Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104795 articles
Browse latest View live

Soma Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo


Bulembo Awasilisha Barua ya Kutogombea Nafasi ya Uenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi

$
0
0
Bulembo Awasilisha Barua ya Kutogombea Nafasi ya Uenyekiti  wa Jumuiya ya Wazazi
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wa Chama cha Mapinduzi(CCM), Alhaj Abdallah Bulembo amewasilisha barua kwa Katibu Mkuu wa CCM kutogombea nafasi ya uenyekiti wa jumuiya hiyo.

Bulembo aliwahi kusema kuwa hatogombea tena lakini baadaye aliamua kuchukua fomu. Hata hivyo Bulembo amesema aliamua kuchukua fomu ya kugombea baada ya kupata shinikizo kutoka kwa makatibu wakuu na wazee wa jumuiya hiyo.

"Sasa leo(Jumanne) nimewaita kuwaeleza sitagombea tena licha ya kuchukua fomu, naamini wagombea 48 waliopatikana, kuna mmoja atatufaa kuongoza jumuiya hii, leo ninapeleka barua kwa katibu mkuu wa chama (Abdulrahiman Kinana) ya kumweleza dhamira yangu hii,” amesema Bulembo leo Jumanne alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa.

Bulembo amesema uchaguzi katika ngazi ya Taifa utafanyika kuanzia Novemba 20 hadi 23, wagombea wote wapo lakini yeyote aliyeanza kampeni mapema huyo ameshajikata," amesema.

Kuhusu hoja ya kuchukua fomu amesema haikuwa dhambi kwa kuwa kanuni za chama zinaruhusu na upo uwezekano wa kuwa na nafasi mbili za uongozi.

"Kumekuwa na upotoshaji kwamba, ukiwa mbunge au waziri hauwezi kugombea nafasi nyingine, sasa hapa nina kitabu cha kanuni za mwaka 2005, 2010, 2012 na 2017 zinasema kiongozi au mbunge, waziri anaweza kugombea ila kamati kuu ya chama itaamua inavyofaa, kama bado anahitajika atapitishwa lakini mie sitagombea tena,” amesema.

     

Wasanii na Viongozi Mbalimbali Watoa Yamoyoni Baada ya Diamondi Kuanika Ukweli wa Mambo Juu ya Mtoto Wake na Mobetto

$
0
0
Wasanii na Viongozi Mbalimbali Watoa Yamoyoni Baada ya Diamondi Kuanika Ukweli wa Mambo Juu ya Mtoto Wake na Mobetto
Baadhi ya wasanii pamoja na viongozi nchini wametoa yaliyomo mioyoni baada ya msanii wa muziki wa kizazi kipya Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’ kuzungumza leo kuhusu uhusiano wake.

Baada ya msanii huyo kukiri kuwa amezaa na mwanamitindo Hamisa Mobetto, baadhi ya wasanii maarufu pamoja na viongozi wameonyesha kumuunga mkono Diamond kutokana na kueleza ukweli.

“Thamani yako kwangu bado ni kubwa sana, kwani uwezo wako wa kupitia kwenye dhoruba na ukabaki imara na familia yako unaendelea kukupa heshima,” maneno yaliyoandikwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kupitia ukurasa wake wa Instagram huku akiwa ameweka picha ya mwanadada Zari.

Zari ni mama wa watoto wawili wa Diamond ambaye anaishi naye kwa sasa.

Pia Mbunge wa Mikumi (Chadema), Joseph Haule maarufu kama Profesa J ameandika kupitia ukurasa wake wa Instagram na Twitter akisema ukweli humweka mtu huru kweli kweli huku akiwa ameweka picha ya Diamond Platnumz.

Si hao tu waliofunguka kueleza hilo bali hata Haji S Manara ambaye ni Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba amempongeza Diamond kupitia ukurasa wake wa Instagram kwa kuzungumza kiume.

Kwa upande wake Soggy Doggy Hunter amempongeza Diamond kwa kuongea yote na kuwa muwazi na kumuombea Mungu amsimamie.

Mkude Simba amenukuu maneno ya msanii huyo aliyosema “Mwanamke yeyote mwenye mtoto wangu na amlete siwezi kukataa damu kama kweli ni mtoto wangu.”



Okwi Akabidhiwa Hundi ya Milioni Moja Zawadi ya Mchezaji Bora Mwezi Augosti

$
0
0
Okwi Akabidhiwa  Hundi ya Milioni Moja  Zawadi ya Mchezaji Bora Mwezi Augosti
Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Uganda ‘The Cranes’ na klabu ya Simba, Emmanuel Arnold Okwi, amekabidhiwa mfano wa hundi ya shilingi milioni moja ambayo ni zawadi yake ya kuibuka mchezaji bora wa mwezi Agosti.

Mara baada ya kupokea mfano huo wa hundi Okwi amesema kuwa katika Ligi Kuu soka Tanzania Bara kuna wachezaji wengi ambao yeye kwa upande wake anavutiwa nao.

“Kwa Tanzania klabu nyingi zina wachezaji wazuri lakini nje ya Simba kuna mchezaji anaitwa Kamusoko ananivutia sana na Donald Ngoma pia”, amesema Emmanuel Okwi, ambaye amekuwa mchezaji bora wa mwezi Agost wa Vodacom Premier League ‘VPL’.

Maneno haya ameyasema Okwi baada ya kukabidhiwa mfano wa hundi ya Tsh 1,000,000 na Meneja Chapa wa Vodacom Tanzania, Yvonne Maruma na Afisa Udhamini, Ibrahim Kaude. Tuambie mchezaji unayemkubali zaidi kwenye ligi.

Hadi sasa Okwi anaongoza katika msimamo wa wafungaji mabao ya Ligi Kuu ya VPL msimu huu kwa kuwa na jumla ya mabao 6 , huku wanaomfuatia wakiwa na mabao mawili.

Polisi Aua Watu Wawili Kwa Risasi Mkoani Morogoro

$
0
0
Polisi Aua Watu Wawili Kwa Risasi Mkoani Morogoro
Watu wawili wamekufa kwa kupigwa risasi na askari polisi baada ya kuibuka mzozo kuhusu ng’ombe waliokamatwa katika Kijiji cha Nyalutanga wilayani Morogoro.

Pia, imeelezwa mtu mmoja amejeruhiwa kwa risasi kwenye makalio na ng’ombe 35 wameuawa na zaidi ya 40 kujeruhiwa katika mzozo huo.

Hata hivyo, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dk Stephen Kebwe ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa amethibitisha vifo vya watu hao wawili, akisema hana taarifa kuhusu aliyejeruhiwa.

Dk Kebwe amesema mzozo huo umeshapatiwa ufumbuzi na waliokufa katika tukio hilo wamezikwa leo Jumanne, huku uchunguzi ukiendelea kuhusu wananchi waliojichukulia sheria mkononi na kumshambulia kwa mawe askari aliyefika kutuliza mzozo huo.

Mkuu wa mkoa amesema ameunda kamati kuchunguza tukio hilo ambalo lilisababisha askari kufyatua risasi hewani kuwatawanya wananchi waliokuwa wamemzonga na kwa bahati mbaya risasi ziliwapata watu wawili.

Amesema watakaobainika watachukuliwa hatua za kisheria. Pia, amewaonya wafugaji wanaoacha mifugo ikizurura ovyo.

Akizungumzia tukio hilo, Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Nyalutanga kilichopo Kata ya Kisaki, Said Masongele amesema mzozo huo ulitokea jana saa saba mchana katika eneo la ofisi za serikali ya kijiji.

Masongele amewataja waliofariki dunia kuwa ni Ramadhan Kiwenge na Kibwana Msipwile.

Amesema mkazi mwingine Ismail Msagule amejeruhiwa kwa kupigwa risasi kwenye makalio na amelazwa katika zahanati hiyo.

Mwenyekiti huyo amesema hilo lilitokea baada ya mifugo kuingia shambani kwenye bonde la Kikwato na kukamatwa na mgambo na walinzi wa jadi (Sungusungu).

Amesema awali, viongozi wa kijiji wakiwa kwenye kikao walipata taarifa kwamba kuna mifugo imevamia mashamba, hivyo walitumwa mgambo kwenda kuikamata.

Muda mfupi baadaye amesema alipokea simu ikieleza Mohamed Kassim alijeruhiwa kichwani na mfugaji wakati wa kukamata mifugo.

Mgambo wa kijiji hicho, Kibwana Mbegu aliyeshiriki kukamata mifugo amesema watu hao watatu walifyatuliwa risasi wakati askari akijihami baada ya wananchi kujaribu kupora silaha.

“Tulikamata mifugo isiyopungua 80 katika mashamba ya Kikwato ikila mazao, wakati tukifanya hivyo mwenzetu alijeruhiwa kwa kupigwa fimbo kichwani na mfugaji.  Tuliwazidi nguvu wafugaji na kuswaga  mifugo hadi ofisi za kijiji kwa hatua za kisheria,” amesema Mbegu.

Mbegu amesema baada ya dakika chache, wafugaji walifika ofisi za kijiji wakiwa na silaha za jadi, wakati huo wananchi wakiwa wanakusanyika huku kukiwa na askari polisi mwenye silaha kulinda amani eneo hilo.

Amesema baada ya wafugaji kufika eneo hilo, walianza kuchukua mifugo kwa nguvu jambo lililosababisha askari kufyatua risasi hewani kuwatawanya.

Mbegu amesema baadhi ya wananchi walimfuata askari kwa lengo la kumnyang’anya silaha, huku wengine wakirusha mawe.

Amesema askari alifyatua risasi ili kuwazuia ambazo ziliwapata watu wawili na baadaye alikimbia eneo hilo.

Mgambo huyo amesema kundi la wananchi lilimkimbiza ndipo alipofyatua risasi nyingine iliyomjeruhi mwananchi mwingine kwenye makalio.

Amesema askari huyo alijificha ndani ya nyumba kijijini hapo na alipiga simu kituo cha polisi Kisaki Gomero kuomba msaada kwa wenzake waliomuokoa katika eneo hilo ambalo lilikuwa limezingirwa na wananchi.

Jeshi La Polisi Laamua Kumjibu Lema Lakanusha Kuwakamata Watu Waliovaa T-shirt za Lissu

$
0
0
Jeshi La Polisi Laamua Kumjibu Lema Lakanusha Kuwakamata Watu Waliovaa T-shirt za Lissu
Jeshi la Polisi limemjibu Mbunge Godbless Lema na kusema hakuna mtuhumiwa ambaye amekamatwa na polisi kwa kuvaa Tshirt za CHADEMA wala za Tundu Lissu na kudai watu watatu waliokamatwa Septemba 17, 2017 walifanya makosa ya kukusanyika bila kibali.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amedai kuwa hakuna watu wowote ambao wanashikiliwa na jeshi hilo kwa kuvaa Tshirt bali walikuwa wanawashikilia watu ambao walikuwa wamefanya uhalifu. Mambosasa amesema hayo siku moja baada ya Mbunge Godbless Lema kupitia mitandao ya kijamii kumuomba IGP Sirro na Waziri Mwigulu Nchemba kuwaachia watu waliokamatwa na polisi kwa kuvaa Tshirt za UKUTA pamoja za Tshirt za 'Pray for Tundu Lissu'

"Hatuna mshtakiwa anaitwa CHADEMA, hatuna mshtakiwa anashtakiwa kwa kuvaa Tshirt ya chama chochote sisi tunachofanya ni kukamata wahalifu wanaotenda makosa ya kijinai, washtakiwa wote wanaokamatwa wanakuwa na mashati, watu wanaokamatwa wanakamatwa kwa kufanya makosa ya jinai, tukikamata mhalifu usiniambie kwamba huyu mhalifu ni CHADEMA mimi hiyo hainihusu" alisema Mambosasa

Aidha Kamanda Mambosasa amesema kuwa vijana watatu ambao walikuwa wamekamatwa kwa kufanya mkusanyiko pasipokuwa na kibali kwa sasa wameachiwa huru kwa kupata dhamana kwani kosa walilotenda ni kosa ambalo linadhamana.

"Walikamatwa watu watatu na walikamatwa kwa kukusanyika kinyume na sheria, nilisimama hapa na nikatoa onyo ni marufuku watu kujikusanya kwa makundi bila ya kibali kwa kisingizio cha kwenda kufanya maombi nikaruhusu watu kwenda kufanya maombi kanisani, misikitini hata wapagani kuna mawe makubwa makubwa nje ya mji wangeenda kuabudu huko, lakini wao walikaidi na walivyoona magari ya polisi walianza kukimbia, na ukianza kukimbia kwamba unanipa mrejesho kwamba unajua ulichotenda kwamba ni kosa ndiyo maana unakimbia" alisema Mambosasa

Aidha Mambosasa anasema kesi ya watu hao kwa sasa inakamilishwa upelelezi na pindi upelelezi utakapokamilika basi watafikishwa mahakamani kwa makosa ambayo wametenda.

Wafuasi wa Kenyatta Waandamana Nje ya Mahakama

$
0
0
Wafuasi wa Kenyatta Waandamana Nje ya Mahakama
Wafuasi wa rais wa Kenya Uhuru Kenyatta wanaandamana nje ya mahakama kuu mjini Nairobi, wakiitaka tume ya kitaifa inayoajiri na kufuatilia mienendo ya majaji iwachunguze.

Kwa mujibu wa ukurasa wa Twitter wa gazeti la kibinafsi la Daily Nation, Wafuasi wa Kenyatta wamekusanyika wakiwashutumu majaji wa mahakama kuu kwa kuwaibia "ushindi wao ".

Majaji wa mahakama hiyo walitoa uamuzi wa kubatilishwa kwa matokeo ya uchaguzi wa urais wa tarehe 8 Agosti yaliyompatia ushindi Bwana Kenyatta baada ya kusema kuwa mchakato wake ulitawaliwa na "ukiukaji wa sheria na makosa"

Maandamano hayo yamefanyika wakati gazeti la The Standard kuchapisha taarifa ya madai kwamba majaji wawili wa Mahakama kuu , Philemona Mwilu na Isaac Lenaola, ambao walipigia kura kubatilishwa kwa uchaguzi, walikutana na mawakili wa kiongozi wa upinzani, Raila Odinga, wakati wa kusikilizwa kwa kesi ya kupinga ushindi wa Bwana Uhuru Kenyatta.

Taarifa hiyo iliyotawala mazungumzo ya raia wa Kenya kwenye mtandao wa Twitter,pia inasema kuwa kuna mazungumzo ya simu yaliyo rekodiwa kuthibitisha kwamba kulikuwa na mawasiliano baina ya majaji na mawakili wa upinzani waketi kesi hiyo ikiendelea.

mwandishi wa habari nchini humo ameripoti kuwa waandamanaji wamekwisha wasilisha madai yao kwa tume ya huduma za mahakama inayowaajiri na kuchunguza mienendo ya majaji nchini Kenya.

Maskini Kichanga cha Siku Tana Chaokotwa Kwenye Mfuko wa Takataka a Kuwekewa Ujumbe Mzito

$
0
0
Maskini Kichanga cha Siku Tana Chaokotwa Kwenye Mfuko wa Takataka  a Kuwekewa Ujumbe Mzito
Mtoto mchanga mwenye siku tano tangu azaliwe ameokotwa na wapita njia katika mji wa East London nchini Afrika Kusini, akiwa kwenye mfuko wa takataka huku akiwa amevirigwa na tshirt, na ujumbe mzito kwa atakayemuokota.

Msemaji wa Polisi wa eneo hilo Nkosikho Mzuku amesema mtoto huyo ambaye ni wa kiume alipatikana siku ya Jumamosi baada ya watoto waliokuwa wakipita kwenda kwa mwalimu wao, na kukuta mfuko huo.

Kwenye mfuko huo walikuta kikaratasi chenye ujumbe ambao unaaminika kuwekwa na mama yake, akiomba kwa yeyote atakayemuokota mtoto huyo ampeleke sehemu salama.

“Tafadhali mchukue mtoto huyu na mpeleke kituo cha polisi, baba yake anataka kumuuza, nimekimbia naye lakini najua atatutafuta, ni bora nife mimi kuliko mtoto kwa sababu hana hatia, nimejifungua mtoto huyu Septemba 14, 2017, ahsanteni na Mungu akubariki”, ulisomeka ujumbe huo ambao ulikutwa kwa mtoto huyo.

Jeshi la polisi nchini Afrika Kusini limesema linaendelea kumtafuta mama wa mtoto huyo na kumtia mikononi mwa sheria.

Jukwaa la Wahariri Tanzania TEF Lapinga Hatua ya Serikali Kulifungia Gazeti la Mwanahalisi

$
0
0
Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) lapinga hatua ya Serikali kulifungia gazeti la MWANAHALISI. Lapanga kujadili hatua za kuchukua.

Shamsa Ford Ajitosa ishu ya Hamisa na Diamond, ‘Hakuna Mwanaume Asiye-cheat’

$
0
0
Msanii wa filamu Bongo, Shamsa Ford ametia neno kile kinachoendelea kwa sasa kati ya Diamond Platnumz na Mwanamitindo Hamisa Mobetto.

Mapema leo hii Diamond amekiri kuwa mtoto wa Hamissa ni mwanaye licha ya kuwa katika mahusiano na Baby Mama wake, Zari The boss Lady. Katika mtandao wa Instagram Shamsa ameandika ujumbe mfupi na kueleza kuwa Zari anastahili pongezi kwa kujua yote na kuamua kukaa kimya.

Kiukweli anasitahili pongezi kubwa sana, najaribu kuvaa viatu vyake kama mwanamke nayaona maumivu yake la pamoja na yote hakuna mwanaume asiyecheat. Zari endelea kumpenda Nassibu wako kamwe usimuache kwa ajili ya mwanamke mwenzio. NCHI YAKO IKIVAMIWA UNATAKIWA KUPAMBANA NA SI KUKIMBIA.

Ujumbe wa Shamsa ni katika post ya Steve Nyerere ambaye naye aliandika, “Wewe ni Malkia wa nguvu na yote yaliyopita bado umesimama na mmeo kuangalia watoto, Be Strong”.


Madam Rita Awacharua Wanaosema ‘BSS’ Hailipi Washindi wake

$
0
0

Kumekuwa na maswali mengi miongoni mwa wafuatiliaji wa shindano la kusaka vibaji Tanzania lijulikanalo kama Bongo Star Search kuhusu uhalali wa zawadi ya milioni 50 kwa washindi wake, huku wengi wakidai kuwa pesa hizo hazilipwi zote kwa washindi.


Sasa Mkurugenzi wa Benchmark Production, Rita Paulsen ameweka wazi tuhuma hizo kwa kuwacharua watu wanaohoji uhalali wa utoaji wa zawadi ya milioni 50 kwa kuwambia ni chuki zao tu kwani wengi wao hawajawahi kukamata hata milioni 10.

“Hii show ipo kwa miaka kumi unategemea mimi na own nchi, unafikiria kwamba hiyo ishu ingekuwa ipo hivyo BASATA ingekuwa haijawahi kufungia Bongo Star Search, watu hawana sehemu ya kwenda kushitaki? kwanini hamuwaiti hapa mkawauliza, nyinyi mnaona kwamba ni kitu hakiwezekani mtu kutoa milioni 5o, kwangu its very easy roho yangu ipo hivyo, kwa hiyo wote hakuna hata mtu mmoja hajawahi kupata hela yake milioni 50,”amesema Madam Rita na kuanza kuwacharua watu wanaohoji mkanganyiko wa utoaji wa zawadi hiyo.


“Tanzania hii mtu atakuwa hajapewa hela zake tuendelee kuwepo BSS iende mwaka wa tisa mwaka wa ngapi, hii nchi ni ya kwangu? hayo ni maswali ya kijinga“,amesema Madam Rita huku  akisisitiza kuwa “Hao wanaosema hivyo wanawaonea wivu, they are just haters, watu wamepata hela zao, huyo aliyeuliza utakuta hajawahi kushika hata milioni 10,“amemjibu mdau  aliyehoji uhalali wa zawadi ya milioni 50 kupitia kipindi cha Maisha Mseto cha Times FM.

Zari Ampa Onyo Diamond ‘Usinijaribu’

$
0
0
Rais wa WCB, Diamond Platnumz bado yupo kwenye kitimoto baada ya kuthibitisha kupata mtoto na mwanamitindo Hamisa Mobetto.

Hatua hiyo imechukua sura mpya baada ya Zari kujibu mapigo katika mtandao wa Snapchat akionya asihusishwe.

Awali katika maelezo yake mwanamuziki Diamond amesema ameshazungumza na mpenzi wake huyo kuhusiana na mtoto aliyezaa na Hamisa na kwamba ameelewa na hakuna tatizo tena.

Wakati Diamond akiendelea na mahojiano katika kituo cha Clouds FM, Zari aliandika katika mtandao huo akisema: “Hahahaha unajidanganya, unasema uongo kuhusu mimi kujua kuhusu michepuko yako, malizana na balaa ulilolianzisha. Mimi kunyamaza haimaanishi ni mpumbavu. Kuwa makini na maneno yako.”

 Aliendelea kuandika: “Inawezekana mimi ni mama wa watoto wako ndio maana nimeamua kunyamaza kimya. Labda ugoogle kuhusu ‘defamation of character law suit’, usinijaribu.”

Diamond alipoulizwa kuhusu kauli hizo amesema anamwelewa kwa kuwa kuna baadhi ya mambo hakumweleza na kwa mara ya kwanza huenda ameyasikia wakati huo.

Breaking News: Saed Kubenea, Mbunge wa Ubungo yupo Chini ya Ulinzi wa Polisi Muda huu

$
0
0
Mh. Saed Kubenea, Mbunge wa Ubungo yupo chini ya ulinzi wa polisi muda huu. Kukamatwa kwake kuna kuja baada ya agizo la spika wa Bunge Job Ndugai kumhitaji afike kwenye kamati ya maadili mjini Dodoma kwa kile kinachoitwa na spika kusema uongo kuhusiana na kupigwa risasi Mh. Tundu Lissu.

Ikumbukwe Mh. Kubenea alikuwepo bungeni wiki hii, lakini akiwa ameshaondoka Dodoma yupo Morogoro akapigiwa simu ya kurudi Dodoma ndipo alipowaambia kuwa asingerudi Dodoma kwa ku...wa alikuwepo huko na walishindwa kumhoji.

Hayo yakiendelea Mapema leo gazeti lake la MWANAHALISI limefungiwa miaka miwili kwa kile kinachoitwa na serikali kuandika habari za kichochezi.

SHINDA GARI LA BUREEEE!!! imebaki siku moja tu wahi sasa

$
0
0
Jee!! Katika Maisha yako umewahi kuwa na ndoto ya kumiliki Gari lako?  Kama jibu ni Ndio Basi Kampuni ya Kijapan inakupa Fasi ya kushinda Gari Buree yani Buree bila kulipa chochote..

Chakufanya ni kubofiya neno SHINDA GARI hapo chini na kisha Bonyeza Neno APPLY NOW kwa kujisajili...

Kumbuka huduma hii ni ya Bure kabisaaaaa...


>> SHINDA GARI <<


Professor Jay Ampongeza Diamond Platnumz, Amwambia Amekuwa Mfano bora

$
0
0
Baada ya msanii wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz kukiri wazi kuwa mtoto wa Mwanamitindo, Hamisa Mobeto kuwa ni wa kwake. Hatimae Mbunge wa jimbo la Mikumi, Joseph Haule a.k.a Professor Jay amempongeza mkali huyo kwa kitendo hicho.

Professor Jay amesema Diamond Platnumz kwa kitendo hicho amekuwa mfano wa kuigwa kwenye jamii kwani kuna watu wengi wanapitia changamoto kama hizo.

“Ukweli humuweka Mtu huru kweli kweli, Big up mdogo wangu @diamondplatnumz Umekuwa Mfano bora sana,“ameandika Professor Jay kwenye ukurasa wake wa Twitter.

Mzazi Awatishia Mabinti zake Wasipo Olewa Hadi Machi Wajiandae Kugegedwa na yeye

$
0
0
Wadau nimeombwa kwenda kusuluhisha mgogoro wa familia ya jirani kesho asubuhi. Katika hali isiyo ya kawaida mabinti watatu wa familia wamenijia usiku huu,kwamba baba yao amewatishia kwamba ifikapo machi wawe wameolewa wote vinginevyo....

Atawagegeda wote watatu kila mmoja kwa muda wake.

Mabinti hao mmoja ana miaka 30 , wa pili 27 na wa mwisho 24 . Maelezo ya mabinti hao wanasema kweli mzazi wao huyo kadhamiria kwani mara nyingi mama yao anapokuwa hayupo wakipita karibu naye huwa anawapiga kofi kwenye makalio .

Hao mabinti wameeleza matukio mbalimbali ambayo yanaonyesha dhahiri kwamba baba yao amedhamiria kweli kuwagegeda kama atapata nafasi .

Huyu binti wa kati ameeleza kwamba mara kwa mara babake huwa anamsifia kwamba ana makalio makubwa yanayopendeza na kuna siku alimwita chumbani ampelekee maji akamshika mkono bahati nzuri akakimbia.

kila binti ameshawahi kukutana na maswahibu hayo. Kinacho onekana kumponza mzee huyo ni tamaa zake tu za kishetani wazee wa kidigitali ni shida.

Sasa nimeona kabla sijafanya lolote niwashirikishe wadau.

Kutana na Mtabibu wa Asili Allan Shariffu Musa Mtabibu wa Nyota za Binadamu na Dawa za Asili

$
0
0
Kutana na Mtabibu Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH shariffu musa Mtabibu wa Nyota za Binadamu na Dawa za Asili ya Africa Mwenye UWEZO Kubaini tatizo lako Pindi tu Utakapo Fanya Mawasilino Kupitia Wasaa Husika..JE UNASUMBULIWA NA Mapenzi? (Umeachwa na Umpendae,Awe Mume,Mke na Bado unampenda?Na Umejaribu Sehemu nyingi Bila Mafanikio?Wasilina na shariffu musa Ujione muujiza wa Papo kwa Papo.. anauwezo WA KURUDISHA MAHUSIANO NA KUIMARISHA NDOA YAKO NDANI YA SAA 12 TU. Umekimbiwa na Mumeo,mkeo au Mpenzi na anaishi na mtu mwingine? Muone akutatulie Anauwezo wa Hali ya Juu wa Kusambalatisha Mahusiano yao Endapo utafata Atakacho kuelekeza.
Atamfanya Atimize Ahadi zote kwa Muda Mfupi.

Maalim Hussein Anatumia Jina la Muhusika au Picha Kumaliza Tatizo lako..
Anatibu kwa Kutumia Vitabu vya QUR-AN Dawa za Asili za Africa,Dawa za Kiarabu na Majini.Anatafsiri Ndoto. Kushinda BAHATI NASIBU, KUSAFISHA NYOTA. Mvuto wa Mwili na BIASHARA, Kinga ya Mwili,ZINDIKO za Nyumba.MIGUU Kufa GANZI.Kufungua KIZAZI kwa wale walio fungwa kwa njia za KISHIRIKINA. Anakupa Jini la Mali kwa yule anaehitaji Utajiri BILA MASHARTI. Nguvu za KIUME, Humaliza Kesi zilishindika ndani ya siku 14 tu..na mengi zaidi

+255 629793352 au watsap
+255 679119679

NB: TIBA KWA DINI ZOTE NA IMANI ZOTE.

Linah Adai Hatoaacha Kupiga Picha za Utata Akibeba Mimba Tena

$
0
0
Msanii wa bongo fleva na mama wa mtoto mmoja Linah Sanga ameibuka na kusema akibeba mimba nyingine hataacha kupiga picha zake tata kama  alizozipiga kipindi akiwa na mimba yake ya kwanza kwa kuwa yeyeni mtu maarufu.

Akiongea kupitia eNewz Linah amesema hajutii kwa picha alizozipiga katika kipindi  cha ujauzito wake wakwanza kwa kuwa yeye ni mtu maarufu  na aliamua kufanya kitu ambacho roho yake ilijisikia kufanya kwa kipindi kile na kuongeza kwamba  hata siku akibeba mimba nyingine anaweza kufanya kitu kama hicho kwa kuwa hakikumuharibia chochote katika maisha yake.

Hata hivyo  Lina aliendelea kusema kwamba "Binadamu ni watu wa ajabu sana na hata ufanye nini huwezi kuwaridhisha kwa kuwa kila mtu anatamani ufanye kile anachokitaka yeye nikivaa gauni refu watasema mimi nimshamba na hata nimevaa hizo nguo fupi bado wanasema hazina maadili hivyo mi nafanya ninachojisikia na waacha waendelee na malumbano yao"alifunguka mbele ya kamera za eNewz

Mbali na hayo Linah amefafanua pia suala la watu kumuona yeye kama amechelewa kujifungua ni kutokana na kwamba watu wengi  waliwahi kufahamu hali yake mapema tangu ikiwa na miezi mitatu hivyo walikuwa kama wanamuhesabia na ilipopitiliza wiki ndipo walipoanza kuhoji.
 Facebook  Twitter  Google+  Pinterest  Linkedin

Zari Aamka Asubuhi Hii na Kuandika Ujumbe Huu Kuhusu Kuchitiwa na Diamond

$
0
0
Zari Aamka Asubuhi Hii na Kuandika Ujumbe Huu Kuhusu Kuchitiwa na Diamond
.
#Zari
Am such an early morning person as some can see on my snap, usually up by 5am. Let's start this day on a different note, shall we🤗
Ladies and gentlemen I've heard you loud and clear, the advises, the consolation, the pity, the hurt you feeling on my behalf most of all the betrayal. But let's look at this on the positive side. When a person chooses to cheat on you it's not YOU actually its THEM which usually turns out that they played themselves while they thought they are playing you. You should never look down on yourself, don't ever think you are worthless because of another person's mistake & never blame yourself. But always look at how to pick yourself up and get going. That said, with my birthday approaching let's put all this negative energy behind us and appreciate, LIFE! 🌹  -

Faiza Ally amuweka Kiporo Hamisa Mobetto, awafumua Team Wema, asema wanatamani Maisha ya Zari ndio sababu ya Kumchukia

$
0
0
Faiza Ally amuweka Kiporo Hamisa Mobetto, awafumua Team Wema, asema wanatamani Maisha ya Zari ndio sababu ya Kumchukia, amsifia Diamond. Faiza ameandika.... .
.
"Nje na ndani ya nchi watanzania wana sifa za ukarimu lkn kwenye uhalisia wana sifa za umbea na chuki na uovu wa chini kwa chini. hlf wanawake wana asili ya uma** ya mnisamehe lkn maana hata ktk safari zangu za maisha ma**la wengi ni kutoka East Africa ni watanzania , wanaona  issue za Mabwana na wanaume ndio mpango wkt kuna mipango zaidi ! Na ndio maana hata ukiachana na mtu unaonekana labda u*hi mmbaya au tabia mbaya maana hawana fikra zaidi ya wanaume ..."

Ameandika na kuendelea "Tukirudi kwenye mada mimi naona zari mnamuonea nyie team wema ndio mliobadilika kusapoti ujinga mnasahau wema ndio alimuacha diamond , hamna mapenzi yoyote na hamisa waongo tu Ila kiukweli mnaweza kuua bila kujua mnaua kwa sababu ya team..." ameangia ndani zaidi kwa kusema

"Kiufupi mna weza mkahisi labda simpendi hamisa au nampenda zari hapana , yaani sijawahi kuwapenda wala kuwachukia lkn nikisimama kama mwanamke sisapoti kinacho endelea zari ni mwanamke kama wengine wote , hamisa ni mwanamke lkn bado mtoto mnajaza ujinga na hamta kuwepo wkt atakapo kuwa na maumivu ... na hamisa Ana jazika kuona labda uzuri wake uta last forever ! Hebu acheni upumbavu.""anyway, nikirudi kwa diamond nimemsifu amesimama kwenye ukweli nimefurahi sana na nimemfurahia hamisa pia maana najua uchungu wa mtoto kukosa baba, hata Kama Ana makosa lkn mtoto hana kosa lkn nimefurahi zaidi diamond kuwa mwananume enough ku simama kwa ajili ya familia yake na mapenzi yake kwa zari !" amesisitiza "Sasa ktk swali nililo uliza hapo juu jibu ni hili ! Zari mzuri,zari kijana, zari Ana maisha mazuri , zari star , zari Ana mume star. Zari Ana watoto wa zuri zari Ana almost kila kitu kizuri nahisi hadi Dudu lake zuri na hichi ndio kinacho wa fanya mmchukie for no good reason na wote mnao mchukia mnatamani maisha yake lkn mnasahau Mungu amemchagua, ""kiukweli hakuna kama zari na akija itakua zilipendwa lkn kwa sasa zari ndio star mwanamke east Africa nzima na sio star njaa... ndio maana mna mnafurahia matatizo yake !
Viewing all 104795 articles
Browse latest View live


Latest Images

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596344.js" async> </script>