii lakini fedha hizo zisingewasaidia kwa lolote. Kuwaleta akina Usher nchini kwetu itakuwa ni zawadi kubwa na muhimu kwa wasanii sababu watajifunza mbinu nyingi za kuboresha biashara ya muziki nchini ambayo kama ikitambuliwa kama ajira rasmi na serikali, itawanufaisha wengi.

Naamini kuna wengi watabeza, wataponda na wataongea kuchafua hatua hii lakini jambo unalopaswa kukumbuka kuwa hata Yesu Kristu licha ya kuja duniani kuwaokoa wanadamu dhidi ya dhambi, walimkejeli na kumsulubu bila huruma. Ungekuwa Rais usiyejali kama marais wengine madikteta duniani basi ungetumia uwezo wako kuwaleta wasanii hao waje wakuburudishe kwenye sherehe zako binafsi. Lakini unawaleta hawa kwa madhumuni na nia halisi ya kuwasaidia wasanii wa nyumbani. Hilo si la kupuuzwa.

Na pia wale ambao wataponda hatua hii, ndio walewale ambao bado wanauchukulia muziki kama anasa, uhuni, starehe na masuala ya kupoteza muda wakati kwa nchi zilizoendelea, muziki na filamu vinachangia pato kubwa katika serikali.

Nausubiria sana ujio wa watu hawa muhimu na bila shaka wasaidizi wako watakuwa werevu wa kutosha kutualika pia sisi waandishi kujifunza yanayotuhusu katika ziara hiyo. Wasiwasi wangu ni kuwa Rais atakayechukua nafasi yako atafuata nyayo zako? Anyway, nisikuchoshe kwa maneno mengi mheshimiwa, nakutakia majukumu mema.

Wako katika ujenzi wa taifa, Sky.

Walimu 298 Walala Sakafuni KSiku 4 Kufuatilia Mishahara Igunga.

$
0
0
JUMLA ya Walimu 298 wa shule za msingi na sekondari walioajiriwa mwaka huu Wilayani Igunga mkoani Tabora, wameendelea na mgomo wa kubaki katika na kulazimika kulala katika viti na meza katika ukumbi wa Halmashauri hiyo siku nne mfululizo wakishinikiza serikali ya Wilaya ya Igunga kuwalipa mishahara yao.

Wakizungumza na FikraPevu leo Jumatatu Juni 16, 2014 baadhi yao wakiwa na watoto wachanga wamelalamikia maisha magumu wanayolazimika kuishi kwa kuomba omba kufuatia serikali ya Wilaya kushindwa kuwalipa mishahara yao tangu mwezi Aprili mwaka huu, na serikali ya Wilaya hiyo kuwa na kauli tata kwa kile wanachodai ni kuwadanganya kuwa wangewalipa fedha zao Juni 13, mwaka huu agizo ambalo uongozi wa Wilaya hiyo lakini leo wanadaiwa kulitupilia mbali.

Aidha, wamesema tamko lililotolewa na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Rustica Turuka kuwa wangelipwa fedha kutokana na mapato yatokanayo na makusanyo ya Halmashauri hiyo, lakini leo wamelitupilia mbali tamko hilo kwa kuwapiga danadana kuwa fedha hazitoki katikahalmashauri hiyo bali zinatoka hazina.

Baadhi ya waalimu hao, Joseph Ndonga, amesema wamekubaliana kwa pamoja na kusisitiza kuwa wataendelea kuishi katika ukumbi wa halmashauri hadi malipo yao yatakapofanyika, kwani baadhi yao wamefukuzwa kwenye nyumba zo walizopanga kutokana na kushindwa kulipa kodi ya nyumba.

“Hapa tulipo ni siku ya nne kuanzia Ijumaa Juni 13, 2014, tutaendelea kuwabana hadi watupe hela zetu kwamaana sisi maeneo tunayoishi tunakabiliwa na ukata wa hela umekopa unajua mwisho wa mwezi unapata hela lakini hadi sasa hawasikilizi kilio chetu tumeitwa na DED kuwa tukubali kupokea shilingi laki moja tumeikataa kwamaana sio hela tunayodai”  alisema Ndonga

Kaimu Afisa Utumishi wa Halmashauri hiyo, Fredi Mhecho, amesema kuwa sababu ya kucheleweshwa malipo ya waalimu hao ni zoezi la kuhakiki majina kuendeshwa kwa awamu na kuanzia Aprili hadi mwezi huu zoezi hilo bado linaendelea na hadi sasa bado wanajaribu kuangalia namna ya kutatua tatizo hilo.

Polisi wazingira eneo walilopo walimu
Katika hali ya kushangaza walimu hao wamedai kuzungukwa na Askari wa kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) mjini humo, hali ambayo imetajwa kuwafanya baadhi ya walimu hao kuingiwa na hofu baada ya kusimamia msimamo wa kutoondoka katika ukumbi wa Halmashauri hiyo.

“Wakuu wa idara wamepiga simu Polisi kuomba msaada ili waweze kutuondoa hapa gari la Polisi liko hapa na polisi wa Kikosi Kutuliza ghasia (FFU) wapo na mabomu ya machozi wakiwa wanazunguka katika maeneo tuliyopo” alikaririwa mmoja wa walimu hao.

Kamanda wa Polisi mkoani humo, Susan Kaganda, amesema “Hakuna Polisi waliopo katika ukumbi wa Halmashauri, ninachojua waalimu wapo pale tangu Ijumaa hadi leo lakini kwa upande wa Polisi kuwepo katika hilo eneo hakuna”.

Tafiti zinaonyesha kuwa, walimu wa shule za msingi na sekondari mkoani humo wakati mwingine hulazimika kuacha kufundisha kutokana na tatizo la ukosefu wa maji kiasi cha kuwalazimu kwenda kutafuta huduma hiyo kwa muda mrefu bila kuingia darasani.

Jackline Wolper: Msaka Pesa toka Machame Aliyeangukia Kwa Matapeli wa Mapenzi Jijini Dar

$
0
0
Jackline  Wolper  ni  mmoja  kati  ya  warembo  wenye  umaarufu  mkubwa  nchini  na  katika   soko  la  Filamu  za  Tanzania.
Anamvuto  unaokubalika  na  wengi  na  ameweza  kujipatia  umaarufu  mkubwa  sana  kupitia  filamu  alizoshirikishwa  na  alizozifanya  chini  ya  kampuni  yake  mwenyewe. Pia  ni  mwandishi  mzuri  wa  Script  na  muongozaji  mzuri  wa  filamu….

Alizaliwa  Moshi  mkoani  Kilimanjaro  na  kupata  elimu  yake  ya  msingi  katika  shule  ya  msingi  Mawenzi  huko huko  Moshi.Baadae  alipata  elimu  ya  sekondari  katika  shule  ya  sekondari  Magreth  Ekenywa  iliyopo  jijini  Arusha  na  inasemekana  aliendelea  na  masomo  nchini  Kenya…..
Rekodi  zinaonyesha  kuwa  alitua  jijini  Dar  kati  ya  mwaka  2005  na  2007  akiwa  na  jukumu  moja  tu  la  kusaka  pesa.Kama  ilivyo  ada  kwa  jamii  ya  watu  wa  kabila  lake  baada  ya  kufika  jijini  Dar  hakulaza  damu, fasta  alicheki  michongo  ilipo  na  kuanza  kuifanyia  kazi..
Kujulikana  kwake  kulianzia  pale  alipoanza  kupita  mitaani  akitembeza  bidhaa  za  mikononi  na  kuziuza  kwa  bei  ya  promosheni. Hakuna  aliyejua  machina  Wolper  angekuja  kuwa  bonge  la  staa  nchini  Tanzania…
Ni  kipindi  hiki  ambacho  wanaume  walimchukulia  poa  na  kumpita  bila  hata  salamu kama  vile  wafanyavyo  kwa  kina  dada  wanaotembeza  bidhaa  za  mikononi.Ni  wanaume  wachache  sana  ndo  waliweza  kugundua  uzuri  wa  Wolper  na  kumtupia  maneno  mawili  matatu  yenye  ushawishi  wa  ngono….
Baadae  aliingia  kwenye  biashara  za  Saluni  maeneo  ya  Tandale  jijini  Dar  kabla  ya  kujiingiza  kwenye  sanaa  ya  uigizaji….
Kipindi  flani  Wolper  akiishi  maeneo  ya  Mwenge  alikutana  na  mtu  mmoja  wa  kabila  lake  aliyefahamika  kwa  jina  la  Injia  Macha  ambapo  jamaa  huyo  alianzisha  utani  wa  kumuita  mjomba  lakini  baadaye  ujomba  ukapitiliza  na  akaanza  kuomba  kulila  tunda….
Inasemekana  kwamba  jamaa  alifanikiwa  kulila  tunda  kwa  kipindi  kirefu  na  aliponogewa  alimuhamisha  Wolper  toka  Mwenge  alikokuwa  akiishi  na  dada  yake  na  kumpangishia  chumba  cha  kwanza  maeneo  ya  Sinza  Mori….

Injinia  huyo  alimpatia  Wolper  gari  chakavu  aina  ya  Toyota  Celica  ambapo  baada  ya  siku  kadhaa  Wolper  aliipiga  bei  gari  hiyo…..

Akiwa  mitaa  ya  Sinza ndipo  akakutana  na  mwanadada  Lucy  Komba  ambaye  ni  msanii  wa  filamu  aliyemshawishi  kujiingiza  katika  tasnia  hiyo….Kipindi  hicho  ilikuwa  ni  mwaka  2009.

Baada  ya  kupata  mtonyo  wa  Movie, Wolper  aliuchangamkia  na  kwa mara  ya  kwanza  akaonekana  katika  filamu  ya  ‘Ama  Zangu  Ama  Zao’  iliyofanywa  na  mwanadada  Lucy  Komba…

Baada  ya  hapo  alianza  kupata  mialiko  toka  kwa  watu  mbalimbali  ili  aweze  kuigiza  kwenye  filamu  zao.Alifanikiwa  kukutana  na  Director  mkongwe,William  Mtitu  na  marehemu  Steven  Kanumba  na  kufanya  filamu  mbalimbali  zilizomjengea  jina  katika  tasnia  hiyo….

Baada  ya  kuanza  kupata  mafanikio, Wolper  alizinguana  na  Injia  Macha  ambaye  alikuwa  amempatia  gari  nyingine  aina  ya  Toyota  GX  100….

Mgogoro  mkubwa  uliibuka  kiasi  cha  Injia  Macha  kuwatumia  polisi  kumnyanga’anya  gari  hilo  Wolper.Polisi  walimkuta  akiwa  na  gari  hilo  maeneo  ya  Ilala  ambapo  alielezwa  kuwa  gari  hilo  linatafutwa  na  mwenyewe  na  lina  kesi  katika  kituo  cha  polisi  Oysterbay.

Wolper  akiwa  hajui  kama  mchongo  huo  ume injiniwa  na  Injia  Macha  alitaka  kuwavimbishia  kifua  maafande  akidai  kuwa  gari  hilo  alinunuliwa  na  mjomba  wake na  kadi  anazo.Lakini  alijikuta  akigonga  mwamba  kuondoka  na  gari  hilo  pale  polisi  walipomtaka  waende  kituoni  kulihifadhi  gari  hilo  kisha  akamlete  huyo  mjomba  wake  pamoja  na  kadi  za  manunuzi  ya  gari  hilo…

Wapekenyuzi  wanaeleza  kuwa  kipindi  hicho  tayari  Wolper  alikuwa  na  bwana  mwingine  na  Injia  Macha  alishaushtukia  mchongo  na  ndio  sababu  alimfanyia  umafia  bila  Wolper  kujua….

Wolper  akaingia  mkenge, akamshtua  bwana’ke  mpya  kuhusu  polisi  wanachotaka  kukifanya.Bwana’ke  akamwambia  asijali, wakutane  Oysterbay  Polisi  ili  akalichukue  hilo  gari  mbele  ya  maafande….

Kilichotokea  ni  kwamba  baada  ya  Wolper  kufikia  kituo  cha  Polisi  alivutwa  sikio  na  afande  mmoja  kwamba  Injinia  Macha  yupo  kituoni  hapo  na  anawasubiri  kwa  hamu  yeye  na  bwanake  waje  na  documents  za  umiliki  wa  gari  hilo  hali  iliyomfanya  Wolper  aingie  mtini….

Inasemekana  kuwa  kama  bwana  mpya  wa  Wolper  angetokea  kituoni  hapo  angetiwa  ndani  yeye  na  Wolper  kwa  kesi  ya  wizi  wa  gari  lakini  machale  yakawacheza  wakalala mbele…..

Baadaye  Wolper  alisikika  kupitia  Radio  Clouds  FM akitangaza  kuwa  amedhulumiwa  gari  na  mjomba  wake  ambaye  alimuongezea  pesa  kidogo  katika  manunuzi  ya  gari  hilo  lakini  baadaye  akawa  anamtaka  kimapenzi  na  kumzushia  kwamba  amemuibia  gari. Huu  ndo  ukawa  mwisho  wa  Wolper  na  Injia  Macha.

Baada  ya  kutemana  na  Injia  Macha, Wolper  alipitia  kwenye  mikono  mingi  ya  kimahusiano  lakini  uhusiano  mwingine  uliompandisha  chati  ni  ule  wa  Abdallah  Mtoro  almaarufu   Dallas….

Dallas  akiwa  hana  jina  la  kutosha  ndani  ya  jiji  la  Dar  es Slaam, ghafla  alikuwa  maarufu  baada  ya  kutangaza  ndoa  na  Wolper  na  hasa  pale  alipompatia  kiasi  cha  Dolla  elfu  10 ( Tsh 16 Milioni)  akampatie  marehemu  Sajuki  kwa  ajili  ya  matibabu. Kitendo  hicho  kilimfanya  Wolper  awafunike  mastaa  wote  wa  kike  akiwemo  Wema  Sepetu……

Hata  hivyo  mahusiano  ya  Dallas  kwa  Wolper  yalijaa  utapeli  mwingi  kwani  wakiwa  bado  hawajafahamiana  na  Dallas  ambaye  inasemekana  ni  mfanyabiashara  wa  ‘Sembe’  alimuingia  kimafia  Wolper  na  kufanikiwa  kumteka  kimapenzi  hadi  akafunga  naye  ndoa…..

Umafia  alioufanya  Dallas  ni  pamoja  na  kumpenyezea  vitu  vya  thamani  kama  vile  magari  ya  kifahari  na  pesa  za  matumizi.

Kwa  kuwa  Wolper  tangu  anatoka  Machame  alijua  anakuja  mjini  kutafuta  pesa, hakupoteza  muda  kutaka  kujua  mambo  mengi  kuhusu  Dallas. Alichoaangalia  ni  Dallas  amekuja  na mkono  gani?  Mkono  mtupu, mkono  wa  birika  au  mkono  wa  madini?



Alipogundua  kwamba  jamaa  alikuwa  na  madini  ya  kutosha  akajitoa  mzima  mzima  na  kumkabidhi  Dallas  moyo  wake  wote , mwisho  wa  siku  akajikuta  akiumbuka  na  kuambulia  maumivu  baada  ya  kumtambua  Dalls  ni  mtu  wa  namna  gani.

Hamisa: Siwezi Kushea Penzi la Diamond na Wema Sepetu

$
0
0
Kiapo:Modo maarufu Bongo, Hamisa Mobeto amefunguka kuwa katika maisha yake, kamwe hawezi kushea penzi na mwigizaji Wema .
Modo maarufu Bongo , Hamisa Mobeto.
Hamisa alisema watu wamekuwa wakimkosea kumtaja kuwa anaweza kutoka na Diamond Platnumz wakati hawezi kufanya hivyo hata iweje !

“Siwezi kushea penzi na Wema hata siku moja, niaminini, nina maisha yangu mengine kabisa wapo wanaoweza kufanya hivyo lakini si mimi , ” alisema Hamisa .

Tatizo la Vodacom (M-PESA) Laua Lushoto

$
0
0
Taarifa zilizonifikia toka Gare LUSHOTO, ni kuwa mama mmoja amefariki dunia kwa kukosa usafiri ulikotana na ukosefu wa fedha japo alikuwa alikua nazo kwenye Simu
M-Pesa (VODACOM).

Itakumbukwa kuwa huduma ya M-PESA haipatikani toka jumamosi iliyopita hadi hivi sasa!!!

SWALI KWA VODACOM;

-Hamuoni mmemleta madhara makubwa kwa wateja wenu?

-Tatizo ni nini ilihali nyie mko kimya na haijawahi kutokea tatizo lika-persist namna hii?

-Fedha za wateja ziko salama?

-Mtamsaidiaje au kumfidiaje mteja wenu alieathirika kama familia ya marehem mteja wenu huyu?

Sikiliza na Download Wimbo Mpya wa Ali Kiba na Abdul Kiba-Pita Mbele

$
0
0

Wimbo huu ulianza kuzinduliwa siku ya Jumapili ndani ya New Maisha Club wakati ndugu hawa walipokua wakifanya show,mashabiki wao walishangilia sana wakati wimbo huu ulipokua unaimbwa,Wameamua kuuachia rasmi hapa unaweza kuusikiliza na kuudownload,wimbo unaitwa Pita Mbele.
Bonyeza play kusikiliza.

Chenge: Serikali Imekosa Ubunifu Vyanzo vya Mapato

$
0
0
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti, Andrew Chenge amesema Serikali imekosa ubunifu na haitaki kupokea ushauri kuhusiana na vyanzo vipya vya mapato.

a uchumi kwa mwaka 2013, Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa mwaka 2014/15 pamoja na utekelezaji wa Bajeti kwa mwaka 2013/14, Chenge alisema kuongeza ushuru katika bia, soda, juisi na vinywaji vikali, kumepitwa na wakati.

Wakati Chenge akieleza hayo, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni imetaja vyanzo mbadala vya mapato vinavyofikia Sh6 trilioni.

Katika taarifa yake, Chenge alisema mpaka mwisho wa mwaka wa fedha 2013/14, Bajeti ilikuwa pungufu kwa Sh2 trilioni, huku Bajeti ya mwaka 2014/15 ikiongezeka kwa asilimia 8.8 (trilioni 1.6), huku ikiwa na deni la Sh1.3 trilioni ambalo halikuingizwa katika Bajeti ya mwaka 2014/15.

“Hali hii inaweza kutafsiriwa kuwa Bajeti ya mwaka 2014/15 tayari ina pengo la Sh4.9 trilioni. Yaani Sh2 trilioni ambazo hazikupatikana mwaka wa fedha 2013/14 na Sh1.6 trilioni ambayo imeongezeka ikilinganishwa na bajeti ya mwaka jana na deni la Sh1.3 trilioni.

“Kuna umuhimu wa kuharakishwa kuletwa bungeni sheria ya bajeti itakayofanya kazi sambamba na sheria mpya ya ununuzi ili kudhibiti matumizi mabaya kwa nia ya kuweka nidhamu katika utekelezaji wa bajeti ya Serikali,” alisema Chenge.

Alisema wakati Serikali ikiwa haina vyanzo vya uhakika vya mapato, Deni la Taifa lililofika Sh30 trilioni sawa na asilimia 57 ya pato la taifa ni mzigo wa taifa na tishio kwa utengamavu wa uchumi jumla.

“Uwiano uliopo wa Deni la Taifa na Pato la Taifa kiuchumi siyo wa kuridhisha. Ukubwa wa deni hili hauwiani na kiwango cha uzalishaji mali na ukuaji wa uchumi wa sasa wa asilimia 7.0,” alisema na kuongeza:

“Yalifanyika manunuzi ya Dola za Marekani 810,000 katika Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) ambayo hayakupata kibali cha Mlipaji Mkuu wa Serikali.”

Alisema tatizo la kutokusimamia kwa umakini matumizi ya Serikali lilisababisha Bajeti ya mwaka 2013/14 kuanza na deni Sh611.4 bilioni, ambazo ni matumizi ya mwaka wa fedha 2012/13 na kwamba deni hilo halikuingizwa kwenye bajeti ya 2013/14... “Hali hii inatarajiwa pia kujitokeza tena kwa kiwango kikubwa zaidi kwenye bajeti ya mwaka 2014/15. Malimbikizo ya madai hayo hadi Desemba 2013, yalifikia Sh2 trilioni sawa na asilimia nne ya pato la taifa. Tatizo hili ni lazima litafutiwe dawa haraka,” alisema Chenge.

Alisema ongezeko la Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2014/15 kwa Sh1.605 trilioni, ikilinganishwa na Bajeti ya Serikali inayomalizika ya mwaka 2013/14 linatia shaka iwapo malengo ya ukusanyaji na matumizi yatafanikiwa.

Alisema katika mwaka wa fedha 2013/14 utekelezaji wa bajeti katika baadhi ya mafungu ulifanyika kinyume na matarajio ya Serikali, kwa maelezo kuwa yapo baadhi ya mafungu ambayo hayakutengewa fedha lakini walipewa fedha nje ya bajeti za fungu husika.

Wakenya Ombeni Msamaha Alshabab ni Habari Nyengine

$
0
0
Ombeni msamaha na mkae meza Moja kudhungumza kuhusu kuyatoa majeshi yenu Somalia mambo yaishe hamna uwezo wakukabiliana Na Alshabab. Kwani ni nyinyi mloanza kuingia Somali na kuuwa wanawake na watoto wa kisomali bila hatia yoyote
Ushahidi kwamba Alshabaab hamuwawezi ni tokeo la Westgate ambapo vijana wanne tu waliwashinda Jeshi zima la Kenya pamoja na Vifaru vyao, ushahidi mwengine ni tukio la juzi, shambulio lilianza saa mbili usiku hadi saa nne Mabenki,Mahoteli,Vituo vya polisi vilihusika,Jeshi la Kenya liliwasili eneo la tukio masaa matano baada ya tukio
Huu ni ushahidi tosha kwamba Jeshi la Kenya liliwakwepa wapiganaji Wa Alshabaab
Hamuwawezi,mnawaogopa,hamjiami ni OMBENI MSAMAHA NA KUTOA MAJESHI YENU SOMALIA HARAKA muwanusuru raia wasio na hatia.

Watoto Pacha Kufanyiwa Operesheni Nyingine Kuwekewa Njia ya Mkojo ya Kawaida

$
0
0
Watoto pacha waliotenganishwa, Eliud na Elikana watafanyiwa upasuaji mwingine ili kuwatengenezea njia ya mkojo ya kudumu.

Pacha hao walizaliwa wakiwa na njia moja ya haja kubwa na ndogo, hali iliyowapa wakati mgumu madaktari wakati wa operesheni ya kuwatenganisha.

Akizungumzia hali ya Eliud baada ya kufanyiwa upasuaji wa kurejesha utumbo wake ambao ulijitokeza, Mkuu wa Kitengo cha Upasuaji wa Watoto, Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Dk Zaituni Bokhary alisema hali yake inazidi kuimarika.

Alisema pia kuwa, wiki hii watamfanyia upasuaji Elikana ili kuirudisha ndani sehemu ndogo ya utumbo wake ambayo nayo ilikuwa nje. Baada ya kukamilika kwa upasuaji huo, tatizo la njia ya haja kubwa itakuwa imetatuliwa kama ilivyo kwa mwenzake.

Dk Bokhari alisema baada ya kupona, watoto hao watafanyiwa upasuaji mwingine ili kurekebisha njia zao za mkojo na kuzifanya za kudumu. Alisema kwa sasa wanatumia njia za haja ndogo walizotengenezewa kwa ajili ya kutumika kwa muda mfupi.

Alisema kabla ya upasuaji wa kuwatenganisha, pacha hao walikuwa na njia moja ya mkojo pamoja na uume mmoja. Hata hivyo, njia ya mkojo ilikuwa chini ya korodani badala ya kupita katika uume.

“Baada ya miezi mitatu, watafanyiwa upasuaji mwingine ili kuziba tundu la njia ya mkojo na kuwatengenezea njia nyingine ya kawaida,” alisema na kuongeza kuwa tatizo hilo linawakumba hata watoto wengine nchini.

Baba wa watoto hao, Eric Mwakyusa alisema Eliud anaonekana mwenye furaha baada ya operesheni hiyo tofauti na alivyokuwa awali utumbo wake ulipokuwa umejitokeza nje.

Pacha hao walipelekwa India mwaka jana kwa ajili ya upasuaji mkubwa wa kuwatenganisha ambao ulifanikiwa. Hata hivyo, sehemu ya utumbo mpana wa Eliud ilijitokeza nje kabla ya kufanyiwa upasuaji mdogo hivi karibuni.

Waliofanyishwa Ngono na Mganga wa Kienyeji Wengi ni Wake wa Vigogo

$
0
0
Stori: Makongoro Oging’ na Haruni Sanchawa
IMEBAINIKA kuwa miongoni mwa wale wanawake 20 waliodai kufanyishwa ngono na waganga wa kienyeji ‘sangoma’ ili kupata ujauzito  baada ya kukaa  muda  mrefu  bila watoto,  wamo wake wa vigogo Bongo, Uwazi limechimba.

Uchunguzi uliofanywa na waandishi wetu kwa baadhi ya wanawake  hao umebaini kuwa,  waume wao wanafanya kazi  katika nyadhifa za  juu serikalini, wengine ni wastaafu  na kwamba waume hao  hawajui kinachoendelea.

Kwa mujibu wa mwanamke mmoja (jina lipo), katika sakata hilo kuna wake wa maprofesa, kanali mstaafu wa JWTZ na mmoja ambaye mume wake aliwahi kuwa kamanda wa polisi wa mkoa (RPC) ambaye kwa sasa naye ni mstaafu.

Mwanamke huyo alizidi kudai kuwa, ndoa moja katika hizo ilivunjika baada ya mume kubaini kuwa, mkewe alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mmoja wa sangoma hao.

‘KUFULI’ ZILISHATUMIKA
Uchuguzi zaidi ulibaini kuwa zaidi ya nguo za ndani  ‘kufuli’ za  wanawake zaidi ya 20 zilizokutwa  na polisi  kwa sangoma hao maeneo ya Tandika jijini Dar es Salaam zilikuwa zimeshavaliwa hivyo hakukuwa na mpya jambo lilionesha kuwa, zilivuliwa wakati wa tukio linalodaiwa lilikuwa na kutengezea dawa.

KWA NINI WALITOA TAARIFA POLISI?
“Sisi tuliamua kutoa taarifa polisi kwa sababu tumekuwa tukifanya ngono na wale waganga kwa muda mrefu bila kupata ujauzito na mbaya zaidi tulishatumia mamilioni ya pesa  baada ya kuuza mali zetu, zikiwemo nyumba,” alisema mwanamke huyo nje ya kituo cha polisi.

Wanawake hao ambao hawakupenda majina yao  yatajwe kwa kuhofia waume zao kujua, walisema  ni  kweli baadhi yao wamekaa katika ndoa kati ya miaka nane hadi  10 bila kupata watoto wala mimba zilizoharibika.

Hata hivyo, baadhi yao walirudishiwa fedha zao baada ya Kamanda Kiondo kuwabana waganga hao.

KAULI YA RPC
Wiki iliyopita Jeshi la Polisi Mkoa wa Temeke chini ya Kamanda, SACP Englibert Kiondo liliwatia nguvuni sangoma wawili wakiwa na matunguli na zana nyingine za kuagulia binadamu.

Vitu hivyo viliteketezwa moto kwenye Kituo cha Polisi Temeke mbele ya  waandishi wa habari.
“Ninaamini kuwa kwa vitendo  hivyo  vya kujamiiana ni hatari na huu ni ubakaji, kwani kuna uwezekano wa kuambukizana maradhi  mbalimbali ikiwemo  Ukimwi, kwa hiyo hizi zana nazichoma moto,” alisema  Kamanda Kiondo.

Waliokamatwa katika zoezi hilo ni Juma Mohamed (32) na Abdallah Musa (25) ambao wote kwa pamoja wanashikiliwa na jeshi hilo.
GPL

Audio: Dayna Nyange afunguka kuhusu uhusiano wake na Nando

$
0
0
Mwimbaji wa Nivute kwako Dayna Nyange amezungumzia uhusiano wake na mshiriki wa Big Brother Africa, Ammy Nando baada ya kuonekana katika picha kadhaa wakiwa katika poz tata.


Dayna amefunguka jana kupitia The Jump Off ya 100.5 Times Fm na kueleza ukaribu wao na kinachoendelea.

“Jamani Nando ni rafiki yangu, hakuna kitu serious,  he’s just a friend tu basi.Sijui nisemeje, ni watu ambao tumefahamiana si kwa muda mrefu sana lakini tumeshibana so imekuwa hivyo tumekuwa karibu mara kadhaa. Haipiti muda mrefu bila kuonana kwa hiyo mara nyingi tunakuwa wote. Ninamkampani kwenye issue zake na yeye ananikampani pia mimi, ni watu ambao tumekuwa karibu sana kwa kweli.” Dayna ameiambia The Jump Off ya Times Fm.

Alipoulizwa kuhusu picha zao zinazoonekana kwenye Instagram ambazo zinaongea zaidi ya urafiki, alifunguka:

“Yeah...sasa mtu na rafiki yake si mnapiga picha mnakuwa free jamani…hivyo (kicheko).”

Hata hivyo, Dayna amesema kuna kitu ambacho wanakifanya pamoja na kitakapokuwa tayari watu watafahamu.

Ufalme Wamtaka Museveni Kuomba Msamaha kwa Kumuita Mfalme Mtoto

$
0
0
Ufalme wa kitamaduni wa Tooro nchini Uganda, umemtaka Rais wa Uganda Yoweri Museveni kumuomba msamaha mfalme wao na kuondoa matamshi yake ambapo alimuita mfalme huyo mtoto.
Taarifa hii ni kwa mujibu wa jarida la Uganda la The observer.

arida hilo liliripoti kuwa waziri mkuu wa ufalme wa Tooro, Minister Steven Kaliba, alionya ikiwa Rais Museveni hatoomba msamaha matokeo yake yatakuwa mabaya.
Hata hivyo waziri huyo amekanusha madai hayo.
Mfalme wa Tooro ana umri wa miaka 22 pekee na anajulikana kama Omukama Oyo. Rais Museveni alimuita mfalme huyo 'Akavuka ke Tooro' ikitafsiriwa kwa kiengereza kama kusema 'Kijana huyu wa Tooro.
Jarida la Observer limedai kuwa mfalme huyo anatishia kususia chakula kutokana na kile anachosema ni njama ya Rais Museveni kuvunja ufalme wa Tooro.
Mfalme Oyoo ni mfalme mdogo zaidi wa ufalme wa kijadi kwa Umri nchini Uganda
Ufalme hata hivyo, umekanusha madai hayo katika taarifa yake ukisema kuwa Mfalme huyo atafunga kula mwezi ujao kwa sababu za kitamaduni na kidini.
Ufame umesema kuwa sio mara ya kwanza kwa mfalme wa Tooro na familia yake kufunga kukula , ukisema kuwa wao hufanya hivyo kila mwaka akitaka kumuomba Mungu kumpa mwongozo katika utawala wake.
Kadhalika ufalme huo umekana kuwa mfalme anafunga kukula kwa sababu ya matatizo ambayo ufalme huo unakumbwa nayo.
Ufalme huo umesema kuwa umekasirishwa sana na matamshi ya Rais Museveni kumuita mfalme kama kijana ukisisitiza kuwa umri, rangi na muonekanao wa mfalme Oyo Nyimba Kabamba sio wa kuzungumziwa hadharani.
Licha ya kwamba kila mtu anaweza kutoa maoni yake kuhusu swala lolote, ufalme umetaka kumjulisha Museveni kuwa mfalme huyo ni fahari ya watu wa Tooro na kwamba awe mtoto au mtu mzima anajulikana tu kama mfalme.
Umemtaka Rais Museveni kukumbuka kuwa yeye ni mlinzi na kiongozi anayepaswa kutunzwa na jamii

Okocha amlaumu kocha wa Nigeria

$
0
0
Nahodha wa zamani wa timu ya taifa ya Nigeria, Jay-Jay Okocha amemlaumu kocha wa timu hiyo kwa matokeo mabomu ya timu ya Nigeria iliyocheza dhidi ya Iran Jumatatu.
Timu hizo zilicheza mechi ya kwanza ya sare tasa katika michuano hiyo nchini Brazil.

"mechi hii ilipaswa kuwa ya ushindi wa Nigeria lakini hatukujitosa kimasomaso kushinda. Hatukufanya vyema , tulishindwa kabisa,'' alisema Okocha.
"Keshi hakufanya kazi ya kutosha kuanda timu. Mchezo wao haukufana hata kidogo Keshi anapaswa kuwajibika,'' aliongeza kusema Okocha
Mechi kati ya Nigeria na Iran haikuwa na msisimuko kama mechi zengina ambazo zimechezwa kufikia sasa.
Okocha, ambaye yuko kwenye kamati ya timu ya taifa ya Nigeria, alionekama kukosoa sana uamuzi wa Keshi kuhusu wachezaji walioshirikisha timu ya taifa.
Alielezea kutofurahishwa, zaidi na kocha kwa hatua yake ya kumuondoa uwanjani mchezaji wa Liverpool,Victor Moses katika kipindi cha pili, na kumbadilisha na Shola Ameobi, ambaye aliondoka Newcastle msimu huu.
"Osaze (Peter Odemwingie) alikuwa na mchezo mzuri alipoingia uwanjani na tulihitaji acheze zaidi,'' alisema mchezaji huyo wa zamani.
Jonathan Akpoborie, ambaye ni mchezaji wa zamani, pia alihisi kuwa Super Eagles walikosa mwelekeo katika mchezo wao.
''Ninaamini kuwa pia tulipoteza mweleko katika mchezo wetu na tukaanza kucheza mipira ya mbali , mchezo ambao sio kawaida yetu, '' alisema Okocha
Mechi itakayofuata katika kundi F itachezwa Jumamosi dhidi ya Bosnia-Hercegovina, walioshindwa katika mechi yao ya ufunguzi kwa mabao 2-1

Hatimaye Mume wa FLORA MBASHA akamatwa na kutupwa rumande

$
0
0
MSANII Emmanuel Mbasha (32) na mume wa Mwimbaji wa Injili, Flora Mbasha, amefikishwa  Mahakama ya Wilaya ya Ilala akikabiliwa na mashitaka mawili likiwemo la ubakaji.
Mshtakiwa huyo ambaye ni mfanyabiashara na mwimbaji alisomewa mashitaka yake mbele ya Hakimu Mkazi Wilberforce Luago.

Wakili wa Serikali Nassoro Katuga alidai kuwa mshtakiwa alitenda makosa hayo mawili maeneo ya Tabata Kimanga, jijini Dar es Salaam.

Katuga alidai katika shitaka la kwanza kuwa, Mei 23, mwaka huu eneo la Tabata Kimanga, Wilaya ya Ilala, jijini Dar es Salaam,  kinyume cha sheria huku akijua ni kosa alimuingilia kwa nguvu msichana anayedaiwa kuwa shemeji yake (jina limehifadhiwa).

Katika shitaka la pili, ilidaiwa kuwa Mei 25, mwaka huu eneo la Tabata Kimanga, jijini Dar es Salaam, kinyume cha sheria, mshtakiwa alimuingilia kwa nguvu  mfanyakazi wake (jina limehifadhiwa).

Hata hivyo, mshtakiwa alikana mashitaka hayo .Upande wa Jamhuri ulidai kuwa hauna pingamizi la dhamana.

Hakimu Luago alitaja masharti ya dhamana kwa mshtakiwa kuwa na wadhamini wawili, mmoja awe mtumishi wa serikali na mwingine kutoka taasisi inayotambulika watakaosaini hati ya dhamana ya Sh. milioni 5.

Mshtakiwa alishindwa kutimiza masharti ya dhamana hivyo alipelekwa rumande na kesi iliahirishwa hadi Juni 19, mwaka huu itakapotajwa.

Mbasha akiwa chini ya ulinzi wa askari polisi alisindikizwa katika basi la Jeshi la Magereza kwa ajili ya kwenda kuanza maisha mapya mahabusu ya Keko, jijini Dar es Salaam.

Akimbiwa na Mkewe baada ya madaktari kuupunguza uume wake kwa bahati mbaya

$
0
0
Madaktari nchini Canada wameingia katika matitizo makubwa baada ya kukosea na kumkata mwanaume mmoja sehemu ya uume wake na kupunguza kwa urefu wa inch 1 (sentimeta 2.5).

Kwa mujibu wa QMI la Canada, mwanaume huyo anadaiwa kufika hospitali akihitaji matibabu baada ya kuumia bahati mbaya wakati wa tendo la ndoa na kupata mshituko hivyo kulazimika kufanyiwa upasuaji ili kumsaidia kuituliza mishipa iliyokuwa hatarini.

Lakini baada ya kumaliza tiba aligundua kuwa amekatwa sehemu ya uume wake na madaktari wakadai ilikuwa bahati mbaya.

Kufuatia tukio hilo, anadai alishindwa kufanya mapenzi kwa muda wa miaka miwili hivyo mke wake ambaye jina lake halikutajwa na vyombo vya habari vya Canada, aliamua kuachana nae

Uamuzi wa mwanamke huyo ulimvuruga zaidi mwanaume huyo ambaye ameamua kufungua mashitaka dhidi ya madaktari waliomfanyia upasuaji.

Mwanaume huyo anadai fidia ya $155, 000 kwa uzembe uliofanywa na madaktari hao kwa kuwa inaelezwa hawakufuata taratibu zote za awali kabla ya kumfanyia upasuaji.
“Hii imenifanyia madhara makubwa katika maisha yangu zaidi ya siku niliyoumia miguu yangu na kushindwa kutembea.”

Matokeo ya Mechi za Jana Kombe la Dunia

$
0
0
Kwenye game zilizochezwa usiku wa June 17 2014 matokeo yake ni Russia 1 (Kerzhakov 74′ ) – 1 Korea Republic goli lao lilifungwa na K Lee kwenye dakika ya 68.
Game nyingine ilikua ya Brazil vs Mexico iliyoisha kwa 0-0 huku ile ya nyingine ya mwanzo ikiwa ni Belgium 2 ( Fellaini 70′ + Mertens 80′) – 1 Algeria (Feghouli aliefunga kwa penati dakika ya 25 )

UPDATE: Majina ya Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga Kidato cha Tano mwaka 2014

$
0
0
Nafasi za kujiunga na kidato cha tano mwaka 2014  kwa wanafunzi waliomaliza mwaka jana zimetangazwa rasmi muda huu jijini dare s salaam na naibu waziri wa TAMISEMI  Bw KHASIM MAJALIWA  ambapo zaidi ya wanafunzi 16800 wamekosa nafasi hizo kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo upungufu wa shule za kidato cha tano….

Akitangaza majina na shule walizopangiwa wanafunzi hao Mh MAJALIWA amesema kuwa jumla ya wanafunzi 54085 sawa na alimilia 75.61 ya wanafunzi 71527 waliostahili kuingia kidato cha tano mwaka huu wamechaguliwa huku wavulanai ni 31352 wakati wasichana ni 22733 ambapo ni sawa na ongezeko la wanafunzi 20402 kwa kulinganisha na wanafunzi 33683 walochaguliwa mwaka jana

Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na shule mbalimbali wataanza kuripot katika meneo yao tarehe 10 julai mwaka huu ambapo mwisho wa kufika katika shule walizopangiwa ni tarehe 30 julai mwaka huu ambapo amesema kuwa kwa wale ambao watakuwa hawajaripot hadi tarehe hiyo nafasi zao zitajazwa na waliokosa nafasi.
——————————————–
Majina  ya  Wanafunzi  waliochaguliwa  kujiunga  Kidato  cha  Tano  mwaka  2014
1. Wasichana — Shule Zote  << BOFYA  HAPA>>

2. Wavulana — Majina ya Shule A Mpaka L    << BOFYA  HAPA>>

3 .Wavulana — Majina ya Shule M mpaka Z      << BOFYA  HAPA  >>

Majibu ya Ridhiwani Kikwete kuhusu NEC na kwa wanaosema anamiliki vituo vya mafuta.

$
0
0
Inawezekana hili likawa moja kati ya maswali uliyonayo na hujawahi kupata nafasi ya kumuuliza muhusika au inawezekana ikawa ni ishu ambayo umewahi kuisikia au kuisoma kwenye chombo chochote cha habari.
Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete ambae ni mtoto wa Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete kwenye exclusive interview na millardayo.com anasema >>> ‘kuwa mtoto wa Rais changamoto kubwa ambayo nimeiona mojawapo ni watu kukupa tafsiri ya vitu vingine ambavyo wewe huvijui, kumekua na malalamiko mengi sana kwamba huyu jamaa ana mali hizi na hizi’
‘Wanasema kampuni za mafuta, Oil Com, Camel Oil na Lake Oil ni za kwangu, sasa unajiuliza huyo mtu ambae anaweza akatengeneza kampuni tatu zinazofanya shughuli moja kwa nini asianzishe kampuni moja ikawa kubwa zaidi ?? kwa hiyo kumekua na manenomaneno mengi, hizo ni changamoto mfano kwenye siasa huku, watu wengi aidha hawajui nimetokea wapi au wanajitoa akili katika maana kwamba hawataki kujua nimetoka wapi’

‘Kuna kipindi unaweza ukashangaa Mwandishi wa habari anachukua kalamu anaandika maneno mpaka unashangaa kayatolea wapi? sitaki kuamini kwamba Mwandishi unaweza kuandika kwamba Ridhiwani kapata UNEC kwa sababu ya baba yake, ungechukua muda ukamsoma Ridhiwani vizuri ukauliza watu waliokaa na Ridhiwani, uliza huyu ameshawahi kuwa kiongozi??’
‘Wako watu ambao kwa kuwa wamemjua Ridhiwani baada ya Jakaya Kikwete kuingia Ikulu basi nao wanaanzia hapohapo Ikulu lakini hawajui Ridhiwani kabla ya baba yake hajawa Ikulu alikua anaishije, mimi nimekua naishi maisha ya kawaida nimekaa boarding school nimesoma Mkwawa baba yangu akiwa Waziri, nilikua na uwezo wa kwenda kusoma Ulaya lakini nimesoma chuo kikuu Dar es salaam pale japo nilikua na uwezo wa kwenda popote pale ninapotaka ila ni kwa sababu tu mzee wangu alitaka kuona naishi kama watu wengine’

Rihanna Anamzimikia Mchezaji wa Ghana Huko Brazil

$
0
0
Rihanna anamzimikia mchezaji wa Ghana, Kevin-Prince Boateng.

Da Bae doe! I might have to be team Ghana on this one idc idc idc pic.twitter.com/3GDQPU5KGe

— Rihanna (@rihanna) June 16, 2014

Kupitia Twitter, Rihanna alisema kuwa kutokana na mchezaji huyo anayekipiga pia FC Schalke 04, alijikuta akiwa shabiki wa Ghana ilipokuwa ikicheza na Marekani jana.

Hata hivyo huenda Riri aliangushwa na timu hiyo baada ya kufungwa bao 2-1.

Exclusive: Meninah asimulia Jinsi Alivyolazimika Kulipa Gharama za Kununua Gari Jipya Baada ya Kuunguza gari Akishoot Video Kenya

$
0
0
Muimbaji wa kundi la Shosteez, Meninah Atick, amesema alilazimika kulipa gharama za kununua gari jipya baada ya kuunguza kwa moto gari lililokuwa limeegeshwa jirani na eneo walilokuwa wakishoot video ya wimbo wake ‘Kakopi Kapesti’ jijini Nairobi, Kenya.

Meninah amesema video ya wimbo wake huo imefanywa na Isaac, aliyeongoza video ya Prezzo ya wimbo wake ‘My Gal’. Amesema katika scene ambayo walikuwa wakihitaji moto, muongozaji aliandaa mapipa ya moto huku wakichukua tahadhari ya kuwa na fire extingusher kama lolote lingeweza kutokea.

Wakati wakishoot, walisikia mlipuko mkubwa wa moto uliosababishwa na mafuta yaliyokuwa yamewekwa pembeni ya mapipa ya moto.

“Hatua kama thelathini kulikuwa na gari limeegeshwa, yale mapipa mawili yote yakaruka kutokana na ule mlipuko, ile gari ya watu ikaangukiwa na yale mapipa,” alisema Meninah. “Tulichanganyikiwa, japokuwa tulikuwa na kibali lakini ni tatizo tayari limetokea. Lile gari tunaliona linateketea, mimi nilikuwa nalia, sikutegemea kwasababu ni gari la watu.”

Amesema polisi walikuja kwenye eneo hilo na kuwaweka chini ya ulinzi. “Tuliambiwa ‘wote mikono juu’, pigeni magoti’. Tulienda chini huku roho zetu zikiwa na huzuni na uoga,” alisema Meninah.

Tukio amesema lilivutia umati mkubwa wa watu waliokuja kuangalia kilichotokea kwakuwa moshi mzito ulikuwa umetanda angani. Walikaa chini ya ulinzi wa polisi hao kwa zaidi ya saa sita huku meneja akijaribu kuongea nao bila mafanikio. Polisi hao walichukua baadhi ya vitu vyao muhimu kama vitambulisho kikiwemo chake.

Polisi hao waliwapeleka kituo cha jirani na muda huo ikiwa ni saa 12 alfajiri. Hatua iliyofuata ilikuwa ni kupiga simu kwa wazazi wake Tanzania kuwaeleza hali halisi na kuomba msaada. Meninah amesema pamoja na baba yake kuwa nje ya nchi, alifanikisha kuwatumia fedha ambazo walichanga na muongozaji ili wamlipe mmiliki wa gari lililoungua.

“Mungu ni mkubwa sana, alitusimamia, ile hela ikaingia, mmoja wetu akatoka na afande akaenda kuchukua na yule mwenye gari akapewa pesa yake nusu kwasababu director hakuwa na pesa muda huo.”

Hata hivyo Meninah amesema video ya wimbo huo imekamilika na inaweza kutoka siku yoyote.
Viewing all 104799 articles
Browse latest View live




Latest Images

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596344.js" async> </script>