Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104803 articles
Browse latest View live

Majambazi Wawili Wameuawa Jijini Dar es Dalaam na Wananchi Katika Tukio la Uporaji Eneo la Benki ya NMB Wilaya ya Ilala.

$
0
0
Watuhumiwa wawili wa ujambazi wameuawa jijini Dar es Dalaam na wananchi katika jaribio la kufanya tukio la uporaji katika eneo la benki ya NMB Wilaya ya Ilala.
Watuhumiwa hao wanadaiwa kuwa walikuwa wakijaribu kumpora mteja aliyekuwa ndani ya benki hiyo akichukua fedha kwa kutumia silaha mara baada ya kutoka ndani ya benki hiyo.
Kamishna wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alisema watuhumiwa hao ambao idadi yao haijafahamika walifika katika eneo la benki hiyo tawi la Uwanja wa Ndege wakiwa na pikipiki tayari kufanya tukio hilo.
“Hawa walikamatwa kufuatia taarifa kutoka kwa msiri kuwa kuna watu wenye pikipiki ambao wanahisi wanataka kufanya uhalifu. Polisi waliweka mtego nje ya benki lakini waliwashtukia polisi na kuanza kukimbia kila mmoja kwa njia yake,” alisema.
Alisema wakati wahalifu hao wakikimbia, mmoja alifyatua risasi kwa lengo la kupambana na askari, lakini askari hao walifyatua risasi juu kwa lengo la kumuamuru asimame.
“Walifanikiwa kumkamata na alipopekuliwa alikutwa na bastola aina ya Browing yenye namba 230787 iliyotengenezwa nchini Chekoslovakia ikiwa na risasi tatu. Hata hivyo wananchi waliokuwa wengi waliwazidi nguvu polisi wakamshambulia.
“Walimshambulia kwa mawe lakini polisi walifanikiwa kumuokoa na kumkimbiza hospitali lakini alifariki akiwa njiani,” alisema Kova.
Alisema jambazi mwingine ambaye alikimbilia katika eneo la Karakata, wananchi na askari walimkimbiza, lakini hakusimama hata askari walipopiga risasi juu kumtaka asimame.
Alisema baada ya polisi kuona mtuhumiwa huyo anakaidi agizo la kusimama, walimpiga riasasi miguuni na alianguka na kuishiwa nguvu kabla ya kufariki akiwa njiani kupelekwa hospitali.
Kova alisema baadaye jioni jana, watuhumiwa wengine watatu walikamatwa. Aliwataja kuwa ni Salum Seleman (28), Samwel Clips (32) na Said Salehe ambaye ni mganga wa kienyeji.
Alisema Seleman na Clips walikamatwa katika Kituo cha Polisi cha Stakishari baada ya kugundulika kuwa ni watuhumiwa wa ujambazi katika tukio hilo, ambalo wenzao waliuawa.
“Hawa walifika kituoni pale wakiwa wamebadili nguo na kujifanya ni wateja wa kawaida, lakini lengo lao ni kuangalia hatma ya wenzao, lakini waligundulika kuwa nao walishiriki na baada ya kuwakamata na kuwahoji wamekiri kuhusika na wao ndiyo walikimbia,” alisema.


Umeipata Hii ya Shilole Kutapeli Hela ya Samir wa Kinyulinyuli? Kisa ni Hiki.

$
0
0
Stori za mastaa wetu wa Tanzania kila kukicha kunakuwa na vitu vipya ambavyo vinajitokeza mara kwa mara,kupitia You heard ya June 16 Soudy Brown ameamplify taarifa ambazo inasemekana Samir wa Kinyuli nyuli alihitaji kuwatumia wacheza show(dancers) wa Shilole na baada ya kuelewana Shilole aliombwa kutumiwa Laki 2 ili awalipe hao wacheza show.

Sasa ishu imekuja baada ya Shilole kupewa zile pesa hakufanikiwa kuwapeleka wale dancers na kitu kinachozungumziwa na Samir na kuhusu pesa aliyopewa anahitaji kurudishiwa maana video waliyotaka kuifanya tayari imekwishafanyika.

Fanya Haya! Unapotokea Kumpenda Mtu aliye na Mpenzi Wake

$
0
0
Tumshukuru Mwenyezi Mungu ambaye ametuwezesha kuonana tena wiki hii tukiwa wazima. Lakini pia tumshukuru kwa kutuletea kitu kinachoitwa mapenzi. 

Mapenzi yamekuwa yakichukua nafasi kubwa sana katika maisha yetu ya kila siku na yamekuwa yakichangia kwa kiasi kikubwa furaha kwa kila mtu.

Kama huamini, angalia wale waliotokea kupenda na wao wakapendwa, utabaini nyuso zao zimetawaliwa na furaha isiyo na kifani. Lakini mapenzi hayo hayo yamekuwa ni chanzo cha vilio kwa baadhi ya watu.

Mpenzi msomaji wangu, kupenda hakuna macho! Moyo ukishapenda hausikii la kuambiwa. Katika hili ndiyo maana unaweza kumuona mwanaume kazimika kwa demu ambaye hawaendani kabisa lakini moyo wake ndiyo umeshapenda.

Ilishawahi kutokea msichana akampenda kijana mmoja ambaye ni fukara kupita maelezo. Yeye akawa ndiyo anamhudumia kwa kila kitu. Akamfanyia mpango wa ajira na mwisho wake wakafunga ndoa.

Sasa hivi wanaishi maisha ya furaha na amani. Wamegeuka mfano wa kuigwa kwa jinsi wanavyopendana lakini huko nyuma msichana huyo alikuwa akichekwa kwa kutoa penzi kwa mwanaume asiye na mbele wala nyuma.

Hayo ndiyo mapenzi jamani! Lakini pia katika kufurukuta kumtafuta mpenzi wa kuwa naye maishani, mwanaume anaweza kujikuta unaangukia kwa demu ambaye tayari ana mpenzi wake. 

Moyo wako unakuambia yeye ndiye mtu sahihi katika maisha yako lakini tayari ana mtu wake, unafanyaje? 

Utapambana kuhakikisha unapata kile ambacho moyo wako umekipenda au utakubaliana na ukweli kwamba huwezi kuwa naye kwa kuwa ana mtu wake? Inapofikia hatua hiyo unaweza kujikuta upo njia panda hasa pale ambapo huyo mwenye mtu wake naye anaonesha kuwa na chembechembe za mapenzi kwako.
Kuna mambo kadhaa ya kukusaidia kukabiliana na hali hii.

Chunguza
Tumia muda wako mwingi kuchunguza juu ya uhusiano wake. Uhusiano wao umesimama na wanaonekana ni watu wenye ‘future’? Nasema hivyo kwa sababu, yawezekana uhusiano wa huyo uliyetokea kumpenda ni wa kuzuga tu na huenda wewe ndiye mwenye ‘future’ naye. Ndiyo maana nikasema chunguza uhusiano wake kwanza.

Usitafute uadui
Baada ya kuchunguza, ukibaini kwamba uhusiano wao hauko ‘siriasi’, vuta subira, lolote linaweza kutokea na likaufurahisha moyo wako. Lakini kama utaona ni watu walio siriasi na wanaelekea kuoana, usitafute uadui bure, kaa pembeni.

Una nafasi kwake?
Sawa umetokea kumpenda msichana aliye na mtu wake, umeshawahi kujiuliza kama una nafasi ndani ya moyo wake? Anaonesha dalili fulani za kukupenda kama unavyompenda na ni mtu anayeonesha kukumisi anapokuwa mbali na wewe? Utakapobaini una nafasi kwake, uamuzi wa kumpotezea hautakuwa na nafasi.

Ni rahisi kubadili uamuzi wake?
Unadhani huyo uliyetokea kumpenda anaweza kubadili maamuzi ya kumuacha huyo aliyenaye kama kweli hawana ‘future’? Utagundua hilo kwa kuongea naye na kumsikia kama anaweza kufanya maamuzi hayo ili awe na wewe.

Pingana na moyo wako
Ifike wakati upingane na moyo wako. Unajua moyo wako kukuambia kuwa unataka kuwa na uhusiano na demu ambaye tayari ana mpenzi wake wakati mwingine utakuwa unakupotosha. 

Kwa hiyo ukiona vipi, pingana nao. Acha kumng’ang’ania msichana mwenye mpenzi wake licha ya ukweli kwamba, huenda wewe ndiye mwenye nafasi ya kuwa mume wake na siyo huyo aliye naye.

Urafiki ni poa?
Umempenda sana na hauko tayari kumkosa katika maisha yako lakini imetokea kwamba tayari yuko na mtu na umebaini huna nafasi kwake kabisa? Usiumie, omba angalau urafiki. Siyo urafiki wa kivile sana ila angalau pale unapotaka kusikia sauti yake kwa kumsalimia tu, upate nafasi hiyo.

Usiumie, yupo mwingine
Haina haja ya kujitafutia vidonda vya tumbo bure kwa kuwa tu umebaini uliyetokea kumpenda tayari ana mtu. Chukulia ni hali ya kawaida, mademu wazuri ambao wanaishi singo wapo kibao huko mtaani, ni suala la wewe kutulia tu. Amini yupo mwingine ambaye atayafanya maisha yako yawe ya furaha.

Naomba nihitimishe kwa kusema kwamba, unapotokea kumpenda mtu fulani, pambana kuhakikisha unampata kwa sababu ukimkosa maisha yako yanaweza kuwa gizani. Ila pale utakapoona uwezekano wa kuwa naye haupo, usilazimishe ndugu yangu. Kumbuka haya ni maisha tu!

Uhuru Kenyatta: Shabaab Hawahusiki Mashambulizi ya Sasa, ni Mtandao wa Wanasiasa Ndani ya Kenya!

$
0
0
Kenyatta: 'Al-Shabaab not to blame' for Kenyan attacks

Two terrorist attacks on the Kenyan coast was not orchestrated by the al Shabaab terrorist network, according to the country's president Uhuru Kenyatta.

Mr Kenyatta said the 65 people were killed by "local political networks", dismissing claims by Somalia's al Shabaab Islamist group that it was behind the assaults.

Speaking to the nation, he said:

"This was not an al Shabaab terrorist attack. Evidence indicates local political networks were involved in the planning and execution of the heinous crime.

"This also played into the opportunist network of other criminal gangs," he said.

Nasubiri Kumfumania Mke Wangu, Naombeni Ushauri

$
0
0
Waku habari za mchana,kama nilivyojieleza hapo juu,ni kwamba nilibahatika kuoa miaka 10 iliyopita iliyopita,tulipata sakrament ya ndoa takatifu tar.7/5/2011.pia katika ndoa yetu tumejaliwa kupata watoto 2.sasa kilichonifanya nije hapa jukwaani ni taarifa nilizozipata toka kwa jirani yangu ambae amenithibitishia kuwa mke wangu anatembea na mtu ambae pia ni jirani yetu kabisa.mke wangu huwa anashinda nyumbani akijishughulisha biashara ya kiduka tulichokifungua karibia mwaka sasa.pia mimi huwa nashinda kibaruani kwangu ambapo mara nyingi huwa nachelewa kurudi nyumbani kutokana na kabiashara kangu kanakonipatia riziki.huyu jirangu kanijulisha huwa wanatoka majira ya saa 1 jioni na kurudi sa 2:30 jioni kabla mimi sijarudi.baada ya kupata tarifa hizi nilijaribu kufanya uchunguzi na nimeanza kuona kuna ukweli juu ya jambo hili.juzi ilipofika saa 1:30 jioni nilimpigia simu kumuulizia jambo fulani nikasikia anaongea taratibu tofauti na siku nyingine,nikamuuliza umeshafunga duka?akanijibu ndio,nikamuuliza mbona mapema akasema kuna mkanda nimeupenda nauangalia..nikakata simu nikampigia yule jirani kumuuliza kama mke wangu yupo nyumbani akasema hayupo na ametoka na jamaa kama kawaida yake,kama huamini uje uone.nilitamani kwenda lakini nilishindwa kujua ni uamuzi gani nichukue kwa sababu,kwanza sikujua wamekwenda guest gani,huyo jamaa anausafiri hivyo wanauwezekano wa kwenda nje ya mji kidogo.nilijikaza sikumuuliza wala kumwonyesha dalili zozote za kufahamu mambo hayo machafu anayoyafanya mke wangu.hivyo naombeni ushauri wenu pindi nikiwafumania au kuwahi kurudi home na kumkosa mke wangu wakati amenijulisha yupo home..naombeni ushauri wenu ni uamuzi gani naweza kuchukua ukawa sahihi.

Lowasa Atangaza Neema Kwa Vijana

$
0
0
Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa amesema vijana 10,500 waliojitokeza hivi karibuni kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kufanya usaili wa nafasi 70 za kazi katika Idara ya Uhamiaji, ni ishara kuwa bomu la ajira litalipuka muda wowote.

Akizungumza na waandishi wa habari jana nje ya Viwanja vya Bunge, Lowassa alisema Serikali ni lazima ihakikishe inatengeneza ajira kwa kuwa kila mwaka zaidi ya vijana 30,000 wanahitimu katika vyuo mbalimbali nchini.

Wasomi hao wa fani mbalimbali walijitokeza katika uwanja huo Ijumaa iliyopita, kuanzia saa 12 asubuhi wakisubiri kufanyiwa usaili huo.

Lowassa ambaye alijiuzulu wadhifa wa Waziri Mkuu mwaka 2008, amenukuliwa mara nyingi akiitaka Serikali kuchukua hatua kukabiliana na tatizo la ajira na akisema ni bomu linalosubiri kulipuka.

Mbunge huyo wa Monduli kupitia CCM, aliwahi kuingia kwenye malumbano makali na Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka kuhusiana na suala la ajira kwa vijana.

Kabaka akiwa bungeni, Machi 21, 2012 alitoa takwimu za namna Serikali ilivyokuwa inatengeneza ajira kwa nia ya kumjibu Lowassa, ambaye alikuwa ameeleza tatizo la ajira linavyowaathiri vijana.

Jana, Lowassa kuongezeka kwa makundi ya vijana wanaopora watu katika maeneo mbalimbali nchini ni ishara ya ukosefu wa ajira. “Watanzania sasa tupo milioni 48 na kila mwaka vijana zaidi ya 30,000 wanahitimu vyuo vikuu na kazi hakuna, pamoja na hilo hatuambiwi ni vijana wangapi ambao hawana kazi,” alisema Lowassa.

Alisema lazima Serikali itengeneze ajira kwa wananchi wake, huku akimtolea mfano Rais wa Marekani, Barack Obama kwamba alishinda awamu ya pili kwa sababu ya kutengeneza ajira.

“Mfano mzuri ni katika uanzishwaji wa viwanda. Tunapofikiria kuanzisha kiwanda cha pamba kwanza lazima tuangalie tutatengeneza ajira ngapi,” alisema.

Katika kuonyesha kuwa ajira sasa ni tatizo nchini, juzi jioni wakati wa mjadala wa Bajeti Kuu, Naibu Spika Job Ndugai alisema Mtanzania mwenye nia ya kugombea urais mwaka 2015 ili aweze kuelekewa kwa wananchi ni lazima aeleze mikakati ya kuwasaidia vijana kupata ajira.

“Ajira ni tatizo kubwa na lazima lishughulikiwe. Kuna vijana hawaendi shule lazima watazamwe. Kuna wanaomaliza darasa la saba, kidato cha nne, cha sita na vyuo vikuu.

Nazungumza kutoka moyoni kabisa. Hizi ni dakika za mwisho za Serikali ya awamu ya nne, wale wanaojipanga kwa awamu ya tano kama hawataongelea ajira basi waandike wameumia.”

Ndugai alisema vijana wasio na kazi ndiyo wapigakura wakubwa na kusisitiza kuwa mgombea yeyote makini ni lazima afikirie suala la ajira kwa vijana.

 Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe alisema: “Vijana 10,500 kufanya usaili wa nafasi 70 ni janga la taifa. Yupo kiongozi mmoja mwandamizi wa CCM aliwahi kulizungumza hili lakini akapondwa kwamba anazungumza mambo kwa kuzua. Sasa huu ndiyo ukweli wenyewe.”
Credit: Mwananchi

Baada ya kuchapwa nne bila, Ureno yaendelea kumeguka vipande vipande

$
0
0
Beki wa pembeni wa klabu bingwa barani Ulaya Real Madrid, Fabio Coentrao ameondolewa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Ureno ambacho kwa sasa kipo nchini Brazil kikishiriki fainali za kombe la dunia.

Coentrao, ameondolewa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Ureno, baada ya kuumia goti akiwa kwenye mchezo wa mzunguuko wa kwanza wa kundi la saba ambapo A Selecção walikubali kupoteza mbele ya Ujerumani kwa mabao manne.

Coentrao, aliondolewa kabisa kwenye kikosi cha Ureno baada ya kufanyia vipimo katika mguu wake wa kulia na kubainika aliumia vibaya, hivyo itamlazimu kukaa nje ya uwanja kwa majuma kadhaa kabla ya kurejea tena.

Kuumia kwa beki huyo mwenye umri wa miaka 26, kunakuwa pigo la pili kwa timu ya taifa ya Ureno ambayo itamkosa beki wa kati Képler Laveran Lima Ferreira Pepe, aliyeonyeshwa kadi nyekundu ya moja kwa moja.

Adhabu hiyo kwa Pepe inamfanya aikose michezo miwiwli ya hatua ya makundi iliyosalia, hivyo kocha mkuu wa timu ya taifa ya Ureno Paul Bento, atalazimika kutumia ubunifu kwa kumpanga beki mbadala wakati wa mchezo dhidi ya timu ya taifa ya Marekani utakaochezwa June 22.

Wachezaji wengine ambao ni majeruhi katika kambi ya timu ya taifa ya Ureno, ni mshambuliaji Hugo Almeida anayesumbuliwa na maumivu ya nyama za paja pamoja na mlinda mlango Rui Patricio anayesumbuliwa na maumivu ya paja.

Jk Atumia Dakika 15 Kumfagilia Diamond

$
0
0
Rais Jakaya Kikwete alianza kwa kusema: “Watanzania hawapaswi kumbeza Diamond kwani pamoja na kukosa tuzo ya MTV lakini kuna juhudi kubwa alionyesha kwa kufanya shoo kubwa ya kwanza na ya kimataifa ambayo niliishuhudia mwenyewe na niliona watu walifurahia sana,”

“Diamond alilitangaza taifa letu kupitia shoo hiyo na muziki wetu wa Tanzania, hivyo hatupaswi kuwa mbali na wasanii wetu kwani natambua wazi Diamond bado yuko kwenye kinyang’anyiro cha tuzo za BET ambazo ni tuzo kubwa sana nchini Marekani na naweza kusema kuwa hata kutambuliwa kwake kuwepo kwenye tuzo hizo nalo ni jambo la kujivunia kwani uwepo wake ni njia moja ya kulitangaza Taifa letu hata kama hatabahatika tena kuchukua tuzo hizo,”

“Najaribu kuwatia sana moyo na kumwambia Diamond kuwa awe na uvumilivu kwani nimeshaanza kuonyesha njia ya kumsaidia maana juzijuzi nilimkuta Marekani na nilimkutanisha na mdau mkubwa sana wa muziki duniani ambaye ndiye alimtoa Jay z, Usher Raymond  na wasanii wengine wakubwa na nilimuomba amsaidie kumwelekeza namna anavyoweza kukua kwenye ulimwengu wa muziki”,

“Nimeshaongea na mmiliki wa kituo cha televisheni ya E ambayo ni kubwa sana Duniani ikiwa ni njia mojawapo ya kuhakikisha naukwamua muziki wetu, hivyo wanatarajia kuja Tanzania hivi karibuni akiwa ameambatana na Usher Raymond na wadau wengine ambao watakuja kukutana na kina Diamond na wasanii wa filamu ili wawape mbinu za kukuza sanaa yetu,” alisema Rais Kikwete.

Diamond alianza kubezwa na baadhi ya mashabiki na wasanii wenzake siku chache baada ya kukosa tuzo na wengine walifanya hivyo siku ya uzinduzi wa Wimbo wa Tulinde Utanzania ambapo walimtania kwamba hana uwezo wa kuchukua tuzo hizo hivyo hata kwenye tuzo za BET asihangaike kwani hatapata chochote.


Picha:Mwanamke Ajifungua Kiumbe cha Ajabu Mkoani Singida.

$
0
0
Mwanamke  mmoja  mkazi  wa  Kintinku, Wilayani  Manyoni  mkoani  Singida  amejikuta  akimwaga  machozi  baada  ya   kujifungua  mtoto  mwenye  kichwa  cha  ajabu (  tepe tepe).
Tukio  hilo  limetokea  jana  asubuhi    katika  hospitali  ya  Kintinku  Health  Center  iliyopo  Wilayani  Manyoni…..


Akiongea  na  Mpekuzi  kwa  sharti  la  kutotajwa  jina  lake  kwa  madai  kuwa  yeye  si  msemaji  wa   hospitali  hiyo, Mkunga  mmoja  wa  hospitali  hiyo  amedai  kuwa  mama  huyo  alifikishwa  hospitalini  hapo  akiwa  katika  hatua  za  mwisho   kujifungua.


“Alifikishwa  hapa  akiwa    katika  hatua  za  mwisho .  Hakuwa  na  kadi  yoyote  ya  Clinic  kwa  kuwa  hakuwahi  kuhudhuria  Clinic  tangu  abebe  mimba  hiyo.

“Pamoja  na  kutokuwa  na   kadi  ya  Clinic, tulianza  kumsaidia  kujifungua, lakini  mtoto  aliyezaliwa  alikuwa  ni  wa  tofauti  kidogo  na  alikuwa  amefariki  dunia.Kichwa  chake  kilikuwa  tepetepe  na  kimebonyea bonyea.

“Ilikuwa  ni  ngumu  kwetu  kutambua  tatizo  alilokuwa  nalo  mama  huyo  kwa  kuwa  hakuwa  na  kadi  yoyote  ya  Clinic  ambayo  ingeweza  kutusaidia  kujua  maendeleo  ya  mtoto  huyo  alipokuwa  tumboni “, alisema  Mkunga  huyo.

Mpekuzi  ilifanya  mahojiano  na  mama  huyo  ambaye  naye  alionyesha  kushangazwa  na  tukio  hilo  na  kusema  hajui  tatizo  lililomfanya  ajifungue  mtoto  huyo  kwa  kuwa  hakuwahi  kusikia  maumivu  ya  aina  yoyote  wakati  wa  ujauzito  huo  hadi  alipofikia  hatua  ya  kujifungua….

Katika  mahojiano  hayo, mama  huyo  alisema  kuwa  huo  ni  uzao  wake  wa  6  na  hajawahi  hudhuria  Clinic

Kingine kipya kutoka kwa mpenzi wa Ney wa Mitego Siwema kuhusu kufukuzwa kazi

$
0
0
Miongoni mwa mastaa ambao wanamake headline sana Tanzania ni pamoja na Ney wa Mitego ambaye siku chache zilizopita aliwaonyesha waandishi habari nyumba yake mpya aliyoinunua na kuimalizia ujenzi na baadhi ya vitu vingine ikiwemo pia gari analotembelea kwa sasa ambalo ni Nissan Murano.
Leo kupitia You heard mpenzi wa Ney aitwae Siwema amehusishwa na taarifa za kupiga picha za utupu ambazo zimesababishwa kufukuzwa kazi kwenye kampuni ya Shirika la ndege alilokua anafanya kazi ambapo Ney alipopigiwa simu haya ndiyo yalikua majibu yake.
Ney amejibu ‘kama umesikia hiyo sawa, nitampa hiyo pole…. sijui kuhusu yeye pia kulipwa kiinua mgongo, hayo unayongea wewe, mimi sijui chochote… ongea mpaka mwisho umalize haya!!
Ili kusikiliza kila kitu bonyeza play hapa chini…

Serikali ya Tanzania imepiga marufuku uvutaji wa Shisha.

$
0
0
Uraibu huo unaohusisha uvutaji wa Tumbaku yenye ladha tofauti tofauti ambayo hutiwa ndani ya chupa kubwa na kuvutwa kwa mirija, umeshika kasi sana Tanzania hasa miongoni mwa vijana wadogo mjini Dar Es Salaam.
Baadhi ya watu wanaiona Shisha kama isiyokuwa na madhara ya kiafya ikilinganishwa na uvutaji wa Sigara.
Lakini wataalamu wanaamini kuwa uvutaji wa Shisha kwa muda wa saa moja ni sawa na kuvuta sigara miamoja.
Madaktari walitoa onyo kuhusu uvutaji wa Shisha wanakabiliwa na tisho la kuugua Saratani sawa na hatari inayowakabili wavitaji wa sigara.

Pic of The Day:Mbunge Akwea Bado Bado Kuwahi Ndege Airport

$
0
0
Adha ya Foleni jijini Dar es Salaam imemkumba mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki kutoka nchini Tanzania, Shy-Rose Bhanji aliyekuwa akisafiri kwa ndege na kulazimika kukwea bodaboda ili imuwahishe Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere Dar es Salaam hii leo.

Flora Lyimo 'Mtitu Ndio Nani Jamani? William Mtitu Mbulula wa Mwisho Tena Anaweza Kuwa Mbakaji! Who Can Say This About Flora Mbasha?

$
0
0
Sio Maneno Yangu Bali ni Maneno ya Flora Lyimo Baada ya William Mtitu Kuandika Maneno ambayo yalionekana yanamponda Flora Mbasha Kuhusu Lile Sakata la Mume wake Kumbaka Mdogo wake Jisomeee hapo chini:

"WHAT'S ON? MTITU NDIYO NANI JAMANI? ''WILLIAMMTITU MBURULA WA MWISHO TENA NAHISI UNAWEZA KUWA MBAKAJI PIA'' WHO CAN SAY THIS ABOUT FLORA MBASHA ? I SAY ''FUCK YOU '' HUWAJALI WATOTO HATA WANAWAKE ? I HOPE HUKO ULIKO WAKUSHIKILIE PIA'' SIYO BURE UTAKUWA MBAKAJI PIA'' UNAWEZAJE KUWATETEA WABAKAJI ? NIMEKUCHUKIA JAPO SIKUFAHAM'I HOPE SITOKAA NIKUFAHAM''' PUMBAVU'''TENA JIFUNZE KUANDIKA FLORA SIYO FROLA'' PUMBAVU MARA ELFU'' Flora Lyimo..


Flora Alifunguka Hivyo Baada ya Mtitu kuandika Haya maneno hapa chini:


Kesi Tano za Mabilioni Uswisi Zachunguzwa Sakata la Mabilioni yaliyofichwa Uswiss

$
0
0
Tanzania imeomba msaada kwa taasisi iitwayo International Centre for Asset Recovery – ICAR (Kituo cha Kimataifa cha Urejeshaji Mali) ya Uswisi kuchunguza kesi tano zinazohusu watu na taasisi zinazotuhumiwa kuficha mabilioni ya fedha nchini humo.

Itakumbukwa kuwa baada ya kuibuka kwa sakata la mabilioni hayo ya Uswisi, Serikali iliunda kikosi kazi chini ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Fredrick Werema kulifanyia kazi.

Gazeti hili lilifuatilia suala hilo hadi Uswisi na kubaini kuanza kwa uchunguzi huo, huku fedha nyingi zikitajwa kwamba zinatokana na vitendo vya rushwa.

Akizungumza na mwandishi wetu mjini Bern, Uswisi hivi karibuni, Mtafiti wa Sheria wa ICAR, Andrew Dornbierer alisema: “Tuna makubaliano na Serikali ya Tanzania hasa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), tunachunguza kwa kina kesi za rushwa na utoroshwaji wa fedha, hivyo tuko katika ukusanyaji wa taarifa. Siwezi kukupa mifano ya moja kwa moja kwa sababu bado tunazifanyia kazi na tunadhibitiwa katika utoaji wa taarifa.”

Mkurugenzi wa ICAR, Gretta Fenner Zinkernagel alithibitisha uwepo wa kesi hizo za Tanzania.

“Ni kweli tumeombwa na Serikali ya Tanzania kusaidia kuchunguza baadhi ya kesi… zilikuwa zimeshachunguzwa lakini kutokana na uwezo wao mdogo tunawasaidia. Kwa harakaharaka naweza kusema tunazo kesi tano hivi… ni kesi za watu binafsi na taasisi na zinahusu masuala ya fedha. Hatuwezi kutaja majina kwa sababu tunakatazwa kabisa na mkataba wetu na taasisi tunazofanya nazo kazi.”

Licha ya kutotaja majina, Zinkernagel alisema wanaochunguzwa katika kesi hizo wanahusishwa na kampuni hewa zilizoanzishwa kwa lengo la kuchota fedha kisha kwenda kuzificha nje ya nchi.

“Kuna watu wenye masilahi binafsi na wamekuwa wakipokea rushwa au wamekuwa wakitumia mashirika kwa ubia au kampuni kivuli na ushirika mwingine wa kimataifa ili kusafirisha fedha kwenda kwenye kampuni fulani kwa lengo la kuzificha. Ni kampuni zinazotumiwa na wafanyabiashara kuhamisha fedha haramu na mwisho hujisafisha,” alisema.

Jaji Werema

Jaji Werema alikiri Tanzania kuiomba ICAR kufanya uchunguzi huo lakini akakataa katakata kutaja watu wala kampuni zinazofanyiwa uchunguzi.

“Hatuwezi kutaja majina ya watu waliofunguliwa kesi kwa sababu kwanza tutakuwa tumeingilia haki zao kisheria. Pili, tunaweza kuwataja lakini baadaye ikabainika kuwa si kweli, bali ni tuhuma tu na wakaja kutushtaki na tatu, tutakapowataja watu hao tuliowafungulia kesi tutaharibu upelelezi wetu.

“Katika kesi hizi, kisheria, tunafanya kazi zetu kwa utaratibu ili tusiharibu upelelezi na tupate mambo mengi. Mnadhani tumekaa kimya hatufuatilii lakini tunafanya kazi yetu. Siku ikifika mtaona na mtasikia.”

Halima Mdee (CHADEMA), Amemtaka Mbunge Mwenzake, Leticia Nyerere, Aache Ubunge na Akajiunge na CCM

$
0
0
MBUNGE wa Kawe, Halima Mdee (CHADEMA), amemtaka mbunge mwenzake, Leticia Nyerere, aache ubunge na akajiunge na Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuliko kuendelea kukipigia debe chama hicho akiwa upinzani.
Kauli hiyo ameitoa jana alipokuwa akichangia bajeti ya serikali kwa mwaka 2014/2015 ambapo alisema matendo anayofanya Leticia ya kujipendekeza kwa CCM yatamgharimu kama ilivyotokea kwa wenzake.
Juzi wakati akichangia bajeti hiyo, Leticia alisema serikali ikifanya vizuri, lazima ipongezwe kwakuwa imepeleka maendeleo katika jimbo analotoka.
“Serikali yangu imefanya mambo mengi, imeniletea maji, walimu katika jimbo langu la Kwimba, ni lazima tuipongeze si kila wakati tunailaumu humu ndani,” alisema.
Katika mchango wake jana, Mdee, alisema jukumu kubwa la upinzani ni kuikosoa serikali na kuonyesha mbadala katika masuala mbalimbali na si kuisifia kwa kutekeleza wajibu wake wa kuwahudumia wananchi.
“Serikali inapata fedha kutokana na kodi za wananchi, inalazimika kupeleka maji, barabara na huduma mbalimbali kwa lazima si hiyari, tunapoikosoa tunatimiza wajibu wetu kama yenyewe inavyotekeleza inapowahudumia wananchi.
“Leticia Nyerere anaweza kwenda CCM, kwakuwa Rais Kikwete ana nafasi mbili za uteuzi wa wabunge, lakini lazima ajue waliojipendekeza CCM wamepigika sana hivi sasa, aachie ubunge aende huko kwakuwa ana mapenzi nao,” alisema.
Mdee alisema kuwa Leticia anaiaibisha kambi ya upinzani inayofanya kazi usiku na mchana kuhakikisha serikali inaboresha huduma inazozitoa kwa wananchi.
“Upinzani si lelemama, kama anafikiria CCM ni kuzuri zaidi ni vema akaenda huko kuliko kubakia hapa pasipomfaa,” alisema

Diva Loveness Aweka Hadharani Kuwa Penzi lake ni la Pesa kwa Mpenzi Wake..'Seriously?"

$
0
0


Jamaa kafunguka Balaaa baada ya post iliyowekwa Instagram na Diva Lovenesss
Jisomee hapa Chini: 
Asante Instagram 

Mchezaji wa World Cup Agundulika Kuwa ana Mguu wa Tatu, Can you See It ?

$
0
0
Jamani Nimeitoa hii Picha mahali eti watu wanasema huyo mchezaji ana mguu wa Tatu , Mbona mimi siuoni au macho yangu mabovu , Je wewe unauona huo mguu wa Tatu? 
Kama unauona embu Comment basi na sisi tujue uko wapi

Mtoto Mchanga Chatupwa Shimoni…Mama Atiwa Mbaroni

$
0
0
MWILI wa kichanga umeokotwa eneo la Njiro jijini Arusha juzi baada ya kudaiwa kutupwa na mama mmoja ambaye hakufahamika jina lake mara moja.

Baada ya kichanga hicho kuokotwa, wananchi walitoa taarifa polisi waliofika na kufanikiwa kumkamata mama mwenye kichanga hicho.

Breaking News:Mume wa Flora Mbasha, Anayekabiliwa na kesi ya Ubakaji Amepewa Dhamana

$
0
0
MUME wa Flora Mbasha, Emmanuel Mbasha (32) anayekabiliwa na kesi ya ubakaji amepewa dhamana katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala, Dar baada ya kutimiza masharti.

Mbasha amefikishwa mahakamani hapo akitokea Gereza la Keko alikopelekwa Juni 17 mwaka huu akikabiliwa na kesi ya kumbaka shemeji yake.

Mbasha baada ya kutolewa kwenye mahabusu ndogo ya mahakamani hapo alionekana mnyonge na aliyechoka hali iliyosababisha simanzi kwa ndugu na jamaa zake waliokusanyika mahakamani hapo.

Baada ya kesi hiyo kutajwa, rafiki wa Mbasha aliyejitambulisha kwa jina la George Mushi na baba wa mtuhumiwa huyo, Mwahimu Juma walifanikiwa kutimiza masharti ya dhamana.

Ndugu Aingia Mitini na Rambirambi za Msiba wa George Tyson

$
0
0
MAMBO yamezidi kuwa mambo! Kifo cha aliyekuwa mwongoza filamu za Bongo, George Otieno ‘Tyson’ kimezidi kuzua mapya, safari hii ikidaiwa ndugu mmoja (jina tunalo) ameingia mitini na pesa za rambirambi zilizochangwa jijini Dar es Salaam wakati wa msiba huo.

Kwa mujibu wa chanzo, ndugu huyo alikabidhiwa mshiko huo kiasi cha shilingi milioni mbili za Kibongo ambapo aliaminika kwamba baada ya kutua Nairobi, Kenya ambako mwili wa marehemu ulipelekwa kwa mazishi kutoka Bongo, angezikabidhi kwa familia, hasa baba na mama wa marehemu.

“Yule jamaa amefika Kenya na hakukabidhi pesa. Wengi waliamini kwamba angezitoa baada ya kumzika marehemu kule kijijini Siaya, lakini baada ya mazishi tu akachomoka na kurudi Nairobi.
“Mbaya zaidi amezima simu, kwa hiyo hayupo hewani. Kuna uwezekano amerejea Dar es Salaam kwa kuogopa msala wa familia,” kilisema chanzo hicho.

Kikaongeza: “Awali wakati msiba upo Dar, kuna mtu alimpa shilingi milioni mbili akampe mama wa marehemu Kenya. Pia kuna michango mingine iliyotolewa pale Leaders Club (Kinondoni) akakabidhiwa yeye. Na kuna pesa ya kusafiria mtoto mmoja pia akapewa.

“Sasa baada ya kuzika tu, yule mtu aliyetoa shilingi milioni mbili akapiga simu kwamba na yeye anakwenda msibani, ndiyo jamaa akaaga haraka na kuondoka.
Yule alipofika akamuuliza mama wa marehemu kama alipewa shilingi milioni mbili, akasema hajapewa, kumbe jamaa aliondoka haraka kwa sababu alijua kitanuka.”

Juzi, gazeti hili lilifanya jitihada za kumtafuta mdaiwa huyo kwa njia ya simu ya mkononi lakini hakuwa hewani kwa muda mrefu.

George Tyson alifariki dunia Mei 30, mwaka huu kwa ajali ya gari akitokea Dodoma kuelekea Dar. Alizikwa Juni 14, 2014 kwenye Kijiji cha Siaya, Kisumu, Kenya. Mungu ailaze pema peponi roho yake. Amina.
Viewing all 104803 articles
Browse latest View live


Latest Images